PADRE✝️ ALIGUNDUA MTOTO 👼🚼WANGU SIO WANGU BALI NI WA KAKA YAKE.
Miriam mke wangu alipokamata ujauzito, 🤰🦋nilifurahia maana nilijiona Sasa mie ni Baba kijacho, mie ni kidume mbegu na baraka zinanitembelea. Basi mie Adam nikafanya kukoreza juhudi za kumtunza mpenzi wangu Miriam pamoja na kuitunza mimba yetu. Mola alijibu maombi 🛐📿🤲yetu Abaya akazaliwa, kizazi chetu cha kwanza kilichotupa furaha, amani na utulivu ndani ya Nyumba.🏡
Tulipokezana kumbeba Abaya wetu iwe usiku iwe mchana. Miriam alifanya kazi ya kumbeba Abaya wetu na mie niliutumia muda wa jioni kumfurahia Abaya wetu. Tulimwogesha, tulimlisha 🍼 na kumpatia huduma zote muhimu mtoto wetu akapendeza na kuvutia.
Basi baada ya mwaka mmoja kutimu mie Asa na mke wangu Miriamu tulikubaliana juu ya ubatizo wa mwanetu Abaya kama zilivyo desturi za Wakristo wengi wakiamini Ubatizo ni ondoleo la dhambi na njia ya kuingia katika Ufalme wa Mbingu tukiwa safi salama.
Tulimwona Padre wa Dhehebu letu, Padre Sisu tukamweleza juu ya tamanio letu kumbatiza mwanetu Abaya, Padre Sisu Padre aliyetufungasha ndoa alikubali na tarehe ya ubatizo ilipangwa, uzuri baada ya miezi mingi ya maandalizi muda mwafaka uliwadia, sala zilifanyika, nyimbo ziliimbwa, maji ya ubatizo pamoja na beseni maalumu kukinga maji ya ubatizo viliandaliwa.
Padre akamchukua mtoto wetu kisha akamtazama sana jambo lililosubiriwa ni kutimia kwa ubatizo tu lakini ghafla Sisu alionekana akitetemeka mara baada ya kuyagusa masikio ya mwanetu Abaya.
"This.... This.... This..." Padre alishindwa kumalizia kauli yake tulibaki kumshangaa
"Nini tatizo, Padre!?" Nilimuuliza.⁉️
"This birth mark..... Hii alama ya kuzaliwa" Padre Sisu aliongea kwa wasiwasi akitetemeka. Nilimsogelea Padre, mke wangu alikua amesimama nyuma ya mgongo wangu.
"Padre Sisi tatizo nini?" 🤷Nilimuuliza.
"Mbona untetemeka alafu unaongelea Birth mark, alama ya kuzaliwa mwanangu?" Nilimuuliza, akanitazama kwa kunikazia macho kisha akamkazia macho👀 Miriam mke wangu aliyeangalia chini ya sakafu kwa woga na kutetemeka.
"Ni juu ya hii alama iliyo nyuma pembeni ya sikio la mwanao Abaya." Alijibu kwa ufupi.
"Kwani alama iliyopo pembeni ya sikio la mwanangu Abaya imefanyaje?" Nilimuuliza.
"Ninajua vema." Sisu aliongea jambo ambalo lilipelekea mke wangu aanze kutetemeka kwa nguvu, Presha ilikua ukimpanda na kumshuka jambo ambalo sikuelewa kilichomsibu atetemeke.
"Alama hii ni alama ya familia yetu, ni alama ambayo Mimi na mdogo wangu Joshua ndio tuliio rithi." Padre aliongea haraka haraka bila kupoteza dakika. Sisu aliinama na kunionesha alama yake ya kuzaliwa iliyokuwa pembeni ya sikio lake, alama Og iliyofanana kabisa na ya mwanangu Abaya.
"Jamani mbona kama sielewi." Nilijikuta naongea kwa sauti ndefu.😦
"Muulize Mama Abaya ataeleza ukweli." Sisu aliingia shaka. Nikamgeukia nyuma kumtazama Ma. Abaya ambaye alionekana kusononeka, Alimwaga chozi la moto🔥. Haraka haraka alitoka ndani ya Kanisa⛪ letu la Mtakatifu Petro Parokia ya Bikira Maria, Mbezi Beach. Akikimbia 🏃♀️na kutoweka ndani ya Kanisa jambo lililoshangaza na kuniachia domo wazi.😟 Kwa kifupi nilikua sielewi Nini kinachoendelea
Ubatizo wa Mwanangu Abaya haukuzaa matunda, uligongwa mwamba, hakubatizwa sababu alama pembeni ya sikio lake ilileta ukakasi. Nilimbeba mwanangu na kuondoka kurejea nyumbani. Nilimkuta Mama Abaya akifanya haraka kupangilia nguo zake ndani ya sanduku lake la nguo,🛄👜🛍️ yamkini alikua tayari kuondoka pale nyumbani kwetu.
"Unataka kwuenda wapi Mama Abaya?!" Nilimshangaa.⁉️
"Nisikilize Mume wangu, nimepoteza hamu ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hii, tangu nimemleta mwanetu Abaya sikumpenda kabisa kumleta ndani ya nyumba hii."Alijieleza.
"Ninamchukia mtoto huyu, sitaweza kuishi naye wala siwezi kumlea, acha niondoke ninakuachia umlee ikiwezekana umrejeshe kwa Baba yake." Duh! Alinishangaza wakati mie najijua kuwa ndie Baba halali wa yule Malaika.
"Mimi si ndie Baba halali wa huyu mtoto?! Niliongea kwa ukali kidogo.😬
"Samahani Baba Abaya, Abaya sio mtoto wako wa damu🩸. Abaya ni mtoto wa rafiki yako Joshua, ilitokea kwa bahati mbaya....." Miriam alianza kulia.🥲🥹
"Ilitokea kwa bahati mbaya kivipi naomba maelezo wacha kulia." Nilimkemea, chozi lake likaambatana na kamasi zilizomtoka kwa fujo, akazifuta kisha akaendelea kusimulia.
Miaka miwili iliyopita ulipata Safari ya kwenda Arusha kikazi niinakumbuka uliketi kule karibia mwezi mzima kipindi hicho kilikua kigumu sana kwangu, nilikumiss sana Baba Abaya, hamu ya kukutana kimwili ilinizidi, hamu ilikua juu na kuongezeka." Alijieleza.
"Nilijiona nipo njia panda, Sina mbele Sina nyuma , mtu wa kunitoka hamu yangu ni wewe pekee, wewe niliyekuzoea, wewe uliyekuwa mbali na peo za macho yangu. Basi siku Moja Rafiki yako Shemeji Joshua alinitembelea hapo ndipo sikua na jinsi zaidi ya kumshawishi kwa mitego na minaso tufanye tendo la ndoa.👩❤️💋👨
Joshua rafiki Yako hakukataa ombi langu la kufanya tendo la ndoa, alinitaka iwe Siri ya milele. Lakini Wahenga walisema Mimba haifichiki,🤰 sikua makini kuzingatia tarehe zangu za hatari na matokeo yake nimeachwa njia panda.
Tangu mtoto huyu azaliwe nimetokea kumchukia sababu ya usaliti Niliofanya miaka miwili iliyopita." Miriamu Alimwaga chozi lenye kilio cha Kwi Kwi Kwi.🥹
Simulizi yake iliniumiza na kunichoma sana moyo wangu, nilikosa raha siku ile lakini kwa busara zangu nilimwambia mke wangu Miriam.
"Moyo wangu umesamehe yote yaliyopita nakuomba rudisha mizigo yako ndani, yaliyopita si ndwele tuyangoje yajayo, Abaya ni mwanangu na wewe ni mke wangu mpenzi Miriam.
"Hapana siwezi Asa siwezi moyo wangu umejawa maumiv. Mimi ni msaliti na nimevunja💔 ndoa yangu kwa ujinga wangu. Alilia Kisha Miriam akabeba mizigo yake naye akatoweka zake akiniacha njia panda nisijue la kufanya.
@@@@@@@@@@
Sikutaka kufanya uzembe kama alioufanya Mke wangu Mama Abaya, kama ni kumkataa mtoto amemkataa, je, na mimi nimkatae sababu tu sio damu yangu? Hapana mtoto huyu nimetoka naye mbali tangu akiwa tumboni kwa mama yake nilimpenda, nilimdekeza Mama yake kwa vinono na vitamu . Mtoto alipozaliwa katika shida na raha nilisimama naye.
Mtoto alipoumwa mimi ndiye niliyeku mstari wa mbele kumhudumia, aliposikia njaa haraka nililihakiksha anapata chakula. Akilia ningelimbembeleza hadi apate usingizi sasa iweje Leo hii nimtelekeze kama alivyomtelekeza Mama yake?
Nikawa karibu na Abaya. Ingawaje ninajua kuwa sio mwanangu ninamchukulia kama mwanangu. Kamwe sintampatia Joshua amguse mwanangu, ninampenda mtoto wangu, ninampenda pendo la sili silali ninamthamini toka rohoni wacha tuelekee Jikoni nikamyweshe uji wake usije poa na kuwa wa baridi
%%%%%%%%
TCHAO
%%%%%%%%

No comments:
Post a Comment