NILIJUA MUME WANGU 👩❤️👨ATAAGA DUNIA KWA MARADHI YA KANSA 🥵💊💉KUMBE MWENZANGU 🧍♂️ ALIPANGA KUFEKI KIFO⚰️☠️ ILI AMUOE MALAYA 🤹♀️ MWENYE TAMAA.
Siku tuliyokwenda Hospitali ya Ocean🌊 Road kumuona Dakta Eze 👨⚕️🩺atueleze majibu ya vipimo vya ugonjwa umsumbuao Mume wangu,🥵 Dakta Eze alituambia majibu yaliyotuvunja mioyo yetu na kutukatisha tamaa ya kufurahia maisha ya ndoa yetu iliyodumu Kwa zaidi ya Miaka kumi.
Majibu ya vipimo yalionesha Mume wangu alisumbuliwa na ugonjwa wa KANSA ya moyo🖤 iliyofikia stage ya kukatisha tamaa😓. Kwa kifupi Dakta Eze alituambia siku za kuishi Mume wangu ni chache na zinahesabika. Tulibubujikwa machozi😭
"Please Dakta🩺 tunaomba utusaidie" Shania mie nilimsihi Dakta.
"Anapaswa kupewa kitanda🛌 cha Hospitali ili huduma zote ziwe karibu."Dakta Eze alitoa ushauri. Mie na Omario tulikumbwa na sura za majonzi na uchungu wa ndimu.😖😩
"Shania tumsikilize Dakta. Wacha nilalae Hospitali🏥 maana Dakta amesema bado mwezi mmoja tu Mola atanichukua. Ugonjwa wa Kansa hautibiki.💉💊" Mume wangu alikataa tamaa.
"Usiseme hivyo Omario, ya Mola mengi na Mola anaweza tenda miujiza kumbuka ninakupenda sana Mume wangu ninakupenda, nisingelipenda kukuacha mpweke." Nilimfariji Huba wangu.💞
"Ninakupenda sana mke wangu Shania, ombi langu Moja ninaomba uwe unakuja kunitembelea Hospital mara zote nipate faraja maana uwepo wako itakua faraja tosha kwangu."Omario alinisihi
"Kila siku nitakuja na Dua 📿🛐🤲 njema nitakuombea." Nilimtia moyo.
"Usiache tafadhali." Mume wangu alirengwa chozi akachukuliwa na kupelekwa Wadi ya kipekee kufika huko akalazwa Ili huduma muhimu zianze kutolewa. Basi ikawa kila siku ni lazima niende Ocean Road Hospital Kumtazama Mume wangu, kumwandalia chakula, 🥣maji 🚰 na huduma nyingine muhimu. Hata siku Moja sikuacha kumuomba Dua na maombi Mola wangu amponye Mume wangu.
Kila nilipoenda kumtazama Omario nilimkuta akiwa katika hali ya kudhoofu na kulalamika😣😖 maumivu makali ya moyo na kila siku alionesha darili za kukata tamaa akiamini kuwa kifo💀 chake kipo karibu.
Siku Moja nikiwa ninarejea nyumbani kichwani nimevurugwa kwa wingi wa Dua, maombi na machozi vilivyoandamana nami kwa jinsi ninavyompenda Omario acheni kupenda kuitwe kupenda yaani siwezi kutoa mfano.
Makusudi tu nikajiketisha pembeni ya Benchi moja lililo ndani ya Bustani ile ya Ocean Road bado Dua zilinitoka moyoni nikimuomba Mola 📿ashushe muujiza ili nimpendaye apone.
"Samahani Sister waweza kuniruhusu niketi pamoja na wewe" NIliyafumbua macho yangu nikayafuta machozi yaliyokua yakimwagika mithiri ya Bomba la maji 🚰⛲
"Keti dada, keti usijari." Nilimkaribisha yule dada ambaye Kwa kumtazama mavazi yake mara Moja nilijua ni Nesi wa ile hospital.👩⚕️
"Pole kuuguza Dadangu na pia punguza kulia sababu machozi yako yanakukondesha." Yule dada mgeni machoni kwangu alinifariji, hakika aliyaona machozi yanikondeshayo.
"Asante Dadangu."🙏😊 Niliitikia faraja yake ingawaje sikupendezwa kuendeleza maongezi naye.
"Niite Rozana, mie ni Nesi katika Hospitali hii dada Kuna jambo naomba nikushauri ikiwezekana ulifanyie kazi haraka sana uwezavyo." Nilimtazama Rozana na aliyeendelea kunena
"Tafadhali funga kamera🎦 ndani ya chumba alalacho Mumeo, Kuna jambo ambalo sio zuri utakuja kuligundua." Alinishitua yule Binti.
"Tatizo Nini ndogo wangu?" 🥺 Nilimkazia macho lakini kama vile alianza kuogopa akamka pale alipoketi hima hima akaondoka kisha akatamka:
"Mumeo sio mgonjwa lakini anajifanya ni mgonjwa, utakapokuja kuligundua jambo lifanyikalo ndani ya chumba alicholazwa Mumeo dada utakuja kunishukuru." Rozana akatoweka.
"Mmh! Niliguna."
"Jambo gani?" Nilihojihoji.
"Huyu Nesi vipi? Ataanzaje kusema Mume wangu sio mgonjwa. Ametumwa huyu Nesi sio haba.👺 Niliwaza na kuchoka kuketi pale Benchini. Nikachukua gari yangu na kuelekea nyumbani Oysterbay. Hakika nilivurugwa.
Usiku wa siku ile🌆 mawazo yalinisumbua, niliwaza juu ya yule Nesi, moyoni Nikajisemea ana maanisha Nini kusema Mume wangu sio mgonjwa? Kwanini aseme Mume wangu sio mgonjwa? Jamani. Haraka nikaingia online nikatazama aina za kamera mbalimbali pamoja na bei zake, nilihitaji kuipata kamera ya uhakika nilipoipata kamera niitafutayo nikaagiza kesho niletewe.
Mtoa huduma(Deriver) alifanya hima kuniletea asubuhi ingawaje mzigo ule ilikua ni mzigo wa bei gharama. Jioni ilipowasili nilielekea Ocean Road Hospital kumuona Mume wangu Mpenzi, nilimkuta amepooza, amelala, Hana furaha na amani. Nikamtaka pole kisha tukaongea mengi na machache pia baada ya maongezi kidogo aliniomba nimsindikize aelekee choo,🚽 nilimsindikiza na kumuacha anaendelea kujisaidia.
Nikatoka chooni na kwenda ndani ya chumba alicholazwa nikayaona Maua 🌼🌺yamepambwa, hapo . Nilipaona ndo' pazuri kuseti kamera ambayo niliiseti na kuunganisha na simu yangu iliyoonesha mandhari ya chumba kizima haswa pale alipolala Mume wangu Omario.
Omario alipotoka choo kama kawaida alilala kitandani Kwa shida mno. Nilimsaidia kupanda juu ya kitanda nikayasikilizia maumivu yake. Mtima wangu ulilia jamani ulilia kwa jinsi nilivyomwona nimpendaye akiugulia maumivu ya kansa ya moyo. Mpendwa wangu niliyelala naye, niliyecheka naye na kutaniana leo hii ananiambia anaumwa ugonjwa wa kufa!? Oh! Nililia kimya kimya moyoni.
......................….
Baada ya kupata chakula Cha usiku nilijiandalia kahawa na vipande vya kashata taratibu niliinywa na kuvitafuna vile vipande pembeni yangu niliiwasha Laptop 💻 niliyounganisha pamoja na USB kutoka kwenye kamera iliyopo kwenye simu. Chumba cha Hospitali kilionekana vizuri, Omario alikua amelala kama nilivyomwacha hapo awali. Dakika zilikatika na masaa yakayoyoma mwenzenu nilianza kujutia tendo la kumuamini Nesi Rozana. Niliona kama upuuzi na upumbavu kumchunguza Mume wangu mgonjwa. Kwani Kuna faida 💰 gani ambayo ningeliipata baada ya kumchunguza Mume wangu?
Lakini ghafra yapata saa sita usiku maajabu niliyoyaona, eeh!🥺😔 Nashindwa sijui nianzie wapi kueleza.. Aliingia mwanamke mrembo kupita maelezo, mrembo zaidi ya Miss World 🗺️Venezuela. Alikua ni mrembo aliyevaa wigi jeusi lililokatwa likaishia masikioni💇♀️ . Uso wake wa Duara, ☺️macho makubwa 👁️ lips zimekoozwa👄 rangi nyekundu, ana ngozi rangi ya maji ya kunde mrefu kama Twiga🦒, mwembamba wa umbo la nyigu.
Mrembo yule alivalia koti rangi ya Kaki na suruali rangi nyeusi iliyombana kisawasawa. Chini ya miguu alitupia viatu virefu vya mchuchumio👠 Tena alibeba mkoba👜 wa bei gharama, mkononi aliishikila simu Bomba 🤳 ambayo hata mie sina. Mume wangu Erick alipomuona tu ni kama vile ugonjwa wake ulimtoweka akatamka pale kitandani Kwa furaha kisha akampokea yule Binti mzuri kama midoli ya kichina. Wawili wale wakaanza kunyonyana ndimi 👨❤️💋👨na kupapasana mipapaso isiyokomabaada ya hapo nilimwona Mume wangu akaelekea kufunga chumba alicholazwa.
Bada ya kuufungua mlango yule Binti akamsogelea Mume wangu na kuanza kumvua nguo Moja baada ya nyingine na yule Binti akafanya vivyo hivyo akamvua yule Binti nguo zake zote wakangukia juu ya kitanda cha Hospitali. Yaani kama notaendelea kuwasimulia kile nilichokiona kikifanywa ndani ya kile chumba jamani! Moyo wangu utaniuma sana mana nilianza kupata Presha na pumzi zilinitoka juu juu.
Nilitamani kuizima ile laptop lakini ndugu zangu nilihitaji kujua mwisho wake ni nini? Maana walipomaliza kufanya zinaa hospitalini
Wakavaa nguo na kuketi kitandani na kuanza kuongea bahati mbaya hakuna neno nililolisikia sababu kamera yangu ilikua haitoi sauti.
............
Siku ile sikupata hata lepe la usingizi badala ya kulia juu ya ugonjwa unamsumbua Mume wangu Omario Sasa nikaanza kulia juu ya usaliti na udanganyifu wa Mume wangu. Jamani! Kila niiendapo Hospitali nilikuta mtu anaugua Hana mbele Wala nyuma alafu ajapo yule Malaya mrembo mwanaume anachangamka, anachek a Cheka, anaruka ruka na kufanya ngono Hospitalini. Hapana jamani Kuna kitu pale. Niliwaza.
Siku iliyofuata nilimtembelea Omario Mume wangu bila kuonesha darili za kuzigundua ule mchezo wake mchafu, nilijinyemyekeza kwake na nikajifanya no mwingi wa huzuni na masikitiko. Nikamsaidia huduma ndogo ndogo na pia nikawa faraja kwake Bada ya hayo yote nilimuaga ninarudi nyumbani.
"Ugu pole my love 😘 Mola akutangulie." Nikatoka Hospitali. Nilivyo mjanja kwani nilirejea nyumbani? Aka! Nilitaka Leo pia nipate ushahidi wa kile wanachonena na kukitenda. Nikajibanza pembeni ya moja ya kona ya ile Hospitali ili nijaribu bahati yangu ya kumuona Mrembo amzuzuaye Mume wangu mgonjwa anayeponan ghafra baada ya kumuona huyo Mrembo.
Mungu ni pendo nilimuona yule Binti, Aliingia chumba alicholazwa Mume wangu nikafanya hima kujibanza pembeni ya mlango wa kile chumba. Nikaiwasha simu yangu sehemu inayorekodi Audio, kisha nikamega sikio nisikie nini wanachozungumza. Safari hii hawakufanya zinaa bali walipigana mabusu 🥰 pale kitandani pale Mume wangu amejaa furaha na tabasamu.
"Afadhali umekuja Daring Veronica" Nilisikia sauti ya mume wangu imejaa Afya tofauti na siku zote nilizomtembelea pale 🏥 Hospitali.
"Nilikumiss sana Daring, leo nimetoka kwa Mwanasheria ⚖️ kuchukua Documentary ambazo zitatusaidia kuhamisha yale Mamilioni ya pesa zilizopo Bank 🏧 mara baada ya kukamilisha hatua zote za kufake kifo ." Uwii! Nilishituka zile kauri.
"Waoo! 🎊Mke wangu" Mume wangu alianza kuruka ruka juu ya kile kitanda cha wagonjwa hakika Sasa alikwishaanza kupona mara baada ya kumuona yule mrembo
"Shania alikuja muda si mrefu, yaani ungelimuona ungelimuonea huruma, amekonda kwa kilio na uchungu." Mume wangu aliongea akipekua pekua zile Documentary
"Achana nae, si unanipenda Mimi? Kwahiyo kuanzia Leo Mimi ndiye Veronica Mkeo. Watakaposikia kuwa umekufa sie tutoroke Tanzania twende kuishi Marekani tukastarehe Kwa kutumia pesa nyingi tutakazo zichukua Bank." Veronica aliongea na kamoyo kangu kalinidunda ndu ndu ndu ndu. Yaani mimi na Mume wangu Omario tumefanya kazi Kwa zaidi ya Miaka kumi kila pesa tuliyoichuma kutokana na kazi zetu tuliiweka kwenye Account ya pamoja (Joint Account) Alafu Leo nisikie ati Mume wangu akiisha feki kifo chake pesa zote atazichukua akatanue Majuu pamoja na huyu Malaya wake. Hapana, haiwezekani.
"Veronica kumbuka bila msaada wa Dakta Eze kamwe tusingelifanikiwa kudanganya kwamba nimepatwa na Maradhi ya Kansa. Tukiishafanikiwa kuzichota pesa zetu tutenge fungu Kwa ajili ya Dakta Eze. "
"Ninakubaliana nawe Daring, si amesema bado siku tatu utakufa kifo bandia?" Veronica alimuuliza Omario.
"Yes my Daring. Unajua ninafurahia kukujua, mapenzi unayaweza, mapenzi unayajua" Omario Alimsifia yule mrembo.
"Asante Daring. Nimekuletea chakula kizuri na kitamu ule ushibe sio kila siku Mkeo akunyweshe uji🫕 utadhani wewe ni katoto kachanga" 👩🍼Veronica alimtania Omario. Wawili wale wakaagua kiicheko cha sauti kuu.😹😹
Nilikwishapata ushahidi sio wa video tu Bali pia wa Audio🔊, nilikwishaijua nia ya mume wangu Omario pamoja na yule mrembo. Kumbe Mume wangu anataka kuniacha Ili amuoe yule Malaya? Kumbe Mume wangu pamoja na Veronica wameshirikiana na Dakta Eze kufake ugonjwa na Sasa wananelekea kufake vifo? Kumbe Omario pamoja na Kimada wake Veronica wamepanga njama ya kuzichota pesa zote nilizozichuma pamoja na Omario Mume wangu baada ya kuhangaikia kufanya kazi nzito zinazochosha Kwa zaidi ya Miaka kumi tangu niingie ndoani? Loh! Ama kweli kilulacho kipo nguoni mwako, kikuuwacho kipo nguoni mwako. Akufukuzaye akwambii toka. Nilijuta.
"Ok. Tuone Sasa wa kwanza atakua wa mwisho na wa mwisho atakua wa kwanza. Nilirejea Oysterbay nyumbani baada ya kuridhika na upuuzi alionifanyia Mume wangu Omario. Yaani mie kila siku ninafanya Dua, ninamwaga chozi ninajinyima mambo mazuri na kujikondesha Bure wakati huo huo mwenzangu anapanga njama za kunihujumu. Tutaona Sasa, nitamkomesha Hadi ajambe cheche.
############
Ziiip'...... Ziiip'.... Ziiip' 📞Nilimpiga simu Bibi Mama Mkwe na Babu Baba mkwe nikawapa taarifa kesho asubuhi wawepo ndani ya jengo la hospitali ya Ocean Road tufanye Dua nzito ya kumuombea na kumuaga mpendwa wetu maana siku zake za kuishi Ulimwenguni zimefika tamati.
Zuuuuu zuuuuu ziiii ☎️Niliwpigia simu ndugu, jamaa na marafiki, majirani na wafanyakazi wenziwe.'Jamani naomba tujikusanye, tuje Ocean 🌊 Road Hospitali tufanye Dua na maombi, tumuombee ndugu, jamaa, rafiki, jirani na mwenzetu mpendwa Omario siku zake za kuliona Jua🌄 zimekaribia kukoma Muda sio rafiki Baba Mungu atamwita.' ikawa hivyo Tena Wakwe zangu, nduguze Erick, jamaaaze, marafikize na wafanyakazi wenza🧑🤝🧑 wakajikusanya na kujazana pale Ocean Road Hospital wamejaa machozi , vilio na sononeko la moyo.
Sikuwasahau mabwana POLISI. 'Kaeni chonjo mambo yashaiva tutajichukulia Sheria mkononi, tutaua jitu huku na jitu litazima tu, lipende lisipende, litake lisitake Bullshit!'👿 POLISI nao wakaja wametinga mavazi ya kiraia bahati nzuri Veronica naye akaja ingawaje hajulikani pale lakini alikuja kujulikana bila kupenda.
""""""""""""""""'"'"""
"Wapendwa Wakwe zangu, ndugu jamaa na marafik, watumishi na majirani asanteni Kwa kuja."✌️ Nilianza kushukuru wakati huo Omario wetu alifeki kujifanya yupo hoi taabani, hawezi Wala hajiwezi tena hajitambui.
"Lengo la kuitana hapa ni juu ya maombi, Dua njema na kumuombea rehema mpendwa wetu Omario maana hatujui saa ambayo Mola wake atampumzisha, kwahiyo tukaze kusali." 🛐Niliendelea kunena.
"Lakini kabla hatujafungua Ibada na maombi ya kumuombea mpendwa wetu ningelipenda kila mmoja aliyepo hapa aitazame hii tape video na kuisikiliza hii tape audio ndipo Kwa moyo wenye umoja tuanze kufanya maombi, kumuombea mpendwa wetu." Watu wote waliojazana ndani na nje ya kile chumba walinitazama niliiweka ile tape video📺 kwenye deki ya Televisheni iliyoukutani kwenye kile chumba alicholazwa Omario.
"Shania unataka kufanya Nini!?" 😶Mgonjwa wetu aliyekua hoi ashindwe kutamka sasa alitamka. Sikumjibu. Video ikaanza kutazamwa na watu wazima ndani ya kile chumba, ilikua ni aibu na fedhea lakini SIKUJALI na sikukomea hapo nilipohakikisha kuwa ile video imeleta taharuki nikachomeka DVD 📀 niliyorekodi sauti za yale mazungumzo kati ya Veronica na Mume wangu Omario.
Jamani! Jamani almanusura Bibi mama Mkwe na Babu Baba mkwe wazirai na kuzima kimoja' hakuna mtu ambaye hakusikia udanganyifu na mipango ile michafu.
"Omario umetufedhehesha na kutuaibisha, yaani sie twajua mwanetu ni mgonjwa tunahangaika huku na kule kukopa mapesa ya matibabu na madawa lakini kumbe wewe unapanga mipango michafu na huyo Veronica Malaya wako." Bibi Mama mkwe aliongea na machozi akabubujikwa.😢
"Nisamehewe Mama, naomba nisamehewe." Mgonjwa aliyekua hoi taabani pale kitandani safari hii akadamka na kupiga goti 🧎♂️Aliomba msamaha.fedhea ilimkamata. Ikawa zamu yake kulia Kwa uchungu
"Sintakusamehe Omario Hadi naingia kaburini. "Bibi mama Mkwe alitoa kiapo. Nyomi la watu waliokusanyika pale lilianza kupiga kelele na majadiliano mazito. Wengi walimlaumu sana Omario kutaka kifo bandia. Polisi waliingia ndani ya ile Hospitali kuanza kumtafuta Dakta Eze. Dakta alikamatwa Kwa kosa la utovu wa madili kazini. Yawezekana vipi akubali kumsaidia mtu afeki kifo chake. Pesa na rushwa ndogondogo zilimponza yeye pamoja na Mume wangu Omario wakapandishwa ndani ya Difenda la Polisi.
Veronica alipoona na kusikia mambo tayari yashaharibika mrembo yule akavua vile viatu vyake vya mchuchumio 👠 alichomoka na kukimbia kama Roketi. Police hawakumuacha walimkimbiza Hadi pale walipomwona anatoka nje ya geti la Hospitali. Ghafla polisi walikuja kusikia sauti kuu ya kilio, Gari iliyokua inaongoza msafara wa Waziri mkuu kuelekea. Ikulu ilimgonga Vero akadondoka chini na kuharibu ule msafara wa Waziri mkuu. Kwani aliachwa afie pale? Never. Alisombwa, pingu🔗mkononi, miguu wake mmoja ulikuwa regerege ushavunjika. Machozi na majuto yalimwandama.
"""""""”"""""""”""""
Wiki Moja baadae nilirejea Hospitali ya Ocean Road, hapo tayari nishaomba Taraka yangu Mahakamani. Sikuona umuhimu au uhitaji wa kuishi na mwanaume mpumbavu na mjinga msaliti. Mie Shania nikajiketisha kwenye bustani ya Maua pale kwenye Bench nililofuatwa na Nesi Rozana. Nesi aliyenisaidia kuwatumbua wale wahujumu watatu: Dakta Eze, Omario Mume wangu na Malaya wake Veronica.
Niliketi pale nikiwa na matumaini ya kumuona Nesi Rozana, pembeni yangu nilikua na Box lenye Zawadi ya gauni 👗zuri nililoagiza kutoka Venezuela🇻🇪. Kama zari vile Rozana alitokeza, nikamkimbilia,🏃♀️ nikamkumbata🫂🤗 na kumbusu viganja vya mikono yake, 😽ishara ya upendo. Akatabasamu na kufurahia.
"Asante sana Nesi, Asante umeniokoa." Nilimshukuru Rozana.
"Siku nilipowafumania wakifanya mapenzi hawakuniona lakini nilijua mambo hayapo sawa." Rozana aliniambia
"Umenifaa sana Nesi, umenifanya niujue moyo wa Mume wangu, kumbe alikua na siri nzito ya kipumbavu. Wacha akaozee Jela na Taraka nishaiomba Mali na pesa tutagawana pasu kwa pasu" Nilimwambia Nesi.
"Pole pia maana alikuweka katika nyakati ngumu za maombi na machozi" Nesi alinifariji.
"Mie nsha' poa." Nikachukua Box zuri lilipambwa Uaridi 🌷 nikamkabidhi Zawadi yake Alipoifungua almanusura macho yamtoke 👀na kumdondoka, aliipenda sana ile Zawadi. Rozana akanikumbatia na kunibusu shavu langu 😙 nikatabasmu.😇☺️
**********
TCHAO 👋👋
No comments:
Post a Comment