Saturday, July 5, 2025

I PROMISE YOU.

 




SURA YA TATU





MIPANGO


Miaka miwili na nusu iliniacha nikiwa ndani ya kiwanda cha TBL, safari hii nilikuwa na cheo changu, sio mpishi tena mpishi wa pombe jikoni, kwa sasa niliketi ofisini nikiunyosha mguu wangu  juu ya meza moja tukufu, safi nzuri yenye kioo kimoja kinene kipana, kioo hicho chafutwa futwa kwa mikono laini ya yule Secretary wetu  Riziki. Nikiwa nimeketi kwenye kiti kimoja chenye magurudumu yazungurukayo nimepozi kwa kutupia suti yangu nadhifu nyeusi pamoja na tai yake, ndani ya hiyo Ofisi ukiingia tu basi lazima uniite meneja msaidizi hicho ndio cheo changu, wacha nijivunie, nimetoka jikoni kupika na sasa naketi Ofisini kupanga na kupangua mipango ya fedha.


               “Nimependelewa, ati eeh!?”
Yawezekana nimependelewa tena nimependelewa na yule aliyeniokota barabarani. Barabara ya Ubungo, kituo kikuu cha mabasi yaendayo na yatokayo mikoani. Nimependelewa na yule Bwana aliyetaka kuniswaga mguu wangu wa mashoto pindi nikiwa navuka barabara, ningeligongwa mguu wangu kwa uzembe na ushamba wangu ndani ya Jiji la watu, watu walioniokota kwa mapenzi na kudra za Mwenyezi Mungu  na uzuri wa mapenzi yake Mola mie leo niko bize nalikokota Gari langu nilillopewa kazini n bosi wangu.


                ********************************
                

         Ndani ya nyumba niliyopewa na Bwana Steven Biko siishi mpweke, Brenda amenifuata, amenifuata kutoka kijijini na kuja mjini, amekuja miezi tisa iliyopita, nimekwisha kumvisha pete nzuri ya uchumba, kwa sasa tunapanga na kupangua mipango ya ndoa yetu. Bado hatujawa radhi kueleza ni lini tunatarajia kufunga ndoa  itakayofanyika kijijini kwa wazazi wetu na wazee wetu, Aki! Hiyo itakuwa ni ndoa ya kimila na baada ya kutimiza mila tulihitaji kufanya sherehe kubwa ndani ya jiji la Dare s saalam.
Bosi wangu pamoja na wafanyakazi wenzangu wametoa ahadi ya kuninunulia bonge la zawadi, zawadi ya kunisapraiz. Mmmh! Sijui ni zawadi gani hiyo? Mmh!  Nisiandike mate wino ukiwepo, lisemwalo lipo kama halipo langojwa, uzuri wa ahadi, ahadi ni deni na deni sharti litimizwe.
Kwa sasa Brenda ni mjamzito, ujauzito wake ni wa miezi miwili, mie ni mwingi wa furaha, najiona nimekwisha kamilika, ni mwanume sasa, mwanaume kamili. Brenda amekuwa Ua linalo chanua moyoni mwangu ninampenda sana, ninampenda kama anavyonipenda, ninampenda kama malenga mshairi mmoja anavo ghani;


Ninampenda mpenzi wangu,nalipenda penzi langu,
Ninalilinda sungu sungu, liondokewe kiwingu,
Sintatenda ya kizungu, penzi hili penzi langu,
Kwa maneno na mizungu, penzi hili penzi langu.
Kila nikifikiria, nilifanye nini pendo,
Fikara zinanijia, nilipende kwa vitendo,
Penzi kujivunia, siwezi litupa kando,
Maisha 'menandalia, pendo lenye mapendo.


Pendo limenipenda, pendo limeniganda,
Pendo sipate shida, pendo tulia tunda,
Pendo litonishinda, pendo kwake tashinda,
Pendo ya kwangu ajenda, pendo penda pendo.
Nataka niwe karibu, daima kwenye mapenzi,
Nipate kila sababu, mapenzi yangu nasibu,
Tabu pamoja na gubu, siweze kuyasulubu,
mapenzi yawe dhahabu, faida kubwa ajabu.


Natoroka naenda kwake, kwa aliyenipendeza,
Mie niwe tulizo lake, yule nino’mchunguza,
Moyo wangu moyo wake, mapenzi twayaongeza,
Mbele sisi twende tufike, tuombe tusitereze.
Moyo wangu moyo wake, mapenzi tuyatulize,
Nani apenda upweke, hilo swali jiulize,
Mapenzi yetu yavumike, mbele sana tuwajuze,
Tupende tuheshimike, maisha mema      tu wajuze.


         **********************************

                “Mmmh!” Niliachia mguno mkubwa ndani ya ofisi yangu. Nalikuwa pamoja na bwana Steven Biko bosi wangu na mwajiri wangu.


                “Usishangae Bwana mdogo, biashara hii ni moja ya biashara itakayo tuletea faida kubwa sana kikubwa ni utayari wako katika kuifanya hii biashara.” Biko aliongea.

Moyoni sikutaka kuamini kama kweli haya ni maneno yatokayo ndani ya mdomo wa bosi wangu  Steven Biko.

                 “Je wewe binafsi umewahi kuifanya hiyo biashara?” Nilimuuliza Bwana Steven Biko.

                “Yes, tena hivi ninavyoongea pamoja na wewe ni mara yangu ya kumi kwenda na kurudi  South Africa kuiendesha hii biashara iliyonitia utajiri na umilionea.” Aliongea bosi wangu Bwana Steven Biko.

Nilivuta pumzi kidogo, kisha nikatafakari maneno aliyonishawishi bosi wangu, siku ya leo, leo tumetumia saa moja na ushee kujadiliana kuhusu hii biashara.

                 “Mmh! Lakini….. Mmh!” Niliguna tena kuonesha wasi wasi wangu, moyo wangu ulisita sita kukubaliana na Bwana Biko.

“Lakini nini tena bwana Job? Kumbuka wewe sio tu ni mtani wangu,  wewe ni ndugu yangu tena ndugu wa kufa na kupona changu chako, damu yangu damu yako au vip mawazo yangu yawe mawazo yako?”

                 “Moyo wangu unasita sita.”

                 “Unasita sita nini?”

                 “Nina hofu ya kukamatwa na maofisa wa Polisi watakao nishuku kuwa nimebeba madawa ya kulevya na kuyapitisha Air port.”

                  “Hilo tu, mbona hilo ni jambo dogo sana, iwapo utatiwa chini ya mikono ya polisi, mimi pamoja na mabosi wangu wengine tutafanya mipango ya kukutoa ndani ya mikono ya makachero wa Polisi tambua kwamba biashara hii ina mtandao mkubwa sana, hii biashara ina watu wakubwa duniani, faida yake ni kubwa sana iwapo utakuwa tayari kujiingiza ndani ya hii biashara nina imani utavuna zaidi ya hapo ulipovuna.” Steven Biko alijaribu kunishawishi.

                 “Ok. Bwana Steven Biko nipo tayari kuungana nawe katika hii biashara ya kusafirisha dawa za kulevya, kutoka  Tanzania kwenda South Africa. Ilihali umenihakikishia kuwa, ulinzi, usalama  na imani vyote ni vya kutosha kwa ajiri ya nafsi yangu na maisha yangu. niliongea pasina kufikiria mara mbili mbili athari zinazoweza kunitokea iwapo nitapatikana na hatia ya kukutwa na  dawa za kulevya mikononi mwangu.”

                Tabasamu lilimtoka Bwana Steven Biko alipohakikisha utayari wangu katika kufanya kazi ile ya hatari pamoja nayeye moyo wake uliripuka kwa shangwe na furaha isiyo na kifani, nilimshangaa mara nilipomwona akisimama pale alipoketi na kuja kunikumbatia kwa nguvu zote akidai kuwa amefurahishwa na ushirikiano wangu, ushirikiano mkubwa niliouonesha mbele yake.

               “Congraturation mtani wangu, now you are going to be a rich person in East Africa, nitakuwa pamoja na wewe kwenye shida na raha, sitakutema kamwe, wala sitakuacha uteseke, jumatatu ni siku special kwa maandalizi ya wewe kwenda Africa ya Kusini, mimi nitafanya juu chini kuhakikisha kuwa unapata passpot size pamoja na Visa yako binafsi.

                 Aliongea bosi wangu usoni kwake ameng’ara kama jua, tabasamu lake pana kama shimo kubwa lililo wazi, wakati wote anacheka cheka kama mwendawazimu, anadai kwamba amependezwa na ushirikiano mwema nilio uonesha.

Itaendelea sehemu ya nne.

No comments:

Post a Comment

OBIMO CHETA

 OBIMO CHETA (MY LOVE REMEMBER). Siku Derila alipokutana na Singa, ilikuwa ni siku nzuri, siku ya kusheherekea sikukuu ya Christmass,🌲🎄⛪...