OBIMO CHETA
REMEMBER MY LOVE 💕
Sehemu ya tatu.
What!!?” Singa aliongea kwa sauti ya yenye msgangazo, Derila alitetemeshwa na hiyo sauti, akamshangaa Singa ambaye hakuwa dhahiri kuyapokea mawazo yake Derila.
“Una mimba? Mimba ya nani? Ni nani aliyekupa hiyo mimba?” Singa aliuliza maswali kibao, maswali ambayo yalimtoka kichwani mwake kama vile mwenda wazimu.
“Singa mpenzi wangu, ndio nina ujauzito, tena ujauzito huu ni wetu mimi na wewe, (mtoto ni wetu mimi na wewe) wewe ndio mbegu iliyosababisha mimi nipate huu ujauzito, mbona unashangaa mpenzi wangu, au haukutarajia kuwa ipo siku utaja kuitwa Baba?” Derila aliongea.
“Derila usiongee upuuzi huo, ulipaswa kuwepo shuleni muda mzuri kama huu, ulipaswa kuyapenda masomo wala sio mimi fukara nisiye na mbele wala nyuma, utaanza anzaje kuniambia ati una ujauzito wangu wakati mimi sikujipanga wala sikuwa tayari kupokea ripoti hizo, ripoti juu ya ujio wa mtoto huyo unayesema ni wa kwangu.”Singa hakutania, aliongea yatokayo moyoni mwake.
“Hivi Derila kwa hali hii kweli niliyonayo waweza kuniambia tunaweza kumtunza mtoto atakayezaliwa? Tizama mimi ni masikini, sio masikini tu, bali ni masikini wa kutupwa, sina ae, wala bae, na wewe ni mtoto wa Shule uliyefukuzwa Shule, nyumbani kwenu hawakutaki, umekuja na virago vyako nakushangaa, hata sijui itakuwaje!” Singa aliongea.
“Singa, usiseme hivyo mpenzi wangu, ujauzito huu sio kitu cha bahati mbaya, ni zawadi kutoka kwake Mola na riziki njema,mimi binafsi sikupenda kufukuzwa Shule, japo nakiri kwa kusema kuwa mapenzi ndio yamenisababishia hali hii, nimepoteza Elimu, ninajuta, wazazi hawanitaki nyumbani hawana haja nami, nipokee my love, nipokee mikononi mwako.” Derila alisihi.
“Siwezi Derila, tena siwezi kabisaa, siwezi kukubali ati nikupokee tuanze kulea mimba, mtoto akizaliwa atakuwa mzigo kwetu, bado sisi ni masikini, tena masikini wa kutupwa.” Singa aliongea maneno yaliyouchoma moyo wake Derila, hakuamini kama ni yule Singa wake wa moyoni, Singa aliyempenda pendo la kupendeka, Singa leo hii anaukataa ujauzito ati kwa sababu ya hali duni ya maisha, hivi je, watu hufanya kuukataa ujauzito ati kwa kisingizio cha umasikini?”
Hapana, yawezekana Singa amekunywa pombe aina ya Banana au amevuta sigara aina ya bangi, lakini ukweli wa mambo ni kwamba Singa hanywi pombe wala havuti bangi, aongeayo yamekuwa maneno yanayomshangaza sana Derila.
“Sikiliza Singa, usinifukuze mpenzi wangu, nionee huruma, katika shida na raha yatupasa tuwe pamoja, kama mwenyezi Mungu atatujalia kupata mtoto, tutamtunza mimi na wewe tena kwa moyo mmoja, kwanini wanitimua mpenzi? Tutavumiliana my love, maisha ni kuvumiliana yote haya yatapita.” Derila aliongea kwa upole.
“Sipo tayari Derila.”Singa alibadilika.
“Umejitakia, haukupenda kusoma uliwaza mapenzi na matokeo yake ndio hayo, tena sijajiandaa kwa ajiri ya matunzo ya mtoto atakayezaliwa, kama upo tayari kumtunza huyo mtoto kazi unayo.”Singa aliongea akitilia mkazo juu ya maneno ayanenayo.
“Derila alimwaga chozi la chini chini, amechanganyikiwa, masikini anakumbuka miezi kumi iliyopita walipendana mithili ya watoto pacha wasiotofautiana, walipendana na mapenzi ya dhati, walipendana sana, tena katika mapenzi hayo ni Singa ndiye aliyekuwa akirudiarudia kumwambia/ kumweleza Derila kwamba ipo siku watafunga ndoa yenye fahari ndani ya kanisa Cathorick, ipo siku watajavishana pete ndani ya kanisa Cathorick, ipo siku watajaishi maisha bora zaidi, maisha matamu, tena matamu kama asali, Mungu yupo, atawasaidia, kikubwa ni pumzi, uhai na maisha.
Inakuwaje leo Singa anaongea maneno yanayouchoma moyo wake Derila? Oooh! Masikini Derila anatoa machozi sio kidogo, ni mengi kama maji ya baharini.
“Nasema ondoka ndani ya chumba changu, sitaki tena kusikia hizo habari za ujauzito wako, nenda na urudi nyumbani kwa Baba na Mama yako ukawaombe msamaha, ujue na ujijue kwamba umekosea, tena kosa ulilokosea sio kosa mtoto, ni kosa kubwa, umeamua kujikatishia masomo, hujatambua umuhimu wa elimu.” Singa aliongea kwa hasira.
“Singa, ninakupenda sana mpenzi wangu, tumetoka mbali, hadi hapa tulipofika sio padogo, tuna safari ndefu mbele ya maisha yetu, kwanini unanitendea hivyo mpenzi, nikumbuke mpenzi, nikumbuke kama ninavyokumbuka nimekubali kufukuzwa Shule, nimekubali kufukuzwa nyumbani, lakini sio kufukuzwa na wewe ninayekupenda.”
“Sitaki kukusikiliza, ondoka.” Singa aliongea kwa sauti kuu, wakati huo huo tayari alikwisha kusimama pale kitandani alipojilaza, akavikusanya virago vyake Derila akavitupa nje, ajabu ya kushangaza akamtimua mpenzi wake kama vile mwizi, Looh! Mapenzi haya jamani.
Derila alilia sana pale nje ya Getto la mpenzi wake Singa, alilia masikini, alilia akimsihi Singa afungue mlango wapate kuongea mawili matatu, wayaweke mambo sawa, wasameheane, wajadili kwa pamoja, lakini Singa hakujali kuhusu hilo, yeye aliufunga mlango na kujilaza kitandani, amenuna mnuno usio wa kawaida, amenuna kama vile kuna mtu aliyemnunisha.
“Nifungulie mpenzi, nifungulie tafadhali, ninakupenda sana Singa, wewe ni wangu, wewe ni wa kwanza kwangu na wewe ni wa mwisho kwangu, ninakupenda Singa, kwanini waniumiza kwa sababu ya ujauzito.”Derila alilia, Singa hakujali, tena alitia pamba masikioni mwake.
************************
Derila alirudi nyumbani kwa Babaye na Mamaye Usa River, alirudi kuomba asamehewe, alirudi kuomba nafasi nyingine ya kuishi tena, hana pakwenda, mpenzi wake aliyekuwa akila na kulala naye leo hii amemtimua ati kwa madai kwamba hakujipanga kwa ajili ya huo ujauzito, bado hajaweka mambo sawa, umasikini ni kikwazo katika maisha yao.
Ingawaje riziki ugawa Mola, Derila amemwambia Singa ya kwamba watashirikiana, watasaidiana na pia wataja yaweka mambo sawa, lakini Singa amekuwa mwamba, anatumia nguvu bila kujali sauti na kilio cha Derila.Alipofika nyumbani Derila alikutana na kwazo lile lile la hapo awali, nduguze bado hawakumtaka, wazazi wamemfukuza kwa madai ya kuwa amewafedhehesha, aibu hiyo iwe funzo kwake, na funzo waliloliona wao ni kumfukuza ili akatangetange na dunia, ulimwengu umfunde kwa sababu asiyesikia la mkuu huvunjika guu, asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, Dunia hadaa, ulimwengu shujaa.
Derila akapata wazo, siku iliyofuata aende kumtembelea tena Singa ambembeleze, hajapata kumwona Singa amekasirika, ndio amemwona kwa mara yake ya kwanza amekuwa na hasira zile. Ile anafika tu akaambiwa na Baba mmwenye nyumba ambaye Singa alipanga chumba kimoja kwake, akaambiwa kuwa Singa ameondoka, ameenda nyumbani kwa Babaye na Mamaye Maasai Land Loliondo, hana matumaini ya kurudi tena Usa River, vyombo vyake vikuukuu ameviuza, kitanda chake kikuukuu amekiuza, vyote alivyomiliki amemuuzia Baba mwenye Getto lake Singa. Yallah! Oooh! Mungu wangu! Derila alilia sana, alilia akijionea huruma yeye na moyo wake, alilia akijuta, alilia masikini, hata hivyo kilio chake hakikumsaidia zaidi ya kumnyima furaha.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment