NILIMLAZIMISHA MWANANGU👱 AKASOMEE📚📖 SHERIA, ⚖️ALIGOMA AKIDAI ATI ANAPENDA MUZIC🎶🎧🎸, NILIPOMFUKUZA🏃💨 NILILETEWA TAARIFA ZILIZOUCHOMA MTIMA WANGU❤️🔥.
"Nasema hivi Jack uende Chuo 🎓 ukasomee Sheria, ⚖️ili uje kuwa Mwanasheria🧑⚖️ mkubwa Duniani kama mimi baba yako na mjomba wako Deo" Niliongea kwa hasira nzito pale sebuleni, jioni ya leo tukiwa tupo mezani tunapata Dinner:🍲🥚🥗 Mimi Baba Jack, mama Jack na Jack mwanangu one and only, wa pekee. Aliyejiandaa wiki ijayo kwenda Chuo.
"Baba nimesema sitaki kusomea Sheria, masomo ya Sheria hayapo moyoni mwangu, sintaweza tena sitaki kuhukumu watu." Tineja wetu aliongea, uso wake wa ujana ulipambwa kwa hasira, tundevu twake tulianza kukikumbatia kidevu chake, ngozi yake safi yenye rangi ya chocolate na uzuri haikua na chunusi usoni sema mwanangu hakua na Hatia angali bado kijana mdogo.
"Kasomee Sheria mwanangu, ukisomea Sheria utakuja kuwa tajiri💰🪙🤑 mwenye heshima ndani ya jamii." Mama yake Jack aliunga mkono kauri yangu.
"Baba na mama mimi haja yangu ni kufanya Muziki🎸🎷🥁 kwasababu Muziki upo ndani ya damu yangu hiyo ndivyo kazi itakayonipa heshima na furaha ya maisha yangu." Jack aliongea akimaanisha.
"Upuuzi huo hatuutaki😡, unataka kutuaibisha mbele ya jamaa, ndugu na marafiki🧑🤝🧑🤼 tuonekane tumekulea vibaya. Hauoni aibu kuonekakana kwenye Televisheni na video ukiwapapasa papasa na kuwachezea wanawake walio uchi,👯 ukinywa vileo vikali🍻🍺🍾 na kutumia dawa za kulevya💊💉." Nilimkaripia Jack ambaye aliacha kula akanuna😠🤢 kwa hasira.
"Baba ninaomba uniruhusu nifanye kile ambacho moyo💖 wangu unakitamani. Ninahitaji pia sapoti ya pesa, mali na faraja. Ili nitimize ndoto na matamanio yangu." Mwanangu Jack aliomba.
"Siwezi kutoa sapoti yangu kwenye mambo ya Dunia, mambo machafu ya kumchukiza Mungu. Ukikubali kusomea Sheria nipo tayari kuuza. Nyumba yetu, magari yetu na kila kitu tulichonacho."Nililishindilia nyundo wazo langu.
"Hapana baba siwezi kwenda kusomea jambo ambalo halipo moyoni
Mwangu." Kijana wangu mwenye umri wa miaka 21 alilitilia mkazo wazo lake.
"Kama hautaki kuheshimu mawazo yetu naomba Jack uondoke nyumbani kwangu nenda ukaishi na ukuungane na hao hao chokoraa wavuta mabangi🚬 Wenzio wanaopenda Muziki😵💫🥴😓" Nilimkaripia akasimama🧍pale chakulani na kuelekea chumbani kwake."
"Baba Jack umefanya nini? Kwanini unamfukuza mtoto? 🙂↕️Ungetumia busara kumtuliza sio matumizi ya hasira zenye hasara" Mama Jack aliongea akasimama pale alipoketi haraka akakimbilia chumbani kwa mwanetu Jack ambaye tayari alikua amefungasha virago vyake akatoka chumbani tayari kuondoka.🎒
"Jack mwanangu, Jack tafadhali usifanye maamuzi mabaya yenye hasira. Tuliza mtima wako na kuketi chini tuzungumze" 🙏Mke wangu Mama Jack alimbembeleza mwanangu Jack.
"Hapana mama, Baba amenifukuza wacha niondoke ipo siku atakuja kunishangaa nitakavyobadilika na kuwa mtu mkubwa Duniani." ✨Jack Alimwambia mamaye mie niliona ni upuuzi na ujanja wa kutaka kujaribu mambo ya Shetani👿
"My son Jack nisikilize mama yako tafadhali usiondoke, nitamshawishi baba yako hadi atanielewa" Mama Jack alimshawish Jack.
"Aondoke haraka kwenye nyumba yangu, 🏚️Aondoke akajifunze kiburi si maungwana." Nilibwata na kubwabwajuka kwa hasira. Jack mwanangu hakua na jinsi alilibeba begi lake la nguo akafanya kuondoka wakati huo mamaye alimwaga chozi🥹 hakika uchungu wa mwana aujuaye ni mama. 🧑💼
:::::::::::::::::::::::::::::: :
Basi baada ya mwanangu Jack kuondoka hakupata tena kuwasiliana na mimi📱, mama yake alikua akimpigia simu mara kwa mara lakini simu Iliita wee! 📲 Hadi Ikamdirect kwenye utumaji wa meseji. Bado tu mama Jack aliendelea kumpigia simu Jack ambaye hatukujua amekimbilia mji gani ndani ya Jiji la Dar es saalam. 🏙️ Baya zaidi hakupokea simu ya mama yake iliyoita tu ikatamani kupasuka.
""""""""""" "" "" "" "" "" "" "" "
Ilipita miaka mitatu hatukupata kusikia au kuwasiliana na Jack. Hatukupajua pahali anapoishi, hatukujua jinsi anavyoishi kijana wetu. Tulijiaminisha ipo siku Jack angelirejea nyumbani lakini wapi! Hakurejea.
Jumapili moja baada ya Sherehe ya Noeli na mwaka mpya Mama Jack akiwa mekoni anamkaangiza Turkey 🍗🦃simu yake ya mkononi Iliita.
"Hallow! 💬"
"Hallow ndugu! 🗨️" Mama Jack alilitikia.
"Ninaogea na Mama Jack Daniel?" upande wa mpigaji uliuliza.
"Ndio, wewe ni nani ndugu na una shida gani nikusaidie." 🤔Mke wangu aliuliza. Mie Baba Jack nalikua nikiteremka ngazi za Horofa ya juu kuja chini. 🪜
"Sisi ni mabwana Polisi 👮🚓 tuna taarifa mbaya kukuambia."
"Taarifa gani?!" Mama Jack aliuliza wakati huo mie naliekua nikiteremka ngazi za juu nalifika Mekoni🧑🍳 nikimsikiza mama Jack akiongea Simuni. 📞
"Jack mwanenu amekutwa amekufa kwa ajali ya gari🏎️ iliyomgonga hadi kupasuka ubongo wake." 🧠
"Jack ame..... 😨 Kufa."😞 Mama Jack alishituka.
"Ndio mama hivi tunavyoongea amepelekwa Amana Hospitali ⚕️kwa uchunguzi zaidi." Polisi alimjibu Mke wangu.
"Jesu!" 🧟Mke wangu akajibwaga sakafuni asielewe wala asiamini kile alichoambiwa.
"Nini Mama Jack?!" 🙄Nilimsogelea mama Jack pale sakafuni alipojibwaga.
"Jack Jamani😭 Jack mwanangu, Jack" 😢Aliongea machozi yakimbubujika. Haraka haraka nikaichukua simu aliyoidondosha chini kisha nikampigia simu Polisi aliyekuwa akiwasiliana naye.
"Hallow! Nitaamini vipi kama kweli mwanangu Jack hatunaye mtu huyo au labda mmekosea nambari." 🤐
"Hapana baba kwasababu tulipokua tunamsachi sachi marehemu tukaiona simu yake Kuna nambari ameisave kwa Jina 'Mamangu mpenzi💖" Tukaona sio mbaya kumpigia simu mama mpenzi. Lakini kama mna mashaka nendeni Amana Hospitali yamkini mtajihakikishia.
Sie tuliopandwa na presha na moyo 🙀❣️ kudondoka tukafanya hima hima🏃 kuelekea Amana Hospitali tujihakikishie kama ni Jack wetu au ni ndoto za majinamizi🦹. Tulipofika tukaoneshwa mwili wa marehemu tuliyeambiwa ni Jack mwanetu.
Toba! 🤯🤧🥹 Tulihisi Dunia imetuangukia. Jack alikua amelala amekufa, Jack wetu yule yule aliyeondoja nyumbani miaka 3 ilopita jaman leo hatunaye mtu huyo😢, amekufa jaman, ameondoka angali kijana ambaye hajaonja chumvi,🧈 asali,🍯 ndimu na sukari. Machozi, vilio na maombolezo vilitufuata.
*********
Tukamfanyia Jack wetu maziko, mamaye akilia na kunilaumu kwanini nilimfukuza Jack wetu mimi pia nililia na kujilaumu kumlazimisha Tineja wetu afuate kitu ambacho moyo wake ulikikataa. Hatimaye kuondoka nyumbani moja kwa moja na kuua mawasiliano.
Baada ya mazishi ⚰️ 🌁 mawazo Yakaanza kunilindimaa kichwani. Nilimuwaza mwanangu Jack, nilijilaumu nafsini kwanini nilimlazimisha kijana wangu afanye jambo ambao halipo mtimani mwake? Kwanini nilimfukuza? Jaman! Nikaangukia ulevini🍻🍶nikiamini ulevi ungelinisaidia kunipunguzia stress juu ya Jack wangu lakini wapi! Stress zilinizingua zaidi. 🤯
*****
Mke wangu Mama Jack akaanzisha utaratibu wa kwenda kila siku kaburini alipolala Jack, akifika huko Angelia wee🤧 angelisari 🤲📿✝️ na kuomboleza. Baada ya vilio na Sara mke wangu angelirejea nyumbani. Ikawa ndio utamaduni wake kila siku angelienda makaburi ya Kisutu kulia na kusali wakati huo huo mie Mzee Danieli nakimbilia Bar🍸🍾 kupiga moja moto🔥 moja baridi💧 nikiamini pombe itanipunguzia mawazo na stress.
Lakini siku moja Mama yake Jack alipoenda Kulitembelea kaburi ⚰️la mwanetu Jack Alishangaa sana kuikuta Midoli 🐻na wanasesere 🎎wakiwa wamewekwa katikati ya kaburi la Jack. Akaitoa na kuweka maua 🌺💐juu ya lile kaburi akalia hapo na kusali Kisha akaenda kuitupa ile Midoli.
SIKU ya pili pia Mke wangu alishangaa kuikuta Midoli na🐼🦖🦍 wanasesere tena safari hii aliikuta Midoli mkubwa zaidi ya ile ya awali. Alijiuliza moyoni Atakua ni nani huyu anifanyiaye yaya hizi? Kwanini ananifanyia hivi?' Hakupata jibu. Aliishia kuondoka zake taratibu na kuelekea nyumbani🏠
Siku ya tatu alifanya uamuzi wa kuwai 🌄 kufika makaburini siku ile alishangaa kumkuta mwanamke kijana mwenye kadirio la miaka ishirini na miwili akiwa amepiga goti pembeni ya kaburi la Jack. Mwanamke yule alikua akisali pembeni yake aliambatana na mtoto wa kiume mdogo mwenye kadirio la miezi mitano pamoja na hilo yule mwanamke alikua na Midoli mkubwa pembeni yake.
Mama Jack hakutaka kumshitua yule Binti alihakikisha yule mwanamke anasali Dua yake Kisha anasimama ili aondoe. Kweli mwanamke yule alipomaliza kusali Dua yake alifanya kuweka Midoli ile mkubwa pale kwenye kaburi la Jack akambeba mtoto wake kujua da kuondoka.
"Excume me Sister." 🙇Mama Jack alimsimamisha yule mwanamke.
"Without excume madame, what can l do for you?" 😊
"Naomba kuuliza kama ni wewe ndiye uwekaye Midoli juu ya kaburi la mwanangu Jack?"🦕🪆 Yule mwanamke alitoka macho👀 kidogo kama ishara ya mshangao.
"Ndio, ni mimi kwani wewe ni mama yake Jack!?" ❓ kko huiAlijibu vizuri na kuhoji.
"Ndio, Jack ni mwanangu na wewe ni nani?"
"Oh! Mama!" Yule Binti alienda kumkumbatia mama yake Jack 🫂🤗 baada ya muda alimuachia.
"Nmefrahia kukujua pia kukuona, mimi nilikua ni mpenzi wa Jack na huyu pembeni ni mtoto wa Jack, first born.🤱
"Mtoto wa Jack?! 🧒Mama aliuliza kwa mshangao. ❗
"Mwanangu Jack hajawai kuwa na mtoto." Mama Jack akamsogelea yule mtoto Kisha akamuangalia usoni. Hakika mtoto yule mwenye kadirio la miezi mitano alifanana sana na Jack kuanzia uso, midomo, macho hata komwe la Jack.
"Ni historia ndefu mama lakini kama hutojali Nipo tayari kukusimulia 📚🔊" Binti aliongea.
"Nisimulie tafadhali, mama Jack aliingia hamu ya kujua.
"Ninaitwa Bella mimi ni Barmaid maarufu ndani ya Bar ya New ukonga. Nilifahamiana na Mpenzi Jack miaka mitatu iliyopita alikuja ndani ya Bar yetu akiwa mchovu asiyeeleweka. Alikuja kuomba kazi, kazi yoyote pale bar 🍾🍸 kama vile kuwauzia wateja pombe, kusafisha kumbi na vyombo vya Bar au kupikia supu🥙🍽️ wateja. Meneja wa Bar ya New ukonga alimkubalia jack. Jack alianza kazi hapo, ndio tulipoona nana na Sie tukapendana sana. Bella aliendelea kusimulia.
"Kipindi Jack amekuja kutafuta kazi👷 alikua Hana pahali pa kulala, alilala chini na kwenye viti vya Bar. Nilimuonea huruma nikamwambia Njoo tuishi wote nyumbani kwangu. Jack alifurahia hapo ndipo penzi la mimi na Jack lilipamba moto." 🔥
"Jack aliniambia ametoroka nyumbani kwa wazazi wake sababu wamekataa kumuunga mkono tamanio la kazi anayotaka kulifanya yaani Muzic.🎶🎼 Nilimfariji Jack kwa kumwambia ipo siku atafanikiwa. Kweli baada ya miaka miwili aliingia studio kuurekodi wimbo wake lakini wimbo wake haukuvuma sana Radioni, hakuwa tawi 🌿 la juu lakini bado hakukata tamaa.
"Mara kwa mara Jack aliniambia anawapenda sana Baba na mama yake, ipo siku atakapokua super star ✨🌟 atawatembelea ili awaoneshe jinsi alivyofanikiwa na kubarikiwa. Baada ya miaka miwili kupita nilishika mimba ya Jack, Jack alifurahia sana. akaingia studio kutengeneza wimbo wa kumshukuru Mola juu ya mtoto wake ajaye. Wimbo wake ulipoingia studio ulipendwa mno basi akiaanza kuitwa kwenye lnterview mbalimbali."
"Miezi tisa kutimu nilipelekwa Leba kujifungua huyu mtoto Charles, nikiwa Leba Jack aliitwa ndani ya moja ya Radio kubwa Dar es saalam. Masikini kama angelijua huo ndio utakua mwisho😔 wake wallah! Asingelienda."Bella alitokwa chozi akalia. 😢
"Kwani nilijua kuwa Jack amepata ajali na kifo? Sikujua hadi pale Polisi waliponipigia simu📞 wakidai kwamba wameiona nambari yangu ya simu kwenye Driving passport ya Jack. Nililia jaman, nililia hadi basi. Nikafanya upelelezi ili kugundua wapi mpenzi Jack amezikwa ndiposa nikajakugundua hapa. " Bella alijieleza.
"Marehemu mpenzi wangu Jack aliniambia anawapenda sana lakini hakuwa na furaha ya kukataliwa timizo la ndoto zake. 🎭" Bella alisimulia akilia, mama Jack pia alilia.
"Nimeumia sana Bella, kama baba jack asingelimlazimisha Jack mwanangu kusomea kitu ambacho hakipo mtimani leo hii angelikupa mbali kimaendeleo. Naomba twende nyumbani kwetu ukapajue na pia umjue baba yake Jack."Mama Jack aliomba.
"Hapana mama labda siku nyingine." Bella aliona aibu.
"Usikatae Bella wewe ndiye mfariji wa mwisho kwangu." Mama Jack alimsihi Bella ambaye hatimaye alikubali na safari ya kwenda nyumbani kwa mama Jack ilifana. Kufika hukowakamsimulia Baba Jack kila kitu. Baba Jack alibaki akimwaga chozi na kilio.
Baba Jack na Mama Jack walimpokea Bella na kumuomba awe anawatembelea mara kwa mara Bella alifanya hivyo Charles mjukuu wa baba na mama Jack aliendelea kukua vizuri akapendeza. Uzuri ni kwamba Charles alionesha Darili za kuupenda Muzic Babu na Bibi yake walipoona mtoto anakipaji cha kuupenda Muzic wakamtafutia Mwalimu wa Muzic ambaye alimfunda Charles Muzic. Wazee wale walitokea kumpenda mtoto Charles Pendo la kupendeka. Ile Hatia ya kumfukuza nyumbani Baba Charles iliisha sababu charles aliwaondolea huzuni na Hatia.
-----------------
TCHAO 👋👋
🎸🎺🎙️
No comments:
Post a Comment