(A SARUGATE WOMAN)
MIMBA TATU 🫄 ZA DADA YANGU ZILICHOROPOKA, HATIMAYE SHEMELA ALINIOMBA NIWAZALIE MTOTO. 👼MTOTO ALIOPOZALIWA WOTE WALIMKATAA NA KUMKIMBIA. 🏃🏃
Katika familia yetu tulizaliwa wasichana wawili, mimi Shelidani na mdogo wangu Miriam. Utotoni tulipendana sana na ukubwan tulipeana ahadi iwapo Mola atatujalia ndoa na familia zetu tutasaidiana kuwalea na kuwatunza watoto wetu. Basi maisha aliendelea.
Maisha ni Safari ndefu, Miriam mdogo wangu alikuja kupata mwanaume mmoja 🧑🦯kutoka kwenye familia na ukoo wa matajiri 🪙🥇💎🕌💰wakafunga harusi nzuri ya bei gharama. 👰Mume wa mdogo wangu aliitwa Zakaria ama kwa kifupi alipendelea tumwite Zaki. Zaki shem wangu alikua na bahati ya kurithishwa mali kutoka kwa wazazi wake. Alimiliki Viwanda na makampuni mengi, hakika maisha yao hayakua na uchache. Yalijaa Mema yaso dhiki na njaa.
Shelidani mimi nikaja kupata mwanaume mzuri aliyeitwa Bonie, hatukupendana ati kwa kigezo cha mali na utajiri, ukitegemea hizo mali na utajiri hatukubahatika kuwa nazo. Tuliridhika na hali zetu. Mume wangu Bonie alikua akijishuhulisha na ujenzi wa majengo mkubwa yaani Bulding constructor👷🏦🏢🏛️🏗️ wakati mie nalibaki home kama mama wa nyumbani, mara moja moja nilimwitaji Mwalimu wa ushoni na udarizi anifunde jinsi ya kutumia cherehani.
Basi mdogo wangu Miriam alikuja kushika ujauzito🫄 ulioleta furaha kuu ndani ya ile familia ya Mamillionea lakini baada ya miezi mitatu mimba ya mdogo wangu Ilikuja kutoka ikamuachia kilio na uchungu, shem wangu Zaki akageuka mfariji, akamfariji sana na kumpooza kwa maneno yaliyojaa faraja na matumaini. Kipindi icho mie Shelidani na Mume wangu Bonie tulijaliwa kuwa na mtoto wetu First born tuliyempa jinale Gadieli,🧒 tukabaki kumfariji Miriam.
Miaka miwili baadae mie Shelidani na Mume wangu Bonie tuliwakaribisha watoto wetu pacha Maiko na Pedro👬 kwa hakika ndoa yetu ilibarikiwa furaha, raha, cheko na tabasamu.😊😍
Jamani sijui niseme ninaona mfadhaiko, huzuni na sikitiko. Embu tusaidiane kutema mate chini puuuu! Tumkanyage ibilisi shetani mwaribifu na mwovu. Ndugu zangu hamuwezi kuamini pale nikiwaambia Miriam mdogo wangu alikamata mimba ya pili lakini loh! 😢Ilichoropoka na kumuachia teseko na sononeko la mtima🖤. Alijiuliza kwa moyo: 'Tatizo nini?🤨' 'Ana changamoto gani?' 😮💨'Kwanini yeye tu!?🤢' Kilio kikuu chenye ndimu kilimnyanyasa.
Nilimshukuru Mola wangu baada ya kumkaribisha last born wetu Ivan baada ya Kipindi kirefu cha kujipumzisha uzazi na kuwalea wale wavulana wangu watatu:Gadi, Maiko na Pedro. Nyumba yetu ikabarikiwa furaha utoto na watoto, elimu na malezi mema. Tukajenga upendo na upendo ukasimama kama nguzo kuu ya familia tukayazidisha mapenzi na Mahaba nyumba ikanukia na kupendeza.
Niwaambieni wapenzi wasomaji hakika nyota✨ yangu iling'ara na kupendeza, nyota🌟 ya mdogo wangu Miriam iling'ara pia na kupendeza, udhaifu wa nyota yake haikuchelewa kufifiana, kiza na utusitusi 🌑 viliifunika ile nyota. Ndiposa mdogo wangu Miriam akawa ni mtu wa kulia na kumuuliza Mola wake kosa lake nini?🤕 Tatizo lake gani?😷
Mimba ya tatu ilipotoka waliwaona madaktari, washauri na wanasaikolojia waliowafariji kwa maneno ya kuwataka wawe wavumilivu na wasubirivu. Safari hii mdogo wangu akawa ni mtu wa kukata tamaa, tulipomwita kwenye Social 💃👯🕺event hakutaka kuhudhuria, alipowaona watoto Wadogo wa majiranize aliwatazama sana na machozi yakamsaliti akawa ni mtu wa kulia chungu.😿
Alihitaji sana mtoto angarau na yeye aitwe mama, angarau na yeye ajivune kwamba maisha ameyapatia. Pasina mtoto alijiona hajakamilika. Ubaya ni pale mimba zilipomsaliti na kuchoropoka. Maisha yetu yakaendelea watoto wangu walipendeza wakawa ni wenye Afya uzuri na ubora wakaboreka.
*****************
Ninakumbuka siku moja juma pili siku ya mapumziko baada ya ibada📿 na kazi za kutwa nzima Miriam mdogo wangu na Mume wake Zaki walitutembelea. Siku ile tulifanya karamu🎂🎊 ya upendo. Vyakula vingi vilipikwa, vinywaji vingi viliandaliwa.🍹🍷🍻🍶 Uzuri ni kwamba katika hiyo karamu sisi hatugharamia hata shilingi mia pesa zote za karamu Shemela wangu Zaki aligharamikia. Maana yeye ni kibosile mwenye pesa zake.
Baada ya karamu Bonie mume wangu alisaidia kuondoka vyombo pale mezani akaelekea kwenye sinki kuvikosha. Pale Sebuleni tulibaki watatu Mie Sheli, Miriam na mumewe Zaki. Katikati ya maongezi yetu Wine ya Mzabibu 🍷 ilifunguliwa Shemela wangu Zaki akayatoa yake ya moyoni.
"Sheli, shemela wangu kuna jambo naomba tulijadili🗣️🔊 itapendeza iwapo tutapata mwafaka"🤝
"Ndio, shemela ongea ninakusikiliza, nilimjibu Shem Zaki nikajimiminia Wine yangu na kupiga funda moja Zito lenye afya.
"Kama ujuavyo Shem mie na Mke wangu tumehangaika sana ndani na nje ya Mahosptali kujua jinsi gani tunaweza kubahatika kupata mtoto ambaye hawez kuharibika sembuse kutoka ndani ya tumbo la Mama yake. Jibu walillotupa Madaktari lilituumiza mioyo yetu maana walituambia kamwe Miriam asingeliweza kudumu na ujauzito lazima uchoropoke na kumuachia kilio na uchungu" Maneno aliyoyaongea niliyafahamu na kulijua tatizo la mdogo wangu.
"Tumehangaika sana na kuwaona madakta, tumewapa pesa nyingi ili watusaidie kuimaliza changamoto ya Miriam Mke wangu, lakini wapi! Kwa pesa au kwa mali haijasaidia. Hatimaye mwisho wa siku Dakta mmoja kutoka India alitupa ushauri. Shem zaki akameza Funda moja ya ile juisi ya Mzabibu namie nilimsikiliza.
"Unajua alitushaurije!? Alisema kwa vile Miriam anachangamoto ya kubeba ujauzito na ujauzito wake kuchoropoka baada ya muda mfupi njia sahihi ni kwa upande wangu kutafuta mwanamke mwingine kisha mbegu zangu kupachikwa kwake ili anizalie mtoto." Shem Zaki aliongea mie nilimsikiliza.
"Lakini...." Alisita kidogo kunena.
"Dakta kutoka lndia amesema itakuavizuri kama atapatikana mtu kutoka familia ya Miriam, itakua vema kama huyo mtu atapewe mbegu na kubeba ujauzito ambao kwetu utakua ni familia."
"Mh! 🤔🥺" Niliguna yale matatizo ya wenzangu.
"Kwahyo mie Zaki na Mke wangu Miriam, tumekuja kwako tunaomba utusaidie kubeba ujauzito ambao hapo baadae utakuja kuwa familia maana damu yako na damu ya Miriam mdogo wako ni damu moja." Nilishituka 😤kusikia kauri ya Shem Zaki.
'Yawezekana vip Shem langu, mbona kama naona ni jambo la aibu.' Niliongea kimoyo moyo nikiwaza labda Shem Zaki na mdogo wangu Miriam wamerukwa na akili, sio kwa kusaka mtoto huko yaani wanasaka mtoto kwa nguvu nzito.
"Ninampenda sana Mke wangu Miriam sijawai kuchepuka au kumsaliti ninataka awe na furaha kwaiyo nimetafakari maneno ya Dakta kutoka lndia nikaona yupo sahihi." Sikumuelewa Shemela wangu Zaki.😕🫨
"Nadhani haitawezekana Shem kwanini usitafute mwanamke mwingine Nawe ukamwage mbegu zako kwake.? Kwani wanawake wameisha Duniani hadi ufikie hatua ya kunichagua mimi tu?" Nirikereka.
"Tusaidie Shelidani, tusaidie tunakuomba. Hatuna nia mbaya." Miriam mdogo wangu alinisihi. Machozi yakamdondoka. Nikamuonea huruma jinsi alivyopitia changamoto ya mimba kuchoropoka. Huruma zile zikanifanya niumie moyoni. Hatimaye nikamwambia.
"Subirini nitayajadili na Bonie mume wangu. Nimsikilize anasemaje!?" Sikuwawavunja mioyo yao. Wakaondoka na kunisihi sana nisiwaangushe. Usiku 🌒🌑Ulipowadia mie na Huba langu Bonie tukiwa kitandani twatomasana tomasana bado kidogo tulipakue Huba Kisha tuanze kulila likiwa lingali la mwoootroo💞🔥 nilianzisha mazungumzo.
"Ndio hivyo Sweet heart 💕Dakta kutoka lndia anamshawishi Shemela wetu Zakaria nimbebee ujauzito ati anadai itapendeza sababu damu yangu na damu ya Miriam zinafanana."🩸🆎
"Duh! Huo sasa Mitihani yaani ujaliwe watoto wanne alafu uongeze mwingine wa tano, si utachoka kuzaa Sweet heart." Bonnie aliongea.
"Mwenyewe nimeshangaa🥺😂, nimeona kama kaupuuzi furani wanakujaje kunivunjia heshima ati niwazalie mtoto wakati kundi kubwa la wanawake limejaa mitahani!🌴🎋🛣️ Hawawaoni hao hadi wanione mimi tu." Niliipinga kauri ya shem Zaki na dadangu Miriam.
"Lakini sio mbaya kama unampenda mdogo wako wazalie tu." Bonie alinishitua.
"Mwanaume mpumbavu wewe😠😧 yaani unaniruhusu nibebe mbegu za shemeji yangu." Nlianza kusinyaa na kudhoofika baada ya kusikia kauri ya mume wangu Bonie.
"Mimi ni mumeo na nime kuruhusu maana ni kitendo cha kupachika mbegu na sio kufanya zinaa..... Sioni tabu wewe kubali tu umuokoe dadako. Nimefikiria sana miaka yote hiyo akiendelea kukaa bila mtoto atadharauliwa sana tena atafukuzwa kama Jibwa koko."🐩🐕🦺 Bonie aliongea kwa kirefu.
"Bonie umerogwa wewe sio mzima👿" Sikutaka tena mazungumzo yaendelee. Nikaamua kulala mzungu wa nne maana nilichukia ujinga ule.
===================
Ghafla moyo wangu ulinishurutisha nikubali Kubeba ujauzito na Kumzalia Shem wangu Zaki na dada yangu Miriam sababu mtima wangu ulisumbuliwa sana na ile kauri aliyoitoa Bonie wiki moja iliyopita. Bonie alisema iwapo Miriam ataendelea kukaa ndani pasina mtoto angelidharauliwa na Taraka ingelimfuata maana kwa muda wote huo angeonekana ni mzigo ndani ya ile familia. Moyo ukaniomba nifanye maamuzi.
Nikaichukua simu yangu ya Mezani ☎️ nikampigia Shem Zaki pamoja Dadangu mdogo Miriam 📞 nikamwambia nimeridhia ombi Lao, Nipo tayari kuwazalia mtoto kilichobaki ni kuapachikwa mbegu. Furaha waliyokuwa nayo haisomeki hata kwenye vitabu 📚au kuonesha kwenye kumbi za sinema📽️📺. Walifurahia sana. Mwezi mmoja baadae Niliingia Hospitali kupandikizwa mbegu za Shemeji yangu. Dakta kutoka lndia 🇮🇳alifanya kazi yake mbegu za shem Zaki zilipandikizwa kwenye kizazi changu.
Mimba ilikubali, mtoto akatungika tumboni. Taratibu alikua na maendeleo yake yalikua ni mazuri yaani Sikupata tabu yoyote ile. Furaha waliyokuwa nayo Zaki na Miriam iliwafanya watumie pesa nyingi kulihudumia tumbo langu. Kila nilichotaka nilipewa na kila nilichoomba nililetewa taratibu wakaanza kukinursery (kukipamba) mchumba ambacho mwanao angelilala, wakakidecorate nacho kikapendeza kila kitu muhimu kiliwekwa ndani. Kilichobaki ni mapokezi ya yule mtoto.👼
Bonie mume wangu hakuuchukia wala kuubeza ule ujauzito niliombebea dadangu mdogo na Shemela wangu Zaki. Wavulana wangu wadogo kila siku waliongea kitotototo wakiuliza 'Mama lini atakuja mdogo wetu?'👶 wakanifurahisha zaidi waliposema 'Akija tutakuwa walinzi wake.'🫡 'Tutamfunda kusoma na kuandika!' 📖🖋️'Akija tutampenda na kumfrahia.' 😍💖 Nyumba yetu ikawa ni bustani 🏡na Paradiso ya furaha.
_________________
Basi siku ya kupata uchungu na kuingia Leba Bonie mume wangu aliwatafuta sana Miriam na Zaki kuwajulisha kwamba ninaelekea Leba miezi tisa ishatimu. Simu zilipigwa 📲📞zilipigwa zikaita wee! Hazikupokelewa📴 meseji zilitumwa Wasap, lnstargrame, Fb na kila mitandao lakini bado hawa wawili hawakupatikana. Wakatutia wasiwasi juu ya pahali waliopo.
Nikaingia Leba🛌, nikauvumilia uchungu wa kizaz na Mola wangu alivyo mwema nikajaliwa kujifungua salama mtoto wa kike baada ya masaa mawili kupita Miriam na mumewe Zaki wakaingia ndani ya Martenity hall (Chumba nilichopewa kupumzika) Usoni walionekana kutokuwa na furaha, wakati mie nilitegemea kupoklewa kwa tabasamu na vicheko nilikuja kushangazwa kwa kauri🗣️😶🗨️ walizozitoa.
"Huyu sio mtoto tuliyemtegemea." Zaki shemela wangu aliongea.
"Una maana gani shem Zaki? 🥺⁉️" Nilihoji kwa mshangao maana mtoto mwenyewe hakuwa na kasoro yoyote ile. Kama ni suala la macho, 👁️ mtoto alitimilika na alikua na macho maangavu, kusikia🧏 mtoto aliisikia na ngozi yake hakuzaliwa Albino.
"Umetuletea mtoto wa aina gani huyu Dada." Miriam alituacha hoi na mshangao mzito🥺 mie na Mume wangu Bonie.
"Kwani nyie mlitegemea niwaletee mtoto wa aina gani jamani🙂? Mlitaka mlemavu au asiye na jinsia?" Nilihoji ningali ninashangaa.
"Dada sisi tulitegemea ungetuletea mtoto wa kiume sio huyu jinsia ya kike, hatumtaki.😠" Jesu! ❗TUlizidi kuishangaa ile Couple ya geti kali.
"Mliniambia kama mlikuwa mna tafuta mtoto wa kiume au mimi ni Mungu hadi nipange juu ya jinsi ya mtoto."Nilibwata.😬🤯
"Dada unawatoto wanne na wote ni wa kiume Maiko, Gadieli, Pedro na Ivan. Kupitia kizazi chako wewe ndiye uliye andaliwa kutuletea mtoto wa kiume kama Dakta🩺🧑⚕️wa India alivyotushauri. Ajabu umetuletea mtoto wa kike." Hatumtaki." Miriam aliendelea kuongea.
"Miriam mmerogwa nyie, mbona siku nilipokua napandikizwa mbegu hamkuniambia kuhusu hilo yaani baada ya maji kumwagika ndo'mnakuja kupiga kelele. "Hasira zilinipanda hadi ndani ya komwe na ugoko.
"Shem Zakaria ninaomba umchukue mwanao uende ukamlee na umwache mke wangu apumzike sasa" Bonie Alimwambia Shem Zaki.
"Siwezi na sitaki."🫥👎 Shem Zaki alianza kuondoka pale Hospitali Sie wawili tukimshangaa.
"Shit👿!!" Bonie alifoka.
"Miriam nieleze mmepatwa na kadhia gani hata mfikie hatua ya kumkataa mtoto mliyeniomba na kunisihi sana niwaletee."
"Dada ninaogopa mpendwa, ni naogopa mimi." Miriam alianza kulia.
"Familia na ukoo wa mume wangu Zakaria wananisumbua sana akidai niwaletee mtoto wa kiume ndani ili hapo baadae mtoto hyu aje kuwa mrithi wa mali na tajiri wao." Miriam aliongea maneno ambavyo hajawai kuniambia.
"Tulipomueleza Dakta wa lndia kuhusu kizazi chako alifurahia sana tena alitushauri kwamba wewe ungelifaa kutuletea mtoto wa kiume ambaye atakuja kuwa mrithi wa mali nyingi na tajiri wa ukoo na Familia ya Mume wangu Zakaria lakini mambo amekua ndivyo sivyo."Aliongea.
"Kwani mtoto wa kike hatoweza kuwa mrithi!?" Niliuluza
"Hawataki dada, wanaamini katika damu ya mtoto wa kiume kama Mila na desturi za zamani walivyozishikilia. Baya zaidi mume wangu Zakaria aliniambia wazi kuwa iwapo utajifungua mtoto wa kike basi ndoa Sina, ndoa itafikua tamati, ataniacha na kunitupa." Aliongea kwa chungu na majuto.
"Miriam mdogo wangu Naomba mchukue mwanzo uende ukamlee, nimefanya kazi mkubwa sana kukusaidia." Nilimsistizia na kumsihi asimtelekeze mwanaye.
"Siwezi dada ninaipenda ndooa yangu." Alianza kuondoka pale Hospitali akimkimbilia mumewe.
"Waache waondoke, wapumbavu wakubwa wale. Ovyo" Bonnie alikasirishwa na hali ile.
"Wabaguzi, wanajali sana mali na jinsi.... Waambie hivi maji 💦haya a jinsia lakini hayatubagui, Milima🗻🏔️ haina jinsia lakini haitubagui."Yalimtoka maneno Bonnie.
" Nitakaa wiki moja Hospitali, tuwape nafasi, wakiingia chungu watamfuata mtoto wao." Nilimwambia Bonnie.
"kuwa na chungu Mama lvan, kama wamekataa mtoto tutamuadopt ili awe wetu." Bonnie alinifariji. Wiki moja lilipita nikiwa ningali Hospitali ninawasubiri Zaki na Miriam wageuze mioyo yao migumu waje wamchukue mtoto niliyewazalia, lakini wapi! hawakutokea Wala hawakuja kuniletea Uji mzito wa moto niunywe na kunipunguzia uchungu. Mwanangu Maiko, Pedro, Gadieli na lvan walinibembeleza nirejee nyumbani maana walinimiss sana. Basi mie mama Ivan nikaomba ruhusa nikarejea nyumbani maana mwanangu walinimiss balaa😂😘. Madakta waliniruhusu nikarejea nyumbani na maisha ya kulea mwana yakanifuata. 🤱.
***_____****____****
Mwezi mmoja kupita nikiwa namnyonyesha Binti yangu Ivanka Nilisikia sauti nje ya nyumba yangu yalikua ni mapokezi ya furaha kutoka kwa mwanangu wapenzi. Nikachungulia kwa dirisha hapo nikawaona wamemrukia kwa furaha Miriam mdogo wangu na kumuwaoooo! 😚🤪🫂🤗 Akayateremsha mabegi yake mkubwa ya nguo na ndani akakaribishwa.
"Kuliko mwenzangu, mbona macho mekundu kama pilipili, huchoki kulia!? Na hayo mabegi ya nguo vipi?" Nilimuuliza Miriam. Wakati huo niliwaruhusu wavulana wangu wakaendelee kucheza 'Hide and seek' 🥷🙈'moja mbili tatu komboreraaa😂'
"Yaani dada ninajuta mie, ninajuta majuto makuu. Tangu nimekutelekeza kule Hospitali na mwanangu hakuna siku niliyopata amani. Niligeuka na kuwa mtu wa kulialia tu. Hatimaye nilipokuja kugundua kuwa Sina changu ndani ya mjumba wa wale mabillionea....." Chozi na kamasi lilianza kumbubujika kama bomba la maji 🚰.
"Kwahyo!?" Nilimuuliza.
"Ninaomba unisamehe dada yangu niaomba unisamehe unipe ruhusa tusaidiane kumtunza na kumlea Ivanka..... Najuta Jamani!!" Kwikwi kwikwi😭😭😿😢🥹 Alilia kwa hisia. Nikavaa vazi la huruma nikampenda na kumjali damu yangu.
"Na Zaki mumeo vipi!? Au ndo kakaupa Taraka kisa tu nimewaletea mtoto wa kike nyumbani?" Nilihoji.
"LA! Hasha dada mpenzi. Hajanipa kwa hiari yake mimi ndiye niliyemwomba Taraka. Nimeumia sana, Nimeumia kumtelekeza mwanangu. Nilikua nikijiuliza mimi ni mama wa aina gani duniani ambaye sioni thamani ya damu ya dadangu? Sioni thamani ya uchungu wako? Sioni thamani ya mtoto? Unisamehe dadangu."Safari hii Miriam alianza kujigaragaza sakafuni akilia kwa hisia.
"Nimekusamehe mdogo wangu, apangalo Mola binadamu hapangui. Tuishi pamoja katikati ya upendo. Tusaidiane kumlea Ivanka, Malaika atakayetuletea Baraka." Nilimfariji Miriam nikamwambia mpakate mwanao mtazame tunyusi usoni, tumasikio kama popo tushavu twenye dimpozi za babake Zaki na tulips twa babake Zaki. Alitulia akafuta chozi akampakata mtoto alipomtazama vizuri anavyotabasamu 😻😇 na tumapengo twake🦷 Miriam naye akatabasam. 😍.
🤱🤱🤱🤱🤱🤱🤱
TCHAO
No comments:
Post a Comment