Thursday, July 24, 2025

MWENZENU N'SHAPENDWA

 


MIPASHO YA MAMSAPU 


MWENZENU N'SHAPENDWA 

Sehemu ya sita


      Nikafanya mara kwa mara kumtembelea Pompo nyumbani kwake, kigamboni huko alikopangisha chumba singo, nikimfulia, nikimpikia, nikimpugutia deki, nikimnyoshea nguo na uzuri wa mwanaume yule mie nilipenda jinsi anavyojituma, moyo wake wa kutafuta, moyo wake wa kuleta vitu muhimu nyumbani moyo wa kujali na kukumbuka. Aki! Moyoni nilijisikia kupendwa.


Nikwambieni, nikwambieni shoga zangu, nikwambieni nisikuficheni, Pompo na mie wakati mwingine tulikuwepo kwenye yetu mahaba, Kumbe Pompo ni fundi eeh!πŸ˜‰ Teeh teeh teeh!πŸ˜‚πŸ˜Š (nacheka mie) Ni fundi seremala, fundi mzuri mambo anayaweza, nisikufiche mwaya, mwenzenu n'shapendwa, Mzee Baba akanikanda kanda kama kando la maandazi, nami nikakandika, akinilainisha kama uji uji wa mrenda kisha akanigeuzageuza kam chapati, ai…. Mwaya nisizidishe chumvi chakula kitadoda.


               Mapenzi yakanoga, Pompo sio mchoyo ana moyo sana ana huruma pia ni muwazi sana, hanifichi kitu, mie ni wake na yeye ni wangu. Kana’mbia mwenyewe anataka kunioa,πŸ’ tena kasemaje, kasema anataka tufunge harusiπŸ’’πŸ€΅πŸ‘°, haijalishi hata kama hiyo harusi haitakuwa ya bei gharama ilimradi Pompo kanipenda, posa tayari, kajitambulisha kwetu, keisha nilipia mahari, Keisha kutambuliwa na wazazi wangu kule Tanga Aloo! Jamani! Kakubaliwa na kupokelewae vema ukweni washampa baraka zote wenyewe wam’tambua.


Pompo akafanya Juhudi akajituma zaidi na zaidi akajibidisha, Mungu wake Mungu wa Ibrahimu, Isack na Jacob akamtangulia mbele ya safari ya Maisha yake, akamsaidia na kumuwezesha. Pompo hakuzichoka zile kazi zake kazi za kusaka tonge la maisha akivuja majasho na maumivu tele, leo akichimba makaburi kesho akifukua vyoo, kesho kutwa akiuza kahawa na kashata siku zingine akijitafutia riziki yoyote ile Riziki popote Mwenyezi Mungu anagawa. Mwanaume wangu hakusahau kuwekeza pesa zake Benki tena hakusahahu kuendelea kujenga nyumba yake huko Kigamboni.


             Kasemaje kasema ati muda si mrefu ataniweka ndani, basi mie nikacheka na kufurahia, kwake mie ni malaika hao wengine ni magubegube na uzuri wa Pompo haraka akaniweka ndani mie nikapata nafasi ya kuwa karibu karibu na yeye, akanipenda zaidi sababu nyumbani kwetu Tanga washamkubali wanamtambua na uzuri wake weshampa Baraka zote za mie Toto la kitanga kuishi na yeye. Tanga ni kwetu kule mapenzi yalikozaliwa. Basi mwaya mie nikastarehe nikajibidisha kwa shuhuli za kijungu jiko nikifua , nikipuguta deki, nikikosha vyombo nikiufwagia uwanja na pia nikijibidisha kujitwika shughuli za kufuma vitambaa, kudalizi na kupamba.


                   ###########################

            “Ninataka niunue Gari, Pompo aliongea na kunishitua siku moja tukiwa chumbani kwetu tumetulia tuli juu ya kitanda chetu chenye mahaba.

              “EboπŸ™„! Mwanaume we, mbona wanishitua?”


              “Ndio hivyo tena wangu, pesa nilizozitunza Benki zatosha kununua Tax.”


                “Kama una lengo zuri wangu mie ninakupa hongera, hiyo ndiyo njia ya mafanikio.” naliongea kisha nikanena tena.


                “Lakini wangu si ungelijifunza namna ya kuliendesha ilo Tax.” Nilimshauri Pompo.


                “Hainipi shida, kuna rafiki yangu pale Magomeni jinale Fred Chirstopher, amenipa Idea ya kunifunda namna ya kuiendesha Gari,”


             “Wanipa furaha Mume,we fanya utakavyo tupate mafanikio maishani mwetu.” Naliongea moyoni n'nacheka.πŸ˜†


              “Ipo siku ile nyumba yetu ndogo tunayoijenga Kigamboni itakamilika, tena…..” Pompo alinitizama kwa matabasamu.


            “Ongea wangu,” nalimsistizia.


            “Tena kwa nguvu za Mwenyezi Mungu sie tutalishusha horofa hapa Kigamboni,” pompo alinishitua roho yangu kwa maneno yale.😟


                “Wanishitua Pompo,” Naliongea domo bumbuwazi.🫒


               “Mungu atupe pumzi wangu,” Naliongea.


               “Ninaona mbali Pompo,” naliongea, Pompo akalivuta shuka la kitanda chetu, akanifunika nayeye akajifunika, tukawa ndani ya hilo shuka gubigubi tunatizamana.

          

        “Mbali sana, mbali kwenye mafanikio”, akanishika kiuno changu, nikampapasa usoni kwake, nikamsikiliza.


               “Ninaiona biashara, ninafikiri ipo siku nitakuja kufanya biashara kubwa huko ng’ambo; Dubai, South Afrika, Amerika, China na Japan.” Akanibusu😘😚 akanibusu midomoni mwangu na mie nikampokea kwa mabusu yake kimya nikamsikiliza.


             “Biashara itatutua, iwe isiwe, tutafanya mengi makubwa zaidi ili sie wawili tunaopendana tuzidi na kuzidia,” Maneno yale matamu yaliingia masikioni mwangu, akanitia hamu ya Mahaba. Aki! Mwanaume wangu anatamani na pia ananitamnisha mapenzi.


              “Ninakuombea mapenzi, ninakuombea mafanikio, wangu upite njia za salama, njia za salama ndizo zitakazo kufanikisha ufike pale tunapotarajia kufika.” Naliongea.


              “Asante wangu basi ujue kuwa mie ninakupenda sana.” Pompo aliongea.


               “Unishindi love, πŸ’• mie nakupenda zaidi ya sana,” Niliongea Pompo akanigawia mabusu yake, akazidisha na kuzidisha wawili tukawa hoi Bini taabani.


          ##########################


Basi miezi kadhaa kupita 'chai wa moyo wangu' alifanikiwa kuipata Tax nzuri ya kuendesha, akafundwa na huyo Fred Chirstopher rafikiye wa Magomeni, wangu akafanya kujibidisha tusikose tena pesa ya mbogamboga nyumbani, maisha yakaendelea tena uzuri wa maisha hayo, yakawa ni maisha matamu yenye unaafu, Mie shoga yenu Mamsapungo nikaona fahari isiyo na kipimo, nikajisikia sana, nikafurahia kupendwa, nikayapata mahita yangu yote, yaani raha na furaha, nimempata wa kunipenda tena yeye mwenyewe kanipenda, nina haki ya kujivunia mie ni mwanamke na mwanamke lazima nipendwe.


           Sasa shoga zangu ikawa siku moja mie nipo barazani nachambua chambua mboga ya harage kwetu twaiita Nguniani , nikitwanga twanga kipome au kwa kifupi karaga za kuchanganya kwenye Nguniani, nikatembelewa na ugeni nyumbani. kanijia huyu mwanamke anitishaye surani, mmh! kwa mwonekano wake si ningelimwita chizi mwenda wazimu, lakini aka! yatanikuta mie, nizibe mdomo wangu, sio kila neno kuropoka.


Itaendelea sehemu ya saba.


   

No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...