OMBI LA KIJINGA
Sehemu ya tatu
Tabia ni mazoea na mazoea yana tabu. Ikawa kila mara H apness akiukamata ujauzito kwa maombi ya mumewe aliutoa bila kukawiza. Furaha alimshawishi Happy wale kwanza ujana (wafanye anasa na starehe) kabla uzee haujawakamata. Ilipita miaka mingi miaka kumi na mitano ya ndoa yao pasina kuwa na mtoto na katika kipindi hiki bwana Furaha alianza kulikumbuka shuka kumbe tayari kumepambazuka.
“My love unajua kwa sasa tumeanza kuzeeka tayari tumekwisha kula ujana na raha zote za dunia, raha za mali na utajiri wetu sisi wenyewe, tumefurahi vya kutosha na kuburudika.” Tajiri Furaha aliongea na mkewe.
“Tungali tumebakiza kitu kimoja muhimu kuwa nacho maishani.” Tajiri aliongea tena.
“Kitu gani hicho mume wangu?”
“Mke wangu tunahitaji mtoto, mtoto wa kurithi mali zetu hizi nyingi pomoni mara baada ya sisi kutoweka duniani.”
“Mtoto? Mmmh! Hivi mume wangu una matatizo gani wewe? Yaani baada ya miaka kumi na mitano ya ndoa yetu leo hii una uona umuhimu wa mtoto, wakati unajua fika ulikua king’ang’anizi ukinitaka nitoe kila ujauzito. Nilioupata..”
“Sikiliza mke wangu, awali mie nilitaka tuponde raha na furaha, sikuwa tayari kuona tunae mtoto, tizama sasa raha na furaha tayari tumekwisha zipata haja yangu kwa sasa ni kupata mtoto wakurithi mali na utajiri wetu.”
“Ok mpenzi, ni vizuri kama upo tayari kwa hilo.” Happy alikubali na kushukuru kwa hilo, sijui kwanini Happy alikuwa duni kiasi kile, kila neno analoambiwa na mumewe hapingani nalo, anakubali, anaunga mkono bila pingamizi lolote.
Wawili wale walianza harakati za kusaka mtoto, hata hivyo kadri siku zilivyozidi kuyoyoma, Happness hakuonesha darili za kushika ujauzito, jambo lililowafanya wawili hawa wafanye maamuzi ya kwenda Hosptali kumwona Dakta. Ili wapate kujua ni nani kati yao anayeshindwa kumleta mtoto duniani. Walipofika Hospitali majibu ya Vipimo yalionesha kwamba tatizo lipo kwa Happness kizazi chake kilionekana kuwa kimehama tena kimeshuka, mji wa mimba umeharibika kutokana na kile kitendo cha yeye kutoa mimba nyingi mara kwa mara, pasina huruma pasina kujari kuwa kufanya hivyo kuna hatarisha maisha yake.
“Madakta walihitimisha kwa kumwambiaHappy asingeliweza kupata mtoto maishani mwake. Looh! Happness alilia kwa uchungu, majuto ni mjukuu, alilia na kuumia. Mwe! Maskini! Wahenga walisema fikiri kabla ya kutenda, tazama Happy na mumewe Furaha hawakufikiri mara mbili mbili juu ya kitendo kile kiovu, juu ya zambi waliyokuwa radhi kuitenda mara kwa mara.
Furaha hakutaka kuamini macho yake juu ya vile vipimo, alihisi vipimo vile vinaongopea, akaomba vipimo virudiwe tena na baada ya kurudiwa majibu yalikuwa ni yale yale Happnesss hawezi kushika ujauzito. Machozi yalimtoka Happness.
“Dakta hivi ni kweli kusema mke wangu hawezi kushika ujauzito?” Furaha aliuliza kwa majonzi.
“Ndo’ hivyo tena yashatokea, maji yakimwagika hayazoleki.
“Ninakuomba urudie kupima Bwana Dakta.” Furaha aliongea kwa huzuni
“Nimepima karbia mara tatu mkuu wangu, majibu ni yale yale hayajabadirika.” Yule Dakta aliyezoea kula rushwa na kufanya tendo la kumtoa mimba Happness leo alimwaga matokeo.
Basi Furaha na Happness wakawa ni watu wa kuhangaika huku na huko ili kutafuta tiba juu ya tatizo linalomkabili Happness. Walipoteza pesa zao nyingi lakini bado hawakuona matokeo, walipoteza muda wao mwingi lakini bado hawakuambulia kitu, waliambulia patupu, hasara kubwa namna gani, furaha yao ikatoweka baya zaidi walikuwa na mali nyingi lakini hawakuwa na mrithi wa hizo mali
Wawili hawa wenye kujutia matendo yao, waliziona mali zao si kitu, pasina kuwa na mtoto, Furaha akawa ni mtu wa kujilaumu kwa jinsi alivyomshawishi mkewe awe ni mtu wa kutoa toa ujauzito looh! Tamaa mbele mauti nyuma, Hasara ilioje lawama pamoja na wingi wa mawazo vilimfanya Furaha akonde na kuisha kabisa.
Akuyatamani tena maisha, aligeukia ulevi wa kutupwa, kila siku ni majuto na masikitiko, looh! masikini! Tizameni ndugu zangu maamuzi mabaya uleta matokeo mabaya, yaliyomkuta Happness yawe funzo kwa wale wote wanao toa mimba au kuua vitoto ndani ya matumbo yao. Ikumbukwe kwamba hata Mwenyezi mungu hapendi matendo haya yanayochukiza, tusiyatende milele maishani mwetu bali tumwombe Mungu atupatie watoto lukuki wawe warithi wa mali zetu hapo baadae.
*************************
TCHAO 💖
No comments:
Post a Comment