MIPASHO YA MAMSAPU
MWENZENU N'SHAPENDWA
Sehemu ya 8
Roho wangu hakuwa na amani siku ile na mie pia sikuwa na amani, Maua katutia Stress, mawazo mgeni huyu aso tutakia mema, katuvuruga siku ya leo, hatukuweza kula vizuri, hatukueza kulala vizuri, basi kati kati ya usiku wa siku ile mie nikamuuliza roho wangu Pompo, nikamwambia.
“Je, Babu utaniwacha kwa sababu ya Maua.?”“Nianze tu! N'taanzaje kumrudia yule msaliti, mbovu aso yajua mapenzi.” Pompo aliendelea kunena.
“Love๐ ninakupenda pekee yako huyo mwingine kwangu ni kama makapi, atupwe jahani hafai kulivuruga vuruga penzi tuliloloshikilia.” Maneno ya Pompo yalinipooza kidonda alichokileta Maua.
“Moyoni umenikaa , moyoni umenikaa,
ingia moyoni mwangu.
Damu yangu imekupenda wewe,
Damu yangu imekupenda wewe,
mimi nimekupenda,
ingia tena moyoni mwangu,
Mimi nimekupenda na wewe
ukinipenda mapenzi milele,"
Pompo alilikoreza pendo kwa maneno matamu yalozidi kukiponya kidonda changu.
“Nikuache niende wapi? Mapenzi najua, mapenzi wayajua. Huyo mgeni mapenzini porojo na vimombo vilipomzidia akageuka Fisi tamaa, Fisi tamaa ajapochanganyikiwa uchana msamba, njia mbili zijapomshinda. Pompo alinichekesha kwa manenoye.
“Uboya wake mwenyewe,” Mie nikachangia hoja.
“akafie mbali, kibudu yule.” Pompo kamlaani yule mwanamke.
“yashamkuta tayari na sasa anasaka naafu ya kuliponya donda limtesalo.” Pompo aliongea tena.
“Sikia love, nishamchunguza,nishapata taarifa zake, leo anaumia kuachwa.” Pompo aliliamsha dude la masimulizi.
“kwni kaachwa? Je, aliolewa tena?” Maswali ya mie yakaanza kusambaa kichwani kwa Pompo roho wangu.
“Yes kaaachwa, katupwa jahani kama takataka, nani amzo? Hakuna”
“ Teeh teeh teeh,(๐๐๐nalicheka mie) na hata akizolewa atatupwa tena?” alizidisha porojo.
“Mie ninatamani nisimwone tena abadani,” Roho wangu aliongea.
“kumbuka tayari ushazaa naye!”
“Kuzaa majaliwa hata wadudu wanazaa, sembuse ndege na mimea, hayo yote mapenzi ya Mola silioni tatizo hapo, tatizo ni usaliti wake na kuniacha solemba.” Pompo aliongea. Leo mwanga wa taa tuliuona hafifu ingawaje taa ilikuwa na mwanga wa kutosha.
“Mwenyewe ushamsikia, kakataliwa na jamaaze, nduguze, mashogaze na jiranize, kafanya juu chini apate kunitia machoni na kwa hilo kasha wini....... nini sasa? Nini ananidai? Atoke huko,๐๐ mie simtaki wala sitaki kumwona abadani, akamrudie mwarabu wake.? Pomp leo kajaa hasira.
“Mwarabu!?” mie kuuliza.
“Yes, aliponzwa na mashogaze wasojua thamani ya ndoa za wengine,akaolewa na mwarabu wake, ndoa ya bei ghrama. Bibie kawekwa ndani hapati mapenzi ya dhati anapangiwa kulala na mumewe sababu mumewe ana bibi watatu wakubwa na yeye ndo’ Bibi wanne tena Bibi mdogo.”
“ Mmh! Mwanamke huyu, lo! Tumpe pole.” Mie nikaongea.
“Alie tu kayakaosa mapenzi, kaumia kaumizwa, baya zaidi magubu ya wake wenza yalivyo kuwa hadimu kupurukutika, huyo kimburukutu yakamshinda, akawa hana mbele hana nyuma, kutwa kuchwa ni kulia na kusikitika, kutwa kuchwa ni kujuta kwa maamuzi yaliyo jaa pupa.”
“ Ndio akome mwanamke mwenzangu,” Naliongea.
“Dunia hadaa, ulimwengu shujaa, hakufundwa na Mamaye sasa ulimwengu umemfunda.” Pompo alitia mafumbo.
“Ona, mshika mbili moja lampokonyoka.”
“ Aibu Pompo!”
“ Amtake nani sasa, wote wanaomtaka wanamtaka kama mtumwa na kumwacha kama mzoga, analazimisha ndoa na hiyo ndoa asiipate.”
“Teeh teeh teeh, ๐๐๐kageuzwa danguro la wahuni,” Nalicheka kimapozi mtoto wa kike.
“Kwani kaachwa!?” Pompo alinigea masikio nimsikilize vizuri.
“Yeye ndiye aliye muacha huyo Mwarabu, kamkimbia kule Pemba, kaona heri amrudie yule aliyemtema.”
“Na aliyemtema kamtema zaidi.” Nilitia neno.
“Hayo ni matapishi, uchafu utiao kinyaa, sipotayari kuyarudia matapiko.” Pompo alizidi kuongea, leo analitoa povu limtokalomoyoni.
“Mie nalijua kaachwa Pompo? Nikachombeza kutafuta umbea.
“Akome kuringia uzuri wake, sikia Love wasoyajua mapenzi daima uchagua, ubagua na kupangua,utazama mali na fahari za Dunia, kama kigenzo ch kuyaendeleza mapenzi, usahau uvumilivu, ungojevu na ustahimilivu, ni watu wenye haraka zilizo jaa pupa.” Pompo roho wangu alinijaza maneno.
“Tuachane na huyo Umbwakoko, keisha na keisha kuchoka, kachunwa sana na kabakia mifupa, liwe fundo kwake na kwa hao shogaze,” Nilimtaka Pompo tulale tushaongea mengi siku ya leo, Maua asituumize vichwa vyetu bado tuna nafsi ya kusonga mbele, mbele kwenye yetu maendeleo.”
######################
Ilipita miezi kadhaa Maua akijaribu kila njia ya kumshawishi wangu wa moyoni ayarudishe majeshi yake ndani ya moyo wa Maua, wangu hakuhitaji kuusikiliza ule upuuzi, hakuhitaji kusumbuliwa na yule kibibi mpuuzi, kama ni kumtema tayari keisha kumtema, kama ni kumfuta mtimani Pompo hana haja naye.
Mie kibedi changu hakikunitupa kikazidi kuongezeka na kutupa matumaini ya kumleta mtu nyumbani, mtu wa kutupa raha na furaha ya ndoa, basi miezi ikapita, ikapita, ikapita, ikapita isirudi nyuma, mie na kibedi๐คฐ changu, kibedi kikainuka kikatuna kikichezacheza kwa furaha na Raha tumboni mwangu, matumaini makubwa ya kukileta Duniani kile kibedi๐ผ๐คฑ yakaongezeka.
“Atazaliwa mtoto a jinsia gani?” Nalijiuliza mie na moyo ๐ wangu, nikatatizika sana lakini yote tisa kumi Pompo alikuwepo ubavuni kwangu.
“Labi atazaliwa wa kiume?” Pompo aliongea.
“Aka! Babu we,mie namtaka mtoto wa kike.” Nilimtania Pompobwa ubani.
“Mitoto ya kike kazi yao kuzaa zaa ovyo, usinilete litoto kama Maua, nitalitupa jahani mie.” Pompo alitania zaidi๐
“ Teeh teeh teeh๐๐
๐๐คฃ Aloo!๐,” nalicheka pompo pia alicheka zaidi.
“Nitakuletea mtoto wa kutusaidia uzeeni, kwanza tumwache akue ili akoshe vyombo, apugute deki, atufulie, akwende kwa soko na kadhalika.” Nalitania.
“Ujue mie napenda toto la kiume sweet love,maana toto la kiume litarithi mali.
“ Ebo! Babu we, kwani mtoto wa kike hawezi kurithi mali?” nalijifanya kuchukia kumbe la! Ndo’ mahaba nibembeleze hayo yashan'jaa.
“Mmh! We mwanamke, mtoto wa kike arithi mali zangu, waumeze watampora na kumpunja.” Teeh teeh teeh, Pompo kacheka mie nikapata raha.
“Kwa hiyo mtoto wa kiume akirithi mali wakeze hawawezi kumpora?” Nilimtega Pompo.
“Mmmh! Mwanamke una maneno weye, mbona wanitega Pompo alipata aibu yake.”
“Si nyie waume zetu ni wakoloni, mwamkandamizaje mtoto wa kike, mwamwona kama vile yeye ni dhaifu na hawezi.” Nilizidisha maneno kuntu.
“Mie sijanena hivyo.” Pompo kajitetea.
“Kwa hiyo kwa maoni na kwa mtazamo wako ungelipenda tumlete Malaika gani hapa Kigamboni, nyumbani kwetu.?” Nikamtwanga Pompo swali tamu
“Malaika Gabrieli.” Pompo alinijibu na kuniacha nacheka kicheko kikuu.
“ The teeh teeh teeh๐คฃ๐๐
๐๐ Aloo! ” nilicheka sana kwa furaha ile nacheka tu mtoto๐ผ wetu karuka ndani ya tumbo langu.
“Wacha matani Pompo mie nauliza jinsia ya mtoto na weye waleta maneno.
“Weye wataka mtoto wa kike na mie nataka mtoto wa kiume, tupo njia panda, basi tufanye kukubaliana jambo moja.” Pompo roho wangu akamemeza mate kisha akanena tena.
“Tuzae mtoto mwenye jinsia mbili, Tomboy au hapo unasemaje?” Pompo alinichekesha sana.
“ Makubwa!๐๐คฃPompo wangu utaniua mie kwa furaha unipayo."
“Au we unasemaje?” Roho ๐จ❤️๐๐จ♥️wangu kanihoji tena.
“Na mie ninakubaliana na mawazo yako, Pompo tuuzike mgogoro wetu, tuksribishe mapacha, dume na Jike.”
“Sio Tomboy mwenye jinsia mbili? Pompo alitania tena.
“Pompo nawe usinitakie mabaya mie toto la kitanga, naombea mapacha na weye wakazia mtoto mwenye jinsia mbili.” Naliongea nikajifanya kuchukia lakini kumbe ni nyodo zangu, nyodo ๐za mwanamke.
##########################
“Mama nakufaaa, nakufaa, nakufaa mie, Pompo niokoe” Nilkipiga ukelele mkuu, nikiendelea kutoka mbio ndani ya kichaka chenye nyasi mingi maua alizidi kunikimbiza, mkononi mwake amekamata kisu kikali chenye makali kuwili.
ITAENDELEA.
No comments:
Post a Comment