Saturday, August 2, 2025

UTABIRI WA KIFO

 


"KUFA UTAKUFA TU"⚰️


MTABIRI ALINITABIRIA KIFO CHANGU LAKINI KWA NASIBU NZURI MOLA ALIBATIRISHA JUU YA KIFO CHANGU.


    Juu ya Meza ya mviringo 🍽️ (Round table) kulikua na glass 🍷🍷 mbili zilizojaa fully wine tamu🍷🍾🥂  ya Zabibu, kuku mzima aliyerostiwa, pilau yenye nyama nyingi za ng'ombe pamoja na mchanganyiko wa Saladi ndani ya bakuri 🍲 kubwa. Mimi Julia niliketi na mpenzi wangu 'chai ya moyo wangu'😍 Enzo. Tulikua tukibugia pochopocho na kugugumia manywaji kwa furaha.


       Nikajichukulia glass yangu ya wine kisha niliweka kinywani wakati huo Enzo ananitazama kwa tabasamu mie huyo nikainywa funda zima kwa mkupuo, nilipomaliza kunywa na kuishusha shingoni Enzo akanipigia kelele:🙄


         "No! No! No! Julia, usimeze." 😱 Tayari niliisha kunywa funda la ile wine.


      "Embu usinisumbue, nisimeze ili iweje." Nilihisi mpenzi Enzo anajifanya kunisumbua. Macho yake yalimtoka pima akanishangaa.👀


       "Unahisi nini baada ya kuinywa hiyo wine?" Aliniuliza akitazamia kama kuna jambo la ajabu laweza kutokea mbele yangu.


     "Kawaida tu mbona sioni jambo la kushangaza."‼️ Ni kweli baada ya kuinywa ile Wine hakuna jambo lolote nililohisi ukitegemea kichwa changu kilijaa lundo la mawazo juu ya Safari🚄🛤️ niliyotarajia kuanza siku ya kesho. Safari ya kwenda Dodoma  kufanya Interview juu ya Kazi ndani ya Kampuni ya Vodacom.


      "Umemeza Pete💍 mpenzi, Pete hiyo niliiweka ndani ya glass la wine. Naomba niahidi jambo Moja je upo tayari nikuone." Aliongea. Mie na Enzo tumedumu mapenzini huu ni mwaka wa Tano lakini hajawai kunitamkia habari za ndoa.👰💒 Ajabu Leo.


       "Enzo wacha kuongea juu ya mambo nisiyoyaelewa yaani mie ninawaza juu ya Safari ya kesho wewe unawaza habari za ndoa. Usinichoshe Bana." Sikumjibu lile wazo la mtima wake zaidi ya kumvunia moyo.💔


   

   "Nahisi kichwa kinanigonga🤕 embu wacha niende Hospitali 🏥kumwona Bana Dakta" 👨‍⚕️ Niliacha kula na kunywa nikaamka pale mezani na kuchukua mkoba 👜wangu nikaelekea Hospitali kumwona Dakta.


 

     "Naweza kukusindikiza."🚶‍♀️🚶‍♂️Mwanaume  wangu anavyojali, nitachoka mie.👌


      "La,asha! We endelea kula na kunywa Leo ninahitaji kutoka pekee." Nilimwacha Enzo pale mezani akinisindikiza kwa macho ya wasiwasi👁️‍🗨️ ambao sikujua Nini haswa tatizo linalomsibu. Baada ya kuchukua Tax🚖 yangu nilielekea Hospitali.


***************************


Nilipofika Hospitali nilielekezwa chumba ambacho  Dakta yumo, lakini kwa bahati mbaya Dakta alikua akimhudumia👨‍⚕️🩺💊 mgonjwa  mwingine. Ilinibidi nisubirie. Nikajiketisha pembeni ya mlango wa Dakta hapo Kuna benchi la chuma. Nilimuona Babu mmoja ameketi nilipomtazama nilimkadiria umri wake kama miaka sabini na ushee alikua amevalia nguo chafu na kuukuu zinazotoa harufu ya kunuka. Nywele zake ndefu alizozisokota zilinuka pia, viatu alivyovaa vilinitia kinyaa,😤🤮 sikupendezwa na uwepo wake lakini tisa kumi mimi nilikuja nikiwa ninashida zangu na yeye alikuja akiwa na shida zake. Nilimpotezea.💩


       "Wanakuita Julia" Toba‼️! Nilishtuka baada ya yule Babu niliyehisi kuwa ni mkichaa alipolitaja jina langu.


      "Ndio, 👍umelijuaje jina langu." Nilimuuliza nikiwa Bado nashangaa.😑


       "Nina uwezo wa kujua, kutamba na kutabiri kuhusu mambo yajayo au yaliyopo, leo una bahati sana ya kuonana na mimi najua umemeza Pete, Pete yenye kito cha Almasi, umemeza pasina wewe kujua." Ah! Jamani! Alinikumbusha kuwa masaa machache yaliyopita Enzo aliniambia kuwa nimemeza pete.💍


      "Yawezekana vip mbona mimi sihisi jambo lolote kuhusu kumeza Pete ambayo unadai nimemeza?" Nilimuuliza.


     "Nisikilize Julia, natambua una mawazo mengi juu ya Safari yako kutoka Dar kwenda Dodoma kufanya Interview." Nilihisi yule mzee atakua mshirikina. Yawezekana vip kuyajua mambo yangu au labda ni tapeli.‼️ Sikuambulia jawabu.


     "Yote unenayo ni kweli tupu lakini umeijuaje mipango yangu?" Hakunijibu zaidi ya mimi kumkazia macho na kumshangaa.👁️🥺


     "Julia!" Aliniita. "Mpango wako wa kusafiri kwa Ndege🛩️ hautafanikiwa sababu mvua kubwa sana itanyesha na hali ya hewa itakua mbaya."🌧️


"Babu tusitishane, unajua ni kiasi gani cha pesa nilizolipia Safari yangu ya kwenda Dodoma?" Nilimkaripia.🤮


      "Kama wadhani mimi ni mwehu wa kuyaamini maneno yako yaliyojaa hasara, umepotea Babu? Nimetoa pesa nyingi kulipia Ndege alafu ajitokeze mtu kudai ati mvua itazuia Safari yangu. Neva, kamwe haitatokea." Sikupendezwa na maneno ya yule mzee.


       "Usikatishe watu tamaa kwa utabiri wa uongo." Sikumuamini.


       "Kwa maneno ni vigumu lakini kwa vitendo jambo lako litatimilika. Naomba ukirudi nyumbani uwe makini na Oven uitumiayo kuoka nyama na mikate itakusababishia kifo."


        "Kwendraaa huko!🫥😶‍🌫️Usinitishe, Maisha yangu yapo mikononi mwangu. Wewe sio Mungu mpaka ujue kuhusu Maisha yangu au kifo changu" Nilimjibu kwa dharau. Bwana Dakta alimaliza kumhudumia mgonjwa aliyetangulia akaniruhusu kuingia chumba chake cha Udakta, nikamuacha yule Babu mtabiri akiwa ameketi benchini anitazama kwa tabasamu.😊😌


~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~


   Jamani! Pozi lote liliniyeyuka baada ya mie kujipamba vizuri nikiwa tayari nimebeba begi langu lenye Kila kikolombwezo pamoja na nguo nzuri za kubadili nikifika Dom kwenye Safari yangu yenye heri na mafanikio maana nilijua iwapo nitapata kazi basi Maisha yangu yatanyoooka kama Rula. Pesa itanitembelea, furaha yangu na ya mpenzi Enzo itaongezeka. Nilishangaa kuona na kusikia paa la nyumba yetu likipigwa na mvua 🏠🌧️. Haikua mvua ya kawaida ilikua ni mvua ya mafuriko.


      Nilichungulia Dirishani kwa masikitiko zaidi maana ilianza kunyesha muda wa asubuhi hadi jioni Bado ilikunya tu bila pumziko. Nikiwa ningali Bado natazama Dirishani simu yangu iliita.📲


       "Hallow Julia." Mpigaji aliniita


       "Hallow, nani anaongea!?"


        "Director, Ofisi za shirika la Ndege hapa. Samahani naomba nikuambie Safari ya Leo kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma haitawezekana sababu ya tokeo la mvua ya mafuriko, hali ya hewa sio Rafiki lakini tutakupa taarifa iwapo Mambo yatakua sawa." Oooohfy😤 nikayakumbuka maneno ya yule Babu aliyejitambulisha kwangu kama mtabiri, nikamkumbuka aliniambia hali ya hewa sio rafiki kwahiyo Safari yangu isingelifanikiwa. Nilisikitika lakini taratibu kadri muda ulivyoyoyoma nilianza kusahau maneno ya yule Babu.


Jioni ilipowadia njaa ilianza kunisumbua nikapata wazo wacha Leo nimwandae kuku mzima nimle pamoja na Saladi niliyoanza kuiandaa.


      Nikafanya hima kumwandaa 🐓 kuku wangu wa kienyeji Kisha baada ya maandalizi nikafanya kumuweka ndani ya Oveni langu, nikawasha ile Oven. Kumbuka wakati huo tayari nimekwisha sahau na kuyapuuza maneno ya yule Babu mtabiri. Nikabinya kitufe cha kuwashia Oveni yangu. Uwii! 🥴Ile nawasha tu nilishtuka nabebwa na nguvu nisizozijua nikatupwa mbali, kichwa changu kikagonga ukuta, damu nyingi zilianza kunichuruza. Nikazimia mtoto wa kike.


       Nilikuja kuzinduka asubuhi tayari kumekucha, majogoo yamechoka kuwika, Jua lishachomoza na waja waendelea kupambana na hali zao. Nilijikagua na kugundua damu🩸 imegandiana sakafuni, sikuumia sana. Nikajisafisha na baada ya hayo yote nikapata wazo wacha nizurure zurure🚶‍♀️ mitaani kumtafuta yule Babu mtabiri sababu matukio aliyonitabiria Jana yametukia kweli alafu mie mpuuzaji nafanya mzaa.


     Sikutaka kutoka na Gari yangu 🚘, nilichofanya ni uamuzi wa kutembea kwa miguu kulizunguka Jiji 🌇sehemu muhimu ambazo nilihisi mtabiri aweza patikana. Sehemu ambazo ndani ya Jiji Kuna ombaomba, waokota chupa au mafukara waliokata tamaa. Mtabiri mwenyewe mwonekano wake ulisadifu ufukara uliopitiliza.


      Ilala boma, nilimwona akiwa ameketi llala boma kituo cha mabasi yaendayo Kigogo na Manzese kuna Shule ya msingi Boma. Moyo wangu uliripuka kwa furaha. Hisia zangu hazikunidanganya alikua ameketi sakafuni pembeni Kuna bango  kaandika  'Nisaidie Leo na mimi nitakusaidia kesho' chini ya lile bango aliweka bakuri kubwa ambalo wapitao njia walidondosha shilingi mia mbili au tatu na vijisenti vingine.


    "Babu!" Niliita mkononi mwangu nilikua nimekumbatia chupa kubwa ya kilevi aina ya Hanschoice. 🍾Nikamwekea pale alipoketi.


       "Hapana mwanangu mimi sijazoea kutumia kilevi." 🍺 Tulikua Bado hatujapeana salamu 🤝lakini ajabu tulizoeana haraka sana.


     "Kamata hizi pesa." Nilitoa bunda la pesa noti mpya za shilingi elf kumi kumi karibu lakini mbili na ushee.💵💲


       "Nitachukua shilingi elfu ishirini tu." Alichomoa noti mbili za elf kumi kwenye zile laki mbili na ushee.


     "Pesa zote hizi nimekuletea wewe tafadhali chukua." Nilimbembeleza.


      "Hapana mwanangu, ninachukua pesa hizo kulingana na Nasibu yako. Nasibu yako ni mara mbili tu." Sikumuelewa amenayo nikajiketisha karibu na pale alipoketi. Wapitao walipita wakamdondoshea vijisenti kadhaa.


       "Maneno uliyotabiri Jana yamenitokea kweli" Nilimwambia, nikamtazama kuanzia miguuni hadi kichwani, angali mchafu mchafukoge, Leo alivaa saa kubwa ya mviringo yenye kamba iliyopita kuzunguka shingo yake.


       "Una bahati sana Julia, muda wako ungali Bado kidogo sana lakini kama ni suala la kufa, kufa utakufa tu."⚰️


      "Nina kosa au hatia gani hadi mimi nife? Ninahitaji furaha na Amani ya moyo wangu." Nilihuzunika.


      "Kila kiumbe kina muda wake wa kuishi, muda wa kiumbe ukiisha lazima kiumbe kife."


     "Kwahiyo muda wangu wa kuishi umeisha?"


      "Una bahati sana Julia, unabahati mara mbili mbili lakini kufa ni jambo la lazima."


     "Unaniumiza unavyoongea maneno machungu kwangu, je wewe haujawai kuumizwa kwa maneno au vitendo usivyopendelea."


     "Nimeumizwa sana Julia, nimetiwa uchungu mwingi sana lakini nimevumilia. Acha nikuambie rejea nyumbani kwako Leo usiku wa saa sita kamili kifo au bahati itakuchagua."


     "Tafadhali nionee huruma, batilisha utabiri wako." Nilimparamia mwilini. Mikono yangu ikagusa ile saa yake kubwa alivyovaa shingoni. Mkono wangu ukaigusaile saa. Akanitazama na kuutazama mkono uliogusa ile saa yake.⏱️


        "Mungu ataamua Julia, ataamua muda wa wewe kuishi au kurudi mavumbini. Rejea nyumbani." Chozi 😿 lilinitoka nikafanya kujitoa mwilini mwake taratibu bila kuaga niliondoka.


     "Nimesema sinywi kilevi, mbona umeacha chupa yako hapa?" Sikumsikiliza moyo wangu uligubikwa woga, hofu na wasiwasi.


___________________________


Baada ya kuambiwa kuwa usiku wa Leo nitapoteza Maisha, nilivirugwa na kuchanganyikiwa. Mchana wa siku ya Leo nilioga vizuri, nikasimama  pale dressing table nikajipaka na kujipodoa, nikachagua mavazi niyapendayo, kisha nikafungulia Radio,🎼 Muziki wa singeli ukanifanya nirukeruke kama mwendawazimu juu ya sofa pale sebuleni.


     "Julia.💖💘" Sauti ya Mpenzi wangu Enzo iliniita. Alikatisha furaha yangu ya mwisho. 


       "Enzo!" Nilimwita mpenzi wangu na kulazimisha tabasamu👩 bandia linitoke asijegundua juu ya changamoto iliyonisibu.


      "Nimegonga sana mlango lakini hujatoka kunifungukia." Enzo alilalamika.


       "Sauti ya Muziki ipo juu, nisingeliweza  kusikia." Nilimjibu Enzo aliyenikumbatia na kunimwagia mabusu tele.


     "Enzo, Kuna jambo nataka kukuambia." Nililazimisha tabasamu la lazima.


       "Niambie Sukari ya moyo wangu, nashangaa umejawa tabasamu. Leo unayofuraha isiyo na kifani. Enzo aliniona mwenye furaha kumbe mwenziwe nimetekwa na wasiwasi.


      "Naomba tucheze 'Pillow fight'  mchezo wa kupigana na mito. lwapo nitaibuka kidedea basi wewe utaninunulia pizza 🍕 na iwapo wewe utaibuka kidedea nitakununulia Baga."  Nilihitaji kula chakula ambacho siku zote nilikichukia maishani mwangu.


      "Julia tangu lini umeagiza 🍕 pizza au kuniruhusu ninunue bagga🍪🍔 si ulisema hauvipendi vyakula hivyo!?" Sikumjibu Enzo. Nikaokota Pillow Moja na kumrushia mimi pia nilibaki na Pillow Moja. Tulianza kuchezea mito. Nilijitahidi kumdunda kwa mto na yeye alifanya hivyo japokua hakufurahia sana sema alipenda akafanya kunirukia pale sofani akanilalia, mdomo wake ukakutana na wangu mie, 👄ndimi zikakutana, mabusu Moto Moto💋, mikono yake ikalipapasa tumbo langu mie. Joto la mapenzi 🔥 likatukamata, tukajikuta watupu kama tulivyo zaliwa. Huba likapamba moto.


                      ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


Enzo aliinunua Pizza 🍕 pamoja na Soda, tulikula na kutaniana. Simu yangu iliita nikaipokea. Walikua ni madirector waliotaka kunifanyia lnterview kule Dodoma waliniuliza iwapo nitakuja kwenye lnterview au ndo basi nimegahiri


Mie na tabasamu 🤗 langu la bandia nilijikuta nasema sintakuja nimegahiri, sababu kuu nilijua mwenyewe nilijua tu Sina muda wa kuendelea na Maisha maana aloyotabiri mtabiri yalinitisha.


                       ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


Nilimwomba Enzo arejee tena saa Tano usiku kupata Dinner ilipofika saa Tano usiku juu ya Meza nilitandaza Wine, vyakula vinono na madikodiko mengine. Mie macho yangu kila dakika yalitizama saa ya ukutani inavyovuta mshare🏹 wake taratibu. Enzo alipowasili tulipokeana kwa furaha kama Njiwa🕊️🕊️ wapendanao, tukajiketisha mezani tukitizamana kwa huba na mahaba.


      Nilimimina wine ndani ya glass zetu🥂 mbili, nikafanya utundu wa kuiweka Pete ya Almasi kwenye glass ya mpenzi wangu Enzo, nilitaka kumfanyia Sapraizment. Tuliendelea kula na kunywa taratibu wakati huo mie naibia kutizama dakika za ile saa ukutani zinavyoyoyoma. Woga moyoni ulinivuruga maana niliishaambiwa ifikapo saa sita kamili Sina changu Duniani.😢😿


     Enzo aliinyanyua ile glass 🍷yake yenye wine mara Moja akagida funda zito la ile wine, hakuweza kumeza nikamwona kama vile anatetereka, mkono wake wa kulia kaupeleka kinywani, akatoa kitu kinywani, Pete 💍 niliyotegesha kama sapraizi. Kwanza alishangaa mie ningali natabasamu.


    "Julia Pete hii....." Hakumaliza kunena niliropoka.


     "Enzo will you marry me👰💒...... Utanioa!?"


Enzo wangu aliingia sura ya furaha na tabasamu 🤗nikamnyoshea Dole langu la chanda 🖐️kwa mapenzi na unyenyekevu Enzo alisimama pale chakulani akanifata na kunipigia goti miguuni akafanya kunishika Dole la chanda Kisha akasema l will marry you Julia akanivisha Pete yenye kito cha Almasi.🤣👩‍❤️‍💋‍👨

     

      Akasimama amejaa tabasamu, akanitazama na kuniangushia busu😚😘 mfululizo. Moyo wangu ukanituma nimwambie kuhusu yule mtabiri na maneno aliyoniambia. Nilitamani kumweleza kuwa ifikapo saa sita mimi sio mtu tena Bali ni maiti. Nikafungua kinywa changu kunena:


     "Enzo nataka nikuambie neno." Bahati mbaya kabla sijanena nitakalo kunena mkono wake ulitua mezani pale mezani glass yangu ya wine ikadondoka chini 'paaa' ikavunjika.


        "Nitasafisha mpenzi Julia."  Enzo akaniachia.


      "Aaah! No, niachie hiyo kazi." Hakusubiria, alitoka nje kwenda kutafuta fagio na zoleo. Mie macho yote juu ya saa ya ukutani iliyoonesha Bado dakika mbili tu saa sita igonge alama. Kama walivyosema wahenga usiku utakucha, mbio za sakafuni uishia ukingoni, lisemwalo lipo kama halipo langojewa saa sita kamili ilitinga Mie nikafumba macho na kuyakaza kwa nguvu maana nilijua mwisho wangu tayari umewadia. Dakika zikayoyoma mie nikafumbua macho kwa hofu na woga. Uwii! Saa ya ukutani ilionesha ni saa sita na dakika Moja.


      "Asante Baba Mungu wewe ni Bwana wa Majeshi ulieniepusha na kifo nilicho tabiriwa Leo" Nilifanya lbada kimoyomoyo nisiamini kama nimekiepuka kifo nilicho tabiriwa. Basi tabasamu na kicheko vikanivaa.


     Enzo aliingia akiwa na fagio pamoja na zoleo mkononi nilikua ningali nikitabasamu  kama domo la kiboko, nikimtazama kwa furaha akija kama Malaika lakini ghafra nilianza kuhisi kizunguzungu kikinipiga kichwani, kilikua ni kipanda uso kama vile nimebeba Mlima kichwani. Nilihisi nakandamizwa na kitu kizito ajabu. Sikumbuki kilichofuatia maana nilidondoka chini sakafuni nikazima moto.


'''''''''''''''''"""""""""""""


     "Julia.... Julia.... Umepatwa na nini?" Enzo Alimikimbilia Julia na kumtikisa asijue Julia amepata changamoto gani.


     "Tafadhali amka Julia." Enzo alichanganyikiwa. Haraka akafanya kuita Ambulance 🚑 


"""""""""""""""""""'""""

      Nilipofumbua macho yangu niliangaza kulia na kushoto nikamuona Enzo 'chai ya mtima wangu' Amenishika mkono alionivisha Pete ya Almasi.


        "Julia, umeamkaje?" Alitamka 


       "Niko wapi hapa!?"  Nilimuuliza Enzo.

 

        "Hospitali 🏥Julia, ulipata kizunguzungu ukaanguka." Tukamwona Dakta anaingia wodini.


    "Hongera Julia, amini upo salama "


    " Hapana Daktari mimi sipo salama ninakufa na muda wangu wa kufa umewadia." Nilikua kama ninechanganyikiwa sikuelewa kinachoendelea. Enzo na Dakta walinishangaa.


      "Upo salama Julia, tendo la kuanguka kwako ni kitu common kwa wanawake wengi wenye mimba changa. Acha nikuambie una mimba yenye wiki kumi na mbili."


    "Eeeh!" Mimi na Enzo tulishtuka na kushangaa Dakta akafanya kuleta picha ya Utra sound akatuonesha picha ya kijusi 👶chenye miezi mitatu tumboni. Wawili sie tulibaki mshangaoni.❗


    "Sasa Bwana Enzo nakuomba usubiri nje kwa masaa machache mgonjwa apumzike anahitaji pumziko la kutosha." Dakta alimwambia Enzo na Enzo alitii akatoka nje mie nikabaki nimesongwa songwa na mawazo Kisha usingizi ukanichota.


     """""""""""""""''“'"""""""

Nilikuja kushituka mara baada ya kuamka usingizini na kumuona mtu amesimama karibu na dirisha la chumba cha Hospitali, alinipa mgongo na alikua amevalia koti la Daktari nywele ndefu na chafu zilinifanya nimtambue. Akageuka kisha akalivua like koti la Dakta na kuliweka juu ya Tenga la makoti ya pale Ofisini. Tukatazamana.


    "Nafikiri mwanao atazaliwa wa kiume." Aliongea na kunisogelea.


   "Hongera umekikwepa kifo zaidi ya mara mbili, Mungu amekupangia siku nyingine, utaishi." Aliongea akiwa amesogelea kitanda nilicholalia.🛏️


   "Asante Babu mtabiri, nilijaa hofu na woga." Nilimweleza.


     "Uwe na Amani," Aliongea "Niite Babu Sam.....Sam ndio, latosha Babu Sam." Nilifurahia kulikua jina lake.


     "Nikuache upumzike." Sikutamani aondoke lakini alifanya kuondoka taratibu, macho yangu yakimsindikiza mlangoni alikotoka akasimama pale lilipo dirisha la chumba nilicholazwa. Alisimama kama mtu anayefikiri na kutafakari kuhusu jambo mara nilimwona Dakta akipita, Uwii! Nilishtuka baada ya kugundua kuwa mtabiri amepotea kimiujiza, haikua ndoto ya kawaida Bali ukweli usio wa kufikirika.


Babu Sam hakuwa ni mtu wa kawaida yamkini ni Malaika aliyetumwa kutabiri kuhusu jambo fulani kama msiba au furaha.


          Kwisha kutoweka kimiujiza  kwa Babu Samu macho yangu yalitua juu kitandani niliona saa, saa ambayo Babu Samu aliivaa shingoni, ile saa ambayo niliigusa pindi  nilipomletea Kilevi aina ya Hanschoice. Kile kipindi mie naomba kuhurumiwa nisijepatwa na  mauti bali Mola ausogeze muda wangu mbele, Niliichukua na kuitazama nisijue ilikua na maana gani Babu Sam kuniachia ile saa juu ya kitanda yamkini ile saa yaonesha majira yangu . Inapotick nitaishi lakini ikiach kutick sina budi kushukuru Mola kwa zawadi njema ya uhai.


~~~~~~~~~


TCHAO 💖 


~~~~~~~~~

No comments:

Post a Comment

BEKA

 SURAYA TATU                        “AKIPITA ATAJIPITISHA.” Beka akawa member wa kampuni ya SIGA, akipelekwa hapa na pale kulinda mali za ma...