Saturday, November 30, 2024

MY STEP MOTHER

 


BABA NA MAMA👨‍👨‍👦 WALIPOAGA DUNIA⚰️ MAMA WA KAMBO👩‍👧 ALlJITOLEA KUNILEA 🧑‍🍼NILIPOFIKISHA UMRI WA MIAKA 18🎉🎊🎂NILIMFUKUZA NYUMBANI🏘️ KAMA UMBWA KOKO🐕🦴.

         Mama yangu alipokua hai alinidekeza na mie nilideka nikapendeza na kudeka kama Yai🐣 lakini Yai nalo lina mwanzo na mwisho, mwisho mwema ni pale Yai linapoleta kilicho bora zaidi na mwisho mbaya ni kuoza, kutoa shombo au kuitwa Yai viza. Ndo' hivyo basi mama yangu Agness akaitwa mbele ya Mola🌨️ nikalia mie na kuomboleza.😿
 
      Nilipokua na umri wa miaka kumi na moja, bado kinda kindaki mie Editha nilimwona Baba akimleta mwanamke nyumbani🧍‍♀️kisha akamtambulisha kwangu akisema Judith atakua ni Mama yangu. Sikumfurahia Judith, nilichukia sana, sikumpenda wala sikupenda aishi nyumbani kwetu. Nilimwona Judith kama shetani, 👹 mwanamke. Bora kuishi pekee yangu kuliko kuishi nikimtazama step Mom Judith.

      Ingawaje Step mother alinipenda pia alionesha darili za kunikubali lakini mie moyo wangu haukutaka hata kumsikia. Kila niliporudi Shule nilijifungia chumbani kwangu (Tena niliubana mlango Kwa kufuli 🔐🗝️) nikalia humo na kumkumbuka Mama yangu Agness, mama aliyetwaliwa na Mola.🪦

     Baba yangu alinisihi nimpende Judith kama Mama yangu mlezi 👨‍🍼lakini hakuna nguvu iliyoniigia kichwani kwangu kukubaliana na kauri za Baba. Lakini siku Moja, siku ambayo kila kitu kilibadilika hadi upendo wangu ulihamia Kwa Mama wa kambo ni siku ambayo  nilikuja kushituka mara baada ya kuota ndoto mbaya (Nightmare) kuhusu Mama yangu Agness.

       Mama alinitokea Ndotoni kama Malkia wa Ibilisi shetani (Devil's👿 Queen 👑) Mama alionekana amevalia vazi refu la rangi nyeusi tiii ⬛Tena kuukuu linalotisha na kuogopesha. Kichwani alivalia Crown ya Malkia wa shetani, 🤴mdomoni alionekana ana meno marefu🦷 kama pembe za ndovu🐘 na ndimi👅 yake ilikua ikiwaka moto 🔥na kutema damu nzito 🩸yenye sumu.

        Kucha💅 za mama yangu zilikua ndefu miguuni na mikononi, 🦵🖐️mkono wa mashoto aliushika upanga 🗡️mrefu uwakao moto, macho yake yalitisha Kwa wekundu wa pilipili zaidi ya hilo masikio yake yalifanana na masikio ya punda 🐴 juu ya kichwa alitoa pembe za mbuzi 🐐. Niliogopa sana.

      "Nimekuja kukuchukua."Mama mzazi aliniambia ndotoni.

      "No, no, no, Mama sipo tayari kuja kuishi huko kwenye moto wa Volcano 🌋💥" Nilimpiga Mama mzazi.

     "Nataka kuishi na wewe mwanangu Bena kubali tafadhali."

      "Hapana Mama, hapana. Ninahitaji kuishi na Baba." Nilimpiga Mama yangu kwenye ndoto💭😴 lakini kupinga kwangu hakukumsaidia nikamwona akipaa Kwa mbawa ndefu zinazotisha, akanifukuzia Hadi pale nilipoganda kama sumaku, akanikaba shingo yangu Kwa mikono yake iwakayo moto Kisha akauyanyua upanga wake wenye makali kuwili haraka bila kupoteza dakika alihitaji kuikata shingo yangu. Hapo ndipo nikashituka kutoka usingizini 😴💤na kuanza kupiga kelele zilizomshitua Mama yangu wa kambo aliyekua Jikoni akikosha vyombo 🧺🏺🍲🫖

       Judithi Mama yangu aliposikia sauti ya kulia 😰🤧kwangu akaacha kukosha vyombo  na kukimbilia chumbani kwangu alikonikuta ninalia Kwa sauti kuu kama vile nimepagawa.wakati huo Dady alikua bado hajarejea kutoka mishe zake.👷🔨 Mama akaufungua mlango niliouwacha w>azi siku ile, akaingia na kuketi kitandani Kisha akanishika mikono yangu taratibu Kwa upendo wa dhati.🌹

      "You are okay now dear.....it's ok, you are safe. Please stay safe."Alinifariji.

      "Hapana Mama ninaogopa.😨" Akachukua upinde wa kanga yake aliyojifunga kisha akanifuta chozi langu lililokua likinitoka Kwa kilio Cha kwikwi.😿

     "Upo salama mwanangu, usiogope, mikono salama." Ni kama vile Mama alilijua tatizo langu akanikumbatia🫂 na Mimi nikamkumbata kwa nguvu sana maana Kwa woga ule nilihitaji faraja isiyochuja

         "Ndoto Mama, ndoto mbaya. Sijawahi mwita Judithi jina la Mama lakini siku ile Nilimwita na pia nikauona upendo wake, wema, uzuri na faraja tele. Kwa hakika moyo wangu ulisikitika sana, kwanini nilikosa upendo wa Mama wa kambo. Siku ile nililala pamoja na Judithi Step mother, Nilimkumbatia Kwa nguvu zote na woga wote uliinikatika.

       Ikawa hivyo basi ile ndoto nzito niliyoiota ikageuka upendo mzito ndani ya familia yetu Judithi akageukia na kuwa Mama yangu, faraja yangu, utulivu na amani yangu. Nilianza kumpenda pendo la kupendeka. Tukicheka wote, tukitaniana na kucheza kama watoto. Uzuri Mamangu wa kambo alinithamini, alinijali kama mwanaye wa kunizaa pia alinihesabia kama mwanae mpenzi.

         Tulipoenda Beach ⛱️ mie, Baba na Judithi pia aliambatana nasi. Tukayachezea maji Kwa furaha 🚣🏄‍♀️🤽‍♂️ Tulipoingia Mall 🏬 au Supermarket🛒 tulinunua kila kitu ambacho niliwaomba waninunilie. Shopping🎁🏪 ndo' usiseme Step mother alinipendelea nichague kila kitu nilichopendelea kuchachambua achilia mbali Hotel na Restaurant 🏨🛋️ nilikula hadi nikaanza kuurejesha ule mwili wangu ilioanza kudhoofu kutokana na msongo wa mawazo juu ya kifo cha mama yangu Agness.

         "Lakini Jamani Dunia ni Mali ya Mungu wanadamu tumepewa kuketi Kwa muda wa siku, saa🕦 na nyakati. Baba yangu akaja kuugua Home Kali 😷🥵 ya Maralia🦟 tulipompeleka Hospitali 👨‍⚕️🏥 dawa 💊 alizopewa anywe zilimkataa na kumsaliti, hatimaye baba mpenzi akaanza kukiona kiza na Malaika🧚 mnyofoa roho za waja wa Mola akaja kuibeba roho ya baba yangu na baba yangu akapumzika pahali Pepa peponi. Sie wawili tulilia na kuomboleza.😭😿

     :::::::::::::::::::::::::☠️::::::::✝️::::::::

Alipokufa⚰️ Baba yangu ndugu zangu wote upande wa Baba walimtaka Step mother afungashe kila kilicho chake na aondoke haraka iwezekanavyo pale nyumbani, 🏘️ pamoja na Hilo Mimi pia sikupendelewa ndani ya koo au familia zao, nilionekana kama mkosi, kizingiti na zigo lisilobebeka. Inakuaje Mama atoweke na baba atoweke tena ndani ya muda mfupi wa maisha⁉️  Hilo kwa ndugu na ukoo lilikua ni fumbo zito.

        Ndugu wa pande zote yaani kwa marehemu baba na kwa marehemu Mama walikataa kunipokea kwa hiyo walinitaka nichukukuliwe na kupelekwa nyumba za kuelekea watoto yatima (Orphanage) Hilo nalo sikulipenda tena nililipinga kwa nguvu ya mikono yangu yote miwili ingawaje bado nalikua ni kinda wa kuyajua mema na mabaya.

       Judith akasimama kidete naye akanitetea akisema: 'Yupo tayari kuishi na Mimi ndani ya nyumba aliyotuwachia marehemu Baba.' Ndugu walimpinga na kumzodoa wakimkashifu Kwa kumwambia hataki kurejea Kijijini kwao kulikojaa umasikini dhiki na njaa ya maisha, walihisi Judithi analeta visingizio lakini uzuri wa Judithi alinitetea nisiende kulelewa nyumba za watoto yatima.

      Maisha mapya yalianza mie Step daughter Editha na Step mother Judith tulianza kuishi katikati ya upendo na mapenzi makuu. Kila niliporejea kutoka Shule nilikuta chakula kimeshaandaliwa, nguo zangu safi tayari zimeshafuliwa na kupigwa pasi, pea  za socks na viatu🧦👞🥿 vilinukia marashi na manukato ya Pemba na Unguja🏝️🗾 kitanda changu haswa Bed mattress zilibadilishwa. Makusheni mapya na Pillow safi. Kila kilichokuwa kipya na kizuri nalifanyiwa basi mie nikapendeza na kunawiri afya yangu. Mama wa kambo akanipenda na kunilea kwa furaha.


BAADA YA KIFIKISHA UMRI WA MIAKA KUMI NA MINANE (18).

     Baada ya kufikisha umri wa Miaka kumi na minane nilihitimu kidato cha sita kisha nika aply kwenda kuchukulua Degree yangu Chuo Cha Dar es saalam kampas ya Mlimani. Hapo ndipo nilipofikiria Sasa napaswa kuanza kumfanyi visa, Mikasa, vitimbi na vibweka Step mother hadi aondoke pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi niliyoachiwa na marehemu Baba yangu. Lakini nikimtimua ataenda wapi!? Nilijua mie jinsi ya kumkimbiza kama kuku🐔🐓.

       Siku ya Birthday 🎂 🎊 yangu, siku njema iliyoonekana asubuhi, Judith mama yangu aliniandalia keki🍰🧁aliyotumia masaa kadhaa kuandaa Kwa bei gharama na kwa nguvu zake zote, kwa hakika mama alinijali sana, alinipenda na kunithamini, alinichukulia kama mwanaye wa kunizaa na sio Step daughter. Alinisikiliza iwe utani, ujinga au masikhara Mama hakunibagua tena alinivumilia.

       "Happy birthday 🎈 🎂 Editha, Happy birthday mwanangu. Mama Alinipongeza kutimiza miaka kumi na nane.🎉🎊

       "Thanks so much Mom, Asante." ninashukuru. Nilimwitikia mama japo sio Kwa furaha Wala Kwa tabasamu😡 Kisha nikaizima mishumaa🕯️🎂ya kumi na nane zangu, tukaikata keki 🍰na kulishana Kwa furaha. Baada ya kukata keki Judith Mamangu wa kambo akanipatia Boks la zawadi🎁💐 Waoo! Nilipolifungua lile Boks nikakutana na gauni zuri la bei gharama yeye binafsi aliniambia materia yake yamenunuliwa Arabuni na mshono umeshonwa U.S.A..We! Jamani kupendwa raha😚😽.

    "Ninakupenda sana my daughter.❤️"Mama aliniambia.
 
    "Ninakupenda sana Ma💜💗. Lakini ninaomba kuanzia muda muda huu ubebe kila kilicho chako ndani ya nyumba yangu ujiandae kuondoka. Niliongea usoni nimejaa kisirani,👺 sikumjali tena Mama yangu wa kambo.

    "Niondoke!?🤨🙄"Aliniuliza Kwa mshangao
    
    "Ndio, uondoke nimechoka kuishi na wewe pahali hapa, ninaomba ubebe kila kilicho muhimu kwako, wakati wa kuishi ndani ya nyumba hii umeisha." Bado Mama alishangaa, mdomo wazi😲.

    "Mwanangu kwanini niondoke na niondoke niende wapi!? Masikini Mama alikua njia panda.

     "Utajiju👌mwenyewe, popote unapotaka kwenda wewe nenda tu. Kusanya kila kitu chako  ndani ya nyumba yangu kisha uondoke."Niliongea usoni nimejaa kisirani sikumjali tena Mama yangu wa kambo akaanza kulidondosha chozi.😿

       "Mwanangu Mimi nilijua fika kuwa nitakuja kuishi pamoja na wewe milele, nilijua hautakuja kinifikuza sasa kwanini uniambie niondoke? Nitaenda wapi na nani atanipokea." Mama alilia kwa uchungu.

      "Mama tafadhali usinipotezee muda ingia chumbani na ubebe kila kilicho chako, Uber ipo nje inakusubiria" Nilimfokea nikaongea kama mtu serous yaani sikumtania. Kwa machozi na kilio cha Kwikwi😰😥 Mamangu Aliingia chumbani kwake akakusanya kila kilicho chake akatoka nacho Safari ya kuondoka iliwadia.

     "Ndani ya Uber Mama aliniuliza: "Sasa mwanangu Bena wapi nitaelekea Mimi? Nilijua tutapendana milele Hadi kifo kitutenganishe, tafadhali urudishe moyo wako nyuma unifikirie na pia unikumbuke ninakupenda Daring."
    
      "Makini Judithi!! Mke na Mume ndio upendana hadi kifo kiwatenge. Sio Mimi na wewe Step mother."Nilimjibu jeuri ingawaje nilijua majibu yangu hayafai hata kidogo Kwa mtu muhimu kama yule aliyekaa kimya na kulia sana pembeni ya dirisha la Gari.🪟

     "Tulifika karibu na eneo la Mwenge🔦 karibu karibu na Chuo kikuu cha Dar es saalam (Mlimani.) Mbele ya Jumba lenye Horofa tatu tulifunguliwa geti la mlango mkuu kisha tukaingia hadi ndani ya lile jengo linalong'ara kama Dhahabu hapo nikaisimamisha Uber yangu kisha nikamwambia Step mother aliyeketi nyuma chozi likimbubujika, chozi la thamani.

       "Nisikilize Mama" Nilianza kuongea. Naye alinisikiliza.

      "Nilipozaliwa Baba aliwekeza Shea 💰💱kwenye kampuni fulani inayolipa na inayofanya biashara Kwa nguvu na kwa faida kubwa"Mama alinisikiliza.👂

     "Baba aliandika Shea zile nilipaswa kupewa iwapo ningelifikisha umri wa Miaka kumi na nane, uzuri ndani ya Account yangu ya Benki bado ningali nina Mamilioni ya Shilingi."💵💹🤑💲

       "Ninakupenda na pia ninakuthamini kama unavyonipenda na kunithamini. Je, yawezekana vipi kumtenga au kumchukia mtu mwema kama wewe mama mpenzi?" Mama alianza kutabasamu.

     "Jiulize kwanini nimekuleta ndani ya mji wa Mwenge🗽🔦  kwa sababu sihitaji kukutenga uwe mbali na mimi, kukutupa sembuse  kukufukuza."Niliendelea kuongea.

     "Jumba🏚️ unaliona mbele yako ni Jumba la Horofa tatu, mama nimekujengea wewe mpenzi, ninahitaji kuishi na wewe eneo la karibu na Chuo. Tambua nimefauru kidato cha sita na nimechaguliwa  kusoma  masomo ya Sheria⚖️ Chuo kikuu cha Dar es saalam Kampas ya Mlimani. Mama sitaraji na sintapenda kuwa mbali na wewe."

      "Ma. Tambua sijakutenga na pia sijakufukuza bali hii ni Sapraizment kwako, nimekujengea mjumba Mamangu ukae pamoja na Mimi kila siku ukinipikia matamu na kunipakulia  manono na Mahanjumanti."🍜🍝🍨🍱 Niliongea na kumkabidhi Mama yangu Hati ya lile Jumba, 📃Hati iliyokua na jina lake.
  
         "Ma. Kama moyo wako wako hautaridhia kuishi na Mimi hapa Mwenge, ninakupa nafasi urejee kuishi kwenye lile Jumba alilotuachia Daring Baba" Niliongea Mamangu aliyafuta machozi yake naye akaongea:

     "Asante mwanangu, Asante kwa upendo na mapenzi bora. Nilijua kuwa Sina changu, Sina maana na Sina thamani lakini kumbe waniona mie ni wa maana. Ndigwako  my daughter (Mimi ni wako) Mimi ni wa thamani kwako. Asante my daughter ninahitaji kuishi na wewe Daring!🥰"

Ma. Alilia machozi ya furaha kisha nikamsogelea na kumkumbatia Kwa nguvu zote🫂😘. Bila kupoteza muda nikamkabidhi funguo zote za ile nyumba, tukateremka Garini na kuelekea kuukata utepe 🎀 wa nyumba yetu mpya. 



******💋😘....👩‍👦

TCHAO 





Sina la mno kuongeza naomba niishie hapo.👋👋.
      

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...