Sunday, July 6, 2025

OBIMO CHETA

 OBIMO CHETA

(MY LOVE REMEMBER).



Siku Derila alipokutana na Singa, ilikuwa ni siku nzuri, siku ya kusheherekea sikukuu ya Christmass,🌲🎄⛪ kama tujuavyo tena sherehe ya Christmass ndani ya mji wa Usa river, unoga na kunogela, hunoga haswa, hupendeza na kuvutia. Christmass ni sherehe inayopendwa na Wachaga, Wameru, Waarusha, Wamaasai na Wapare, kila mwenye nyumba yake humkaribisha jirani, ndugu au jamaa wapate kufurahia sherehe pendwa ya Christmass, kila mwenye nacho hukitumia kwa furaha pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.🎁🎅🍝🍜🍱

        Siku njema huonekana asubuhi, hakika siku ilionekana, kila mja alikuwa katika pirika pirika zake za kila siku ili apate kujitafutia riziki , riziki popote, Mwenyezi Mungu hugawa. Sokoni ndio ulikuwa mpango wa kila mpenda Christmass, basi siku hiyo Derila alitumwa na wazazi wake kwenda sokoni japo apate kununua hiki na kile, waandae maakuli, waandae mapochopocho, wale wao na jirani zao, katika kuchagua chagua vyakula alivyoagizwa alete kwa ajiri ya Christmass, mara ghafla macho👁️👁️‍🗨️ yake Derila yaligongana na macho ya kijana Singa. Wakatizamana sio kwa sekunde, wala sio kwa nukta bali ni kwa muda mrefu ajabu.🕦

        “Vipi dada mbona umezubalia kule?” Muuza mchele alimuuliza Derila huku akinyosha kidole 👉chake kuelekea eneo ambalo Derila alikuwa akitazamia.

        “Aaah No! Kawaida kutizama.” Derila aliongea.

        “Poa, sasa utachukua kilo ngapi za mchele dadangu?” Aliulizwa swali.⁉️

        “Kilo sita ⚖️pamoja na viungo vya pilau.” Derila alimjibu muuza mchele ambaye muda huo alianza kupima zile kilo sita alizoambiwa apime na mrembo Derila, mrembo ambaye wakati wote huo macho yake yalitizama mbele sehemu ambayo alikuwepo yule kijana mzuri machoni.💕

        Yawezekana walipendana, tena walipendana sio machoni tu, bali pia moyoni, mawazoni na fikrani, yote kwa sababu Derila aliyapenda macho ya yule kijana aitwaye Singa. Singa pia aliyapenda macho ya Derila, Derila aliipenda midomo yake Singa. 👄💋💄Derila aliyapenda meno yake Singa mara ile alipoyaona yakichomoza kutoka kwenye tabasamu la midomo yake, Singa pia alivutiwa na kuvutwa na meno mazuri yaliyopangiliwa ndani yamdomo wake Derila, walitazamana, nywele zao ni za asili, nzuri za Kiafrika, safi zilizokolezwa mafuta ya asili, zinavutia na kupendeza machoni. Mara baada ya Derila kununua mahitaji yake yote kutoka kwenye kile kigenge, alitembea hatua mbili tatu akimfuata yule kijana aliyeyapendeza macho yake, hapakuwa na umbali sana, mita chache tu akamfikia wangali bado wanatizamana.

        Singa kijana mweusi wa Kiafrika, yaani mweusi tii kama chungu, ana meno meupe mithili ya maziwa safi, ni mrefu kama mlingoti, kumbe ni Mmasai kwa kabila, mwembamba japo yeye havai kama wanavyovaa vijana wengine wa Kimaasai. Kastaarabika, anajitambua kifikra na kiakili, ndio maana anaenda na wakati pamoja na mazingira yanayomzunguka. Derila yeye ni binti wa kichaga, mweupe pee, mweupe wa rangi ya chungwa lililoiva sana, hiyo ndiyo rangi ya Wachaga, sio mrefu wala mfupi, ni wa Wastani, sio mwembamba wala mnene, ni wa wastani.


        Wakati Derila yupo kidato cha nne amekwisha kuwa mtu mzima, Singa hana lolote la kufanya yupo yupo tu, darasa la saba ndio elimu yake, amemaliza miaka saba iliyopita, tena alifeli, nani wa kumsomesha? Hakuna wa kumsomesha, babaye Singa alimtaka ajiunge na kikundi cha Morani, wakateke na kuiba wanyama (cattle raiding) ndio, alijiunga akiamini kuwa iwapo angelileta nyumbani kwao kundi dogo la ng’ombe, mbuzi au kondoo,🐄🐐🐏 wangeliupunguza umasikini uliotawala nyumba yao. Haki ya Mungu umasikini mbaya, mbaya tena mbaya zaidi. Walilia njaa wale wanafamilia, tena njaa isiyokoma, pesa lilikuwa nitatizo, tena tatizo la dunia ndio maana babaye alimtaka mwanaye aende Cattle raiding, akawateke na kupora mifugo, babaye alijiaminisha kuwa kufanya hivyo kutapunguza umasikini unaowanyanyasa. Babaye alitamani achekecheke kidogo nayeye aonekane kuwa ni mtu mbele za watu, yote kwa sababu kidogo ambacho mwanaye atakileta nyumbani, hicho ndicho kitakachompunguzia njaa na kiu ya pesa.

        Singa alienda? Ndio, alienda, alienda kupora wanyama, lakini asilolijua lilimsumbua, matokeo yake alijuta, tena alijuta juto la mjukuu naye aliapa kamwe asingelirudi tena. Walipora? Ndio, walifanikiwa kupora wanyama, tena walipora vizuri sana. Wakiharakisha kuondoka, walishtuka wakivamiwa na polisi waliokuwa bize wakiwarushia risasi. Duh! Mbona mkosi, duh! Mbona Singa alishuhudia Morani wenzake wakidondoka chini na kufa kwa pigo la risasi.


        Singa alichoropoka na kukimbia mbio za farasi, aliponea chupuchupu kuuawa au kutiwa mbaroni, hata hivyo alimshukuru Mungu kwa wokovu aliomtendea, haikuwa jambo rahisi na jepesi sana kushinda kifo cha risasi, alikimbilia msituni, alikimbilia porini, hakutaka tena kurudi nyumbani kwa babaye na mamaye waliomsubiria kwa matumaini ya kupata kile wanachoamini kuwa kingeliwapunguzia njaa na umasikini nyumbani kwao.


        Singa hakurudi nyumbani kwao Loliondo, alikimbilia Arusha mjini, huko nako hakukaa sana zaidi ya kwenda katika Wilaya ya Meru, ndani ya mji mdogo wa Usa River, Basi huko Singa alijibidisha na shughuli ya kusomba takataka za pale sokoni, naye akalipwa ujira kiduchu. Hakuchoka kubeba mizigo inayoingia sakoni, bado malipo aliyolipwa kiduchu, akivumilia tu, akivumilia kazi hizo nzito kuliko ile ya kuiba mifugo ya Wamaasai wengine.


Itaendelea

Saturday, July 5, 2025

MTEKAJI

 



MTEKAJI.


       Ilikua yapata saa sita usiku,⌚🌆 siku hyo niliwai kurejea nyumbani kwangu Airport🛬  maeneo ya Kipawa nilifanya kurejea ghafla sababu nilikua nimeisahau Documentary 📃muhumu ajili ya Interview niliyopangiwa kufanya usiku ule mbele ya Mabosi wangu wapya yaani Waasia watokao Japani kwa ufupi nilikua nasaka Ajira kiprofeshono mimi ni Mhasibu.💰🖥️


         Nilipofika nyumbani niliufungua mlango wa Sebuleni kwa kutumia ufunguo 🗝️🔐wangu private baada ya kufungua mlango nikaurudisha kwa bamizo lililotoa sauti iliyolia 'mbaaa'. Taa 💡 ya sebuleni ilikua ikiangaza Jerome mume wangu alisahau kuizima, sikujali. Nikaliita jina la mume wangu Jerome karibia mara tatu🔊 lakini hakuitikia, sikutia hofu moyoni nilijua keisha lala.😴 Nikafanya kuelekea chumbani kwetu, Master.🛌


     ''Daring Jerome.'' 😘Niliita tena nikiwa ninatembea kwa madaha pale ukumbini. Nisilolijua kama usiku wa kiza kumbe pindi ninamwita mwenzangu mwenzangu alikua katika harakati za kimvua nguo ili amlale mwanamke nisiyemjua Wala nisijue wapi alipomtoa. 


Alipoisikia sauti yangu haraka haraka akili zilimcheza akafanya hima kuchukua mabranket na mashuka akamfunika yule Malaya aliyekua hoi amelala 'fofofo'🛌 baada ya hapo akaichukua mito na kumfunika vizuri yule Malaya ambaye nakili kwa kusema nilipoingia chumbani sikumuona bali nilimkuta mume wangu ameketi kitandani kamziba yule Malaya nisipate kumuona.😔


     "Maya mbona umerejea mapema si uliniambia utalala kwenye interview?" Aliniuliza.Aliniuliza ila mtimani sikupenda kwanini ninamwita alafu anikaushie kibubu🥺🤫


      Nikamjibu "Oh Daring Kuna Documentary muhimu zinahitajika kwenye lnterviwe nimeziacha kabatini." Wakati huo nimeketi juu ya mapaja ya mume wangu aliyenikumbatia kwa huba maridhawa.👩‍❤️‍💋‍👨💘


     "Ah! Usijali Maya  waweza zichukua." Aliniambia lakini ghafla hamu ya kufanya mapenzi na mume wangu Jerome ilinivamia. Kwa pupa nikaanza kukitoa kikoti nilichokivaa nikakitupa juu ya kitanda, nikavamia lips za mume wangu Jerome na kuanza kunyonya ulimi wake kama Sina akili.💋👩‍❤️‍💋‍👨

    "Mume wangu nataka tufanye mapenzi kitandani." Nilianza kudeka.

     "Maya my Love ungefanya kwenda Interview kwanza kesho ukirejea tutainjoi balaa." Alinipooza.
    

"Kwahiyo mpenzi unataka nizidiwe na kuchepukia huko kwenye interview?" Nilimnunia. 🛌☺️


     "Hapana my Queen 👸 naomba Leo tubadilishe mazingira hivyo basi twende tukafanyie bafuni si unajua raha ya maji💦 mapenzini." Alinikubalia akanibeba juu juu kama furushi la pamba na kunikimbiza bafuni ambako mchezo wetu wa ngono ulipamba moto🤡

....................

Tulipomaliza kuifurahia ngono Jerome aliniomba nielekee Jikoni kumwandalia kikombe cha Kahawa. ☕Yeye alitangulia kuelekea chumbani. Mie kufika Jikoni nilipigwa na butwaa‼️ : 'eeh! Jamani kuna mwanamke ameketi chini karibu na makabati ya vyombo kakunja miguu na kujishika tama.' Niliogopa, nilishtuka na kuingia hofu 🥺😶‍🌫️🫥nikafikiria yamkini mwanamke huyu ni mlozi au mwizi ama mtu mbaya.

    "Wewe ni nani ndani ya Jiko langu?" Nilimuuliza nikiwa nimeshika mwiko mzito ili akitaka kunidhuru nipambane naye, kama Waswahili wanavyosema Hamadi kibindoni siraha mkononi. Hakunipa jibu zaidi ya kunitazama.

     "Ninakuuliza tena wewe ni nani na pia unatafuta nini ndani ya nyumba yangu tena umeingiaje humu?" Nilimuuliza wakati huo Jerome alikua ametoka kwa kasi kule chumbani kwetu na Sasa amekuja kule Jikoni anashangaa. Nikamgeukia Jero na kumtwanga swali:

     "Jerome huyu ni nani na ameingiaje humu ndani?" Jerome alinisikiliza kwa makini bila kuonesha hofu Wala wasiwasi.


      "Simjui mtu huyu." Jerome alinijibu.


     "Una hakika kwamba haumjui mtu huyu mume wangu?" Nilimuuliza Jerome.⁉️


     "Aki ya Mungu! Ni mara yangu ya kwanza kumuona." Alinijibu akaongea tena: "Tufanye kupiga simu Polisi 👮🚓tuwape taarifa kwamba tumevamiwa na mwanamke asiyejulikana.

      
      "No no no! Tusifanye kuharakia huko cha msingi tumhoji na kumjua zaidi." Nilitia wazo.


       "Hapana Maya, huyu sio mtu nzuri." Jerome aliitetea kauli yake. Akafanya kuchukua simu 📱 yake awapigie Polisi haraka nikamzuia.


     "Usipige Jerome, usipige tafadhali." Alinisikiliza. Tukamgeukia yule mwanadada aliyeketi pale chini sakafuni tama shavuni tukaendelea kumhoji. 


     "Tueleze, umeingiaje humu ndani?" Nilimuuliza, taratibu aliinua USO wake na kututazama naye akaufungua mdomo👄 akajibu.



     "Sifahamu na sielewi nimeingiaje humu ndani mimi binafsi ninajishangaa na kujiuliza niko wapi jamani?!"‼️ Alijibu mie moyoni💜 nikajisemea yawezekana mwanamke huyu amepatwa na matatizo makubwa, yapaswa kumsaidia.



      "Ok. Amka twende ukaketi sebuleni. Nilimshika 🤝mkono nakumuinua pale alipoketi tukaelekea  Sebuleni.


     "Mume wangu mwandalie huyu Bi.Dada maji, pia huyu Bi. Dada atalala hapa hapa." Niliongea baada ya kuketu sofani pale sebuleni.

      "Nini!? Alale hapa hapa mwanamke tusiyemjua." Jerome alipinga.


     "Jerome uwe na huruma sasa hivi ni saa saba usiku tena huyu Dada hajui yupo wapi? Kwahiyo unataka aondoke aende wapi?" Nilimuuliza Jerome.


      "Popote Kambi,🏡 lazima aondoke." Aliongea.


     "Hawezi kuondoka hadi kesho na mimi muda huu ninawai lnterview kwahyo mgeni wetu atalala sebuleni ninaomba umjali na kumlinda." Niliongea wakati huo tayari nishachukua Documentary zilizoitajika kwenye Interview, nikaufunga 🚪mlango wa sebuleni na kutoweka. 👣Nimewaacha Jerome na Dada mgeni pale Sebuleni tena sikua na wasiwasi juu ya mume wangu kumtaka kingono yule mgeni maana ninamjua Jerome wangu hanaga tabia hiyo ni mtulivu na mwaminifu.


*........*.........*......*.....

      "Unataka kuniambia haukumbuki ni wapi ilipotoka na wapi hupo kwa Sasa? Jerome alimhoji yule Dada mgeni na mpotevu.


      "Sikumbuki kwa kweli lakini mara ya mwisho Ninakumbuka nilikua Maisha Club nikinywa pombe, nikicheza muziki na baada ya hapo nilihisi kizunguzungu kunikamata nikalala usingizi wa pono."😪 Yule Dada mrembo alijieleza.


      "Naweza kukapa maji 💧unywe." Jerome aliongea.


     "Bila shaka waweza nipa." Mdada alimjibu Jerome. Jerome akaelekea Jokofuni na kumimina maji baridi lakini pasina yule Dada kumuona Jerome au kujua jambo lolote Jerome alitoa kikopo chenye vidonge 💊vya usingizi akachukua kidonge kimoja na kukidumbukiza ndani ya bilauri ya maji🍸 Kisha akaelekea kumpatia yule mrembo.


       "Karibu mrembo, karibu maji." Alimkabidhi yule mgeni ile birauli ya maji mdomoni amejaa tabasamu. Mrembo yule aliyapokea kwa shukrani lakini kabla hajayanywa aliyatazama sana yale maji na kushituka 😶😶‍🌫️😱kidogo.

        "Jesu!" ‼️Aliyakodolea macho yake maji.

       "Tatizo nini?"Jerome alimhoji.


      "Kumbukumbu zangu zinarejea." Alianza kurejewa na kumbukumbu za usiku alipokua Maisha Club.


      "Hiki kidonge ndani ya maji........." Aliongea akiyakodolea macho maji yaliyokilainisha kile kidonge alichokiona ndani ya maji.

      "Usiku wa Leo tulikua tunacheza muziki 🕺💃pale Maisha Club mimi pamoja na wewe. Ukanitilia kidonge, nilipokunywa tu nilianza kusinzia." Kumbukumbu zilimrejea.


      "Sasa wewe si ni Malaya?! Embu ondoa ushamba njoo chumbani tufanye ngono." Jerome aliongea, akadamka pale alipoketi na kuelekea pale alipoketi yule Dada mgeni.


     "Pumbavu wewe,😬😡 shindwa kabisa nitamueleza mkeo na pia nitaenda Polisi kuripoti" Yule Dada alijitetea 


      "Una ushahidi!?"Jerome alimuuliza yule Dada. Dada wa watu hakuwa na jibu tosha yeye akajidamsha pale alipoketi tayari kuanza kuondoka kutoka ndani ya ile nyumba hata kabla hajatoka alimsikia Jerome akitamka.🗨️

      "Wewe ni chombo tu tena chombo cha kufurahisha wanaume." Mrembo wa watu hakuyajali maneno ya Jerome alichofanya yeye ni kuondoka kiustaarabu.

*.....*.......*.......*


Asubuhi mapambazuko mie Maya nilirejea nyumbani kwetu tena sikumkuta yule Bi. Dada niliyemuacha usiku wa Jana akiwa pamoja na Jerome mume wangu. Jerome aliniambia yule Dada alipata kumbukumbu zake na kutambua pahali alipotoka. Kwa ufupi yule Dada aliondoka nyumbani kwetu.

     Basi mie huyo nikakusanya kusanya nguo chafu za mume wangu Jerome nikaziloweke na kuanza kufua maana  ni wajibu wangu mimi kama mke katika nyumba. Katika kukagua kagua ndani ya mifuko ya Suruali za mume wangu ili niondoe vilivyomo kama vile pesa💸 au chochote muhimu  kilichomo, nilishtuka baada ya kuikuta Ticketi ya kuingilia Maisha Club imetulia na kujaa tele ndani ya mifuko ya mume wangu. Nikaiangalia ile Ticketi mara mbili mbili nishindwe kuimaliza.

        "Jerome!" Nilimwita mume wakati huo nimeificha ile Ticketi asipate kuiona.

      "Laazizi🥰" Aliniitikia na kutoka kule sebuleni alikokua akitazama marudio ya Dabi ya watani wa jadi yaani Simba na Yanga.⚽

     "Hivi karibuni umeendapo Club?"♣️ Nilimuuliza.

     "La,asha!🙂‍↔️ My Daring. Kwanini umeuliza." Alinitazama bila hofu ilihali ananisoma  na kutaka kuijua hofu yangu.

    "Ah! Nimemiss tu kwenda Club pamoja na wewe sweet ❤️" nilimficha ilikuuficha wasiwasi wangu.

     "Tufanye kwenda Leo My love🥰." Wangu alinibembeleza.

      "Kwa Leo haitawezekana Huba langu si unajua Leo natakiwa kwenda kukabidhiwa Ofisi maana Interview niliyoifanya jana ilienda poa." Niliyaficha yangu yatiayo hofu juu ya Jerome.


    "Sawa Laazizi utaniambia ukiwa tayari." Aliongea kwa tabasamu. Mie huyo nikaelekea kufua kumbe mtimani Kuna fundo☹️ limenikaba. Eti jamani nirejee usiku wa Jana kisha nikute mlango umefungwa ajabu nimkute mwanamke mwenzangu Jikoni kalewa🍾🥃 hajielewi!? Hapana. Baya zaidi nakutana na Ticketi ya kuingilia Club kubwa yenye hadhi ya nyota✨ tano.😢 N'tangoja mie👌na stress zitanipanda kwa juu💓.

""""""""*""""""""""*"""""*

Jioni ilipowadia mie nikiwa natembea Barabarani 🛣️🚸kuelekea kule Ofisi niliyopangiwa, maana nilikwishafauru Interview yangu, kidogo nilishtuka baada ya mtu kunigusa bega langu la mashoto nyuma mgongoni. Nilipogeuka kumtazama, macho yetu yakagongana👀 

       "Aah!" ☺️Nilitabasamu mara baada ya kukutana na mdada ambaye usiku wa Jana nilimkuta ameketi Jikoni haelewi na hajielewi. 


     "Habari Yako Dada!?"👊 Alinisabahi na mie kwa mbwembwembwe nilimuitikia.

    "Njema tu!"👍 Akaongea:

     "Niite Zendaya. Samahani ile siku uliponikuta Jikoni kwako sikuweza kujitambulisha maana nilikua sijitambui."

    "Haina shida waweza kuniita Maya Nina furaha uliporejewa na kumbukumbu ukakumbuka kurudi nyumbani kwako."

     "Asante kwa upendo wako." Alinishukuru kisha akaendelea kunena.

     "Dada Kuna jambo nataka nikueleze kuhusu mumeo, kwa kweli anatabia chafu sana.😾

       "Tabia chafu!!!? 😼Embu nieleze kwa urefu zaidi." Nilikua na shahuku 🤭😋ya kutaka kujua zaidi.

       "Kikubwa usijekunifikiria mie kama adui aliyekuja kuiharibu ndoa Yako, hapana Sina lengo hilo ila tu nikuambie mumeo anatabia chafu kwa kweli." Aliendelea kueleza.

     "Ni ukweli usiopigika kusema kuwa usiku wa Jana nilipoteza kumbukumbu lakini nyuma ya pazia mumeo anahusika kwa asilimia mia moja.💯 Tulikutana Maisha Club tukala, 🍔tukanywa 🍻na kucheza Muzik🎼 lakini katikati ya Muzik na ngoma mumeo alinitilia dawa ya usingizi hatimaye nilijikuta nimezima na kuzinduka nikiwa nimelala juu ya kitanda chenu hapo ndipo nilipata mwanya wa kutangatanga na kujikuta naangukia Jikoni ulikonikuta nimeketi " Zendaya alinishutua kwa yale maelezo.

    "Ulinipigania nisiondoke usiku wa Jana ajabu mumeo alilazimisha kuita Polisi ninashukuru ulinilinda. Ulipoondoka aliniletea maji 💦ambayo ndani yake nilikuja kugundua yana kidonge kidogo  cha usingizi ambacho kilikuja kunipa kumbukumbu ya matukio yaliyofanyika Jana. Kwahiyo Dada uwe makini na tabia za mumeo." Aliongea kwa hisia.

      
     "Mungu wangu Ina maana mie nahangaika kutafuta mkate 🥪wa Kila siku alafu mume wangu Jerome anaenda kusaka Malaya kwenye vilabu vya pombe"  Niliongea kwa uchungu mkuu.

       "Dada yangu unahitaji kupata vithibitisho sababu mumeo Jerome kila siku huja Maisha club na kuopoa madada poa wapya wapya tena wanaojiuza." Zendaya aliongea.
     
      "Jamani !! Jamani 😿! We Zendaya acha kunitisha mie 😢" Nilianza kuogopa.

   "Nina Ombi moja siku ya Leo omba ruhusa kazini ifikapo usiku nipigie simu tukutane Maisha Club ili ujionee uchafu wa mumeo. Wakati wewe unafanya kazi za usiku kumbe yeye kazi yake kufucky Malaya. Dadangu UKIMWI upo usije ukaangamia bure😁." Zendaya aliongea na kuagua cheko.😅😂🤣


     "Vizuri sana Zendaya, mume wangu anajifanya mtakatifu kumbe hamna kitu pale" Nilimuunga mkono Zendaya.👊👏

*.........*.........*........

Usiku wa siku ile niliaga kazini kwa kudanganya kwamba kichwa kilikua kinanisumbua ruhusa yangu ilikubaliwa ilimradi nilikua bukheri mzima. Nilipotoka tu Ofisini nilimpigia simu Zendaya:

 ' Shogangu tukutane Maisha Club' 


Baada ya kumpigia simu Zendaya nikamkumbuka kibaka mmoja hapa mitaani kwetu, muhuni asiyestafu uhuni wahuni wenzie wanamwita 'Baasha mchovu' nikamweleza Baasha mchovu 'Kuna mchumba nataka kukukabidhi we jiandae tukutane Maisha Club mida hii hii ya Jua kuzikwa'  🌄 Baasha  akafurahia.😉

Mie huyo na kiherehere changu nikawai na kuwa wa kwanza kufika Maisha Club yaani lengo likiwa ni kumfumania mume. Zendaya na Baasha walipowasili Moja moto na Moja baridi zililetwa 🍻🍺na kutandazwa juu ya Meza yetu. Hapo kumbuka tumeketi pamoja na kujibanza upenuni kwenye kiza ambacho hakuna Mtu ambaye angeweza kutuona ilihali sie wenye macho ya popo tuliona Kila kilichoendelea mwangani.

.
     Kama zari ☺️ Jerome aliingia Club akajiketisha mbele ya Caunta na kuagiza manywaji ayapendayo wakati huo huo Muzik 🎷🎶uliendelea kutema sauti.za burudani, mabanati na warembo walicheza kuifurahia ile siku. Wenye macho tulimuona Jerome akiongea na mrembo mmoja nzuri wa kuvutia walipomaliza maongezi walijipeleka katikati ya dimba la Muzik hapo ndipo Zendaya akamwambia Baasha mchovu Kuna taa💡🏮 ya hatari inawaka mbele ya yule Binti.

       Pasina kupoteza muda Baasha mchovu alisogelea mbele ya kaunta angarau asipitwe na matukio yanayomhusu yule mwovu Jerome. Kama alivyohisi Zendaya hakukosea Jerome alionekana akikitoa kikopo chenye rangi nyeupe na kutoa kidonge kimoja👍💊 ndani ya kile kikopo cheupe kidonge kile alikirushia haraka ndani ya bilauri yenye Juisi aliyokua akiinywa yule binti aliyekua akiyarudi mapigiti.

     Kumbe Baasha mchovu alikwishaona lile tukio akajipanga akiwa na dawa ya kumvuruga Jerome pamoja na juisi safi mkononi. Akachanganya na kuyakoroga yote kwa kasi ya ajabu akaelekea pale ilipo birauri yenye Juisi ya yule Binti akaichukua na kuimwaga chini pasina yule Binti kuona. Basi Jerome kuona vile alipigwa butwaa.🤔

     "Nini wewe! Umetumwa Nini?" Jerome alimpigia Baasha mchovu ukelele lakini Baasha alikua na mbavu zilizopanda juu na misuri iliyoshiba tofauti na Jerome ambaye alikonda na kutia huruma kama bati lililoliwa na kutu.

         "Embu kunywa hii juisi🍹 pasina ubishi." Kitendo bila kuchelewa Baasha alimywesha Jerome ile juisi iliyotiwa dawa ya kumvuruga kichwa na kumpotezea nguvu za mwili.

      "Umeninywesha Nini?...... Umeninywesha Nini!?..... Kwanini umeforce kuninywesha?"  Jerome alianza kuvurugwa 

   "Mimi sio semaji semaji wako yule pale anakuja." Baasha  mchovu alitupungia mkono ishara ya kumfuata maana kazi ya kumuingiza nyoka pangoni ilitimia. Mie na Zendaya tulifuata pale aliposimama Baasha na mume wangu Jerome.


     "Maya my Daring....." Jerome aliongea kwa kutetemeka 🫥😰🤯mara baada ya kuniona nimesimama pamoja na Zendaya.🧍‍♀️🧍‍♀️

    
     "Jerome mie Maya nahangaika kufanya kazi kwa bidii ili wewe mbaba ule, unywe na kuyafurahia Maisha kumbe wewe mwenzangu kazi yako ni kutafuta Malaya, kuwapeleka nyumbani Kisha kuzini nao juu ya kitanda tunachotumua kulala?😿 " Nilimuuliza macho kayatoa pima👀 akitutazama kwa zamu. 


      "Samahani Maya nitajieleza mpenzi...... Tafadhali sana nisamehe." Kichwa chake kilivurugwa Sasa akawa kama teja mlevi.


     "Sina haja ya kusikiliza maelezo yako labda ujieleze kwa huyo mume niliekutafutia anaitwa Baasha mchovu." Mie na Zendaya tulianza kuondoka.


     "Maya mke wangu..... Maya wangu..... Maya" Aliongea japokua sauti haikumtoka vizuri dawa ilianza kumlevya.


        "Wewe ni chombo tu,chombo Cha starehe." Baasha mchovu alimwambia Jerome, akamkumbatia yule dhaifu aliyevurugwa akampiga mabusu👨‍❤️‍💋‍👨 mfululizo shavuni.


      "Tuondoke my Baby." 😍Baasha mchovu alimwambia Jerome ambaye macho yalimtoka pima asielewe kamchezo alikochezewa.


******..........*****

TCHAO

******.......*******
     

      


        

MWENZENU N'SHAPENDWA.

 MIPASHO YA MAMSAPU

 

MWENZENU N'SHAPENDWA 


(PASHO LA KWANZA)


Sehemu ya pili



Nyonyo👌pale tulipokomea.

              Nshapendwa na yule anayejua kupenda, yule anayejua nini maana ya upendo mapenzi na mahaba, n’shapendwa na yule aliyenikuta hoehae sina mbele sina nyuma. Leo hii ukija Kigamboni kwenye mjumba wetu wenye horofa tatu mwaya utanikuta nimetulia tuli kama Dhahabu safi mgodini, najibidisha kusuka ukindo (mikeka) kufuma vitambaa vya mezani, kudalizi, kusoma vitabu au kuandika Hadithi, kupika na kupakua kumpeti peti wangu wa rohoni wangu anayenithamini anayejali na kunijali anajua maana ya mwanamke thamani ya mwanamke na kadharika.


Basi shogangu tuendelee.

       Yeye keishanijua na mie n’shamjua mapungufu yangu na mapungufu yake kwa pamoja tunayaweka mezani tunayatatua, sie sio watu wa kulumbana ovyo, 🧨🥵sie sio watu wa songombingo vibweka na vituko, sie sio watu wa kupishana kauli, amani yetu haipimwi kwenye mizani ⚖️au kwenye vibaba hayo ndiyo  mapenzi mapenzi kuvumiliana, mapenzi kungojeana, kusaidiana na kubebeana mizigo ndo’ maana kukwambieni mwenzenu n’shapendwa kan’penda mwenyewe. Aliyen’penda namshikilia hadi tufike Mbinguni, ya kwetu mapenzi hayadodi,hayavundi, si ya kwenu yanavunda na kuvurunda? Teeh teeh teeh😄 (Nacheka mie) 


       Babu! Hilo shombo mnuko mie wapi na wapi.
Basi mwaya maneno mengi yala vitendo, mie sio muongeaji sana, mie ni mtu wa vitendo zaidi acheni ninengue baikoko 🥁 ngoma ya kitanga, acheni nikate viuno vyangu feni kwa baikoko ngoma ya kitanga. Mie hapa sishindwi, mambo ninayaweza ndo’ maana Babu haniwachi, Babu yenu kalewa kwangu, karegea kwangu na kama ni kufa basi atafia mikononi mwangu kwa haya machezo wacha tutoke ngoma droo. Teeh teeh teeh😘🤣😂 nacheka mie niliyependwa.


         Simbagui hanibagui kama wahenga wasemavyo “Mapenzi hayabagui hayachagui, kupenda mpende yeyote hata kama ana kilema.” Basi natabasamu😋😊 moyoni, Mpopo wangu mie hajanibagua kama hao waso yajua mapenzi. Hao ambao ili wakupende sharti waijue elimu yako tena elimu yenyewe iwe ile ya Madgree, Maproffes, Madoctor na maPHD, Mmmh! (nimejishika tama) Shoga kwa hali hiyo sie ambao hata elimu ya vidudu na chekechea hatujaigusa tufanyeje sasa? Au ndo’ Mungu kaandika, ati’ “Waso na elimu wasipendwe?” Nijibu shoga hilo nalo swali. Mmmh! (naguna mie) mmmmh! Makubwa, madogo yana wadogo zake.🫣😶‍🌫️🙈

          Wapuuzi hao ili wakupende sharti wavijue vyeo na kazi yako tena iwe kazi yenye mshahara mnono mnonozi na posho nzuri, sharti waijue dini yako, sharti wakuchague kutoka kwenye kabila lao, rangi yao, lugha yao na utaifa wao baya zaidi wapuuzi hawa wanahakikisha kuwa hauna ulema au ulemavu, wowote ule, kasoro zozote zile usiwe nazo shogangu. Mmmh! Haya mapenzi ya kuremba na kurembua naona kinyaa na kutapika🫢🥱🫣, haya mapenzi ya kupotezeana muda naona kichefu chefu na kutapika.

      Mie nazidi kujiuliza ndani mtimani, hivi hadi weye shogangu kufikia hapa ulipofika wapuuzi hawa wamekuwezesha wapi? Wamekusaidia kwa lipi mwaya?⁉️  Wamelikupigania weye hadi upate elimu vyeo na mshahara mnono? Mwaya mbona wanakupangia masharti kwenye maisha yako weye? Ajabu shosti! Kumbe hawajui kuwa weye shogangu umetaabika sana kufika hapo ulipofika, kumbe hawajui kuwa ni Mungu tu ndiye aliyekufikisha hapo ulipofika. Aki! Nyonyo kama wangelijua kwamba umepitia magumu maishani mwako kamwe wasingelikuwa mstari wa mbele kukupangia majukumu uso weza kuyabeba. Teeh teeh teeh 😂😂Shogangu watemeni watu hao wakanyageni na tena msiwape mioyo yenu.

Waangalieni watu hao kwa jicho la tatu wangalieni mbele na nyuma, msijaribu kuanzisha uhusiano wa malove pamoja nao. Mwaya watakufirisi hao, mwaya watakutesa hao, mwaya watakunyanyasa hadi unikumbuke mie shogako Mamsapu, mie kungwi la makungwi, mie Mama la kitanga, mie niliyependwa na aliyenipenda kan’penda kweli kweli, kwangu hameguki kwangu habanduki. Aloo!👌

             Kwa kifupi shoga ukiisha kuwajua firauni hawa, Bedui na makafiri hawa , hauna haja ya kuwasoma mara mbili mbili, weye waambieni kwa kifupi, “Pita kushoto, Babu we! Mnikome.” Wapotezee mwaya, watakuharibia time zako, hawa waja waso na akili timamu akili zao zimepalalayizi, kwetu tunawaita vichuna, vichuna Mbuzi, wakati huo huo kumbe hawajui kuchuna, hawajui kumchuna Babu kisomisomi, wapo vile vile “primitive mode of production,” kutwa kuchwa kumwomba Babu pesa za mapodozi, pesa za manukato, pesa za vitu lakshari, ati hereni, bangiri, shedo, mawigi, sendo, vitopu na vimini, teeh teeh teeh 👌😂mwaya nacheka mie.

Ngoja nikupe somo shogangu, hivi umewahi kumsikia khadija Kopa yule mtunzi na mwimbaji wa nyimbo za taarabu, Khadija anatuambia “kalichuna buzi kulila limemshinda.” Ndo’ hapo sasa!! Ndo’ hapo shogangu, mie nakwambieni weye ulichune buzi kisomisomi. Shogangu ukishampata Babu ambaye hana malengo ya kukuoa, we chunia tu, chuna pambee😂👌 ubavuni(mtimani) mwako japo asijue kuwa huna malengo naye.

               Fanya hivi shogangu, mpe Babu mapenzi moto moto yeye mwenyewe apagawe, mwimbie nyimbo za taarabu mwenyewe achanganyikiwe ujue kumbembeleza mwaya, Babu ubembelezwa kama anavyobembelezwa mtoto, kama hujui shauri yako, haya ndo yetu sie watoto wa kitanga, tunajua kubembeleza hadi Babu akabembeleka, tunajua kupuliza hadi moto ukawaka, tunajua kushika pale panaposhikika nakwambieni shoga sie watoto wa kitanga tukipenda tushapenda, hatumeguki hapo, hapo ndo’ safari, kufika kimoja, kurudi ‘never,’ kama ni kuhamia tushahamia na kuweka mji hapo.

              Waambie shogangu, waambieni hao wanaopenda kukuru kakara, hawatulii kama kijogoo tamaa.

Somo embu nitegee sikio nisikilizeni,

              Mwaka wa kwanza mapenzini, shoga punguza deko na utoto, acha utoto shoga, usithubutu kumuomba Babu vitu vya kijinga jinga kama nilivyotaja hapo juu, ati “Nataka hela nikanunue chupi, nataka hela nikanunue wigi, nataka hela nikanunue sendo, my kuna della jipya lishatoka, my mchango wa harusi, my mama anataka kusafiri , my …..” Mmmh! Shoga kwa madai hayo Babu atakuchoka, wenzio hawachuni hivyo. Yote hayo madogo madogo sio ya kumtesa Babu sababu hata weye unaweza kuyagharamia, japo kwa kudunduliza dunduliza kwenye kibubu, kuweka akiba kwenye makundi ya mashoga wanao weka upatu, au ikiwezekana fanya juu chini ukibana bana matumizi angarau upate hivyo vidogo vidogo unavyomsumbulia Babu.

N'do kukwambieni lichune buzi lako kisomi somi, si weye wajua kumpetipeti Babu, si weye wajua kumbembeleza si weye wajua kumpa malavidavi, si weye wayajua mambo yakitanga, ai! Shoga mambo ya sita kwa sita yataka mastaili, ukizubaa shauri yako, watakuibia mabinti wa kitanga, ndo’ kukwambia usiwe regerege kitandani, mperekeshe Babu hadi afie mgongoni kwako, kwa hayo mastaili shoga ai! Babu Hakuachi, au bado hujanisoma? Kama haujanisoma kawaulize wale vimburukutu shombo minuko kwanini wameachwaa solemba? Watakujibu mwaya, watakujibu kuwa mambo yamewashinda, mastaili hawayawezi muziki mzito shoga, hawawezi kukata uno, hawana vyura hawana mizigo! Teeh teeh. Lichune buzi lako kisomisomi, lichune buzi lako kimipango , usilichune kizembe.

                Shost, narudia tena kukwambieni kama ushagundua Babu hana malengo na weye, weye chunia tu au sio, weye bania , jifanye kuzuga lakini usizingue Babu asitake kujua, mpe mahaba niue, mpe mahaba nikekete, mpe mahaba niangamize, mpe mahaba ninogeshe, mpe mahaba kilio, mpe mahaba nizike, mpe mahaba nisikuache. Mwaka wa kwanza huo, kwisha mwaka wa kwanza ndo uanze kudai haki yako! Upo hapo shosti, najua bado haunisomi, embu ngoja kungwi nikupe somo. 

Maisha ni gharama usithubutu kuona unapoteza muda na mtu aso na malengo na weye, mpeleke kigamboni mwambie “My kiwanja kile kinauzwa ninunulie pesa si nyingi milioni mbili na nusu,” Teeh teeh teeh! Najua Babu lazima atakununulia tu, najua Babu lazima atakutafutia hiyo milioni mbili na nusu, najua Babu lazima ataanza kukujengea nyumba hapo Kigamboni, penzi lishanoga lishanogela, weye mwenyewe usiwe msumbufu, lichune buzi kimipango. Andaa maisha yako shoga, Maisha haya ni yako ushakuwa mtu mzima ujue. Hizo shedo, hizo lipstick, hayo mawigi hayo madelIa, ni mapito shogangu, ni vitu vya muda na kupurukutika, ni anasa na starehe za kisuIi suIi (kama ujuavyo shogangu upepo wa kisulisuli ni upepo unaovuma kwa ghafla na kutoweka, aka! Shoga usiuruhusu upepo wa kisuli suli ukutawale, hautadumu nao huo upepo utapata hasara na madhara makubwa, majuto ni mjukuu, utajuta mwaya.)


                Shoga,ukiisha kununuliwa kiwanja chako huko kigamboni hakikisha ushajengewa na weye endeleza makamuzi, mpe mpe mpe mpe mpe mpe mpe mapenzi, mpe huyo Mtumishi wa umma, mpe huyo bosi mwenye pesa zake, mpe huyo meneja wa benki, mpe huyo pendeshee mwenye pesa zake,mpe huyo papa mwenye miradi na makampuni yake mpe shogangu mpe si kwa uandunje (uchoyo) na kwa ubahiri, mpe japo hana malengo na weye lakini weye chunia tu ukiweka moyoni mwako ujumbe unaosomeka hivi, “Lazima nikuchune kisomi hadi ubakie mifupa.”

               Mwaya, mwaka wa pili mapenzini, nadhani tayari ushawekewa mradi wako mwenyewe, nyumba tayari isha simama, pesa zipo Benki Account, una gari yako weye mwenyewe kutembelea, una mashamba yao huko Kyera Mbeya ukilima mpunga mtamu unaonukia, una kibedi tumboni, basi linogeshe penzi, linogeshe hadi akupende, hayo ndo maisha mwaya, kungwi nakufunda, acha utoto wa kulilia lilia madella wakati wenzio wana nyumba wana magari wana miradi wanapesa nyingi Benki, washa jirahisishia maisha yao, maisha yao yamekuwa simple na uzuri wa akili zao tayari wana bima za afya, weye je? Weye uliyekalia anasa na starehe za kulilia kwenda kwenye makasino, kwenye mabar, kwenye makumbi ya starehe kwenye disco na muziki wa uchi utupu, mmmh! Ama kweli wahenga walisema fuja mali kufa kwaja. Mmmh! Shauri yako shoga utanikumbuka mwaya, utakumbuka kuwa Mamsapungo alisema:

                   “Umekalia kuti kavu, bado kidogo kudondoka, muda ni wakati na wakati ni muda, utumie muda vizuri kupanga mipango ya kiamendeleo, utumie muda vizuri kujijengea maisha ya baadaye, utumie muda ili muda ukufaidishe, usiwe nyuma nyuma shoga, usiwe nyuma nyuma kama mkia wa nguruwe, usiwe nyuma nyuma kama ng’ombe apelekwaye machinjioni, usiwe nyuma nyuma kama umbwa amfataye tajiri wake, usiwe nyuma nyuma kama bendera fata upepo, huku upo na kule upo, japo wahenga walisema njia mbili zikimshinda fisi msamba atachana. Watakucheka, watakucheka hadi Nyani na viumbe viso na akili, watakucheka mwaya.”

               Shoga tuendelee na mada yetu, tuliishia wapi….? Ok tuliishia pale tulipo wasuta hawa mashosti wabaguzi na wachaguzi, hawa wanaoangalia elimu kama kigenzo cha kuyajenga mapenzi, hawa wanao angalia vyeo, lugha, utaifa ukabila na udini,

                   Ndio maana hawoi wala hawaolewi, kutwa kuchwa kupodoa sura zao zile sura za majivu na masizi ati wanataka ziwe sura za Dhahabu au machungwa yaliyoiva balaaa!! Kutwa kuchwa kwenda saluni kuseti nywele zao na kuvaa mawigi, kwanza hizo nywele zenyewe haziwapendezi ni nywele mbaya kama vile wamezipaka mavi. Jamoni!! Waogopeni watu hawa hawaoi wala hawaolewi, wanaringia uzuri wakati uzuri wenyewe hawanaga, wanasaka na kutafuta wazuri huko kwenye mitandao ya kijamii (Google, Face book, Wasp na Insta.) wakati wenyewe ni wenye sura za Mazombi na mazumbukuku, wenye mioyo yenye tufani majanga na majonzi. Teeh teeh teeh, my wangu (Shogangu) mpende akupendae yule ajuaye thamani yako yule anayejua kuwa duniani kupendana.

               Tena shogangu, usipende mapito maana mapito ni yale mapenzi ya kukurupuka kurupuka kama myama aso na akili weye shogangu uwe na moyo wenye akili usibwabwatuke bure, usijipendekeze bure mbele ya wanamume, uwe makini na wanamume, maana wanamume wengine ni waongo malengo yao kukugeuza chapati kisha wakiisha kukutafuna wakuteme mkavu kama vipeke vya ubuyu na machungwa.

Shogangu Leo nimenena sana kesho nitakupa mfano.

I PROMISE YOU.

 




SURA YA TATU





MIPANGO


Miaka miwili na nusu iliniacha nikiwa ndani ya kiwanda cha TBL, safari hii nilikuwa na cheo changu, sio mpishi tena mpishi wa pombe jikoni, kwa sasa niliketi ofisini nikiunyosha mguu wangu  juu ya meza moja tukufu, safi nzuri yenye kioo kimoja kinene kipana, kioo hicho chafutwa futwa kwa mikono laini ya yule Secretary wetu  Riziki. Nikiwa nimeketi kwenye kiti kimoja chenye magurudumu yazungurukayo nimepozi kwa kutupia suti yangu nadhifu nyeusi pamoja na tai yake, ndani ya hiyo Ofisi ukiingia tu basi lazima uniite meneja msaidizi hicho ndio cheo changu, wacha nijivunie, nimetoka jikoni kupika na sasa naketi Ofisini kupanga na kupangua mipango ya fedha.


               “Nimependelewa, ati eeh!?”
Yawezekana nimependelewa tena nimependelewa na yule aliyeniokota barabarani. Barabara ya Ubungo, kituo kikuu cha mabasi yaendayo na yatokayo mikoani. Nimependelewa na yule Bwana aliyetaka kuniswaga mguu wangu wa mashoto pindi nikiwa navuka barabara, ningeligongwa mguu wangu kwa uzembe na ushamba wangu ndani ya Jiji la watu, watu walioniokota kwa mapenzi na kudra za Mwenyezi Mungu  na uzuri wa mapenzi yake Mola mie leo niko bize nalikokota Gari langu nilillopewa kazini n bosi wangu.


                ********************************
                

         Ndani ya nyumba niliyopewa na Bwana Steven Biko siishi mpweke, Brenda amenifuata, amenifuata kutoka kijijini na kuja mjini, amekuja miezi tisa iliyopita, nimekwisha kumvisha pete nzuri ya uchumba, kwa sasa tunapanga na kupangua mipango ya ndoa yetu. Bado hatujawa radhi kueleza ni lini tunatarajia kufunga ndoa  itakayofanyika kijijini kwa wazazi wetu na wazee wetu, Aki! Hiyo itakuwa ni ndoa ya kimila na baada ya kutimiza mila tulihitaji kufanya sherehe kubwa ndani ya jiji la Dare s saalam.
Bosi wangu pamoja na wafanyakazi wenzangu wametoa ahadi ya kuninunulia bonge la zawadi, zawadi ya kunisapraiz. Mmmh! Sijui ni zawadi gani hiyo? Mmh!  Nisiandike mate wino ukiwepo, lisemwalo lipo kama halipo langojwa, uzuri wa ahadi, ahadi ni deni na deni sharti litimizwe.
Kwa sasa Brenda ni mjamzito, ujauzito wake ni wa miezi miwili, mie ni mwingi wa furaha, najiona nimekwisha kamilika, ni mwanume sasa, mwanaume kamili. Brenda amekuwa Ua linalo chanua moyoni mwangu ninampenda sana, ninampenda kama anavyonipenda, ninampenda kama malenga mshairi mmoja anavo ghani;


Ninampenda mpenzi wangu,nalipenda penzi langu,
Ninalilinda sungu sungu, liondokewe kiwingu,
Sintatenda ya kizungu, penzi hili penzi langu,
Kwa maneno na mizungu, penzi hili penzi langu.
Kila nikifikiria, nilifanye nini pendo,
Fikara zinanijia, nilipende kwa vitendo,
Penzi kujivunia, siwezi litupa kando,
Maisha 'menandalia, pendo lenye mapendo.


Pendo limenipenda, pendo limeniganda,
Pendo sipate shida, pendo tulia tunda,
Pendo litonishinda, pendo kwake tashinda,
Pendo ya kwangu ajenda, pendo penda pendo.
Nataka niwe karibu, daima kwenye mapenzi,
Nipate kila sababu, mapenzi yangu nasibu,
Tabu pamoja na gubu, siweze kuyasulubu,
mapenzi yawe dhahabu, faida kubwa ajabu.


Natoroka naenda kwake, kwa aliyenipendeza,
Mie niwe tulizo lake, yule nino’mchunguza,
Moyo wangu moyo wake, mapenzi twayaongeza,
Mbele sisi twende tufike, tuombe tusitereze.
Moyo wangu moyo wake, mapenzi tuyatulize,
Nani apenda upweke, hilo swali jiulize,
Mapenzi yetu yavumike, mbele sana tuwajuze,
Tupende tuheshimike, maisha mema      tu wajuze.


         **********************************

                “Mmmh!” Niliachia mguno mkubwa ndani ya ofisi yangu. Nalikuwa pamoja na bwana Steven Biko bosi wangu na mwajiri wangu.


                “Usishangae Bwana mdogo, biashara hii ni moja ya biashara itakayo tuletea faida kubwa sana kikubwa ni utayari wako katika kuifanya hii biashara.” Biko aliongea.

Moyoni sikutaka kuamini kama kweli haya ni maneno yatokayo ndani ya mdomo wa bosi wangu  Steven Biko.

                 “Je wewe binafsi umewahi kuifanya hiyo biashara?” Nilimuuliza Bwana Steven Biko.

                “Yes, tena hivi ninavyoongea pamoja na wewe ni mara yangu ya kumi kwenda na kurudi  South Africa kuiendesha hii biashara iliyonitia utajiri na umilionea.” Aliongea bosi wangu Bwana Steven Biko.

Nilivuta pumzi kidogo, kisha nikatafakari maneno aliyonishawishi bosi wangu, siku ya leo, leo tumetumia saa moja na ushee kujadiliana kuhusu hii biashara.

                 “Mmh! Lakini….. Mmh!” Niliguna tena kuonesha wasi wasi wangu, moyo wangu ulisita sita kukubaliana na Bwana Biko.

“Lakini nini tena bwana Job? Kumbuka wewe sio tu ni mtani wangu,  wewe ni ndugu yangu tena ndugu wa kufa na kupona changu chako, damu yangu damu yako au vip mawazo yangu yawe mawazo yako?”

                 “Moyo wangu unasita sita.”

                 “Unasita sita nini?”

                 “Nina hofu ya kukamatwa na maofisa wa Polisi watakao nishuku kuwa nimebeba madawa ya kulevya na kuyapitisha Air port.”

                  “Hilo tu, mbona hilo ni jambo dogo sana, iwapo utatiwa chini ya mikono ya polisi, mimi pamoja na mabosi wangu wengine tutafanya mipango ya kukutoa ndani ya mikono ya makachero wa Polisi tambua kwamba biashara hii ina mtandao mkubwa sana, hii biashara ina watu wakubwa duniani, faida yake ni kubwa sana iwapo utakuwa tayari kujiingiza ndani ya hii biashara nina imani utavuna zaidi ya hapo ulipovuna.” Steven Biko alijaribu kunishawishi.

                 “Ok. Bwana Steven Biko nipo tayari kuungana nawe katika hii biashara ya kusafirisha dawa za kulevya, kutoka  Tanzania kwenda South Africa. Ilihali umenihakikishia kuwa, ulinzi, usalama  na imani vyote ni vya kutosha kwa ajiri ya nafsi yangu na maisha yangu. niliongea pasina kufikiria mara mbili mbili athari zinazoweza kunitokea iwapo nitapatikana na hatia ya kukutwa na  dawa za kulevya mikononi mwangu.”

                Tabasamu lilimtoka Bwana Steven Biko alipohakikisha utayari wangu katika kufanya kazi ile ya hatari pamoja nayeye moyo wake uliripuka kwa shangwe na furaha isiyo na kifani, nilimshangaa mara nilipomwona akisimama pale alipoketi na kuja kunikumbatia kwa nguvu zote akidai kuwa amefurahishwa na ushirikiano wangu, ushirikiano mkubwa niliouonesha mbele yake.

               “Congraturation mtani wangu, now you are going to be a rich person in East Africa, nitakuwa pamoja na wewe kwenye shida na raha, sitakutema kamwe, wala sitakuacha uteseke, jumatatu ni siku special kwa maandalizi ya wewe kwenda Africa ya Kusini, mimi nitafanya juu chini kuhakikisha kuwa unapata passpot size pamoja na Visa yako binafsi.

                 Aliongea bosi wangu usoni kwake ameng’ara kama jua, tabasamu lake pana kama shimo kubwa lililo wazi, wakati wote anacheka cheka kama mwendawazimu, anadai kwamba amependezwa na ushirikiano mwema nilio uonesha.

Itaendelea sehemu ya nne.

MWENZENU N'SHAPENDWA



      MIPASHO YA MAMSAPU.


     ( PASHO LA KWANZA)



    “MWENZENU N’SHAPENDWA.”💕


Sehemu ya kwanza.


Bibi we! Mwenye wivu ajinyonge, mwenye wivu asage chupa, mwenye wivu ajitose baharini aliwe na Papa. Maisha haya ni ya yangu mie, mie Mama la kitanga, Tanga ni kwetu kwa asilia, Lushoto ndio nyumbani, nyumbani kule mapenzi yalipozaliwa, kule mapenzi yanamea kama maua, kule ndo’ kwetu kwetu kwa mapenzi, Huba mahabuba💕🥰


      Enyoooo!😉  Unaambiwa Shoga kalichuna Buzi kulila limempiku,  teeh teeh teeh!! 😂😂👌(Nacheka mie) kicheko changu mwenyewe, kicheko dawa, napenda sana kucheka, tena kucheka kwenyewe nakwambieni nacheka na mboni 👁️‍🗨️wangu, Tende wangu Arua wangu, wangu wa ubani, Pompolimpopo kwa kifupi mwite Pompo au ukipenda mwite Mpompo, yote haya ni majina yake, yeye ni wangu na mie ni wa wake kanipenda mwenyewe.



                 Shoga nakwambieni huyu nitamshikilia sana, kama ni kun’torosha kan’torosha Mbinguni na kama ni kueleka nitamshikilia hata nifike naye Peponi,🌬️🌁 simwachi hasirani, simtemi abadani, ninampenda, 😍😙ninampenda pendo la kupendeka, ninampenda ajabu sioni mfano.‼️ Tena nikuombe kitu shoga'ngu nasema hivi siku ujapomkuta  Pompo anaongea ama amesimama pembeni na mwanamama mwingine usisite kuniambia. Mwaya nilivyo na gere Aki! Nitaua mtu mie, 🔪🗡️nitachoma nyumba ya mtu mie,🔥 nitakwenda kwa Babu Sangoma nyumbani Tanga ili nipate kumfanya mtu kitu  mbaya.


                Aki! Mapenzi ni wivu na ili mapenzi yanoge na kunogela, acheni nimshikilie wangu wa rohoni,  Pompo ndio jinale, acheni nimchunguze wangu wa moyoni Mzaramo aso na mapepe, makeke, michepuko  na micharuko. Ndo’ mjue kuwa yeye kazaliwa pwani 🌊🚣kule wataalamu wa kupika na kupakua. 


Babu! Usipokuwa makini waweza kulishwa hata visoliwa, teeh teeh teeeh😂😂👌 (Nacheka mie) mwenzio n’shapendwa.
 
Basi nisikilizeni nyonyo, mapenzi ustaarabu, mapenzi uungwana, mapenzi upendo wa dhaati, ndo’ maana malenga Washairi wengi wanasema, wanasemaje.


Pendo penda popote,☺️

Popote penye mapenzi, 😍

popote panopendeka😉

Hapo pana matatuzi,😻

Moyo wangu upate pite,😜

Mema yanifuate,🥳

Na mabaya yasinikute.🥹


           Teeh teeh teeh! 😂😘Ai! N’cheke mie, 😄nimelipenda Shairi hili, mwenyewe utapenda. Mwaya nikwambie nini? Mpende akupendaye hata kama ana kilema, mpende umpendaye hata kama ana maisha ya kikabwela, ndo’ maana waswahili wanasema, mpende umpendaye simche akutendaye. Kipenda boga penda na Ua 🌺lake, kipenda moyo nyama mbichi  au sio nyonyo, hupo hapo? Mapenzi kikohozi, mie n’shapendwa na mie tena n’shalipenda boga pamoja na Ua lake.


        Akuu! Mtoto wa kitanga nisiyajue mambo?  Mbona kichekesho, n’shafundwa Bibie, n’shafundwa jinsi gani nimkande kande Babu, namna gani nimpeti peti na kumfariji, 😽kutwa kuchwa namwimbieni nyimbo za mapenzi. Nisikufiche Bibie nshafundwa mie nshafundwa namna gani niiamshe mizuka iliyo lala, ile mizuka ya kwenye sita kwa sita, pale kwenye mastyle kama yote, pale penye uturi na upepo mwanana wa kizanzibari. Bibi! mwenzenu  n’shapendwa kanipenda mwenyewe. Anafurahia pochopocho nimpalo, kazidi kunenepa, kaboreka, kanawili nae katanuka, afya hiyo si mchezo!! Yeye menyewe akili kwa kusema “Mambo ninayaweza.”👌👏 Shoga weye si wamlisha mumeo madikodiko,  Nyonyo kumbe kuivisha mahanjumati hauwezi?😱🥹 .Aibu🙈🙊

 
Kumbe wewe bado ni wa rojorojo,  bokoboko, dikodiko na mitori yenye  maji mengi, mmmh! Shoga mbona una haraka kama  upepo wa kisulisuli, 💨wan’fanya  nahisi kutapika. Utangoja👌😂


             Nisikilize nyonyo👂 some time mwanamke mabadiliko, kwanza kabisa kabla haujawekwa ndani muhimu upitie unyagoni, ukafundwe huko Tanga, ukafundwe usafi  sio wa nyumba pekee hata mwili bibie  ili ukiwa ndani usimpe kero babu kwa huo mnuko wa kikwapa,🙀 mmmh!  Yaani  bibi kwapalo linuke kama panya alofia ndani, 🙊hapana, hapana jamani Babu atakutorokeni,  aibu nyonyo!!

                Tena shoga'ngu ukiisha kuwekwa ndani, uaminifu mia kwa mia, 💯💝hao vijibwakoko wenye tamaa za Fisi waambie wapite kushoto, wakafie mbali, vibudu hao, vinyamkera hao, waone sura zao kama Popobawa, washachelewa, wewe ushapendwa yanini tena upendwe na hao viroboto, hao kunguni, hao chawa, hao kupe, papasi na funza, waeleze  Bibi waambie mwenzenu n’shapendwa kanipenda mwenyewe👌

                Muhimu, tena muhimu nyonyo, nisikilize mwenzio, mie ndie kungwi, kungwi la kitanga, nakufunda, nakufunda shoga, uwe na heshima Bibie, vaa mavazi yenye stara, 🥻usiuoneshe  utupu wako kwa hao waso na hekima. Jifunze kupika ama ikiwezekana niite mie  kungwi la kitanga, niite nikufunde namna ya kumpikia babu, kumpikia  wali wa nazi na manjonjonjo mengine kibao hapa siyataji hapa sio pahali pake labi tukutane mekoni, huko ndo’ utanijua kuwa mie ndie kungwi la mapishi, mie ndo ticha mwalimu na mwalimu n’shapendwa.

Bibi, kumbuka wako wa rohoni sharti abaki kuwa wa rohoni umuwazie yeye, umlilie yeye, stress zako zote ziwe kwa ajili yake yeye. Bibi tena ujue namna ya kukaa na mashoga maana mashoga wengine nuksi mikosi, wanaweza kukupotosha pasina wewe  kujua kuwa wanakuharibia, watakuvuruga kama ungelijua kuwa wanakuzunguka mbuyu wala usingelipata shida kujua kuwa habari zingine zinafirisi ndoa. Basi shoga'ngu uwe na jicho la tatu kuwasikiliza mashoga, maana mashoga wengine hawana dogo dogo watajifanya kama wanakuja kuomba chumvi mekoni kwako, kumbe wanakuja kumkoroga mumeo na mumeo akikorogeka basi ujiandae kuachwa solemba🥹, utaliwa kasumba, shanga zote zitakupwerepweta.  Ai! we! Mwenzako n'shapendwa.


              Nshapendwa na yule anayejua kupenda, yule anayejua nini maana ya upendo mapenzi na mahaba, n’shapendwa na yule aliyenikuta hoehae sina mbele sina nyuma. Leo hii ukija Kigamboni kwenye mjumba wetu wenye horofa 🏢tatu mwaya utanikuta nimetulia tuli kama dhahabu,💛 najibidisha kusuka ukindo (mikeka) kufuma vitambaa vya mezani,kudalizi, kusoma vitabu au kuandika Hadithi, kupika na kupakua kumpeti peti wangu wa rohoni wangu anayenithamini anayejali na kunijali anajua maana ya mwanamke thamani ya mwanamke na kadharika.

Tukutane kesho Mwaya wa mie

DESPERATE WOMAN

 

DESPERATE WOMAN.🥹

       Mita chache kutoka pale tuliposimama Barabara kuu pembeni Kuna kichaka kilichoota nyasi zilizokauka. Tulikua tunapigisha moshi wa Dawa 🚭pamoja na kustawisha mioyo kwa Visungura na Double kiki 🍾tulimuona Demu 🚶‍♀️flani matata akija location yetu. Kwa appearance yake 
alionekana kavalia gauni 👗Moja refu lenye kitambaa laini na chepesi lililoendana na umbo lake umbo la Kuku wa kizungu 🐓 (Modo).

       Mkono wake wa mashoto alishikilia Kikoba👜 kidogo chenye rangi nyeusi, Cheni ya Dhahabu Og iling'ara shingoni kwake, vitobo pua na hereni masikioni.

 Chini miguuni alitinga kiatu 👠Cha mchuchumio ulioambatana na vikuuku miguuni. Aliendelea kujivuta kwa mwendo wa Nyau (Cat 😺 walk) kainamisha kichwa chini, 😞huzuni flani ilifunika na kugubika sura yake nzuri, muda wote alitizama aridhi, lakini Who cares!! Ni nani anajali?🤷 Kama Mie Nyanda na kaka yangu Kabundi tuko bize kusaka mali za wizi, unyang'anyi, pick pocket na magendo.

       Yule mdada mwenye Figure ya kizungu aliendelea kuja usawa wetu, Mwendo wa Nyau haukumtoka kwenye Malundi yake.🐆🐾 Uzuri mkononi aliishikilia simu ya Iphone 19📱🧐😋

        "Oyah! Kabundi zamia huko mpakani." Nilizima kipisi changu Cha Dawa nikaamuru Kaka Kabundi afichame kwenye kichaka kidogo kilichokuwepo pale tulipozamia, alitii na mie nilifuatia, tulijipanga kumfanyia 'ambush' yule mrembo.

     "Kitu hicho mwanangu mali ya Dhahabu."Kabundi alininong'oneza sikioni.👂


     "Ulaji" 😜Nilimsapoti kaka yangu. Yule Dame alijikatisha na kutuachia mgongo.Kitu pasina kuchelewa tulinyata mfano wa Chui 🦁🐆amvamiaye Umbwa koko🐕 aliyelala. Hatua ya kwanza ilikua ni kuikwatua ile l phone 19 🤳kutoka mkononi mwake. Holla! Kama upepo vile hatukupata tabu kuinyakua ile simu, tendo lile lilikua kama vile kumsukumiza mlevi adondokee kisimani. I phone 19📱 tuliiweka kibindoni.


        Alitutazama kwa jicho la upole👁️‍🗨️ na madaha, hakusema neno, hakupiga kelele🧟 za kutuitia watu nyomi. Kawaida tumepigiwa sana kelele za 'Mwizi! Mwizi ! Mwizi' pindi tufanyapo uarifu kama ule. Hatukufika mbali mbio za sakafuni uishia ukingoni tuligeuka kumtazama yule Dada. 'Duh!' Mbona hapigi kelele 🔊🫨 za kutuitia mwizi! Mimi na kakangu tulitazamana kwa mshangao, Dame aliendelea 'kumuvu on' kwa mwendo wa Nyau kama vile yupo kwenye Jukwa la maonesh ya mavazi ya Louis Vuliton.


    'Twende tena' Uporaji ulitunogea. Tukamkimbilia. Kitendo pasina kuzembea tulizinyofoa cheni zake za Dhahabu shingoni, zilikua ni Mali ya mamilioni maana ni Og, kutoka Uingereza🇬🇧 au Arabuni 🇦🇪sio kama zile feki za Manzese na Kariakoo.🇹🇿

     "Naomba mchukue pia Pesa zangu zilizo ndani ya mkoba." 💰Aliongea wakati huo sie tuloanza kumkimbia tulijiona kama tumeupiga mwingi.🤪😜😝


 "Twende tuchukue." Nilimwambia Kabundi. Tulimvua ile saa ya Dhahabu mkononi,⌚ tukauchukua mkoba wake ambao ndani kulikua na Madolari 💵💵💵💰. Aliendelea kutembea usoni akiwa mnyonge mnyong'evu na dhaifu.


       "Whuuuza! Wizi wa Leo ni Noooma" Kaka alifurahia.🤪

      "Woooooh!"🤪🤪Tulijipagaza baada ya kuiona simu 📱 Babu kubwa tena ya bei Kali, cheni za Dhahabu na Madolari bunda💸 ya kutuheshimisha mjini kwa hakika Pombe🍺 ingetukoma, vyuku🐓 vingetukoma, vyura👩‍❤️‍💋‍👩 vingenesanesa juu ya viuno vyetu, mende wangekufa miguu juu, kwetu ilikua zari.

      Macho yangu yakatua kule anakoelekea yule Mwanadada, taa 💡🔦 ya ubongo 🧠🤯wangu iliwaka ghafla, nilihisi Kuna hatari💥 anaelekea kuitafuta. 'Mbona kama anataka kuvuka Barabara wakati Magari🚘🚗🚕 ya mwendokasi yanakimbizana. Nikamwacha Kaka Kabundi anaifurahia ile pochi yenye mapesa, nikakimbilia yule mrembo kwa kasi ya ajabu.🚀 Pale Zebra cross🦓🚸 alikua anavuka🛣️ wakati Magari hayajasimama kuruhusu watembeao kwa miguu kupita.

         Nikafanya kuwai, nikaushika mkono wake kwa nguvu zangu zote kiumeni nikamsukumia kifuani kwangu, Gari lilikuja kwa kasi ya mshare🏹 tukadondokea upande wa nje ya Barabara, ilibaki kidogo litugonge na kututupilia mbali.

       "Kwanini unataka kujiua!?"⁉️ Nilimuuliza nikiwa nimemkumbata kiunoni mwake baada ya kudamka kutoka pale sakafuni.

     "Niache tafadhali," Alinijibu akijaribu kujitoa mikononi mwangu.

      "Nikuache ili ujiue" ⚰️Nilimfokea. Kaka Kabundi alitufuata pale tulipokua tunabishana.

      "Vyovyote vile, kama mnataka mali🌟🚕💒 zangu zingine twendeni nyumbani niwape, sioni faida ya kuishi, sioni faida ya hizo mali." Lugha yake ilinipa wasiwasi 

      "Mambo moto!"🔥 Kaka aliongea kwa furaha.

      "Tupeleke please!" Kaka alitabasamu hadi majino yake Therathini  mdomoni 🦷yalichomoza, tamaa iliwaka.🎆🔥 Dame akageuza kuelekea  nyumbani 🏠 kwake, tulifuata, Safari iliiva wakati Kaka akifurahia twaweza pata mali nyingi mie moyoni nilikua nawaza kuhusu yule Dame aliyejikokota akitembea kwa huzuni.😭

Tulifika nyumbani kwake, Horofa 🏘️ya pili kati ya tatu alizomiliki. Bila woga bila wasiwasi Wahuni tuliingia ndani ya Sakafuni la sebule ile nzuri ya kuvutia kama imepakwa Dhahabu, Almasi na Lulu. Majumba ulipendeza: Kuna sofa za bei gharama, kuna makabati yenye vyombo vya China, America na Jerumani. Kuna Tv screen Moja kubwa ukutani, Zuria chini lina mvuto yaani Zuria Og. Sifa zitajaa Viroba, tukomee hapo. Kabundi alitabasamu mara Moja akakimbilia kabati la vyombo vya China macho pima akilishangaa.👀

     "Tumetajirika Nyanda." 🌟🌟Furaha yake haikumiridhika. Niliisikia vibaya kwanini tumuibie Mwanamke akiwa anatukodolea macho. 'Sio poa.' 👎 Nikamchukua yule Dame nikampeleka Restroom (Toilet.)🚻 Nikamfungia mlango kwa nje Kisha nikamfuata Kaka Kabundi aliyekua akifurahia Kila kitu chenye thamani ndani ya ile nyumba utadhani ni Mali zake halali.☺️💩

     "Kabundi nikabidhi Simu ya huyu Dame"☎️ Nilimwambia Kaka.

      "Nini!? Nikupe simu iliuongee na nani? Mbona umeanza kubadilika ghafla mdogo wangu, ucheshi uliokua nao siku zote umetoweka."🙂‍↕️Kabundi alianza kuhisi mabadiliko yangu ghafla.

     "Nipe nahitaji kumpigia mtu muhimu, yamkini mume wake. Je, huoni Dame huyu anaonekana ana stress." Niliongea.

     "Nyanda una matatizo wewe, yaani tumpigie mumewe alafu kitukute kisanga.🧨🎇🔥🥵 Tupo hapa kubeba Mali sio kupigia Simu watu." Sikujali kauli zake.

      "We nipe tu." 👿 Nilimkasirikia. Aliitoa na kunikabidhi ile Simu akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wake na wangu."

Niliwasha ile Simu, nikaingia missed call📞 Kisha nikasechi nambari ambayo nilihisi yule Dame anawasiliana nayo sana, sikukosea niliiona Moja imeandikwa 'Habibu wangu." Nambari hiyo alioneka ameitumia sana kuwasiliana. Nikafikiria huyu atakua ndio mumewe basi nianze na yeye.

     'Driiip.....driiiip....driiiii' 📳Simu iliita. Muda si mrefu yule aliyeitwa 'Habibu wangu' akaipokea. Kabla sijajitambulisha na kuongea neno Habibu alianza kufoka, bahati nzuri niliweka loud 🔊 speaker kaka Kabundi aliyasikia maongezi yale.


      "SAMOA, UNAMATATIZO GANI WEWE MWANAMKE MPUMBAVU? 👿 NIMEKWAMBIA SIKUTAKI, SIKUPENDI, WALA SINA HAJA NAWE. MWANAMKE MNUKA KWAPA WEWE, MIE N'SHA MPATA💘 BIBI WA KITANGA ANANIPA HUBA💕 NA VITAMU VYENYE MAFUTA NA SUKARI YA TENDE NA ARUA. KUANZIA LEO STOP 🚫KUNIPIGIA SIMU. NAWEZA KUKUUA AU KUKUFANYIA KITU KIBAYA MAISHANI MWAKO, KENGE WEWE .MXIIIUUU🥴😠😵‍💫." Habibu alikata simu mimi na Kaka tulitazamana kwa mshangao uliojaa viulizo tele. ‼️‼️

      Tukiwa tungali twashangaa Ghafla mlango wa Sebuleni ulifunguka. Tulitetemeka kidogo tukijihoji wapi tufichame, aibu yaweza kutuzika ndani ya nyumba ya watu tusowajua. Lakini tulikuja kupoozeka tulipomwona mtoto👼 mwenye kadirio la miaka mitatu alkiingia pale sebuleni. Mtoto hakuonesha darili za kutuogopa alitusalimia kwa adabu na heshima Kisha akatuuliza sie ni wakina nani?

      "Sisi..... Mmmmh ......mmmh!"😎😶‍🌫️ Tulijing'ata ulimi tusijue tumweleze Nini mvulana yule  mwenye  tabia nzuri.

      "Sisi ni marafiki 💑🤞wa Mama yako" Kabundi alimjibu yule mtoto.

     "Mama yupo wapi!? ⁉️Au yupo chumbani kumeza dawa zake." 💊💉 Alitushitua zaidi tusijue Mama yake anameza dawa gani na kwanini anameza dawa!?"  Mimi na Kaka tukatazamana.👁️👁️‍🗨️

    "Hapana Dear ☺️....... Rafiki tunaweza kwenda Jikoni tuandae chai na mayai mchemsho?" 🍵🥚 Kaka alihitaji kufanya jambo la ziada.

    "Ndio tunaweza." ☑️Mtoto yule mwerevu alielekea Jikoni kuandaa chai na mayai pamoja na kaka Kabundi. Chale zilianza kunicheza 'Yamkini huyu Dame atakua yupo hatarini,⚠️ embu ngoja nimfate huko aliko chooni.  Nikaelekea Maliwato nikaufungua mlango wa chooni 🚽na kujitoma ndani.

 'Makubwa!' ⁉️😥

Nilimkuta yule Dame ameketi chini ya sakafu yenye marumaru pale chooni, chozi 😢 lambubujika, ameshikilia kikopo cha rangi nyeupe ndani Kuna Dawa 💊💊tayari kakifungua na kuujaza mkono wake kwa Dawa lukuki, bado kidogo kumeza. Nilimkimbilia na kumpokonya vile vidonge vingi mkononi mwake Kisha nilimkemea.😡😧

    "Unataka kujiua? Kwanini unataka kujiua?"😡

     "Niache Bwana, niache nimeumizwa sana, nimechoka kuishi Bora kujiua. 😿 aliongea akilia kwa uchungu.

     "Hapana Daring 💕kujiua sio suluhu ya matatizo yanayokuandama." Niliongea kwa upole.

     "Suluhu ni nini baada ya kuumizwa na mwanaume niliyempenda hatimaye kunibwaga!?" Nikamwambia 'Calm down baby' nitakusaidia. Kisha nikaendelea kunena.🗣️

      "Kumbuka Bado unae mtoto mdogo anayehitaji mapenzi 👩‍❤️‍💋‍👨ya Baba na Mama Sasa wewe hujui ni nani  atakayeonesha upendo kwa mwanao, ikiwa Baba yake mwenyewe haeleweki,  nani atamuelewa mwanao? Aliinua macho yake kisha akanitazama kwa uchungu mkuu, akaanza kulia kilio cha Kwi Kwi Kwi uwiiii! 😿😭Hisia za uchungu zilimpanda.

      "Hivi Samoe unajua ni kwanini mimi Nyanda na kaka yangu  Kabundi tunavamia watu mitaani tukiwapora na kuibia Mali zao. Unafikiri twalipenda jambo hili?⁉️ Hapana, tunasababu zetu na sababu zetu zinatuumiza. Nikaanza kumwadithia kwa ufupi Story yetu sie wenye dhiki.💩

       "Mama yetu alipokua hai tuliishi kama Malaika ndani ya Bustani ya Edeni.🏡 Kila hitaji letu nyumbani tulilipata: Kila hitaji letu muhimu na liso muhimu tulilipata : chakula, 🍔🥙manywaji,🍷🍶🥂 malazi,💤🛌 pesa, 🏧💰amani, upendo na furaha. 

Ghafra Mama yetu alipata homa kali, Mola akamchukua mambo yote mazuri tuliyoyapata pale nyumbani yalibadilika na kuwa ovyo.🤬 Baba alianza kuondoka Alfajiri na kurejea usiku wa manane akiwa Bwiii! Kalewa chakali, 🍻hapo haulizi Wala hajui, tumekula Nini!? Tumevaa  ninii? Je, twahudhuria masomo shuleni!? Tumepata ule upendo, amani na furaha⁉️ Hakua  na muda huo Baba yetu. Kwa ufupi Baba yetu alituacha njia panda, hakuna jipya tulilolifurahia mbele zake.

Kwa sababu tuliachwa ilitubidi tuanze kuhaso tungali makinda ya Darasa la tatu na nne. Kuiba ikawa ni kazi yetu, kutekanyara, kupora na kuvamia likua kawaida kwetu. Huwezi kuamini hadi ukubwani tumeikomalia hii shuhuli hatarishi inayotutia wasiwasi juu ya kesho yetu. Kwahiyo Daring mimi nipo tayari kukusaidia.💕

     Nilimfuta chozi na kumpokonya vile vidonge alivyoshika mkononi, Kisha nikavitupa ndani ya sinki la kunawia mikono. Vidonge vile sometime vilikua vinampunguzia strees, masikitiko na mawazo juu ya Habibu mumewe.
    
     "Have peace Samoa." Nilimpooza  nikajitambulisha tena kwake: 'Niite Nyanda' akachangamka kidogo🌞☺️'Mimi Samoa' Samoa alijitambulisha pia, moyoni nilihisi ushindi utapatikana tu hata kwa ncha ya Upanga.🗡️🔪

******:::::::::::::*******

     Basi kuanzia siku ile mimi Kabundi na kaka yangu Nyanda tulianza kumjenga kisaikolojia  Samoa na uzuri wa sie 'Shameless men' tukafanya kuhamia nyumbani kwa Samoa. Tulifanya kila tendo na kila neno la kumrudisha Samoa katika ubora aliokua nao zamani.

     Tiki ikatiki🫰✔️ kwa ubora wa mashauri yetu Samoa alianza kupona kisaikolojia. Mimi nae nikaona hapo Sasa ni nafasi ya kujiongeza. Nikajenga ukaribu  na Samoa akanipokea na kuniweka moyoni mwake, penzi likazaliwa likapendeza na kumea kama Maua  bustanini🌺🌹💐. Samoa akawa ni mtu wa furaha, Raha na amani tele. Hakuwa na muda wa kumuwaza tena Ex- Husband  wake Habibu bali aliniwaza mie Nyanda.


    Uzuri kumbe Samoa alikua anamiliki  Kampuni ndogo,  hilo likaleta 'Blessing' zingine kwetu. Kaka Kabundi akapewa Umeneja wa Kampuni ya Samoa mie nikapewa cheo cha juu  ndani ya Kampuni, 'General Director.' Aki! Maisha yakaanza kutunyokea  from Zero to Hero, Waooo! Leo hatuwapoli tena Raia, hatuwanyag'anyi  au kuwaibia Bali twaendesha Magari ya fahari, utajiri na pesa 💰💰🏧 zimetutembelea hadi zinatuogopa.


     Huu ni mwaka wa tatu tangu mie na sweet Love 😘 wangu Samoa tuingie penzini🔥 miezi miwili ijayo anatarajia kuingia Leba, Mtoto 🤱 tunaye na kutamba tunatamba naye👌💕😹. Nashukuru Mola Samoa alikua anataka amani, upendo, furaha na Raha vyote hivyo sasa amevipata na pia vimerejea baada ya kuvipoteza akiwa Desperate Woman  (Mwanamke Aliyekata tamaa.)



"************
TCHAO 

 💖 LOVE  MUST LEADY

"************
 





Wednesday, July 2, 2025

I PROMISE YOU

 


Tendo  la mie kujiuzuru kunywa matapu tapu likawa  pia ni mwisho wa Brenda kunywa . Maji ufuata mkondo, Brenda alinifuata aliungana nami ili kumpiga vita adui pombe. Nakumbuka vizuri, naikumbuka tarehe 25 mwezi wa pili mwaka 2016  ni tarehe iliyonifanya nichukue uamuzi mgumu wa kwenda nje ya mkoa wetu Iringa, nikaelekea ndani ya jiji la Dare s saalam.


Lengo likiwa kutafuta shughuli yoyote ile ya kunitotongotongo. Sio tu kunitoa kimaisha pia kunitimizia malengo yangu mengine kama vile kumtimizia Brenda furaha ya mtima wake. Si anataka nimuoe? Yes, anataka nimuoe lakini siwezi kumuoa pasina kufuata mila na desturi za kiafrika, ni lazima nimtolee mahari, sherehe kubwa ya kupendeza na baada ya hapo nimuweke ndani ili awe wangu, wangu wa milele.

             Sikupenda kuwa mbali na walezi wangu, babu na bibi, sikupenda kuwa mbali na macho ya Brenda, ilinibidi nikubali kuwa napaswa kuondoka, napaswa kwenda mbali na mji wa Iringa, nikatafute riziki na iwapo nitafanikiwa napaswa kurejea nyumbani haraka iwezekanavyo, haraka  mara baada ya kufanikiwa nikijua fika kuwa mwenda kwao si mtoro, mjasiri aiwachi asili.
Basi mpenzi wangu Brenda akaniandalia kila kitu kwaajiri ya safari yangu na uzuri wake nauri ya kwenda jijini Brenda alinitafutia. Babu na bibi walinitafutia  pesa ya makuli na malazi mara nifikapo jijini. Sikua na jinsi ilinibidi niondoke niende ndani ya jiji nililo amini kuwa nitapata kazi. Penye wengi pana mengi, nilijiamini na pia niliamini kwa kudra za Mwenyezi Mungu kazi nitapata, kazi ya kunitoa kimaisha. Japo mie ni mvivu wa kufanya kazi sina udhoefu wa kufanya kazi yoyote ile, nilikuwa ni mzoefu wa kunywa pombe. Pombe pekee ilikuwa fani yangu sikuwa na kazi nyingine niliyoipenda kama kunywa matapu tapu.

                 Looh! Ndugu zangu pombe iliniharibu, kimwili na kisaikolojia, sikuhitaji kufanya kazi yoyote ile, nilikuwa mzoefu wa pombe na kunywa pombe ilikuwa ni kazi yangu, sikuwa na kazi yoyote ile ya kuniwezesha kimaisha, kilimo kilikua ni cha babu na bibi, walilima walipanda walivuna waliuza na kunipatia pesa ambazo kila siku ziliishia kwenye bunge la walevi, nami nikachangia pesa ya pombe, kila siku ili nipate kiburudisho cha mdomo wangu.
        *******************************
              Saa nane mchana niliingia ndani ya jiji la Dare s saalam, sikuelewa nitaanzia wapi kwenda au nitafikia kwa nani? Nimeondoka kijijini na kuja mjini ati kutafuta maisha, hivi mimi ni mpuuzi wa maisha ya aina gani? Nilijiuliza mara baada ya  kutoka Ubungo Bus terminal. kituo kikuu cha mabasi yaendayo na pia yatokayo mikoani.

             “Hivi nimefanya uamuzi gani mimi?” nilijiuliza tena safari hii moyo ulianza kunilaumu kwa uamuzi wangu wa kutoka kijijini kuja mjini kutafuta maisha, kwenye mji wa watu nisio wajua, sina undugu nao, sina ujamaa nao wala sina mahusiano nao.

              “kwanini nimeondoka kijijini, sehemu ambayo kuna kila kitu ninachohitaji haraka ningelipata, chakula cha kutosha, maji, matunda ya kutosha, pahali pazuri pa kulaza kichwa changu, marafiki wenye heshima zao, ndugu jamaa na majirani, mimea wadudu na wanyama. Mmmh!” Niliguna mimi na moyo wangu bado mawazo yalilindimaa.

“Nina  nini mimi?je hakuna kazi yoyote ile ya kuniwezesha nitoke vema kimaisha nikiwa kijijini? Mbona wapo wasusi wanasuka mikeka , makapu, kofia na nyungo? Mbona wapo wafinyanzi? Wasanii wa vikundi mbali mbali vya ngoma wanatumbuiza na kuvuna fedha zao? Wawindaji hawakosi nyama, matunda, mayai na asali ya kuleta nyumbani. Wakulima ni wengi wenye faida, wanailisha dunia  matunda ya aina mbali mbali; mafenesi machungwa mapeasi, mabohora, matango, matikiti maji mapera ndizi na mananasi. Kilimo cha mahindi, viazi mtama, uwele, ulezi, mpunga, maharagwe, kunde na mbaazi.” Vyote hivyo mie goi goi nilikuwa msindikizaji tu, nikiwasindikiza wakulima wajibidishe katika shughuli za kilimo japo mie mzembe na mvivu kazi yangu kula, kunywa na kulala.

                 “Je kijijini hakuna ulinzi? Nilishindwa kujiunga na jeshi la wana mgambo? Je kijijini hakuna biashara? Mbona zipo nyingi zile za masokoni, zile za madukani, zile za kuingiza na kutoa mali ndani na nje ya kijiji. Kuna uvuvi, kuna ufundi uwashi, kuna mengi ya kujivunia, nimeshindwaje kujibidisha katika hayo, nimefanya maamuzi ya kuushangaza mtima wangu, maamuzi ya kuondoka  kijijini na kuja mjini kutafuta maisha. Nimekuja kutafuta maisha gani ikiwa ningali ninajua kuwa hata kijijini maisha ambayo nimekuja kuyatafuta mjini yapo. Tena yapo fresh tu.” Niliwaza sana siku ile.
                 ‘Piiiiiiiiiiii…..Pooooooo………Piiiiiiiii!’ ilikua ni sauti ya gari, Mitisubish pajero kama sikosei, ilifunga breki karibu karibu na miguu yangu, wakati huo huo mshamba mie  nilikua najiandaa kuvuka barabara kuu ya lile eneo la ubungo.

               “Yallah! Toba! Nimepona mie.” Niliongea mie na mtima wangu mara baada ya kuiona ile gari ikiwa imesimama pembeni ya miguu yangu dereva aliyekuwa ndani ya ile gari alinitizama kwa chuki na kwa hasira. Aliugundua uzembe wangu uzembe barabarani, nilivuka barabara pasina kuzingatia sheria za brabarani, nilivuka tu kama mwendawazimu, nilivuka pasina kujielewa elewa, nilivuka pasina kutazama wapi  utokao wa yale magari na wapi uendao wa yale magari pamoja na motokaa zilizoongozana kama farasi.

                “Una nini wewe kijana?” Mwanaume mtu mzima aliyeonekana kushiba vya kutosha, alichomoka ndani ya gari yake mara baada ya kuiegesha ile pajero  pembeni ya barabara. Ana nywele nadhifu nyeusi  zilizonawili amevalia shati ya blue tai nyeusi na koti moja yenye rangi nyeusi,, ni mnene kiasi,  katupia miwani machoni.
                Ukimtazama mara mbili mbili waweza sema moyoni mwako mwanaume yule ni mwenye pesa zake anajiweza kiuchumi, ni kibosile fulani ndani na nje ya serikali kama sio kibosile basi ni kigogo fulani hivi ndani ya nchi. Any way hisia hazijengi sikuhitaji kuziruhusu hisia za moyo wangu kutawala fikra na mawazo yaliyojaa moyoni mwangu kama ni kupona nimepona, nisije nikapoteza miguu na viungo vyangu vingine nikiwa ugenini, nipo salama salimini, kwanini nisimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniepusha na majanga yale.

Aki! mbona ningeteseka ugenini kama ningelipoteza miguu yangu au kama nigelipoteza jicho langu la kushoto, wakati huo huo nimekwisha poteza jicho la upande wa kuume mmh! Nilipoteze na hili lililobaki kwa bahati nasibu? Mmmh! Janaba,mmmh!  Huruma jamani.

                “Samahani Bwana mkubwa nina upofu jicho langu la kulia hili lililosalia halioni vema, ndio maana nimevuka pasina kuwa mwangalifu.” Nilijitetea ili kupunguza hasira za yule Bwana mkubwa macho ya wengi yalinitazama , macho ya wengi yalitamani kujua mwisho wa ile sinema yetu.

                “Aaahh! Kumbe una upofu wa macho, ooh! Pole sana kijana.”  Yule kibosile alinipatia mkono  wa faraja mara baada ya kumueleza matatizo yangu.

              “Pole sana kijana wangu, embu nieleze ni wapi unaelekea ndani ya jiji ?” Bwana mkubwa aliniuliza.

              “Sina pahali pa kwenda bwana mkubwa, mimi ni mgeni ndani ya jiji, nimetokea Iringa kijijini nimekuja jijini japo kubahatisha  labda nitapata kazi itakayo niwezesha na  itakayonibadirisha kimaisha.” Niliongea kwa kirefu, nilitia huruma kama kondoo mwenye kuhitaji maji na chakula,  nikiwa nimeshikilia kibegi changuo chenye nguo mbili tatu pamoja na fedha za kujikimu.
                

“Oooh! Pole sana mdogo wangu, embu tuokoe muda kidogo, ingia ndani ya Gari yangu tutoke eneo hili, niko bize kidogo ninaelekea Kariakoo kwenye mishe mishe zangu? Yule bosi aliongea.

Je, niingie au nisiingie ndani ya ile Gari ya huyu kibosile? Nilijiuliza. Swali lililonijia ghafla ndani ya kichwa changu.

Wacha niingie tu, yawezekana ikawa ni zari la mentari. Nilijisemea mimi na moyo wangu kisha nikaingia ndani ya gari ya yule Bwana mkubwa. Nilipotaka kuketi nyuma ya siti ya ile gari Bwana mkubwa alinikataza nisikae nyuma akaniruhusu nikae mbele ya Gari.

               Harufu nzuri ya marashi pamoja na manukato yalipamba pua zangu, nilijisikia aibu  kidogo sababu mnuko wa mavazi yangu niliyotoka nayo kijijini uliingia ndani ya ile Gari na kutibua hali ya hewa, japo yule bwana mkubwa hakujali  kuhusu hali yangu ya kutibua hewa alikwisha kufungua vioo vyote vya ile Gari ili hewa nzuri ipite na kuingia au kutoka ndani na nje ya ile Gari na uzuri wake yule Bosi aliwasha kiyoyozi (AC) kilichofungwa ndani ya Gari yake kikatuperuzi peruzi kwa ubaridi wake na kutumiminia hewa safi ya kupendeza.

                “Niite Bwana Steven Biko, ni meneja wa kiwanda cha kutengeneza, kusambaza na kuuza bia ndani na nje ya Tanzania.” Yule Bwana alijitambulisha kwangu.

               “Je wewe ni nani mwenzangu? Ningependa kukujua zaidi.” Aliongea yule bosi akiendelea kuiendesha Gari yake, wakati huo huo nilijua kuwa tunaelekea kariakoo, kama alivyonieleza.”

                “Asante sana kwa utambulisho wako Bwana mkubwa.” Nilimshukuru yule bosi nikimtizama kwa kutumia kile kijicho changu kimoja kilicho hai, ukitegemea jicho langu moja lilikwisha kupoteza uzuri wa kutazama.     

              “Mie naitwa  Bwana Job Mkwawa, ni mzaliwa wa Iringa kijijini, kabila langu mhehe umri wangu miaka ishirini na mitano, sina mwenyeji hapa mjini, kama nilivyokueleza , nimekuja mjini kutafuta maisha nitafurahi kama nitafanikiwa kupata nafasi ya kazi, sijali ni aina gani ya kazi, yoyote ile nipotayari kuifanya Bwana wangu niliongea kwa matumaini ya kusaidiwa,

               “Ah! Kumbe Bwana Job wewe ni mwenyeji wa Iringa?” yule bosi aliyejitambulisha kwa jina la Steven Biko aliniuliza akiwa na kiasi kikubwa cha tabasamu mdomoni mwake.

                   “Ndio Bwana  Steven Biko .” nilimjibu yule bosi, wakati huo huo jicho langu moja linalofanya kazi lilikua likishangaa shangaa umati mkubwa wa watu waliokuwa bize wakielekea kwenye miangaiko yao.


                    “Waooo! Kumbe nimekutana na mtani wangu, mimi ni Mnyakyusa nyumbani kwetu Tukuyu Mbeya, nilizaliwa huko nikapewa elimu yangu na baada ya kumaliza chuo nilipata ajira ndani ya kampuni ya Bia.” Steven Biko aliongea, mie nikajawa na furaha mara baada ya kugundua kumbe nina mwenyeji wangu amabaye ni mtani wangu na uzuri wa yule mtani anatokea mkoa ulio karibu karibu na nyumbani Iringa.

Gari iliendelea kuchanja mbuga mie mshamba na mgeni ndani ya Jiji hili nilikuwa mtazamaji, nikitizama uzuri na urembo wa lile Jiji, lililopangiliwa na kupangika kwa wingi wa mahorofa, balabala zenye ubora na uzuri wake, wafanyabiashara ni wengi pomoni kila mtu yuko bize na shughuli zake, shughuli  za kujitafutia riziki na bahati ya kila siku.

                 “Tupo wapi hapa mtani wangu?” nilimuuliza Biko mtani wangu.

“Hapa ni katikati ya jiji panaitwa Kariakoo, mbele kidogo njia ilee (akainyoshea mkono) ni barlabala ya kwenda Posta. Posta ni sehemu wanayoishi watu wenye fedha zao, wazito wa ndani na nje ya nchi, kule kuna maofisi ya viongozi wa serikali mabalozi wa mataifa mbali mbali wapo kule, kule ni paradise ndogo yenye kuvutia.”

               “Kumbe Jiji hili ni lenye fahari kubwa sana?”

                “Yes, huu mji ni johari ya watalii na wgeni wengine wengi, wanaokuja kwa ajiri ya shughuli zao za kila siku.”

                “Dah! Nitafurahia sana iwapo siku moja nikipata nafasi ya kulizunguka jiji.” Niliongea kama vile tayari nimekwisha kulizoea hilo jiji.

                 “Ondoa hofu mtani wangu, ipo siku nitakupeleka baharini ukazione meli, si unazijua meli au unazisikia tu?”
                 “Nazisikia tu wala sijapata kuziona.”

                  “Hilo sio tatizo kikubwa ni kumwomba Mwenyezi Mungu uhai na uzima ili siku moja tupate kwenda kufurahia raha za jiji.” Biko aliongea.

                 “Pesa pekee ndiyo inayoongea kijana wangu, hili ni Jiji la raha na starehe. Raha na starehe pasina pesa ni kazi bure.” Biko aliongea kama vile mie na yeye tumejuana muda mrefu sasa kumbe tumefahamiana dakika chache zilizopita, tena kufahamiana kwetu ni kwa bahati tu.”

               “Shukrani mtani wangu, siku nitakayotembezwa ndani ya Jiji itakuwa ni siku ya furaha kubwa kwangu,” niliongea kwa furaha.

                “Bwana Job nina swali nahitaji kukuuliza” Biko alinishitua kidogo, nikamuitikia kwa kutingisha kichwa kumuashiria kuwa ruhusa ya kuuliza imekubaliwa.

                “Vipi kuhusu elimu yako, umesoma hadi kufika levo gani?”wakati huu Gari ya bwana Biko ilikua ikingia ndani ya kiwanda cha BIA, nilikitambua kiwanda kile kuwa ni cha BIA kwa sababu kilikua na bango lililoandikwa Tanzania Brew company limited (TBL)

                “Kidato cha nne ndio kiwango changu cha elimu,” Niliongea

                 “Oooh! Safi sana, kijana unaonekana unanguvu za kutosha kufanya kazi, kwa juhudi kwa maarifa na kwa ufanisi mkubwa pamoja na moyo wa kujituma.” Biko aliongea maneno ya kutia matumaini nami nikakoleza chumvi.

                “Yes l can do so soninaweza.” Nilimjibu kwa kimombo kilichochanganyikana na Kiswahili. Bosi aliipaki Gari yake karibu na Ua kubwa lililiopo ndani ya kiwanda kile.
                “Safi……Good.”  Biko aliongea , tukatelemka kwenye Gari yake, nikamfuata kule anakoelekea, nikiwa nyuma nyuma kama umbwa amfuataye Bwana wake, mikononi nalikua nimekumbatia  Begi langu kuukuu lenye nguo kuukuu.

                 “Wacha nikwambie kwa kifupi bwana Job, wewe una bahati kubwa sana kuonana na pia kujuana na mimi, kampuni imepungukiwa wafanyakazi, kwa hiyo tunahitaji wafanyakazi wa kutosha, jihesabie kuwa ni mtu mwenye bahati, kazi tayari ipo mikononi mwako, wewe utakuwa ni miongoni mwa wafanya kazi wa kampuni yetu. Usijiulize moyoni kwanini nimekupatia nafasi hii ni kwa sababu ninajua kuwa wewe unahitaji kazi na kazi tayari umekwishaipata.

                “Waoooo! Moyo wangu uliliripuka kwa shangwe japokuwa bado sikujua ni nafasi gani ya kazi ambayo napaswa kuishughulikia hilo halikunitia wasiwasi nilihitaji kuwa na subira subira yavuta heri, nitaambiwa hapo baadaye ninapaswa kufanya nini?

               “Bwana Job nitakupatia nafasi ya kuingia kwenye utengenezaji wa kilevi hiki kinachopendwa na  watu wengi ndani na nje ya Afrika mashariki. Kwanza kabisa utafundwa namna ya kutengeneza Bia na baada ya  sisi kuridhia uelewa wako katika utengenezaji wa Bia ndipo utaingia jikoni kuuchochea moto ili tengenezo lako likamilike na uzuri wa kazi yako  hautakuwa pekee utaambatana na wenzi  wako wengi  mtagawana majukumu mbali mbali ya jikoni.” Aliongea Steven Biko ameniacha mdomo wazi nisitake kuamini bahati kubwa kama hii , yaani leo hii hii ninaingia ndani ya Jiji  ninabahatika kupata nafasi ya kazi hata kabla ya kutanga tanga na njia.

              Bwana Steven biko aliniingiza ndani ya  Ofisi yake, Ofisi moja nzuri ya kitalii, ofisi ile ina mvuto, sio wa kuhadithia kwa maneno matupu yatokayo mdomoni mwa watu, bali ni kwa matendo thabiti kwamba imeboreka na kuboreshwa. Imepambwa kwa tunu na medali mbali mbali ambazo kampuni hiyo ilizitwaa baada ya ushindi mnono uliotokana na ushindani wa makampuni.
      
        “Nitakupeleka kinyerezi, nje kidogo ya mji wa tabata ninamiliki nyumba yangu moja huko, ipo ipo tu hakuna mkaaji wewe ndiye utakaye kuwa mkaaji hapo,” Biko aliongea moyo wangu ulifulumia kwa furaha na shangwe isiyo na kifani. Kitendo cha Biko kuniamini namna ile kilinishangaza,  bado ni mgeni kwenye macho yake hanijui wala simjui vizuri. Jambo hili ni lenye heri na fanaka ni Baraka tele  kwangu, nikajiona na kujisikia kuwa ninapendwa pendo ndani ya pendo.

  Muda si mrefu alikuja binti mmoja mrefu mwembamba, ana macho  yenye mboni za paka, ngozi yake ya kiaribino nywele zake zina rangi ya kaki, haijakolea sana. Biko alinitambulisha kwangu kuwa huyo ni Secretary wake. Jinale Riziki. Riziki akatuburudisha kwa kutuandalia vinywaji  soft, matunda na  vitafuno vya kuburudisha midomo yetu. Sikupenda mtoto riziki apite zake na kuondoka kabla sijajitambulisha.

 nikajitambulisha kwake  Riziki alifurahishwa na uwepo wangu akanikaribisha kwa moyo wote mimi kama mfanyakazi wa pale.

                  Hatukukaa sana pale kiwandani Steven biko alihitji nikapumzike kwenye nyumba aliyo niandalia, nilikuwa na shauku ya kutaka kuiona hiyo nyumba aliyonieleza Steve.
                     ################################
                  Looh! Kumbe Dar es salaam ni Jiji zuri machoni kwa wengi wanao ingia na kutoka, kweli macho hayana pazia mtu usikubali kuambiwa  njoo ujionee wewe mwenyewe.  Juma mosi ya leo Bosi wangu alimuomba Secretary wake Riziki anitoe out. Nikaangaze angaze macho yangu huku na huko, nikapoteze ushamba wangu wa kihehe, nikafurahie mandhari ya waswahili,  wapemba, wazaramo na waruguru. Nikajionee fukwe za bahari ya Hindi, majumba ya kisanaa pamoja na mitaa mbali mbali iliyopo ndani ya jiji lililobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa na kila kizuri majaliwa. Kwa kifupi Dar es salaam ni mbingu moja nzuri yenye paradise ndani ya dunia.

              Kizuri, hakikosi kasoro, jiji la Dare s saalam sawa ni Jiji zuri linalopendeza machoni, lakini pia hata hivyo Jiji lina mapungufu yake kwa mfano mitaa ya kariakoo kama vile Faya, Big bone, na Mnazi mmoja Sekondary ni maeneo yaliyo jaa vibaka, mateja na wahuni wengine wengi. Mitaa ya Buguruni haswa  haswa Buguruni sokoni uchafu umerindimaa ni rahisi sana kwa magonjwa kupenya.
Nenda kigogo  ya mburahati, nenda jangwani, maisha ya watu wa huko ni ya chini sana umasikini uliopo maeneo hayo ni umasikini wa kuogopesha ni kama vile hawana serikali waungwana hawa ni kama vile Serikali haiwasaidii waja wa Mwenyezi Mungu, majanga mbali mbali kama vile magonjwa ya milipuko (kipindu pindu) na mafuliko ni moja ya taabu zinazo watesa waja hawa.
Kwa kifupi mtoto Riziki alinionesha uzuri na ubaya wa Jiji lenye mamilioni ya watu, jiji lenye maelfu ya Magari majumba ya fahari na biashara za kila aina. Binafsi nilihisi kukaribishwa, binafsi nilijiona nipo nyumbani, ukarimu na mapenzi niliyopewa ulinihamasisha na kunitia moyo wa kutafuta yale maendeleo ambayo ndiyo nimekuja kuyatafuta ndani ya jiji la Bongo land.

Hazikupita siku nyingi nilianza kazi ndani ya  kile kiwanda cha BIA, nilifunzwa  nini ninachopaswa kufanya mimi kama mimi ndani   ya ilekampuni, nilifunzwa nikafunzika, upishi wa pombe  ndio ulikuwa wajibu wangu niliwajibika ipasavyo. Nikikumbuka kuwa hapo awali kabla ya kuja ndani ya jiji nilikuwa mlevi wa kutupwa mlevi mwenye cheo ndani ya Bunge la walevi, Spika wa Bunge la walevi. ajabu iliyoje mara baada ya kulihama Bunge la walevi cheo changu kimeshuka kwa asilimia 95 kutoka kwenye uspika wa Bunge la walevi hadi kuwa mpishi wa pombe ya walevi mmmh! Mengine makubwa, madogo yana nafsi zake, sio mbaya yajayo yanafurahisha.

                    Any way nisiache mbachao kwa msala upitao, mcheza kwao utunzwa, mjasiri  aiwachi asili, kila ndege ana kwao kuzuri kwenye matunzo, na mimi ninaye mama, mama yangu  hakukwama kunilea na mama yangu si mwingine zaidi ya Bibi mlezi wangu, yule aliyenipatia deko na madekezo. Na mimi ninaye Baba na Baba yangu si mwingine ni yule yule Babu yangu aliyenilea nami nikaleleka kwa deko na madekezo. Upendeleo wao ni upendeleo mkuu, malezi yao ni malezi ya kuku na yai, hawakunipiga, hawakunifokea, hawakunikemea na kunikwaza kwa jambo lolote lile.
                ##########################
Miezi sita ndani ya kile kiwanda cha bia, nilibadilika sana, tabia ni mazoea, mjasiri aiwachi asili. Ule ulevi wangu wa kutupa ulinivamia tena ulinivamia kwa kasi ya ajabu, muda mwingi niliutumia kunywa pombe na uzuri wa hiyo pombe naliipishi mie mwenyewe, nilikua huru kunywa pombe mara baada ya kumaliza kazi yangu ya upishi. ‘Mie ndie mpishi, muda mwingi nipo mekoni, wacha niitumie hiyo fursa kuuburudisha mtima wangu kwa pombe,’ Naliwaza.

                Ndio maana kusema mazoea yana tabu,mtu kuzoea kitu, Aki! kukiwacha ni vigumu ajabu, muda wote uwaza jinsi gani lile pendo alilolipenda liingie moyoni mwake tena. Bosi wangu, Bwana Steven Biko hakuwa na longolongo juu ya ulevi wangu, aliniachia uhuru wa kuamua nilitawale Jiko nililo achiwa ili nipike na kupakua.
Mshahara wangu, marupu rupu pamoja na posho za mara kwa mara, bosi wangu Steven Biko alinipatia tena alinizidishia mara mbili zaidi, akinitaka niendelee kuchapa kazi pasina longolongo, pasina matata uvivu na uzembe, nilikua mtiifu kwenye ile mishe(kazi) nilikuwa siriasi japo ulevi kwangu ilikuwa ni vigumu kuukataa.

Itaendelea



OBIMO CHETA

 OBIMO CHETA (MY LOVE REMEMBER). Siku Derila alipokutana na Singa, ilikuwa ni siku nzuri, siku ya kusheherekea sikukuu ya Christmass,🌲🎄⛪...