Sunday, November 10, 2024

DARUBINI YA UMBEA.

 

DARUBINI YANGU ILIPELEKEA NDOA YA JIRANI KUVUNJIKA. 


      Niite Shadya Momama mie ni aina ya wadada special tunaopendwa na ndugu, jamaa, marafiki special yaani ninajiona muhimu Japokuwa mie sio keki. Teh teh teh πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜˜. Dada zangu wawili Sia na na Sella anafanya kazi nje ya taifa, shuhuli za hayo Mabenki ya Dunia wakati kaka yangu Salehe yeye ni Mwanasheria mkuu huko Marekani kwaiyo mie Shadya ninajiona special ingawaje sio keki kivile. 

         Ni mtu ambaye kile ninachokitaka lazima niagize online na kuletewa kinaletwa si chini ya dakika tano au kumi. Usishangae Shadya Momama kuagiza tunda la Apple online, chumvi, majani, maji au sukari vyote naletewa nikiwa ndani nimejiketisha sofani nacheki Tamthiliya au kuchezea game ndani a Simu yangu

 Nimeyachagua maisha haya.,kwanza nimekosea nini au nimekosea wapi? Ikiwa watu wanachagua maisha ya kushinda Bar au Pub, watu  wanashinda Beach au kumbi za dance, watu wanatravel kila kona ya Dunia mie Shadya ninayetumiwa mahella kutoka kwa kaka pamoja na dada zangu nipungukiwe nini? Wacha last born ni enjoy life kwanza maisha yenyewe mafuuupi  kama kiuno cha nyigu. 

        Basi mie Shadya Momama nalikuwa na Darubini yangu machoni, pembeni Kuna kijimeza nimejimiminia wine ya Zabibu kwenye Bilauri special nimetulia juu ya Apartment yangu nyumba yenye kila kitu ndani yaani horofa ya nne huku Oysterbay. Nikachungulia upande wa kushoto Darubini ikanionesha Apartment ya Mzee Jose ambaye kwangu namwita Babu J. Ni Mzee mwenye kadirio la miaka mia πŸ’― Kala munyu hadi kaanza kuukataa. 

Uzuri wa babu J yeye yupo kama mie  kwa starehe ya kujiketisha ndani kila siku yeye atapiga kinandache kinachotoa Muziki mtamu mwororo hadi mie kupata raha na hisia za kwenda kumwambia anifunde kubinyabinya keyboard ya kinandache. 

Darubini yangu ikanivuta upande wa kulia huku nikamuona Bwana John kijana mmoja mzuri mwenye kadirio la miaka ishirini na saba  akiwa jikoni akaangiza Kuku wa mrija pembeni yake nilimwona Sarai mkewe akichambua chambua Mchele na kupima  pima spices mbali mbali kutoka Zenji kwa haraka nilijua leo Biriani litashitua mtaa. 

          Waoo! Kawivu mara moja moja unisumbua niionapo hii Couple ilivyochangamka yaani kila siku jioni wao ukaangiza vinono vilojaa mahaba, afya na pochopocho. Nikapiga Funda moja la wine yangu ya Zabibu Kisha nikaichukua Dayali ya umbea nikaandika andika umbea niliouona kwa Babu Jose na nyumbani kwa Bwana John

***************

          Imekua kama mazoea mie Shadya Momama kuketi  dirishani kujimiminia Zabibu yangu na kuyasikiliza mapigiti ya Muziki wa Babu J ama kunusanusa pishi la Bwana John na mkewe Sarai nisichoke kuandika andika Dayalini. 

        Basi mie SHADYA MOMAMA SIKU MOJA NIKIWA Nimeketi Dirishani wine yangu ya Zabibu pembeni nikazifurahia zile DO LE MI FA SO LA SI Do muziki kutoka kwa Babu J, nilipoligeuza jicho langu kodo kuitazama Apartment ya bwana Jose nilishituka kuliona pande la Jibaba likimvunjavunja samaki, likimparura na kumuoka kwenye Eaflaya baada ya hapo nikaliona likiandaa Unga na kando la Unga, sijui yalikua ni maandalizi ya pishi la Pizza? Mmh! Umbea umekosa adabu. 

Sarai aliingia Jikoni amejaa tabasamu muda huo huo baada ya kuingia Jikoni akaipitisha mikono yake kwenye kiuno ch lile Jibaba lenye mikono na mabavu kama mwana mieleka wa zamani, John Cena. Midomo yao ikakutana wakanyonyeshana NDIMI. 

          Jesu! Kidogo Darubini yangu inipokonyoke nashukuru Mungu niliikaza  isinipokonyoke. 

       'Sarai anachepuka!' Wazo Liliniingia. 

        'Miaka na miaka sijawai kumuona huyu mbaba mwenye sura pana kama kando la Pizza mikono migumu yenye vidole virefu kama miguu ya pwezza.... Mh! Niliguna nikaishiwa pozi. 

 Nikarudia tena kuitazama ile video ya bure safari hii nisingeliweza kuvumilia kuiona ile sinema maana Sarai alipandishwa juu ya meza pale Jikoni akavuliwa kila alichovaa na lile Jibaba likavua kila lilichovaa mambo waliyoyatenda nilificha macho yangu nikakimbilia bafu kujibwaga Jakuzini nikaoshe macho yangu yasiuone tena ule umbea

****************

Jua lilipozama  nilitoka chumbani kwangu nilikojilaza takribani masaa saba tangu tukio lile la Sarai kuchepuka kwa kweli sikupenda Ila acheni tu umbea uchemke. Kama kawaida nilichungulia kushoto  kumuangalia babau Jose nisimuone yamkini alienda lala. Nikaigeuza darubini yangu upande wa kulia huku nikakutana na bwana Jose  kaingia Jikoni apika Nyama na Ugali Sarai mkewe alikua akikosha vyombo kwenye Sink sura yake imejaa furaha na tabasamu. 

Jamani mambo anayoyafanya Sarai sio mazuri ni Infidelity. Mchana kagonoka na Jibaba lenye mabavu na kifua kizito kama jiwe alafu jioni ajifanya yupo Beneti na Bwana John' Mtima ulininong'oneza. 

       'NDOA HAIJENGWI KWA TOFALI INAJENGWA KWA UAMINIFU NA UPENDO' NILIWAZA NIKIWATAZAMA WALE WANANDOA WALIOMALIZA SHUHULI YA KUPIKA NA KUPAKUA WAKAINGIA MEZANI KUTUPIA MAWE PANGONI. 


********

IKAWA SASA NI KAMCHEZO KATAMU KWA SARAI NA LILE JIBABA. JOHN AKIONDOKA kwenda kazini Sarai alilipigia simu lile Jibaba lenye kifua cha mazoezi  wakapika na kupakua bila kusahau kufanya ngono tendo lililonikera mie Shadya Momama  maana tabia ni mazoea na mazoea hayana rangi. Moyoni nilikereka na kutapika nikatamani lakini kutapika kwangu kusingelimsaidia BwanaJohn niliyemuonea huruma. 

      Siku ya nne tangu niliona lile Jibaba ilikua ni Jumamosi nzuri siku hii Sarai uchukua Gari yake na kuenda kariakoo  kuchaguachagua mbogamboga na mahitaji mengine ya Jikoni. Siku ile nijuavyo mie Bwna John angelishinda nyumbani kupuguta deki Apartment yao, kufua nguo kwa kutumia mashine maalumu ya Kufulia  yaani Washing mashine and Laundry Kisha mchana wa siku ile angeliingia Jikoni kuandaa Lunch. 

       Babu Jose angeliendelea kulikunguta lile dude lake linalotoa Muzik mtam masikioni, mtam kumponya aumwaye kitandani, mtamu kupooza hasira hasara, mtamu kutuliza stress na makwazo au matatizo ya saikolojia, mtamu kwangu mie mpweke nipendaye raha na utulivu

     'Nifanye nini ili Bwana John ajue kwamba mkewe sio  mwaminifu? "Niliwaza. 

     'Mh! Nikamwambie? Mie nisiye na ndugu au urafiki naye atanielewa kweli? Njia panda'  Nilijikatisha tamaa. 

        'Oh!' taa ya ubongo iliwaka. 

    ' Nitaandika ujumbe, ujumbe kumtahadarisha juu ya mwenendo wa mkewe. ' Nililiona lile ndio wazo bora nikazama Library kwangu na kutandaza karatasi karamu na Bahasha. Taratibu nikaandika na kufuta, nikaandika na kufuta nikiwaza maskini nisijejiponza mwandiko. 

 JIRANI BWANA JOSE, SALAM. 

SIKUTEGEMEA KUKUANDIKIA HUU UJUMBE LAKINI IMENIBIDI. TAFADHALI MCHUNGUZE MKEO HASWA HASWA ULE MUDA UNAOTOKA NA KWENDA KAZINI. 

         MIMI KAMA JIRANI YAKO MWEMA SIJAPENDA MATENDO ANAYOYATENDA, SITAKI KUYASEMA NI MATENDO GANI LAKINI UNA HAKI YA KUMCHUNGUZA HADI UPATE VITHIBITISHO KISHA UFANYE MAAMUZI YALIYO SAHIHI. 

 NDIMI JIRANI MBEA

SHADYA MOMAMA

__________
 TAFADHALI UKIISHA SOMA HUU UJUMBE UPIGE KIBERITI MKEO ASIJESHITUKA IKAWA BAADA YA KISA MKASA. 

 Nilipomaliza kuandika ule ujumbe nikachukua kile kipande cha barua na kukiweka ndani ya bahasha ya kaki  nikaelekea pale pale Dirishani nikiburudikia Muziki wa Babu Jose

      'Sasa nishauandika ujumbe hatua inayofuata ni kuupeleka, oh! My God nitaupelekaje? Sina mazoea na Bwana John, atauelewa huu ujumbe? "Niliwaza

     'Wangelikuwepo ndege waruke ili niwatume' Niliwaza mambo ya kufikirika. 

      'Any way nishayavulia nguo Budi niyakoge' nikafanya kuteremka ngazi za Horofa yangu ya nne nikashuka chini, Jua na mwaga wa Dunia kwangu ilikua kama ni vitu vigeni maana ni miaka mingi nimejichimbia juu Horofani nisitake kuizunguka Dunia. 

 Nikatembea kuelekea upande wa kulia eneo ilipo Horofa na Apartment y Bwana John

     Nilipofika nikapanda ngazi tena kwa tahadhari asijitokeze mkewe John Bi. Sarai akanifumania nimesimama na mumewe. Nikafika  kwenye Apartment yao nikataka kubisha hodi lakini mikono yangu ilikua mizito  kutenda kile kitendo  yote tisa kumi nikakiona kitufe kinachotoa sauti ndani kudhihirisha Kuna mgeni nje ya nyumba. 

        Hazikupita dakika tano mlango ulifunguliwa nikashukuru Mungu kumuona Bwana John, bila kumsabahi nilimkbidhi ule ujumbe bahashani haraka haraka Nikaigeuza njia na kutoweka yeye binafsi akinishangaa. Nilipofika juu ya Apartment yangu moyo ulikua wanidunda ovyo jasho lanichuruza hadi makwapani. Jaman mwanadada muoga mie ah! Embu ngoja nikajibwage dimbwini nikoge kuondoka hofu yangu. 

*******

SIKU iliyofuata kama kawaida Babu Jose alipiga kinandache  Sarai alifurahia kuchepuka na lile Jibaba siku ya pili pia, moyoni nilianza kumlaumu Bwana John kwanini amejigeuza dume Suruali yaani anaoa lakini ajifanya kipofu ina maana kusoma  hajui na kuitazama picha hajui? Ah! Asinikere mie Shadya Momama

    SIKU ya tatu  nisiwaambie wajameni labda darubini yangu ndivyo itakayowaambia, maana kwa fumanizi lile hakika Bwana John lazima aje anishukuru. Zilipigwa, Zilipigwa, Zilipigwa wee! Mwenye nguvu alikua na nguvu zaidi na dhaifu alidhoofu vibaya. Vyombo vya Jikoni vilitoa muzik usio halali Muzik wa kushangilia na kuzomea yamkini kwa muda ule mfupi vyombo vilimchoka yule Jibaba aliyekuwa akimgonga Sarai sasa navyo vilipata raha ya kuligonga lile Jibaba  likaumuka na kuvimba mfano wa kando la maandazi yaliyozidi Amira. 

*****************
         Sarai akapewa TARAKA yake, TARAKA ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa ile siku alipofungasha na kubeba virago vyake Darubini ya umbea nilimuona analia kwa chungu. Jioni ya siku ile nikiwa nimetoka kukoga nikasikia kengere ya mlango wangu ikiita na kulia kwa huruma  ya kufunguliwa, nikatoka hima kwenda kufungua. 

Jesu! Almanusura nidondoke, macho ya Bwana John yaligongana na macho yangu Bila salamu au kusema neno alinikabidhi Bahasha nyeupe yenye Ua la Rose🌹 Kisha akatoweka pasina kumtamka neno, 

        Mie nae nikiwa na kiherehere changu  nikaelekea Dirishani kwangu nikisikiliza Muziki mtamu kutoka kwa Babu J, nikaifungua ile Bahasha niliyokutana na viemoji vya tumoyo ❤️πŸ’–πŸ˜»πŸ’ na tumaua πŸŒΊπŸ’Kisha nikaisoma. 

MAMBO SHADYA 

ASANTE SANA KWA KUNIFUNGUA MACHO YALIYOFUNGWA NISIONE MABAYA YA MKE WANGU SARAI. NIMEPENDEZWA NA USHIRIKIANO WAKO MWEMA KWA JAMBO HILO NINAKUSHUKURU PIA NAOMBA JIONI YA LEO JIANDAE TUTOKE TUTAENDA LAMADA HOTELI, MSIMBAZI CENTER TUKAPATE DINNER. 

 Ni MIMI JIRANI MPENZI

 JOHNπŸ’Œ

   Uwii! Kamoyo kakanidunda dundapo

  Ndu! Ndu! Ndu! Ndu! 





No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...