Monday, November 4, 2024

CULT HUSBAND




 CULT HUSBAND

(HALF AND SECRET.) 

Baada ya harusi yetu mie Sophy na Mume wangu Nebokadreza tulielekea ndani ya chumba cha mapumziko yaani MASTER BEDROOM. Siku hiyo nilikua ndani ya Shera zuri jeupe na Nebo alikua ndani ya Suti maridadi nzuri nyeusi. Chumba chetu kilijazwa zawadi za kila aina. Siku ile nilikua nimechoka sana maana nilicheza sana Muziki  ukumbini hadi kufika saa Saba usiku, kwa ufupi mambo yalikua mengi.
   
        "Sophy naomba tupeane haki ya wanaondoa."Nebo Mume wangu aliyekua akinipapasa papasa sehemu mbalimbali za mwili wangu aliniambia macho yake yakiwa yamejaa hisia na matamanio. 

        "Sweet heart."Nilimwita kichovu.

       "Naomba nipumzike nimechoka sana. Niache nilalae Leo kesho tutapeana haki yetu." Nilimwambia macho yangu yakiwa yamejaa usingizi na pia yalikua mazito.

      "Sophy natamani Daring." Alinibembeleza.

      "Vumilia Kwa Leo Daring kesho utafurahia." Niliongea kwa sauti ya kuvutwa na usingizi. Kweli Mume wangu aliziheshimu hisia zangu akauchupa kitandani tukalala tukiwa tumekumbatiana kumbikumbi mithilia.

      'Ngaaa ngaaaa ngwaaaaa.' Saa mbili asubuhi nilishituliwa na sauti ya kilio cha mtoto  mchanga chumbani kwetu. Nikafumbua macho na kutazama kule sauti ya kilio ilikotokea. Jambo la kushangaza Nilimuona Mume wangu Nebo akiwa amempakata mtoto mchanga. Nikafadhaika, moyoni nikajiuliza maswali yaliyokosa majibu 'Ninaota?' 'mtoto ameingizwa saa ngapi ndani ya Master bedroom?' 'Mtoto wa nani huyu?' 'Mbona sielewi?.' Nikadamka na kuketi juu ya kitanda nikimshangaa Nebokadreza.

        "Nebo mtoto wa nani huyu na ameletwa vipi chumbani kwetu?" Nilimuuliza nikimshangaa shangaa.

      "Nitaeleza Sophy?"Alinijibu Kwa ufupi.

    "Tafadhali eleza nazidi kufadhaika."Niliongea.

    "Sophy mtoto huyu ni mtoto wa dada yangu wa kambo.

      "Mbona hujawai niambia kama una dada wa kambo mwenye mtoto tena mtoto anaonekana ni kama ana miezi mitatu tu?"

       "Sophy nilikua nataka kukwambia kila siku lakini imetokea hivi."

        "Kwanza naomba unieleze mtoto huyu ameingizwaje ingizwaje ndani ya chumba chetu na Dada wako kambo yupo wapi?"

        "Mimi pia nimeshangaa nisijue Dada amekimbilia wapi baada ya kumbwaga mtoto wake."

      "Ataanzaje kufanya hivyo? Mama mwenye akili ataanzaje kumbwaga mtoto wake na kukimbia?" Nilimuuliza, akaniambia:

    "Dada yangu Sarah ana changamoto ya ubongo Kuna wakati akili zake ukaa sawa na Kuna wakati hutoweka kwa hiyo tendo la yeye kumbwaga mtoto ni kwamba akili zake hazipo sawa. Nina Imani atarejea tu." Alijieleza nikamsogelea yule mtoto alikua ni mzuri wa kupendeza. Nikamuuliza jina la yule mtoto akaniambia anaitwa Carolina.

       "Naomba tusaidiane kumtunza na kumlea "Aliniambia.

     "Ni vizuri umtafute mama yake hadi apatikane baada ya hapo tutaangalia namna gani ya kumsaidia Carolina na Sara mwenyewe," Nilitoa wazo.

      "Wazo lako zuri Sophy lakini nipe ahadi ya kutomtenga mtoto wa Dadangu"Aliniomba

      "Sintamtenga nimampenda pia Lakini ni vizuri uwe muwazi, usifiche jambo ulitakiwa kunipa taarifa hapo awali kama unaye dada na ni mwenye mtoto" Moyoni nilijilaumu sababu sijamjua vizuri Mume wangu Nebo. Tumejuana Miezi miwili iliyopita tena haraka haraka akaangaikia mambo ya harusi na sherehe ndogo ambayo imetimia.

*****************

 Nikachukua jukumu la kumlea Carolina mtoto wa Sara na huyo Sara  wifi nisiyemfahamu sijapata kumuona akija au akiletwa nyumbani. Siku zilikatika, miezi ikakimbia Sophy nikawa mama mlezi wa Caro.  Nikimfulia nguo, nikimuogesha, nikimwandalia uji na kumpatia maziwa, wakati mwingine nilimmpeleka Clinick na kumbembeleza alipokataa kulala, lilikua jukumu langu. Ilikua kazi ngumu lakini nilijitahidi kadri ya uwezo  wangu.

       Basi siku moja niliamua kufanya usafi chumba chetu Master bedroom. Nikazipangua pangua nguo safi na chafu zilizokuwa ndani ya kabati na mabegi ya nguo za Mume wangu. Nikaiona picha moja ambayo iliniita wasiwasi, ile picha ilidondoka chini ya miguu yangu kutoka kabatini. Picha ile kubwa ilimuonesha Mume wangu Nebo akiwa amemkumbatia mwanamke mjamzito mwenye kadirio la miaka ishirini na tatu Tena Mume wangu alionekana akiwa anampiga 😘 kiss shavuni, nilipomtazama sana yule mwanamke niligundua anafanana sana na Carollia mtoto ninayemlea.

 Moyoni nilihisi vibaya lakini nikajiambia 'Ngoja Nebo akuje nimuulize juu ya mwanamke nimuonaye pichani.' Hasira zilinivaa kooni, wivu ulinibamba nikajiuliza ni nani huyu mwanamke mjamzito baya zaidi Nebo anampiga kiss  akiwa mtupu wa mwili? Sikupata jawabu, bahati nzuri Nebo aliwasili jioni nikamuuliza baada ya kumuonesha ile picha


      "Ni nani huyu uliyemkumbatia pichani?" Alipoiona ile picha hakuonesha darili za wasiwasi au kushituka 

    "Huyu ndiye Sara Mama yake Carolina"Alinijibu.

    "Sasa mbona hujawai kunionesha hii picha?"

     "Nisamehe Sophy bahati mbaya Leo nina taarifa mbaya kuhusu Sara mama yake Carolina amekutwa amekufa baada ya kugongwa na Gari lililomsaga vibaya asitambulike,"

     "Oh! Masikini lakini Nina swali jingine mbona kwenye hii picha umemkumbatia Sara akiwa nusu utupu?" moyo wangu bado ulikuwa na mashaka juu ya ile picha.

      "Kama nilivyokueleza Sophy Sara alikua na matatizo ya akili kwahiyo Mimi ndiye  nilikua mstari wa mbele kujitolea kumsaidia jambo lolote lile,"Alijitetea.

    "Hata uwe mpumbavu wa aina gani hauwezi kupiga picha na Dada yako aliye nusu utupu." Nilifura.

      "Kwahiyo hauniamini mke wangu?"Aliniuliza,

       "Nitaaminije baada ya kuiona picha hii? Nebo kama Kuna jambo unanificha naomba unizindue Ili nikujue zaidi.

      "Kama hauniamini sawa tu Sophy lakini tambua huyo alikua ni dada yangu mwenye tatizo la uwendawazimu" Alijieleza.

Sikupendezwa na Lile jibu, nilichokifanya ni kumbeba  Carolina nikatoka nje nikiwa na hasira, nikamuacha Nebokadreza pekee yake pale sebuleni nikaeleka Magogoni Beach karibu na Soko la Ferry mana nyumba yetu ilikuwa pale Kivukoni karibu na Kigamboni.

     'Kuna jambo geni ambalo Nebo ananificha?" Nilijiuliza nikiwa pale Beach nayachezea chezea maji Kwa kutumia miguu yangu, nilimpakata Carolina aliyekua ametulia akiyafyonza maziwa yake niliyomwifadhia kwenye kopo.

       'Tangu nimeolewa na huyu mwanaume hakuna jambo ambalo ameniweka Wazi kuanzia ujio wa Carolina na hizi picha alizomkumbatia mama yake Carolina. Je, huyu mama Carolina ni nani kwake? Kweli ni dada yake wa kambo na kweli Sara alikua na matatizo ya akili?' nilivamiwa na Lundo la mawazo.

       Mmh! Nitamuaminije!?" Stress zilinisumbua.

       "Hallow!" Ghafla nilisikia sauti ya mwanamke ikinishitua kutoka mawazoni. Nikamtazama yule mwanamke hakuwa pekee yake aliongozana na Binti mwenye kadirio la miaka saba hivi.

     "Hallow!" nlimwitikia sio mtu mzima sana Kwa kumtazama ana kadirio la miaka therathini na mitano.

    "Binti huyo ni mzuri." Nilimshangaa alipoanza kumsifia Caro.

     "Asante Dada," Nilimwitikia.

      "Umeolewa na Nebo," Swali lake lilinishitua kidogo.

     "Ndio. Je, wamjua?" Nilimuuliza.

      "Nisimjue Nebokadreza, hata huyu Binti uliyembeba hajazaa na wewe."Alinishangaza lakini ilibidi nikubali kila kitu ili nimjue zaidi Binti yangu Carolina.

     "Ni kweli sijazaa na Nebo lakini  je, unamjua?"

     "Najua kila kitu amekudanganya kwamba huyu mtoto ni wa Dada yake Marehemu Sara, hakuna ukweli hapo Carolina sio Mjomba wake bali ni mwanaye aliyezaa na marehemu Sara.Toba! Nilishituka huyu Msamaria mwema kunipa taarifa za kushangaza.

       "Angalia kinywa chakoDada kisije kikakuponza unaongea ukweli au unatafuta kitu kutoka kwangu?" Nilijaribu kuwa mkali Ili kumtisha yule Dada,

     "Ukweli ndio huo mwanaume unayekaa naye ana siri nyingi pia ni mdanganyifu sema wewe  haumjui vema." Aliongea Kisha akaanza kuondoka.

    "Tafadhali usiondoke nina maswali ya kukuuliza" Nilimpazia sauti asiondoke.
   
     "Tutaonana siku nyingine, siku tukionana nitakupa taarifa zaidi kuhusu Mumeo" Aliongea akiniacha nikiwa nimechanganyikiwa. Haraka haraka nikafanya kuondoka pale Magogoni Beach nikaeleka nyumbani nilipomuacha Nebo.

*****************

     "Tafadhali nieleze ukweli Carolina ni mwanao au ni Mjomba wako?" Niliongea Kwa hasira.

      "Umepatwa na Nini Sophy ina maana hauniamini kila nikikueleza kuhusu Carolina au mamaye  Sara?"

       "Nitakuamini vipi mwanaume usiyeeleweka. Leo hii nimekutana na mwamnamke mtu mzima nisiyemfahamu ameniambia unanificha Carolina sio Mjomba wako bali ni mwanao."Nilipomwambia vile alishituka sana,  alitetemeka pia, macho yake yakiwa hayana amani alishindwa kunitazama.
    
      "Nieleze ukweli Mume wangu, ukweli pekee ndio utatuweka salama. Je,  nikikataa kumlea  huyu Binti ni nani ambaye atajitolea kumlea?" Nilimuuliza akiwa na wasiwasi 

        "Ok. Daring nitakueleza." Alianza kuongea.
         
         "Carolina ni mwanangu nilizaa na Sara kwa bahati mbaya sikumpenda Sara ila sema ujana una mambo mengi." Alijieleza, nilimsikiliza.

     "Sijawai  kumpenda Sara japokua alikua ni mpenzi  wangu niliachana nae Ili nikuoe wewe." Aliongea
    
     "Sasa kwanini ulinificha Nebo?" Machozi yalitamani kunitoka.

      "Niliogopa nikikumbia ukweli utaniacha na kunikimbia. Nakuomba umkubali Caro kama mtoto wetu sababu anahitaji malezi ya Baba na Mama."Alinibembeleza.

       "Nitaishi vipi na mwanaume ambaye ananiambia habari nusu nusu, Nebo kwanini usiniambie ukweli? Kwani ukiniambia ukweli nitajinyonga?" Safari hii chozi la hisia lilinidondoka.

    "Nisamehe Sophy sikua na Jinsi pia niliogopa kuchwa na mwanamke nimpendaye." Alijitetea.

       "Hapana Nebo. Mke na Mume hawapaswi kufichana mambo  madogo madogo na makubwa pia."Nililia Hadi kwikwi ilinitoka. Sikutaka tena kuishi naye. Haraka nikamkabidhi mtoto wake. Nikaingia chumbani, chumbani kwetu na kuanza kupangilia pangilia nguo na vikorokoro vyangu baada ya kuridhika na ubebaji wa vikorokoro vyangu nikatoka na kumuacha Nebo.

      "Unaenda wapi Sasa?" Aliniuliza.

       "Ninaondoka, siwezi kuishi na mtu anayeniumza moyo."

      "Nisamehe Sophy, nisamehe Dear." Alinishika mkono Ili kutoniruhusu niondoke.

        "Never, let me go." Nilijitoa mikononi mwake nikaondoka pale ukumbini, nikaichukua Gari yangu na moja kwa moja nikaeleka kwenye nyumba niliyoachiwa na wazazi wangu waliofariki zamani kidogo.

************

Bahati nzuri mara baada ya kuondoka kivukoni na kuelekea Mbezi Beach niliona haitakua vema kukaa tu bora nifanye shuhuli yoyote. Binafsi ninapenda sana mitindo na fasheni, ninaujuzi wa kushona mavazi ya kila aina. Basi nikaanza kujibidisha Kwa ushoni wa nguo za wanawake. Siku si nyingi Mume wangu Nebo akaanza kuja nyumbani kwangu akiniomba msamaha Kwa ubaya alionitendea yaani kuficha siri. Sikua tayari kumkubalia na yeye alikazana sana kuja mara kwa mara nyumbani kwangu lakini bado tu niliushikilia msimamo wangu wa kutokurejea tena nyumbani kwake.



Lakini baada ya kupita miezi mitatu alikuja na mtoto wake Carolina mtoto alikua yu mchafu sana amekonda na kudhoofika. Nilipomuona mtoto jinsi alivyo tofauti na miezi mitatu iliyopita huruma zilinivaa.

        "Sophy. Mtoto anakulilia kila siku, mtoto hawezi kula au kulala kila siku analitaja jina la Mama mama mama." Nebo aliongea

     "Tafadhali Sophy ninaomba urudi nyumbani mtoto anakuhitaji."Alipigia magoti na kuniomba.

     "Nina majukumu mengi ya kiofisi pia ninapata tabu sana kubaki nyumbani kumuangalia mtoto, ninaomba urejee nyumbani tusaidiane kumlea mtoto wetu."Alinibembeleza.

       "Sawa nitarejea lakini usithubutu kunificha jambo, siri mara nyingi hutatiza moyo ,"Nilimwambia.

    "Sintarudia tena My Daring."Alitoa kiapo. Basi wiki iliyofuata nikarejea nyumbani tukaungana kumlea Carolina.


MIEZI MITATU BAADAE,

Ninakumbuka siku Moja Nebo Mume wangu alipoondoka nyumbani kuelekea kazini nilitoka nje ya ubalaza kwa lengo la kupuguta deki. Nilipoufungua mlango macho yangu yalitua juu ya bahasha moja kubwa yenye rangi nyeupe ikiwa imeachwa chini ya mlango. Nikaiokota kisha nikaifungua ndani ya ile bahasha nilikuta kijikaratasi kidogo kilichoandikwa nambari za simu na nambari ya nyumba ya mtumaji ile bahasha  pamoja na ilo nilikuta picha moja kubwa ambayo Mume wangu Nebo alionekana kuwakumbatia watoto wawili pacha wenye umri wa miaka mitano.

 Sikuielewa ile picha lakini moyoni nilijiambia ni vizuri nipige simu kupitia nambari zilizoachwa kwenye ile karatasi ambayo pia ilikua na nambari ya nyumba ya mtumaji bahasha

    "Hallow!" Mpokeaji aliita baada ya kupokea simu.

     "Sophy hapa, mke wa Bwana Nebo. Je, ni wewe ndiye uliyeiacha bahasha kubwa rangi nyeupe mlangoni kwangu?" Niliuliza,

     "Oh! Sophy, niite Amanda." Nilisikia sauti ambayo haikuwa ngeni masikioni mwangu, ni ile sauti ya mwandada niliyekutana naye Beach miezi kadhaa iliyopita,"

      "Ndio, ninakukumbuka."Nilimjibu.

       "Vema, basi ninahitaji uje tuongee mengi ambayo bado kuyajua kuhusu Mume wako Nebo."Amanda aliongea na kunishitua Mtima.

      "Mengi yanayomhusu Nebo?"Nilimuuliza.

      "Ndio Dear, fanya haraka ujiokoe huyo sio binadamu huyo ni mnyama mkali wa porini. Atakumaliza taratibu kama Zimwi likujualo halikukuli likakumaliza" Amanda alinishitua zaidi.

      "Poa basi ngoja nijiandae." Nilimjibu kisha akaniomba niikalili nambari ile ya nyumba aliyoiandika kwenye karatasi. Akaniambia nipande magari yanayoenda Temeke nishukie Tandika, Mie nae Kwa kiherehere nikambeba Carolina wangu nikakodi Uber tukaelekea Tandika tulipofika nikaisaka nyumba husika sikupata changamoto kuipata.   

                     *******************

 Hao watoto pacha uliowaona kwenye picha ni watoto wangu na EX HUSBAND WANGU Nebo."Nilishituka niliposikia kuwa Mume wangu Nebo aliwai kuwa na mke hapo zamani. Kikombe Cha tangawizi  alichonipa ninywe almanusura kinidondoke na kuanguka

      " Usiogope Sophy, unahitaji kumjua zaidi Nebo ndipo ufanye maamuzi ya kuishi nae au kuachana nae."Nilimsikiliza.
 
     "Mumeo Nebo ni mshirikina ambaye amejiunga na chama cha wachawi chama ambacho kinamtaka akifanikiwa kupata mtoto wa kiume lazima amtoe kafara. Mimi nilizaa naye watoto wawili mkubwa ni yule uliwai kunioa nae  Magogoni Beach na Hawa pacha ni wangu pia wote ni majike,"Nilimsikiliza.

    "Sheria za wachawi alioungana nao Mumeo zinamkataza kuwatoa kafara watoto wa kike, Sheria zao zinaamini kuwa Ili nyota yake Nebo Ing'are na  na kupendeza ni lazima atoe kafara ya mtoto wa kiume ambaye anamtafuta Kwa udi na Kwa vumba" Maneno yale ya kushituka moyo yalinishangaza nami sikusita kumuuliza ameyajuaje yote hayo. Akaniambia,

    "Nadhani umewai kumsikia akimtaja Sara mama yake Carolina?"nikamjibu ndio ninamfahamu kupitia picha.

    Akaniambia "Nebo ana siri nyingi nzito ambazo hataki kukwambia wewe. Jiulize kwanini anatafuta kumpata mtoto wa kiume li amtoe kafara? Lengo lake ni kupata Mali za kishirikina, pesa na Utajiri wa kishirikina.Sara alikua ni mkewe mara baada ya kuachana na mimi ambaye alinitimua kwasababu sikumzalia watoto wa kiume na baya zaidi niliishi naye pasina kuzijua tabia zake mbaya. Sikujua kama amejiunga na chama cha washirikina miaka yangu yote saba ya kuishi na Nebo nilizubaa bure."

     "Sara ndiye aliyekuja kuzigundua tabia za Nebo, alipogundua kuwa Nebo amejiunga na chama cha watoa kafara '(Cult)  alimwambia ukweli na akatamka waachane. Nebo Kwa shingo upande alikubali kwa shart moja kwamba Sara amzalie mtoto kwanza. Sara alipojifungua na Nebo alipokuja gundua kwamba mtoto aliyezaliwa sio wa kiume haraka haraka akamuua Sara aliyeigundua siri, siri yake baadae akakuoa wewe na kukupakazia mtoto Carolina  ambaye alikudanganya akwamba ni mtoto wa Dada yake," Maneno yale yaliniogopesha na kunitetemesha. Kumbe Mume wangu Nebo ana siri nzito masikini mimi Sophy nimeolewa na Nyoka mwenye sumu Kali.

      "Duh! Kwahiyo Nebo Mume wangu ni mshirikina pia ni muuaji?" 

    "Jawabu unalo na usithubutu kumwambia haya tunayoyazungumza siku ukija kumwambia mwenzangu tumekwisha lazima ataanza kukuua na kuniua Mimi pia. Usimweleze kitu maana hata yeye hajui kama Mimi nimeigundua siri yake," Amanda aliongea.

      "Oh! Amanda kwahiyo unataka kuniambia Mimi sio mke wa kwanza wa Nebo?" Nilimuuliza Amanda.

        "Nebo ataendelea kukudanganya Ili ayatimize matamanio ya moyo wake. Kama Mimi ni mke wake wa kwanza, Sara wa pili na wewe utakuwa wa ngapi hapo?" Kuwa makini mwanamke mwenzangu."Alinifumbua akili.

     "Nilikua ninakufuatilia sana, moyoni nilikua ninakuonea huruma  maana hauzijui siri alizonazo Nebokadreza, huruma zangu ziliniambia ipo siku moja atakufanyia ubaya. Kama aliweza kumwangamiaza Sara wewe ni nani ambaye atakuacha iwapoa atakuja kugundua kuwa umeisha zingudua siri zake?" Amanda alinipasua kichwa.


*****


Nilimshukuru Amanda Kwa taarifa aliyonipa kuhusu Nebo, niliposhika njia kuondoka Tandika na kurejea nyumbani kwangu Kivukoni mawazo yalinisumbua sana, nilikua na huzuni baada ya kuzijua siri zake Nebokadreza. Kumbe aliwai Oa! Kumbe ni mshirikina anayeshirikiana na wachawi! Kumbe ni muuaji! Kumbe lengo la kunioa Mimi ni kupata mtoto wa kiume Ili amtoe kafara! Jamani nilichoka mie🧟😡😭

   Ghafla nilianza kuona kizunguzungu kichwa changu kilichoka. Kipindi icho nipo Barabarani ndio narejea nyumbani kwangu Kivukoni. Uwii! Kizunguzungu kilinipanda zaidi, nikahisi kudondoka chini nikapoteza fahamu na kutokujua Nini kilichoendelea,

*********
     Nilikuja kuzinduka na kushituka nipo Hospitali ya Temeke pembeni yangu alikuwepo DAKTA aliyeonekna kutabasamu mara baada ya kuniona nimezinduka.

      "Pole sana binti Wasamaria wema walikuleta hapa Hospitali wakidai wamekuokota barabarani ukiwa hauna fahamu, Dakta aliongea

    "Pole Sana, mawazo ndio yaliyokupelekea uanguke na kupoteza fahamu kwahiyo punguza mawazo."Alinishauri.

     "Asante bwana Dakta umeyaokoa maisha yangu. "Nilimshukuru,

    "Sister katika kukupimapima afya yako, vipimo vilionesha una mimba changa yenye mwezi mmoja."

      Jesu! Nilishituka  'nina mimba? Mbona hatari' nimetoka kuambiwa habari mbaya kuhusa Nebo alafu Leo naambiwa Nina mimba! Uwii! nimekwisha mie! Nikawaza, sijui niitoe? Nikawa njia panda
****

   Niliporuhusiwa kurejea nyumbani nilikuta Nebo ameketi SEBULENI anangalia Televisheni akanitwanga swali "Mbona umechelewa kurudi ulikuwa wapi?"Macho  yalipomuona huyu mwanaume moyo ulianza kumchukia

    "Nimetoka Hospitali,"Nilimjibu Kwa ufupi maana sikumfurahia.

    "Hospitali ulienda kufanya Nini?"Nilijua tu ataniuliza lile swali.

   "Sikiliza Nebo Hospitali niliambiwa Nilikuwa nina mimba"Nilimjibu yule mdadisi.

    "Ulikuwa una mimba, mbona sikuelewi hiyo mimba unayo au hauna"  sikutaka kuficha ficha mambo nikampa vidonge vyake.

   "Nimeitoa mimba"

   "Nini?" Kama shoti ya umemem aliamka pale alipoketi akanisogelea macho pima mfano wa mjusi aliyebanwa mlangoni. akanipigia kelele.

   "Umeitoa mimba?" Sauti yake kali iliambatana na mate kumchuruza.

    "Ndiyo nimetoa mimba"Sikutetereka nilitaka kumuona anataka kufanya Nini.

    "Pumbavu mkubwa wewe" Ghafla akanirukia na kuninasa ubao wa nguvu shavuni kwangu. Uwii! Niliona nyota nyota ✨✴️niliona kizungu zungu na niliona Dunia ikiniangukia.

     "Mjinga mkubwa wewe unaanzaje kuitoa mimba yangu haujui kwamba watoto ni wenye faida?"Aliongea Kwa hasira usoni,

      "Faida eeh! Faida ya kuzaa na Amanda watoto watatu Kisha umtekeleze? Sababu tu ni watoto wa kike. Faida ya kuzaa na Sara Kisha unidanganye kuwa alikua ni ni dada yako kumbe ni Mkeo wa pili.

  "Ah! Kumbe ushazijua siri zangu? Sasa leo utanikoma Malaya Jibwa wewe"Alinisogelea ili apate kunipiga haraka bila kupoteza muda nikakimbilia  kuufungua mlango mkuu wa sebule Ili nimtoroke  nilipoufungua tu mlango nikakutana uso kwa uso na wanaume wawili waliova nguo za kipolisi. Nebo aliyenikimbiza hadi pale mlangoni alikutana na ma bwana polisi pia.


    "Bila shaka wewe ndiye Bwana Nebo?"Polisi mmoja mwenye umbo Nene mrefu kiasi aliuliza

  "Ndiye huyu Bwana polisi "Niliongea kwa kubwata.

   "Naona mnakimbizana kama Paka na panya na nyumba ina amani kweli?"POLISI aliongea na kumsogele Nebo aliyeganda pale mlangoni.

   "Upo chini ya ulinzi Bwana Nebokadreza Jeshi la POLISI limefanya uchunguzi na kuja kugundua wewe ndiye uliyemuua Bi. Sara,"Bwana POLISI aliongea.

    "Mimi , Mimi, Mimi"Nebo aliishiwa kauri pingu zikakamata mikono yake akasombwa sombwa Hadi kwenye gari ya POLISI  akiniangalia Kwa huzuni na wasiwasi.

     ***************

Amanda alinitembelea baada ya siku tatu mbele tukajifungulia chupa ya Wine tukajimiminia Kinywaji chetu tukajipongeza

    "Hongera sana Sophy Kwa ujasiri uliouonesha Nebo atahukumiwa kunyongwa au hukumu ya MAISHA Jela. Mtunze Carolina pia itunze hiyo mimba yako changa" Amanda niliyemzoea ghafla aliniambia

     "Nilichanganyikiwa Amanda, nilichanganyikiwa. Nilitaka kumpima Nebo Kwa kumzingua nilipomwambia Mimba imetoka. Nilitaka kuona Reaction yake angelinichukuliaje. Lakini ninashukuru Mungu yote yamepita yote yamepita na MAISHA yanaendelea. Niliongea na Amanda aliyetabasamu.tukaendelea kujipigia chiazii glass zetu🥂🍾🍷




************************

TCHAO 🍾





No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...