Wednesday, November 20, 2024

BWANA HARUSI TAPELI

 



MASIKINI MAMA YANGU ALIITAFUNA AIBU. 


      Daegy ni jina langu na kwa bahati nzuri mie Egy Nina kazi nzuri inayoniweka mjini, kazi niliyoiridhia mimi wenyewe. Nimeajiriwa katika shirika la Ndege la Ndege, Tanzania Air way. Nimeajiriwa kama muhudumu yaani Fry attendant, kazi yangu ni kuhudumia wasafiri (Air traverer) wanaoenda kwenye mataifa mbali mbali ya Dunia:China, lndia, Australia, South Africa, Uganda, Rwanda, Burundi na Commorrow. 

Mie Daegy ninacho kisa kimoja Naomba kushea nanyi wapendao visa na Mikasa.

      Kisha changu kinaanzia mwezi September mwaka 2024 siku hiyo Mwanamama tajiri Africa Mashariki Bi. Shyrose alikodisha Fry jet, Ndege ndogo binafsi kwa lengo la kujifurahisha angani. Hakuwa pekee bali aliambatana na kijana mmoja mzuri shababi wa sura na sauti ya kipekee, nilikuja kumjua kwa majina Amboni Ambrose. Usiniulize niliwajuaje hawa wapendanao nitakujibu mimi ni Fry attendant lazima ni wajue wateja wetu.

     "Daegy keti hapa tuikate keki yetu ya furaha" Mwana a matajiri Shyrose alikua akifanya shereh ndani ya ile Ndege ndogo binafsi.

      "Asante madame, niliketi Karibu na dirisha upande wa kushoto wao aliketi upande wa kulia. Kipande cha keki, 🎂🍰kilikatwa Kisha Mwanamama akanilisha kwa tabasamu nono.

    "Happy birthday madame." 🎂Nilimwambia.

     "Thanks🥰🙏 Daegy Naomba nikutambulishe kwa mchumba wangu tarajiwa Amboni Ambrose," Alimgeukia yule kijana mzuri wa sura.

     "Please my sweet Ambrose meet Our fry attendant Daegy."

     "I'm pleased to meet you Daegy." Ambrose alinijibu kimomboo akanipiga kiss😘 mkononi, ishara ya upendo na kujali.

      "I'm pleased to meet you too nilimrudishia kiss ya upendo mkononi. Shyrose akamwambia Amboni:

    "Leo ni siku yangu ya kuzaliwa lakini pia anataka nikufanyie sapraiziment ambayo hufanywa na wanawake wachache Duniani" 

    "Waooo! Daring 😍nitaifuraia." Amboni alijidekeza.

    "Fumba macho yako Baby" Amboni alitii. Akayafumba macho yake. Shyrose akakitoa kibox kimoja kidogo kwa umbo alikifungua na kutoka na Pete moja mashallah😘yenye madini ya Almasi 💎 katikati. Taratibu na kwa madaha Shyrose akamvisha ile Pete bwana Amboni. Kisha kwa mwingi wa tabasamu Mwanamama akasema.

      "Sasa yafumbue macho yako mume wangu tarajiwa."
   
       "Waoo😻💖!" Amboni alipoiona ile Pete yenye kito cha Almasi alimkumbatia Shyrose kwa furaha wakapigana kiss😘 na kuibadilishana ndimi😉😊🥰 baada ya lile tendo la furaha wine ya Mzabibu ilifunguliwa, birauri zilimiminwa ile wine sie tukanywa kwa furaha, raha na tabasamu, watatu sie tulijihisi kama tunaelekea Jerusalem kuijenga mbingu☁️🌤️ ya raha starehe na sherehe kwa jinsi furaha zetu zilivyonoga.

____________

Madame Shyrose alitokea kunipenda na kuniamini sana siku ile baada ya sherehe aliniachia kitita cha shilingi million tano pamoja na nambari yake ya rununu.🤳📞 Aliniambia zile pesa alizonipa ni kama Asante kwa kampani. Jamani🤭 nilijiona siku ile hadi nikaanza kumuonea Gere yule hensam wake Amboni, moyoni nilijisemea 'Huyu anafaudu vingi kutoka kwa madame Shyrose'🤪

       Shuhuli ile fupi ilipofika kikomo nikafanya kurejea nyumbani kwangu kigamboni huko nikajibwaga kitandani na kulala kwa furaha. Siku mbili baadae Mama yangu Bi. Benedetha alinipigia simu akaniita nyumbani na kuniambia Kuna jambo zuri angelipenda kushea Nami. Hima hima 🏃nikaichukua Prado yangu rangi ya kijivu niliyoinunua kwa mshahara wangu mwenyewe.

Nilifika Oysterbay ndani ya mjumba wa mama yangu mwenye pesa zake, sema Baba yangu aliaga Dunia na kutuachia mali nyingi na pesa nyingi ndani ya Bank, kiwanda kidogo cha kutengenezea mikate na sabuni huko Pugu, Super market ndogo kule Barabara ya Kamata, aliacha pia majumba sita katikati ya Jiji, pia aliacha magari yake.

      Mama alinipokea kwa bashasha,☺️ tukaelekea sebuleni tuketi na kuongea mengi. Nilipoingia tu sebuleni nilishangaa kumkuta Bwana Amboni ameketi sofani kapigisha pozi miguu yake nambari nne anakunywa Whsky🍷 Bila wasiwasi kama yupo nyumbani kwake.

"Mpenzi mwanangu mimi mama yako ile miaka yote ya upweke imefikia kikomo leo nimeona nikutambulishe kwa mchumba wangu na Mume wangu tarajiwa Bwana Amboni Ambrose" 😷Jesu! Nilipigwabutwa

'Mpenzi na mchumba mtarajiwa!?' Nilijiuliza mtimani.

'Jamani huyu Amboni ana akili kweli au amerogwa!?' Sikupata jawabu. Niliishia kumtazama yule Bwana Amboni kwa jicho lamshangao sema yeye hakutaka kukutanisha macho yake yakutane na yangu. Aliishia kutazama Tv na kugugumia mafunda ya ile Whsky.

     "Ninampenda sana Bwana Ambrose tumekubaliana tufunge ndoa mwezi ujao." Mama alizidi kunishangaza. 🤭😶🤥
   
    "Mimi pia ninampenda sana mama yako Bi. Benedetha, Mungu bariki ndoa yetu ipendeze" Alipoongea hivyo mama alifurahi sana akijua Bwana Amboni yupo siriasi na hatanii.

    "Mama mbona wanishangaza yaani ukutane na mtu ndani ya wiki kisha ndoa ifanyike mwezi ujao? 🙄" Nilimuuliza Mama.

      "Ninampenda sana Bwana Amboni, ameniondolea upweke, huzuni na majonzi ya kufiwa na baba yako." Mama alijibu

    "Kwahiyo ninataka ndoa👰 ya haraka haraka, tukae ndani tuyafurahie maisha." Mama aliongea. 

     "Ma, Naomba tutoke twende pahali tukaongee." Nilimwambia mama aliyenisikiliza tukatoka na kwenda chumbani kwake.

     "Mama unamjua vizuri huyu Bwana Ambrose?" Nilimuuliza.

     "Mwanangu nimefall in love💕😍💖💞💘 sisikii Wala sielewi kwa ajili ya Ambrose. He is kind of charmistick man. Nitamjua vizuri tukiwa ndoani."

     "Mama nadhani umeingia ndani ya pango la Simba na mdomo wa Mamba bado  kidogo utaliwa." Niliongea fumbo tungali tumeketi kitandani, chumbani kwa mama.

    "Unamaanisha nini mwanangu?"🤔 Benedetha mamangu aliuliza.

  "Usolijua ni kama usiku wa kiza, huyo bwana Ambrose ana mchumba wake jinale Shyrose Mwanamama tajiri Afrika Mashariki." Nilianza kumtobolea mama siri.

    "Nini!?" 😶‍🌫️🫥 Mama alianza kubadilika, hasira juu ya komwe lake zilionekana kutuna

    "Belive me or not my Mom huyu mwanaume yawezekana ni tapeli. Anawafuata wanawake wenye pesa zao ili awaingize mitini akiisha laghai na kuwatapeli." Niliendelea kuongea.

   "Majuzi nimewahudumia Shyrose na Bwana Amboni ndani ya private fry jet, Shyrose alikua na birthday akanitambulisha kwa bwana Amboni kama mchumba wake akamvisha Pete yenye kito cha Almasi na uzuri Shy ameniambia ndoa lazima ifungwe mwezi ujao." Nilimfunulia mama ukweli. 

   "Stapenda kusikia uongo huo Daegy,😒😵‍💫 tangu lini mwanaume akavishwa Pete ya uchumba? Mbona hiyo Pete yenye kito cha Almasi hajavaa kidoleni? 🤷Wanionea wivu eeh! Wanionea wivu sababu tu nimependwa na kijana mzuri wa sura ya kupendeza machoni? Mama  aliwaka hasira.😡

     "Sio hivyo mama..... 😢" 

     "Ila... Ila unataka kunitenganisha na mpenzi wangu? Nakwambia ushindwe🤢 uregee. Ninampenda, amenipenda mapenzi motomoto huyu simuachi ng'o hadi nirogwe" 👌 Nilimshangaa mama anavyoongea 🙌

    "Tena haya mazungumzo yafie hapa hapa Usije ukamuudhi mpenzi wangu na kuniharibia mipango yetu. Kama hauniungi mkono juu ya kumpata mwanaume mzuri kama Ambrose Naomba niache na maisha yangu. Mama has life mama need to live. Mama pia ana maisha, mama pia anahitaji kuishi. " Alinifokea na kuniacha chumbani kwake akarejea sebuleni kule alikomuacha yule Conman (Tapeli) Ambrose. 

************

Ilipita wiki moja mamangu hakuongea na mimi binafsi nilikua nawaza nitamsaidiaje mamangu atoke kwenye mikono ya yule mwanaume Tapeli. Yamkini ndio tabia na mazoea yake  kuwalaghai wanawake wenye pesa zao akiisha kuwachezea angeliwabwaga na kuwaachia maumivu. Hapana kama anataka kumchezea mama yangu hapa amebuma, hafiki mbali kipungu hata angeenda mbinguni. Niliwaza lazima nimuokoe mama. 

      Ghafla nikapata wazo nikamkumbuka Shyrose yule Mwanamama tajiri Afrika mashariki, roho yangu ikaniambia fanya hima umtafute Kuna mazuri utayapata kutoka kwake aweza kuwa msaada tosha. Nikampigia simu madame Shyrose tukakubaliana tukutane LAMADA HOTELI iliyopo Msimbazi Center. Kama wazungu vile tulikutana tukaongea. 

     "Juzi hapo ameniomba millioni hamsini amedai anaenda kununua Shamba lakini bado hajanipa data juu ya shamba hili. Binafsi nimeanza kuingiwa wasiwasi juu ya Ambrose ananiomba pesa nyingi ambazo hata sijui anavyozitumia." Madame Shyrose alionesha wasiwasi wake 

   "kwanini tusimchunguze, tumchunguze ili tujue labda Kuna wanawake wengi wengine amewachezea na bado tu anaelekea kuwachezea wengine." Nilitoa wazo. 

    "Wazo lako zuri sana Daegy, mwanaume huyu atakua Conman haiwezekani anipe proposal ya kunioa mwezi ujao wakati huo huo unaniambia anataka kumuona mama yako. 🙄 Haiwezekani Daegy huyu ni tapeli." Shyrose aliongea kwa hasira. 

    "Tuliza komwe madame nimepata wazo kama utaliafiki yamkini litakua msaada kwetu." Wazo zuri liliniingia kichwani. 

     "Wazo gani hilo uniambie hata kama Lina gharama Nipo tayari kugharamia" Madame hakunivunja moyo. 

     "Fanya kumwita mimi nitajifanya mhudumu wa hii hoteli, lazima tupate majina ya wanawake wote anaowatapeli kupitia simu yake. Kisha tutamkomesha kupitia hao wanawake." Niliongea yangu. 

"Bright and beautifully. Nimelipenda wazo lako lazima tumuaibishe na kila pesa au mali aliyotapeli Lazima ataitema na kutapika mbele ya Polisi, Mahakamani au Magereza. Madame alipendezwa na wazo langu. Amboni alipigiwa simu akuje pale LAMADA. Madame akaongea na meneja wa ile hoteli juu ya mpango wetu, pesa ilifanya kazi faster nikavaa mavazi ya wahudumu wa ile Hoteli nikajifanya na mimi kama muhudu.

Ambrose walifika pale Hoteli akiwa amejaa tele, Pete ile yenye kito cha Almasi imetulia chandani, wakapiga story mbili tatu Kisha wakaagiza manywaji mie niliyebadilika mwonekano nikaenda kuwahudumia. Nilipofika tu nikafanya ujanja nikajitegesha mezani ile wine iliyokuwa ndani ya Bilauri la Bwana Amboni ikatenguka na kumwagikia Ambrose, akaghafirika. Sikupoteza muda niliiwai simu yake aliyoiwacha pale meza pasina yeye kuniona nikajifanya Naomba msamaha. Aliponiona alishangaa nimefuata nini Hotelini.

        Haraka haraka nikaenda Restroom (Choo cha kike) karatas na karamu yangu mkononi na uzuri wa simu yake haikua rocked nikafanya faster kuiba nambari za wanawake wote aliowasave. Walikua wengi yapata miamoja mama yangu akiwa miongoni mwao. Nikasave zile nambari kwenye karatasi yangu Dakika therathini kupita nikashangaa bwana Amboni yupo miguu kwangu.

     "Pumbavu 😡nilijua tu ni wewe uliyeichukua simu yangu" Alinifokea na kunipokonya ile simu.📱

    "Unadhani sintamuoa mama yako? Lazima nimuoe, nyau 🐈‍⬛wewe hauwezi kunizuia." Alinifokea tena.

     "Haya Bana tapeli tutaona kama utafanikiwa." Nilimjibu nyodo. 

    "Nimefanikiwa mengi hili  nitashindwa?" 🤪😜😛 Alijigamba.

    "Lazima ushindwe, usishindwe wewe kama nani tapeli la mapenzi😵‍💫" Nilimfokea Kisha nikaondoka na kumuacha anakodoakodoa macho ndani ya Choo cha kike. 
                   --------------
Sie wawili tukashirikiana kuwapigia simu wale wanawake mia moja tuliohisi na kudhania ni wahanga wa utapeli kutoka kwa bwana Ambrose. Walijikusanya na kwa kilio kikuu wakaeleza machungu yao ya kutapeliwa na mwanaume mtanashati mwenye ahadi nono kumbe ahadi na promise zote zimejaa uongo. Hatimaye mwisho wa mipango yetu tulikubaliana tumuumbue Bwana Amboni Ambrose siku ya harusi yake na mama yangu Bi. Benedetha. 

     Siku ya harusi ilipofika wale wanawake mia wahanga wa kutapeliwa na bwana Amboni walijipanga, wengi wamebeba mafimbo, mijeledi, mawe, kuni, chupa, viatu na kila aina ya bakora ili kumtia adabu yule mpuuzi anayewadanganya wanawake kwa kisingizio cha ndoa Kisha kuwatapeli na kuwatelekezea umasikini. 

Madame Shy pamoja na mimi tulijitenga ili tuwe watazamaji tujionee video ya bure, video ya kufunga mwaka video ya kumwaibisha bwana harusi tapeli. 

      Mbele ya mchungaj mama yangu na bwana Ambrose walikua wanajiandaa kula kiapo cha ndoa ndipo kanisa lilishituliwa na ujio wa wanawake walioshika silaha za maangamizi waliingia kanisani wakipiga kelele:

    'Bwana Amboni, bwana harusi tapeli, tapeli mkubwa' 

    'Turudishie mamilioni ya pesa zetu ulizotutapeli ukituahidi ndoa' 

    'Magari yetu, nyumba zetu, mshamba yetu umetutapeli.' Walipiga kelele nyingi mno mama yangu aliishia kutetemeka. 🤣🤑. Bwana Amboni alitazama chini kwa aibu, mchungaj na wahudhuriaji wa harusi walishangaa kelele zile. 🔊

    'Utazirudisha au hautazirudisha???💰💸 " Walimuuliza. Kwani aliweza kujibu zaidi ya kutetemeka. Lile kundi la wanawake lilianza kumpiga kwa mawe, mangumi, fimbo na kuni. Walimchania suti yake nzuri aliyonunuliwa na mama yangu. Waliendelea kumpiga na kumfedhehesha, Japokuwa mchungaj aliwasihi wasifanye hivyo lakini wapi! Hawakumsikiliza roho ziliwauma mno. 

Wakamtoa nje ya kanisa wakaendelea kumpiga kipigo cha paka mwizi bahati nzuri  madame Shyrose aliwapigia simu POLISI walifika na kumsomba hadi kwenye Diffenda lililompeleka hadi kituo cha POLISI huko nako akaandikiwa tarehe ya kupanda Mahakamani.

'' '' '' '' '' '' '' '' '' '' " '' '' '' '
Tukio lile kanisani lilimwaibisha sana mama yangu, alijifungia chumbani kwake akilia na kujutia 😢😭🥹kwanini hakunisikiliza nilipomwambia yule Bwana ni tapeli, Baya zaidi ile HABARI ya bwana harusi kula kichapo kanisani iliandikwa sana juu ya magazeti na kusambaa vibaya mno  kama moto wa nyikani 🔥. Kwenye mitandao ya kijamii, wapendao UMBEA wakayakuza yakawa marefu yaliyojaa chumvi na ndimu. 

Picha za mama zilizagaa mitandaoni📡🛰️, alishindwa kuishika simu yake azisome zile HABARI maana aliaibishwa. 

Binafsi namshukuru Mola wangu nimemuokoa mama kutoka kwenye makucha ya Simba 🦁na mdomo wa mamba.🦛 Mama yangu kama angelizubaa Angelikua miongini mwa wale wanawake wanaolia kutapeliwa mashamba yao, majumba yaliyouzwa kinyemela na magari yaliyoibwa yakauzwa black market (Magendoni) 


####### Tchao
*********
     

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...