Friday, August 8, 2025

MWENZENU N'SHAPENDWA


MWENZENU N'SHAPENDWA 



Sehemu ya tisa (Mwisho)


     "Nina kuua mwanamke wewe, ninakuaa unieleze kwanini unipokonye mume wa moyo wngu," Maua alinikimbiza mie pia nilikimbia pamoja na ujauzito wangu. Pindi Maua ananikimbiza ndio mabadiliko mbali mbali yalitokea mwilini mwake, kichwa chake kiliota pembe mbili ndefu kama kama za Ng’ombe, meno yake yale madogo yakawa marefu kama pembe za mbuzi, kucha zake zikaongezeka zikatisha zaidi, Maua akaongezeka urefu akawa mrefu tena mrefu zaidi.

        
      “Mwenyewe ulimkataa sasa wamtakani?” niliongea kwa ujasiri nimedondoka chini ya aridhi mara baada ya kukimbia na kuchoka.


           “Sijali maneno uyasemayo ninachojali ni kumrudisha Pompo wangu. Nasemaje utamrudisha Pompo mikononi mwangu au hautamrudisha?” Safari hii mdomo wa Maua ulikuwa ukitema damu, niliogopa mie, niliogopa hali ile, niliogopa sana, kumbe Maua ni Jini, lo! Ama kweli leo nimepatikana.



          “Kamwe, Pompo haumpati tena usijisumbue bibie, acha nijilie vyangu, mwenzio n’shapendwa wewe endelea kukonda na kudhoofika.” Nilimjibu Maua ambaye alizidi kunisogelea pale nalipokuwepo anatisha kweli, nguo zake kuukuu kama vile mfu aliye fufuka muda si kitambo.



           “Wanijibu jeuri si ndio, sasa nataka nikuue wewe na mtoto wako ili nimpate Pompo wangu Maua alinitisha alinitisha zaidi tena zaidi sana. Nikasikia miungurumo ya radi, mvua ilianza kunya taaratibu tna kwa ghafla.


         “Ninasema hivi mie sifi, Pompo hafi wala mwanangu, kama ni kufa utakufa wewe mwenyewe tena utakufa kifo kibaya kifo cha kugongwa na gari. Nilimtolea kiapo Yule mwanamke mwenzangu.



           “ Umbwa wewe mwenye bahati, mie ningelijua nibora nisingeli muacha Pompo wangu,tamaa na starehe za dunia ndizo zilizo niponza. Ona mwanamke mwenzio mie leo ninajuta.” Jini Maua aliongea kwa kusikitika.



         “lwe fundo kwako na kwa wenzio, iwe fundo kwamba umpendaye mpende, akupendaye usimuache solemba, haijalishi ana maisha ya kikabwela, ana ulema au ulemavu, kasoro, hali ya umasikini au utajiri. Mpende kiroho safi na uzuri wa mapenzi Mwenyezi Mungu atajalia.leo hii Mume wangu kaanza kuusimamisha mjengo wa Horofa tatu na wewe kimburukutu fukara umeanza kuutamania, leo hii Mume wangu kanunua Tax gari yake mwenyewe weye mjaa tama umetamania, nakwambia hivi mazuri mengi yanazidi kutufuata.” Nilijigamba


          “Ndo’ maana waswahili wanasema yajayo yanafurahisha, ulimdharau, yule muuza kahawa, mzibua vyoo, mwosha magari, muuza pipi na karanga, msukuma guta, fundi mjenzi asiyechagua. wala kubagua kazi, leo hii amefika mbali kimaisha ndio weye mjaa laana umtake.” πŸ‘ŒπŸ™Š Niliongea kwa kirefu, Maua tayari alikwisha fika magotini kwangu ananitazama kwa hasira, macho yake yalikuwa yakiwaka moto, mvua nayo haikukoma, hakika siku ile niliyatimba mtoto wa kike, kifo kilikuwa karibu yangu, lakini yote tisa kumi mie nilijitetea.


        “Tukubaliane jambo moja," Maua alionge amejaa tamaa ya kunipoka roho wangu.


         “Kuniachia Pompo wangu au kufa kwa ajili ya Pompo wangu.” Jini Maua aliongea na mie nikamwambia.


         “Sikia Maua, tukubaliane jambo moja, waniachia Pompo wangu au kufa kwa ajili ya Pompo wangu,”


           “ Teh teh teh,πŸ˜…πŸ˜… aaah!” Jini Maua alicheka sana, damu zikimtoka mdomoni radi ikapamba moto. Mie nikaogopa zaidi nikatetemeka tetemeko kuu.


          “Unajitia jeuri au sio , nilikwisha kuambia mie ndio Maua mtoto wa kizaramo, nimezaliwa uzaramoni nimekulia uzaramoni, nimefundwa nikafundika ninafanya kwa kadri moyo wangu unavyonitaka nifanye.” Maua aliongea kwa hasira.πŸ‘Ώ


            “Na mie nilikwambia mie ndiye Mamsapungo toto la kitamga , nimezaliwa Tanga, Lushoto ndio nyumbani kwetu, nimefundwa nikafundika, Mapenzi ninayajua tena mapenzi ninayaweza, thubutu jaribu kushindana na mie ili uone kuwa sinaga utani na mtu.” Nilimjibu Maua


           “Sasa ninakuchagulia kifo kama komesha yako, Maua alinitisha zaidi, ingawaje nilipoteza matumaini lakini nilikuwa na moyo wa imani na ujasiri wa kuokoka, Mungu alibaki kuwa tumaini langu.


             “Sifi wala nini kufa utakufa wewe usiyeyajua mapenzi, usiyejua uvumilivu tena usiyejua nini maana ya kupenda.” Nilimnanga adui yangu.


Mara ghafla –pasina muda kupoteza Jini Maua alikinyanyua kile kisu chake chenye makali kuwili, Mola we Uwii! Alikitua katikati ya tumbo langu pale alipolala mwanangu mtarajiwa, maumivu, maumivu makali maumivu ambayo sijapata kuyaona, Maua akaachia tabasamu, tena akacheka kicheko kikuu kicheko chenye makali ya radi, Mie nikapiga ukelele mkuu.


            “Mama nakufaaaaa”πŸ”ŠπŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­


            “Mamasapungo, Mamsapu, Mamsapu…….” NILISHITULIWA NA SAUTI YA Pompo roho wangu, nikashituka shituko kuu, macho pima kama Jusi 🦎 aliyebanwa mlangoni, nikiangaza huju na huko nisijuwe nipo wapi hapo.


             “Pompo nipo wapi hapa.” 😢‍🌫️Bado fahamu hazikurudi kiwepesi.


              “Upo nyumbani, nyumbani Kigamboni, mama wa moyo wangu.”


              “ Mbona damu sizioni tumboni kwangu,” Nilijikagua kagua sehemu ambayo nilisadiki kuwa Maua kanichoma kwa kile kisu chenye makali kuwili.

                “Ni ndoto Mamsapungo, ni ndoto moyo wangu, ndoto ndiyo iliyokufanya uweweseke.” Pompo alinifungua milango ya fahamu. Mara kwa ghafla nikaanza kusikia maumivu ya tumbo, ni uchungu, uchungu wa ghafla uliotokana na kushituka, shtuko kuu shituko lililotokana na ile ndoto yangu ya usiku ule mzito wa manane.


                 “Pompo maumivu, uwiii…..Maumivu….ya tumbo.” Nalianza kulia, nikijishika urwanda rwangu ( tumbo langu)


                    “TATIZO NINI WANGU WA MOYONI?” Pompo alihoji.

                  “Uchungu Baba, uchungu roho wangu, naumia mie.” Pompo alinishangaa hakutaka muda kuupoteza alihitaji kunisaidia.

                “Pole love, pole sweet heart, twende Kigamboni Hosptali. Haraka sana Pompo alibadili nguo za kulalia akavaa za kutembelea usiku ule, tayari keisha nibebea vitu vyangu muhimu vinavyohitajika Hosptali, kanitoa njee ya nyumba yetu na sasa ananipeleka Kigamboni Hosptali, kwa ile Tax gari yetu.


           “uwiiiii, uwiiii, uwiii! Oooh! 😒😒😒😿Nafwa mie” Nalilia nikiwa nyuma ya gari ambayo Pompo alikuwa akiiendesha.

             “Pole moyo wangu, Subira yavuta heri, ngojea weye mwenyewe utafurahia.” Pompo alinifariji Gari ikazidisha mwendo.


                    ##################


“Pole sana dadangu” Nesi aliyenihudumia usiku wa jana alinifariji.

           “Asante sana Nesi, Mwanangu anaendeleaje.” Nilimuuliza Nesi tabasamu langu mdomoni, hamu ya kumuona Malaika wangu ilinipanda.

             “Nesi, mdogo wangu mbona wanikalia kibubu, nijibiwe mie mzazi, leo ninafuraha ya kuitwa Mama, nimeleta mtu katika familia, heshima kubwa katika jamii inizungukayo.” Niliongea na yule Nesi aliyeekuwa angali bado kimya ananitazama mie kama kitu kipya machoni kwake. zilipita sekunde chache yule Nesi akafungua kinywa chake.


                 “Nina masikitiko bibie.” Nesi hakuonesha furaha tena, mara ile nikamuona Pompo roho wangu, akiufungua mlango mkuu wa kile chumba nalicholazwa, akaingia Maua πŸ’mkononi, Juisi πŸ§ƒna matunda mkononi.πŸ‡πŸŒπŸ₯­


                 “Niambiwe Nesi wasikitikani?” naliingiwa na hofu, Pompo alisogea karibu na kitanda nilicholazwa ayasikie maongezi yetu.


                  “Mwana uliyemzaa, hatunaye tena mtu huyo, si riziki yako Mamie” Nesi aliongea kwa masikitiko. 


                “What!?” Mie na Pompo tulitamka kwa umoja.


               “ Wamaanishani Nesi?” Pompo alimuuliza Nesi.

                “ Mwanao alipotoka tumboni akaaga Dunia, tusijue nini kilichomuua lakini bwana Dakta kasema mtoto alishindwa kupumua mara baada ya kuzaliwa.” Nesi aliongea kaniachia SIMANZI Mie na roho wangu Pompo. Machozi yakanisururuka, nikalia mie, nikalia Mamsapungo, nikalia masikini.


         “Pole sana mke wangu.” Pompoj alinifariji, ningali bado namwaga machozi.


          “ Asante sana roho wangu ya Mungu mengi, ametupa na wakati huo huo ametuchukulia"


             “Ipo siku atatupa tena.”

            “ Najua Pompo najua Love.” Nililia kwa uchungu, nililia kumpoteza pacha wangu.


             “ Unasikia my love,” Pompo alihitaji kuendelea


             “ Nakusikia my love” Mie nikamwaga tena bomba la machozi ikawa ni kazi ya pompo kunifuta yale machozi na kunifariji.


            “Kuna habari mbaya nimeipata kuhusu Maua, Maua hatunaye mtu huyo,”

             “ Mmh!" Niliguna mie nikamtazama roho wangu Pompo nisitake kuamini yale ayanenayo.

            “Maua kaaga Dunia?!” nikamhoji Pompo.


             “Ndio kagongwa na Gari, asubuhi ya leo, kagongwa vibaya sana,kichwa kule, kiwiliwiili kule. Ati alichanganyikiwa kama majiranize wanavyo sema, akili zillimruka, aeshi kulitaja jina languπŸ”Š, Pompo pompo, pompo kama mwendawazimu” Pompo kanieleza.

        “Oooh! “ nilisikitika nikaikumbuka ile ndoto niliyoiota usiku wa kuamkia jana. Je, ndoto niliyoiota jana inaendana na matukio yaliyotokea siku ya leo? Nilijiuliza nisipate jibu.


          “Mola amlaze pazuri Maua.” M ie niliongea


          “ Nyota mbaya imedondoka.” Pompo kaongea, mie mawazo yananizidia kichwani.


          “Shauri ya wivu na tamaa, ndio sababu ya kufa kile kifo, ona sasa ,ona wivu kidonda, wivu unaua.” Pompo alizidi kumlaumu marehemu.


         “Acha Pompo , acha usiendelee kunena, acha ujue kuwa na sie tushampoteza Malaika wetu. Roho wetu, mtu wetu katika familia.hatunaye tena mtu huyo.” Niliongea machozi yamenijaa tele.


           “ Nikwambie Pompo,”Nilimwambia Moyo wangu.


           “SEMA Love, mama wa watoto wangu.”


            “Yaliyopita si ndwele, tulilinde penzi letu lisiingiwe na soko.” Nliongea ningali bado nina sikitika.


             “Tutalilinda my love, kwa nguvu zetu zote, ata kwa bunduki na kwa risasi.” Pompo aliongea.


            “Kwa amani upendo, furaha uvumilivu na ustahimilivu.” Nikamjibu Pompo

               “Penye chuki pawe upendo, penye dhiki pawe faraja, penye mateso pawe raha na amani tele.”


              “Ujue mie napenda sana amani Pompo, amani hiyo ni kila kitu kwangu, amani hiyo ni wewe unitulizaye mtima wangu, nakupenda sana Pompo roho wangu, nakupenda mume wangu, ninafuraha kupendwa na wewe.” Niliongea.


             “Ninakupenda pia amani wa moyo wangu, pompo alinikumbatia nikampiga mabusu πŸ‘©‍❤️‍πŸ’‹‍πŸ‘¨elfu nyingi na yeye akaniiiibusu elfu nyingi😚😘, faraja ile ilinifanya nijisikie kupendwa. Aki! Mwenzenu n’shapendwa, sijui nyie shoga labda niwaambieni, ukipendwa pendeka, mpende akupendaye, mwache asie kupenda ukimpenda aso kupenda atakutesa mtu huyo. Aku! Mie n’shapendwa.


           ******************************


   Nyonyo mie nipo kuuguza tumbo langu, tumbo la uzazi, nipo kwenye machungu ya kufiwa na Malaika wa moyo wangu, faraja zenu shoga zangu faraja zenu niambiwe “Pole Mama la kitanga, ugua pole” ili mie shoga yenu niliyependwa nipoe nifarijike,


            Nyonyo, shoga zangu, mie nakomea hapa, naomba tukutane tena kwenye simulio langu la pili linalo enda kwa jina “ WATABAKI NA LABDA.” Usingoje mwaya, usingoje kuambiwa, macho hayana pazia, kama huwezi kusoma basi picha tazama.



          “Mie nipo kuugua. Nauguza mwenzenu.”             

No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...