Thursday, November 21, 2024

GOLDEN DIGGER HUSBAND




 INTO LADIES ROOM


(NDANI YA CHOO CHA KIKE)

      Niite Tunda au ukipenda refusha, Matunda🍎🤣 ninacho kisa kinachoelimisha na kufundisha wanawake na mabinti wanaokimbilia kuolewa pasina kujua mwenza (Mwanaume) uliyempenda anania mbovu, tamaa, matamanio na ubaya kwa mwenza wa kike.  Ninakubali pia ninaunga mkono pale mtu akisema mapenzi ni upofu, mapenzi ni kupendana💕 na mapenzi kukubaliana lakini yaliyomkuta Binti yangu Semi kama ningelichelewa kuyavulia nguo sijui nani angeliyaoga. 

     Semi Binti yangu kesho anaweza kutimiza miaka ishirini na mitano pia miaka mitatu ya kuachwa na Teo mwanaume aliyemdanganya kupitia kigenzo cha ndoa. kweli alimuoa lakini moyo unaficha mengi na mengi hayo ni mazito ya Dunia. 

Binti yangu alipendana sana na Boyfriend wake Mateo au kwa kifupi Teo, Hatimaye walikubaliana ndoa, harusi nzuri ndani ya Kanisa la mtakatifu Maiko, baada ya harusi mie Tunda mamaye Semi, Semi Binti yangu, Teo mkwe wangu pamoja na Sesi: best woman (Msindikizaji wa BIBI harusi) tulielekea ROYAL HANDZABE HOTEL kufurahia Sherehe. 💃🕺🎶

     Wahudhuriaji walikula, walikunywa na Muziki mwororo walicheza, macho yangu yalitua na kumuona Teo akimnong'oneza Sesi sikioni jambo fulani ambalo yamkini walipatana kwenda pahali kunena jambo wakati huo Binti yangu Semi alikua akiserebuka na kufurahia Muziki pamoja na waalikwa.💃🕺 Ghafra mkojo ulinibana pwiiii nikapata wazo la kwenda Washing room kujisaidia haja ndogo. Wakati huo Muziki uliendelea furaha na pongezi zililiminika. 

       LADIES ROOM 🚺 maandishi makubwa yalisomeka mlangoni mie Tunda nikaufungua ule mlango nikaingia kujisaidia.  Ningali bado ninatabasamu 'sasa Binti yangu mpendwa anaolewa na Bwana wa mtima wake💖.' Taa zilimulika vizuri room ikapendeza lakini ghafla macho yangu yalikua mbele ya watu wawili niwajuao tena waliniachia mshangao🙄 nilipowaona tu nilijificha kona moja ya chemba ya kuhifadhia vifaa vya usafi wa choo, moyo wangu ulienda ndu ndu ndu! Mapigo maana nilichokiona kilinistaajabisha. 

Mateo alikua amepitisha mikono yake mizito kiunoni kwa Sesi naye Sesi aliizungusha mikono yake kwenye shingo ya Teo. Walikua wakipeana ndimi💏 wakadendeka. Moyo ulinienda mapigo, pumzi zilinitoka kama vile mwanariadha Usain Bolt alivyochoka baada ya Kukimbia masafa marefu. Niliichomoa Enka yangu nikaziba mdomo pumzi zisiendelee kunitoka kwa kasi.

   'Jesu! Teo mkwe wangu anafanya nini Restroom?' Nilijiuliza.🤔

   'Teo anamsaliti mwanangu Semi kwa kupigania mabusu na Sesi rafiki wa Semi' Nilijiambia.🤭

    'Jamani kumbe Mateo mkwe wangu hajajivika ngao ya uaminifu!!'🫣 Nilishangaa na pia nilijishangaa. wakaacha kudendeka Kisha wakaongea maneno ambavyo hadi leo hii naapa kama nisingeliyafanyia juhudi zangu hakika ningelifirisika.

       "Mpenzi fanya hima umuue Tunda Bibi mama mkwe wako ili Semi aachiwe urithi wa familia na baada ya kumuua Bibi mama mkwe utauamishia utajiri wote mikononi mwako tuwe matajiri wa kutupwa" Rafiki wa Bi. Harusi aliongea.

    "Sesi ninakupenda 😘kuliko Semi kile kinyago cha mpapure. Pale ndoa hamna ninajifanya kuzuga tu, wewe nipe miezi michache jambo letu litatimia" Teo yule ninayemwita mkwe wangu aliongea.

      "Unachelewa nini Dear?😒😬 Mbona unakuwa kama mwanaume wa Dar!😡 Hauyaoni yale magari kumi ya fahari na bei ya kutupwa? Hauyaoni yale mashamba mkubwa ya mpunga kule Mbeya? Hauoni Malodge, mahotel na kumbi nyingi za starehe? Au hauoni biashara na pesa nyingi anazozimiliki mamaye Semi. Ukiisha muua Tunda mamaye Semi muue pia Semi Kisha fanya kubadilisha Majina ya urithi kwenye documentary.... Jiandikie majina yako Kisha tuanze kuyachezea mahella. " Sesi alimshauri Teo.💰💸

      "Usijari mpenzi nitafanya yote kwa ajili yako mapema ndani ya mwezi huu" Teo alimjibu Sesi. Mie mapigiti ya moyo yalinienda kasi nikiwa ningali nimefichama pembeni ya chemba ya kuhifadhi vifaa vya usafi wa choo nikawaona Sesi na Teo wakiondoka mule Restroom.

Nikakitoa kitambaa nilichokiweka kinywani ili kuzuia presha iliyonipanda, nikawaza kuondoka Ladies room maana hata mkojo uligoma kutoka baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa Teo na Sesi rafiki wa mwanangu.

      'Umdhaniaye ndiye kumbe sie' Niliwaza.🤨

      'Heri nusu Shari kuliko Shari kamili' Niliwaza tena.🙂‍↕️

      'Yakimwagika hayazoleki.' 😶‍🌫️Nilijiambia lazima niizuie tufani inayotaka kupiga chombo kiende mlama nikatembea nikiwa natetemeka.

*******

Siku iliyofuata Teo Mkwe wangu pamoja na Semi mwanangu walinisindikiza uwanja wa Ndege wa Arusha lnternational Airport kwa ajiri ya Safari ya kurejea Dar es saalam. Nilikata tiketi Lever ya juu yaani High class. Niliwaomba waniache Airport Kisha warudi makwao.

Mwanangu Semi aliniaga akisema ataelekea Ofisini kwake kukata keki🎂 ya pongezi ya kuolewa, angeliikata na rafiki zake. Teo alimwomba Semi kurejea 🏕️ nyumbani Kuna shuhuli ya kiofisi alidai angelienda kuimaliza. Niliwaaga kila mmoja alienda njia zake. 

        Lakini kumbe mie nilikua na mpango wangu, mpango wa kumuokoa Binti yangu mpenzi Semi kutoka kwenye mikono ya Tapeli anayetaka kuniua ili amdanganye mrithi wa mali zangu, Mali zangu ziandikwe kwa jina lake Mateo na sio kama Documentary mbalimbali zinavyolitaja jina la Binti yangu Semi. 

Sikuipanda Ndege niliyokodisha siku ile nilichofanya mimi ni kuichukua Uber🚗 iliyonipeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwa Binti yangu Semi pahali anapoketi yeye na Mumewe tapeli Teo. Nilifika na baada ya kufika kwenye ile nyumba nikamuona Mkwe wangu Teo akiteremka kutoka Garini ameambatana na Sesi wanapigana mabusu na kutomasana kama wanandoa.

      Nilikereka na kuudhika kuona Binti yangu anahujumiwa na Best friend wake pamoja na mumewe tapeli aliyekula njama ya kuniua ili hapo baadae mali zangu zihame kutoka kwa Binti yangu kwenda kwa mpuuzi Teo baada ya kuniua na kumuua Binti yangu. 

       Nikiwa ningali ndani ya ile Uber niliyokodisha nikaichukua simu 📳yangu ya mkononi na kumpigia Semi mwanangu aliyekuwa Ofisini akifurahia pongezi kutoka kwa watumishi na wafanyakazi wengine wa kampuni yake.

        "Hallow! Binti yangu mpendwa Naomba uje Nyumbani kwako haraka iwezekanavyo."🏃

      "Mama si wewe upo ndani ya Ndege✈️ na waelekea Dar es saalam, jambo gani limekusibu hadi uende nyumbani kwangu?" Binti yangu aliuliza.

      "Nimepata homa ya ghafra Binti 🤒💊💉 yangu imenibidi kuongea na uongozi wa Ndege kwamba leo sintasafiri, nimehairisha."
 
      "Sawa mama basi niruhusu muda huu niutumie🎂🍰 pamoja na marafiki Kisha baada ya hapo nitakuwepo nyumbani."

     "Hapana mwanangu mimi ni mama yako Naomba unijali Nina tatizo tafadhali fanya hima."

    "Sawa mama nipe dakikachache nitakuwepo hapo." Semi aliliheshimu wazo langu. Ndani ya dakika kumi na tano aliisimamisha gari🚘 yake pembeni ya ile Uber niliyokodisha Karibu na nyumba yake.

*********

      "Samahani Binti yangu🙏" Nilianza kumueleza Semi.

     "Kuna jambo nilitamani kukueleza usiku wa Jana kwenye ukumbi wa🏰 sherehe  lakini niliona haitapendeza, basi leo nataka nikueleze yote." Nilimwambia, nikaanza kumpasha. 

     "Teo sio mume wa kumuamini, Teo ni muuaji aliyekula njama ya kutaka kuniua ili mali zote nilizoziandika kwa jina lako ziwe zake akiisha kukusonga na kukushawishi." Semi hakunielewa.

     "Najua haunielewi lakini nakuambia Binti yangu muda huu mumeo Teo na rafiki yako Sesi wapo sebuleni wanafanya mapenzi. Amini usiamini Jana niliwafumania wakiwa chooni wakipigana mabusu na kupanga mipango ya kutuua na kutuangamiza ili mali zetu ziwe zao.

      "Mama bado sikuelewi."Binti yangu hakunielewa kwa maneno 🔊ilibidi nimueleweshe kwa vitendo.📚📖💥

    "Twende ndani na tuwafumanie." Tulitoka ndani ya geti kuu la kuingilia nyumba ya Binti yangu tukaelekea ukumbini huko nilisikia sauti za miguno baini ya Teo na Sesi hakika nilighadhibika, Binti yangu aliisikia lakini alinyamaza kimya kimya kama bubu🧏😵 kiziwi.

     Kwiyoooo Lango la sebuleni lilifunguka, nilikua wa kwanza kuingia nadhani hapa nilifanya kosa, Binti yangu alinifuata nyuma ghafra Teo na Sesi waliponiona wakaacha kunyonyana ndimi haraka haraka kama mshare 🏹 waliikimbilia meza iliyojaa madokumentary na makabrasha ya Ofisi wakajifanya wanaandika andika.

    "Umeona mwanangu? 👀Umeona washenzi hawa wakinyonyana ndimi" Niliropoka ingawaje Sesi alichelewa kuliona lile tukio.

     "Bibi mama mkwe unataka kusema nini juu ya uongo wa macho yako?" Teo aliropokwa

      "Teo nilikuheshimu sana nilikuchukulia na kukuhesabia wewe kama mkwe wangu na mwenza💑 kwa mwanangu Semi, lakini kauri nilizozisikia Jana usiku Restroom 🚺ninaapa sintakusamehe" Niliongea kwa kujiamini.

     "Unataka kusema nini Bibi mama  mkwe mbona sikuelewi?"🙄 Teo aliongea akivifungafunga vifungo vya juu vya Shati yake nyeupe iliyopata mikunjo kutokana na upuuzi waliokua wanaufanya pale ukumbini.

      "Kubali au kataa wewe na Sesi ni wapenzi, 💏Jana niliwaona Restroom mkipeana ndimi na kupanga njama za kuniua na kumuua Binti yangu ili mpate kurithi mali nyingi nilizochuma kwa jasho langu" Niliongea kwa hasira hasara

     "Samahani Bibi mama mkwe ninakuheshimu, yote unayoongea ni uongo pamoja na hilo umedhamiria kunigombanisha🥷🗯️ na mke wangu Semi." Teo aliongea, Semi mwanangu akamsogelea mumewe.

      "Teo ni kweli wewe na rafiki yangu Sesi ni wapenzi wa siri?" Semi alimuuliza Teo.

      "Semi ninakupenda lakini kwa hili aliloongea Bibi mama mkwe ni uongo. Tazama Documentary hizi hapa Mimi na Sesi tulikua tunajadiliana juu ya nyumba. Mpya niliyokununulia kwa sapraizment." Teo akatoa funguo🗝️🔐 za nyumba anayodai kuwa ni mpya amemnunulia Semi.

    "Waooo! ☺️🙌Asante My Daring husband." Semi alimrukia Teo na kunyakua kwa furaha zile funguo za nyumba ambayo Teo alidai amemnunulia.

      "Niamini mpenzi ninakupenda hadi kukufanyia Sapraizment, 🙀kama utaendelea kusikiliza maneno ya Bibi mama mkwe niruhusu niondoke nirudi kwenye nyumba yangu nikuacheni." Teo aliongea.

      "Hapana, siwezi kukuacha mume wangu mpenzi, ninakupenda. maneno ayaongeayo mama siwezi kuyaamini sababu hata ushahidi wa picha📷, video📹au audio Hakuna. Nitaaminije." Mwanangu Semi aliongea.

   "Sawa mwanangu kama hauniamini lakini kumbuka majuto ni mjukuu, mimi ninarejea Dar es saalam siku utakapozinduka akili Nina imani utanikumbuka." Niliongea kwa hasira na kutoka ndani ya nyumba ya mwanangu nikaichukua Uber yangu na moja kwa moja nikaelekea Arusha lnternational Airport🛬 nilale hapo ili kesho nirejee Dar es salaam.🌆
============

Lilipita juma moja sikuwasiliana na Semi mwanangu lakini bado moyo uliniuma kuona mwanangu ameolewa na muuaji ☠️🏴‍☠️ tena mwenye tamaa. Sikupendezwa, basi nikampigia simu Semi wangu.

     Ngriii Ngriii ngroooo📞📲 Simu iliita mara tatu. Kisha Semi aliipokea baada ya salamu na maamkizi Nilimuuliza.

       "My daughter🧖bado Unataka kuishi ndani ya ndoa ya huyo mpuuzi muuaji mwenye tamaa, Mateo?"

     "Siwezi kumuacha mama, ninampenda💘. Mimi na Teo tumetoka mbali, tumedumu mapenzi kwa zaidi ya miaka saba hadi hapa tulipofika ninamjua vizuri pia ninamuelewa kama anavyonijua na kunielewa." Semi mwanangu aliongea.

    "Semi mapenzi kila mtu anayataka na kuyalilia lakini kuishi na huyo Bwana msaliti mwenye tamaa naomba nikuambie vunja nazi 🥥chini maji yamwagike, achana naye tafadhali."😢 Nilimshawishi tena na tena.

     "l'cant mama💔, siwezi tafadhali ninampenda Teo, he his charming man, mwanaume wa kipekee." Alinijibu.


    "OK, Semi ninajua mapenzi yana nguvu za kuvunja vunja milima au kupasua anga la Dunia basi ninaomba nikuambie muda huu ninamwita Mwanasheria wangu nitamwambia alifute jina lako kwenye Documentary za urithi ambao kama ningeliitwa na Mungu ☁️⚰️wewe ungelirithi kila kitu ambacho nimevuna kwa jasho langu. "Nilimwambia.

   "Jamani mama!!!" 🙄Aliongea kwa mshangao mkuu.

     "Tena mali zangu zote ninaelekeza iwapo nitachukuliwa na Mola ziwaendee watoto yatima, 🧒👶watoto wa mitaani, wajane na wenye shida. Wewe hutopata hata mia mbili." Nilimwambia Binti yangu ambaye hakuonesha darili za kumwaga chozi Wala kuniomba niubadilishe uamuzi wangu.

**********

Miezi sita baadae nilikuja kusikia mtu akigonga mlango wa nyumba yangu nzuri iliyopambwa maua. 🌺🌹🌸💐🌻🥀 Nikaenda kumfungulia mgongaji kidogo nilishituka nilipomuona Semi amesimama Langoni 🚪nywele zake tipwa tipwa zimekosa mafuta yaani hazitamaniki. Nguo alizovaa kama visepe au vigagula. Binti alidhofika, machozi abubujika. 😭

     "Nisamehe mama🙊🙏🙈, Nisamehe mwanao" Alikimbilia kunikumbatia🫂 akilia chozi zito la ndimu, chozi lililojaa tongotongo.

    "Sikukusikiliza kumbe ni kweli Teo alikua ananidanganya, amenitimua ndani ya nyumba anayodai ameninunulia, amemuweka rafiki yangu Sesi kama mkewe mimi ananiona takataka na uchafu nyumbani." Alilia Binti yangu.

      "Kisa nini? Si ni wewe uliyesema unamjua na yeye anakuja vema mmedumu kwa zaidi ya miaka misaba tangu mkiwa chuo hadi ndoa imepamba moto?"

    "Mama asiyesikia la mkuu atavunjika mguu. Kila neno uliloniambia miezi sita iliyopita lina ukweli. Siku Teo alipokuja kugundua kuwa mali zote ulizoziandika kwa jina langu zimefutwa na kuwahamishia kwa yatima, wajane na wenye shida ndio siku niliyokuja kugundua rangi yake halisi, makucha yake na tamaa zake.👿Amenifukuza kama Umbwa 🐕‍🦺nisiye na mbele Wala nyuma" Semi mwanangu alibwaga chozi.😿😿🥹

      "Pole mwanangu Zimwi 🧞likujualo litakukula kidogo kidogo likumalize, heri mie mamayo nililijua Zimwi mapema kabla halijatumaliza."  Nilimfariji mwana mpotevu nikamkaribisha tena nyumbani lakini nafasi ile nono ya kupata urithi wangu hana tena na sintaibadili nia kamwe never, ever and forever."

**********
 TCHAO. 👋

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...