Saturday, November 30, 2024

MY STEP MOTHER

 


BABA NA MAMA👨‍👨‍👦 WALIPOAGA DUNIA⚰️ MAMA WA KAMBO👩‍👧 ALlJITOLEA KUNILEA 🧑‍🍼NILIPOFIKISHA UMRI WA MIAKA 18🎉🎊🎂NILIMFUKUZA NYUMBANI🏘️ KAMA UMBWA KOKO🐕🦴.

         Mama yangu alipokua hai alinidekeza na mie nilideka nikapendeza na kudeka kama Yai🐣 lakini Yai nalo lina mwanzo na mwisho, mwisho mwema ni pale Yai linapoleta kilicho bora zaidi na mwisho mbaya ni kuoza, kutoa shombo au kuitwa Yai viza. Ndo' hivyo basi mama yangu Agness akaitwa mbele ya Mola🌨️ nikalia mie na kuomboleza.😿
 
      Nilipokua na umri wa miaka kumi na moja, bado kinda kindaki mie Editha nilimwona Baba akimleta mwanamke nyumbani🧍‍♀️kisha akamtambulisha kwangu akisema Judith atakua ni Mama yangu. Sikumfurahia Judith, nilichukia sana, sikumpenda wala sikupenda aishi nyumbani kwetu. Nilimwona Judith kama shetani, 👹 mwanamke. Bora kuishi pekee yangu kuliko kuishi nikimtazama step Mom Judith.

      Ingawaje Step mother alinipenda pia alionesha darili za kunikubali lakini mie moyo wangu haukutaka hata kumsikia. Kila niliporudi Shule nilijifungia chumbani kwangu (Tena niliubana mlango Kwa kufuli 🔐🗝️) nikalia humo na kumkumbuka Mama yangu Agness, mama aliyetwaliwa na Mola.🪦

     Baba yangu alinisihi nimpende Judith kama Mama yangu mlezi 👨‍🍼lakini hakuna nguvu iliyoniigia kichwani kwangu kukubaliana na kauri za Baba. Lakini siku Moja, siku ambayo kila kitu kilibadilika hadi upendo wangu ulihamia Kwa Mama wa kambo ni siku ambayo  nilikuja kushituka mara baada ya kuota ndoto mbaya (Nightmare) kuhusu Mama yangu Agness.

       Mama alinitokea Ndotoni kama Malkia wa Ibilisi shetani (Devil's👿 Queen 👑) Mama alionekana amevalia vazi refu la rangi nyeusi tiii ⬛Tena kuukuu linalotisha na kuogopesha. Kichwani alivalia Crown ya Malkia wa shetani, 🤴mdomoni alionekana ana meno marefu🦷 kama pembe za ndovu🐘 na ndimi👅 yake ilikua ikiwaka moto 🔥na kutema damu nzito 🩸yenye sumu.

        Kucha💅 za mama yangu zilikua ndefu miguuni na mikononi, 🦵🖐️mkono wa mashoto aliushika upanga 🗡️mrefu uwakao moto, macho yake yalitisha Kwa wekundu wa pilipili zaidi ya hilo masikio yake yalifanana na masikio ya punda 🐴 juu ya kichwa alitoa pembe za mbuzi 🐐. Niliogopa sana.

      "Nimekuja kukuchukua."Mama mzazi aliniambia ndotoni.

      "No, no, no, Mama sipo tayari kuja kuishi huko kwenye moto wa Volcano 🌋💥" Nilimpiga Mama mzazi.

     "Nataka kuishi na wewe mwanangu Bena kubali tafadhali."

      "Hapana Mama, hapana. Ninahitaji kuishi na Baba." Nilimpiga Mama yangu kwenye ndoto💭😴 lakini kupinga kwangu hakukumsaidia nikamwona akipaa Kwa mbawa ndefu zinazotisha, akanifukuzia Hadi pale nilipoganda kama sumaku, akanikaba shingo yangu Kwa mikono yake iwakayo moto Kisha akauyanyua upanga wake wenye makali kuwili haraka bila kupoteza dakika alihitaji kuikata shingo yangu. Hapo ndipo nikashituka kutoka usingizini 😴💤na kuanza kupiga kelele zilizomshitua Mama yangu wa kambo aliyekua Jikoni akikosha vyombo 🧺🏺🍲🫖

       Judithi Mama yangu aliposikia sauti ya kulia 😰🤧kwangu akaacha kukosha vyombo  na kukimbilia chumbani kwangu alikonikuta ninalia Kwa sauti kuu kama vile nimepagawa.wakati huo Dady alikua bado hajarejea kutoka mishe zake.👷🔨 Mama akaufungua mlango niliouwacha w>azi siku ile, akaingia na kuketi kitandani Kisha akanishika mikono yangu taratibu Kwa upendo wa dhati.🌹

      "You are okay now dear.....it's ok, you are safe. Please stay safe."Alinifariji.

      "Hapana Mama ninaogopa.😨" Akachukua upinde wa kanga yake aliyojifunga kisha akanifuta chozi langu lililokua likinitoka Kwa kilio Cha kwikwi.😿

     "Upo salama mwanangu, usiogope, mikono salama." Ni kama vile Mama alilijua tatizo langu akanikumbatia🫂 na Mimi nikamkumbata kwa nguvu sana maana Kwa woga ule nilihitaji faraja isiyochuja

         "Ndoto Mama, ndoto mbaya. Sijawahi mwita Judithi jina la Mama lakini siku ile Nilimwita na pia nikauona upendo wake, wema, uzuri na faraja tele. Kwa hakika moyo wangu ulisikitika sana, kwanini nilikosa upendo wa Mama wa kambo. Siku ile nililala pamoja na Judithi Step mother, Nilimkumbatia Kwa nguvu zote na woga wote uliinikatika.

       Ikawa hivyo basi ile ndoto nzito niliyoiota ikageuka upendo mzito ndani ya familia yetu Judithi akageukia na kuwa Mama yangu, faraja yangu, utulivu na amani yangu. Nilianza kumpenda pendo la kupendeka. Tukicheka wote, tukitaniana na kucheza kama watoto. Uzuri Mamangu wa kambo alinithamini, alinijali kama mwanaye wa kunizaa pia alinihesabia kama mwanae mpenzi.

         Tulipoenda Beach ⛱️ mie, Baba na Judithi pia aliambatana nasi. Tukayachezea maji Kwa furaha 🚣🏄‍♀️🤽‍♂️ Tulipoingia Mall 🏬 au Supermarket🛒 tulinunua kila kitu ambacho niliwaomba waninunilie. Shopping🎁🏪 ndo' usiseme Step mother alinipendelea nichague kila kitu nilichopendelea kuchachambua achilia mbali Hotel na Restaurant 🏨🛋️ nilikula hadi nikaanza kuurejesha ule mwili wangu ilioanza kudhoofu kutokana na msongo wa mawazo juu ya kifo cha mama yangu Agness.

         "Lakini Jamani Dunia ni Mali ya Mungu wanadamu tumepewa kuketi Kwa muda wa siku, saa🕦 na nyakati. Baba yangu akaja kuugua Home Kali 😷🥵 ya Maralia🦟 tulipompeleka Hospitali 👨‍⚕️🏥 dawa 💊 alizopewa anywe zilimkataa na kumsaliti, hatimaye baba mpenzi akaanza kukiona kiza na Malaika🧚 mnyofoa roho za waja wa Mola akaja kuibeba roho ya baba yangu na baba yangu akapumzika pahali Pepa peponi. Sie wawili tulilia na kuomboleza.😭😿

     :::::::::::::::::::::::::☠️::::::::✝️::::::::

Alipokufa⚰️ Baba yangu ndugu zangu wote upande wa Baba walimtaka Step mother afungashe kila kilicho chake na aondoke haraka iwezekanavyo pale nyumbani, 🏘️ pamoja na Hilo Mimi pia sikupendelewa ndani ya koo au familia zao, nilionekana kama mkosi, kizingiti na zigo lisilobebeka. Inakuaje Mama atoweke na baba atoweke tena ndani ya muda mfupi wa maisha⁉️  Hilo kwa ndugu na ukoo lilikua ni fumbo zito.

        Ndugu wa pande zote yaani kwa marehemu baba na kwa marehemu Mama walikataa kunipokea kwa hiyo walinitaka nichukukuliwe na kupelekwa nyumba za kuelekea watoto yatima (Orphanage) Hilo nalo sikulipenda tena nililipinga kwa nguvu ya mikono yangu yote miwili ingawaje bado nalikua ni kinda wa kuyajua mema na mabaya.

       Judith akasimama kidete naye akanitetea akisema: 'Yupo tayari kuishi na Mimi ndani ya nyumba aliyotuwachia marehemu Baba.' Ndugu walimpinga na kumzodoa wakimkashifu Kwa kumwambia hataki kurejea Kijijini kwao kulikojaa umasikini dhiki na njaa ya maisha, walihisi Judithi analeta visingizio lakini uzuri wa Judithi alinitetea nisiende kulelewa nyumba za watoto yatima.

      Maisha mapya yalianza mie Step daughter Editha na Step mother Judith tulianza kuishi katikati ya upendo na mapenzi makuu. Kila niliporejea kutoka Shule nilikuta chakula kimeshaandaliwa, nguo zangu safi tayari zimeshafuliwa na kupigwa pasi, pea  za socks na viatu🧦👞🥿 vilinukia marashi na manukato ya Pemba na Unguja🏝️🗾 kitanda changu haswa Bed mattress zilibadilishwa. Makusheni mapya na Pillow safi. Kila kilichokuwa kipya na kizuri nalifanyiwa basi mie nikapendeza na kunawiri afya yangu. Mama wa kambo akanipenda na kunilea kwa furaha.


BAADA YA KIFIKISHA UMRI WA MIAKA KUMI NA MINANE (18).

     Baada ya kufikisha umri wa Miaka kumi na minane nilihitimu kidato cha sita kisha nika aply kwenda kuchukulua Degree yangu Chuo Cha Dar es saalam kampas ya Mlimani. Hapo ndipo nilipofikiria Sasa napaswa kuanza kumfanyi visa, Mikasa, vitimbi na vibweka Step mother hadi aondoke pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi niliyoachiwa na marehemu Baba yangu. Lakini nikimtimua ataenda wapi!? Nilijua mie jinsi ya kumkimbiza kama kuku🐔🐓.

       Siku ya Birthday 🎂 🎊 yangu, siku njema iliyoonekana asubuhi, Judith mama yangu aliniandalia keki🍰🧁aliyotumia masaa kadhaa kuandaa Kwa bei gharama na kwa nguvu zake zote, kwa hakika mama alinijali sana, alinipenda na kunithamini, alinichukulia kama mwanaye wa kunizaa na sio Step daughter. Alinisikiliza iwe utani, ujinga au masikhara Mama hakunibagua tena alinivumilia.

       "Happy birthday 🎈 🎂 Editha, Happy birthday mwanangu. Mama Alinipongeza kutimiza miaka kumi na nane.🎉🎊

       "Thanks so much Mom, Asante." ninashukuru. Nilimwitikia mama japo sio Kwa furaha Wala Kwa tabasamu😡 Kisha nikaizima mishumaa🕯️🎂ya kumi na nane zangu, tukaikata keki 🍰na kulishana Kwa furaha. Baada ya kukata keki Judith Mamangu wa kambo akanipatia Boks la zawadi🎁💐 Waoo! Nilipolifungua lile Boks nikakutana na gauni zuri la bei gharama yeye binafsi aliniambia materia yake yamenunuliwa Arabuni na mshono umeshonwa U.S.A..We! Jamani kupendwa raha😚😽.

    "Ninakupenda sana my daughter.❤️"Mama aliniambia.
 
    "Ninakupenda sana Ma💜💗. Lakini ninaomba kuanzia muda muda huu ubebe kila kilicho chako ndani ya nyumba yangu ujiandae kuondoka. Niliongea usoni nimejaa kisirani,👺 sikumjali tena Mama yangu wa kambo.

    "Niondoke!?🤨🙄"Aliniuliza Kwa mshangao
    
    "Ndio, uondoke nimechoka kuishi na wewe pahali hapa, ninaomba ubebe kila kilicho muhimu kwako, wakati wa kuishi ndani ya nyumba hii umeisha." Bado Mama alishangaa, mdomo wazi😲.

    "Mwanangu kwanini niondoke na niondoke niende wapi!? Masikini Mama alikua njia panda.

     "Utajiju👌mwenyewe, popote unapotaka kwenda wewe nenda tu. Kusanya kila kitu chako  ndani ya nyumba yangu kisha uondoke."Niliongea usoni nimejaa kisirani sikumjali tena Mama yangu wa kambo akaanza kulidondosha chozi.😿

       "Mwanangu Mimi nilijua fika kuwa nitakuja kuishi pamoja na wewe milele, nilijua hautakuja kinifikuza sasa kwanini uniambie niondoke? Nitaenda wapi na nani atanipokea." Mama alilia kwa uchungu.

      "Mama tafadhali usinipotezee muda ingia chumbani na ubebe kila kilicho chako, Uber ipo nje inakusubiria" Nilimfokea nikaongea kama mtu serous yaani sikumtania. Kwa machozi na kilio cha Kwikwi😰😥 Mamangu Aliingia chumbani kwake akakusanya kila kilicho chake akatoka nacho Safari ya kuondoka iliwadia.

     "Ndani ya Uber Mama aliniuliza: "Sasa mwanangu Bena wapi nitaelekea Mimi? Nilijua tutapendana milele Hadi kifo kitutenganishe, tafadhali urudishe moyo wako nyuma unifikirie na pia unikumbuke ninakupenda Daring."
    
      "Makini Judithi!! Mke na Mume ndio upendana hadi kifo kiwatenge. Sio Mimi na wewe Step mother."Nilimjibu jeuri ingawaje nilijua majibu yangu hayafai hata kidogo Kwa mtu muhimu kama yule aliyekaa kimya na kulia sana pembeni ya dirisha la Gari.🪟

     "Tulifika karibu na eneo la Mwenge🔦 karibu karibu na Chuo kikuu cha Dar es saalam (Mlimani.) Mbele ya Jumba lenye Horofa tatu tulifunguliwa geti la mlango mkuu kisha tukaingia hadi ndani ya lile jengo linalong'ara kama Dhahabu hapo nikaisimamisha Uber yangu kisha nikamwambia Step mother aliyeketi nyuma chozi likimbubujika, chozi la thamani.

       "Nisikilize Mama" Nilianza kuongea. Naye alinisikiliza.

      "Nilipozaliwa Baba aliwekeza Shea 💰💱kwenye kampuni fulani inayolipa na inayofanya biashara Kwa nguvu na kwa faida kubwa"Mama alinisikiliza.👂

     "Baba aliandika Shea zile nilipaswa kupewa iwapo ningelifikisha umri wa Miaka kumi na nane, uzuri ndani ya Account yangu ya Benki bado ningali nina Mamilioni ya Shilingi."💵💹🤑💲

       "Ninakupenda na pia ninakuthamini kama unavyonipenda na kunithamini. Je, yawezekana vipi kumtenga au kumchukia mtu mwema kama wewe mama mpenzi?" Mama alianza kutabasamu.

     "Jiulize kwanini nimekuleta ndani ya mji wa Mwenge🗽🔦  kwa sababu sihitaji kukutenga uwe mbali na mimi, kukutupa sembuse  kukufukuza."Niliendelea kuongea.

     "Jumba🏚️ unaliona mbele yako ni Jumba la Horofa tatu, mama nimekujengea wewe mpenzi, ninahitaji kuishi na wewe eneo la karibu na Chuo. Tambua nimefauru kidato cha sita na nimechaguliwa  kusoma  masomo ya Sheria⚖️ Chuo kikuu cha Dar es saalam Kampas ya Mlimani. Mama sitaraji na sintapenda kuwa mbali na wewe."

      "Ma. Tambua sijakutenga na pia sijakufukuza bali hii ni Sapraizment kwako, nimekujengea mjumba Mamangu ukae pamoja na Mimi kila siku ukinipikia matamu na kunipakulia  manono na Mahanjumanti."🍜🍝🍨🍱 Niliongea na kumkabidhi Mama yangu Hati ya lile Jumba, 📃Hati iliyokua na jina lake.
  
         "Ma. Kama moyo wako wako hautaridhia kuishi na Mimi hapa Mwenge, ninakupa nafasi urejee kuishi kwenye lile Jumba alilotuachia Daring Baba" Niliongea Mamangu aliyafuta machozi yake naye akaongea:

     "Asante mwanangu, Asante kwa upendo na mapenzi bora. Nilijua kuwa Sina changu, Sina maana na Sina thamani lakini kumbe waniona mie ni wa maana. Ndigwako  my daughter (Mimi ni wako) Mimi ni wa thamani kwako. Asante my daughter ninahitaji kuishi na wewe Daring!🥰"

Ma. Alilia machozi ya furaha kisha nikamsogelea na kumkumbatia Kwa nguvu zote🫂😘. Bila kupoteza muda nikamkabidhi funguo zote za ile nyumba, tukateremka Garini na kuelekea kuukata utepe 🎀 wa nyumba yetu mpya. 



******💋😘....👩‍👦

TCHAO 





Sina la mno kuongeza naomba niishie hapo.👋👋.
      

A SARUGATE WOMAN

 



(A SARUGATE WOMAN)


MIMBA TATU 🫄 ZA DADA YANGU ZILICHOROPOKA, HATIMAYE SHEMELA ALINIOMBA NIWAZALIE MTOTO. 👼MTOTO ALIOPOZALIWA WOTE WALIMKATAA NA KUMKIMBIA. 🏃🏃

Katika familia yetu tulizaliwa wasichana wawili, mimi Shelidani na mdogo wangu Miriam. Utotoni tulipendana sana na ukubwan tulipeana ahadi iwapo Mola atatujalia ndoa na familia zetu tutasaidiana kuwalea na kuwatunza watoto wetu. Basi maisha aliendelea. 
 
      Maisha ni Safari ndefu, Miriam mdogo wangu alikuja kupata mwanaume mmoja 🧑‍🦯kutoka kwenye familia na ukoo wa matajiri 🪙🥇💎🕌💰wakafunga harusi nzuri ya bei gharama. 👰Mume wa mdogo wangu aliitwa Zakaria ama kwa kifupi alipendelea tumwite Zaki. Zaki shem wangu alikua na bahati ya kurithishwa mali kutoka kwa wazazi wake. Alimiliki Viwanda na makampuni mengi, hakika maisha yao hayakua na uchache. Yalijaa Mema yaso dhiki na njaa. 

       Shelidani mimi nikaja kupata mwanaume mzuri aliyeitwa Bonie, hatukupendana ati kwa kigezo cha mali na utajiri, ukitegemea hizo mali na utajiri hatukubahatika kuwa nazo. Tuliridhika na hali zetu. Mume wangu Bonie alikua akijishuhulisha na ujenzi wa majengo mkubwa yaani Bulding constructor👷🏦🏢🏛️🏗️ wakati mie nalibaki home kama mama wa nyumbani, mara moja moja nilimwitaji Mwalimu wa ushoni na udarizi anifunde jinsi ya kutumia cherehani.

       Basi mdogo wangu Miriam alikuja kushika ujauzito🫄 ulioleta furaha kuu ndani ya ile familia ya Mamillionea lakini baada ya miezi mitatu mimba ya mdogo wangu Ilikuja kutoka ikamuachia kilio na uchungu, shem wangu Zaki akageuka mfariji, akamfariji sana na kumpooza kwa maneno yaliyojaa faraja na matumaini. Kipindi icho mie Shelidani na Mume wangu Bonie tulijaliwa kuwa na mtoto wetu First born tuliyempa jinale Gadieli,🧒 tukabaki kumfariji Miriam.

Miaka miwili baadae mie Shelidani na Mume wangu Bonie tuliwakaribisha watoto wetu pacha Maiko na Pedro👬 kwa hakika ndoa yetu ilibarikiwa furaha, raha, cheko na tabasamu.😊😍

       Jamani sijui niseme ninaona mfadhaiko, huzuni na sikitiko. Embu tusaidiane kutema mate chini puuuu! Tumkanyage ibilisi shetani mwaribifu na mwovu. Ndugu zangu hamuwezi kuamini pale nikiwaambia Miriam mdogo wangu alikamata mimba  ya pili lakini loh! 😢Ilichoropoka na kumuachia teseko na sononeko la mtima🖤. Alijiuliza kwa moyo: 'Tatizo nini?🤨' 'Ana changamoto gani?' 😮‍💨'Kwanini yeye tu!?🤢' Kilio kikuu chenye ndimu kilimnyanyasa.

      Nilimshukuru Mola wangu baada ya kumkaribisha last born wetu Ivan baada ya Kipindi kirefu cha kujipumzisha uzazi na kuwalea wale wavulana wangu watatu:Gadi, Maiko na Pedro. Nyumba yetu ikabarikiwa furaha utoto na watoto, elimu na malezi mema. Tukajenga upendo na upendo ukasimama kama nguzo kuu ya familia tukayazidisha mapenzi na Mahaba nyumba ikanukia na kupendeza.

       Niwaambieni wapenzi wasomaji hakika nyota✨ yangu iling'ara na kupendeza, nyota🌟 ya mdogo wangu Miriam iling'ara pia na kupendeza, udhaifu wa nyota yake haikuchelewa kufifiana, kiza na utusitusi 🌑 viliifunika ile nyota. Ndiposa mdogo wangu Miriam akawa ni mtu wa kulia na kumuuliza Mola wake kosa lake nini?🤕 Tatizo lake gani?😷

       Mimba ya tatu ilipotoka waliwaona madaktari, washauri na wanasaikolojia waliowafariji kwa maneno ya kuwataka wawe wavumilivu na wasubirivu. Safari hii mdogo wangu akawa ni mtu wa kukata tamaa, tulipomwita kwenye Social 💃👯🕺event hakutaka kuhudhuria, alipowaona watoto Wadogo wa majiranize aliwatazama sana na machozi yakamsaliti akawa ni mtu wa kulia chungu.😿

Alihitaji sana mtoto angarau na yeye aitwe mama, angarau na yeye ajivune kwamba maisha ameyapatia. Pasina mtoto alijiona hajakamilika. Ubaya ni pale mimba zilipomsaliti na kuchoropoka. Maisha yetu yakaendelea watoto wangu walipendeza wakawa ni wenye Afya uzuri na ubora wakaboreka. 

*****************

         Ninakumbuka siku moja juma pili siku ya mapumziko baada ya ibada📿 na kazi za kutwa nzima  Miriam mdogo wangu na Mume wake Zaki walitutembelea. Siku ile tulifanya karamu🎂🎊 ya upendo. Vyakula vingi vilipikwa, vinywaji vingi viliandaliwa.🍹🍷🍻🍶 Uzuri ni kwamba katika hiyo karamu sisi hatugharamia hata shilingi mia pesa zote za karamu Shemela wangu Zaki aligharamikia. Maana yeye ni kibosile mwenye pesa zake.

   Baada ya karamu Bonie mume wangu alisaidia kuondoka vyombo pale mezani akaelekea kwenye sinki kuvikosha. Pale Sebuleni tulibaki watatu Mie Sheli, Miriam na mumewe Zaki. Katikati ya maongezi yetu Wine ya Mzabibu 🍷 ilifunguliwa Shemela wangu Zaki akayatoa yake ya moyoni.

     "Sheli, shemela wangu kuna jambo naomba tulijadili🗣️🔊 itapendeza iwapo tutapata mwafaka"🤝

    "Ndio, shemela ongea ninakusikiliza, nilimjibu Shem Zaki  nikajimiminia Wine yangu na kupiga funda moja Zito lenye afya.

    "Kama ujuavyo Shem mie na Mke wangu tumehangaika sana ndani na nje ya Mahosptali kujua jinsi gani tunaweza kubahatika kupata mtoto ambaye hawez kuharibika sembuse kutoka ndani ya tumbo la Mama yake. Jibu walillotupa Madaktari lilituumiza mioyo yetu maana walituambia kamwe Miriam asingeliweza kudumu na ujauzito lazima uchoropoke na kumuachia kilio na uchungu" Maneno aliyoyaongea niliyafahamu na kulijua tatizo la mdogo wangu.

       "Tumehangaika sana na kuwaona madakta, tumewapa pesa nyingi ili watusaidie kuimaliza changamoto ya Miriam Mke wangu, lakini wapi! Kwa pesa au kwa mali haijasaidia. Hatimaye mwisho wa siku Dakta mmoja kutoka India alitupa ushauri. Shem zaki akameza Funda moja ya ile juisi ya Mzabibu namie nilimsikiliza.

       "Unajua alitushaurije!? Alisema kwa vile Miriam anachangamoto ya kubeba ujauzito na ujauzito wake kuchoropoka baada ya muda mfupi njia sahihi ni kwa upande wangu kutafuta mwanamke mwingine kisha mbegu zangu kupachikwa kwake ili anizalie mtoto." Shem Zaki aliongea mie nilimsikiliza.

     "Lakini...."  Alisita kidogo kunena.

     "Dakta kutoka lndia amesema itakuavizuri kama atapatikana mtu kutoka familia ya Miriam, itakua vema kama huyo mtu atapewe mbegu na kubeba ujauzito ambao kwetu utakua ni familia."

     "Mh! 🤔🥺" Niliguna yale matatizo ya wenzangu.

      "Kwahyo mie Zaki na Mke wangu Miriam, tumekuja kwako tunaomba utusaidie kubeba ujauzito ambao hapo baadae utakuja kuwa familia maana damu yako na damu ya Miriam mdogo wako ni damu moja." Nilishituka 😤kusikia kauri ya Shem Zaki. 

     'Yawezekana vip Shem langu, mbona kama naona ni jambo la aibu.' Niliongea kimoyo moyo nikiwaza labda Shem Zaki na mdogo wangu Miriam wamerukwa na akili, sio kwa kusaka mtoto huko yaani wanasaka mtoto kwa nguvu nzito.

      "Ninampenda sana Mke wangu Miriam sijawai kuchepuka au kumsaliti ninataka awe na furaha kwaiyo nimetafakari maneno ya Dakta kutoka lndia nikaona yupo sahihi." Sikumuelewa Shemela wangu Zaki.😕🫨

      "Nadhani haitawezekana Shem kwanini usitafute mwanamke mwingine Nawe ukamwage mbegu zako kwake.? Kwani wanawake wameisha Duniani hadi ufikie hatua ya kunichagua mimi tu?" Nirikereka.

     "Tusaidie Shelidani, tusaidie tunakuomba. Hatuna nia mbaya." Miriam mdogo wangu alinisihi. Machozi yakamdondoka. Nikamuonea huruma jinsi alivyopitia changamoto ya mimba kuchoropoka. Huruma zile zikanifanya niumie moyoni. Hatimaye nikamwambia.

      "Subirini nitayajadili na Bonie mume wangu. Nimsikilize anasemaje!?" Sikuwawavunja mioyo yao. Wakaondoka na kunisihi sana nisiwaangushe. Usiku 🌒🌑Ulipowadia mie na Huba langu Bonie tukiwa kitandani twatomasana tomasana bado kidogo tulipakue Huba Kisha tuanze kulila likiwa lingali la mwoootroo💞🔥 nilianzisha mazungumzo.

       "Ndio hivyo Sweet heart 💕Dakta kutoka lndia anamshawishi Shemela wetu Zakaria nimbebee ujauzito ati anadai itapendeza sababu damu yangu na damu ya Miriam zinafanana."🩸🆎

       "Duh! Huo sasa Mitihani yaani ujaliwe watoto wanne alafu uongeze mwingine wa tano, si utachoka kuzaa  Sweet heart." Bonnie aliongea.

      "Mwenyewe nimeshangaa🥺😂, nimeona kama kaupuuzi furani wanakujaje kunivunjia heshima ati niwazalie mtoto wakati kundi kubwa la wanawake limejaa mitahani!🌴🎋🛣️ Hawawaoni hao hadi wanione mimi tu." Niliipinga kauri ya shem Zaki na dadangu Miriam.

       "Lakini sio mbaya kama unampenda mdogo wako wazalie tu." Bonie alinishitua.

     "Mwanaume mpumbavu wewe😠😧 yaani unaniruhusu nibebe mbegu za shemeji yangu." Nlianza kusinyaa na kudhoofika baada ya kusikia kauri ya mume wangu Bonie.

         "Mimi ni mumeo na nime kuruhusu maana ni kitendo cha kupachika mbegu na sio kufanya zinaa..... Sioni tabu wewe kubali tu umuokoe dadako. Nimefikiria sana miaka yote hiyo akiendelea kukaa bila mtoto atadharauliwa sana tena atafukuzwa kama Jibwa koko."🐩🐕‍🦺 Bonie aliongea kwa kirefu.

    "Bonie umerogwa wewe sio mzima👿" Sikutaka tena mazungumzo yaendelee. Nikaamua kulala mzungu wa nne maana nilichukia ujinga ule.

         ===================

Ghafla moyo wangu ulinishurutisha nikubali Kubeba ujauzito na Kumzalia Shem wangu Zaki na dada yangu Miriam sababu mtima wangu ulisumbuliwa sana na ile kauri aliyoitoa Bonie wiki moja iliyopita. Bonie alisema iwapo Miriam ataendelea kukaa ndani pasina mtoto angelidharauliwa na Taraka ingelimfuata maana kwa muda wote huo angeonekana ni mzigo ndani ya ile familia. Moyo ukaniomba nifanye maamuzi.

    Nikaichukua simu yangu ya Mezani ☎️ nikampigia Shem Zaki pamoja Dadangu mdogo Miriam 📞 nikamwambia nimeridhia ombi Lao, Nipo tayari kuwazalia mtoto kilichobaki ni kuapachikwa mbegu. Furaha waliyokuwa nayo haisomeki hata kwenye vitabu 📚au kuonesha kwenye kumbi za sinema📽️📺. Walifurahia sana. Mwezi mmoja baadae Niliingia Hospitali kupandikizwa mbegu za Shemeji yangu. Dakta kutoka lndia 🇮🇳alifanya kazi yake mbegu za shem Zaki zilipandikizwa kwenye kizazi changu.

       Mimba ilikubali, mtoto akatungika tumboni. Taratibu alikua na maendeleo yake yalikua ni mazuri yaani Sikupata tabu yoyote ile. Furaha waliyokuwa nayo Zaki na Miriam iliwafanya watumie pesa nyingi kulihudumia tumbo langu. Kila nilichotaka nilipewa na kila nilichoomba nililetewa taratibu wakaanza kukinursery (kukipamba) mchumba ambacho mwanao angelilala, wakakidecorate nacho kikapendeza kila kitu muhimu kiliwekwa ndani. Kilichobaki ni mapokezi ya yule mtoto.👼

       Bonie mume wangu hakuuchukia wala kuubeza ule ujauzito niliombebea dadangu mdogo na Shemela wangu Zaki. Wavulana wangu wadogo kila siku waliongea kitotototo wakiuliza 'Mama lini atakuja mdogo wetu?'👶 wakanifurahisha zaidi waliposema 'Akija tutakuwa walinzi wake.'🫡 'Tutamfunda kusoma na kuandika!' 📖🖋️'Akija tutampenda na kumfrahia.' 😍💖 Nyumba yetu ikawa ni bustani 🏡na Paradiso ya furaha.

_________________

Basi siku ya kupata uchungu na kuingia Leba Bonie mume wangu aliwatafuta sana Miriam na Zaki kuwajulisha kwamba ninaelekea Leba miezi tisa ishatimu. Simu zilipigwa 📲📞zilipigwa zikaita wee! Hazikupokelewa📴 meseji zilitumwa Wasap, lnstargrame, Fb na kila mitandao lakini bado hawa wawili hawakupatikana. Wakatutia wasiwasi juu ya pahali waliopo.

         Nikaingia Leba🛌, nikauvumilia uchungu wa kizaz na Mola wangu alivyo mwema nikajaliwa kujifungua salama mtoto wa kike baada ya masaa mawili kupita Miriam na mumewe Zaki wakaingia ndani ya Martenity hall (Chumba nilichopewa kupumzika) Usoni walionekana kutokuwa na furaha, wakati mie nilitegemea kupoklewa kwa tabasamu na vicheko nilikuja kushangazwa kwa kauri🗣️😶🗨️ walizozitoa.

      "Huyu sio mtoto tuliyemtegemea." Zaki shemela wangu aliongea.

      "Una maana gani shem Zaki? 🥺⁉️" Nilihoji kwa mshangao maana mtoto mwenyewe hakuwa na kasoro yoyote ile. Kama ni suala la macho, 👁️ mtoto alitimilika na alikua na macho maangavu, kusikia🧏 mtoto aliisikia na ngozi yake hakuzaliwa Albino.

       "Umetuletea mtoto wa aina gani huyu Dada." Miriam alituacha hoi na mshangao mzito🥺 mie na Mume wangu Bonie.
     
     "Kwani nyie mlitegemea niwaletee mtoto wa aina gani jamani🙂? Mlitaka mlemavu au asiye na jinsia?" Nilihoji ningali ninashangaa.

     "Dada sisi tulitegemea ungetuletea mtoto wa kiume sio huyu jinsia ya kike, hatumtaki.😠" Jesu! ❗TUlizidi kuishangaa ile Couple ya geti kali. 

     "Mliniambia kama mlikuwa mna tafuta mtoto wa kiume au mimi ni Mungu hadi nipange juu ya jinsi ya mtoto."Nilibwata.😬🤯

    "Dada unawatoto wanne na wote ni wa kiume Maiko, Gadieli, Pedro na Ivan. Kupitia kizazi chako wewe ndiye uliye andaliwa kutuletea mtoto wa kiume kama Dakta🩺🧑‍⚕️wa India alivyotushauri. Ajabu umetuletea mtoto wa kike." Hatumtaki." Miriam aliendelea kuongea. 

   "Miriam mmerogwa nyie, mbona siku nilipokua napandikizwa mbegu hamkuniambia kuhusu hilo yaani baada ya maji kumwagika ndo'mnakuja kupiga kelele. "Hasira zilinipanda hadi ndani ya komwe na ugoko. 

     "Shem Zakaria ninaomba umchukue mwanao uende ukamlee na umwache mke wangu apumzike sasa" Bonie Alimwambia Shem Zaki. 

      "Siwezi na sitaki."🫥👎 Shem Zaki alianza kuondoka pale Hospitali Sie wawili tukimshangaa.

     "Shit👿!!" Bonie alifoka. 
   
      "Miriam nieleze mmepatwa na kadhia gani hata mfikie hatua ya kumkataa mtoto mliyeniomba na kunisihi sana niwaletee." 

      "Dada ninaogopa mpendwa, ni naogopa mimi." Miriam alianza kulia. 

     "Familia na ukoo wa mume wangu Zakaria wananisumbua sana akidai niwaletee mtoto wa kiume ndani ili hapo baadae mtoto hyu aje kuwa mrithi wa mali na tajiri wao." Miriam aliongea maneno ambavyo hajawai kuniambia. 

       "Tulipomueleza Dakta wa lndia kuhusu kizazi chako alifurahia sana tena alitushauri kwamba wewe ungelifaa kutuletea mtoto wa kiume ambaye atakuja kuwa mrithi wa mali nyingi na tajiri wa ukoo na Familia ya Mume wangu Zakaria lakini mambo amekua ndivyo sivyo."Aliongea.

      "Kwani mtoto wa kike hatoweza kuwa mrithi!?" Niliuluza

      "Hawataki dada, wanaamini katika damu ya mtoto wa kiume kama Mila na desturi za zamani walivyozishikilia. Baya zaidi mume wangu Zakaria aliniambia wazi kuwa iwapo utajifungua mtoto wa kike basi ndoa Sina, ndoa itafikua tamati, ataniacha na kunitupa." Aliongea kwa chungu na majuto. 

     "Miriam mdogo wangu Naomba mchukue mwanzo uende ukamlee, nimefanya kazi mkubwa sana kukusaidia." Nilimsistizia na kumsihi asimtelekeze mwanaye. 

     "Siwezi dada ninaipenda ndooa yangu." Alianza kuondoka pale Hospitali akimkimbilia mumewe. 

     "Waache waondoke, wapumbavu wakubwa wale. Ovyo" Bonnie alikasirishwa na hali ile. 

     "Wabaguzi, wanajali sana mali na jinsi.... Waambie hivi maji 💦haya a jinsia lakini hayatubagui, Milima🗻🏔️ haina jinsia lakini haitubagui."Yalimtoka maneno Bonnie. 

   " Nitakaa wiki moja Hospitali, tuwape nafasi, wakiingia chungu watamfuata mtoto wao." Nilimwambia Bonnie. 

      "kuwa na chungu Mama lvan, kama wamekataa mtoto tutamuadopt ili awe wetu." Bonnie alinifariji. Wiki moja lilipita nikiwa ningali Hospitali ninawasubiri Zaki na Miriam wageuze mioyo yao migumu waje wamchukue mtoto niliyewazalia, lakini wapi! hawakutokea Wala hawakuja kuniletea Uji  mzito wa moto niunywe na kunipunguzia uchungu. Mwanangu Maiko, Pedro, Gadieli na lvan walinibembeleza nirejee nyumbani maana walinimiss sana. Basi mie mama Ivan nikaomba ruhusa nikarejea nyumbani maana mwanangu walinimiss balaa😂😘. Madakta waliniruhusu nikarejea nyumbani na maisha ya kulea mwana yakanifuata. 🤱. 

***_____****____****

Mwezi mmoja kupita nikiwa namnyonyesha Binti yangu Ivanka Nilisikia sauti nje ya nyumba yangu yalikua ni mapokezi ya furaha kutoka kwa mwanangu wapenzi. Nikachungulia kwa dirisha hapo nikawaona wamemrukia kwa furaha Miriam mdogo wangu na kumuwaoooo! 😚🤪🫂🤗 Akayateremsha mabegi yake mkubwa ya nguo na ndani akakaribishwa. 

      "Kuliko mwenzangu, mbona macho mekundu kama pilipili, huchoki kulia!? Na hayo mabegi ya nguo vipi?" Nilimuuliza Miriam. Wakati huo niliwaruhusu wavulana wangu wakaendelee kucheza 'Hide and seek' 🥷🙈'moja mbili tatu komboreraaa😂'

     "Yaani dada ninajuta mie, ninajuta majuto makuu. Tangu nimekutelekeza kule Hospitali na mwanangu hakuna siku niliyopata amani. Niligeuka na kuwa mtu wa kulialia tu. Hatimaye nilipokuja kugundua kuwa Sina changu ndani ya mjumba wa wale mabillionea....." Chozi na kamasi lilianza kumbubujika kama bomba la maji 🚰. 

      "Kwahyo!?" Nilimuuliza. 

      "Ninaomba unisamehe dada yangu niaomba unisamehe unipe ruhusa tusaidiane kumtunza na kumlea Ivanka..... Najuta Jamani!!" Kwikwi kwikwi😭😭😿😢🥹 Alilia kwa hisia. Nikavaa vazi la huruma nikampenda na kumjali damu yangu. 

       "Na Zaki mumeo vipi!? Au ndo kakaupa Taraka kisa tu nimewaletea mtoto wa kike nyumbani?" Nilihoji. 

    "LA! Hasha dada mpenzi. Hajanipa kwa hiari yake mimi ndiye niliyemwomba Taraka. Nimeumia sana, Nimeumia kumtelekeza mwanangu. Nilikua nikijiuliza mimi ni mama wa aina gani duniani ambaye sioni thamani ya damu ya dadangu? Sioni thamani ya uchungu wako? Sioni thamani ya mtoto? Unisamehe dadangu."Safari hii Miriam alianza kujigaragaza sakafuni akilia kwa hisia. 
        
     "Nimekusamehe mdogo wangu, apangalo Mola binadamu hapangui. Tuishi pamoja katikati ya upendo. Tusaidiane kumlea Ivanka, Malaika atakayetuletea Baraka." Nilimfariji Miriam nikamwambia mpakate mwanao mtazame tunyusi usoni, tumasikio kama popo tushavu twenye dimpozi za babake Zaki na tulips twa babake Zaki. Alitulia akafuta chozi akampakata mtoto alipomtazama vizuri anavyotabasamu 😻😇 na tumapengo twake🦷 Miriam naye akatabasam. 😍.

🤱🤱🤱🤱🤱🤱🤱
TCHAO 

      


   

Wednesday, November 27, 2024

MUZIC AND LAW (MUZIC NA SHERIA)

 


NILIMLAZIMISHA MWANANGU👱 AKASOMEE📚📖 SHERIA, ⚖️ALIGOMA AKIDAI ATI ANAPENDA MUZIC🎶🎧🎸, NILIPOMFUKUZA🏃💨 NILILETEWA TAARIFA ZILIZOUCHOMA MTIMA WANGU❤️‍🔥.



      "Nasema hivi Jack uende Chuo 🎓 ukasomee Sheria, ⚖️ili uje kuwa Mwanasheria🧑‍⚖️ mkubwa Duniani kama mimi baba yako na mjomba wako Deo" Niliongea kwa hasira nzito pale sebuleni, jioni ya leo tukiwa tupo mezani tunapata Dinner:🍲🥚🥗 Mimi Baba Jack, mama Jack na Jack mwanangu one and only, wa pekee. Aliyejiandaa wiki ijayo kwenda Chuo.

     "Baba nimesema sitaki kusomea Sheria, masomo ya Sheria hayapo moyoni mwangu, sintaweza tena sitaki kuhukumu watu." Tineja wetu aliongea, uso wake wa ujana ulipambwa kwa hasira, tundevu twake tulianza kukikumbatia kidevu chake, ngozi yake safi yenye rangi ya chocolate na uzuri haikua na chunusi usoni sema mwanangu hakua na Hatia angali bado kijana mdogo.

   "Kasomee Sheria mwanangu, ukisomea Sheria utakuja kuwa tajiri💰🪙🤑 mwenye heshima ndani ya jamii." Mama yake Jack aliunga mkono kauri yangu.

     "Baba na mama mimi haja yangu ni kufanya Muziki🎸🎷🥁 kwasababu Muziki upo ndani ya damu yangu hiyo ndivyo kazi itakayonipa heshima na furaha ya maisha yangu." Jack aliongea akimaanisha.

      "Upuuzi huo hatuutaki😡, unataka kutuaibisha mbele ya jamaa, ndugu na marafiki🧑‍🤝‍🧑🤼 tuonekane tumekulea vibaya. Hauoni aibu kuonekakana kwenye Televisheni na video ukiwapapasa papasa na kuwachezea wanawake walio uchi,👯 ukinywa vileo vikali🍻🍺🍾 na kutumia dawa za kulevya💊💉." Nilimkaripia Jack ambaye aliacha kula akanuna😠🤢 kwa hasira.

    "Baba ninaomba uniruhusu nifanye kile ambacho moyo💖 wangu unakitamani. Ninahitaji pia sapoti ya pesa, mali na faraja. Ili nitimize ndoto na matamanio yangu." Mwanangu Jack aliomba.

       "Siwezi kutoa sapoti yangu kwenye mambo ya Dunia, mambo machafu ya kumchukiza Mungu. Ukikubali kusomea Sheria nipo tayari kuuza. Nyumba yetu, magari yetu na kila kitu tulichonacho."Nililishindilia nyundo wazo langu.

      "Hapana baba siwezi kwenda kusomea jambo ambalo halipo moyoni 
Mwangu." Kijana wangu mwenye umri wa miaka 21 alilitilia mkazo wazo lake.

     "Kama hautaki kuheshimu mawazo yetu naomba Jack uondoke nyumbani kwangu nenda ukaishi na ukuungane na hao hao chokoraa wavuta mabangi🚬 Wenzio wanaopenda Muziki😵‍💫🥴😓" Nilimkaripia akasimama🧍pale chakulani na kuelekea chumbani kwake."

   "Baba Jack umefanya nini? Kwanini unamfukuza mtoto? 🙂‍↕️Ungetumia busara kumtuliza sio matumizi ya hasira zenye hasara" Mama Jack aliongea akasimama pale alipoketi haraka akakimbilia chumbani kwa mwanetu Jack ambaye tayari alikua amefungasha virago vyake akatoka chumbani tayari kuondoka.🎒

     "Jack mwanangu, Jack tafadhali usifanye maamuzi mabaya yenye hasira. Tuliza mtima wako na kuketi chini tuzungumze" 🙏Mke wangu Mama Jack alimbembeleza mwanangu Jack.

     "Hapana mama, Baba amenifukuza wacha niondoke ipo siku atakuja kunishangaa nitakavyobadilika na kuwa mtu mkubwa Duniani." ✨Jack Alimwambia mamaye mie niliona ni upuuzi na ujanja wa kutaka kujaribu mambo ya Shetani👿

      "My son Jack nisikilize mama yako  tafadhali usiondoke, nitamshawishi baba yako hadi atanielewa" Mama Jack alimshawish Jack.

     "Aondoke haraka kwenye nyumba yangu, 🏚️Aondoke akajifunze kiburi si maungwana." Nilibwata na kubwabwajuka kwa hasira. Jack mwanangu hakua na jinsi alilibeba begi lake la nguo akafanya kuondoka wakati huo mamaye alimwaga chozi🥹 hakika uchungu wa mwana aujuaye ni mama. 🧑‍💼

:::::::::::::::::::::::::::::::

Basi baada ya mwanangu Jack kuondoka hakupata tena kuwasiliana na mimi📱, mama yake alikua akimpigia simu mara kwa mara lakini simu Iliita wee! 📲 Hadi Ikamdirect kwenye utumaji wa meseji. Bado tu mama Jack aliendelea kumpigia simu Jack ambaye hatukujua amekimbilia mji gani ndani ya Jiji la Dar es saalam. 🏙️ Baya zaidi hakupokea simu ya mama yake iliyoita tu ikatamani kupasuka.

""""""""""" "" "" "" "" "" "" "" "

    Ilipita miaka mitatu hatukupata kusikia au kuwasiliana na Jack. Hatukupajua pahali anapoishi, hatukujua jinsi anavyoishi kijana wetu. Tulijiaminisha ipo siku Jack angelirejea nyumbani lakini wapi! Hakurejea. 

      Jumapili moja baada ya Sherehe ya Noeli na mwaka mpya Mama Jack akiwa mekoni anamkaangiza Turkey 🍗🦃simu yake ya mkononi Iliita.

    "Hallow! 💬" 

     "Hallow ndugu! 🗨️" Mama Jack alilitikia. 

      "Ninaogea na Mama Jack Daniel?" upande wa mpigaji uliuliza. 

     "Ndio, wewe ni nani ndugu na una shida gani nikusaidie." 🤔Mke wangu aliuliza. Mie Baba Jack nalikua nikiteremka ngazi za Horofa ya juu kuja chini. 🪜

       "Sisi ni mabwana Polisi 👮🚓 tuna taarifa mbaya kukuambia."

     "Taarifa gani?!" Mama Jack aliuliza wakati huo mie naliekua nikiteremka ngazi za juu nalifika Mekoni🧑‍🍳  nikimsikiza mama Jack akiongea Simuni. 📞

    "Jack mwanenu amekutwa amekufa kwa ajali ya gari🏎️ iliyomgonga hadi kupasuka ubongo wake." 🧠

    "Jack ame..... 😨 Kufa."😞 Mama Jack alishituka. 

    "Ndio mama hivi tunavyoongea amepelekwa Amana Hospitali ⚕️kwa uchunguzi zaidi." Polisi alimjibu Mke wangu. 

    "Jesu!" 🧟Mke wangu akajibwaga sakafuni asielewe wala asiamini kile alichoambiwa. 

     "Nini Mama Jack?!" 🙄Nilimsogelea mama Jack pale sakafuni alipojibwaga. 

    "Jack Jamani😭 Jack mwanangu, Jack" 😢Aliongea machozi yakimbubujika. Haraka haraka nikaichukua simu aliyoidondosha chini kisha nikampigia simu Polisi aliyekuwa akiwasiliana naye. 

    "Hallow! Nitaamini vipi kama kweli mwanangu Jack hatunaye mtu huyo au labda mmekosea nambari." 🤐

     "Hapana baba kwasababu tulipokua tunamsachi sachi marehemu tukaiona simu yake Kuna nambari ameisave kwa Jina 'Mamangu mpenzi💖" Tukaona sio mbaya kumpigia simu mama mpenzi. Lakini kama mna mashaka nendeni Amana Hospitali yamkini mtajihakikishia. 

     Sie tuliopandwa na presha na moyo 🙀❣️ kudondoka  tukafanya hima hima🏃 kuelekea Amana Hospitali tujihakikishie kama ni Jack wetu au ni ndoto za majinamizi🦹. Tulipofika tukaoneshwa mwili wa marehemu tuliyeambiwa ni Jack mwanetu. 

      Toba! 🤯🤧🥹 Tulihisi Dunia imetuangukia. Jack alikua amelala amekufa, Jack wetu yule yule aliyeondoja nyumbani miaka 3 ilopita jaman leo hatunaye mtu huyo😢, amekufa jaman, ameondoka angali kijana ambaye hajaonja chumvi,🧈 asali,🍯 ndimu na sukari. Machozi, vilio na maombolezo vilitufuata. 

*********

Tukamfanyia Jack wetu maziko, mamaye akilia na kunilaumu kwanini nilimfukuza Jack wetu mimi pia nililia na kujilaumu kumlazimisha Tineja wetu afuate kitu ambacho moyo wake ulikikataa. Hatimaye kuondoka nyumbani moja kwa moja na kuua mawasiliano. 

Baada ya mazishi ⚰️ 🌁 mawazo Yakaanza kunilindimaa kichwani. Nilimuwaza mwanangu Jack, nilijilaumu nafsini kwanini nilimlazimisha kijana wangu afanye jambo ambao halipo mtimani mwake? Kwanini nilimfukuza? Jaman! Nikaangukia ulevini🍻🍶nikiamini ulevi ungelinisaidia kunipunguzia stress juu ya Jack wangu lakini wapi! Stress zilinizingua zaidi. 🤯

*****

Mke wangu Mama Jack akaanzisha utaratibu wa kwenda kila siku kaburini alipolala Jack, akifika huko Angelia wee🤧 angelisari 🤲📿✝️ na kuomboleza. Baada ya vilio na Sara mke wangu angelirejea nyumbani. Ikawa ndio utamaduni wake kila siku angelienda makaburi ya Kisutu kulia na kusali wakati huo huo mie Mzee Danieli nakimbilia Bar🍸🍾 kupiga moja moto🔥 moja baridi💧 nikiamini pombe itanipunguzia mawazo na stress. 

Lakini siku moja Mama yake Jack alipoenda Kulitembelea kaburi ⚰️la mwanetu Jack Alishangaa sana kuikuta Midoli 🐻na wanasesere 🎎wakiwa wamewekwa katikati ya kaburi la Jack. Akaitoa na kuweka maua 🌺💐juu ya lile kaburi akalia hapo na kusali Kisha akaenda kuitupa ile Midoli. 

     SIKU ya pili pia Mke wangu alishangaa kuikuta Midoli na🐼🦖🦍 wanasesere tena safari hii aliikuta Midoli mkubwa zaidi ya ile ya awali. Alijiuliza moyoni Atakua ni nani huyu anifanyiaye yaya hizi? Kwanini ananifanyia hivi?' Hakupata jibu. Aliishia kuondoka zake taratibu na kuelekea nyumbani🏠


Siku ya tatu alifanya uamuzi wa kuwai 🌄 kufika makaburini siku ile alishangaa kumkuta mwanamke kijana mwenye kadirio la miaka ishirini na miwili akiwa amepiga goti pembeni ya kaburi la Jack. Mwanamke yule alikua akisali pembeni yake aliambatana na mtoto wa kiume mdogo mwenye kadirio la miezi mitano pamoja na hilo yule mwanamke alikua na Midoli mkubwa pembeni yake. 

Mama Jack hakutaka kumshitua yule Binti alihakikisha yule mwanamke anasali Dua yake Kisha anasimama ili aondoe. Kweli mwanamke yule alipomaliza kusali Dua yake alifanya kuweka Midoli ile mkubwa pale kwenye kaburi la Jack  akambeba mtoto wake kujua da kuondoka.

     "Excume me Sister." 🙇Mama Jack alimsimamisha yule mwanamke.

     "Without excume madame, what can l do for you?" 😊

      "Naomba kuuliza kama ni wewe ndiye uwekaye Midoli juu ya kaburi la mwanangu Jack?"🦕🪆 Yule mwanamke alitoka macho👀 kidogo kama ishara ya mshangao.
    
      "Ndio, ni mimi kwani wewe ni mama yake Jack!?" ❓ kko huiAlijibu vizuri na kuhoji.

    "Ndio, Jack ni mwanangu na wewe ni nani?"

      "Oh! Mama!" Yule Binti alienda kumkumbatia mama yake Jack 🫂🤗 baada ya muda alimuachia.

        "Nmefrahia kukujua pia kukuona, mimi nilikua ni mpenzi wa Jack na huyu pembeni ni mtoto wa Jack, first born.🤱

     "Mtoto wa Jack?! 🧒Mama aliuliza kwa mshangao. ❗

   "Mwanangu Jack hajawai kuwa na mtoto." Mama Jack akamsogelea yule mtoto Kisha akamuangalia usoni. Hakika mtoto yule mwenye kadirio la miezi mitano alifanana sana na Jack kuanzia uso, midomo, macho hata komwe la Jack.

      "Ni historia ndefu mama lakini kama hutojali Nipo tayari kukusimulia 📚🔊"  Binti aliongea.

      "Nisimulie tafadhali, mama Jack aliingia hamu ya kujua.

   "Ninaitwa Bella mimi ni Barmaid maarufu ndani ya Bar ya New ukonga. Nilifahamiana na Mpenzi Jack miaka mitatu iliyopita alikuja ndani ya Bar yetu akiwa mchovu asiyeeleweka. Alikuja kuomba kazi, kazi yoyote pale bar 🍾🍸 kama vile kuwauzia wateja pombe, kusafisha kumbi na vyombo vya Bar au kupikia supu🥙🍽️ wateja. Meneja wa Bar ya New ukonga alimkubalia jack. Jack alianza kazi hapo, ndio tulipoona nana na Sie tukapendana sana. Bella aliendelea kusimulia.

     "Kipindi Jack amekuja kutafuta kazi👷 alikua Hana pahali pa kulala, alilala chini na kwenye viti vya Bar. Nilimuonea huruma nikamwambia Njoo tuishi wote nyumbani kwangu. Jack alifurahia hapo ndipo penzi la mimi na Jack lilipamba moto." 🔥

     "Jack aliniambia ametoroka nyumbani kwa wazazi wake sababu wamekataa kumuunga mkono tamanio la kazi anayotaka kulifanya yaani Muzic.🎶🎼 Nilimfariji Jack kwa kumwambia ipo siku atafanikiwa. Kweli baada ya miaka miwili aliingia studio kuurekodi wimbo wake lakini wimbo wake haukuvuma sana Radioni, hakuwa tawi 🌿 la juu lakini bado hakukata tamaa. 

      "Mara kwa mara Jack aliniambia anawapenda sana Baba na mama yake, ipo siku atakapokua super star ✨🌟 atawatembelea ili awaoneshe jinsi alivyofanikiwa na kubarikiwa. Baada ya miaka miwili kupita nilishika mimba ya Jack, Jack alifurahia sana. akaingia studio kutengeneza wimbo wa kumshukuru Mola juu ya mtoto wake ajaye. Wimbo wake ulipoingia studio ulipendwa mno basi akiaanza kuitwa kwenye lnterview mbalimbali."

     
       "Miezi tisa kutimu nilipelekwa Leba kujifungua huyu mtoto Charles, nikiwa Leba Jack aliitwa ndani ya moja ya Radio kubwa Dar es saalam. Masikini kama angelijua huo ndio utakua mwisho😔 wake wallah! Asingelienda."Bella alitokwa chozi akalia. 😢

     "Kwani nilijua kuwa Jack amepata ajali na kifo? Sikujua hadi pale Polisi waliponipigia simu📞 wakidai kwamba wameiona nambari yangu ya simu kwenye Driving passport ya Jack. Nililia jaman, nililia hadi basi. Nikafanya upelelezi ili kugundua wapi mpenzi Jack amezikwa ndiposa nikajakugundua hapa. " Bella alijieleza.

     "Marehemu mpenzi wangu Jack aliniambia anawapenda sana lakini hakuwa na furaha ya kukataliwa timizo la ndoto zake. 🎭" Bella alisimulia akilia, mama Jack pia alilia.
      
       "Nimeumia sana Bella, kama baba jack asingelimlazimisha Jack mwanangu kusomea kitu ambacho hakipo mtimani leo hii angelikupa mbali kimaendeleo. Naomba twende nyumbani kwetu ukapajue na pia umjue baba yake Jack."Mama Jack aliomba.

      "Hapana mama labda siku nyingine." Bella aliona aibu.

      "Usikatae Bella wewe ndiye mfariji wa mwisho kwangu." Mama Jack alimsihi Bella ambaye hatimaye alikubali na safari ya kwenda nyumbani kwa mama Jack ilifana. Kufika hukowakamsimulia Baba Jack kila kitu. Baba Jack alibaki akimwaga chozi na kilio.

Baba Jack na Mama Jack walimpokea Bella na kumuomba awe anawatembelea mara kwa mara Bella alifanya hivyo Charles  mjukuu wa baba na mama Jack aliendelea kukua vizuri akapendeza. Uzuri ni kwamba Charles alionesha Darili za kuupenda Muzic Babu na Bibi yake walipoona mtoto anakipaji cha kuupenda Muzic wakamtafutia Mwalimu wa Muzic ambaye alimfunda Charles Muzic. Wazee wale walitokea kumpenda mtoto Charles Pendo la kupendeka. Ile Hatia ya kumfukuza nyumbani Baba Charles iliisha sababu charles aliwaondolea huzuni na Hatia. 


-----------------
TCHAO 👋👋

🎸🎺🎙️

Monday, November 25, 2024

ALIFEKI KIFO





 NILIJUA MUME WANGU 👩‍❤️‍👨ATAAGA DUNIA KWA MARADHI YA KANSA 🥵💊💉KUMBE MWENZANGU 🧍‍♂️ ALIPANGA KUFEKI KIFO⚰️☠️ ILI AMUOE MALAYA 🤹‍♀️ MWENYE TAMAA.


       Siku tuliyokwenda Hospitali ya Ocean🌊 Road kumuona Dakta Eze 👨‍⚕️🩺atueleze majibu ya vipimo vya ugonjwa umsumbuao Mume wangu,🥵 Dakta Eze alituambia majibu yaliyotuvunja mioyo yetu na kutukatisha tamaa ya kufurahia maisha ya ndoa yetu iliyodumu Kwa zaidi ya Miaka kumi.
 
      Majibu ya vipimo yalionesha Mume wangu alisumbuliwa na ugonjwa wa KANSA ya moyo🖤 iliyofikia stage ya kukatisha tamaa😓. Kwa kifupi Dakta Eze alituambia siku za kuishi Mume wangu ni chache na zinahesabika. Tulibubujikwa machozi😭

      "Please Dakta🩺 tunaomba utusaidie" Shania mie nilimsihi Dakta.

        "Anapaswa kupewa kitanda🛌 cha Hospitali ili huduma zote ziwe karibu."Dakta Eze alitoa ushauri. Mie na Omario tulikumbwa na sura za majonzi na uchungu wa ndimu.😖😩

        "Shania tumsikilize Dakta. Wacha nilalae Hospitali🏥 maana Dakta amesema bado mwezi mmoja tu Mola atanichukua. Ugonjwa wa Kansa hautibiki.💉💊" Mume wangu alikataa tamaa.

     "Usiseme hivyo Omario, ya Mola mengi na Mola anaweza tenda miujiza kumbuka ninakupenda sana Mume wangu ninakupenda, nisingelipenda kukuacha mpweke." Nilimfariji Huba wangu.💞

     "Ninakupenda sana mke wangu Shania, ombi langu Moja ninaomba uwe unakuja kunitembelea Hospital mara zote nipate faraja maana uwepo wako itakua faraja tosha kwangu."Omario alinisihi

        "Kila siku nitakuja na Dua 📿🛐🤲 njema nitakuombea." Nilimtia moyo.
      
          "Usiache tafadhali." Mume wangu alirengwa chozi akachukuliwa na kupelekwa Wadi ya kipekee kufika huko akalazwa Ili huduma muhimu zianze kutolewa. Basi ikawa kila siku ni lazima niende Ocean Road Hospital Kumtazama Mume wangu, kumwandalia chakula, 🥣maji 🚰 na huduma nyingine muhimu. Hata siku Moja sikuacha kumuomba Dua na maombi Mola wangu amponye Mume wangu.

         Kila nilipoenda kumtazama Omario nilimkuta akiwa katika hali ya kudhoofu na kulalamika😣😖 maumivu makali ya moyo na kila siku alionesha darili za kukata tamaa akiamini kuwa kifo💀 chake kipo karibu.

Siku Moja nikiwa ninarejea nyumbani kichwani nimevurugwa kwa wingi wa Dua, maombi na machozi vilivyoandamana nami kwa jinsi ninavyompenda Omario acheni kupenda kuitwe kupenda yaani siwezi kutoa mfano.

        Makusudi tu nikajiketisha pembeni ya Benchi moja lililo ndani ya Bustani ile ya Ocean Road bado Dua zilinitoka moyoni nikimuomba Mola 📿ashushe muujiza ili nimpendaye apone.

       "Samahani Sister waweza kuniruhusu niketi pamoja na wewe" NIliyafumbua macho yangu nikayafuta machozi yaliyokua yakimwagika mithiri ya Bomba la maji 🚰⛲

    "Keti dada, keti usijari." Nilimkaribisha yule dada ambaye Kwa kumtazama mavazi yake mara Moja nilijua ni Nesi wa ile hospital.👩‍⚕️

      "Pole kuuguza Dadangu na pia punguza kulia sababu machozi yako yanakukondesha." Yule dada mgeni machoni kwangu alinifariji, hakika aliyaona machozi yanikondeshayo.

      "Asante Dadangu."🙏😊 Niliitikia faraja yake ingawaje sikupendezwa kuendeleza maongezi naye.

      "Niite Rozana, mie ni Nesi katika Hospitali hii dada Kuna jambo naomba nikushauri ikiwezekana ulifanyie kazi haraka sana uwezavyo." Nilimtazama Rozana na aliyeendelea kunena
     
       "Tafadhali funga kamera🎦 ndani ya chumba alalacho Mumeo, Kuna jambo ambalo sio zuri utakuja kuligundua." Alinishitua yule Binti.

      "Tatizo Nini ndogo wangu?" 🥺 Nilimkazia macho lakini kama vile alianza kuogopa akamka pale alipoketi hima hima akaondoka kisha akatamka:
    
      "Mumeo sio mgonjwa lakini anajifanya ni mgonjwa, utakapokuja kuligundua jambo lifanyikalo ndani ya chumba alicholazwa Mumeo dada utakuja kunishukuru." Rozana akatoweka.

      "Mmh! Niliguna."

      "Jambo gani?" Nilihojihoji.

      "Huyu Nesi vipi? Ataanzaje  kusema Mume wangu sio mgonjwa. Ametumwa huyu Nesi sio haba.👺 Niliwaza na kuchoka kuketi pale Benchini. Nikachukua gari yangu na kuelekea nyumbani Oysterbay. Hakika nilivurugwa.
    
     Usiku wa siku ile🌆 mawazo yalinisumbua, niliwaza juu ya yule Nesi, moyoni Nikajisemea ana maanisha Nini kusema Mume wangu sio mgonjwa? Kwanini aseme Mume wangu sio mgonjwa? Jamani. Haraka nikaingia online nikatazama aina za kamera mbalimbali pamoja na bei zake, nilihitaji kuipata kamera ya uhakika nilipoipata kamera niitafutayo nikaagiza kesho niletewe. 

       Mtoa huduma(Deriver) alifanya hima kuniletea asubuhi ingawaje mzigo ule ilikua ni mzigo wa bei gharama. Jioni ilipowasili nilielekea Ocean Road Hospital kumuona Mume wangu Mpenzi, nilimkuta amepooza, amelala, Hana furaha na amani. Nikamtaka pole kisha tukaongea mengi na machache pia baada ya maongezi kidogo aliniomba nimsindikize aelekee choo,🚽 nilimsindikiza na kumuacha anaendelea kujisaidia.

       Nikatoka chooni na kwenda ndani ya chumba alicholazwa nikayaona Maua 🌼🌺yamepambwa, hapo . Nilipaona ndo' pazuri kuseti kamera ambayo niliiseti na kuunganisha na simu yangu iliyoonesha mandhari ya chumba kizima haswa pale alipolala Mume wangu Omario.

           Omario alipotoka choo kama kawaida alilala kitandani Kwa shida mno. Nilimsaidia kupanda juu ya kitanda nikayasikilizia maumivu yake. Mtima wangu ulilia jamani ulilia kwa jinsi nilivyomwona nimpendaye akiugulia maumivu ya kansa ya moyo. Mpendwa wangu niliyelala naye, niliyecheka naye na kutaniana leo hii ananiambia anaumwa ugonjwa wa kufa!? Oh! Nililia kimya kimya moyoni.

     ......................….
Baada ya kupata chakula Cha usiku nilijiandalia kahawa na vipande vya kashata taratibu niliinywa na kuvitafuna vile vipande pembeni yangu niliiwasha Laptop 💻 niliyounganisha pamoja na USB kutoka kwenye kamera  iliyopo kwenye simu. Chumba cha Hospitali kilionekana vizuri, Omario alikua amelala kama nilivyomwacha hapo awali. Dakika zilikatika na masaa yakayoyoma mwenzenu nilianza kujutia tendo la kumuamini Nesi Rozana. Niliona kama upuuzi na upumbavu kumchunguza Mume wangu mgonjwa. Kwani Kuna faida 💰 gani ambayo ningeliipata baada ya kumchunguza Mume wangu?

      Lakini ghafra yapata saa sita usiku maajabu niliyoyaona, eeh!🥺😔  Nashindwa sijui nianzie wapi kueleza.. Aliingia mwanamke mrembo kupita maelezo,  mrembo zaidi ya Miss World 🗺️Venezuela. Alikua ni mrembo aliyevaa wigi jeusi lililokatwa likaishia masikioni💇‍♀️ . Uso wake wa Duara, ☺️macho makubwa 👁️ lips zimekoozwa👄 rangi nyekundu, ana ngozi rangi ya maji ya kunde mrefu kama Twiga🦒, mwembamba wa umbo la nyigu.

        Mrembo yule alivalia koti rangi ya Kaki na suruali rangi nyeusi iliyombana kisawasawa. Chini ya miguu alitupia viatu virefu vya mchuchumio👠 Tena alibeba mkoba👜 wa bei gharama, mkononi aliishikila simu Bomba 🤳 ambayo hata mie sina. Mume wangu Erick alipomuona tu ni kama vile ugonjwa wake ulimtoweka akatamka pale kitandani Kwa furaha kisha akampokea yule Binti mzuri kama midoli ya kichina. Wawili wale wakaanza kunyonyana ndimi 👨‍❤️‍💋‍👨na kupapasana mipapaso isiyokomabaada ya hapo nilimwona Mume wangu akaelekea kufunga chumba alicholazwa.

Bada ya kuufungua mlango yule Binti akamsogelea Mume wangu na kuanza kumvua nguo Moja baada ya nyingine na yule Binti akafanya vivyo hivyo akamvua yule Binti nguo zake zote wakangukia juu ya kitanda cha Hospitali. Yaani kama notaendelea kuwasimulia kile nilichokiona kikifanywa ndani ya kile chumba jamani! Moyo wangu utaniuma sana mana nilianza kupata Presha na pumzi zilinitoka juu juu.
   
     Nilitamani  kuizima ile laptop lakini ndugu zangu nilihitaji kujua mwisho wake ni nini?  Maana walipomaliza kufanya zinaa hospitalini 
Wakavaa nguo na kuketi kitandani na kuanza kuongea bahati mbaya hakuna neno nililolisikia sababu kamera yangu ilikua haitoi sauti.
 ............
Siku ile sikupata hata lepe la usingizi badala ya kulia juu ya ugonjwa unamsumbua Mume wangu Omario Sasa nikaanza kulia juu ya usaliti na udanganyifu wa Mume wangu. Jamani! Kila niiendapo Hospitali nilikuta mtu anaugua Hana mbele Wala nyuma alafu ajapo yule Malaya mrembo mwanaume anachangamka, anachek a Cheka, anaruka ruka na kufanya ngono Hospitalini. Hapana jamani Kuna kitu pale. Niliwaza.

         Siku iliyofuata nilimtembelea Omario Mume wangu bila kuonesha darili za kuzigundua ule mchezo wake mchafu, nilijinyemyekeza kwake na nikajifanya no mwingi wa huzuni na masikitiko. Nikamsaidia huduma ndogo ndogo na pia nikawa faraja kwake Bada ya hayo yote nilimuaga  ninarudi nyumbani.     

       "Ugu pole my love 😘 Mola akutangulie." Nikatoka Hospitali. Nilivyo mjanja kwani nilirejea nyumbani? Aka! Nilitaka Leo pia nipate ushahidi wa kile wanachonena na kukitenda. Nikajibanza pembeni ya moja ya kona ya ile Hospitali ili nijaribu bahati yangu ya kumuona Mrembo amzuzuaye Mume wangu mgonjwa anayeponan ghafra baada ya kumuona huyo Mrembo.

       Mungu ni pendo nilimuona yule Binti, Aliingia chumba alicholazwa Mume wangu nikafanya hima kujibanza pembeni ya mlango wa kile chumba. Nikaiwasha simu yangu sehemu inayorekodi Audio, kisha nikamega sikio nisikie nini wanachozungumza. Safari hii hawakufanya zinaa bali walipigana mabusu 🥰 pale kitandani pale Mume wangu amejaa furaha na tabasamu.

      "Afadhali umekuja Daring Veronica"  Nilisikia sauti ya mume wangu imejaa Afya tofauti na siku zote nilizomtembelea pale 🏥 Hospitali.

        "Nilikumiss sana Daring, leo nimetoka kwa Mwanasheria ⚖️ kuchukua Documentary ambazo zitatusaidia kuhamisha yale Mamilioni ya pesa zilizopo Bank 🏧 mara baada ya kukamilisha hatua zote za kufake kifo ." Uwii! Nilishituka zile kauri.

    "Waoo! 🎊Mke wangu" Mume wangu alianza kuruka ruka juu ya kile kitanda cha wagonjwa hakika Sasa alikwishaanza kupona mara baada ya kumuona yule mrembo

        "Shania alikuja muda si mrefu, yaani ungelimuona ungelimuonea huruma, amekonda kwa kilio na uchungu." Mume wangu aliongea akipekua pekua zile Documentary

      "Achana nae, si unanipenda Mimi? Kwahiyo kuanzia Leo Mimi ndiye Veronica Mkeo. Watakaposikia kuwa umekufa sie tutoroke Tanzania  twende kuishi Marekani tukastarehe Kwa kutumia pesa nyingi tutakazo zichukua Bank." Veronica aliongea na kamoyo kangu kalinidunda ndu ndu ndu ndu. Yaani mimi na Mume wangu Omario tumefanya kazi Kwa zaidi ya Miaka kumi kila pesa tuliyoichuma kutokana na kazi zetu tuliiweka kwenye Account ya pamoja (Joint Account) Alafu  Leo nisikie ati Mume wangu akiisha feki kifo chake  pesa zote atazichukua akatanue Majuu pamoja na huyu Malaya wake. Hapana, haiwezekani.

       "Veronica kumbuka bila msaada wa Dakta Eze kamwe tusingelifanikiwa kudanganya kwamba nimepatwa na Maradhi ya Kansa. Tukiishafanikiwa kuzichota pesa zetu tutenge fungu Kwa ajili ya Dakta  Eze. "

       "Ninakubaliana nawe Daring, si amesema bado siku tatu utakufa kifo bandia?" Veronica alimuuliza Omario.

     "Yes my Daring. Unajua ninafurahia kukujua, mapenzi unayaweza, mapenzi unayajua" Omario Alimsifia yule mrembo.
     
        "Asante Daring. Nimekuletea chakula kizuri na kitamu ule ushibe sio kila siku Mkeo akunyweshe uji🫕 utadhani wewe ni katoto kachanga" 👩‍🍼Veronica alimtania Omario. Wawili wale wakaagua kiicheko cha sauti kuu.😹😹

        Nilikwishapata ushahidi sio wa video tu Bali pia wa Audio🔊, nilikwishaijua nia ya mume wangu Omario pamoja na yule mrembo. Kumbe Mume wangu anataka kuniacha Ili amuoe yule Malaya? Kumbe Mume wangu pamoja na Veronica wameshirikiana na Dakta Eze kufake ugonjwa na Sasa wananelekea kufake vifo? Kumbe Omario pamoja na Kimada wake Veronica wamepanga njama ya kuzichota pesa zote nilizozichuma pamoja na Omario Mume wangu baada ya kuhangaikia kufanya kazi nzito zinazochosha Kwa zaidi ya Miaka kumi tangu niingie ndoani? Loh! Ama kweli kilulacho kipo nguoni mwako, kikuuwacho kipo nguoni mwako. Akufukuzaye akwambii toka. Nilijuta.

      "Ok. Tuone Sasa wa kwanza atakua wa mwisho na wa mwisho atakua wa kwanza. Nilirejea Oysterbay nyumbani baada ya kuridhika na upuuzi alionifanyia Mume wangu Omario. Yaani mie kila siku ninafanya Dua, ninamwaga chozi  ninajinyima mambo mazuri na kujikondesha Bure wakati huo huo mwenzangu anapanga njama za kunihujumu. Tutaona Sasa, nitamkomesha Hadi ajambe cheche.

############

        Ziiip'...... Ziiip'.... Ziiip' 📞Nilimpiga simu Bibi Mama Mkwe na Babu Baba mkwe nikawapa taarifa kesho asubuhi wawepo ndani ya jengo la hospitali ya Ocean Road tufanye Dua nzito ya kumuombea na kumuaga mpendwa wetu maana siku zake za kuishi Ulimwenguni zimefika tamati.

        Zuuuuu zuuuuu ziiii ☎️Niliwpigia simu ndugu, jamaa na marafiki, majirani na wafanyakazi wenziwe.'Jamani naomba tujikusanye, tuje Ocean 🌊 Road Hospitali tufanye Dua na maombi, tumuombee ndugu, jamaa, rafiki, jirani na mwenzetu mpendwa Omario siku zake za kuliona Jua🌄 zimekaribia kukoma Muda sio rafiki Baba Mungu atamwita.' ikawa hivyo Tena Wakwe zangu, nduguze Erick, jamaaaze, marafikize na wafanyakazi wenza🧑‍🤝‍🧑 wakajikusanya na kujazana pale Ocean Road Hospital wamejaa machozi , vilio na sononeko la moyo.

      Sikuwasahau mabwana POLISI. 'Kaeni chonjo mambo yashaiva tutajichukulia Sheria mkononi, tutaua jitu huku na jitu litazima tu, lipende lisipende, litake lisitake Bullshit!'👿 POLISI nao wakaja wametinga mavazi ya kiraia bahati nzuri Veronica naye akaja ingawaje hajulikani pale lakini alikuja kujulikana bila kupenda.

""""""""""""""""'"'"""
          "Wapendwa Wakwe zangu, ndugu jamaa na marafik, watumishi na majirani asanteni Kwa kuja."✌️ Nilianza kushukuru wakati huo Omario wetu alifeki kujifanya yupo hoi taabani, hawezi Wala hajiwezi tena hajitambui.

   "Lengo la kuitana hapa ni juu ya maombi, Dua njema na kumuombea rehema mpendwa wetu Omario maana hatujui saa ambayo Mola wake atampumzisha, kwahiyo tukaze kusali." 🛐Niliendelea kunena.

         "Lakini kabla hatujafungua Ibada na maombi ya kumuombea mpendwa wetu  ningelipenda kila mmoja aliyepo hapa aitazame  hii tape video na kuisikiliza hii tape audio ndipo Kwa moyo wenye umoja tuanze kufanya maombi, kumuombea mpendwa wetu." Watu wote waliojazana ndani na nje ya kile chumba walinitazama niliiweka ile tape video📺 kwenye  deki ya Televisheni iliyoukutani kwenye kile chumba alicholazwa Omario.

     "Shania unataka kufanya Nini!?" 😶Mgonjwa wetu aliyekua hoi ashindwe kutamka sasa alitamka. Sikumjibu. Video ikaanza kutazamwa na watu wazima ndani ya kile chumba, ilikua ni aibu na fedhea lakini SIKUJALI na sikukomea hapo nilipohakikisha kuwa ile video imeleta taharuki nikachomeka DVD 📀 niliyorekodi sauti za yale mazungumzo kati ya Veronica na Mume wangu Omario.

        Jamani! Jamani almanusura Bibi mama Mkwe na Babu Baba mkwe wazirai na kuzima kimoja' hakuna mtu ambaye hakusikia udanganyifu na mipango ile michafu.
     
       "Omario umetufedhehesha na kutuaibisha, yaani sie twajua mwanetu ni mgonjwa tunahangaika huku na kule kukopa mapesa ya matibabu na madawa lakini kumbe wewe unapanga mipango michafu na huyo Veronica Malaya wako." Bibi Mama  mkwe aliongea na machozi akabubujikwa.😢

      "Nisamehewe Mama, naomba nisamehewe." Mgonjwa aliyekua hoi taabani pale kitandani safari hii akadamka na kupiga goti 🧎‍♂️Aliomba msamaha.fedhea ilimkamata. Ikawa zamu yake kulia Kwa uchungu

       "Sintakusamehe Omario Hadi naingia kaburini. "Bibi mama Mkwe alitoa kiapo. Nyomi la watu waliokusanyika pale lilianza kupiga kelele na majadiliano mazito. Wengi walimlaumu sana Omario kutaka kifo bandia. Polisi waliingia ndani ya ile Hospitali kuanza kumtafuta Dakta Eze. Dakta alikamatwa Kwa kosa la utovu wa madili kazini. Yawezekana vipi akubali kumsaidia mtu afeki kifo chake. Pesa na rushwa  ndogondogo zilimponza yeye pamoja na Mume wangu Omario wakapandishwa ndani ya Difenda la Polisi.

     Veronica alipoona na kusikia mambo tayari yashaharibika mrembo yule akavua vile viatu vyake vya mchuchumio 👠 alichomoka na kukimbia kama Roketi. Police hawakumuacha walimkimbiza Hadi pale walipomwona anatoka nje ya geti la Hospitali. Ghafla polisi walikuja kusikia sauti kuu ya kilio, Gari iliyokua inaongoza msafara wa Waziri mkuu kuelekea. Ikulu ilimgonga Vero akadondoka chini na kuharibu ule msafara wa Waziri mkuu. Kwani aliachwa afie pale? Never. Alisombwa, pingu🔗mkononi, miguu wake mmoja ulikuwa regerege ushavunjika. Machozi na majuto yalimwandama.

 """""""”"""""""”""""
         Wiki Moja baadae nilirejea Hospitali ya Ocean Road, hapo tayari nishaomba Taraka yangu Mahakamani. Sikuona umuhimu au uhitaji wa kuishi na mwanaume mpumbavu na mjinga msaliti. Mie Shania nikajiketisha kwenye bustani ya Maua pale kwenye Bench  nililofuatwa na Nesi Rozana. Nesi aliyenisaidia kuwatumbua wale wahujumu watatu: Dakta Eze, Omario Mume wangu na Malaya wake  Veronica.


Niliketi pale nikiwa na matumaini ya kumuona Nesi Rozana, pembeni yangu nilikua na Box lenye Zawadi ya gauni 👗zuri nililoagiza kutoka Venezuela🇻🇪. Kama zari vile Rozana alitokeza, nikamkimbilia,🏃‍♀️ nikamkumbata🫂🤗 na kumbusu viganja vya mikono yake, 😽ishara ya upendo. Akatabasamu na kufurahia.

      "Asante sana Nesi, Asante umeniokoa." Nilimshukuru Rozana.

       "Siku nilipowafumania wakifanya mapenzi hawakuniona lakini nilijua mambo hayapo sawa." Rozana aliniambia

       "Umenifaa sana Nesi, umenifanya niujue moyo wa Mume wangu, kumbe alikua na siri nzito ya kipumbavu. Wacha akaozee Jela na Taraka nishaiomba Mali na pesa tutagawana pasu kwa pasu" Nilimwambia Nesi.

      "Pole pia maana alikuweka katika nyakati ngumu za maombi na machozi" Nesi alinifariji.

      "Mie nsha' poa." Nikachukua Box zuri lilipambwa Uaridi 🌷 nikamkabidhi Zawadi yake Alipoifungua almanusura macho yamtoke 👀na kumdondoka, aliipenda sana ile Zawadi. Rozana akanikumbatia na kunibusu shavu langu 😙 nikatabasmu.😇☺️

**********
TCHAO 👋👋






      

       


     



       

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...