Wednesday, April 30, 2025

I promise you

  

I PROMISE YOU.

(NINAKUAHIDI.)






SURA  YA KWANZA.


UBAYA WA POMBE.


“Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini lakini? Kwanini unanifanyia hivyo?” Brenda alinilalamikia. Machozi yake yakimtiririka kwa wingi kama mvua inayomwaga maji yake jangwani, mara baada ya ukame wa muda mrefu sana kulitikisa hilo jangwa.

               Ni ukame? Ndio ni ukame na ukame huo kwangu mimi Job naweza kuuita umasikini, umasikini uliokithiri, umasikini mkubwa haswa, umasikini wa kutupwa, umasikini ambao kamwe mpenzi msomaji hauwezi kuuokota, lakini looh! Sina jinsi ninakubaliana na hali halisi ya maisha  yangu mimi na huyu anipendaye Brenda. Machozi yake yanaumiza tena yanaumiza sana. Brenda wangu analia lakini nifanyaje mie job ningali bado ninafikra zile zile kwamba ipo siku mimi na Brenda tutakuja kuuaga umasikini na kuja kuishi maisha ya furaha na starehe.

                “Ipromise you, Ipromise you Brenda, I will fulfill all of your demand, you just have to wait , a beautiful time and a beautiful moment will come.” Ilo lilikua jibu langu, jibu ambalo nimekuwa nikimjibu Brenda kila siku ya leo, nikiziona hasira zake zinamtuma kugadhibika mambo yasije kuharibika.

               “Mpaka lini Job? Mpaka lini mpenzi? Niambie ni lini utatafuta mahari ili niwe wako  milele? Ni lini utaniweka ndani ya nyumba yako ili siku moja nije nipate kuishi kwa furaha pamoja na wewe? Ni lini Job?” Brenda aliongea tukiwa tungali ndani  pori lenye nyasi fupi,  wawili tupendanao .

             “Tambua kwamba na mimi pia ni mwanamke, tena ni mwanamke sawa sawa na wanawake wengine walio olewa, ndani na nje ya kijiji chetu wapo mikononi mwa waume zao wanafurahia mapenzi, nina imani kwamba mapenzi yao ni zaidi ya mapenzi, mapenzi matamu kama pipi, hayo ndiyo nina haja nayo, ya kwamba nina kuhitaji sana Job, ninahitaji niwe moyoni mwako nipate raha na furaha, nipendwe kama wanavyopendwa wanawake wengine” Brenda alilia.

               Nilimsikiliza tena nilimsikiliza vizuri sana Brenda wangu daima sina ile tabia ya kumkwaza mwanamke huyu, daima nimekuwa msikilizaji wa  wa shida na malalamiko yake lakini ubaya wa masikio dume niliyo nayo nimekua mgumu kumtimizia yale yote ambayo Brenda wangu amekuwa king’ang’anizi wa hayo anayo yatamani.

              “Hupaswi kutumia imani pekee mpenzi wangu Job, imani isipokuwa na matendo hiyo sio imani imani hiyo ni imani iliyokufa, imani batiri. Tafuta kazi, kazi nzuri itakayo kulipa mshahara mnono, au  jaribu kutafuta mtaji jiajiri, kazi yako binafsi. Mpenzi nimekuwa nikikushauri kila siku juu ya jambo hilo la thamani ajabu sikio la kufa halisikii dawa, unanipuuza mpenzi, wanisikiliza lakini hautendi kama ninavyokushauri, ushauri bora kama huu.” Brenda alinishutumu.

              Alikuwa na haki ya kunishutumu, kwa sababu mimi binafsi nimekuwa mzembe sana kwake,daima sina mbele wala sina nyuma, nipo nipo tu hapa kijijiini  goigoi ndilo jina langu, kila mwanakijiji ananijua na kunitambua kwa jina hilo, jina la goigoi, yaani mvivu mzembe, kijana dhaifu. Burudani yangu kuu ni kushinda kwenye bunge la walevi huko nitayapiga maji, nitapiga nitapiga hadi nivae miwani nikiisha kuvaa miwani nitajikokota kokota kwa kujilazimisha nifike nyumbani kwa babu na bibi yangu waliionilea kama yai la kuku. Njiani nitajibwaga bwagaza nitaongea kila neno la kilevi nitachekwa na wapitao njia, watoto watanizomea hilooo! Hiloooh! Hilooo! Yuuuuuu! Yuuuuu! Yuuuuu! Lilevi hilo, goigoi hilo!” loo! Mazomeo hayo ni mazomeo ya kila siku, watoto hawachoki kunizomea


            Watoto wataniimbia nyimbo za dhihaka, yote kwa sababu mimi mwenyewe ninafanya dhihaka. Pombe sio chai, tayari sarawili yangu imeloa mkojo, imezingarwa na inzi kibao wanaoimba ‘ziii….. ziii…ziii’ nyuma ya matako yangu, looh! Jamani kweli pombe sio chai, mwenzenu tayari nimejinyea tena nimeharisha. Vibaya mno, watoto hawakomi kunidhihaki kwa nyimbo zao.

Jobu akilewa lewa,
Anashindwa kujielewa lewa.
Kikojozi huyo, kikojozi huyo,
Avishwe nepi huyo, kajinyea huyo,
Huyoooo, huyoooo, huyooo,
Mtu mzima ovyo.

Oosh nyimbo zao haziniingi ndani ya ubongo wangu, ninaona ni kama burudani , nami ninaimba kwa kuwaigiliza, ninacheza kama wanavyocheza wenyewe, looh! Ama kweli pombe sio  chai, watoto wamenizoea vibaya sana, hawachoki kunikebehi kwa nyimbo zao haweshi kunizomea, haweshi kunirushia mawe haweshi kunipiga kwa bakora, yaani hadi aibu, aibu jamani aibu mtu mzima ovyo ninapigwa kwa bakora, ninapigwa kama mwanafunzi wa praimari skuli.

                 Hili jicho langu la mashoto halijapotea bure, nimekuwa chongo kwa sababu ya kujitakia mimi mwenyewe, nilijitakia kijana wa kijijini, ndo’ kusema pombe sio chai, walinena wahenga; “kipofu akimwongoza kipofu mwenziwe wote watatumbukia ndani ya shimo.” Mimi ni kipofu wa pombe (ulevi) na pombe yenyewe pia ni kipofu ambaye hachoki kunipotosha pamoja na kunipitisha njia zenye hitilafu.

                Pombe ni kipofu, ndio ni kipofu, kwa sababu haoni mdudu huyu, haoni mbele, haoni nyuma, kazi yake kubwa kupotosha vijana wa kijiji ninacho ishi.
Ninaukumbuka ule usiku usio na mbalamwezi, usiku ambao almanusura niwe kipofu wa macho yangu yote mawili lakini hata hivyo ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, niliponea chupu chupu kufa, nusu kufa, mjiti uliniingia ndani ya jicho langu la kuume, duh! Ni kama vile ulikua mtego, mtego uliotegwa kwa makusudi ili unikomeshe mie goi goi nisiye taka kufanya kazi.

               Niliteleza kwenye tope ambalo lilijikusanya pahali mara baada ya mvua kunya usiku kucha. Ilikua ni usiku, usiku usio na mbalamwezi, sikumbuki ilikua yapata saa ngapi, usiku ule mie kijana goi goi mvivu nisiyetaka kufanya kazi nilitoka kwenye bunge letu, bunge la walevi. Nimegida mitungi ya kutosha, sina hofu, nimekwisha kuzoea kwenda bungeni saa za majogoo na kurejea nyumbani saa za kulia kwa mabundi na mapopo. Mimi ni Mbunge mtiifu wa  gongo, changaa na matapu tapu mengine mengi yaliyopitwa na wakati.

Daima nipo, sikosekani kwenye bunge letu la walevi wa kijiji chetu,  huu ni mwaka wangu wa tano ningali bado nipo bungeni na uzuri wake  kwa sababu nina maudhurio mema sina budi kujitapa kwa cheo chema nilichopewa na walevi wa kijiji chetu. Spika wa bunge la walevi, hilo ndilo jina langu, jina tukufu ulevini.

                Nisikufiche mpenzi msomaji, nilijikuta najistafisha kuhudhuria vikao vya bunge la walevi, nilijiuzuru mimi mwenyewe pasina shinikizo la wabunge au mawaziri wa bunge letu, bunge la walevi, sababu kuu ikiwa ni kukumbwa na mkosi huu mzito wa kugeuka chongo na chongo yenyewe niliivuna kutokana na ulevi wangu wa kupindukia.

                Usiku ule nilikua bize nagara gara ndani ya dimbwi lenye tope, ili nipate chance ya kujiokoa na kutoka ndani ya lile dimbwi nililo tumbukia kutokana na ulevi. Nilikuwa bwii kwa pombe ya gongo,  nilifanya kila niwezalo nipate kujiokoa kutoka kwenye lile shimo lenye tope,  nikiwa bado ndani ya lile dimbwi nilijiuliza nitatokaje ili nipate chance ya kwenda nyumbani kwa babu na bibi nikajibwage kitandani, niusake usingizi wa pono ili nipate kujiandaa  asubuhi na mapema niwahi bungeni  kupiga mitungi. Haki nilikuwa mlevi, mlevi mbwa, mlevi aliyeshindikana.

Jitihada za kutoka ndani ya lile dimbwi hazikuzaa matunda, nikajikuta napiga kelele za zilizotokana na maumivu makuu, maumivu yasiyo na kipimo, maumivu yasiyo na kikomo.

                 “uwiii! Uwiii! Uwiiii! Yallah toba we! Jicho langu jamani jicho langu! Nafwa mie, nafwa jamaa” kilio kilinitoka, kilio cha mlevi mwendawazimu, kumbe nilidondoka, kumbe nilidondokea kwenye shimo lililokuwa na miiba mirefu, mikavu iliyochongoka kama pini, ikauchoma choma mwili wangu na ubaya wake jicho langu la kuume(kulia) halikupona lilikua ni miongoni mwa sehemu zilizoonja shubiri ya mwiba, lilikua kwenye ile ajari ajari ya mlevi, ajari ya kujitakia.

                Ndio maana nimekwambia mpenzi msomaji nilijikuta naachana na ulevi, nilijikuta naachana na mazowea ya kwenda kwenywe bunge la walevi, nilijikuta najiuzuru cheo na wadhifa wakuwa spika wa bunge la walevi, ilinibidi niachane kabisa na pombe. Walisema wenye hekima asiye fundwa na mamaye ulimwengu utamfunda. Mama na baba yangu walikwisha tangulia mbele za haki sikupata nafasi ya kufundw a na wazazi wangu, malezi yaliyo jaa madekezo mapendeleo na matunzo ya kiyai yai ndiyo niliyapata kutoka kwa babu na bibi wazazi wa baba.

                Mapendeleo yasiyo  na kipimo, mtoto toka utotoni hadi baleghe sikua na nafasi ya kujishughurisha na shughuri yoyote ile ndani ya nyumba ya babu na bibi yangu, ni madekezo tu madekezo na mapendeleo, nililishwa vizuri, nilinyweshwa vizuri, niliogeshwa, nilibebwa nikapewa kila kitu nilicholilia na baya zaidi nikawa mtoto msumbufu, mwenye masumbufu makuu.

                Kila lenye mwanzo halikosi mwisho, kwenye kuzaliwa kuna kufa, kwenye raha kuna karaha, kwenye amani vita pia ipo, sikutilia imani mawazo hayo hapo juu , ubongo wangu ulikorea pombe, pombe ya matapu tapu, ubongo huu mbovu usojua la muadhini au mnadi swala maisha yangu yalikua ni maisha ya kunywa matapu tapu ya aina mbali mbali, iwe umkombothi, iwe ulanzi, iwe mbege, iwe chibuku, ubwala, gongo, pombe ya minazi, pombe,  pombe, pombe,  pombe…….. Kila aina ya pombe kali mie nilikunywa, pombe kali kuliko sumu ya panya mie nilikunywa, pombe chungu kuliko nyanya chungu mie nilikunywa, nilijisikia fahari kunywa, nikalewa, nikasaza nikaburudika nikausuuza mtima wangu.

                 Leo nimeona wacha nifanye maamuzi magumu, maamuzi ya kuachana na pombe, pombe ni kipofu hawezi kuniongoza, ndiye aliyesababisha nitumbukie kwenye dimbwi lenye tope na katika harakati za mie kujiokoa nikajikuta natumbukia tena kwenye shimo lenye miiba iliyonigeuza chongo  jicho la kulia. Leo nifanye maamuzi ya kuikacha pombe, sio tu kuikacha pamoja na kujiweka mbali na pombe kusisitisha yale mazoea ya kwenda bunge lao bunge la walevi. Kama ni hasara jamani hasara kubwa nimeipata, hasara ya kulipoteza jicho langu la upande wa kuume. Sio hasara hiyo tu pia kuna ile hasara ya kujifedhehesha na kujiaibisha mbele ya watoto waliokuwa wakinizomea na kunichapa bakora.

                Katika kipindi chote hicho Brenda alinivumilia, Brenda hakuniacha japo nilikuwa mlevi nisiye na kikomo, na uzuri wa Brenda yeye kama mwanamke alijiweka tayari kunishauri niachane na hiyo tabia mbaya ya kupiga miknge, nalikuwa sikio lililokufa halisikii dawa, Brenda aliponiongelesha sikio la mashoto mie  nilijigeuza kiziwi, tena kiziwi anayesikia sauti lakini maneno hayaingii sikioni, Brenda akiniongelesha sikio la kulia bado nalijigeuza kiziwi nisielewe wala nisijielewe.

                Wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, tena wanasema ukijenga urafiki na mwendawazimu tegemea na wewe pia kuwa mwendawazimu, waswahili wako sahihi . mwanzo mgumu, lakini mwisho ni mazoea Brenda aliyekuwa kinara wa kunipinga nisinywe  matapu tapu kwa utundu wangu mie mwenyewe nikamuweka mtu kati nikamwonjesha matapu tapu kidogo kidogo, pole pole ndio mwendo, tabia ni mazoea Brenda akawa nguli wa kunywa matau tapu, akaifuata tabia yangu, tabia ya kunywa  kama mwendawazimu na kwa hilo mwenzangu mbona alitia fora. Alikunywa zaidi ya chupa kumi  za matapu tapu, zile chupa zenye ujazo wa bia aina ya Safari zilimtosha  usiku na mchana, Jua likichomoza jua likizama siku nzima.


                #########################################

Itaendelea



OMBI LA KIJINGA

 

OMBI LA KINGA.





SURA YA PILI


OMBI LA KIJINGA.


Ilipita miezi miwili, miezi ya ndoa yao, Happy aliukamata ujauzito, moyoni alikuwa na wingi wa furaha na raha tele, mumewe aliporejea nyumbani kutoka kazini akafanya hima hima kumweleza juu ya furaha iliyo moyoni mwake. Ilikuwa ni jioni moja tulivu, wawili hawa walikua na maongezi yao mara baada ya chakula Happness alianzisha maongezi.


                  “Mume wangu mpenzi leo nina taarifa njema ajabu.” Happy aliongea kwa furaha, akicheka cheka na kuichezea mikono ya mumewe.


                  “Taarifa gani hiyo mama.”Furaha alidadisi.


                  “Ndoa yetu imejibu, ningali nina ujauzito wa miezi miwili sasa.” Happy alitarajia mumewe angelionesha uso wa furaha lakini bila matarajio alishangazwa na mabadiliko aliyoyaonesha mumewe mpenzi. Sura yake ilijikunja, macho ya mumewe yakawa makali kama pilipili.


                   “What?!........ Nini?” Furaha aliuliza kwa ukali, happness alishangazwa na muitiko wa mumewe.


                  “ Mume wangu mbona unashanga au haujapendezwa na ujio wa taarifa hii njema?” Happy alimuuliza mumewe. Furaha aliyekuwa ametulia juu ya moja ya masofa mazuri ndani ya nyumba yao akanena:


                   “Sina maana hiyo, lakini mke wangu mbona mie sijajipanga kuitwa baba.” Furaha aliongea jibu lililomshangaza mkewe.


                   “Mume wangu haujajipanga kivipi wakati sie tuna kila kitu ndani na nje ya familia yetu!!?” Happness alimuuliza mumewe kwa mshangao mkuu.


                   “Mke wangu umri huu nilionao, umri wa miaka ishirini na minane ni umri ambao bado mimi ninapaswa kutafuta mali zaidi, tukiharakia kuwa na mtoto huyo mtoto atatusumbua.”


                  “kwa hiyo wewe unataka tufanye nini sasa? Wakati mie ninaujauzito wa miezi miwili.” Happness aliongea.


                   “Utanisamehe sana mke wangu kwa haya machache ninayotaka kuongea ninaomba ombi moja kwako, enenda ukautoe huo ujauzito.”


                   “What? Nikautoe ujauzito wangu? Hivi mume wangu una akili timamu wewe?”


                   “Utanisamehe mke wangu, sina nia au dhamira mbaya, kama ujuavyo tena hilo ni ombi langu.” Furaha aliongea, Happness alichukia. Zilipita siku tatu wawili hawa hawakuongea pamoja hawakula, hawakunywa wala kulala pamoja. Wakati furaha akimsistizia mkewe akautoe huo ujauzito kwa madai ati ajajipanga kumpokea Malaika mtarajiwa, Happness alitia mkazo hakutaka kuusikia upuuzi huo.


Ghafla upepo ukabadirika, Happness alibadiri nia, Ibilisi wa kutoa ujauzito alimwingia, aliona kuwa maombi ya mumewe ni bora zaidi kama ajuavyo yeye Binafsi ameolewa na bada ya kuolewa alipaswa kuheshimu mawazo ya mumewe. Alimpenda sana mumewe japo alisita sita kufanya kitendo kile kiovu, afanye nini jamani? Hana la kufanya roho yake ilimlazimu akubali na baada ya kukubali alimwambia mumewe yupo tayari kuutoa ule ujauzito.


                     Mume kusikia mkewe amekubali kuutoa ujauzito alifurahi sana, furaha iso na kifani, akamchukua mkewe ndani yamoja ya magari yake ya kifahari haraka akampeleka mkewe kwenye moja ya hosptali kubwa ndani ya jiji la Dar es saalam.


                     “Salamu Bwana Dakta, habari za kazi?” Furaha alimsabahi Dakta aliyemhitaji.


                    “Salamu bwana mdogo kazi yangu yaenda Vema, sijui nikusaidie nini?” Dakta alimuuliza Boss Furaha. Wakati huo wawili wale yaani Furaha na Happness walikuwa wapo ndani ya Ofisi ya Dakta. Dakta alikuwa na kiasi cha furaha usoni kwake, sababu alimjua vema Bwana furaha, ni miongoni mwa matajiri vijana ndani ya jiji la Dar e saalam. Basi Bwana Dakta alijiweka tayari kwa lolote lile jema la kumfaidisha.


                   “Bwana Dakta tumekuja mbele zako tuna tatizo, ni tatizo dogo sana, nina hitaji umflash mke wangu…..” Furaha hakumaliza sentensi yake. Alichukulia tendo la kutoa mimba kama jambo la kawaida sana.


                  “Una maanisha nimtoe Mimba?”


                  “Ndio bwana Dakta au mpaka sasa haujanielewa?”


                  “Ah! Hapana mkuu, lakini mkuu si unajua fika kuwa serikali inapiga vita utoaji mimba kwa wanawake na iwapo nikitenda hilo tendo ovu nitahatarisha ajira yangu, “ Dakta aliongea kwa miguno na wasi wasi.


                   “Sikiliza Dakta ninahitaji utende tendo hili uwezavyo, nitayaboresha maisha yako ukinisaidia.” Furaha alimshawishi Dakta.


                  “Lakini…………!” Dakta alionesha wasi wasi wake.


                  “Lakini nini bwana Dakta, embu tizama iwapo utanisaidia nitayaboresha maisha yako na wa kuyaboresha hayo maisha si mwingiune ni mimi.”


Dakta hakuwa na jinsi aliamua kula mlungula, alipokea rushwa ya pesa mingi, alikubali kutenda tendo la utoaji mimba, alikubali kumtoa mimba mwanamke yule, na baada ya kumtoa ujauzito alipewa chake, pesa mingi kweli, maisha yake yakawa bora na kuboreka.


Itaendelea sehemu ya  3


Friday, April 25, 2025

OMBI LA KIJINGA.

 

OMBI 🤲 LA KIJINGA.

 


 

 

 

 

SEHEMU YA KWANZA

WANAKUTANA.

           Bwana Masumbuko pamoja na bibi Mwema waliishi ndani ya jiji la Dar es saalam,🌃 Mbezi beach kwenye makazi yao, wana mjengo wa fahari bonge la jumba 🏘️na uzuri wa kujenga nyumba yao katika mazingira yale kuna utulivu mwingi pia kuna hali nzuri ya hewa. Wawili hawa hawakuwa ni watu wa daraja  la chini bali wawili hawa ni watu wa daraja la kati (middle class) yaani watu ambao wanajiweza kiasi fulani hawana shida sana💰💸, kama ni chakula basi chakula 🥪🍕kipo tele nyumbani kwao, kama ni manywaji 🍻🍷🥂basi manywaji yapo tele nyumbani  kwao, kama ni pesa hawana shida wanazo pesa nyingi na za kutosha.

               Mungu akuwatupa bali mungu aliwajaria kuwa na mtoto mzuri wa kiume 👼waliyekuja kumpa jina la Furaha, wakiwa na wingi wa furaha ya kumpata mtoto mwenye siha na afya tele. Kwa ujumla mtoto Furaha alizidi kukua na kuwapendeza wazazi  wake, kwa vile mtoto Furaha alilelewa katika maadili mema, alisoma   📚vema  kwa bahati nzuri Furaha aliweza kuhitimu elimu ya chuo kikuu, kwisha kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, furaha alipata kazi nzuri ya Ukurugenzi, akaketi Afisini, 📝akijizungurusha zungurusha juu ya kiti chake💺, kwa wingi wa furaha, raha na mapozi, hana shida tena, yeye ni mtu wa kuandika🖋️✍️ andika Afisini, yeye ni mtu wa kutia tia saini mikataba mbali mbali, akiwalipa watumishi wa kampuni aliyoajiriwa na kufanya kazi nyinginezo nyingi na muhimu kwake.


                Furaha hana shida tena, mshahara wake ni mkubwa wa kumtosha kununua Gari🚘 au kujenga nyumba na uzuri waa maarifa ya Furaha tayari amekwisha jenga nyumba na kununua gari zuri la fahari anapesa mingi ana raha tele, ametunzwa kimaadili ndio maana ana juhudi kazini kwake ana bidii pia.


                  Basi siku moja yapata juma tatu asubuhi Furaha alitembelewa na mgeni ambaye alikua ni binti👩 mmoja mzuri sana, anavutia kama Malaika ni mwema machoni na pia mzuri moyoni. Wakati yule binti anaingia ndani ya Afisi ya Furaha Furaha alijiweka bize akiandika andika mambo yake ya kiafisi. Akamkodolea macho yule binti mzuri kama uaridi, 🌹mkononi kwake alikua ameshikirilia bahasha ambayo kwa fikra za haraka ungelisema ni barua ameileta maalumu ajiri ya Bosi.


                 “Karibu sana Dadangu, ingia usiogope keti kunako hicho kiti” 🪑Furaha aliongea akimwelekeza mgeni aketi kunako moja ya viti vya pale Afisini.


                “Asante sana Bwana mkubwa. Habari za kazi, pole na majukumu.” yule binti mrembo aliongea maneno mazuri ya kutia moyo na faraja.


                “Kazi ziko poa, namshukuru sana Mungu pamoja na faraja zako.” Furaha alimjibu yule mgeni.


                 “Kwa jina ninaitwa Happness Magessa, mimi ni mzaliwa wa Musoma, hapa Dar es saalam ninaishi Kinondoni, kwa mara yangu ya kwanza nimejitokeza kuja kuomba nafs ya kazi kwenye kampuni yako.” Happness aliongea kwa ufasaha zaidi.


                   “Oooh! Karibu sana, mimi ninaitwa Bwana Furaha, nimefurahi sana kukufahamu Happness Magessa.” Furaha Aliongea


                  “Jambo jema ninalofurahia ni kwamba maana za majina yetu zinafanana, mimi ndiye Mkurugenzi mkuu wa kampuni hii.”


                 “Nimefurahi pia kukufahamu,” Happness Magessa aliongea naye akaendelea kunena.


                 “Bahasha hii ina CV zangu.” Akamkabidhi Furaha ile bahasha yenye Barua ya kuomba maombi ya kazi.


                  “Ok. Ok no problem, naomba uniache niipitie pitie, uje kesho kuchukua majibu ya maombi yako, uje muda wa saa tano nitakuwa tayari nimepata jibu sahihi.” Furaha aliongea maneno mazuri yenye kumpa yule binti matumaini.


                   “Asante🙏 ninashukuru, kazi njema.” Happness aliinuka pale alipoketi, apate kuondoka.


                    “Uwe na siku njema, 👋have a nice day.” Furaha alimuaga mgeni wake.


                    “Nawe pia, have a nice day too.”👋 Happness alirejesha majibu. Akatoka ndani ya ile Afisi akaelekea ilipo lift iliyomteremsha hadi Horofa ya chini .


Mara baada ya Happness kutoka ndani ya ile Afisi, Furaha akaifungua Bahasha aliyokabidhiwa na Happness, akaifungua kwa pupa pupa, alimradi apate jua nini kimeandikwa ndani.


                    “Waaoooooo!” ☺️Furaha alijikuta akiongea kwa furaha kuu, akiyashangaa shanga yale makaratasi yaliyokuwa ndani ya ile bahasha iliyoletwa kwa mikono ya Hapness mtimani akajisemea. “Duh! Kumbe huyu binti mrembo amesoma Oxford university? Mashallah! Vyeti na wadhifa uliopo humu unafaa kwa mtu huyu kufanya kazi hapa.” Furaha amejaa tabasamu, aliendelea kuongea.

                  “Lazima nimpe nafsi ya kazi ndani ya kampuni hii.” Furaha alihitimisha kwa furaha.

                                      ##########################

Yapata saa nne na robo asubuhi, Happness alikuwa tayari yupo Afisni, amewahi mapema ili asikilize majibu juu ya nafsi ya kazi aliyoitafuta, alimkuta secretary  wa ile Afisi ametulia tuli anakunywa chai ya maziwa na chapati, hana shida Binti yule analipwa vizuri ndio maana anazidi kunawili na kupendeza.

                  “Samahani ndugu Secretary  je nimemkuta Mkurugenzi?” Happness alimuuliza huyu binti ambaye hapo baadaye alikuja kugudua kuwa anaitwa Amina.

                   “Yeah! Umemkuta, utasubiri kidogo sababu ana maongezi na mgeni wake.”

                   “Ooooh! Sawa sawa  sio vibaya nitamsubiria.” Happness aliongea kwa matumaini.

                    “Waweza keti katika kiti hicho dada.” Amina alimweleza Happness mahali pa kuketi, Happness aliketi pale alipo elekezwa.

                     “Eliza!” Amina alimwita kwa sauti mmoja wa watumishi wa pale Afisini.

                      “Abee.” Eliza aliitikia na kuja pale alipoketi Amina.

                      “Embu mletee Dada supu aendelee kunywa wakati anamsubiria Mkurugenzi.” Amina alimtuma Eliza alete supu Happness apate kunywa. Happness aliona aibu kuikataa ile ofa alijikuta anakunywa kwa moyo mmoja. Akainywa ile supu iliyoletwa na Eliza na baada ya dakika kama 45 kupita alimwona mtu akitoka ndani ya Afisi ya bwana Furaha.


                      “Dada sasa unaweza kuingia, mgeni tayari amekwisha kuondoka.” Amina alimpatia ruhusa Happness apate kuingia Afisini kwa Bosi Furaha.


                       “Oooh! Thanks so much.” Happness alishukuru akainuka pale alipoketi akaingia Afisini kwa Boss Furaha. Happness alikuwa amependeza sana, ananukia marashi na manukato, wakati huo tayari Happness alikwisha kuinywa ile supu tamu iliyoandaliwa kwa wingi wa chapati.


                      “Oooh! Verly good, ni wewe Happness karibu sana, karibu uketi.” Aliongea Mkurugenzi mkuu, aliongea kwa bashasha hali ambayo ilimshangaza sana Happness ambaye hakutarajia kama angelipokelewa kwa wingi wa furaha ile.


                 “Asante sana bwana Furaha,” Happness aliketi kwenye kiti chake, wakatizamana uso kwa uso yeye na Bosi Furaha. Wakati huo Bwana Furaha alionekana kuwa ni mwingi wa tabasamu.


                   “Habari za toka jana?”🤝 Furaha alimsabahi Happy.


                   “ Nzuri,👍 ninamshukuru Mungu, je wewe una endeleaje Bosi?”


                   “Nami ninamshukuru Mungu.”


                  “Uliniambia nije leo baada ya jana kukuachia Bahasha ile yenye barua yangu ya kuomba kazi!”


                  “Ndio ninakumbuka vema, nimeisoma Barua yako na pia nimetizama wasifu wako, nimeona kumbe unafaa kufanya kazi pamoja nami.” Furaha aliongea maneno mazuri kwa Happness.


                  “Ooooh!” ☺️Happness alipumua kwa furaha.


                  “Asante sana Jehova.” Alimshukuru mungu kwa mazuri aliyomtendea. Basi kuanzia siku ile Happness alifanikiwa kufanya kazi katika kampuni ambayo Furaha alikuwa Mkurugenzi mkuu. Happy na Furaha walifanya kazi kwa pamoja kwa muda wa miezi saba, ndani ya muda huo walipata faida kubwa sana ukilinganisha na muda uliopita kabla Happy hajaajiriwa.




,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,




Furaha alipendezwa na uchapakazi aliouonesha Happy, Furaha alipenda Happy aje kuwa mke wake siku moja, mke wa ndoa, ukitegemea Furaha alikuwa angali bado hajaoa na pia Happy alikua hajaolewa. Furaha akamueleza Happy Hisia zake, hisia za mapenzi, pasina kuficha neno kumbe Happy naye alikuwa akimpenda Furaha, labda tuseme aliogopa kumwambia kwa hofu ya kuona kibarua chake kikiota nyasi. Wawili hawa wakapendana na kupatana kwenda kwa wazazi kujitambulisha


                   Uzuri wa kujitambulisha kwa wazazi wao waliwapokea kwa shangwe nderemo, vifijo na chereko, halikuwepo pingamizi juu ya hawa wawili waliopendana, kwa Baraka za wazazi wao walikubaliwa.


 Kama alivyofurahi Furaha ndivyo Happness alivyofurahi pia, awali alikuwa na hofu, hofu waliyo nayo wanawake wengi, wanaopelekwa nyumbani kwa wakwe zao, alitia hofu yawezekana wazazi wa mchumba wake wakamkataa mwanamke huyo, kwa madai kwamba wamemtafutia Furaha mchumba wa kumuoa. Mungu yu mwema kwa Happnes haikuwahivyo.


 Hatua iliyofuata ilikua ni kufunga ndoa, karamu kubwa ilifanyika, ilikua ni bonge la karamu, karamu ya kifalme. Baada ya kumaliza fungate maisha ya ndoa yalianzia hapo. Wakaishi kwa kujitegemea, uzuri wa maisha yao wawili hawa walikwisha kujijenga kiuchumi, wangali wana mali nyingi pamoja na vitenga uchumi kibao. Kwa kifupi hawakuwa na shida.

 Itaendelea sehemu ya pili. 


WATABAKI NA LABDA

 




MIPASHO YA MAMSAPU

WATABAKI NA LABDA


Sehemu ya nne


Bwaga moyo wako chini, ubwage huo moyo wa tamaa, bibi litafute ‘solution’  juu ya tatizo la mumeo. Kwanini USIMRUDIE MUNGU? Mwaya, MUNGU NI PENDO, APENDA WOTE. Wenye madhambi na waso na madhambi mbele ya mungu wote ni waja wake, Vijori wake na kondoo wa malisho yake. Basi bibie yasije yakakufika shingoni mwenzetu ukazama. Jijue kuwa bado unayo nafasi ya kumuokoa mumeo. Anza sasa, anza leo, wakati ni mida na mida ndio sasa.”

 

 Ngoja nikupe mfano mmoja Sophia wangu. Ni hivi bibie, huko ZAMBIA kuna mwanamama alijaa wivu na gere, maneno ya majirani, wambea na washambea yalimpatia Stress isiyokwisha. Mara wamtonye, ooh, mumeo hajatulia, ooh, mumeo yupo na huyu yupo na yule, ooh, mumeo…..oh, mumeo……. Ndo ikawa hivyo Mzambia huyu alibaki na Labda, akijisemea moyoni mwake, Labda kweli jamoni, lisemwalo lipo kama halipo langojewa. Pasina kufanya uchunguzi wa dhati bibie Mzambia akapata wazo, wazo lililomsukuma afunge Safari kwenda kwa waganga wa kienyeji, ati, Kusaka dawa ya kumtuliza mumewe,  ‘Teeh teeh teeh,’ Bibie Mzambia alibaki na labda, ai! Jamani, ati tangu lini mume atulizwe kwa dawa za Kienyeji?

            Jamani mapenzi hayatafutiwi dawa kwa waganga wa kienyeji, mapenzi ni maelewano, mapatano na makubaliano, maagano na masikilizano, dawa ya mapenzi ni kutenda kile ulichonena, kwenda kwa waganga wa Jadi ni kuyavuruga mambo na kujiongeza matatizo nyumbani.

            Eh, ikawaje? Kama wahenga walivyosema mwanzo wa hadithi kuna mwisho wa hadithi. Hadithi yaweza kufurahisha au kuchukiza kuonya au kukosoa, yalomkuta Mzambia Mwaya enenda kawaulize Wazambia, kamwe wasisite kukudodosa mawili matatu waliyoyaona huko. LIMBWATA , jina baya kama shetani, alipewa akarikoroga kwenye mlo wamlo wa mumewe, mtoto akafanya kama alivyo ambiwa, sasa kumbe alisahau ule msemo wa watasha “TOO MUCH IS HARMFUL” Ikizidi inaua, ikizidi ni hatari hatarishi.

            Mzambia akazidisha madawa, ati apendwe sana na mumewe, Shoga yaliyomkuta ni aibu na fedhea, Ghafla bin vuuu mara baada ya mumewe kubugia matonge mawili ya NGUNA,  papo hapo akajikunja kunja akabadirika na kuwa Nyoka, lolioooh!  Mbona nyoka sio nyoka bali ni Chatu jeusi tii kama chungu. Lile Joka likamwandama Mzambia Popote pale aendapo wacha na lenyewe liende, Jamani aibu woga na fedhea, kila dawa aliyoitumia ili kumrudisha mumewe katika hali yake ya ubinadamu haikuzaa matunda na ajue fika kuwa ALIYEMSAIDIA KUMROGA MUMEWE TAYARI AMEKWISHA KUFA, sijui kama atafufuka.

            Maji yakamwagika, ndugu, jamaa na marafiki wakapigilia msumari ili kieleweke, liwalo na liwe tunamtaka ndugu yetu, tena umrudishe katika hali ya ubinadamu. Ikawa hivyo tena, MASENGENYO na MANENO VUNDO MNUKO yakapamba moto, tena yakafika mbali na kudondokea kwenye Vyombo vya Habari, Mwanamke akachafuka sana hata ashindwe kujua ni dawa gani aitumie ili kumrudisha mumewe katika hali yake ya ubinadamu. Ndo’ ikawa hivyo tena SOPHIA shogangu wivu mwingine uwe ni wivu wa kutafakari, waganga wengine Noma. Angalieni jamani waliomsaidia Sophia  kumroga Mumewe tayari wesha kufa, Oooh! Sijui ataipata wapi dawa ya kumrudisha mumewe kutoka kwenye ujoka kwenda kwenye  ubinadamu

            ‘Teeh teeh teeh,’ Mzambia alibaki na labda, aibu na fedhea, ndo maana kusema  maneno mengine yanafirisi, maneno mengine hasara.

Safari yangu mie Mamsapu mlo wa mumewe, mtoto akafanya kama alivyo ambiwa, sasa kumbe alisahau ule msemo wa watasha “TOO MUCH IS HARMFUL” Ikizidi inaua, ikizidi ni hatari hatarishi.

            Mzambia akazidisha madawa, ati apendwe sana na mumewe, Shoga yaliyomkuta ni aibu na fedhea, Ghafla bin vuuu mara baada ya mumewe kubugia matonge mawili ya NGUNA,  papo hapo akajikunja kunja akabadirika na kuwa Nyoka, lolioooh!  Mbona nyoka sio nyoka bali ni Chatu jeusi tii kama chungu. Lile Joka likamwandama Mzambia Popote pale aendapo wacha na lenyewe liende, Jamani aibu woga na fedhea, kila dawa aliyoitumia ili kumrudisha mumewe katika hali yake ya ubinadamu haikuzaa matunda na ajue fika kuwa ALIYEMSAIDIA KUMROGA MUMEWE TAYARI AMEKWISHA KUFA, sijui kama atafufuka.

            Maji yakamwagika, ndugu, jamaa na marafiki wakapigilia msumari ili kieleweke, liwalo na liwe tunamtaka ndugu yetu, tena umrudishe katika hali ya ubinadamu. Ikawa hivyo tena, MASENGENYO na MANENO VUNDO MNUKO yakapamba moto, tena yakafika mbali na kudondokea kwenye Vyombo vya Habari, Mwanamke akachafuka sana hata ashindwe kujua ni dawa gani aitumie ili kumrudisha mumewe katika hali yake ya ubinadamu. Ndo’ ikawa hivyo tena SOPHIA shogangu wivu mwingine uwe ni wivu wa kutafakari, waganga wengine Noma. Angalieni jamani waliomsaidia Sophia  kumroga Mumewe tayari wesha kufa, Oooh! Sijui ataipata wapi dawa ya kumrudisha mumewe kutoka kwenye ujoka kwenda kwenye  ubinadamu

            ‘Teeh teeh teeh,’ Mzambia alibaki na labda, aibu na fedhea, ndo maana kusema  maneno mengine yanafirisi, maneno mengine hasara.

Safari yangu mie Mamsapu


na roho wangu Pompo ingali bado ndefu, ndefu ya kula chumvi nyingi, kama ni sukari, tayari tushalamba kama ni asali tushalamba sana, sasa nyie akina Mariamu pamoja na Sophia mwatutakia nini sie? Au ndo hivyo tena mnahitaji kubaki na labda, LABDA ETI: pompo atanitupa na kuniacha aje kujipendekeza kwenu nyie viroboto ‘teeeh teeh teeh ‘ kamwe Pompo hawezi kunitema kaniweka moyoni anashindwa kunitapika, kaniijua na mie n’shamjua , kanivaa na mie n’shamvaa, mapenzi maelewano, yenu nyie macho.


            Hana Siri Pompo yeye ni mtu mzima, mzima wa 40 hivi na mie ni mwanamke wa 32 hivi tunayala maisha yenye tunu, tunu za raha na mustarehe, mahaba na mahabati, tushavumilia mengi lakini haya tena ya kuibiana waume zetu hapana jamani hayavumiliki, lazima niseme ukweli toka moyoni na ukweli huo unauma na kuchoma mtima


            Nishasema Pompo hanaga Siri kwangu lazima aseme aseme yalo moyoni mwake ili hao waso na makabati wajichange wakanunue makabati tena makabati yenyewe yawe ni makabati yenye vitasa na funguo nzito zisofunguka. Mbona Mariamu alipojipendekeza kwa mume wangu Pompo , POMPO ALINIMWAGIA MTAMA na mie nikaelewa, ndo hivyo tena Sophia naye kaingia kwenye anga za wenyewe amekuja na gia ya kudai ati Mumewe kibamia chake Kimelegea mlaini kama mrenda, hakiwaki bali kimezima kama mshumaa uliokwisha mafuta yake na suluhisho la yeye kuupooza mtima wake ni kwenda kwenye hayo MADANGURO yaso mbele yaso nyuma


            Bibie hana haya huyu kutwa kuchwa kigulu na njia KUDANGA na KURUKA UKUTA wakati huo huo Issa mumewe yupo, yule mume wa ukweli, dume la zamani halina mbele halina nyuma ni mfano wagari lililokwisha isha mafuta. Teeh teeh teeh sijui Shoga zangu sijui kama hilo gari litakwenda Salama


             Jamoni, mie naumia, ninamwonea huruma Issa angali baddo ni kijana mdogo, kijana wa 30 hivi, ana umbo la kimazoezi ‘Body bulder’ ana sura nzuri ya kutamanisha, amekamilika kila idara, ndo hivyo tena Sophia kaharibu mambo hata asijue nini cha kufanya Ilihali mganga aliyemkorogea mumewe tayari Keisha fariki, kafariki na zile dawa za kumfungua Issa mume wa SOPHIA, kutoka kwenye ULIMBWATA kwenda kwenye UTIMAMAU wake


            Sophia, naanza kumchukia bibi huyu, namchukia kama nini? Ndo’ maana sipiki chungu kimoja na yeye, yeye mwenye roho ya kutu, Si alijifanya yeye ndo nambari one katika kujishaua na kujipendekeza kutongoza waume za watu, basi akafanya KUMTOKEA mume wangu , roho wangu Pompo.

Monday, April 21, 2025

WATABAKI NA LABDA

 





MIPASHO YA MAMSAPU

WATABAKI NA LABDA

SEHEMU YA TATU


Keisha kuyavulia nguo na sasa ayakoge, jamoni  taarifa zingine zinafirisi, sio kila biashara yazalisha faida zipo hasara pia, maneno ya shogaze yashamtia DOA, doa ambalo yeye binafsi hajui ataliondoaje Keisha zidisha maji kwenye unga, hicho KIDUDE kilicho ndani ya SEREWILI ya mumewe teeh teeh teeh 😅🤣, HAKINYANYUKI wala HAKISIMAMI, kime SINYAA balaa, yote kwa sababu Sophia kayakoroga ajabu yashamrukia usoni yana muwasha kuliko kawaida, anajuta majuto mjukuu.


 Ooh! Jamani, hapo zamani za kale mumewe alikuwaga ni dume la nguvu, DUME LA SHOKA, ajabu leo mumewe hana mbele hana nyuma na baya zaidi hiyo nyumba ya Sophia hawakosekaniki wanawake wawili ambao ni Sophia na mumewe Issa.🧍‍♀️🧍‍♀️


Mmh! Bora aibu kuliko fedhea, mwaya mnakumbuka zile zama za mapenzi moto moto ambayo Sophia aliyapata kutoka kwa mumewe Issa, leo hii hata akitaka kuzrudisha kamwe hazitarudi tena, Ijulikane kwamba muda ni wakati na wakati yapaswa utunzwe vema na pia utumiwe vema. Kuishi na mume hakumaanishi ati unatakiwa uachiwe pesa mingi za matumizi bali kuishi na mume ni kwa kutumia hekima, busara na akili nyingi. Ndo’ maana hata Baibo inasema:✝️


“Enyi wanaume muishi kwa kutumia akili pamoja na wake zenu, enyi wanawake muwaheshimu waume zenu.”


            Je, Sophia alimuheshimu mumewe? Kama kweli Kama kweli angelimuheshimu mumewe asingelikwenda kwa waganga wa jadi kumchimbia miti shamba ambayo leo hii mumewe amegeuka mwehu, ubaya wa kumlisha mumewe limbwata, leo hii Sophia  anatanga tanga na njia KUDANGA, KUDANGARUKA na KUDANGANYIKA kageuzwa KIPORO cha hao majanaume tamaa, hana mbele hana nyuma AMEBAKI NA LABDA


Shoga, wenye hekima tunamwambiaje, afanye Juu chini kuliokoa Jahazi SIO POA atachepuka hadi lini? Wakati anajua fika kuwa MWAJABU yule jirani yake yalomkuta hawezi kuyasimulia MWAJABU alijifanyaga bibi mtukufu na mwaminifu  ndoani, wakati huo huo kumbe anamtoroka mumewe anakwenda ‘GESTI RUMU’ kudanga na hao wahuni wenzie wapendao  anasa za dunia ya leo ambayo hata hivyo ishageka Kijiji.


            Basi babu we! Yalomkuta Mwajabu leo ashindwe kuhadithia. Mumewe alikwisha kuambiwa yote juu ya huyo bibie mdangaji. Akafanya uchunguzi wake, katika kuchunguza chunguza naye akagundua, alah! Kumbe, mkewe sio mwaminifu…………. Ukweli ndio huo sioni haja ya kuirefusha simulizi lenyewe.


            Shoga njoo nyumbani Kigamboni  nitakupeleka  makazi anayoishi Mwajabu, yule mrembo aliyetikisa Jiji kwa kung’ang’aniwa sana na vidume mchepuko ukimwona huwezi kuamini, yaani mwaya sio yeye tena bali ni kicheko na kichekesho😆😅

            “BUBU,” Nisimwite Bubu jamani, Keisha laaniwa mdomo wake.

            “KIZIWI,” Mwaya, Mwajabu hasikii tena, kawa kiziwi ngoma masikio

            “KIPOFU,”  Huruma shoga, mdangaji kawa kipofu kwa kumwagiwa TINDIKARI na Tindikari yenyewe alimwagiwa usoni, ile amefumaniwa kule  Gesti rumu

            “KIWETE,” Oh! Jamani, 😭Mwajabu hana hana miguu tena. Nakwambie shoga kakatwa katwa ‘Mapangashwaaa’ yaani hana hips hana paja kabakia mifupa kama miguu ya kuku. Oneni sasa mashoga zangu hayo ndio malipo ya usaliti.


Na alie tu! Asijue kuwa aliyemtendea yote hayo ni mumewe bwana Abdul, mpole machoni, huruma mikononi lakini kumbe ABDUL ni pili pili moyoni. Haki! Tusolijua litatusumbua.


            Shoga, waweza kuyateka MAWAZO ya mtu mdomoni lakini usijiaminishe ati, waweza kuuteka MOYO wake mazimaa. Teeh teeh teeh (nacheka mie), UTABAKI NA LABDA


Nilimwambia tena Sophia nilimwambia pale alipokosea aparekebishe la sivyo yatazuka yakuzuka, muda ni wakati na wakati ndio sasa, yakizuka yale ya kuzuka jamoni! Sijui kama atapona mtu hapo, sijui kama atabaki mtu hapo, vumbi si vumbi, upepo si upepo, ndugu Wataliamsha DUDE, itakuwaje jamani? Bora nusu shari kuliko shari kamili. Basi mie Mamsapu, mama wa kitanga nikampa Sophia VIDONGE VYAKE, akimeza akitema shauri yake. Japokuwa mie na Sophia HATUIVI CHUNGU KIMOJA lakini Shosti, Baibo inasema “ Adui yako mpende kama unavyojipenda wewe mwenyewe.” Duniani kuonyana sio kwa maneno matupu bali pia maonyo yaendane na mifano kuntu iliyo hai.


            “Sophia mwaya nisikilize.” Nikamuweka Sophia kati nimmalize kwa mifano iliyo hai na madhubuti.


            “Yote hayo uliyotenda ni MAPITO mwanamke, unapaswa kujielewa, wewe ni nani? Unakazi gani ya kufanya au hauna kazi gani muhimu ya kufanya? ISSA ni mumeo, ulimpenda sana zamani lakini kwa sasa USHAYAGEUZA, USHAYAHARIBU USHAYAKOROGA. Mmh! Sijui USHABAKI NA LABADA?”


            “LABDA! LABDA! LABDA!LABDA! Teeh teeh teeh, labda ufanye nini ili kumrudisha mumewe, kwenye ‘Position’ yake, kwenye ile hali yake aliyokuwa nayo hapo awali, kwenye wajibu na jukumu lake kitandani. POLE dada, pole sana, yalokukuta ndo’ hayo, mawazo mengi hasara.”


My wangu sio poa niruhusu nikomee hapa kwa Leo

Kesho mapema tu LABDA nikipata bando  nitakutafuteni 

Tulinywe libeneke.

Saturday, April 12, 2025

WATABAKI NA LABDA





MIPASHO YA MAMSAPU


WATABAKI NA LABDA


Sehemu ya pili.



                 “kaolewa?”👰💍 Yes, Kaolewa,kawekwa ndani akiwa na mtoto mmoja wa KUPANDIKIZWA, yaani mwaya mtoto aliyenaye Mariamu sio wa huyoo mumewe anayedunda naye, shauri ya umalaya na ufuska ndo’ maana kamsaliti mumewe na ubaya wa yule mwanamke mumewe hana habari kwamba huyo binti mtoto aliyezaliwa kwake sio mwanaye bali ni mwana wa JIBABA lingine  lisilojulikana.


               Shoga, embu nikuulizeni :” Sasa kama Mariamu ana wa kwake mume, inakuaje anamfuatilia roho wangu Pompo? Ama labda anataka NIMKWIDE 🧨blauzi yake,nimtwage makofi,  nimjazie watu NYOMI, nimwaibishe mbele ya KADAMNASI, NIMPAKE MATOPE  achafuke, ‘teeh teeh teeh’🤣😅 uwezo huo ninao, niko fiti najiweza, nishindwe nini na huyo KIMBURUKUTU tamaa, kwanza yeye bado kwangu ni mtoto dogo dogo , MCHELE MCHELE, haniwezi kwa lolote lile, ‘ ‘mfyuuuuu’ (Namfyonya, afyonyeke)


            Dunia 🌍🗺️ishakuwa kijiji kuna mengi ya kujifunza na  kukumbuka mengine ovyo ovyo tu, kama alivyo Mariamu, yupo Ovyo ovyo LAFU LAFU. Ndo’ kafanya KUMMENDEA mume wangu Pompo n’shasema Dunia ishakuwa kijiji hakuna siri tena, Ulifichalo ⚫gizani litaonekana💡 mwangani,ulifichalo mwangani litaonekanagizani, kwanza mapenzi sio kulazimisha Mariamu kamtaka Pompo Moyo wangu kwa lazima, ajabu Pompo kamkataa na ubaya wa huyu bibi MCHEPUKO angali analazimisha.


               Nyonyo embu niulizeni, “ Ni kwanini Mariamu amekuwa king’ang’anizi? Ni kwanini Mariamu ana mg’ang’ania Pompo roho wangu?” ipo sababu nitawajibu shoga zangu, nitawajibu ni kwasababu wangu anauwezo, wangu sio mtu wa kukanyaga vumbi bali ni mtu mwenye hadhi 💰🏧yake, ana gari zake za kubadili badili, biashara zake zinaenda good, ni mtu anayejielewa na pia anaelewa maisha yanataka nini. Kwasasa tayari tume kwisha wekeza kwenye nyumba zetu tatu, moja  ipo MBEZI BEACH, ya pili ipo KIMARA TEMBONI  ya tatu ndo’ hii  yenye HOROFA TATU tunayoishi hapa KiGAMBONI.


          Jamani niachwe niishi, niachwe nijilie matunda yangu, niachwe nipumue na Pompo roho wangu. Kama ni kupanda  tushapanda mie na Pompo, kama ni kuvuna sioni aibu kusema ninavuna na roho wangu Pompo, kula lazima nile na roho wangu Pompo, ai! Babu we, mambo baaaaaadro.


                Kama ni dhiki basi hiyo dhiki ikupate wewe mwenyewe Mariamu, mie sinaga njaa kamwe, sinaga shida, NIMETULIA TULI KAMA MAJI MTUNGINI, sioni raha  ya KUDANGA   kama ewe bibi MDANGAJI,  huchoki KUTANGA TANGA KAMA KUKU, KUTWA KUCHWA  KIGUU NA NJIA, lo! Jamani ushayamaliz Malapa kwa kunyunda aridhi, ushavikomaza visigino kwa kutanga tanga kama kuku, lo! Wewe ni KAUKA NIKUVAE huna mbele huna nyuma, bado upo upo tu kama kichaa mwendawazimu.


               ‘Teeh teeh teeh🤤😆 (Nacheka mie) bibie haridhiki au labda haridhishwi ndo sababu haeshi kumsema mumewe kitaani ati mumewe  ana KIBAMIA, na kibamia chenyewe KIMEDODA, KIMEBUMA na KUCHACHA  kama vile MAHARAGWE YA MBEYA maji mara moja tu tayari yashaiva. Mmmh! Yangu mie macho mwenye masikio asikie.


           Amepungukiwa nini Mariamu, mbona hajitumi? Hajui kuwa yeye ndiye mwenye jukummu kubwa la kumjenga Mzee baba (mumewe), amjenge kwanza kwa vyakula bora vinavyotia NGUVU na MAFUTA,amjenge mumewe kwa MAZOEZI ya mara kwa marra, muhimu amjenge, yeye binafsi anajua fika kuwa NDOA HAIJENGWI KWA TOFALI, sawa anapaswa kumjenga mumewe kwa kutumia hekima, busara, saburi , uvumilivu, stara na mengi mengine yajayo yanafurahisha.


            Amjenge babu kisaikolojia, amwandae kwa kumkanda kanda kando la maandazi (massage) amgeuze geuze kama chapati (ampagawishe kimahaba) amfanyie maaandalizi yote hata yale ambayo babu yupo mgeni machoni kuyatazama


            Ndo’ maana nimewauliza waungwana enyi wajuzi wa KUTWANGA NA KUPETA, enyi wajuzi wa SITA KWA SITA, enyi wataalamu wamastyle kama yote kitandani:


 “kapungukiwa nini Mariamu?”


 “ANAFELI WAPI?”


“MBONA HAJITUMI?”


          Bibi ngoja nikwambieni, siku zote kwenye mapenzi babu hupenda kudekezwa  chumbani, babu hupenda kubembelezwa chumbani, lishike hilo  shoga, lishike hilo neno, usije ukaachwa solemba, usije ukaliwa kasumba, shanga zote zitakupwerepweta, si weye  mwanakwetu kutwa kuchwa walilia babu akubembeleze na pia babu akudekeze, shauri yako sie wakina mama wa kitanga tutakuibieni, maana sie wa kitanga kwa kubembeleza mume na kumdekeza, hatujambo👌, hapo ndo petu, patamu hapo, na ujue kwanini hatuachwi wala hatuachiki mapema kama nyie   mabibi wenye macho ya kutegemea mume akaufanyie kila kitu nyumbani. Eeenyooo, aibu shoga.👌


             Niambienini mwaya, kapungukiwa nini Mariamu hata afanye kumfuatilia pompo roho wangu?

 Kapungukiwa nini hata asidumu ndoani? Kutwa kuchwa anamtega wangu wa moyoni Pompo? 

Nyoooo, ATABAKI NA LABDA, Labda aende kwa sangoma apewe dawa ya kumteka kimahaba yule aliye wangu wa moyoni, labda aniroge ili nimteme Pompo  lakini hapa neva, hawezi, ajue tu kuwa mie ni toto la kitanga N’SHAFUNDWA N’KAFUNDIKA, Mapenzi ninayaweza, riziki nina jirizikia.


Ndo’ hivyo Jamoni nisiwafiche mie Mamsapu  Mama la kitanga, nikamvaa Mariamu nikampa VIDONGE VYAKE, akimeza akitema shauri yake, dawa ilimwingia kwa vijembe na kwa kejeli, Leo hii Mariamu akipita mitaani ananiogopa, ananipa heshima yangu tena ananisalimu kwa stara.


LISHAMUUMA Anajua sasa, anajua fika kuwa MUME WA MTU SUMU. Pompo ni wangu na wangu KEISHANIPENDA MWENYEWE. Nasemaje Mariamu akirudia , akijikoroga koroga Haki mie namgea NGEU namjazia watu NYOMI,  nd'o ajue fika kuwa mie SIO TYPE YAKE , atoke zake, atoke huko hana haya mwanamke huyu.


            Lina muuma hata leo hii lina muuma  na kumchoma mfano wa yule KIMBURUKUTU mwenzie SOPHIA.  Soph, alijitakia yeye mwenyewe KARIKOROGA na kulinywa kalinywa bila kupenda, Nakwambie shoga jamii kama lote inamwona Sophia kama KIDUDU MTU.

Mashoga na Maanti EMBU NGOJA NIWAAMBIENI, Sophia anaye mume, na mumewe lazima apate raha,  lazima mume apewe matunzo yote asilimia mia, lakini ubaya wake Sophia jamoni walimtibua hao mashogaze,  wasomtakia heri na fahari, wakamsonga na  kumgea ushawishi kumwambia kuwa sasa ni wakati wake, wakati wa yeye kuwa BENETI na mumewe. Wivu shosti wivu ni jipu la kutumbuka na jipu likitumbuka utamwagika usaha mwaya, vundo hilo, vumba hilo, shombo sio shombo! La kubunda limekosa ubani.


            Sophia akawasikiliza shogaze wakimwambia ati mumewe ISSA hampendi, hampi mapenzi na nafasi ya kuwa karibu karibu nayeye kwa muda na kwa wakati wa mapenzi, yote kwa sababu Issa ANAJIWEKA BIZE, iwe usiku iwe mchana yupo ‘JOB’ kazini, iwe juma mosi iwe juma pili Issa hapati nafasi ya KUPETIWA PETIWA na Sophia. Ikawa hivyo basi Shoga, Sophia kiguu na njia, anakichakaza kisigino chake hadi huko kwenye Milima na Mapori ya MASANGOMA  wajuzi na wataalamu wa miti shamaba.


            Wajuzi na wataalamu wa miti shamba hawakumwacha, walimuhudumia kwa kadri ya yeye binafsi alivyotaka, pesa sabuni ya moyo, pesa tamaa ya moyo, pesa tamu na uzuri wa pesa chema lazima kijiuze kibaya kitembeze, Sophia akaikoroga dawa na dawa ikakarogeka, ikawa tepe tepe mfano wa uji uji wa bamia na mrenda. Teeh teeh teeh (Nacheka mie🤣😅) Mpuuzi  huyu, alikwisha kusahau kuwa TAARIFA NYINGI ZINAFIRISI.


            Loe hii mumewe Sophia yupo yupo HOME LAND haendi kazini wala hataki kwenda kazini hadi pale Sophia ajapomtaka afanye kwenda. Basi shogangu nakwambieni ukitaka kwenda nyumbani kwa Sophia Usishangae nyonyo   ukimkuta Issa yule Bosi wa ofisini Leo hii anakosha vyombo anapuguta deki,  anafua nguo, anaenda sokoni kununua hiki na kile tena sio kwa mabembelezo bali ni kwa amri za mkewe. Lo! Kwa mtindo huo Issa Keisha kamuliwa kama tambala la deki. Ndio madhara ya hilo dude linalo itwa LIMBWATA.


Issa sio tena yule Issa kidume mchapakazi. Basi leo ukienda nyumbani kwa Sophia Mwaya tegemea kukutana na wanawake wawili wanaoishi nyumba moja. Na hao wanawake si wengine bali ni Issa na Sophia. Jamoni sio aibu hiyo, mmh! Nigune mie, mbona n’shapewa taarifa ati hilo limdawa la limbwata lishamwathiri Issa mumewe Mariamu naambiwa ati hicho kibamia chake Issa hakiendi walah! Hakirudi KIMEDODA, KIMEREGEA na ajabu HAKILIKI. Jamoni mwanamke mbaya Sophia. Teeh teeh teeh, atabaki na labda, kayataka yeye mwenyewe na saa Keisha yapata. Ama! alisahau yale maneno ya WATASHA waliposema “TOO MUCH IS HARMFUL.” Teeh teeh teeh 😄😃😁(nacheka mie)  ATABAKI NA LABDA.


:::::::::::::::::::::


Mwaya, nyonyo wangu naomba tuvumiliane next time tukutane hapa hapa, nikupe ubuyu uongeze tarehe za kuliona Jua. Huna baya kipenzi, uishi miaka ya Kobe, ukifa usioze maana hujarogwa my wangu.


 Nakupenda.💖💞

 

           

            

                         

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...