Friday, August 8, 2025

BARUA YA MPENZI NUHU

        


      MAMA ALITAKA NIOLEWE NA MABWANA HARUSI WAWILI KWA MPIGO.

         Nilijigeuza juu ya kitanda changu kikubwa cha sita kwa sita๐Ÿ›Œ kitanda chenye matandiko safi na mito mikubwa laini ya kulalia, taa๐Ÿ’ก ya chumba changu ilikua ingali inawaka na kukifanya chumba changu kionekane katika ubora wake, kikang'ara mfano wa chokaa mpya. Niligeuka upande wa kulia kisha nikaupiga mwayo wa nguvu Aaaahhh๐Ÿ˜ฎ' ile nafumbua macho yangu nilijikuta nashtuka mshituko ๐Ÿ˜ฑ uliotaka kuuvunja mtima wangu.

   Jesu!! ๐Ÿ˜ณ Wewe nani? Macho yangu yalikutana na sura ngeni ya mwanaume mmoja tanashati ametinga suti moja nyeusi kwa rangi, Tai safi nadhifu, uso wake umeboreshwa kwa mafuta na mapodali. Aliniangalia.

      "Mie Bwana Harusi?"๐Ÿคต๐Ÿ’’Aliongea kwa tabasamu nono lisilokauka mtimani.

      "Mie pia,"๐Ÿ’’๐Ÿคต ๐Ÿค—Ghafla niliisikia sauti nyingine ya kiume nyuma ya mgongo wangu. Nilijigeuza kwa hofu na woga nikakumbana na mwanaume mwingine  zaidi ya tanashati, suti yake ya Blue na tai Moja safi akiwa amelala juu ya kitanda changu.

         "Jamani nyinyi ni wakina nani,❗ mbona siwaelewi?" Nilihisi nipo ndotoni japokua haikua ndoto zaidi ya uhalisia.

       "Funua blanketi, mwenyewe utaamini," Haraka pasina kupoteza muda nililifunua blanketi langu pale kitandani, Toba!๐Ÿฅบ Nilishangaa kuliona gauni zuri la Bibi Harusi likiwa limekaa mwilini mwangu.๐Ÿ‘—

      "Mambo yote haya yametendekaje? Nilijiuliza mtimani.๐Ÿ™ƒ

       Ghafla mlango wa chumba changu ulifunguliwa. Mama aliingia akiwa ameshikilia Bunda la Maua,  ๐Ÿ’๐Ÿต️alipofika kitandani kwangu akalitupa lile bunda la Maua katikati ya mapaja yangu  kisha akanena.๐Ÿ™„

       "Pamela nimeisubiria sana siku ya Leo, tayari umetimza miaka ishirini na mmoja nimekubembeleza sana mwanangu tafuta mchumba akuoe๐Ÿ’ lakini ulivyo 'mkaidi hafaidi' umenipuuza, hautaki mwanaume, hautaki kuolewa sasa nakuambia hivi utaolewa na hawa wanaume wawili๐Ÿ‘ฌ kwa siku moja. Toba! ๐ŸฅนMamangu alinishtua.

     "Mama sitaki kuolewa na kamwe haitatokea."Nililalamika.

     "Kama hautaki kuolewa na wanaume hawa wawili naomba uondoke ndani ya nyumba yangu" Mama alinifokea.

          Sitaki na  tena sitaki" Nilimpinga Ma'

   "Mimi sio muongeaji sana Pamela, wacha niingie chumbani kwako nikutolee kila ulichonacho nitupe nje ili tuone sasa nani mshindi kati ya wewe au mimi." Mama alidhamiria kunidharilisha. Akaelekea chumba changu cha siri, chumba nilichomficha mpenzi wangu Nuhu Mziwanda, yule ninayempenda na yule tutakaye funga pingu za Maisha siku moja. ๐Ÿ’


      "No Mama." Nilitoka pale juu ya kitanda nikakimbia mbio ๐Ÿƒ‍♀️kuelekea mbele ya mlango wa chumba changu cha siri kule nilikomficha Nuhu. Nikasimama mlangoni, nikamzuia na kuziba Mama asiingie asijemkuta niliyemficha chumbani.


       Mama tafadhali naomba usiingie chumbani, ninaomba unipe muda wa dakika ishirini nitafanya maamuzi na machaguzi juu ya mchumba nimtakaye." Wakati huo nilikua nimeziba mlango wa chumba changu taiti Mama asiingie.


      "Ok. Ninakupa dakika ๐Ÿ•›ishirini tu uwe tayari sebuleni kufanya maamuzi la sivyo nitakuvuruga Binti yangu." Mama aliongea kwa hasira ๐Ÿ˜กmoyoni sikupendezwa na maamuzi yake. Nilimwona akielekea sebuleni pamoja na wale wachumba alionichagulia. Mie haraka nikaingia chumba cha siri, chumba nilichomficha Nuhu Mziwanda.


Chumba nilichomficha Nuhu sio chumba kama vyumba vingine vya kulala bali ni  sebule fulani yenye Meza ndogo, sofa  chache, ๐Ÿ›‹️bafu la kukogea, choo ๐Ÿšปna kitanda ambacho Nuhu mpenzi wangu angelitumia kulala Mama asimwone. Hakika kile lilikua ni chumba cha siri.


   
       Haraka haraka nikalibadili lile gauni la Harusi, gauni ambalo sikuelewa muda gani nilivishwa, yamkini nilipuliziwa dawa za kunipa usingizi nisielewe kinachoendelea. Nikalivaa shati la Nuhu,Suruali ya Nuhu na singled ya Nuhu, wakati huo Pete nzuri alionivisha Nuhu miaka mitatu iliyopita iling'ara na kung'ang'ania kidoleni kwangu.๐Ÿ’


       Nuhu hakuwepo chumbani lakini nilijua pahali alipo, 'Bafuni' sababu asikiapo kelele ๐Ÿ”Šza Mama ujificha bafuni mama asipate kumuona. Nilielekea bafuni nikamkuta Nuhu ameketi chini, pakavu, nadhifu, safi pasipo na tone la maji, miguu yake ameikuja kama mwislamu alaye daku na waislam wenziwe. ๐Ÿ•‹☪️๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ•ŒNikamtazama na yeye akanitazama, macho yake mazuri yaliyojaa ๐Ÿ‘️๐Ÿ˜ Huba yalikutana na macho yangu. Lips zake nene zilizonona ziliachia tabasamu.๐Ÿ‘„๐Ÿ˜š Nikamwambia:


        "Nuhu mpenzi ninajua umesikia Kila neno ambalo Mama ameongea kuhusu ndoa ya lazima lakini mpenzi ninakupenda ๐Ÿ’™na sintakuacha maisha yangu yote." Nuhu alinitazama lakini hakusema neno.๐Ÿฅธ

       "Ninakupenda pekee yako wewe ndie mwanaume wa moyo wangu. Bado Nuhu alitabasamu akinitazama kwa jicho la Huba zito. Nilipomaliza kuongea na aNuhu nikatoka pale shower nikaelekea sebuleni kule Mama ameketi na wale vijana wawili aliotaka kuniozesha kwa lazima. Nikiwa ninateremka ngazi za Horofa ya pili kuelekea chini sebuleni nilijisemea mtimani.

     
      'Mama anadhani nitamuacha Nuhu"๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚  Anajidanganya Nuhu ameingia moyoni mwangu.๐Ÿ’•


      "Nitafanya Kila kituko kuhakikisha ninawakataa hawa wanaume ili niolewe na Nuhu, nimpendaye nimemuweka moyoni mwangu naye ametulia" Nikatelemka ngazi, chini nikafika, uso wangu ukamkabili Mama.


      " Siwezi kuolewa iwapo sijawajaribu Hawa wanaume ili nifahamu kama kweli wananipenda au la!" Nilimwambia Mama.


       "Ilo tu! sio tatizo tunaweza kuanza."Mama Aliongea.


        "Nitakuwa wa kwanza katika jaribio lako, ninakupenda" Bwana wa Kwanza Aliongea.☺️


     "Mimi pia ningehitaji kuanzia jaribio lako"Bwana wa pili mpole mwenye uso wa tabasamu Aliongea.☺️


      "Wewe  MPUMBAVU NINAOMBA UKAE KIMYA UTULIE mimi niliyewai nianze majaribu," Bwana wa Kwanza mwenye sura chungu, hasira na haraka alidakia.๐Ÿฅด Mama akasema.


        "Bwana Harusi wa kwanza mfate Bibi Harusi chumbani kwake mkaongee."


       "Very nice." Bwana Harusi wa kwanza akifurahia akanifuata tukaelekea chumbani kuongea, chumba CHANGU cha siri chumba nilichomficha Nuhu Mziwanda ambaye Bado alikua ameketi bafuni akiogopa kama Mama angelimuona ingekua mtihani.


 ##############

         Tuliketi juu ya sofa zilizo ndani ya kile chumba pembeni ya kijimeza kulikua na mvinyo wa bei ghari ambao yule Bwana aliuleta. Bila kupoteza muda alipiga magoti chini akatoa pete yenye kito cha Diamond akaniambia "Naomba nikuvishe Pete." Hapo tayari goti chini amepiga.


         "Sawa niviishe." Nilimwambia nikiwa nimesimama akanivisha Kisha akaongea.


       "Hii Pete ni Pete ya bei Kali Sana nikikuoa nitahakikisha Maisha Yako yote unavaa Vito vya bei gharama, unatembelea usafiri wa bei gharama, Kila kitu chema ukitakacho kitakua ni cha bei ya kutupa."Alijigamba akijua kuwa nitafurahia mali zake.


        "Hayo ndiyo malengo uliyoyaweka tukiwa ndani ya ndoa ?" Nilimuuliza,


     "Sasa kumbe! Ninataka uishia Maisha ya anasa wakati wote utahudumiwa na vijakazi, utaishi kama Malkia mie nikiwa Ofisini nikitafuta pesa."Bado tu hakunishawishi.


      "Bado haujanishawishi Bana Joshua  unanipenda kwa dhati?"Bila kutarajia Joshua aliyejitambulisha kwangu alinijibu.


      "Sikiliza Pamlela sio kwamba nimekupenda kutoka moyoni mwangu, Kuna kitu muhimu ninakitafuta kutoka kwako."


      "Ni kitu gani hicho?" Yule tajiri akanijibu.


        "Mama Yako amenileta hapa akishinikiza nikuowe kwa sababu nyumbani kwetu kuna matatizo kibao, Moja ya tatizo linalosumbua nyumbani ni utajiri na mali nyingi alizozoacha Baba yangu aliyefariki hivi karibuni," Alimeza mate na kupumzika kunena,

        "Pole kufiwa na Babako" Nilijua kumfariji.


      "Asante. Baba ameacha makampuni mengi na hisa nyingi ndani ya hayo makampuni, hivyo basi ndugu zangu hawataki kunipa mgao wa hizo hisa na Mali nyingine nyingi  kwa shariti moja tu ni lazima nioe haraka ndipo wanigawie mali, wana hofu kubwa kuwa nisipooa nitachezea huo mgao nitakaopewa lakini nikiona mke , mke atakua mshauri mzuri wa maendeleo yetu, ninakuhitaji  tafadhali kubali nami nipewe mgao wangu wa hisa alizoziacha marehemu Baba." Alimaliza kunena.


      "Sidhani kama itawezekana Bana Joshua maana sikuoni kama una mapenzi ya dhati kwangu ninachoona mimi kwako ni hamu yako ya kukomboa utajiri na Mali ulizoahidiwa na ndugu zako. Yamkini ukiisha fanikiwa kuzipata mali hizo haraka utanigeuka na kunitupa"


        "Na hii Pete yako ninaitoa siitaki na Wala sikutaki," Kwa hasira niliivua ile Pete ya Diamond nikaitupa ndani  ya Birauli lililojaa ule mvinyo wa bei gharama,


      "Naomba uondoke na uniache ninahitaji kuwa mpweke" Nilimfukuza naye akatoa kiapo kwamba  mimi ni wake na kunioa lazima anioe,  machozi yalinitoka nikiwa ndani ya chumba changu Nuhu alisimama pembeni ya mlango wa Shower alinitizama kwa hasira kama vile anataka animeze, Nuhu alipoteza natumaini juu yangu,

       "Nuhu mpenzi ninaomba unisamehe kamwe sintakubali kuolewa na yule mwanaume asiye na malengo na mimi zaidi ya kunicheza kama karata ili avune utajiri,"Nikaangalia kidoleni Pete alionivisha Nuhu sinayo, Uwii! Nilipagawa tena haraka haraka nilianza kuitafu ile Pete aliyonivalisha Nuhu Miaka mitatu nyuma, hakika nilivurugwa, NIKAANZA kuitafuta Kila Kona ya kile chumba.........  Sofani na mezani nilitafuta Pete ya Mziwanda hatimaye nilikuja kiona Pete aliyonivisha Mziwanda kisha kwa furaha nilimuonesha Mziwanda wangu.

      "Hii ni Pete uliyonivisha Mziwanda wangu, nitawezaje kuitupa ikiwa wangu wa moyoni Bado ungali upo nami"Ghafla mlango wa chumba changu ulifunguliwa Nuhu  aliingia haraka ndani ya bafu na kufichama,

       "Ulikua unaongea na nani wewe?" Mama aliniuliza baada ya kuingia chumbani na yule Bwana Harusi wa pili.
 
       "Sijaongea na mtu Mama?"  Nilimjibu haraka kumzuia mama kuijadili ile ishuu.

        "Haya nenda Jikoni na mchumba wa pili kuna kahawa ☕na kashata nimekuandalieni ni matumaini yangu kwamba mtaelewana,"  ๐Ÿ‘Mama litoka chumbani, mimi pamoja na yule Bwana Harusi wa pili tulitoka tukaelekea Jikoni kunywa Kahawa,
     
                ###

Jikoni tulisimama karibu na karo ya kukoshea vyombo yaani Sink la vyombo upande wa kushoto kulikua na fridge yetu nzuri na kati kati ya Jiko letu Meza ya mviringo pamoja na viti vya mbao havikukosekana achilia mbali Jiko letu zuri linalotumia gesi ⛽ oven na umeme.

       "Ni kweli unahitaji kuishi na mimi?" Nilimuuliza na yeye akanijibu

       "Yes of course ninahitaji kuishi na wewe?

   "Nitaamini vipi kama una malengo ya kuishi na mimi au labda upo hapa kunichezea" Yule kijana mwenye uso mtanashati wenye nyingi aibu na macho mazuri yaliyojaa huruma kwangu alijitambulisha kwa jina la Mode Mario, Akanijibu,

        "Subiri,"Nikamwona afungua fridge na kutoa kopo kubwa lenye pilipli pamoja na vikombe viwili kisha akamimina ile pilipli kwenye vile vikombe naye akatamka

       "Kila ukweli nitakao sema kwako nitameza kikombe cha pili pili na wewe pia Kila ukweli utakao Nena kwangu utameza kikombe cha pili pili." Nilimshangaa, maana ukali wa pilipli MWENZENU ninajua

       "Mario pilipli kawaida ina ukali na uchungu"


         "Yes, ukweli pia lazima uwe mchungu" Alinijibu, Kisha akanipa nafasi ya kuuliza maswali

        "HAUNIJUI NA MIMI SIKUJUl KWANINI UNATAKA KUISHI NA MIMI?"

            "Nafasi inaniruhusu kufanya hivyo,"

       "Je, unanipenda?" Hakunijibu swali langu zaidi ya kunitazama machoni na kugugumia funda la pipipili ile nzito na chungu,

         Uwii! Nilibaki nashangaa Mario pale alipogugumia lile funda la pilipili nzito na chungu lakini pia nilianza kumpenda nakumfurahia moyoni mwangu. Aliniingia akilini mwangu kwa kasi ya ajabu, haraka haraka nikakimbilia fridge na kuifungua Kisha nikayachukua maziwa fresh nikampa ayanywe, akayagugumia yale maziwa kama mwendawazimu baada ya dakika chache mbele yetu tukatazamana kwa vicheko kisha tukafanya kuhamia pahali Meza na viti vilipo kisha tukaketi pale.

         "Nataka kumjua mtu ambaye ulikua unaongea naye pindi mimi na Mama yako tulipoingia chumbani kwako"

          "Ni boyfriend wangu."Nilimjibu kwa ufupi.

       "Kwahiyo unae Boyfriend?"

         "Ndiyo na NINATARAJIA yeye ndie atakae nioa mbeleni"Nilimjibu bila kupepesa macho naye akaniuliza swali lingine zito.
      
       "Je, unanipenda na upo tayari nikuoe?" Nilishindwa kujibu haraka zaidi ya kumimina ile pilipili mdomoni mwangu, Uchungu wa ile pilipili hakika siwezi kuhadithia. Mario akafanya haraka kuelekea kwenye fridge na kuniletea maziwa niliyoyagugumia kama mwendawazimu,

         "Pole,"Alinifariji.

           "Duh! Ama kweli ukweli lazima uwe mchungu,"Wawili tulicheka kwa furaha, tabasamu likatufanya tujisikie kama tumezaliwa upya,

       "Naomba tupeane ahadi" Mario aliongea

     "Nipo tayari."Nilianza kumpenda yule kijana asiye na makuku

      "Anza wewe kunipa ahadi yako na mie nitaitekeleza" kama nilivyosema Mario amenyimwa roho ya majivuno akanitaka nianze kumpa ahadi yangu,

        "Naomba uniache niishi pekee yangu," sikumtania nilimaanisha

        "Sawa, kwa sababu natambua unaye Boyfriend  nipo tayari kukuacha uishi naye. Alikubali matamanio yangu. Ikawa zamu yake kueleza ya moyoni,

      "Kuna kipande cha barua nimekiona ukikiweka mfukoni muda ule tulipoingia Jikoni ninaomba nikisome nijue kinahusu nini?!" Duh! Alinishitua.

    "No! Kipande cha barua yangu hakikuhusu" Nilichelewa kujizuia Mario akanivamia na kukichukua kile kipande cha barua niliyoihifadhi juu ya mfuko wa shati nililovaa, shati la mpenzi wangu Nuhu,

         "Hapana tafadhali usithubutu kukifungua kipande cha barua iyo na kukisoma," Niliisha chelewa Mario alikwisha fungua kile kipande cha barua naye akasoma:

           MPENZI  PAMELA
NINAJUA UNANIPENDA SANA NA MIMI NINAKUPENDA ZAIDI YA UNAVYONIPENDA, NAOMBA NIKUAMBIAE JAMBO MOJA. HUU UGONJWA WANGU UMEZIKATAA DAWA NA MIMI SIJAKATA TAMAA LAKINI MUDA WANGU UMEFIKIA KIKOMO .........

Mario hakuweza kumaliza kusoma kile kipande cha barua naye akaniuliza:
  
     "Mpenzi wako anaumwa?!"Sikua na jibu zaidi ya kumwambia Ndio.

       "Ok. Basi nenda kamuuguze" machozi yalianza kunibubujika nikatoka Jikoni na kukimbilia sebuleni lengo langu lilikua ni kumfuata mpenzi wangu Nuhu kule chumbani nilikomwacha mpweke

     Nilidhamiria kumwomba Msamaha Daring Mziwanda maana nilijiaibisha kuongea mambo yanayohusu mapenzi  na wanaume wengine. Nilipofika sebuleni nilimkuta Mama ameketi pamoja na Bwana Joshua wanasubiria Jibu langu. Mama alisimama kisha akaniuliza.


       "Eeh! Niambie jaribu limefika mwafaka gani?"


       "Nimemwambia Mario aniache niishi pekee yangu.


     "Kwahiyo Mario ameshindwa mtihani?"Mama aliniuliza. Kabla sijajibu Joshua alidakiza.


        "Nilisema mimi, nilisema utakuja kuwa wangu, Ona sasa, ona ninaenda kujinyakulia urithi kiulaini"Alijigamba haraka haraka akaja kunikumbatia kwa nguvu,

  
       "Sasa tuondoke"Alianza kutumia nguvu kuniondoa pale sebuleni.


      "Hapana, Bwana Joshua mambo Bado na taratibu lazima zizingatiwe"


      "Mambo gani? Taratibu zipi? Mama sitaki ushenzi wa kunipotezea muda wangu mzuri. Nasema hivi Binti yako ni Mali yangu, ndoa lazima ifungwe Leo hii hii," Aliendelea kujipamba.


       "Umenileta hapa nyumbani kwako ili kunionesha Binti yako ulidhani nitashindwa kumpata? Chezea hella ooh!" Akamsukuma Mama yangu kwa nguvu Mama akaanguki juu ya sofa akakibamiza kichwa chake ukutani nakwambieni maumivu aliyoyasikia mbona alijuta. Bwana Joshua aliendelea kunikaba mabega akanikokota kwa nguvu na kwa lazima ya kuondoka kama Mbuzi aliyenunuliwa Mnadani.


        'Nguuuuuu,' Ngumi nzito ilitua juu ya uso wa Bwana Joshua, Joshua aliona kizunguzungu akaanguka chini kama zigo la mapumba, moja kwa moja akazima na kupoteza fahamu.



        "Mshenzi mpuuzi huyu"Mario aliongea. Ngumi nzito aliyomlisha Bwana Joshua ilitosha kuniokoa. Tuliketi juu ya sofa ili kumhudumia Mama ambaye kidogo alianza kupata ahueni.


     "Niruhusu niende chumbani nikampe taarifa mpenzi wangu Nuhu." Nilimwambia Mario. Hata kabla sijapewa ruhusa nilichoropoka pale tulipoketi Mimi, Mama na Mario nikakimbilia chumbani kwangu 

     "Anampenda sana Nuhu, ngoja nikamuona huyo Nuhu maana ameniambia anaumwa?"Mario alimwambia Mama.


          "Mpenzi gani?"Mama alimvuta Mario sofani akamketisha na kumpa simulizi.


         "Pamela Hana mpenzi wala mchumba huyo Nuhu aliyekuambia alikuwa ni mpenzi wake aliyefariki miaka mitatu iliyopita. Nuhu aliugua kansa ya koo basi tangu afariki Pamela haachi kumuwaza huyo marehemu. Amini usiamini kila siku Pamela anavaa nguo za Nuhu, huu ni mwaka wa tatu amevurugwa na amechanganyikiwa. Imekua kama Hadithi kila siku Pam anaongea pekee akilitajataja jina la Nuhu Mziwanda." Mama alihadithia juu ya Nuhu mpenzi wangu

      "Unataka kuniambia huyo Nuhu ni kivuli tu kisumbuacho Pamela"Marioo alimuuliza Mama.


    "Ndio sababu y mimi kuwatafuta wanaume wawili mumshawishi Pamela hadi akubali kuingia ndoani, jambo la kushangaza mnaniangusha hadi mnaanza kupigana ajili yake."

     "Mama NINAKUAHIDI jambo Moja mimi sio mama zuzu Joshua. Nipe dakika chache nikamshawishi PAMELA amini usiamini nitaibuka kidedea" Mario alimwaminisha Mama.


      "Haya Baba  ninakutakia fanikio jema."Mario alipanda Horofa ya pili akaelekea ndani ya chumba nilalacho akanikuta nimepoa juu ya kitanda nimelala nikiitazama sehemu ulipo mlango wa bafu.


       "Pamela."Aliniitia, akajiketisha juu ya kitanda changu.


    "Abee!"Niliitikia wito.


    "Bado unampenda Nuhu?"Aliniuliza.


     "Ndio tena sana, tumepanga mipango Mingi sana ya maisha yetu, nilimpa ahadi ya kutomwacha,"


      "Lakini Pamela Nuhu alikwisha kufa na kutangulia mbele za haki. Ukionacho mbele yako ni kimvuli chake, kivuli  ksichotulia zaidi ya kukuwinda na kukupumbaza."


      "Hapana, Nuhu yupo hai Wala hajafa, ninatazamana naye, yule pale amesimama pembeni ya mlango wa bafu."


      "Nikuulize swali." 


      "Uliza tu Bwana Mario."

      
          "Tangu Nuhu alipokukabidhi icho kipande cha barua je, umewai kukisoma"


        "La, asha!" Mario akaingia woga na hofu ya kutaka kujua ni niniNuhu alichoniandikia miaka mitatu iliyopita.



     "Hilo ndilo tatizo inaonekana mzimu wa Nuhu unakufuata popote pale ulipo, ukiwa umelala unamuona, ukiwa unaoga unamuona, ukiwa unakula unamuona, kivuli cha Nuhu hakijapumzika kwa amani, hivyo basi jaribu kuifungua hiyo barua uisome" Mario alinishauri .


        "I cant Mario, I cant please!"


       "Unaweza."Mario akaitoa ila barua aliyonikabidhi Nuhu Kisha nami nikaisoma."


        NINAKUPENDA NA NITAENDELEA KUKUPENDA......... Nilishindwa kumaliza kusoma kile kipande cha barua machozi yalinibubujika maana nilimuona Nuhu amesimama pembeni ya mlango wa shower akitabasamu.


       "I cant finish reading it Mario." Chozi lilinibubujika


        "Nipe nikusomee." Nilimpa Mario akisome kile kipande cha barua Mario akasoma.


NINAJUA SINTAWEZA  KUENDELEA KUISHI DUNIANI UGONJWA HUU UNANIMALIZA BASI NINAKUOMBA MPENZI WANGU IKITOKEA UMEPATA MPENZI MWINGINE KUBALI KUISHI NAE, OLEWA UISHI KATIKA MAPENZI.


         SINA MENGI ZAIDI YA KUSEMA NINAKUPENDA.


        WAKO AKUPENDAE,


NUHU.

Mario alipomaliza kukisoma kile kipande cha barua nilimuona mpenzi wangu Nuhu akinipungia mkono wa kwaheri, ghafla akatoweka ndani ya chumba changu, kuanzia siku ile sikupata kumuona tena Nuhu wangu. Mario alifanikiwa kunioa mapenzi yetu yalipamba moto tukapendana na kuishi katikati ya raha na starehe. Uzuri wa mapenzi mwaka huu ninatarajia ifikapo mwezi wa Tisa niingie Leba, niilete nyumbani zawadi Bora ya maisha.

     Kila nikikumbuka Mama yangu, Mama mpole mwenye huruma na busara alitaka niolewe na wanaume wawili mmoja mwenye majivuno na mwingine mwenye busara nikikumbuka mie nachekaGa tu.


~~~~~~~~

TCHAO ๐Ÿ’– 

~~~~~~~~



   


          
       

   

No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...