Saturday, August 2, 2025

NIMEYATIMBA MIE KIDAWA

 



NIMEYATIMBA MIE KIDAWA


Mchezea nyuki 🐝 ung'atwa. Mwenzenu nimeona heri nianze na ako ka msemo sio kwamba ninalilia huruma za waja la, hasha! Kwa yaliyonikuta mie kidawa ninahitaji maombi na ibada sio haba niliyatimba mwenzenu. Sijui nianzie wapi kuwasimulieni maana chenye mwanzo haikosi tamati.


👇👇💕


       'Ngo no ngo,' 🤛 mlango wa Jirani yangu Dafroza na Mumewe Bwana James uligongwa karibia mara tatu.


       "Nani mwenzangu?" 🤨Dafroza alimuuliza Mgongaji. Aliyegonga kwa fujo utadhani pale ni Nyumba ya kulala wageni waliokumbwa na fumanizi. Mgongaji alivyozidi kugonga mlango wa Jirani yangu mie niliyejificha kona ya mlango wangu mtimani nilishangilia maana nilijua Bomu 💥 litaripuka muda si refu.


      "Fungu malaya mkubwa wewe,🤯 fungulia Askari 👮please!" Dafroza hakupoteza muda aliufungua mlango wa sebule yake.


      "Nd'o nini kunigongea mlango utadhani umekuja kumsaka mwizi wa kuku 🐓nyumbani kwangu?"😕 Dafroza alimuuliza Bwana Askari.


    "Nisigonge?😼 Hivi Dafroza yote yanayoendelea mitandaoni unadhani ni mazuri na yanamfurahisha mumeo?"Dafroza hakumuelewa Bwana  Askari aliyetupia mavazi ya kjani, kofia ya kijani na Buti zito lenye Rangi nyeusi. Mkononi kashika pingu zake safi.


        "Mambo yapi hayo mbona twatishana Bwana Askari" Maneno ya Dafroza yalianza kunipa furaha ya kuliona Bomu💥 likikaribia kulipuka,


           Bwana Askari akatoa simu📱 yake aina ya Samsung akaiwasha na kumuonesha Dafroza picha na video akiwa anacheza uchi  sema kibikini👙 kilimstiri.


    "Huyu ni nani kama sio wewe mwanamke? Una ndoa yako ajabu unacheza uchi mitandaoni baya zaidi unaandika unajiuza Bwanako hajui mambo ya sita kwa sita kitandani, huoni kama unamdharirisha mumeo? Jamii yote inakujadili mitandaoni." Bwana Askari aliongea kumchamba👌 Dafroza . Dafroza alipewa simu ajitazame  Gugo, FB NA IG. Macho yalimtoka pumzi zilimkata hakuamini  akionacho hakutaka moyo wake uruhusu kuuaamini ushenzi ule.


        "Jamani nini hiki?⁉️ Mimi huyu ninayeonekana nimepiga picha za utupu na kucheza nikiwa uchi kitandani??" 


      "Sasa kumbe ulijua ni nani huyo!? Sister usijizime data twende Polisi ukajieleze kwanini unapiga picha na kurekodi video za uchi kisha kuzisambaza mitandaoni." Askari alitoa pingu ili amfunge Dafroza.


       "Jamani jamani jamani! Sio mie niliyepiga picha na video hizi za uchi Kisha kuzisambaza mitandaoni. Ninajiheshimu, nina mume pia"Muda si mrefu mume wa Dafroza aliwasili, mkomoni kashikilia Bunda la Maua aina ya Rose kayanunua Maua💐🌺 hayo kama zawadi ya mkewe Mpenzi Dafroza .


      "Nini kinaendelea!? James mume wa Jirani yangu Dafroza aliuliza kwa mshangao, hakutegemea kama atamkuta mkewe kasimama na Bana Askari pale mlangoni kwake.


         "Basi mie Kidawa kusikia sauti ya Bwana James mumewe Dafroza nikatoka  konani na kuropoka " Mkeo huyo anapiga picha na kurekodi video za utupu kisha kwa upuuzi wake anazirusha mitandaoni kama sifa anaandika  NATAFUTA MABWANA MUME WANGU HANITOSHI. Eeeh! Aibu naona mimi binti wa Kizaramo." Niliropokwa kwa nguvu zangu zote ili lengo langu litimie nianze kumfaidi James mume wa Jirani yangu Dafroza Kwa jinsi nilivyomwonea gere Dafroza hapana jamani ninaweza kujinyonga bila sababu.


       "Picha na video za uchi!!?🤭🥺" James alipigwa na butwaa akashangaa 


        "Bana Askari embu muonesha shemeji picha za uchi na video alizopiga Dafroza na kuzisambaza mitandaoni kutafuta mabwana"Niliongea kwa kebehi na kubetua mdomo kwa dharau. Askari bila aibu akamuonesha mume wa Dafroza zile picha na video, 


       "Dafroza Nini hiki!" Ni wewe huyu au naota ndoto za mchana" Mumewe  Dafroza alikuwa wa moto kama tanuri🔥 hasira ziliiva juu ya shingo yake.


        "Mume wangu kusema kweli hata mie sielewi kinachoendelea labda huu ni mtego wa kutuharibia ndoa yetu tamu yenye mafanikio" Dafroza alijitetea


        "Nyamaza mpuuzi mmoja wewe." James alimkaripia Dafroza aliyeanza kuingiwa na tetemo akiogopa balaa litakalofuatia, wakati huo mie mtimani naimba nyimbo za tarabu na kupiga hesabu juu ya masaa ambayo nilimkadiria lazima Dafroza ataondoka kwa mumewe ili mie nichomeke gia


     "Yaani unaamua kujidharilisha mitandaoni kupost picha na video chafu ambazo sio wazee tu bali hata vijana na watoto Duniani kwote watakuzomea. Unanidharilisha Dafroza."James Alimkaripia na kumkolomea Dafroza.


        "James Mume wangu......" Hakuweza kuimaliza kauli yake


       "Ondoka mara Moja nyumbani hapa,  Nyau🐈 mkubwa wewe." Waooo! Moyoni nilianza kujihesabia ushindi na mafanikio ya mipango yangu michafu niliyompangia Dafroza. Hakika nilijiona nina bahati ya kuokota embe dodo katikati ya Mayai ya kuku.

 

    "Ondoka tafadhali kama ni suala la talaka utaisubiria  na nitaileta nyumbani kwenu." Jamesi alifoka kwa  hasira.


    "Tafadhali James. Dafroza alijitetea.


      "Ni kitu gani ambacho unakikosa hapa nyumbani kwangu mwanamke? Kama ni suala l kula mbona unakula vizuri, Kila wiki ninajitahidi kukununulia mavazi mapya, unakaa ndani ya mjumba wenye fulu kiyoyozi. Ajabu ya kwenda kujinadi mitandaoni ili upate Nini haswa?"James alifura kwa hasira👿 Wala hakutaka  kumpna Dafroza nafasi ya kujitetea.


Kwa hasira Dafroza alinivamia pale niliposimama akataka kuniponda kama kisamvu ndani ya kinu. Maana alikua mie nd'o mharibifu wa ndoa yake sababu nilijipendekeza kuchomga maneno.


      "Mshenzi mkubwa wewe shetani 👹 mharibifu wa ndoa za watu" Dafroza alinikemea akataka kunivaa ili tuzichape ngumi na makonde mazito lakini alichelewa Askari wangu alitumia nguvu zake zote kuachanisha ule ugomvi usio na uwanja au refali.


       "James mimi ninaondoka lakini nakwambia usije ukajuta kama utampenda Kidawa jirani mnafiki na mpumbavu kupita maelezo.


        "Unikome Babu👌."Nilimjibu Dafroza aliyeanza kuondoka akikimbia kushuka ngazi za ile Horofa tuliyopanga. James alihitaji kuingia ndani akankabidhi yale Maua aliyonunua  ajiri ya Dafroza . Waoo! Mtimani nilifurahia nilihisi sasa mambo yangu yamejipata, mpango wangu haujadunda. James akazama sebuleni kwake.

     

            "Safi sana, kazi tuliyopanga imeenda poa." Nilimwambia Bwana Askari kisha nikazama ndani ya mifuko wangu wa sketi nikachomoa noti kumi za shilingi elf kumi kumi nikamkabidhi yule Bwana Askari.


         "Ukihitaji msaada wangu tena Niite nami nitaitika." Askari alikenua  meno baada ya kutokea kitita, akateremka ngazi za Horofa apate kuondoka.


       "Duh! Hata Asante hauna Askari wewe"😚 Nilimtania kwa sauti yangu iliyojaa mahaba😘.


        "Sorry madame. Asante na ninashukuru.🙏


          "Haya nakutaka kazi njema," Mie nikaingia ndani ili nianze kupanga mipango ya haraka nimpate James mwanaume ninayemtamani balaa! Sipati usingizi juu yake, siamki kitandani vizuri juu yake nipo taabani ninamuota yeye tu..


         Mie huyo nikaingia bafuni kuosha mwili wangu mwororo mzuri kama Malaika ukitegemea mwenyezi Mungu amenipendelea urefu wa twiga si mwembamba si mnene nipo wastani siku zote. Guu la Bia🍺 Paja kama mti wa ubuyu mtoto namiliki kiuno cha nyigu, kitovu cha yule msanii wa Bongo fleva aitwaye Yamm, wowowo  kwangu kama sosholist aitwake Nicole Jolly Baby, Titi za Wema Sepetu yule Miss Tanzania, Sina kope za bandia au kucha feki. Mie Dimpozi nimemzidii Ommy Dimpozi Nywele zangu ndefu kama mtoto wa kisomali. Jicho kama nimetafuna Kungu, weeeuweee! Bado sijakwambia ninayo sauti ya kumtoa Nyoka pangoni.


          Kwisha kubafu mtoto nikajiketisha pale dressing table hapo lazima nijipake na kujipakua  marashi na Manukato, hapo lazima nijitafakarishe aina ya Lipstick inayoendana na gauni langu refu la rangi nyekundu ile ragi ya Valentine. Mtoto nikapendeza nikng'ara kama lulu


      "Nock nock nock!"Mtoto nikamgongea James lango la sebule yake


        "Karibu, pita mlango upo wazi"James Aliniruhusu kuingia nilipoingia sebuleni nikaiambaukiza ile Sebule harufu nzuri ya malashi na manukato yangu. Kwa mwendo wa Nyau yaani Cat walk nikajiburuza pale sakafuni  kumsogelea James Mume wa Dafroza Jirani niliyemtimua baada ya kula njama chafu.


      "Unafanya Nini James!? Ingawa nilimKuta anashuhulika mie sikukosa maneno ya uchokozi,


      "Dah! Kila nikatafakari naona kama mambo yashaharibika tayari," Akageuza  ILE KOMPYUTA YAKE AINA YA LAPTOP  akafanya kunionesha ile picha niliyoituma mitandaoni kumchafua Dafroza.


       "Kivipi Bana James." Nilimuuliza nikijifanya ninampetipeti mgongoni.


      "Leo Bosi wangu alipanga kuja kun'tembelea nyumbani ili anipe taarifa za   kupandishwa cheo kwa shart Moja tu awepo mke wangu nyumbani apate kufurahia . Nipo njia panda, sielewi nifanye Nini Mimi." James alionesha sura ya masikitiko,


     "Mbona ilo sio tatizo Bana James, Duniani Kuna wanawake wengi na unaweza kumtafuta mmoja wapo haraka ili uweke mambo sawa." Nilimshauri.


       "Kidawa ushauri wako ni mtamu kama asali 🍯lakini nipo njia panda sielewi nitampata wapi mwanamke ambaye atakubali kuigiza kama mke wangu mbele ya Bosi ili mie nipandishwe cheo," James alionesha sura ya masikitiko.


      "Yote haya Dafroza ndie aliyesababisha, bila yeye leo hii Bosi angekuja nakwambia mshahara💰🏧 wangu ungeliongezeka kutoka millioni mbili kwenda milliomi tatu. Duh! Kidawa mie niliposikia habari za mshahara mkubwa kama ule anaopewa James macho yalinitoka pima,👀 mtimani nilijua hapo nimepata nisiache mbachao kwa msala upitao.


       "Kwanini usinichukue mie niigize kama mkeo mbele ya Bosi wako" Mate ya tamaa🤤 yalinitoka mie Kidawa.


     "Utaezana!?"


      "Ulidhani mie hoehae?" Nikajifanya kucheka nikiwa nimeinamisha kichwa changu chini ya Meza ile yenye Laptop mikono yangu imeshikilia ile Meza. Kwa kifupi nilijibinua kihasara hasara ili James apagawe na matiti yangu makubwa.


    "Uhakika!" Alihitaji  ukweli.


    "Niviishe hiyo Pete ya Dafroza uone maajabu." Ile Pete yenye kito cha Almasi ilikua juu ya Meza bila kupepesa Macho James alinivisha.  Waooo! Kimoyo moyo nilichekelea maana nillijua tayari nishaibuka na Jocker. Bingo takatifu. Basi hatukupoteza muda na maandalizi ya kumpokea Bosi wa Bwana James yalipamba moto.


         "Saa kumi na mbili jioni  Gari ya Bosi wa Bwana James iliwasili James alitoka kumpokea na kumkaribisha ndani. Bosi alikua amevalia mavazi ya kiarabu. Kanzu mpya nzuri ya bei gharama, kiremba kichwani kilichozungushwa na mtandio wenye rangi nyeusi, saa mkononi mpya yenye rangi ya Dhahabu. Chini miguuni alivalia Sendo zilizotegenezwa Paris Ufaransa. Ndani alikaribishwa.


        "Karibu Bosi wangu Bwana Araba huyu ni mke wangu mpenzi Mwite Kidawa." James alinitambulisha kwa yule mwarabu wa kiarabu


      "Waoo! James  una mwanamke mrembo na mzuri" Bosi Araba alinipatia mkono wa salamu kwa mapozi na madaha.


      "Salama Bibi," Alinisalimia akabusu kiganja changu kisha akaendelea kutelezesha ulimi 🤪wake kutoka kwenye kiganja cha mkono wangu kuelekea mabegani kwangu. Jamani nilianza kuogopa na aibu ilinifunika


    "Salama tu sijui wewe" Niliitikia Salamu yake nikiwa na haya usoni lakini yeye bila haya aliendelea kunilamba 😜 mkono wangu.


    "No! No! No! Ungehitaji kikombe cha Kahawa ☕au chai?"🍵 Nilijilazimisha kutoka mkononi mwake nikafanya kuongeza maneno ya ukarimu kwa mgeni


   "La! Hapana mimi sikufuata kikombe cha Kahawa au chai, nimefuata kumuona mke mzuri wa rafiki yangu. Kama utamaduni wetu ulivyo mke wa rafiki yangu ni mke wangu pia. Hivyo basi Kila neno au Kila tendo nitakalo amuru ufanye lazima kutii. Toba!" Nilishtuka mie kwa yale masharti mapya.


      "Ndio, Kidawa mpenzi Kila neno atakalo kuambia fanya wewe usiogope kufanya." James alimuunga mkono Bosi wake, wawili wale wakaelekea Sofani kuketi.


        "Bwana James tafadhali washa Muziki 🎼💽weka ule wimbo mtamu wa Shakira Hips Don't lie " Bosi Araba alimuamuru James ambaye mara moja alitii.


    "Shem anza kucheza tena ucheze kama Shakira anavyoyakata mauno." Araba aliniamuru.


        "Mie!!!?"🤔 Nilijikuta nashangaa.


         "Yes wewe Daring ulidhani nani mwingine? Embu mfurahishe Bosi wangu ili mumeo nipandishwe cheo na nipate nyongeza ya mshahara mnono," James Aliongea kwa upole. Lo! Nilikua njia mpanda, Kweli mie na urembo wangu huu nianze kukata mauno kama ya Shakira mbele ya Bosi wa Bwana James? Tisa kumi sikufurahishwa nilianza kuyakata mauno wakinitazama nikiwa nimegubikwa aibu.


     "Mbona una mwili mzito hivyo? Embu kazana kukata uregee kama bamia" bila aibu Araba aliniambia nilishindwa cha kufanya zaidi ya kuangalia chini nikitazmwa na wanaume wale wawili


        "Geuka nyuma, geuka nilione hilo kalio la Nicole Jory Baby linavyonesa nesa" Uwii!  Yule mwarabu aliniitia kinyaa. Sikumjibu Wala sikugeuka zaidi ya kutazama chini. Araba akaichukua simu yake akawa ananirekodi jinsi ninavyocgeza kwa aibu, jasho lilianza kunitoka, nilihisi fedhea.

 


     "Geuka, geuka please," Alinibembeleza lakini wapi! Niliona aibu kucheza mbele ya yule ambaye baadae nitamwita Shemeji mtarajiwa. Akamwamuru James austopishe Muzik kisha akanifata pale niliposimama.


    "Tamaduni za waarabu sio mbaya ndugu wa damu mmoja kushea mapenzi, vivyo hivyo kwa marafiki. Kwahiyo mimi nataka nilale na wewe tufanye mapenzi tulizike.


      Uwii!! Nilihisi labda sijasikia vizuri yaani mie mrembo Kidawa naanzaje kugonoka na huyu mgeni ambaye Leo nimetambulishwa kama Bosi wa Bwana James. Ewe Mola nisamehe mie Kidawa nitauficha wapi uso wangu iwapo nitashiriki ngono na huyu Bwana nisiyemjua, nitauficha wapi uso wangu  mbele ya James, atanielewa vipi?


   Sijawai kuusikia utamaduni kama huo bila aibu Bosi kuniomba tufanye mapenzi mbele ya mtu aliyeniomba nijifanye kuigiza uhalisia wa Maisha ya ndoa yake nikijiaminisha kuwa sasa amekua wangu na penzi nono nitampatia.


    "Hapana, hapana jamani siwezi." Niliongea kwa kujitetea maana nilikwisha ona maji yanakaribia kuzidi unga. Lo! Wacha nitapetape.


     "Kubali mke wangu, kubali kufanya ngono na Bosi wangu. Je, hautaki mumeo nipandishwe cheo!? James alipigilia msumari ile kauri yake. Pozi lote likanipwerepweta, chozi nikabubujika maana nilikwisha ona ninavyofedheheka.


    "No, Hapana. Nisikilize Bwana Araba mimi sio mke halali wa Bwana James, kama ndivyo haya mnayofanya na Dafroza mimi siwezi hata kidogo." Nikamgeukia James nikamwambia.


  "Nisamehe Bwana James kama una amini kuwa mkeo anajiuza mitandaoni ninaomba ulifute hilo wazo. Hakuna ukweli juu ya suala hilo bali ni hila na tamaa zangu binafsi."


        Baada ya kukiri na kuishiwa pawa nilikuja kushituka kusikia sauti ikitokeza nyuma ya mgongo wangu. Alikua ni Dafroza aliyeingia pale sebuleni akitokea mlango wa nyuma wa ile nyumba.


      "Waooo! Safi sana, Kila neno ulilonena na kukiri siku ya Leo nimerekodi ndani ya simu yangu." Dafroza alinishitua.


   

       "Video na picha ukikata mauno tayari zimerekodiwa." James alimuunga mkono mkewe.


      "Jamani Nini mbona sielewi kinachoendelea?" Nilijikuta nashangaa mimi mwenyewe.


     "Utaelewa tu embu sikiliza." Dafroza akaanza kusimulia.


      "Wiki iliyopita nilikua nikipitapita mitandaoni, nilishtuka kuiona Account feki ndani ya FB na IG. Picha zangu na Video zilinadiwa  nikijitangaza kuwa nauza mwili. Nilipoziona hizo picha na maneno yaliyoandikwa binafsi nilishtuka nikamwita mume wangu James na kumweleza  kuhusu ile Account fake, James alishangaa pia lakini kwa sababu yeye ni mwanaume mwenye akili na busara aliniambia tuwe na subira tuone Nini matokeo yake.


       "Uzuri matokeo yametoka na wewe umekiri kuwa ni muhusika wa matukio hayo, lengo lako lilikua ni kuniibia mume wangu mpenzi. Sasa nasema hivi picha zako na video ukiwa unacheza Muziki ninazo. Maneno yote uliyonena na uliyokiri kujidharilisha mitandaoni nimekwisha rekodi hatua inayofuata ni kusambaza mitandaoni ili watu wajue kuwa wewe ni mnafiki, mwizi, shetani"


    "Tafadhali ninaomba usinifaniye hivyo Dafroza, ninaomba unisamehe nmekosea, ninaogopa naweza kula aibu ya milele." Nilijitetea woga wa kuaibika mitandaoni ulinienyesha, majuto mjukuu nilianza kujuta.


   'Teh teh teh 🤣.Aloo!👌Unaogopa kuaibika  mitandaoni na ulivyoniaibisha mimi mitandaoni unadhani nilijisikiaje!? Mwanamke mbovu wewe yaani ukaona haitoshi hadi uniletee Polisi 🤣. Sasa sikia ninakupa amri Moja haraka futa yale mapicha na mavideo yanayosambaa mitandaoni tena uhame hapa nyumbani, uhame hii Horofa, Nyau wewe!" Dafroza aliongea kwa hasira, akaniachia mtihani mzito.

        


     "Nihame niende wapi? Sina pesa za kushuhulikia makazi mapya, Pesa ya Kodi sembuse ya kubebea mizigo yangu." Nilikua njia panda kwa adhabu niliyopewa.


     "Babu we! Hilo lako halituhusu. Eti huna pesa za kushuhulikia Nini sijui! Kwani pesa za kunidharilisha mitandaoni ulizipata wapi? Tafadhali, hama ndani ya hili jengo kama unataka mambo yawe mengi basi subiri. Subiri nikudhalirishe mitandaoni." Dafroza hakunitania.


     "Any way, nisikilize Kidawa."  Niligeuka na kusikiliza sauti ya Mwarabu. Safari hii aliondoa kile kiremba chake kichwani nikamuona sura yake ilivyo jamali.


     "Kwa sababu hauna pahali pa kwenda nafikiri itakua vema twende tukaishi wote nyumbani kwangu."


      Mola we!  Sikupendezwa na maneno ya Mwarabu. Kwanza sikumpenda pili hakuwa chaguo langu tatu simjui hanijui.


     "Upo tayari Mpenzi." Alinishika mashavu yangu na kunifuta chozi lililokuwa likinibubujika. Lo! Maskini nilikosa la kujibu mie ukitegemea n'shapewa amri ya kuhama pale ninapoishi na jirani yangu Dafroza, Jirani niliyetamani kumpokonya tonge mdomoni Sasa nimeyatimba hakika mume wa mtu sumu.


~~~~~~~~


TCHAO 💖 


~~~~~~~~


No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...