Sunday, July 6, 2025

OBIMO CHETA

 OBIMO CHETA

(MY LOVE REMEMBER).



Siku Derila alipokutana na Singa, ilikuwa ni siku nzuri, siku ya kusheherekea sikukuu ya Christmass,πŸŒ²πŸŽ„⛪ kama tujuavyo tena sherehe ya Christmass ndani ya mji wa Usa river, unoga na kunogela, hunoga haswa, hupendeza na kuvutia. Christmass ni sherehe inayopendwa na Wachaga, Wameru, Waarusha, Wamaasai na Wapare, kila mwenye nyumba yake humkaribisha jirani, ndugu au jamaa wapate kufurahia sherehe pendwa ya Christmass, kila mwenye nacho hukitumia kwa furaha pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.πŸŽπŸŽ…πŸπŸœπŸ±

        Siku njema huonekana asubuhi, hakika siku ilionekana, kila mja alikuwa katika pirika pirika zake za kila siku ili apate kujitafutia riziki , riziki popote, Mwenyezi Mungu hugawa. Sokoni ndio ulikuwa mpango wa kila mpenda Christmass, basi siku hiyo Derila alitumwa na wazazi wake kwenda sokoni japo apate kununua hiki na kile, waandae maakuli, waandae mapochopocho, wale wao na jirani zao, katika kuchagua chagua vyakula alivyoagizwa alete kwa ajiri ya Christmass, mara ghafla machoπŸ‘️πŸ‘️‍πŸ—¨️ yake Derila yaligongana na macho ya kijana Singa. Wakatizamana sio kwa sekunde, wala sio kwa nukta bali ni kwa muda mrefu ajabu.πŸ•¦

        “Vipi dada mbona umezubalia kule?” Muuza mchele alimuuliza Derila huku akinyosha kidole πŸ‘‰chake kuelekea eneo ambalo Derila alikuwa akitazamia.

        “Aaah No! Kawaida kutizama.” Derila aliongea.

        “Poa, sasa utachukua kilo ngapi za mchele dadangu?” Aliulizwa swali.⁉️

        “Kilo sita ⚖️pamoja na viungo vya pilau.” Derila alimjibu muuza mchele ambaye muda huo alianza kupima zile kilo sita alizoambiwa apime na mrembo Derila, mrembo ambaye wakati wote huo macho yake yalitizama mbele sehemu ambayo alikuwepo yule kijana mzuri machoni.πŸ’•

        Yawezekana walipendana, tena walipendana sio machoni tu, bali pia moyoni, mawazoni na fikrani, yote kwa sababu Derila aliyapenda macho ya yule kijana aitwaye Singa. Singa pia aliyapenda macho ya Derila, Derila aliipenda midomo yake Singa. πŸ‘„πŸ’‹πŸ’„Derila aliyapenda meno yake Singa mara ile alipoyaona yakichomoza kutoka kwenye tabasamu la midomo yake, Singa pia alivutiwa na kuvutwa na meno mazuri yaliyopangiliwa ndani yamdomo wake Derila, walitazamana, nywele zao ni za asili, nzuri za Kiafrika, safi zilizokolezwa mafuta ya asili, zinavutia na kupendeza machoni. Mara baada ya Derila kununua mahitaji yake yote kutoka kwenye kile kigenge, alitembea hatua mbili tatu akimfuata yule kijana aliyeyapendeza macho yake, hapakuwa na umbali sana, mita chache tu akamfikia wangali bado wanatizamana.

        Singa kijana mweusi wa Kiafrika, yaani mweusi tii kama chungu, ana meno meupe mithili ya maziwa safi, ni mrefu kama mlingoti, kumbe ni Mmasai kwa kabila, mwembamba japo yeye havai kama wanavyovaa vijana wengine wa Kimaasai. Kastaarabika, anajitambua kifikra na kiakili, ndio maana anaenda na wakati pamoja na mazingira yanayomzunguka. Derila yeye ni binti wa kichaga, mweupe pee, mweupe wa rangi ya chungwa lililoiva sana, hiyo ndiyo rangi ya Wachaga, sio mrefu wala mfupi, ni wa Wastani, sio mwembamba wala mnene, ni wa wastani.


        Wakati Derila yupo kidato cha nne amekwisha kuwa mtu mzima, Singa hana lolote la kufanya yupo yupo tu, darasa la saba ndio elimu yake, amemaliza miaka saba iliyopita, tena alifeli, nani wa kumsomesha? Hakuna wa kumsomesha, babaye Singa alimtaka ajiunge na kikundi cha Morani, wakateke na kuiba wanyama (cattle raiding) ndio, alijiunga akiamini kuwa iwapo angelileta nyumbani kwao kundi dogo la ng’ombe, mbuzi au kondoo,πŸ„πŸπŸ wangeliupunguza umasikini uliotawala nyumba yao. Haki ya Mungu umasikini mbaya, mbaya tena mbaya zaidi. Walilia njaa wale wanafamilia, tena njaa isiyokoma, pesa lilikuwa nitatizo, tena tatizo la dunia ndio maana babaye alimtaka mwanaye aende Cattle raiding, akawateke na kupora mifugo, babaye alijiaminisha kuwa kufanya hivyo kutapunguza umasikini unaowanyanyasa. Babaye alitamani achekecheke kidogo nayeye aonekane kuwa ni mtu mbele za watu, yote kwa sababu kidogo ambacho mwanaye atakileta nyumbani, hicho ndicho kitakachompunguzia njaa na kiu ya pesa.

        Singa alienda? Ndio, alienda, alienda kupora wanyama, lakini asilolijua lilimsumbua, matokeo yake alijuta, tena alijuta juto la mjukuu naye aliapa kamwe asingelirudi tena. Walipora? Ndio, walifanikiwa kupora wanyama, tena walipora vizuri sana. Wakiharakisha kuondoka, walishtuka wakivamiwa na polisi waliokuwa bize wakiwarushia risasi. Duh! Mbona mkosi, duh! Mbona Singa alishuhudia Morani wenzake wakidondoka chini na kufa kwa pigo la risasi.


        Singa alichoropoka na kukimbia mbio za farasi, aliponea chupuchupu kuuawa au kutiwa mbaroni, hata hivyo alimshukuru Mungu kwa wokovu aliomtendea, haikuwa jambo rahisi na jepesi sana kushinda kifo cha risasi, alikimbilia msituni, alikimbilia porini, hakutaka tena kurudi nyumbani kwa babaye na mamaye waliomsubiria kwa matumaini ya kupata kile wanachoamini kuwa kingeliwapunguzia njaa na umasikini nyumbani kwao.


        Singa hakurudi nyumbani kwao Loliondo, alikimbilia Arusha mjini, huko nako hakukaa sana zaidi ya kwenda katika Wilaya ya Meru, ndani ya mji mdogo wa Usa River, Basi huko Singa alijibidisha na shughuli ya kusomba takataka za pale sokoni, naye akalipwa ujira kiduchu. Hakuchoka kubeba mizigo inayoingia sakoni, bado malipo aliyolipwa kiduchu, akivumilia tu, akivumilia kazi hizo nzito kuliko ile ya kuiba mifugo ya Wamaasai wengine.


Itaendelea

No comments:

Post a Comment

OBIMO CHETA

 OBIMO CHETA (MY LOVE REMEMBER). Siku Derila alipokutana na Singa, ilikuwa ni siku nzuri, siku ya kusheherekea sikukuu ya Christmass,πŸŒ²πŸŽ„⛪...