Monday, November 25, 2024

MY BODY SHAPE, MY BENEFITS

 


MUME WANGU ALINIPA TARAKA 📃 ATI KWA SABABU NINA SHAPE🕴️ MBAYA NILICHOKUJA KUMFANYANYIA HATOKAA ASAHAU.


        Sydney aliporejea kutoka kazini alirejea akiwa amevaa sura ya chuki 😠usoni ile furaha iliyozoeleka  siku zote hakuwa nayo tena. Siku ya Leo alirudi amekunja ndita👊 Yale macho yake yenye mboni nyeusi iliyokooza yakawaka moto🔥, kinywa chake kilichozoeleka kwa upole na tabasamu kikawa ni kinywa kikali kama katafuna lundo la pilipili kichaa mdomoni

       "Nimechoka Abigair, nimechoka kuishi na wewe Tena nimekuchoka. Mwanamke haunivutii Wala haunipendezi"Aliongea Kwa jaziba. Mie nalifikiria yamkini mwenzangu kabanwa kiu ya maji nifanye hima kumletea maji baridi💦 🥛lakini maji yangelisaidia Nini kupooza hasira za Mume wangu!? 😔

        "Shida Nini my sweet husband Sydney🙍?" Nilijaribu kumsogelea pale sofani alipoketi lakini bila kutegemea alinionesha ishara ya kustop✋ kusogelea Huba langu.

       "Umepoteza mvuto wako ule mvuto wa msichana mbichi umekuwa tufe, bonge nyanya🍅 kama mti wa mbuyu🌳, umbo lako limekua baya halinivutii tena maana umekorogeka, hautamanishi mahabani. Ajabu mapenzi hauyawezi siku hizi" Kauri za mume wangu hazikua na mashiko nilihisi utoto, ujana na ujinga umemrudia.

        "Ni Hilo tu au kuna la mno linakukera?" Nilimuhoji.

        "Mapenzi huyawezi na yamekushinda Abigair unene wako kama kitimoto 🐷🐖🐽aliyenona unanifanya nipoteze hisia na hamu ya kufanya mapenzi na wewe. kila siku Moyo wangu unakuchukia. Ujinga wako umeendekeza tabia ya kubugia mayai,🥚🐣pizza 🍕, maziwa🐄🥛, Baga🥯 na vyakula vyenye mafuta 🐷" Alinikemea.

       "Sydney Mume wangu mbona silioni tatizo hapo! nipe siku mbili tatu nianze kufuatilia mlo kamili, balance diet 🥩na mazoezi ya mara 🚶‍♀️🏋️🏊🚴kwa mara umbo langu litarejea na kuwa normal yaani chembamba ukipendacho" Nilijaribu kujitetea.

      "Ushachelewa Abigair naomba Leo iwe ovar yaani penzi lifikie kikomo. Taraka hii hapa📃📜 ikikupendeza Saini ✍️📝leo au Kwa muda wako." Alinishitua.🧟lna maana umbo na mwonekano wangu ndio upelekee afanye jambo la kipuuzi kwenda Mahakamani👨‍⚖️ kuchukua taraka? Jamani! Mbona hajawai kuniambia kuhusu ubaya wa umbo langu? Mbona hatujawai jadiliana kuhusu mwonekano wangu?  Mume wangu mekurupuka kufanya maamuzi.

     "Ninakupenda Mume wangu siwezi kuishi pasina wewe, please futa mawazo hayo, mawazo ya kuniacha hayapendezi katika ndoa. Ndoa ni uvumilivu na mapatano yanayoendana na maelewano." Nilimwaga chozi niliposikia Mume niliyempenda alinitaka nisaini taraka.📝 Mbona ghafla.

       "Sina muda wa kupoteza, Leo ninaondoka, naondoka na Shebimu👠 Secretary wangu yupo ndani ya Gari ananisubiri."Aliongea. Akaendeleza.

      "Mtoto slim, slim, English figure ni mrefu wa asili ya mti wa mkaratusi, mwembamba kama kiuno cha nyigu, mapenzi anayaweza na mapenzi yake ni matamu kuliko asali."Alimsifia na kugamba sifa za Secretary wake.

      "Ina maana Kwa muda wote huo tukiwa ndoani wewe uliishia kuchepuka  na Secretary wako?" Nilimuuliza.

      "Sasa kumbe! Ulitaka nichepuke na nani?"Alinijibu ovyo. Akaingia chumbani kwetu na kupanga panga nguo zake na vikorokoro mbalimbali Kisha akatoka na Begi kubwa la nguo.

      "Sikiliza wewe nguruwe chibonge nataka ufanye hima kutia Saini yako kwenye hio karatasi ya Taraka, siku yoyote ile nitakuja kuichukua." Sikuamini kauri alizotoa Mume wangu nilihisi utani, nilihisi ndoto lakini kumbe mwenzangu alimaanisha.

       "Sydney Mume wangu tafadhali badili maamuzi ya moyo wako sababu jambo ulifanyalo sio sahihi Kwa wanaondoa."Nilipiga magoti chini anisikilize lakini wapi! Mwenzangu hakunisikiliza, alichofanya yeye ni kuufungua mlango wa sebule akatoweka kimya kimya Kwa kuliburuta lile Begi lenye nguo na vikorokoro vyake. Nikamsindikiza Kwa machozi yaliyojaa mapenzi.😢💧

Nje Nilimuona huyo Secretary wake Shebimu akija Kwa mapozi na madaha ya Mbuni mbungani akampokea lile Begi lenye nguo. Gari ikawashwa moto na kutoweka.

         *********
Tangu siku ile Mume wangu Sydney aondoke sikuwa na amani, furaha na Raha. Nilijinyima kupika na kula chakula changu kitamu, nikageukia unywaji wa pombe Kali na uvutaji wa sigareti kali nikijiaminisha kuwa vitu hivyo vitaupooza Mtima 💔ulioachwa. Ghafla nikaja kukikumbuka kisa cha rafiki yangu  LOVE 💕 WA JUAKALI. Rafiki yangu aliyeolewa takribani miaka Mitano iliyopita, kisa chake na changu vilishabihiana.
    
      Love alikua ni mfanyajazi wa kampuni ya Airtel Tanzania. Yeye ni Bi. Dada mwenye umbo tipwatipwa kibonge mwenye kilo zake miambili na hamsini, kusema kweli rafiki yangu huyu alikumbwa na unyanyapaa mkubwa kutoka Kwa marafiki zake wengi wakimcheka Kwa kudai kuwa hakupendeza. Shingo yake Nene hata ashindwe kutazama miguu yake, mikono yake minene na mizito yenye minyama uzembe, tumbole lenye kitambi lilimsaliti na kuimba shape ya tako lake ambalo lilionekana kama karatasi, yaani hakuwa na tako zaidi ya kitambi.

      Basi rafiki yangu Love wa Jua Kali akaanza kupendwa na kijana mmoja aitwaye Zeidi, Zeidi akamwambia Love Mama yangu mpenzi anatarajia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 20 mwezi October, karibu uungane nasi. Kama alivyomweleza kweli tarehe 20 ya October ilifika lakini sijui Zeidi hakutaka kuisherekea ile sherehe pamoja na Love!? Basi akampigia simu Love📲 akamwambia samahani siku ile asingelisheherekea ile sherehe ya mama yake maana amepata dharula ya kwenda Zanzibar 🇹🇿 Kuna shuhuli Bosi wao amemkabidhi.

Love alihuzunika lakini Mtima wake ukamwambia haitakua vema iwapo atakaa tu Bure pasina kumwandalia mama wa boyfriend wake ZAWADI. Basi Love wa Jua Kali akaenda Sokoni Kariakoo, akachagua vitenge viwili vitatu na batiki Moja akafikiria kuvipeleka vile vitu nyumbani kwao Zeidi, amkabidhi mamaye Zeidi. Ingawaje aliambiwa na Zeidi hatokuwepo nyumbani alichofikiria yeye ni kueleka nyumbani kwao Zeidi kupeleka zawadi.

      Alipofika nyumbani kwao Zeidi aligonga mlango na mamaye Zeidi akaja fungua.
   
         "Hallow!" Love Alimsabahi mama Zeidi.

         "Hallow! Karibu sweet heart." Ma Zeidi aliitikia salamu.

         "Naitwa Love, 💕 ni mchumba wa Zeidi aliniambia unasheherekea furaha ya birthday nimeona heri nikuletee zawadi" Love akamkabidhi mama Zeidi ile Zawadi ya birthday 🎈 🎊🥳🎉

      "Love 💕!!? Mchumba wa Zeidi!!?" Mama Zeidi alionekana Kupigwa butwaa.🙃🤔

     "Yes Mama. Je, Zeidi hajakwambieni?"Aliuliza.

      "Sio hajatuambieni! Ila Binti wanishangaza sababu Zeidi yupo ndani na Binti aitwaye Love 💕" Mama aliongea maneno yaliyomshangaza Love wa Juakali.

      "Nitaamini vipi!? Embu nimuone huyo Love. Ingawaje Mimi ndiye mchumba wake Zeidi."
     
      "Ingia ndani ujihakikishie." Love wa Juakali akaingia sebuleni, macho yake yalipogota mbele ya macho ya Zeidi, Zeidi alishituka😰 kombe alilolitumia kunywea wine ya Mzabibu 🍷lilidondoka chini puu🥂 likavunjuka mdomo wazi hadi lnzi 🐝walitamani kuingia walambelambe juisi tamu ya Mzabibu. Macho pima kama Jusi lililobanwa mlangoni, pembeni yake aliketi demu mmoja mrembo , mwembamba wa umbo, mrefu mwenye figa ya kizungu alionekana kumkumbatia Zeidi kimahaba.👩‍❤️‍💋‍👨.

      "Zeidi huyu ni nani?!" Love wa Juakali aliuliza Kwa Mshangao.

    "Nitaeleza Love...... nitaeleza please!"Zeidi akatetemeka.

      "Nieleze Please😡🗯️"

      "Huyu ni Love...... Ni......!"Alishindwa kuimaliza sentensi yake.

        "Ni mchumba wako si ndio? Ina maana Mimi unanichezea sababu ya umbo na mwonekano wangu."Juakali alipayuka.

       "Samahani Love, samahani please. Zeidi alitetemeka mamaye alishangaa, love chembamba alishangaa pia.

      "Basi Love chibonge aliondoka pale sebuleni Kwa hasira huku nyuma Zeidi alijaribu kumkimbilia lakini wapi! Aliitisha Uber akaipanda na kutoweka.

********
Siku iliyofuata Love alipokwenda kazini alishangaa kuwaona wafanyakazi wenziwe wote wamejikusanya ukumbini wanamshangaa Zeidi aliyekua amepiga goti akilia. Aliposogelea zaidi ndipo akakutana na bango kubwa limeandikwa kwa herufi kubwa:

 'NINAKUPENDA 💖 PEKEE YAKO LOVE 💕 WA JUAKALI.💘'. 

Alipolisogelea zaidi ndipo wafanyakazi wenza wakampisha na kumpa nafasi ya kumuona Zeidi aliyekua akilia Kwa uchungu wa machozi ya damu. Zeidi alipomuona Love akamkimbilia na kumpigia goti 🧎akamuomba 🤲 msamaha akilia😭.

      "Nisamehe Love, nisamehe mpenzi. Nilifanya uamuzi mbaya kukubagua kutokana na umbo lako nene lakini Leo nimekuja kugundua wewe ndiye mpenzi wangu sahihi."Alilia Zeidi hadi kamasi 🤧kumtoka.

      "Sikupaswa kukubagua Love, nilipaswa kuwa na mapenzi ya dhati, nilipaswa kukupenda na sio kuupenda mwili ambao unaweza kubadilika nyakati zozote. Please nisamehe love😥🙏"Juakali alimsikiliza Zeidi.

      "Yule Love uliyemkuta nyumbani amenisusa na kuniacha 💔baada ya kugundua kuwa Nina uhusiano na wewe. Please ninaomba tulirudishe penzi letu liendelee. Ninakupenda sana love.Zeidi alililia😿😿 Basi Love akamnyanyua Zeidi pale
sakafuni alipopiga goti akamwambia:

      "Maamuzi yako hayakuwa sahihi Zeidi, kama ulilipenda umbo kuliko moyo wenye mapenzi ungeliniambia mapema Ili nijijue naelekea wapi na njia ipi niishike"

      "Nisamehe 💕 "Zeidi Aliomba tena.

      "Sawa nimekusamehe mpenzi, usirudie tena sababu ubaguzi uwatenganisha watu"Love wa Juakali akamkumbatia Zeidi naye Zeidi akamkumbatia Kwa nguvu zote Hadi wafanyakazi wote wakafurahia Kwa kupiga makofi na kushangilia.👏👏👯‍♀️.

**********

Ngo' ngo' ngo👊 nilisikia sauti ya mtu akigonga mlango🚪 wa sebule yangu. Wakati huo nalikua katikati ya mawazo juu ya kisa cha Love wa Juakali na Zeidi, nikaacha kunywa vileo vyangu vikali🍺nikaeleka kuufungua mlango. Oh! Nilipoufungua mlango nilikutana na sura ya shogangu Sabienjo. Waooo! 😹🙋🫂🤗Nilimfurahia.

      "Karibu shogangu karibu mwaya!😗" Nilimkaribisha Sabi.

       "Unaniweka tumbo joto Abigair."Alianza kunichamba👌pasina salamu wakati huo mie kilevi kishashiba tumboni.

      "Nimepiga simu🤳 mara Mia lakini mwenzangu hupokei, ninatuma meseji Fb na Wasap lakini sijibiwi. Jamani Abi! Wanifanya nihisi mazito yamekukamata." Aliongea kihasira 🤕fulani kimemkwama shingoni.
      
     "Jamani Sabi!!🤔" Niliongea kilevilevi.

     "Umeanza kunywa pombe kali lini?!🍾"

      "Nina mazito yanayonichanganya."Nilimjibu.

 Tukaelekea sebuleni tukaketi nikaanza kumueleza Sabi matatizo yaliyonikuta.

    "Mwenzio nimeachwa💔." Niliongea kilevi levi.

    "Unasemaa!🧟 Sabienjo alishituka kidogo chupa ya bia aliyojichukulia kwenye Jokofu almanusura impokonyoke na kudondoka, na kwa jinsi ilivyokua ya baridi ingemtetemesha.

        "Hivyo hivyo kama ulivyosikia👂" Nikajimiminia kilevi kwenye Birauli Sabi alinitazama tu.

     "Abi, tafadhali wacha kunywa pombe yamkini pombe inakupumbaza."Alinishauri.

    "Nimefall in love 💕 with pombe." Nikacheka Kwa sauti kuu kisha nikaongea serous.
   
    "Sabi shogangu shemejio anadai siyajui mapenzi na nipo ovyo. Umbo langu halimvutii mapenzini tena halimpendezi kama alivyonikuta zamani nikiwa Kuku wa kizungu, slim body, English figure. Amenichukia, amenidharau, hajaupenda mwili wangu, amenikataa na taraka ameniachia niitie Saini. Nikubali tuyamalize."

      "Maria mama wa Yesu!🤯 Sabienjo aliishia kushangaa kisha akaongea.

      "Nilijua mapenzi yatoka moyoni, mapenzi uvumilivu, mapenzi maelewano na mapenzi ni vile mtu anavyokupenda na kukubali. Inakuaje Sasa alichukie umbo ambalo laweza kubadilika iwapo unania ya kulibadilisha.🥴

     "Ndo' hivyo Sabi moyo wa mtu umeficha mengi, mie nilimpenda Kwa dhati kumbe mwenzangu kapenda kidogo." Nikachomoa pisi ya Sigareti na kuiwasha kwa kutumia kiberiti cha gesi, pisi nyingine nikamgea Sabi, akaivuta. Uzuri ni kama vile alianza kunogewa na kunoga kwa ile story akaacha kunywa kale kabia kake akachukua Birauli na kujimiminia Jack Daniel pale mezani tukawa sawa mwendo wa kugugumia zile pombe Kali.

      "Kwahiyo hiyo Taraka chafu ushaisaini?"Aliniuliza.

      "Nangoja mwenzangu aje kuibeba. Sina jinsi, ninampenda lakini kitendo cha yeye kuniletea Secretary wake nyumbani kwangu ni dharau na kunishusha cheo cha kuitwa mama wa nyumbani."


     "Jamani! Jamani! Yaani Kwa upumbavu wake kaamua kukuletea mwanamke mwingine nyumbani" Sabi alizidi kuudokoa dokoa ule umbea uliokolezwa na kuchagizwa na vilevi vilivyotuweka huru kuondoka aibu na stress.
   
      "Nakwambia mwanaume yule ni kama Umbwa🐕 alidhani ukewenza👩‍❤️‍💋‍👩 nitauweza"Teh teh teh 😂😹🤣🤭Nilicheka Kwa sauti kuu.

     "Mmh! Sasa mwaya usikae kizembe ukazidi kuugua kwa stress na ukafa kizembe. Mwenzio ningali bado sijaingia ndoani 💍lakini ninamfrahia Mr. wangu James ambaye hanibagui Wala hanichagui. Embu tufanye jambo moja la faida."Sabi aliichukua simu yake nzuri na njema machoni, Samsung Galaxy 📱 simu ya bei gharama. Kisha akaniambia.

      "Niruhusu tufanye mchakato wa kutafuta Boyfriend mtandaoni" Mmmh!☺️ shogangu alinishangaza.

        "Mmh!🤭 Mwenzangu mbona umeenda mbali ina maana unataka wanaume wote Duniani wanifikirie Mimi kama Malaya ninayejiuza mitandaoni 🌍?"

     "Sio kwamba unajiuza Abi, move on dear, usikae kizembe. Achana na Shemela Sydney huu ni wakati wa kumuonesha kama yeye anasema chanini hiki wewe mjibu Dhahabu hii💛🌟" Maneno ya Sabi yakaniamsha na kunifariji mie niliyeachwa kizembe.

     "Aya mwaya tufanye jambo la faida💰" Tukazama mitandaoni🌏 tukazifungua zile channel za watafutanao, wale watafutao wapenzi, wachumba, mashangazi , maanko na faraja ya moyo. Basi Sabi akanifungulia Account yangu akanipiga mapicha na kuposti mtandaoni. Babu 😂😂  mie tipwatipwa chibonge nyanya niliyeachwa nilijiachia Kwa mapozi mbali mbali. Tena sie wawili siku ile tukaendekeza starehe, tuliipiga mitungi na Sigareti hadi mitungi na Sigareti ziliomba poo😂😂🤣😗.

******
Asubuhi ya siku iliyofuata nilijidamsha kivivu, Sabienjo alikwisha chukuliwa na Boyfriend wake James. Mie niliamshwa na mlio wa simu yangu, macho yalinijaa tongotongo, mekundu kama nilijipakaza pilipili kichaa nywele tipwatipwa hazitamaniki. Bado pombe ya Jana ilikua ikivuruga vuruga kichwa changu. Basi nikaichukua simu yangu iliyokua ikiita pasina kupokelewa. Video call!!🤔Wasap! Mie huyo nikaiwasha.

Nikatazamana na mwanaume mtu mzima mwenye kadirio la miaka harobaini na tano, mwanaume yule alinipungia mkono 🙋‍♂️Kwa tabasamu mwanana. Aibu ilinijaa, mwanaume safi kama yule kutazamana na mwanamke mwenye tongotongo nzito machoni, nywele tipwatipwa, mwanamke mwenye macho mekundu ya kilevi na baya zaidi ningali nimetoka kudamka kitandani. Oohsh!!😤 Nikaizima ike video call Kisha nikaingia mesenja kuandika ujumbe.

     'Tafadhali nipe dakika kumi nijisafishe, ninaona aibu kutazamana.' Nilipoituma ile meseji jibu likaja haraka haraka.

   "Usijari rafiki yangu, Nina mengi ya kuongea nawe" Oh! Nilifarijika kibonge mie haraka haraka nikaingia bafu kuswaki ovyoovyo, nikazititimua nywele zangu ndefu Kwa maji ya vuguvugu kisha nikazama ndani ya sinki la kuogea nikaukosha mwili wangu ule mchovu ulionogewa vilevivya jana Ili kupunguza stress.

      Dakika kumi kupita nilikwisha maliza kujikwatua pale Dressing table, 👗 nikametameta kwa  kujiremba na kupendeza. Mie mshamba baada ya kujilipstick nikajimwagia marashi ya Pemba na Unguja: Udi, iriki, mdalasini na vumba.... Teh tah teh🤣🤣 sikutaka kupoteza muda nikarejea ile video call nikatazamana na yule mwanaume mtanashati.

     "Niite Dakta Dario" Alijitambulisha.

      "Niite Abigair." Nilijitambulisha pia.
     
        "Waooo! Jinalo zuri, mwaaa😘."

        "Lako pia 😋"

        "Nimeichukua Nambari yako kule Dating network. Nimeipenda introduction yako, nimependa kila kitu kinachokuhusu wewe, zaidi nimelipenda umbo lako. "

 Woyooo!🤣😗 Mambo si ayo! Mie nikatabasmu

     "Asante Dakta Dario." Aibu 🙈kidogo ilinivaa.

     "Dear, naomba kama Leo utakuwa na muda tuonane LAMADA HOTEL. Tutafurahia Dinner."🍝🍽️ Mtanashati wangu aliniomba Leo tutoke.

        "Mh!" Niliguna Kwa aibu.

         "Ninaheshimu mawazo yako."Aliniambia Lugha
 tamu kutamka.

        "Sawa, Dakta Dario. Jioni ya Leo nitakua na muda mzuri wakuonana LAMADA HOTELI " Nilimjibu Kwa kiaibu kidogo kilicho nifunika, Kisha nikamuaga na kuikata simu. Moyoni  nikichekelea, mwili wangu ukarukaruka na kufarijika. Sauti ya Dakta ilitosha kuniponya stress zangu, sura yake tanashati ilizuia ugonjwa wowote kunivamia. Umbo lake jembamba na mavazi yake nadhifu yalinipendeza. Nikajiambia bahati nasibu haiji mara mbili mbili kwahiyo nisiichezee.

 ''''''''’''''''''''''''''''''''''''''''''

Saa kumi na mbili jioni niliingia bafu kukoga kisha niliyabadili mavazi yangu nami nikapendeza kwa mtoko wa jioni. Basi mie Abi nikiwa nataka kutoka sebuleni kwangu akaingia Mume wangu wa zamani, mtaraka wangu Sydney,  akanitizama kuanzia kiguu Hadi unyweleni.😶

       "Nyooo! ☹️😖 Unadhani ukivaa hivyo ndo' utapata mwanaume wa kukupenda!?"Aliniponda lakini mie sikumjibu nilimkalia kibubu.

       "Ninakuapia juu ya Jua 🌞na Mwezi ☪️hutopata mwanaume wa kukupenda kwa umbo lako hilo baya kama Andazi la kihindi." Alinikashifu lakini bado sikumjibu.

     "Hupendezi lakini unang'ang'ania kupendeza! Nimeifata Barua yaTaraka, ushaisaini!!?" Bado sikumjibu nikaingia chumbani na kutoa ile Barua ya Taraka Kisha nikamkabidhi.

        "Huna adabu Nguruwe  wewe, yaani ninaongea na wewe lakini haunipi majibu! Kibonge mpumbavu wewe"Aliingia chumbani kisha akatoka na makoti yake matatu aliyoyasahau ile siku anaondoka na Secretary wake Shebimu.

     "It's over now Sydney. N'shapata kipepeo🦋💗 wangu wa kunipendeza usitegemee kama nitayabadili maamuzi."Alinitazama Kwa Jicho la dharau Kisha akaubamiza mlango na kutoweka. Nilimshukuru Mola wangu hajaharibu jambo ingawaje alinipoteze muda wa kuonana na Dakta Dario.


###########

       Saa Moja kamili, mida ya usiku nilifika LAMADA HOTEL moyoni nikijuta kuchelewa maana sikumuona Dakta Dario. Nikamuita mhudumu nikamuuliza iwapo amemuona mwanaume wangu,mwenye sura ya Kiarabu, nyele ndefu Singa za kichotara, mwenye mustach wa kihindi, sauti tamu ya kizungu tena kavalia miwani ya glass.👨‍🏫🤓🥸 Mhudumu alimtambua Kisha akaniambia: 'huyo alikuwepo hapa muda si mrefu kaondoka' Yallah!🧟  Niliumia na kulialia mtimani🥲. Nilichelewa siku tamu ya kuonana na Dakta Dario. Huzuni ikanikumbata.

    "Wacha niondoke."Nilijisena moyoni,

     "Au nimpigie simu." Mtima ulipata wazo. Ile natoa simu yangu ya mkononi nikasikia sauti nyuma ya mgongo wangu. Alikua ni Dakta Dario.

     "Sweet  heart❤️ umefika mapema." Niligeuka, nikamkumbata na kumpiga kiss shavuni.😘 Hmmwaaa

        "Nilifikiria haitapendeza mrembo kama wewe kuja na kuondoka pasina zawadi ya Maua 🌹🌷🌺. Alinikabidhi lundo la Maua ya Rose, mie nikatabasmu, tabasamu la bahati.

   "Asante Daring💞🥀", Tuliketi pale mezani, manwyaji na malaji yakaandaliwa, tulianza kula kunywa na kutambulishana. Nilimweleza mie ni Mama wa Nyumbani niliyeachwa Kwa Taraka na yeye akanieleza ni Dakta aliye Singo Hana mtu, Hana kitu zaidi ya kunipenda mie. Nikamkubali basi tuliendelea kula, kunywa na kucheza Muziki🎺🎻🎶💽 baada ya hayo yote Dakta wangu akafanya kunirudisha nyumbani kwangu.🏘️

      Ikawa hivyo Tena mapenzi kati ya mie Abigair na Dakta Dario yakapamba moto, yakaiva na kututosha kushiba na kunenepa tulinenepa. Nilianza kimsahahu mtaraka wangu Sydney yule aliyedai kamwe sintakuja kumpata mwanaume mzuri kutokana na umbile langu ambalo halikumpendeza.

Basi siku Moja tukiwa pale LAMADA HOTEL Dario Mpenzi wangu alienda kaunta kuagiza wine ya Mzabibu mie niliachwa pale mezani nikinyofoa nyofoa vipande vya nyama ya kuku kwa mrija. 🐓🍹Ghafra akaja na kusimama mwanaume aliyenikera  na kunifanya nijisikie kichefu chefu na kutapika. Nilimtazama jinsi alivyokonda na kudhoofika, nilimtazama alivyoisha kisaikolojia. Hakuwa yule Sydney niliyemzoea Mwaka mmoja uliopita, tangu tutarikiane. Alipoona nikamtazama Kwa utulivu akaniambia.

        "Ninaomba unisamehe Abigair mpenzi wangu ninajua nilikukosea lakini sikupaswa kufanya hivyo." Kama kawaida yangu Nilimsikiliza kimya na kumkalia kibubu.

          "Nisamehe Abi mwenzio niliingia choo cha kike🚻 na Sasa majuto yamenivaa na yanalazimisha niyabebe. Nilikudharau my ulipokua mke wangu na nikakuapia kwamba hutokuia kupata mwanaume atakayekuja kukupenda kumbe viapo vile nilijiapia mie. Shebimu amenikataa 💔na tena ameenda kuolewa na mwanaume mwingine. Chozi lilitamani kumdondoka.😿

     "Kisa Nini mwenzangu au na wewe hauyajui mapenzi?" Nilimtania.

       "Bora nisiyajue mapenzi lakini sio Kwa dharau hii ya kunikataa kisa tu nimefirisika. Sina hella na sifai kuitwa mwanaume, imagine starehe zote tumezifanya kama pesa kutumia tumetumia pesa nyingi alafu baada ya kuona zimeisha ndipo mwanamke ananikataa na kunikimbia." Safari hii chozi lilidondoka naye akachukua leso akajifuta.

          "Pole," Niliongea Kwa ufupi.

          "Sijapoa Abigair Nina donda moyoni. Ninakuomba unipe nafasi turudiane tena na tupendane tena, tuishi wote Kwa furaha kama zamani." Aliitamani kunipigia goti,🧎‍♂️ viganja vya mikono yake amevikunja ishara ya kuniomba na kunisihi.🙏

      Teh teh teh, 😁🤣 nilicheka Kwa dharau.

      "Wewe usiyeyajua mapenzi na Mimi nisiyeyajua mapenzi tutaendana vipi? Nyota 🌠 zetu hazifanani lazima mmoja wetu awe anayajua zaidi ya mwingine. Mpendwa Ex naomba usijisumbue." Nilimwambia wakati huo Dakta wangu, Dakta Dario alirejea pale mezani

     "Niite Dakta Dario, huyu ni Abigair my sweet heart,💘 wangu wa moyoni kufa na kuzikana." Akanibusu Kinywani na mie nikamshikiria ili aendelee kunipa ndimi 👩‍❤️‍💋‍👨 kitendo kile kilimkera EX wangu.

     Mie na Dario wangu tukasimama pale tulipoketi tukajiandaa kuondoka, Dario alivyo na roho nzuri akakitoa kikadi 💌 cha mwaliko wa harusi yetu kisha akamkabidhi Ex wangu.

       "Wiki ijayo mie na Abigair tunatarajia kufunga ndoa,👰💍👰‍♂️ karibu sana tusheherekee pamoja. Dakta Dario aliongea. Tuliondoka pale mezani kuelekea nyumbani tukamuacha Sydney amesimama palepale mezani, abubujika machozi, hakika majuto yalimsumbua.




..................
TCHAO 💌 👋👋






   

     ,








    


      

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...