"Sabi." Mama wa kambo aliniita kwa sauti ya juu yenye kuniogopesha.
"Abee Mama." Nilimwitikia Mama wa kambo.
"Embu nenda ukaoshe vyombo, upugute deki, ufue nguo na ukiisha maliza ukateke maji Kisha upige pasi nguo za Fatuma mdogo wako. Mama wa kambo aliongea kwa ukali.
"Sawa Mama nilitii kwa unyenyekevu. Ndivyo ninavyoishi na Mama wa kambo tangu Mama yangu aage dunia miaka kumi na misaba iliyopita sijawai pata amani, ni mwendo wa kazi na makazi lukuki tena kazi nzito kutamka pale nyumbani.
"We Sokwe embu rudi hapa," Aliniita jina baya la wa nyama wa Porini
"Abee mama," Niliitikia na wakati huo huo nilikua nishafika mlangoni ilibidi nirudi maana kama ningelikaidi mwenzenu ningelikiona kilichomtoa Kanga manyoya,
"Nataka ufanye kazi haraka ukiisha maliza kazi nilizokugea haraka uende Sokoni kununua mahitaji ya nyumbani pia utaenda mashine kusaga yale mahindi uliyoyaloweka Jana." Duh! Sabina mie Binti wa kazi na makazi
"Sawa Mama" haraka haraka nilienda kujishuhulisha na kazi za pale nyumbani.
Wakati Fatuma anajisomea na kudekezwa na mama wa kambo mie ambaye hata baba yangu hakutaka kunilinda niliishia kuteseka kwa kazi nzito, mapigo na mapigiti kama ngoma, matukano makali kama sauti za redioni.
Nilipomweleza baba yangu mzazi kuhusu kadhia anifanyiayo mama wa kambo kwani baba mzazi alijali kilio changu aliishia kunipa adhabu kali ya kufinywa mashavu yangu kwa kutumia kisu kikali kilichonitoa makovu mazito ambavyo hadi leo nikijitizama kwenye kioo ninalia masikini. Embu niambieni jamani kama baba tu ameshindwa kunilinda na kunitetea ni Nani atakayeweza kunilinda na kunitetea?
Fatuma mdogo wangu alikula vizuri, alivaa vizuri, alideka mtoto akadekeka na kupendeza. Zawadi nyingi zilimiminika chumbani kwake akajiona Malaika pendwa.
Basi siku moja mie Sabina baada ya kuchoshwa na mateso ya pale nyumbani roho yangu ikaniambia 'Toroka mwaya utaendelea kuishi katikati ya haya mateso hadi lini? Vaa yako tu inakunyanyasam, utavaa kaukanikuvae hadi lini? Miguu imepigwa Jua hadi imeota sagamba. Tumbo launguruma njaa na kiu, haupakai mafuta au sabuni mwilini zaidi ya kupakaa tongotongo na machozi.' Jaman!! Chozi lkanimwagika mie Sabina.
Binti nilidhamiria kutoroka na kutoroka huko nitaenda popote pale penye maisha. Labda Posta, Mnazi mmoja au Ferry nikajiunge na machokoraa na ombaomba nijenge urafiki nao. Labda Kariakoo, Gerezani Muhimbili au, Manzese nikajiunge na magenge ya wauzao Unga (teh teh teh 😅😅😂 SIO Unga wa ngano au Sembe bali ni Unga special). Labda nikimbilie Buguruni Sheli, Tandika Sokoni au Mwananyamala nikajiunge na Dada poa niuze uchi wangu. Uwii!! ðŸ˜ðŸ˜Naogopa kukufuru Mungu, Mwili wangu sio hazina ya Ibilisi mwovu mwili wangu ni Hekalu takatifu la Bana Yesu.
Basi mie huyo hima hima kupanga vinguo na vigangura vyangu nikajiwekea kwenye fuko la Maliboro Kisha niondoke Oysterbay.
Vuuuuu, Mlango wa chumba changu ulifunguliwa ovyo. Kha! Nilishituka na kutetemeka nilipokuja kugundua mbovu aliyeingia ni Fatuma moyo wangu ulisuuzika Maana Angelikua ni Step mother ningelikoma kutoroka, ningelichomwa na kuiva kwenye maji moto yanayochemwa ndani ya pipa, Ningelipigwa kwa vigigi, vigogo na kuni nzito hadi maji niyaite Maa! Ningelikesha naosha na kuogesha kuta za mjumba wetu wote kuanza sakafu hadi juu ya Dari We! Naogopa mie.
"Sabina nipo njia panda mie. " Alianza kuongea mara baada ya kunibamizia mlago wa chumba changu
"We naye ndio nini kunishitua na kuniweka roho yangu juu tipwa tipwa hadi nidondoke chini puuu povu kinywani kama nina kifaa" Nilimjibu kihasira kwambalii kilinichota.
"Wewe embu nisikilize mimi kisha unipe ushauri sitaki mahasira yako" Binti wa kumi na saba alinijibu mie wa ishirini na tatu.
"Embu ongea haraka mie nina kazi za kufanya" Sikutaka mengi maana ningeliyaleta mengi angeyapeleka kwa Mamaye na Kwa jinsi alivyo domo la uongo na umbea atafurahia akiona ninapigwa, ninatukanwa na kufedheheshwa. Jaman ndani ya nyumba ya baba yangu niliishi kwa hofu na amani kupotea.
"Sabi mie Nina mimba ya Dani Boyfriend wangu na Dani kaikataa" Aliongea akiyaregeza macho ili kuyabembeleza yatoe chozi na kamwe macho yake hayakumuunga mkono
"Toba! Fatuma" Nilishituka.
"Ndo' Maana nimekwambia Nipo Dillema nisijue lakufanya nipe ushauri au niitoe?" Binti madekezo aliropokwa na kujikurupusha.
"Fatuma wewe Binti wa kumi na saba tayari ushabeba mimba? Yote ni shauri ya deko na madekezo kutoka kwa mama" Nilimjibu yeye kaketi kimya na kujilaza kitandani atazama juu darini kitopu chake chaonesha kitovu alichokibana kwa hereni yenye kito cha Almasi. Suruali yake aina ya Jeans ina michano chano mfano wa tambaa la deki.
"Sielewi Sabi nasema Sielewi"
"Kwani Baba na mama wanasermaje?" Nilimuuliza
"Hawajui, they know nothing about it" Aliongea kiswahili kilichochangizwa kimomboo.
"Ndo' uwaambie kwanza na uwasikilize wanasema nini"
"Kwahyo wewe hautaki kunishauri eti eeh! Sawa" Yallah! Fatuma hakunipa nafasi ya kuongea neno akafanye hima kutoka chumbani kwangu haraka haraka nikamsikia akishuka kwa kasi ngazi za horofa ile ya pili kuelekea sebuleni. Moyoni nilihisi anaweza fanya ubaya maana Binti mcharuko yule hajatulia. Nikaacha na na mpango wangu wa kutoroka nikamfuata.
"Baba na mama Kuna jambo ni Naomba niwaeleze" Mh! Kwangu yamemshinda ndo' ayakimbize Sebuleni kuwaeleza wazazi. Fatuma mdogo wangu kweli kuishi kizungu Kuna shida.
"Eleza Binti yetu, Our gorgeous, Our beautiful life and Our everything" Mama wa kambo aliporomosha kimomboo kumsifia bintiye.
"Baba na mama mie nimekamta mimba ya Dani Boyfriend wangu na Dani Boyfriend ameikataa." Aliongea maneno yaliyowashitua Baba na mama wa kambo, wakati huo mie Sabina nimejibanza moja ya kona ya pale sebuleni ninasikiliza.
"Unasema kweli Fatu" Unasema kweli wewe una Mimba? " Baba alimuuliza Fatuma
"Nilete kipaza sauti nipaze sauti au nilete Sabufa nifungulie sound ya juu?" Binti madekezo alimjibu vibaya baba Kisha kwa madekezo akaongea tena.
"Mama nitoe au niilee? " Mama wa kambo akamjibu Binti madekezo
"Hapana Binti yangu usiitoe hiyo mimba sie wazazi wako tutakusaidia kuibembeleza" Sikuyategemea yale maneno yaliyomtoka step mother, nilitegemea angemkaripia na kumponda hadi mtoto ajinyee tumboni.
"Itunnze mwanangu mtunze huyo Malaika ni Zawadi yako, Zawadi hadimu." Baba aliunga mkono. Ikawa hivyo basi Mie Sabina nikalifuta wazo la kutoroka safari hii nikachukua jukumu la kumlea Fatuma mjamzito. Kila shughuli au tamanio lililohitajika nililihangaikia, Grocery, dukani, Sokoni au kumsindikiza Clinick. Iwe kumpikia atakacho na kunimwagia usoni kimkeracho akinilaumu nampikia uchafu, dikodiko rojorojo na tope. Ah! Iogopeni mimba baguzi,
Kumfulia kila alichochafua au kutapikia kumuogesha na kumhadithia soga za kina Sungura na Fisi ilimradi tu mdogo wangu aridhike, Hatimaye siku ya kuingia Leba ilifika akajifungua mtoto wa kiume akampa jinale Patrick bado tu mie Sabi niligeuzwa nyanya wa kumlea yule mtoto, Nikimwogesham nikimfulia nikimbadilishia Pampasi, nikimlisha na kumbembeleza hadi mwili wangu ukanichukia kwa jinsi nilivyojitoa ajiri ya Fatuma na Patrick mwanaye.
_____________
Basi baada ya mwaka mmoja kupita nikiwa nakabembeleza katoto tayari kulala, aya sasa nikakalaze kitandani. Nilipoingia chumba cha Fatuma mamaye P nilikutana na Mastaajabiko, Binti deko alikua akipanga na kuzipangua nguo zake alizoziweka kwenye begi, alizozihitaji na kuziondoa zile asizozihitaji
"Eh! Nambie mwenzangu kupanga na kupangua Safari ya wapi Sasa?" Nilimuuliza?"
"Sikiliza Sabi. " Aliongea kwa haraka.
"Hivi sasa mie nishatimiza umri wa miaka kumi na minanae, umri wa kula Raha na starehe za ujana, nilichukia sana kitendo Cha kubeba mimba iliyoniharibia starehe zangu. Sasa Wacha nikazamie Nairobi nikaponde Raha na Boyfriend wangu Dani." Aliongea Kwa kujiamini.
Dani Tena!!🥺 Nilishangaa.
"Fatuma umerogwa wewe si mzima. Yaani unataka kuondoka uende Nairobi na huyo Dani aliyemkataa Patrick, baya zaidi tangu Patrick amezaliwa hakuna siku ambayo Danny amekuja kumtazama sembuse kumletea Pampasi na visepe" Nilimfokea madogo wangu ambaye hakuonesha darili za kujali.
"Tafadhali Sabi usinifokee" Alielekea dressing table kujichora chora lips rangi nyekundu mdomoni.
"Nakuachia Patrick umtunze, umlee akue apendeze. Ole wako nikirudi nisikie ati ulikuwa unamtesa " Teh teh teh, 🤣 nacheka kama ni mazuri. Binti deko yamkini alirogwa akachanganyikiwa.
"Unaongea Kwa kutumia amri na mamlaka, Mama gani wewe unayemtelekeza mwanao kwasababu ya mapenzi ya kinafki. Fatuma rejesha akili ubongoni usitumue uchi wako kufikiria" Nilimtusi.
"I don't care." Alinikoromea. Akaitazama saa yake mikononi "Ninachelewa, ndege ya kwenda Nairobi itaniacha." Aliongea haraka haraka kama Mwendawazimu. Akalikokota kokota Begi lake haraka haraka akashuka ngazi za horofa ya pili, Uber ilikua ikimsubiri, Dani alikua akimsubiri pia. Akapakia na kutoweka hata kumbusu mwanae alishindwa. Mie Sabina nikaeleka Sebuleni pale Baba na Mama wameketi.
"Baba na Mama hivi mnajua Fatuma amebeba Begi lake la nguo na kutoweka?" Nilipaza sauti Baba na Mama wa kambo wakatazamana Wala hawakujishuhulisha kunijibu.
"Baba na Mama Fatuma ameondoka na kumuacha mwanaye mikononi mwangu." Nilirudia kuongea.
"Hivi wewe nguruwe mweusi hauoni kama tupo kujadili jambo muhimu." Mama alifoka.
"Tafadhali ondoka ustuharibie project zetu. Mambo ya Fatuma hayana umuhimu Kwa Sasa" Baba alifoka pia wakaendelea kusaini saini Document ambazo hata sikujua zinahusu Nini? Nikaondoka pale sebuleni nikaeleka chumbani kwangu na kuubamiza mlango wa chumba changu 'Mbaaa' mtoto alishitukana kuanza kulia aliposikia sauti ile kubwa ya mlango.
"Nyamaza mwanangu nyamaza kuanzia Leo wewe na Mimi, Mimi na wewe. Nitakua mama yako milele. Nilimwambia Patrick. Basi kuanzia siku ile Patrick Akawa wangu na Mimi wake, nikahangaikia ili na lile Kwa ajiri yake. Akisikia njaa mama yake nilimwandalia uji, maziwa, maji safi, matunda na juisi. Nilimwogesha mwanangu, Nikimfulia, nilimbadili Pampasi, nikamlea mwanangu aliyekua taratibu.
Bahati nzuri Sabina mie Nina akili za maisha, nikafungua ubanda yaani Gengela mahitaji ya jikoni nikauza nyanya, vitunguu, hoho karroti, mbogamboga, mkaa na pia nilipika mabumunda wateja wale wafurahie kazi ya mikono yangu.
Mungu hamtupi mja akajitokeza huyu mkaka jinale Thomasi mie namwitaga Mwanasheria.' Yeye ni Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Ilala. Ati Toma akasema ananipenda. Teh teh teh🤓 😘🤣🥰 Mie bila kinyongo nilimkubalia na Kwa jinsi nilivyoyachoka maisha ya pale nyumbani Acheni tu. Toma akanitaka tuishi wote tupike na kupakua.
Ulikuwa ni wakati wangu, wakati wa maringo kumuonesha Baba na Step mother kwamba na mie n'shapendwa. Sikuwaambia goodbye bin kwaheri nikabeba vyangu na kumbeba Patrick mwanangu tukahamia nyumbani Kwa Mwanasheria. Maisha matamu yakanifuata.
________________
Miaka mitano kupita nikaja kusikia mtu akigonga ovyo mlango wa sebule yangu mie niliyekua namenya matoke. Nikadamka pale sebuleni kitumbo ndiii🤰 bado miezi mitatu tu niingie Leba. Nilielekea kuufungua mlango Patrick mwanangu akiwa amenishikilia miguu asitake kuniacha.
'Eh! Toba!' Nilishangaa 🥺ðŸ¤Fatuma huyu huyu Binti madekezo karejea baada ya miaka Mitano ya kuponda raha na starehe. Karejea kawa mkondefu asitamanike, kadhoofu tena kapooza hata inzi wasitamani kumsogelea.
"Nimekuja kumfuata Patrick mwanangu." Hata salamu haijui yeye anachojua ni jina la Patrick tu.
"Patrick yupi au umekosea njia." Nilimuuliza Binti deko.
"Si huyo chini ya miguu yako, tafadhali Sabi usinizuie kumuona mwanangu, ni haki yangu" Alibwata.
"Haki hiyo kwioooo!😹😹 Nilimbetulia mdomo na kumfyonya mxiuuuu😣.
"Hakuna mtoto aitwaye Patrick hapa, labda huyo unayemtaja alikufa zama za kale za mawe." Nilimpa vidonge vyake.
"Mpumbavu wewe miaka Mitano imepita sasa hujawai kumkumbuka mwanao Leo hii baada ya starehe kukutema ndio umeona Bora uje uteme mate yako mlangoni kwangu, Bibi umechelewa.👌
"Sabi nitaenda kumuona Mwanasheria." Aliropokwa.
"Eeh muone na ukae ukijua na mie ninaye Mwanasheria wangu" Sikutishika na yule nguruwepori. Akaondoka amejaa hasira.
____________
Niliitwa Mahakamani, yule mshenzi Fatuma eti alinifungulia kesi akidai ati nimekataa kumruhusu amuone na kumchukua mwanaye Patrick. We! Mbona mjadala uliiva mahakamani nilizipika kelele Hadi zilipikika, nilitema cheche Hadi moto uliwaka, nilimpandishia ruhani👿👾 Hadi shetani 👹wake akaomba poo, yaishe. Mahakama ilinielewa na Fatuma akaambiwa ingawaje mtoto amemzaa lakini sio wake. Hakuna mama mwenye akili ambaye angefanya maamuzi ya kijinga kumtelekeza mwanaye ati kutafuta starehe na Raha za ujana.
Kesi ikaunguruma mie Sabi nikashinda ile kesi, Patrick Akawa mwanangu tena Toma akanishauri nimuadopt kabisa Ili awe wangu halali. Jamani mie Sina hasara maana wahenga walisema 'Aso na mwana akumbate jiwe, kizuri kiuze. Ukisema chanini hiki kumbe wenzio tunasema Dhahabu hiyo.😹
Wacha nimfunike shuka Patrick mwanangu, kesho afanye Kuwahi kindergarten. Mwanangu kimomboo kimeanza kufanya kazi mdomoni mwake ati anasema:
"I LOVE YOU MOM💗"🥰😘🤣. Na mie ninamjibu P. Wangu
"I LOVE YOU TOO MY PRECIOUS BOY💕. NINAKUPENDA💖, NINAKUJALI NA PIA NINAKUTHAMINI P. WANGU"
-------------
TCHAO.💕
No comments:
Post a Comment