Saturday, August 23, 2025

WATOTO WANGU FREDO NA NELISO ๐Ÿ’•๐Ÿ˜ฟ

 



NILIWASOMESHA WATOTO WANGU KWA TABU SANA,๐Ÿ“š๐Ÿ“‘ WALIPOISHIWA ADA๐Ÿ’ฐ YA CHUO๐Ÿ‘จ‍๐ŸŽ“ WAKANITIMUA NYUMBANI KAMA PAKASHUME๐Ÿˆ‍⬛.


WEMA WA MUNGU ULIPONIZUNGUKA GHAFRA NIKAWA BILLIONEA๐Ÿฆ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ธ๐Ÿ’ฒ WALIPOSIKIA ๐Ÿ‘‚KUWA NIMEKUA BILLIONEA WAKAANZA KUNITAFUTA ATI NIWASAMEHE.๐ŸงŽ‍♂️๐ŸงŽ๐Ÿ›


    "Maua ๐ŸŒนpamoja na wewe Adam  kuanzia Leo hamtakiwi kuonekana hapa shuleni,๐Ÿšท kosa mlilolitenda ni kosa kubwa, kufukuzwa kwenu Shule ๐Ÿซ๐ŸŽ’iwe fundo Kwa wengine."Mwalimu mkuu Bwana Chikoko๐Ÿ‘จ‍๐Ÿซaliongea kwa ukali.


      "Tunaomba utusamehe Mwalimu mkuu, hatukujua kama lile tendo lingelipelekea matokeo haya." Adam alilia,na mimi  Maua pia nililia.๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ฟ Ilikua ni lazima tuondoke pale shuleni sababu baada ya mie Maua kukutwa na ule ujauzito nililazimishwa kumtaja aliyenipa ule ujauzito.


    "Hamkuwekeza akili zenu kwenye elimu mkombozi wa maisha mkawekeza elimu kwenye tamaa za mwili zinaa na ujinga. Bodi ya Shule haiwezi kuwaacha mkasababisha Samaki mmoja aoze na wengine wafuate kuoza. Kamateni Barua๐Ÿ“ƒ zenu, wapelekeeni wazazi wenu na muwaambie hamtakiwi Tena kuwepo hapa Shuleni." Mwalimu mkuu alipaza sauti.


      "Please forgive us Sir." Tulipiga goti chini ndani ya Ofisi ya Mwalimu mkuu lakini Mwalimu mkuu hakutujali wala kutusikiliza, tukaondoka kuelekea nyumbani kwetu, tumejaa machungu, majuto na masikitiko.Tulipofika majumbani kwetu, nyumba hazikukalika, fimbo hazikutulia, fimbo nzito ziwakazo moto zilitua makalioni mwetu. Tulifinywa kwa visu vilivyopakwa mapilipili. Tulitukanwa na kuonekana kuwa hatuna maana ndani ya jamii iliyotuzunguka


Mateso hayakukoma, ilikua kila siku tunateswa na ukitegemea mie Maua nalikua tayari mjamzito, nalihitaji amani na utulivu sio stress ambazo kwa bahati mbaya zingelipelekea mimba kuchoropoka. Adam akanishawishi  tuutoroke Mkoa wa Bongo na kuelekea Lushoto Tanga. Ikawa hivyo basi tuliiba nauri na vijipesa kidogo vilivyotusaidia kuingia Lushoto Kijiji cha Magamba. 


"""""""""""""""""""""""""""

      Miezi Tisa kutimu mie Maua nilikuja kujifungulia nyumbani watoto pacha ๐Ÿ‘ฌ Fredo na Nelso, wavulana Wazuri tuliowalea katikati ya maadili, uvumilivu, heshima, utii na kuipenda elimu. Kilimo kwetu kilikua ni utukufu tuliipanda miti ๐ŸŒด๐ŸŒณndani ya shamba kubwa alilolinunua Adam, tuliipanda pia viazi, ๐Ÿฅ”karroti,๐Ÿฅ• makabeji ๐Ÿฅฌna matunda kama ma tufaa ๐Ÿ na mapeas๐Ÿ. Kila senti tiulioipata kutokana na kilimo tuliitunza kununulia mifugo ya nyumbani: Ng'ombe๐Ÿ‚, mbuzi๐Ÿkondoo ๐Ÿ‘kuku๐Ÿ“๐Ÿˆ๐Ÿ–๐Ÿฐ na mabata๐Ÿฆ†. Kidogo kidogo maisha ya uvumilivu yalitukubali.



    Fredo na Nelso  walikuwa na kuongezeka haraka sana. Tuliwapeleka Shule na kuwataka wasome sana Ili siku moja waje kuwa Madaktari bingwa waje kuwasaidia binadamu maana kusaidia binadamu ni wajibu wa kila mwenye moyo na roho nzuri. Hatukuwashauri wajiingize kwenye kilimo maana kilimo kilivyokua kigumu sijui kama wangeliweza.



      Ghafla janga zito likaibuka na kuikumba familia yetu, Adam akiwa Shambani akilima kwa kutumia Jembe la mkono alishituka kumwona Ng'ombe aliyepandwa wazimu akimwendea kwa kasi na kumfuata pale alipokua akilima. Adam wangu Aliogopa akaacha kilimo akaanza kukimbia lakini walisema wahenga mbio za sakafuni uishia ukingoni, hakuna marefu yasiyo na ncha Adam aligongwa kwa pembe ya yule Ng'ombe kichaa akapigishwa huku na kule tena akapiga kelele za kuomba msaada, wakulima wenziwe waliposikia kelele zake wakaacha kulima na kwenda kumpa msaada mwenzao.


     Yule Ng'ombe๐Ÿ„ kichaa tayari alikwisha toweka, wakulima walipofika pahali alipolala Adam wakamkuta Adam wangu anakata roho. Tumboni damu ๐Ÿฉธzimejaa na utumbo umetoka nje ya tumbo maana yule Ng'ombe alimbutua tumboni. Wakulima wakiwa ni wenye uchungu na majonzi wakambeba Adam na kumleta nyumbani. Huku kilio kikuu kilipasua anga. Nililia mie Maua, walilia wanangu pacha Fred na Nelson.


Kumpoteza Adam Mume bora na Baba bora kwetu tulihisi tufe la Dunia limetuangukia.๐ŸŒ Uchungu mzito ulituvaa miilini tukajivisha magunia na kujimwagia majivu kama tumepandwa Maruhani.๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ‘น


         Baada ya mazishi ya Adam Mume na kichwa cha familia yule mbeba majukumu ya nyumbani, nyumba yetu ikapooza sababu mahitaji mengi yalikosekana tofauti na Kipindi alichokuwepo Adam tuliyafurahia maisha ya uvumilivu sio haya ya mie kuitwa Singo mama, mengi mazito kupambania.


Ilinibidi nianze kufanya kazi mbili kwa nyakati tofauti angarau nipate pesa za kuhudumia familia, nikapambana na kilimo wakati huo huo nikaanza kufanya vibarua vya kusafisha nyumba za mabosi: kupuguta deki, kufua na kuhudumia meza. Hakika Jua๐ŸŒž lilinikomesha.


     Nilihitajika nyumbani kuandaa chakula, nilihitajika Shambani kulima, bado vibarua vidogo vidogo viliniita na kunifuata. Nilihakikisha watoto wanakula, kunywa na kuvaa.Tena watoto wanasoma kwa bidii Ili watimize ndoto zao za kuja kuwa Madaktari bingwa na Mola wetu asivyo mbahiri wala choyo wanangu walikaza kamba hadi kuingia Muhimbili university kusomea mambo ya Udaktari.๐Ÿฉบ⚕️๐Ÿ’Š


     Maisha ya Chuo yalikua magumu sana, ada ya Chuo ilikua mzigo ingawaje walikubaliwa kupata mikopo ya masomo lakini bado tu mahitaji yao yaliongezeka ukijumlisha starehe na anasa zao za ujanani. Wakati Mama yao nikipambana na kilimo pamoja na kusafiri masafa marefu hadi Tanga mjini kusafisha majumba ya mabosi na majumba ya wenye pesa zao, huku nyuma wanangu walifanya anasa na starehe za ujanani. Hatimaye sasa pesa sabuni ya roho ziliwaishia vibaya wakakosa ada ya Chuo na kurejeshwa nyumbani.



     Walipofika nyumbani nilimwambia acheni Mama yenu nipambane lazima mtarudi Chuo kuendelea na masomo. Kweli kweli walikubali kubaki nyumbani kunisaidia kilimo๐Ÿช“๐Ÿ…๐Ÿฅ” na shuhuli za ufugaji, ๐Ÿ‚๐Ÿ๐Ÿ„๐Ÿwakati huo mie Mama yao ninafanya vibarua kwenye majumba ya mabosi na watu wenye pesa zao.


     Siku moja niliporudi kutoka kwenye vibarua vyangu niliwakuta wanangu wanajadiliana kuhusu shamba lile kubwa ambalo Adam baba yao alipanda miti:๐ŸŒณ๐ŸŒฒ๐ŸŽ‹


    "Maisha ni magumu Mama tukiendelea kukaa hivi hivi tutapoteza nafasi ya kusoma Chuo" Fredo aliongea.


     "Vumilieni wanangu, pesa zitapatikana tu. Mbali na kufanya vibarua nitawaomba mabosi wanipe mikopo itakayowawezesha mrudi Chuo." Niliwapooza Kwa maneno ya matumaini.


     "Mama hatuwezi na kamwe hatuwezi kuendelea kusubiri masomo yaaendelee kutupita." Nelso aliongea.


     "Wanangu Mimi kama Mama yenu nimewaambia msubirie na nyie hamtaki kwahiyo nifanye nini?"๐Ÿ˜” Niliwauliza.


     "Huna la kufanya Mama lakini sisi tutafanya jambo la maana." Fredo aliongea maneno ambayo sikuyaelewa.


     "Mtafanya kitu gani? Mnataka kurejea Chuo mikono mitupu." Nilihoji.


      "Pesa zipo Mama na pesa lazima tuondoke nazo." Fredo alijibu.


       "Unajua sikuelewi Fredo au siku hizi mmeanza kuvutwa bangi mchana kweupe? Pesa ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ดziko wapi?" Nilianza kuzichukia akili za vijana wangu.


    "Baba si alituachia shamba, Hilo Hilo litatutosha kurejea Chuo." Neliso alinishitua.


     "Nini!? Mnalitaka shamba aliloliacha marehemu Baba yenu liuzwe? Haitawezekana, shamba Hilo ndilo litupalo kula na kutuweka hapa kijijini." Niliwaonya wasithubutu kuligusa shamba aliloliacha Baba yao Adam.


     "Huwezi kutuzuia Mama elimu ni bora kuliko kilimo kinachoumuza migongo na mikono. Lazima shamba liuzwe Ili turejee Chuo ili hapo baadae tuje kuwa msaada kwako." Fredo alitilia mkazo wa kuliuza shamba.


     "Never Fredo, never. Mkitaka nitoe radhi na kuwakasirikia jaribuni kuligusa Shamba aliloliacha Baba yenu." Niliwapiga kibuti kisha waliketi kimya. Muda si mrefu waliondoka kwenda  Bar ๐Ÿป, Ili kupooza koo zao kwa moja moto, moja baridi. Sikujali maana ujana ulianza kuwasumbua. Miaka ishirini na mitatu sio umri mdogo ni umri wa kijana kuanza kutamani vingi.

  
                                 ๐Ÿง‍♂️๐Ÿง‍♂️

Toba! Baada ya siku tatu kupita nilishangaa wanangu Nelso na Fredo wameongozana na Mzee mmoja aliyejulikana Kwa jina la Mzee Kapusi.๐ŸˆWaliponifikia waliamuru niache kulima lile Shamba ambalo Baba yao Adam alilinunua miaka 23 iliyopita.


       "Niache kulima ili iweje?" Niliwahoji.❓


       "Shamba tushaliuza Mama na Hati ๐Ÿ“ƒya shamba hii hapa. Bahati nzuri Baba kabla hajaaga Dunia aliandika majina yetu kwenye Hati kama walinzi wa hili Shamba. Fredo ambaye ndiye mkubwa aliongea.


        "Mmeliuza Shamba." Nilipata mshituko.

        "Hatukupi nafasi ya kusikiliza mara mbili mbili Mama, kuanzia Leo hili shamba sio lako au letu tushaliuza  kwa huyu Bwana Kapusi."

    
      "Wanangu mmeniua." Machozi na kilio cha kwikwi kilinitoka.


       " Mmeniua wanangu, mmeua rasilimali ya pekee inayotupa maisha hapa kijijini, tutakuwa wageni wa nani. Ooh! Nilijitupa juu ya shamba langu na kuanza kujigaragaza.


     " Sasa wewe ukitegemea tukae tu kusubiri iyo mikopo unayokopa Kwa mabosi? Tutasubiri Hadi lini? Jua likizama na siku kuyoyoma" Fredo aliniita uchungu na hasira


     "Mgekua na Subira wanangu lakini sio kuuza Shamba ambalo ndilo tegemeo la maisha yetu."


      "Hatuwezi kukitegemea kilimo, hatukuzaliwa kuwa wakulima. Tulizaliwa kuwa wasomi na Madaktari" sikutaka tena kuendelea kusikiliza ule upuuzi wa watoto wangu. Nikafanya kuondoka pale Shambani nikaeleka mtoni huko Nililia sana, machozi YANGU yakawa sawa sawa na maji ya mto. Jioni ilipoingia sikutaka kurejea nyumbani sababu nilikua nikilia tu na kumkumbuka Adam Mume wangu aliyeniachia watoto wasiokithamini kilimo.

Kiza kilipoanza kuingia niliona sio vema kuketi mtoni umbu wakinisumbua na kuninyanyasia damu yangu. Nikafanya kurudi nyumbani.


     Nilipofika nyumbani nilishituliwa na sauti za maradio๐Ÿ“ป๐Ÿ”˜☢️ spika yaliyokua yakitoa sauti za Muziki mzito wa Bongo freva. Sauti zilipanda juu Hadi ikawa kero kwa majirani hali ambayo haijazoeleka nyumbani kwetu.


     Ngo' ngo' ngo' ๐Ÿค›๐Ÿค›๐Ÿค›. Niligonga mlango Kwa hasira  mara baada ya kuchungulia dirishani na kuwaona vijana wangu Fredo na Nelson wakinywa vilevi vikali vilivyojazana juu ya meza  iliyopo sebuleni baya zaidi vijana wangu waliwakodi wasicha warembo kutoka mjini waje kucheza Muziki wakiwa nusu utupu.


    Ngo' ngo' ngo๐Ÿคœ๐Ÿคœ๐Ÿคœ' niligonga Tena lango la sebuleni.

       
    "We nani? "Fredo aliipunguza sauti ya Muziki na kuja mlangoni akiwa amelewa apepesuka.


    "Tafadhali Fredo nifungulie mlango muda si mrefu mvua itanyesha." Niliongea.


  "Mama hauna chako hapa nyumbani, shamba sio lako na nyumba sio yako pia." Neliso alipaza sauti wangali wameufunga mlango, Safari hii wote wamesimama Dirishani.


   "Nini nyie vijana? Mmerogwa nyie! Mnazipata wapi kauri hizi za kumvunjia Mama yenu heshima? Ama Kwa vile Adam Baba yenu aliwapa kipaumbele cha kuwaachia urithi? Urithi huo haukupaswa kuuzwa Mama yenu nikiwa hai."


    "Ukiwa hai au usipokua hai haitatusaidia sababu nyumba ni yetu na Shamba ni letu. Uzuri tushaliuza na nyumba hii tupo mbioni kuiuza." Fredo aliongea Kwa sauti Kali ya makaripio.


    "Fredo na Neliso, Mimi ndiye Mama yenu niliyewatunza ndani ya tumbo langu Kwa zaidi ya miezi Tisa ni Mimi ndiye niliyewalea Kwa tabu na Kwa shida Hadi mfike Chuo, Chuoni mnafundwa kuwadharau wazazi wenu?" Niliongea chozi likinibubujika.๐Ÿฅฒ๐Ÿฅน


     "Tafadhali ondoka Mama hapa hauna chako, kama ni suala la kututunza au kutusomesha tunasema Asante hata sisi tutazalisha, tutalea na kusomesha." Wanangu walitumia Lugha Kali sana.



     "Wanangu naomba mfanye utu na kufikiria Mama yenu asiye na baya, angalieni mtapata radhi na laana juu ya yule aliyewatabikia na kuwaangaikia. Tafadhali nifungulieni." Wanangu hawakutaka kunisikiliza, mvua kubwa ilianza kunyesha⛈️, wakayafunga madirisha na kuniacha nje. Tayari walikwisha kunitupia nguo zangu na vitu vichache muhimu, hawakutaka Mama yao niingie nyumbani kwangu.


       Nililia sana, Nililia machozi ya ndimu, Nililia na kumlilia adam Mume wangu aliyenijali na kunithamini inashangaza mara baada ya kifo chake watoto wananitia aibu. Oh! Masikini niliendelea kulia pale mlangoni.


       Watoto wamekataa kuniheshimu, watoto wamekataa kuwa watiifu yote sababu ya ujana, pesa, pombe na wanawake,wamenidharau Mama yao na kuniacha nje mvua ikiniadhibu. Loh! Kosa langu Nini mie?๐Ÿฅฒ Nilijiuliza lakini sikupata jawabu.



                        ๐ŸŒง️๐ŸŒง️๐ŸŒฉ️⛈️


Ile mvua kubwa uliendelea kunyesha, radi nzito ilipiga, niliogopa sana, niliogopa radi inaweza kuniua, watoto wangu hawakujali wala kunionea huruma. Nilifikiria labda niende kuomba msaada kwa majirani. Lakini nilihisi wazo hilo laweza kuwa ni usumbufu kwa majirani. Nikakimbilia kule shambani kwangu, kule shamba lishapigwa maokoto.


Nilijificha migombani, nikajizuia kwa kutumia majani ya migomba, baridi ilinitesa, mvua ilinitesa hadi pale ilipokata mbu nao waliona wamepata chakula, wakanifyonza damu yangu hakika ile ilikua siku nzito tena kwangu.


     Hasubui pambazuko ilinikuta nimepooza kwa kukesha shambani bila kupata lepe la usingizi, akili zilinitumaa kurudi nyumbani kwa watoto wangu nikaongee kiustaarabu na watoto wangu yamkini ni ujana ndio unaowasumbua, sio wale niliowazoea miaka yote ya furaha na huzuni. Basi mie huyo nikajibeba na kuelekea nyumbani kwangu nguo zangu zikiwa tipwa tipwa kwa kuliwa maji ya mvua.


     Nilipofika nyumbani kwangu 'eh!๐Ÿค”' nilijikuta nashangaa kumkuta Mzee kapusi๐Ÿ† akiwa katika hatua za mwisho za kufunga milango ya Nyumba yangu. Baada ya salamu nilimuuliza:


     "Kulikoni Mzee kapusi uifunge milango ya Nyumba yangu?" Mzee kapusi akanijibu kwa ufupi.


       "Haujui, au watoto wako hawajakushirikisha!?"⁉️


     "Sijui nini na wao kunishirikisha Nini?!"๐Ÿ˜•


     "Mama Nelso usijizime data na kujitoa ufahamu tafadhali. Watoto wako wameniuzia hii nyumba na tayari wameondoka kurudi Dar es saalam, Ina maana hawajakushirikisha."



    "What!?⁉️" Presha ya taratibu ilianza kupanda na kushuka, mwili wangu ulichoka nilikua kama mzigo mzito ulio karibu kudondoka. Lo! Nguvu ziliisha, nilidondoka chini puui! Kama gunia la mapumba.



     "Nilikuja kuzinduka nikiwa nimezingirwa na majirani kibao wakinipulizia pulizia kwa vitenge vyao wengine wakilia wakidhani tayari nimeaga Dunia. Kumbukumbu ziliponijia nilianza kulia kama mtoto nikiwalaani watoto wangu Fredo na Neliso kwa ubaya walonitendea Mama yao mzazi.


     Majirani wema walinichukua na kunihifadhi majumbani kwao, kisa changu kiliwahuzunisha sana, wao pia walishangaa wakashindwa kuamini kama kweli Fredo na Neliso wanaweza kunitendea ubaya ule mimi mama yao jamani, ilikua ngumu kumeza.


~~~~~~~~~~~~


    Wiki mbili kupita nilihitaji kurejea kazini Nyumbani kwa Mzee Bushiri, nikafunga Safari hadi Nyumbani kwa Mzee Bushiri, yaani Bosi wangu Mzee yule mpole hakuniuliza Wala kunifokea kwanini nimechelewa kurudi kazini? Niligundua Mzee Bushiri alikua na wasiwasi juu ya mwonekano wangu tangu niliporejea kwake nilikua ni mnyonge, ile furaha na uchangamfu niliiozoeleka kua nao sikua nao tena, lile tabasamu alilozoea kuniona nalo Kila siku likachukua nafasi ya huzuni. Mara nyingi niliinama na kuitazama chini machozi yaishe nibubujika.



       Siku tatu mbele nikiwa ndani ya Mjumba ๐Ÿก๐Ÿ˜️wa Mzee Bushiri baada ya kumaliza shuhuli za kila siku nilitoka na kwenda katikati ya bustani huko niliketi pekee yangu nikilia kwa uchungu na kuomboleza juu ya kifo cha mume wangu Adam, pamoja na huzuni waliyoniachia watoto wangu Fredo na Nelso. Kumbe wakati mie namwaga chozi Mzee Bushiri aliniona akanifata.


       "Maua Mtumishi wangu Kwanini unalia, nieleze sababu nini hadi ulie kila siku." Alinishika bega jambo ambalo sikulitarajia kama Kuna mtu anitazama ninalia pale Bustanini.


     Mazito yamenikuta mie Mzee wangu." Nilisitasita kueleza changamoto iliyonisibu lakini 'piga ua' Nilipiga moyo konde na kumueleza changamoto zangu.


      "Mazito gani embu nieleze naweza kukusaidia." Mzee Bushiri Baba aliye jaa wema na hekima hakunibagua zaidi ya kunionesha faraja na upendo.


     "Nilimpoteza Mume wangu ambaye alikua ni nguzo muhimu ya familia hata baada ya kumpotezea mume wangu watoto hawaoneshi kunijali au kunithamini, hawatambui kuwa damu ni nzito kuliko maji, wamesahau uchungu wa Mwana mzazi anaujua, wameuza mashamba aliyoyaacha mume wangu baya zaidi watoto wangu wamenifukuza Mama yao kama Umbwa๐Ÿ• koko." Machozi yalishindwa kunivumilia yakarejea tena kunidondoka.๐Ÿ˜ฟ


     "Dah! Kizuri mpe ng'ombe sio binadamu." Mzee Bushiri aliongea.


     "Nahitaji kukusaidia." Mzee Bushiri aliongea tena. Niliacha kulia,nikamtazama usoni nikiwa nimeivaa sura ya kuonewa huruma.๐Ÿฅน


     "Nitashukuru Baba yangu utakua umenifuta chozi la uchungu maana jasho la mnyonge haliendi tupu, chozi lilinibubujika upya.


     "Usilie kesho jiandae tutoke twende Lushoto pale pale ulipodhurumiwa haki zako, pale ulipotimuliwa na kufukuzwa kama Umbwa. Kila ulichpoteza kitarudi pale pale." Moyo wangu ilianza kuingiwa tumaini, furaha yangu ilianza kurudi kwa kasi. Tabasamu lililopotea lilianza kurudi kwa kasi. Nilihisi zile ni ndoto za akina Abunuwasi, lakini wapi! Kila neno alilonena Mzee Bushiri lilijaa ukweli. Akanikumbatia katikati ya faraja kuu.


                               ๐Ÿค—๐Ÿฅน๐Ÿค—

Siku iliyofuata tulifunga Safari ya kuelekea Lushoto Kijiji Cha Magamba tulifika pahali pale haki zangu zilipopokonywa kwa nguvu za watoto ๐Ÿค—๐Ÿค—wangu. Mzee kapusi aliitwa mbele ya tajiri wangu Bushiri ambaye alimshawishi Kapusi kuiuza upya ile nyumba aliyoinunua kwa watoto wangu Fredo na Neliso. Kapusi mbele ya pesa hakuwa mdogo alishawishika kuipokea offa ya shilingi million Therathini ukitegemea yeye aliinunua ile nyumba kwa kiasi cha shilingi millioni kumi na Tano.  Shamba langu alilolinunia shilingi million Tano Bushiri alimpa offa ya shilingi millioni kumi na Tano.


    Mali zangu zilirudi, furaha yangu iliongezeka Sasa nikawa mmiliki wa zile Mali ambazo Adam alitoa wosia watoto wetu wawe warithi. Pamoja na huruma zote alizonifanyia Mzee Bushiri Bado tu aliingia gharama za ukarabati wa nyumba aliyoninunulia upya. Shamba langu liliboreshwa na uzuri wa yale maboresho Bushiri alininunulia mashamba  mengine matatu na vifaa vipya vya kilimo. Furaha yangu ikarejea, shukrani nyingi na sadaka zenye furaha, Mola wangu alizipokea. Nikajiona mimi ni mwingi wa bahati.

๐Ÿค›๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š


      Miaka mitano ilipita nikiwa ningali ndani ya nyumba ya Tajiri wangu mzee Bushiri, Mwarabu kutoka Omani,๐Ÿ‡ด๐Ÿ‡ฒ mzee aliyekula  chumvi nyingi, yaani mpole na mwenye huruma kwa watu, mtoa misaada na ufadhiri kwa wenye dhiki, shida na masumbuko. Alianza kuuugua homa za uzeeni na uchovu wa mwili aliugua sana hata macho yake yakawa mazito kufungua. Muda mwingi aliutumia kulala kitandani Mie Maua nikawa bize kumhudumia huduma zote muhimu  ili kuirejesha afya yake iliyoteteleka. lakini ya Mola mengi ya binadamu machache, Mola akamtwaa yule mzee, ๐Ÿฅน๐Ÿฅน Mzee akaaga Dunia na kuniachia machozi na kilio. Mzee alifariki juu ya mikono yangu, alifariki akiwa tayari amewatendea watu mengi mema na Bado tu alitamani kuendelea mema yake. Watu wengi walilia msibani kwake wakikumbuka mema na mazuri aliyowatendea, mtu mwenye roho ya huruma na kutenda mema pasina kungoja shukrani.


      Yakaanikwa matanga na matanga yakaanuliwa hapo ndipo nilijipapasa na kujua kwamba sina changu na pale nyumbani kwa marehemu Mzee Bushiri sio pangu nilitakiwa kuondoka haraka sana iwezekanavyo. Nikarejea nyumbani kwangu Lushoto Tanga.



   Harobaini kupita baada ya kifo cha Mzee Bushiri nilishangaa kuona magari yaapatayo kumi na tano yanaongoza na kusimama mbele ya nyumba yangu, nyumba alonijengea Mzee Bushiri. Kwanza niliogopa moyoni nilijua ni yale yale waliyonifanyia watoto wangu Fredo na Nelso kuuza nyumba yangu kinguvu pasina kinishirikisha lakini hapa hawawezi maana hati ya nyumba na shamba ina majina yangu.


  Yale malori yalikua yamejaa vitu mbali mbali vya nyumbani, kuanzia masofa, makabati , mafridge,vitanda na vyombo vya gharama. Yalipotua mlangoni kwangu akasimama mwanaume mmoja nadhifu, safi aliyevaa suti nyeusi na kiatu cheusi Cha kupendeza.



      "Bibi Maua huu ni wasia uliachwa na mzee Bushiri aliundika kabla ya kifo chake akikutaka uwe mmiliki wa mali zake zote, utajiri wake, mashamba yake, magari na makampuni."


     "Jesuu! Nilipigwa kelele na kunyanyua mikono juu kumshukuru Mola, majirani pia walishangilia kwa furaha,


       "Mzee Bushiri hakubahatika kuwa na ndugu au jamaa ndani ya Tanzania ndugu zake wote wapo, Oman na ni matajiri wa kutupwa kwahiyo mzee Bushiri aliona Hana mtu wa kumwachia Mali zake nyingi, utajiri na mapesa yaliyovundikwa Banki anakukabidhi wewe Bibi Maua" Nyie mimi ninashindwa kuieleza furaha yangu.



      "Lakini........" Mwanasheria aliyevalia suti safi na kiatu kinachompendeza aliongea.



      "Lakini Mzee Bushiri ameandika ndani ya wosia wake Mali na utajiri wako wote usithubutu hata siku Moja kuwaachia watoto wako, ndugu na jamaa zako. Iwapo Mola atakupenda na kukuchukua⚰️☠️ Mali zako zote zitwaendea watoto yatima. Wajane wagane watotot wa mitaani masikini na wahitaji." Mwanasheria alimaliza kuongea, nilipiga makofi  ๐Ÿ™๐Ÿ‘na kufurahia kwa Raha zangu zote. Nikaupokea ule Wosia na kuubariki. Basi yale maroli yakaanza kupangilia Mali zote ndani, nikawa Tajiri na Bilionea wa ghafra.

             ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ด๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ด


Fredo na Nelso walikuja kupata fununu Mama yao amepata Bingo la utajiri, Bilionea wa ghafra. Wakafunga Safari kutoka Dar es salaam hadi Tanga kwa lengo la kumuomba mama yao msamaha. Basi walipofika waliukuta ule mjumba alioniachia Mzee Bushiri getini Kuna walinzi wengi pamoja na mijibwa Mikali  inayotisha na kuogopesha. Waliishia kuogopa pale nje wakamwita mlinzi na kumweleza shida yao, mlinzi alikuja kunipa taarifa na mie niliyeishi kama Malkia๐Ÿ‘ธ nikatoka nje nipate kusikiliza shida zao, niliwakuta wamepiga magoti chini nje ya ule majumba wangu.



       "Karibuni nyinyi ni wakina nani na mnashida gani ambayo naweza kuwasidia."Waliposikia maswali ninayoqauliza walijikuta wanapigwa na butwaam wakanishangaa.


    "Mama umetusahau, mimi ni Fredo na huyu ndugu yangu Neliso. Sisi ni watoto wako tumemaliza Chuo lakini tunatangatanga mitaani kuokota chupa tupu๐Ÿผ๐Ÿงด na makopo tuuze ili tupate pesa ya Dagaa chukuchuku  na ugali. Vijana wangu walionekana kuchoka na kuchakaa tongotongo machoni, nywele tipwatipwa zenye mba chawni viroboto na papasi . Nguo zao zilijaa kunguni, miili yao iliota  ukurutu, visigino vya miguu yao  virijaa funza, fangasi na magamba kama ya Kobe.



         "Siwafahamu nyie na Wala Sina watoto wanaoitwa Fredo na Neliso. "Nikijifanya kuwasahau ingawaje uchungu uliniingia na kuniumiza moyo wangu pale nilipowaona wanangu waliopotea Leo wamepatikana wakiwa wameoza.



       "Mama, Mama, Mama  sisi ni watoto wako Baba yetu Adam alituachia Nyumba na Shamba tuka........" Fredo hakumaliza sentensi yake walianza kulia na kuumwaga chozi.๐Ÿ˜ฟ๐Ÿ˜ญ


        "Ondokeni hapa kwangu siwajui nyinyi rudini kwenye ile nyumba na Shamba la Baba yenu Adam" Niliongea kwa ukali ulioficha maumivu na uchungu juu ya wale watoto wangu. Nilitoa amri kwa walinzi wangu wafanye haraka kuwafukuza wale ombaomba waliowai kuninyanyasa hapo zamani. Umbwa ๐Ÿ•๐Ÿ•wakali walifunguliwa wakawatisha wale ombaomba waokotao chupa, wale omba omba wakatoka nduki na kukimbia kama vichaa wendawazimu.


Nilikua na maumivu makali hata nikajifungia chumbani na kulia  sana, Bado nilikua ninawapenda watoto wangu ingawaje wosia wa mzee Bushiri ulinitaka nisithubutu kuwapa kitu chochote kile alichoniachia.



       Basi nikamwita mmoja wa walinzi wangu nikamwambia enenda ukawatafute wale vijana wangu wawili Fredo na Neliso, wanunulie nyumba ya kuishi yenye kila kitu ndani, waketi humo, wale wanywe, wapewe chakula chao na mavazi tena wahudumiwe huduma zote muhimu, nikamwambia wape pia Pesa za kuwasaidia maishani mwao la zaidi watafutiwe kazi wanayoipenda kuitenda yaani Udakta ๐Ÿฅผ๐Ÿฉบlakini wasithubutu kuja kugusa Mali aliyoniachia Mzee Bushiri mali hizi sio mali zao Bali mi Mali zangu pamoja na watoto yatima, wajane., wagane, masikini na wahitaji. Mlinzi wangu akaenda kuwatafuta naye akawapata.



๐Ÿ˜š๐Ÿ˜™๐Ÿ˜—๐Ÿ˜š

TCHAO

☺️๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜Œ

Let love ๐Ÿ’ž lead.




 

No comments:

Post a Comment

BEKA

 SURAYA TATU                        “AKIPITA ATAJIPITISHA.” Beka akawa member wa kampuni ya SIGA, akipelekwa hapa na pale kulinda mali za ma...