OBIMO CHETA
Sehemu ya tano
Mimba ya Derila ilikuwa kubwa, kubwa tena ya kutaka kujifungua, hakuwa na jinsi, kuombaomba ndio kazi, kazi ya kumpatia Riziki yeye na Frank. Hawana pahali pazuri pa kuishi, popote pale penye nafasi wanalala kwenye maboma, majengo ambayo hayajakamilika kujengwa, Derila haachi kumuwaza Singa, amemmisi sana, ni muda mrefu hajamtia machoni.
Leo yupo ndani ya Boma, wamelala yeye na Frank, hawana kitu zaidi ya chungu na sufuria wanayotumia kupikia ugali, hawana kitanda wala godoro, wanalalia maboksi, mbu huwachosha, popo huruka ruka, mbwa na paka nyakati za usiku huranda randa kutafuta riziki yao. Leo ameshindwa kwenda mjini kuomba omba, badala yake ametulia ndani ya boma wanalolala, na baada ya mda aliamka kuchambua chambua mboga za majani akazikata kata na kuzibandika kwenye chungu chao kikuukuu. Mboga hiyo (sukuma wiki) ilipoiva iliepuliwa, na baada ya kuepuliwa, Derila alitenga maji ya ugali.Frank atakuja mda si mrefu kula kidogo alichokuta, na baada ya hapo Frank angelirudi tena barabarani kuimba na kuomba omba wapitao njia vijisenti viwili vitatu.
“Oooh! Oooh! Oooh!” Derilka alianza kuhisi kama tumbo lake linachezacheza naye akapumua kwa kasi, akaendelea kuusonga ugali.
“Oooh!” Alilalamika Derila, tumbo lake lilikuwa kama vile linanguruma, kitu kinatembea tembea na kumkanyaga kanyaga, ilimbidi aache kupika ule ugali, nguvu zilimuishia, akajilaza juu ya boksi moja walilotumia kulalia, uchungu ulimkamata, alianza kupiga kelele za kuomba msaada.
Nani aliyejitokeza, hakuna aliyejitokeza, eneo analolala yeye na Frank hakuna watu wengi, ni eneo lililojificha sana, hata wao wamejificha kwa sababu pahali hapo sio pao. Frank alikuwa akikaribia kurejea hapo kwenye Boma lao, alisikia sauti ya mwanamke aliyekuwa akiomba msaada, haraka haraka Frank alielekea kule sauti ya kilio cha Derila iliposikika. Oooh! Alimkuta Derila yupo katika uchungu mkuu, analia peke yake, analia damu zikimtoka na kupita juu ya lile boksi alilolalia Derila.
Frank alipofika alimkimbilia Derila na kumuuliza;
“Tatizo nini Derila?”Frank alijaa hofu na mashaka asijue nini afanye kumsaidia Derila.
“Nisaidie Frank, sina pa kwenda, Hospitali ipo mbali, sijui nifanye nini mie?”Derila alilia kwa uchungu. Frank akaangaza huku na kule akauona ugali unaungulia, haraka haraka akauepua na kuuweka pembeni, kisha akaenda pale alipolala Derila, akamlaza vizuri asijue la kufanya.
“Sijui Derila, Sijui kuzalisha mie, sijui mambo ya udakta.”Frank aliongea, ni kijana mpole, hata sauti yake imejaa upole mwingi.
“Nisaidie, hakuna mtu wa kunisaidia, uwiii, uwiii, Yalaah!”Derila alilia kwa uchungu, amelala pale juu ya boksi lililojaa damu.
****
“Ok, mtoe, mtoe basi Derila.”Frank aligeuka Daktari, amekinga mikono yote miwili, anamsubiria huyo malaika atakayekuja.Derila aliendelea kulia kilio cha uchugu. Ndani ya dakika tano zilizofuata, Frank alikiona kichwa cha mtoto kinaanza kuchomoza.
“Ameanza kutoka, kazana Derila, kichwa chake kimeanza kutoka, je nimvute?” Frank aliongea, hajui kitu, amechanganyikiwa.
“Hapana Frank, usimvute, atatoka yeye mwenyewe, ukimvuta atapatwa na madhara makubwa.” kisha Derila akaendelea kulia. Frank alikuwa na subira, akamsubiria mtoto, mtoto akatoka tumboni mwa Mamaye, naye akalia kitoto kitoto ‘ng’aaa, ng’aaaa-ng’aaaa.” Hiyo ni ishara ya kwamba mtoto yupo hai, Frank akatabasamu, Derila akachekacheka na kukipakata kitoto chake.
**************
MIAKA MITSTU MBELE
Miaka mitatu imepita sasa, tangu Derila amezaa mtoto mzuri wa kiume aliyempa jinale ‘uche’, mtoto huyu mzuri amefanana kila kitu na Babaye mzazi Singa. Anacheza cheza pembeni ya Mamaye ambaye wakati wote huo ni mwingi wa mawazo, anawaza juu ya mpenzi wake Singa, anamkumbuka sana Singa, hana amani wala hana furaha juu ya penzi liolilopotea na kuzimika mikononi mwake.
Mara ile Derila anamkumbuka Frank, machozi yanamtoka, masikini loh! Frank yule kijana aliyekuwa ndoto za kuja kuwa Mwanamuziki mkubwa sana ndani ya Afrika ya Mashariki pamoja na Afrika yote kwa ujumla, ajabu mipango ya Mungu.
Derila analia akikumbuka ile siku anashuhudia Frank akikata roho yake mbele ya macho yake. Ooh! Masikini ya Mungu, ajari ya Gari lililokimbia force force kuingia eneo ambalo wao wameketi kuomba omba kwa waja wake mwenyezi Mungu.
Derila alipona, mwanaye Uche alipona pia, ajari ile ilikuwa mbaya ilitafuna uhai wake Frank, masikini Frank alikata roho yake mbele ya Derila, masikini Derila akalia na kuomboleza kifo cha rafiki mwema kama Frank.
Wakati wote huu, miaka mitatu baada ya kuzaliwa Uche, Derila hakuacha kuwekeza kidogo kidogo alicho nacho, na Mungu yu mwema, haba na haba hujaza kibaba, alipata pesa ya kutimiza mapenzi ya rafiki yake mpendwa Frank, mwanamuziki kwake na daktari kwake, msaada na faraja kwake, Frank aliahidiana na Derila kuingia studio, kufanya kazi ya kuimba, hata kama walitamani kujaribu, waliamini kuwa kujaribu sio kushindwa, mbuyu ulianza kama mchicha.
Yule omba omba aitwaye Derila aliingia studio, amejiandaa na kujipanga aimbe wimbo wake, wimbo mtamu uliojaa mapenzi.
“Nimekumiss mpenzi,
Nimekupenda sana,
Nitakua pamoja na wewe
Wakati sio muda
Uwe na mimi mpenzi,
Uwe na mimi Baby,
Nitakua pamoja na wewe,
wakati sio muda.
Nilikumiss miss kumiss,
Nilikumiss Baby,
Nitakua pamoja na wewe
Wakati sio muda.
Waooh! Ile sauti yake tamu, tamu ya kumtoa nyoka pangoni ilimvutia sana produzer aliyekuwa akirekodi wimbo wa Derila.
Producer alihitaji kufanya kazi na yule mwanamama. Produzer Moe- Joe, sio mtu mdogo katika fani hiyo ya Muziki, alikuwepo studio miaka kumi na mitano iliyopita, naye amefanya kazi na wasanii wengi, ndani na nje ya Afrika.
Mbali na kufanya kazi na wasanii wengi, Moe-Joe amewasaidia wengi ambao hawakuchoka kumrudishia fadhila na shukrani nyingi.
“Dada, nahitaji kufanya kazi na wewe.” Joe alimwambia yule mrembo ombaomba.
“Asante sana Produzer, nimefurahi kusikia hivyo.”Derila alitabasamu, yupo pamoja na mwanaye Uche, wametulia tuli ndani ya chumba cha studio ya produze Moe- Joe.
“Sauti yako inavutia sana, mashairi yako yana ujumbe pia ambao ni rahisi kueleweka, nahisi nikurekodi bure wimbo huu na pia video nitagharamia mimi, kila kitu nitafanya mimi, ilimradi usiniangushe tuweze kuingia mkataba ili tuvune mamilioni ya pesa.” Moe- Joe aliongea, amemfurahisha sana yule mwanamama, mwanamama anayeona bahati ikimtembelea pasina kujua fika kuwa ingelimtembelea mapema namna ile.
“Unaishi wapi, na pia unaishi na nani?” Produzer Moe- Joe alitaka kujua.
“Naishi hapa hapa Njiro, nipo mie na mwanangu, japo maisha yangu yamekuwa magumu kutafsiriwa.”
“Haujaolewa?”
“Ndio sijaolewa japo tayari nimezaa mtoto.”
“Ok,. Usijari, nitakusaidia.”
Moe-Joe alianza kumsaidia Derila, alikwisha kugundua kuwa Derila hana pahali pazuri pa kuishi, hapo ndipo alipojitolea kumpangishia chumba kizuri tofauti na lile Boma lililojaa mbu na viroboto, chakula kizuri Derila na mwanaye walikula, mavazi pia walivaa na afya zao zilianza kurejea. Derila tayari alikwisha tengeneza Video yake ya kwanza akiimba wimbo wake mtamu masikioni mwa wengi. 'Nimekumiss.' Ndio jina la huo wimbo, hakika wengi waliopata kumwona walivutiwa na jinsi alivyokuwa na sauti njema.
*********************
Singa alipigwa na bumbuwazi pale alipomwona mpenzi wake wa zamani yule aliyempenda kwa mapenzi ya dhati, Derila akiimba kwa hisia na hisia, alimshangaza Singa, alionekana kwenye Televisheni, anasomwa kwenye vitabu na magazeti, anaimba, anaalikwa kwenye matamasha mbali mbali apate kutumbuiza. Ooh! Singa alipigwa na butwaa, macho yakamtoka, akalia ndani ya Getto lake, akalia kwa uchungu, yupo vile vile kama alivyotoka Usa-River miaka minne iliyopita, ameukuta umasikini wa wazazi wake ni mkubwa, tena hautamaniki, amewakuta wazazi wake wanamtupia lawama na kumlaani kwa kitendo cha kuwatoroka na kushindwa kurejea. Singa alijitetea, akajitetea akisema, alinusurika kuuawa na Polisi, ndio maana alikimbilia mjini kuukwepa mkono wa sheria. Utetezi wake haukufaa kitu, bado wazazi wake walimlaani na kumlaumu.
“Nitafunga safari, nami nitaenda Arusha nikamwombe msamaha Derila.” Singa alijipa tumaini, machozi yakimtoka, ameishikilia picha aliyoipiga pamoja na Derila miaka minne iliyopita.
“I’am Sorry Derila, please, forgive me.”Singa alilia akijutia tendo la yeye kumtelekeza Derila yule waliyependana mapenzi ya dhati.
“Nisamehe Derila.” Singa alilia akipita pita ndani ya kiijiji chao, kijiji cha Maasai Land,wanajamii wakiendelea na shuhuli zao za kijamii, wanawake walionekana wakijenga nyumba, wengine wakikamua maziwa, vijana wadogo wakirejesha mifugo nyumbani kutoka malishoni, wakati wazee wakiketi vikundini wakijadiliana.
**********************
No comments:
Post a Comment