Saturday, August 23, 2025

BEKA

 




BEKA


(ANA SURA YA MAUZO.)


SURA YA KWANZA.

“SIIONI KAZI YOYOTE YA KUFANYA DINGI.”

Ile Beka anamuona Bella akipita pita barabarani, Sultan Hoteli, moyo wake ulikuwa ukiugua, ukiugua ndani kwa ndani, ukiugua kwa mapenzi, ukiugua kwa kumpenda msichana mdogo aitwaye Bella, mwenye kadirio la miaka kumi na mitisa, Beka ana umri wa miaka Therathini na moja ni mtu mzima mzima wa umri mwili akili na majaliwa.


        Jina lake halisi anaitwa BAKARI ARMOUR lakini alipoingia KIWENGA alibadili jina akajiita BEKA ARMOUR sijui kwanini aliamua kufanya hivyo au ni kwa sababu ya ujana na kupenda mabadiliko?  Labda! Lakini ndani ya vyeti vyake vya elimu ya msingi, Sekondari na kile alichokipata alipokuwa amehitimu mafunzo ya Ulinzi kwenye kampuni ya SIGA, jina lake bado litabaki kuwa ni lile lile, BAKARI ARMOUR.


        Ni Mzaramo kwa kabila, kijana wa Jiji la DAR ES SALAAM, amesoma shule ya Msingi Buguruni Moto, akabahatika kwenda shule ya Sekondari Msimbazi, matokeo ya mitihani yake hayakuwa mazuri, upepo ukabadilika, akawa ni mtu wa kuketi Vijiweni, akijifunza uhuni na tabia zingine mbaya zinazotendwa na vijana wa Jiji la Dar es salaam.


Beka hakuwa na jambo lolote lile la msingi  au la maanaa kulitendea haki, ili apate maendeleo, ajiotambue kuwa yeye ni kijana wa kiume, hapaswi kufanya mambo ya ajabu yaliyojaa uhuni. Bbabaye mzee Armour kipato chake ni kidogo, kidogo hiki kilitosheleza mahitaji ya familia, biuashara yake ya kuuza Mboga mboga haikumlipas sana, japo ilimtoa kimaisha ilimsaidia katika malezi ya watoto wake watatu BEKA, Aisha na Tunu.


        Mzee armour alipoona mwanaye anakoenda ndiko siko, huruma juu ya Beka ziliongezeka, alimuonea huruma mwanaye na hatimaye akafanya juu chini kumketisha chini, akamtaka mwanaye yeyue na moyo wake atamke  ni aina gani ya kazi ambayo ingelikuwa naafu ya maisha yake , kukaa bure hakutoshi, kuomba omba wapitao njia hakuridhishi, kuiba, kutapeli au kutumia nguvu za lazxima huo ni uvunjifu wa sheria, na uvunjifu wa sheria ni makosa, makosa yana adhabu yake. Sio haba baba alihisi anaweza kumpoteza mwanaye, akafanya juu chini, hana Budi kumnusuru mwanaye na majanga ya dunia.

Beka angali akikuna kuna kichwa chake kilicho jaa Umba, viroboto, chawa na kungtuni, nywere zake ni ndefunamezisokota sokota, midomo yake imekomaa na kuonesha rangi ya kijivu ni kutokana na moshi wqa bange macho yake mekundu kama pili pili iliyo ivaa yamezoea kupora, kunyang’anya, kubaka, kulawiti na kudhurumu kwa kutumia silaha zenye ncha kali. Beka Yule wa vijiweni tayari alikwisha haribika.


“Sioni kazi yoyote ile ya kufanya dingi wacha mie niendelee kusota kijiweni.” Beka alimjibu mzee Armour kijeuri jeuri pasina kutafakari vema.

“Beka mwanangu, Dunia ni nzuri lakini  lakini wanadamu sisis ni wabaya, yatazame maisha yako yalivyo haribika na kukongoroka, utamlilia nani kipindi cha dhiki kuu, mateso na maumivu, kumbuka ukimtegemea ndugu utakufa masikini, ukidharau mwiba utakuchoma, mdharau Jembe si mkulima. Tafakari ni aina gani ya kazi unayoweza kufanya ili mimi baba yako nifanye juu chini kukutafutia. Mzee Armour aliongea.


“siioni kazi yoyote ile ya kufanya Dingi, niache nitulie kijiweni nile raha za duniaq,, nile ujana kwa mudaa wangu, maisha ni mafupi, uzee hauko siku hizi tofauti na  zamani.”  Beka aliongea kwa dharau.

“majuto ni mjukuu mwanangu,asiyefundwa na babaye ulimwengu utamfunda, kiburi sio maungwana, kumbuka hiyo ni misemo tu lakini ukweli ujapodhiirika wewe utalia na kusikitika.kazi ni maisha ni kufanya kazi, mwenda bure hakai bure ataokota, mgaa gaa na pwa hali wali mkavu, fanya juu chini ufikirie aina yoyote ile ya kazi ambayo wewe unaweza ukaitendea haki.” Mzee Armour alimsihi mwanawe.


“mwanangu, ndani ya Jiji la Dar es salaam kuna kazi nyingi sana, ukitaka utoke vizuri unaweza ukajiajiri kwenye kilimo cha mboiga mboga, biashara ya kuuza maji, chakula cha migahawani, sokoni na kadharika, utatoka tu mwanangu, Binafsi sidharau kazi za kuajiriwa, zinaweza kukutoa kimaisha, lakini kujiajiri ni bora zaidi ya kuajiriwa. Sema ni kazi gani unaipenda na pia unaweza kuitendea haki.” Babaye Beka alimhoji Beka aina mbali mbaliu za kazi ambazo zingelimsaidia katika kuyaboresha maisha yake.
Beka alikataakata kata, alidai kwamba aina za kazi ambazo baba yuake anamtaka afanye ni kazi  zinazowafaa wanawake, yeye ni kijana wa kiume hawezi kuuchoshaa mwilio na akili zake kujishughurisxha na shughuri kama zile.

                        ##########

No comments:

Post a Comment

BEKA

 SURAYA TATU                        “AKIPITA ATAJIPITISHA.” Beka akawa member wa kampuni ya SIGA, akipelekwa hapa na pale kulinda mali za ma...