Saturday, July 5, 2025

DESPERATE WOMAN

 

DESPERATE WOMAN.🥹

       Mita chache kutoka pale tuliposimama Barabara kuu pembeni Kuna kichaka kilichoota nyasi zilizokauka. Tulikua tunapigisha moshi wa Dawa 🚭pamoja na kustawisha mioyo kwa Visungura na Double kiki 🍾tulimuona Demu 🚶‍♀️flani matata akija location yetu. Kwa appearance yake 
alionekana kavalia gauni 👗Moja refu lenye kitambaa laini na chepesi lililoendana na umbo lake umbo la Kuku wa kizungu 🐓 (Modo).

       Mkono wake wa mashoto alishikilia Kikoba👜 kidogo chenye rangi nyeusi, Cheni ya Dhahabu Og iling'ara shingoni kwake, vitobo pua na hereni masikioni.

 Chini miguuni alitinga kiatu 👠Cha mchuchumio ulioambatana na vikuuku miguuni. Aliendelea kujivuta kwa mwendo wa Nyau (Cat 😺 walk) kainamisha kichwa chini, 😞huzuni flani ilifunika na kugubika sura yake nzuri, muda wote alitizama aridhi, lakini Who cares!! Ni nani anajali?🤷 Kama Mie Nyanda na kaka yangu Kabundi tuko bize kusaka mali za wizi, unyang'anyi, pick pocket na magendo.

       Yule mdada mwenye Figure ya kizungu aliendelea kuja usawa wetu, Mwendo wa Nyau haukumtoka kwenye Malundi yake.🐆🐾 Uzuri mkononi aliishikilia simu ya Iphone 19📱🧐😋

        "Oyah! Kabundi zamia huko mpakani." Nilizima kipisi changu Cha Dawa nikaamuru Kaka Kabundi afichame kwenye kichaka kidogo kilichokuwepo pale tulipozamia, alitii na mie nilifuatia, tulijipanga kumfanyia 'ambush' yule mrembo.

     "Kitu hicho mwanangu mali ya Dhahabu."Kabundi alininong'oneza sikioni.👂


     "Ulaji" 😜Nilimsapoti kaka yangu. Yule Dame alijikatisha na kutuachia mgongo.Kitu pasina kuchelewa tulinyata mfano wa Chui 🦁🐆amvamiaye Umbwa koko🐕 aliyelala. Hatua ya kwanza ilikua ni kuikwatua ile l phone 19 🤳kutoka mkononi mwake. Holla! Kama upepo vile hatukupata tabu kuinyakua ile simu, tendo lile lilikua kama vile kumsukumiza mlevi adondokee kisimani. I phone 19📱 tuliiweka kibindoni.


        Alitutazama kwa jicho la upole👁️‍🗨️ na madaha, hakusema neno, hakupiga kelele🧟 za kutuitia watu nyomi. Kawaida tumepigiwa sana kelele za 'Mwizi! Mwizi ! Mwizi' pindi tufanyapo uarifu kama ule. Hatukufika mbali mbio za sakafuni uishia ukingoni tuligeuka kumtazama yule Dada. 'Duh!' Mbona hapigi kelele 🔊🫨 za kutuitia mwizi! Mimi na kakangu tulitazamana kwa mshangao, Dame aliendelea 'kumuvu on' kwa mwendo wa Nyau kama vile yupo kwenye Jukwa la maonesh ya mavazi ya Louis Vuliton.


    'Twende tena' Uporaji ulitunogea. Tukamkimbilia. Kitendo pasina kuzembea tulizinyofoa cheni zake za Dhahabu shingoni, zilikua ni Mali ya mamilioni maana ni Og, kutoka Uingereza🇬🇧 au Arabuni 🇦🇪sio kama zile feki za Manzese na Kariakoo.🇹🇿

     "Naomba mchukue pia Pesa zangu zilizo ndani ya mkoba." 💰Aliongea wakati huo sie tuloanza kumkimbia tulijiona kama tumeupiga mwingi.🤪😜😝


 "Twende tuchukue." Nilimwambia Kabundi. Tulimvua ile saa ya Dhahabu mkononi,⌚ tukauchukua mkoba wake ambao ndani kulikua na Madolari 💵💵💵💰. Aliendelea kutembea usoni akiwa mnyonge mnyong'evu na dhaifu.


       "Whuuuza! Wizi wa Leo ni Noooma" Kaka alifurahia.🤪

      "Woooooh!"🤪🤪Tulijipagaza baada ya kuiona simu 📱 Babu kubwa tena ya bei Kali, cheni za Dhahabu na Madolari bunda💸 ya kutuheshimisha mjini kwa hakika Pombe🍺 ingetukoma, vyuku🐓 vingetukoma, vyura👩‍❤️‍💋‍👩 vingenesanesa juu ya viuno vyetu, mende wangekufa miguu juu, kwetu ilikua zari.

      Macho yangu yakatua kule anakoelekea yule Mwanadada, taa 💡🔦 ya ubongo 🧠🤯wangu iliwaka ghafla, nilihisi Kuna hatari💥 anaelekea kuitafuta. 'Mbona kama anataka kuvuka Barabara wakati Magari🚘🚗🚕 ya mwendokasi yanakimbizana. Nikamwacha Kaka Kabundi anaifurahia ile pochi yenye mapesa, nikakimbilia yule mrembo kwa kasi ya ajabu.🚀 Pale Zebra cross🦓🚸 alikua anavuka🛣️ wakati Magari hayajasimama kuruhusu watembeao kwa miguu kupita.

         Nikafanya kuwai, nikaushika mkono wake kwa nguvu zangu zote kiumeni nikamsukumia kifuani kwangu, Gari lilikuja kwa kasi ya mshare🏹 tukadondokea upande wa nje ya Barabara, ilibaki kidogo litugonge na kututupilia mbali.

       "Kwanini unataka kujiua!?"⁉️ Nilimuuliza nikiwa nimemkumbata kiunoni mwake baada ya kudamka kutoka pale sakafuni.

     "Niache tafadhali," Alinijibu akijaribu kujitoa mikononi mwangu.

      "Nikuache ili ujiue" ⚰️Nilimfokea. Kaka Kabundi alitufuata pale tulipokua tunabishana.

      "Vyovyote vile, kama mnataka mali🌟🚕💒 zangu zingine twendeni nyumbani niwape, sioni faida ya kuishi, sioni faida ya hizo mali." Lugha yake ilinipa wasiwasi 

      "Mambo moto!"🔥 Kaka aliongea kwa furaha.

      "Tupeleke please!" Kaka alitabasamu hadi majino yake Therathini  mdomoni 🦷yalichomoza, tamaa iliwaka.🎆🔥 Dame akageuza kuelekea  nyumbani 🏠 kwake, tulifuata, Safari iliiva wakati Kaka akifurahia twaweza pata mali nyingi mie moyoni nilikua nawaza kuhusu yule Dame aliyejikokota akitembea kwa huzuni.😭

Tulifika nyumbani kwake, Horofa 🏘️ya pili kati ya tatu alizomiliki. Bila woga bila wasiwasi Wahuni tuliingia ndani ya Sakafuni la sebule ile nzuri ya kuvutia kama imepakwa Dhahabu, Almasi na Lulu. Majumba ulipendeza: Kuna sofa za bei gharama, kuna makabati yenye vyombo vya China, America na Jerumani. Kuna Tv screen Moja kubwa ukutani, Zuria chini lina mvuto yaani Zuria Og. Sifa zitajaa Viroba, tukomee hapo. Kabundi alitabasamu mara Moja akakimbilia kabati la vyombo vya China macho pima akilishangaa.👀

     "Tumetajirika Nyanda." 🌟🌟Furaha yake haikumiridhika. Niliisikia vibaya kwanini tumuibie Mwanamke akiwa anatukodolea macho. 'Sio poa.' 👎 Nikamchukua yule Dame nikampeleka Restroom (Toilet.)🚻 Nikamfungia mlango kwa nje Kisha nikamfuata Kaka Kabundi aliyekua akifurahia Kila kitu chenye thamani ndani ya ile nyumba utadhani ni Mali zake halali.☺️💩

     "Kabundi nikabidhi Simu ya huyu Dame"☎️ Nilimwambia Kaka.

      "Nini!? Nikupe simu iliuongee na nani? Mbona umeanza kubadilika ghafla mdogo wangu, ucheshi uliokua nao siku zote umetoweka."🙂‍↕️Kabundi alianza kuhisi mabadiliko yangu ghafla.

     "Nipe nahitaji kumpigia mtu muhimu, yamkini mume wake. Je, huoni Dame huyu anaonekana ana stress." Niliongea.

     "Nyanda una matatizo wewe, yaani tumpigie mumewe alafu kitukute kisanga.🧨🎇🔥🥵 Tupo hapa kubeba Mali sio kupigia Simu watu." Sikujali kauli zake.

      "We nipe tu." 👿 Nilimkasirikia. Aliitoa na kunikabidhi ile Simu akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wake na wangu."

Niliwasha ile Simu, nikaingia missed call📞 Kisha nikasechi nambari ambayo nilihisi yule Dame anawasiliana nayo sana, sikukosea niliiona Moja imeandikwa 'Habibu wangu." Nambari hiyo alioneka ameitumia sana kuwasiliana. Nikafikiria huyu atakua ndio mumewe basi nianze na yeye.

     'Driiip.....driiiip....driiiii' 📳Simu iliita. Muda si mrefu yule aliyeitwa 'Habibu wangu' akaipokea. Kabla sijajitambulisha na kuongea neno Habibu alianza kufoka, bahati nzuri niliweka loud 🔊 speaker kaka Kabundi aliyasikia maongezi yale.


      "SAMOA, UNAMATATIZO GANI WEWE MWANAMKE MPUMBAVU? 👿 NIMEKWAMBIA SIKUTAKI, SIKUPENDI, WALA SINA HAJA NAWE. MWANAMKE MNUKA KWAPA WEWE, MIE N'SHA MPATA💘 BIBI WA KITANGA ANANIPA HUBA💕 NA VITAMU VYENYE MAFUTA NA SUKARI YA TENDE NA ARUA. KUANZIA LEO STOP 🚫KUNIPIGIA SIMU. NAWEZA KUKUUA AU KUKUFANYIA KITU KIBAYA MAISHANI MWAKO, KENGE WEWE .MXIIIUUU🥴😠😵‍💫." Habibu alikata simu mimi na Kaka tulitazamana kwa mshangao uliojaa viulizo tele. ‼️‼️

      Tukiwa tungali twashangaa Ghafla mlango wa Sebuleni ulifunguka. Tulitetemeka kidogo tukijihoji wapi tufichame, aibu yaweza kutuzika ndani ya nyumba ya watu tusowajua. Lakini tulikuja kupoozeka tulipomwona mtoto👼 mwenye kadirio la miaka mitatu alkiingia pale sebuleni. Mtoto hakuonesha darili za kutuogopa alitusalimia kwa adabu na heshima Kisha akatuuliza sie ni wakina nani?

      "Sisi..... Mmmmh ......mmmh!"😎😶‍🌫️ Tulijing'ata ulimi tusijue tumweleze Nini mvulana yule  mwenye  tabia nzuri.

      "Sisi ni marafiki 💑🤞wa Mama yako" Kabundi alimjibu yule mtoto.

     "Mama yupo wapi!? ⁉️Au yupo chumbani kumeza dawa zake." 💊💉 Alitushitua zaidi tusijue Mama yake anameza dawa gani na kwanini anameza dawa!?"  Mimi na Kaka tukatazamana.👁️👁️‍🗨️

    "Hapana Dear ☺️....... Rafiki tunaweza kwenda Jikoni tuandae chai na mayai mchemsho?" 🍵🥚 Kaka alihitaji kufanya jambo la ziada.

    "Ndio tunaweza." ☑️Mtoto yule mwerevu alielekea Jikoni kuandaa chai na mayai pamoja na kaka Kabundi. Chale zilianza kunicheza 'Yamkini huyu Dame atakua yupo hatarini,⚠️ embu ngoja nimfate huko aliko chooni.  Nikaelekea Maliwato nikaufungua mlango wa chooni 🚽na kujitoma ndani.

 'Makubwa!' ⁉️😥

Nilimkuta yule Dame ameketi chini ya sakafu yenye marumaru pale chooni, chozi 😢 lambubujika, ameshikilia kikopo cha rangi nyeupe ndani Kuna Dawa 💊💊tayari kakifungua na kuujaza mkono wake kwa Dawa lukuki, bado kidogo kumeza. Nilimkimbilia na kumpokonya vile vidonge vingi mkononi mwake Kisha nilimkemea.😡😧

    "Unataka kujiua? Kwanini unataka kujiua?"😡

     "Niache Bwana, niache nimeumizwa sana, nimechoka kuishi Bora kujiua. 😿 aliongea akilia kwa uchungu.

     "Hapana Daring 💕kujiua sio suluhu ya matatizo yanayokuandama." Niliongea kwa upole.

     "Suluhu ni nini baada ya kuumizwa na mwanaume niliyempenda hatimaye kunibwaga!?" Nikamwambia 'Calm down baby' nitakusaidia. Kisha nikaendelea kunena.🗣️

      "Kumbuka Bado unae mtoto mdogo anayehitaji mapenzi 👩‍❤️‍💋‍👨ya Baba na Mama Sasa wewe hujui ni nani  atakayeonesha upendo kwa mwanao, ikiwa Baba yake mwenyewe haeleweki,  nani atamuelewa mwanao? Aliinua macho yake kisha akanitazama kwa uchungu mkuu, akaanza kulia kilio cha Kwi Kwi Kwi uwiiii! 😿😭Hisia za uchungu zilimpanda.

      "Hivi Samoe unajua ni kwanini mimi Nyanda na kaka yangu  Kabundi tunavamia watu mitaani tukiwapora na kuibia Mali zao. Unafikiri twalipenda jambo hili?⁉️ Hapana, tunasababu zetu na sababu zetu zinatuumiza. Nikaanza kumwadithia kwa ufupi Story yetu sie wenye dhiki.💩

       "Mama yetu alipokua hai tuliishi kama Malaika ndani ya Bustani ya Edeni.🏡 Kila hitaji letu nyumbani tulilipata: Kila hitaji letu muhimu na liso muhimu tulilipata : chakula, 🍔🥙manywaji,🍷🍶🥂 malazi,💤🛌 pesa, 🏧💰amani, upendo na furaha. 

Ghafra Mama yetu alipata homa kali, Mola akamchukua mambo yote mazuri tuliyoyapata pale nyumbani yalibadilika na kuwa ovyo.🤬 Baba alianza kuondoka Alfajiri na kurejea usiku wa manane akiwa Bwiii! Kalewa chakali, 🍻hapo haulizi Wala hajui, tumekula Nini!? Tumevaa  ninii? Je, twahudhuria masomo shuleni!? Tumepata ule upendo, amani na furaha⁉️ Hakua  na muda huo Baba yetu. Kwa ufupi Baba yetu alituacha njia panda, hakuna jipya tulilolifurahia mbele zake.

Kwa sababu tuliachwa ilitubidi tuanze kuhaso tungali makinda ya Darasa la tatu na nne. Kuiba ikawa ni kazi yetu, kutekanyara, kupora na kuvamia likua kawaida kwetu. Huwezi kuamini hadi ukubwani tumeikomalia hii shuhuli hatarishi inayotutia wasiwasi juu ya kesho yetu. Kwahiyo Daring mimi nipo tayari kukusaidia.💕

     Nilimfuta chozi na kumpokonya vile vidonge alivyoshika mkononi, Kisha nikavitupa ndani ya sinki la kunawia mikono. Vidonge vile sometime vilikua vinampunguzia strees, masikitiko na mawazo juu ya Habibu mumewe.
    
     "Have peace Samoa." Nilimpooza  nikajitambulisha tena kwake: 'Niite Nyanda' akachangamka kidogo🌞☺️'Mimi Samoa' Samoa alijitambulisha pia, moyoni nilihisi ushindi utapatikana tu hata kwa ncha ya Upanga.🗡️🔪

******:::::::::::::*******

     Basi kuanzia siku ile mimi Kabundi na kaka yangu Nyanda tulianza kumjenga kisaikolojia  Samoa na uzuri wa sie 'Shameless men' tukafanya kuhamia nyumbani kwa Samoa. Tulifanya kila tendo na kila neno la kumrudisha Samoa katika ubora aliokua nao zamani.

     Tiki ikatiki🫰✔️ kwa ubora wa mashauri yetu Samoa alianza kupona kisaikolojia. Mimi nae nikaona hapo Sasa ni nafasi ya kujiongeza. Nikajenga ukaribu  na Samoa akanipokea na kuniweka moyoni mwake, penzi likazaliwa likapendeza na kumea kama Maua  bustanini🌺🌹💐. Samoa akawa ni mtu wa furaha, Raha na amani tele. Hakuwa na muda wa kumuwaza tena Ex- Husband  wake Habibu bali aliniwaza mie Nyanda.


    Uzuri kumbe Samoa alikua anamiliki  Kampuni ndogo,  hilo likaleta 'Blessing' zingine kwetu. Kaka Kabundi akapewa Umeneja wa Kampuni ya Samoa mie nikapewa cheo cha juu  ndani ya Kampuni, 'General Director.' Aki! Maisha yakaanza kutunyokea  from Zero to Hero, Waooo! Leo hatuwapoli tena Raia, hatuwanyag'anyi  au kuwaibia Bali twaendesha Magari ya fahari, utajiri na pesa 💰💰🏧 zimetutembelea hadi zinatuogopa.


     Huu ni mwaka wa tatu tangu mie na sweet Love 😘 wangu Samoa tuingie penzini🔥 miezi miwili ijayo anatarajia kuingia Leba, Mtoto 🤱 tunaye na kutamba tunatamba naye👌💕😹. Nashukuru Mola Samoa alikua anataka amani, upendo, furaha na Raha vyote hivyo sasa amevipata na pia vimerejea baada ya kuvipoteza akiwa Desperate Woman  (Mwanamke Aliyekata tamaa.)



"************
TCHAO 

 💖 LOVE  MUST LEADY

"************
 





Wednesday, July 2, 2025

I PROMISE YOU

 


Tendo  la mie kujiuzuru kunywa matapu tapu likawa  pia ni mwisho wa Brenda kunywa . Maji ufuata mkondo, Brenda alinifuata aliungana nami ili kumpiga vita adui pombe. Nakumbuka vizuri, naikumbuka tarehe 25 mwezi wa pili mwaka 2016  ni tarehe iliyonifanya nichukue uamuzi mgumu wa kwenda nje ya mkoa wetu Iringa, nikaelekea ndani ya jiji la Dare s saalam.


Lengo likiwa kutafuta shughuli yoyote ile ya kunitotongotongo. Sio tu kunitoa kimaisha pia kunitimizia malengo yangu mengine kama vile kumtimizia Brenda furaha ya mtima wake. Si anataka nimuoe? Yes, anataka nimuoe lakini siwezi kumuoa pasina kufuata mila na desturi za kiafrika, ni lazima nimtolee mahari, sherehe kubwa ya kupendeza na baada ya hapo nimuweke ndani ili awe wangu, wangu wa milele.

             Sikupenda kuwa mbali na walezi wangu, babu na bibi, sikupenda kuwa mbali na macho ya Brenda, ilinibidi nikubali kuwa napaswa kuondoka, napaswa kwenda mbali na mji wa Iringa, nikatafute riziki na iwapo nitafanikiwa napaswa kurejea nyumbani haraka iwezekanavyo, haraka  mara baada ya kufanikiwa nikijua fika kuwa mwenda kwao si mtoro, mjasiri aiwachi asili.
Basi mpenzi wangu Brenda akaniandalia kila kitu kwaajiri ya safari yangu na uzuri wake nauri ya kwenda jijini Brenda alinitafutia. Babu na bibi walinitafutia  pesa ya makuli na malazi mara nifikapo jijini. Sikua na jinsi ilinibidi niondoke niende ndani ya jiji nililo amini kuwa nitapata kazi. Penye wengi pana mengi, nilijiamini na pia niliamini kwa kudra za Mwenyezi Mungu kazi nitapata, kazi ya kunitoa kimaisha. Japo mie ni mvivu wa kufanya kazi sina udhoefu wa kufanya kazi yoyote ile, nilikuwa ni mzoefu wa kunywa pombe. Pombe pekee ilikuwa fani yangu sikuwa na kazi nyingine niliyoipenda kama kunywa matapu tapu.

                 Looh! Ndugu zangu pombe iliniharibu, kimwili na kisaikolojia, sikuhitaji kufanya kazi yoyote ile, nilikuwa mzoefu wa pombe na kunywa pombe ilikuwa ni kazi yangu, sikuwa na kazi yoyote ile ya kuniwezesha kimaisha, kilimo kilikua ni cha babu na bibi, walilima walipanda walivuna waliuza na kunipatia pesa ambazo kila siku ziliishia kwenye bunge la walevi, nami nikachangia pesa ya pombe, kila siku ili nipate kiburudisho cha mdomo wangu.
        *******************************
              Saa nane mchana niliingia ndani ya jiji la Dare s saalam, sikuelewa nitaanzia wapi kwenda au nitafikia kwa nani? Nimeondoka kijijini na kuja mjini ati kutafuta maisha, hivi mimi ni mpuuzi wa maisha ya aina gani? Nilijiuliza mara baada ya  kutoka Ubungo Bus terminal. kituo kikuu cha mabasi yaendayo na pia yatokayo mikoani.

             “Hivi nimefanya uamuzi gani mimi?” nilijiuliza tena safari hii moyo ulianza kunilaumu kwa uamuzi wangu wa kutoka kijijini kuja mjini kutafuta maisha, kwenye mji wa watu nisio wajua, sina undugu nao, sina ujamaa nao wala sina mahusiano nao.

              “kwanini nimeondoka kijijini, sehemu ambayo kuna kila kitu ninachohitaji haraka ningelipata, chakula cha kutosha, maji, matunda ya kutosha, pahali pazuri pa kulaza kichwa changu, marafiki wenye heshima zao, ndugu jamaa na majirani, mimea wadudu na wanyama. Mmmh!” Niliguna mimi na moyo wangu bado mawazo yalilindimaa.

“Nina  nini mimi?je hakuna kazi yoyote ile ya kuniwezesha nitoke vema kimaisha nikiwa kijijini? Mbona wapo wasusi wanasuka mikeka , makapu, kofia na nyungo? Mbona wapo wafinyanzi? Wasanii wa vikundi mbali mbali vya ngoma wanatumbuiza na kuvuna fedha zao? Wawindaji hawakosi nyama, matunda, mayai na asali ya kuleta nyumbani. Wakulima ni wengi wenye faida, wanailisha dunia  matunda ya aina mbali mbali; mafenesi machungwa mapeasi, mabohora, matango, matikiti maji mapera ndizi na mananasi. Kilimo cha mahindi, viazi mtama, uwele, ulezi, mpunga, maharagwe, kunde na mbaazi.” Vyote hivyo mie goi goi nilikuwa msindikizaji tu, nikiwasindikiza wakulima wajibidishe katika shughuli za kilimo japo mie mzembe na mvivu kazi yangu kula, kunywa na kulala.

                 “Je kijijini hakuna ulinzi? Nilishindwa kujiunga na jeshi la wana mgambo? Je kijijini hakuna biashara? Mbona zipo nyingi zile za masokoni, zile za madukani, zile za kuingiza na kutoa mali ndani na nje ya kijiji. Kuna uvuvi, kuna ufundi uwashi, kuna mengi ya kujivunia, nimeshindwaje kujibidisha katika hayo, nimefanya maamuzi ya kuushangaza mtima wangu, maamuzi ya kuondoka  kijijini na kuja mjini kutafuta maisha. Nimekuja kutafuta maisha gani ikiwa ningali ninajua kuwa hata kijijini maisha ambayo nimekuja kuyatafuta mjini yapo. Tena yapo fresh tu.” Niliwaza sana siku ile.
                 ‘Piiiiiiiiiiii…..Pooooooo………Piiiiiiiii!’ ilikua ni sauti ya gari, Mitisubish pajero kama sikosei, ilifunga breki karibu karibu na miguu yangu, wakati huo huo mshamba mie  nilikua najiandaa kuvuka barabara kuu ya lile eneo la ubungo.

               “Yallah! Toba! Nimepona mie.” Niliongea mie na mtima wangu mara baada ya kuiona ile gari ikiwa imesimama pembeni ya miguu yangu dereva aliyekuwa ndani ya ile gari alinitizama kwa chuki na kwa hasira. Aliugundua uzembe wangu uzembe barabarani, nilivuka barabara pasina kuzingatia sheria za brabarani, nilivuka tu kama mwendawazimu, nilivuka pasina kujielewa elewa, nilivuka pasina kutazama wapi  utokao wa yale magari na wapi uendao wa yale magari pamoja na motokaa zilizoongozana kama farasi.

                “Una nini wewe kijana?” Mwanaume mtu mzima aliyeonekana kushiba vya kutosha, alichomoka ndani ya gari yake mara baada ya kuiegesha ile pajero  pembeni ya barabara. Ana nywele nadhifu nyeusi  zilizonawili amevalia shati ya blue tai nyeusi na koti moja yenye rangi nyeusi,, ni mnene kiasi,  katupia miwani machoni.
                Ukimtazama mara mbili mbili waweza sema moyoni mwako mwanaume yule ni mwenye pesa zake anajiweza kiuchumi, ni kibosile fulani ndani na nje ya serikali kama sio kibosile basi ni kigogo fulani hivi ndani ya nchi. Any way hisia hazijengi sikuhitaji kuziruhusu hisia za moyo wangu kutawala fikra na mawazo yaliyojaa moyoni mwangu kama ni kupona nimepona, nisije nikapoteza miguu na viungo vyangu vingine nikiwa ugenini, nipo salama salimini, kwanini nisimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniepusha na majanga yale.

Aki! mbona ningeteseka ugenini kama ningelipoteza miguu yangu au kama nigelipoteza jicho langu la kushoto, wakati huo huo nimekwisha poteza jicho la upande wa kuume mmh! Nilipoteze na hili lililobaki kwa bahati nasibu? Mmmh! Janaba,mmmh!  Huruma jamani.

                “Samahani Bwana mkubwa nina upofu jicho langu la kulia hili lililosalia halioni vema, ndio maana nimevuka pasina kuwa mwangalifu.” Nilijitetea ili kupunguza hasira za yule Bwana mkubwa macho ya wengi yalinitazama , macho ya wengi yalitamani kujua mwisho wa ile sinema yetu.

                “Aaahh! Kumbe una upofu wa macho, ooh! Pole sana kijana.”  Yule kibosile alinipatia mkono  wa faraja mara baada ya kumueleza matatizo yangu.

              “Pole sana kijana wangu, embu nieleze ni wapi unaelekea ndani ya jiji ?” Bwana mkubwa aliniuliza.

              “Sina pahali pa kwenda bwana mkubwa, mimi ni mgeni ndani ya jiji, nimetokea Iringa kijijini nimekuja jijini japo kubahatisha  labda nitapata kazi itakayo niwezesha na  itakayonibadirisha kimaisha.” Niliongea kwa kirefu, nilitia huruma kama kondoo mwenye kuhitaji maji na chakula,  nikiwa nimeshikilia kibegi changuo chenye nguo mbili tatu pamoja na fedha za kujikimu.
                

“Oooh! Pole sana mdogo wangu, embu tuokoe muda kidogo, ingia ndani ya Gari yangu tutoke eneo hili, niko bize kidogo ninaelekea Kariakoo kwenye mishe mishe zangu? Yule bosi aliongea.

Je, niingie au nisiingie ndani ya ile Gari ya huyu kibosile? Nilijiuliza. Swali lililonijia ghafla ndani ya kichwa changu.

Wacha niingie tu, yawezekana ikawa ni zari la mentari. Nilijisemea mimi na moyo wangu kisha nikaingia ndani ya gari ya yule Bwana mkubwa. Nilipotaka kuketi nyuma ya siti ya ile gari Bwana mkubwa alinikataza nisikae nyuma akaniruhusu nikae mbele ya Gari.

               Harufu nzuri ya marashi pamoja na manukato yalipamba pua zangu, nilijisikia aibu  kidogo sababu mnuko wa mavazi yangu niliyotoka nayo kijijini uliingia ndani ya ile Gari na kutibua hali ya hewa, japo yule bwana mkubwa hakujali  kuhusu hali yangu ya kutibua hewa alikwisha kufungua vioo vyote vya ile Gari ili hewa nzuri ipite na kuingia au kutoka ndani na nje ya ile Gari na uzuri wake yule Bosi aliwasha kiyoyozi (AC) kilichofungwa ndani ya Gari yake kikatuperuzi peruzi kwa ubaridi wake na kutumiminia hewa safi ya kupendeza.

                “Niite Bwana Steven Biko, ni meneja wa kiwanda cha kutengeneza, kusambaza na kuuza bia ndani na nje ya Tanzania.” Yule Bwana alijitambulisha kwangu.

               “Je wewe ni nani mwenzangu? Ningependa kukujua zaidi.” Aliongea yule bosi akiendelea kuiendesha Gari yake, wakati huo huo nilijua kuwa tunaelekea kariakoo, kama alivyonieleza.”

                “Asante sana kwa utambulisho wako Bwana mkubwa.” Nilimshukuru yule bosi nikimtizama kwa kutumia kile kijicho changu kimoja kilicho hai, ukitegemea jicho langu moja lilikwisha kupoteza uzuri wa kutazama.     

              “Mie naitwa  Bwana Job Mkwawa, ni mzaliwa wa Iringa kijijini, kabila langu mhehe umri wangu miaka ishirini na mitano, sina mwenyeji hapa mjini, kama nilivyokueleza , nimekuja mjini kutafuta maisha nitafurahi kama nitafanikiwa kupata nafasi ya kazi, sijali ni aina gani ya kazi, yoyote ile nipotayari kuifanya Bwana wangu niliongea kwa matumaini ya kusaidiwa,

               “Ah! Kumbe Bwana Job wewe ni mwenyeji wa Iringa?” yule bosi aliyejitambulisha kwa jina la Steven Biko aliniuliza akiwa na kiasi kikubwa cha tabasamu mdomoni mwake.

                   “Ndio Bwana  Steven Biko .” nilimjibu yule bosi, wakati huo huo jicho langu moja linalofanya kazi lilikua likishangaa shangaa umati mkubwa wa watu waliokuwa bize wakielekea kwenye miangaiko yao.


                    “Waooo! Kumbe nimekutana na mtani wangu, mimi ni Mnyakyusa nyumbani kwetu Tukuyu Mbeya, nilizaliwa huko nikapewa elimu yangu na baada ya kumaliza chuo nilipata ajira ndani ya kampuni ya Bia.” Steven Biko aliongea, mie nikajawa na furaha mara baada ya kugundua kumbe nina mwenyeji wangu amabaye ni mtani wangu na uzuri wa yule mtani anatokea mkoa ulio karibu karibu na nyumbani Iringa.

Gari iliendelea kuchanja mbuga mie mshamba na mgeni ndani ya Jiji hili nilikuwa mtazamaji, nikitizama uzuri na urembo wa lile Jiji, lililopangiliwa na kupangika kwa wingi wa mahorofa, balabala zenye ubora na uzuri wake, wafanyabiashara ni wengi pomoni kila mtu yuko bize na shughuli zake, shughuli  za kujitafutia riziki na bahati ya kila siku.

                 “Tupo wapi hapa mtani wangu?” nilimuuliza Biko mtani wangu.

“Hapa ni katikati ya jiji panaitwa Kariakoo, mbele kidogo njia ilee (akainyoshea mkono) ni barlabala ya kwenda Posta. Posta ni sehemu wanayoishi watu wenye fedha zao, wazito wa ndani na nje ya nchi, kule kuna maofisi ya viongozi wa serikali mabalozi wa mataifa mbali mbali wapo kule, kule ni paradise ndogo yenye kuvutia.”

               “Kumbe Jiji hili ni lenye fahari kubwa sana?”

                “Yes, huu mji ni johari ya watalii na wgeni wengine wengi, wanaokuja kwa ajiri ya shughuli zao za kila siku.”

                “Dah! Nitafurahia sana iwapo siku moja nikipata nafasi ya kulizunguka jiji.” Niliongea kama vile tayari nimekwisha kulizoea hilo jiji.

                 “Ondoa hofu mtani wangu, ipo siku nitakupeleka baharini ukazione meli, si unazijua meli au unazisikia tu?”
                 “Nazisikia tu wala sijapata kuziona.”

                  “Hilo sio tatizo kikubwa ni kumwomba Mwenyezi Mungu uhai na uzima ili siku moja tupate kwenda kufurahia raha za jiji.” Biko aliongea.

                 “Pesa pekee ndiyo inayoongea kijana wangu, hili ni Jiji la raha na starehe. Raha na starehe pasina pesa ni kazi bure.” Biko aliongea kama vile mie na yeye tumejuana muda mrefu sasa kumbe tumefahamiana dakika chache zilizopita, tena kufahamiana kwetu ni kwa bahati tu.”

               “Shukrani mtani wangu, siku nitakayotembezwa ndani ya Jiji itakuwa ni siku ya furaha kubwa kwangu,” niliongea kwa furaha.

                “Bwana Job nina swali nahitaji kukuuliza” Biko alinishitua kidogo, nikamuitikia kwa kutingisha kichwa kumuashiria kuwa ruhusa ya kuuliza imekubaliwa.

                “Vipi kuhusu elimu yako, umesoma hadi kufika levo gani?”wakati huu Gari ya bwana Biko ilikua ikingia ndani ya kiwanda cha BIA, nilikitambua kiwanda kile kuwa ni cha BIA kwa sababu kilikua na bango lililoandikwa Tanzania Brew company limited (TBL)

                “Kidato cha nne ndio kiwango changu cha elimu,” Niliongea

                 “Oooh! Safi sana, kijana unaonekana unanguvu za kutosha kufanya kazi, kwa juhudi kwa maarifa na kwa ufanisi mkubwa pamoja na moyo wa kujituma.” Biko aliongea maneno ya kutia matumaini nami nikakoleza chumvi.

                “Yes l can do so soninaweza.” Nilimjibu kwa kimombo kilichochanganyikana na Kiswahili. Bosi aliipaki Gari yake karibu na Ua kubwa lililiopo ndani ya kiwanda kile.
                “Safi……Good.”  Biko aliongea , tukatelemka kwenye Gari yake, nikamfuata kule anakoelekea, nikiwa nyuma nyuma kama umbwa amfuataye Bwana wake, mikononi nalikua nimekumbatia  Begi langu kuukuu lenye nguo kuukuu.

                 “Wacha nikwambie kwa kifupi bwana Job, wewe una bahati kubwa sana kuonana na pia kujuana na mimi, kampuni imepungukiwa wafanyakazi, kwa hiyo tunahitaji wafanyakazi wa kutosha, jihesabie kuwa ni mtu mwenye bahati, kazi tayari ipo mikononi mwako, wewe utakuwa ni miongoni mwa wafanya kazi wa kampuni yetu. Usijiulize moyoni kwanini nimekupatia nafasi hii ni kwa sababu ninajua kuwa wewe unahitaji kazi na kazi tayari umekwishaipata.

                “Waoooo! Moyo wangu uliliripuka kwa shangwe japokuwa bado sikujua ni nafasi gani ya kazi ambayo napaswa kuishughulikia hilo halikunitia wasiwasi nilihitaji kuwa na subira subira yavuta heri, nitaambiwa hapo baadaye ninapaswa kufanya nini?

               “Bwana Job nitakupatia nafasi ya kuingia kwenye utengenezaji wa kilevi hiki kinachopendwa na  watu wengi ndani na nje ya Afrika mashariki. Kwanza kabisa utafundwa namna ya kutengeneza Bia na baada ya  sisi kuridhia uelewa wako katika utengenezaji wa Bia ndipo utaingia jikoni kuuchochea moto ili tengenezo lako likamilike na uzuri wa kazi yako  hautakuwa pekee utaambatana na wenzi  wako wengi  mtagawana majukumu mbali mbali ya jikoni.” Aliongea Steven Biko ameniacha mdomo wazi nisitake kuamini bahati kubwa kama hii , yaani leo hii hii ninaingia ndani ya Jiji  ninabahatika kupata nafasi ya kazi hata kabla ya kutanga tanga na njia.

              Bwana Steven biko aliniingiza ndani ya  Ofisi yake, Ofisi moja nzuri ya kitalii, ofisi ile ina mvuto, sio wa kuhadithia kwa maneno matupu yatokayo mdomoni mwa watu, bali ni kwa matendo thabiti kwamba imeboreka na kuboreshwa. Imepambwa kwa tunu na medali mbali mbali ambazo kampuni hiyo ilizitwaa baada ya ushindi mnono uliotokana na ushindani wa makampuni.
      
        “Nitakupeleka kinyerezi, nje kidogo ya mji wa tabata ninamiliki nyumba yangu moja huko, ipo ipo tu hakuna mkaaji wewe ndiye utakaye kuwa mkaaji hapo,” Biko aliongea moyo wangu ulifulumia kwa furaha na shangwe isiyo na kifani. Kitendo cha Biko kuniamini namna ile kilinishangaza,  bado ni mgeni kwenye macho yake hanijui wala simjui vizuri. Jambo hili ni lenye heri na fanaka ni Baraka tele  kwangu, nikajiona na kujisikia kuwa ninapendwa pendo ndani ya pendo.

  Muda si mrefu alikuja binti mmoja mrefu mwembamba, ana macho  yenye mboni za paka, ngozi yake ya kiaribino nywele zake zina rangi ya kaki, haijakolea sana. Biko alinitambulisha kwangu kuwa huyo ni Secretary wake. Jinale Riziki. Riziki akatuburudisha kwa kutuandalia vinywaji  soft, matunda na  vitafuno vya kuburudisha midomo yetu. Sikupenda mtoto riziki apite zake na kuondoka kabla sijajitambulisha.

 nikajitambulisha kwake  Riziki alifurahishwa na uwepo wangu akanikaribisha kwa moyo wote mimi kama mfanyakazi wa pale.

                  Hatukukaa sana pale kiwandani Steven biko alihitji nikapumzike kwenye nyumba aliyo niandalia, nilikuwa na shauku ya kutaka kuiona hiyo nyumba aliyonieleza Steve.
                     ################################
                  Looh! Kumbe Dar es salaam ni Jiji zuri machoni kwa wengi wanao ingia na kutoka, kweli macho hayana pazia mtu usikubali kuambiwa  njoo ujionee wewe mwenyewe.  Juma mosi ya leo Bosi wangu alimuomba Secretary wake Riziki anitoe out. Nikaangaze angaze macho yangu huku na huko, nikapoteze ushamba wangu wa kihehe, nikafurahie mandhari ya waswahili,  wapemba, wazaramo na waruguru. Nikajionee fukwe za bahari ya Hindi, majumba ya kisanaa pamoja na mitaa mbali mbali iliyopo ndani ya jiji lililobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa na kila kizuri majaliwa. Kwa kifupi Dar es salaam ni mbingu moja nzuri yenye paradise ndani ya dunia.

              Kizuri, hakikosi kasoro, jiji la Dare s saalam sawa ni Jiji zuri linalopendeza machoni, lakini pia hata hivyo Jiji lina mapungufu yake kwa mfano mitaa ya kariakoo kama vile Faya, Big bone, na Mnazi mmoja Sekondary ni maeneo yaliyo jaa vibaka, mateja na wahuni wengine wengi. Mitaa ya Buguruni haswa  haswa Buguruni sokoni uchafu umerindimaa ni rahisi sana kwa magonjwa kupenya.
Nenda kigogo  ya mburahati, nenda jangwani, maisha ya watu wa huko ni ya chini sana umasikini uliopo maeneo hayo ni umasikini wa kuogopesha ni kama vile hawana serikali waungwana hawa ni kama vile Serikali haiwasaidii waja wa Mwenyezi Mungu, majanga mbali mbali kama vile magonjwa ya milipuko (kipindu pindu) na mafuliko ni moja ya taabu zinazo watesa waja hawa.
Kwa kifupi mtoto Riziki alinionesha uzuri na ubaya wa Jiji lenye mamilioni ya watu, jiji lenye maelfu ya Magari majumba ya fahari na biashara za kila aina. Binafsi nilihisi kukaribishwa, binafsi nilijiona nipo nyumbani, ukarimu na mapenzi niliyopewa ulinihamasisha na kunitia moyo wa kutafuta yale maendeleo ambayo ndiyo nimekuja kuyatafuta ndani ya jiji la Bongo land.

Hazikupita siku nyingi nilianza kazi ndani ya  kile kiwanda cha BIA, nilifunzwa  nini ninachopaswa kufanya mimi kama mimi ndani   ya ilekampuni, nilifunzwa nikafunzika, upishi wa pombe  ndio ulikuwa wajibu wangu niliwajibika ipasavyo. Nikikumbuka kuwa hapo awali kabla ya kuja ndani ya jiji nilikuwa mlevi wa kutupwa mlevi mwenye cheo ndani ya Bunge la walevi, Spika wa Bunge la walevi. ajabu iliyoje mara baada ya kulihama Bunge la walevi cheo changu kimeshuka kwa asilimia 95 kutoka kwenye uspika wa Bunge la walevi hadi kuwa mpishi wa pombe ya walevi mmmh! Mengine makubwa, madogo yana nafsi zake, sio mbaya yajayo yanafurahisha.

                    Any way nisiache mbachao kwa msala upitao, mcheza kwao utunzwa, mjasiri  aiwachi asili, kila ndege ana kwao kuzuri kwenye matunzo, na mimi ninaye mama, mama yangu  hakukwama kunilea na mama yangu si mwingine zaidi ya Bibi mlezi wangu, yule aliyenipatia deko na madekezo. Na mimi ninaye Baba na Baba yangu si mwingine ni yule yule Babu yangu aliyenilea nami nikaleleka kwa deko na madekezo. Upendeleo wao ni upendeleo mkuu, malezi yao ni malezi ya kuku na yai, hawakunipiga, hawakunifokea, hawakunikemea na kunikwaza kwa jambo lolote lile.
                ##########################
Miezi sita ndani ya kile kiwanda cha bia, nilibadilika sana, tabia ni mazoea, mjasiri aiwachi asili. Ule ulevi wangu wa kutupa ulinivamia tena ulinivamia kwa kasi ya ajabu, muda mwingi niliutumia kunywa pombe na uzuri wa hiyo pombe naliipishi mie mwenyewe, nilikua huru kunywa pombe mara baada ya kumaliza kazi yangu ya upishi. ‘Mie ndie mpishi, muda mwingi nipo mekoni, wacha niitumie hiyo fursa kuuburudisha mtima wangu kwa pombe,’ Naliwaza.

                Ndio maana kusema mazoea yana tabu,mtu kuzoea kitu, Aki! kukiwacha ni vigumu ajabu, muda wote uwaza jinsi gani lile pendo alilolipenda liingie moyoni mwake tena. Bosi wangu, Bwana Steven Biko hakuwa na longolongo juu ya ulevi wangu, aliniachia uhuru wa kuamua nilitawale Jiko nililo achiwa ili nipike na kupakua.
Mshahara wangu, marupu rupu pamoja na posho za mara kwa mara, bosi wangu Steven Biko alinipatia tena alinizidishia mara mbili zaidi, akinitaka niendelee kuchapa kazi pasina longolongo, pasina matata uvivu na uzembe, nilikua mtiifu kwenye ile mishe(kazi) nilikuwa siriasi japo ulevi kwangu ilikuwa ni vigumu kuukataa.

Itaendelea



OMBI LA KIJINGA

 



OMBI LA KIJINGA

Sehemu ya tatu

Tabia ni mazoea na mazoea yana tabu. Ikawa kila mara H  apness akiukamata ujauzito kwa maombi ya mumewe aliutoa bila kukawiza.  Furaha alimshawishi Happy wale kwanza ujana (wafanye anasa na starehe) kabla uzee haujawakamata. Ilipita miaka mingi miaka kumi na mitano ya ndoa yao pasina kuwa na mtoto na katika kipindi hiki bwana            Furaha alianza kulikumbuka shuka kumbe tayari kumepambazuka.

                     “My love  unajua kwa sasa tumeanza kuzeeka tayari tumekwisha kula ujana na raha zote za dunia, raha za mali na utajiri wetu sisi wenyewe, tumefurahi vya kutosha na kuburudika.” Tajiri Furaha aliongea na mkewe.

                     “Tungali tumebakiza kitu kimoja muhimu kuwa nacho maishani.” Tajiri aliongea tena.

                     “Kitu gani hicho mume wangu?”

                     “Mke wangu tunahitaji mtoto, mtoto wa kurithi mali zetu hizi nyingi pomoni mara baada ya sisi kutoweka duniani.”

                      “Mtoto? Mmmh! Hivi mume wangu una matatizo gani wewe? Yaani baada ya miaka kumi na mitano ya ndoa yetu leo hii una uona umuhimu wa mtoto, wakati unajua fika ulikua king’ang’anizi ukinitaka nitoe kila ujauzito. Nilioupata..”

                    “Sikiliza mke wangu, awali mie nilitaka tuponde raha na furaha, sikuwa tayari kuona tunae mtoto, tizama sasa raha na furaha tayari tumekwisha zipata haja yangu kwa sasa ni  kupata mtoto wakurithi mali na utajiri wetu.”

                   “Ok mpenzi, ni vizuri kama upo tayari kwa hilo.” Happy alikubali na kushukuru kwa hilo, sijui kwanini  Happy  alikuwa duni  kiasi kile, kila neno analoambiwa na mumewe hapingani nalo, anakubali, anaunga mkono bila pingamizi lolote.

Wawili wale walianza harakati za kusaka mtoto, hata hivyo kadri siku zilivyozidi kuyoyoma, Happness hakuonesha darili za kushika ujauzito, jambo lililowafanya wawili hawa wafanye maamuzi ya kwenda Hosptali kumwona Dakta. Ili wapate kujua ni nani kati yao anayeshindwa kumleta mtoto duniani. Walipofika Hospitali  majibu ya Vipimo yalionesha kwamba tatizo lipo kwa Happness kizazi chake kilionekana kuwa kimehama tena kimeshuka, mji wa mimba umeharibika kutokana na kile kitendo cha yeye kutoa mimba nyingi mara kwa mara, pasina huruma pasina kujari kuwa kufanya hivyo kuna hatarisha maisha yake.

                   “Madakta walihitimisha kwa kumwambiaHappy asingeliweza kupata mtoto  maishani mwake. Looh! Happness alilia kwa uchungu, majuto ni mjukuu, alilia na kuumia. Mwe! Maskini! Wahenga walisema fikiri kabla ya kutenda, tazama Happy na mumewe Furaha hawakufikiri mara mbili mbili juu ya kitendo kile kiovu, juu ya zambi waliyokuwa radhi kuitenda mara kwa mara.

                 Furaha hakutaka kuamini macho yake juu ya vile vipimo, alihisi vipimo vile vinaongopea, akaomba vipimo virudiwe tena na baada ya kurudiwa majibu yalikuwa ni yale yale Happnesss hawezi kushika ujauzito. Machozi yalimtoka Happness.

                 “Dakta hivi ni kweli kusema mke wangu hawezi kushika ujauzito?” Furaha aliuliza  kwa majonzi.

                 “Ndo’ hivyo tena yashatokea, maji yakimwagika hayazoleki.

                  “Ninakuomba urudie kupima Bwana Dakta.” Furaha aliongea kwa huzuni

                  “Nimepima karbia mara tatu mkuu wangu, majibu ni yale yale hayajabadirika.” Yule Dakta aliyezoea kula rushwa na kufanya tendo la kumtoa mimba Happness leo alimwaga matokeo.



Basi Furaha na Happness wakawa ni watu wa kuhangaika huku na huko ili kutafuta tiba juu ya tatizo linalomkabili Happness. Walipoteza pesa zao nyingi lakini bado hawakuona matokeo, walipoteza muda wao mwingi lakini bado hawakuambulia kitu, waliambulia patupu, hasara kubwa namna gani, furaha yao ikatoweka baya zaidi walikuwa na mali nyingi lakini hawakuwa na mrithi wa hizo mali


               Wawili hawa wenye kujutia matendo yao, waliziona mali zao si kitu, pasina kuwa na mtoto, Furaha akawa ni mtu wa kujilaumu kwa jinsi alivyomshawishi mkewe awe ni mtu wa kutoa toa ujauzito looh! Tamaa mbele mauti nyuma, Hasara ilioje lawama pamoja na wingi wa mawazo vilimfanya Furaha akonde na kuisha kabisa.


Akuyatamani tena maisha, aligeukia ulevi wa kutupwa, kila siku ni majuto na masikitiko, looh! masikini! Tizameni ndugu zangu maamuzi mabaya uleta matokeo mabaya, yaliyomkuta Happness yawe funzo kwa wale wote wanao toa mimba au kuua vitoto ndani ya matumbo yao. Ikumbukwe kwamba hata Mwenyezi mungu hapendi matendo haya yanayochukiza, tusiyatende milele maishani mwetu bali tumwombe Mungu atupatie watoto lukuki wawe warithi wa mali zetu hapo baadae.


                                                   *************************


TCHAO 💖 


LOVE BEGGOTIS LOVE

 



NILIPORUDI VITANI NILIMKUTA MUME WANGU AMEOA MKE MWINGINE KWA HASIRA NIKAIVUNJA NDOA LAKINI MIAKA SITA MBELE TULIKUJA KUONANA TENA.


Ninakumbuka ilikua ni asubuhi Moja tuli tulivu kama maji mtungini, upepo💨 mwanana uliifanya miti 🌲🌴itabasamu☺️ Ndege 🐦🦜🕊️ juu mitini waliimba Tenzi na Mashairi 🎶 Vipepeo 🦋 na wadudu 🦗🐛🐝🐞🐌 wengi wengineo hawakukoma kujinadi kwangu mie Sheira Lulu niliyepita kwa furaha ya kurejea nyumbani kwa mume wangu, Huba na penzi 💖💘langu la thamani up nililoliacha miaka miwili na ushee baada ya mie kukimbizwa DRC Congo kwa tamko la Umoja wa Mataifa nilikua ni mmoja wa waliochaguliwa  kwenda kupambana na waasi wa M-23.🔫

     Mapambano ☠️💥ya kuwaondoa Waasi walioiteka miji mbali mbali ya DRC hayakua poa, ndani ya ile miaka miwili tulipambana kiume tukishuhudia wenzetu Lukuki wakiaga Dunia,⚰️💀 tisa kumi nilimshukuru Mola wangu 🙏🙇‍♀️baada ya kumaliza mapambano na Sasa ilikua ni furaha ya kurejea nyumbani kwangu kumfurahia Habibu wangu anipaye Cha mtoto🍆 🍑maana sio kwa upwiru ule nilimiss sana cha Mtoto.🍆😂.

      👣Step kwa step🦶🦶 mara baada ya kushuka kutoka ndani ya Gari yangu nilitembea pole pole na kwa madaha ya Tausi Ndege 🦚🕊️ mzuri Polini, begi langu mgongoni liliosheheni vifaa vya aina mbali mbali nilivyorejea navyo pasina kusahau zawadi tele kwa ajili ya Habibu wangu wa moyo.💞

Nilipogusa mlango wa sebuleni, 🚪mlango wenye kitasa kizuri kilichonakishiwa dhahabu🌟🔑 Og, ulilia 'Fyuuu' ishara ya kunikaribisha👐 kwa tabasamu la 'Karibu mama mpenzi' 🤗 Nikajitoma 'inside' Lundi 🦶 la mashoto lilitangulia Kisha Lundi la kuume lilipokea kijiti.

Mboni za macho yangu👀 ziligota juu ya picha iliyogogomewa na kugota juu ya kuta 🖼️ niliitazama nikamuona Mikali wangu amenikumbata asitake kuniacha mithilia kumbukumbi. 🐜 Mtimani nilifurahia sababu lile kumbato 👥ni ishara njema ya mapenzi yasiyochuja.

 Sebule haikubadirika sana kama nilivyoiwacha ndivyo nilivyoikuta; Meza ndogo ya duara mbao ya Mninga, Kuna Ua💐juu yake kama darizi. Sofa mbili kubwa za usasa zimepambwa vitambaa vyenye darizo la maua, kabati liliosheheni vyombo kutoka China, 🍽️chini ya sakafu Zulia la plastick lilipendezesha nyumba yetu. Labda kilichoongezeka ni Televisheni 📡📺 kubwa ya usasa na simu ya mkonga.☎️📞

Nikafanya kutembea kuelekea Jikoni nlikohisi yamkini Kuna mpishi akataye  Nyanya,🍅 vitunguu🧅 au  carrot🥕 maana niliskia sauti ya bao la makato likipiga kelele ndogondogo.

    Nilipofika mbele ya mlango wa jiko nikatupa jicho langu na kukutana na mwanamke mrefu wa kimo, mweusi wa rangi, tumbo lake limefutuka 'futuuu' mimba kamili🤰, mimba ya miezi tisa, aliacha kukatakata vitunguu🧅🧅kwenye bao la makato akanitazama na mie nikamtazama, tukatazamana 👀 👁️👁️‍🗨️tena kwa mshangao. Wakati mwenzangu akijiuliza kimoyo 'Ninani huyu ?! Mwanajeshi🤷 atafuta Nini kwangu? Kuna Nini jamani?' Mie pia kimoyo nilijitwika kiroba cha maswali 'Ni nani huyu? Mjamzito? Mikali kaoa au ni nduguye. Eeh!' Sikuambilia jibu la moyoni.

      "Karibu." Alinikaribisha. Sikumwitikia zaidi ya kumtazama.

      "Wewe ni nani!?" Alinihoji. Baada ya kuona ukimya wangu.

      "Labda nikuulize wewe ni nani katika nyumba hii."⁉️ Hakulaza mdomo alikua mnenaji na mdadisi akanijibu;

     "Mie ni Lela Mama mwenye nyumba hii" Alijitambulisha. Nilibaki bumbuwazi Ina maana Mikali tayari ameoa!! Hata kabla sijamuuliza swali jingine Mikali aliingia pale sebuleni kutoka mlango wa master bedroom.
 
      "Sheira Lulu." Aliponiona aliongea kwa mshituko kama Jusi🦎 lililobanwa mlangoni, macho yake pima👀.

      "Mikali mpenzi umeoa!!?" Nilimuuliza.

     "Nilijua umekufa Sheira, nilijua umekufa vitani baada ya miaka miwili ya kukusubiria na kukata tamaa." Hakunijibu swali langu zaidi ya kutoa maelezo.
    
       "Si ulisema utanisubiria milele, kwenye Jua na kwenye mvua." Kabla hajanijibu mkewe aliingilia kati.

      "Mikali hii takataka ni nani kwako ninaomba itoke nje, sihitaji upuuzi kwenye nyumba yetu."Aliongea kwa hasira.

     "Usimwite takataka yeye ndiye mmiliki wa hii nyumba."

    "Hata kama, ninaomba atoke nje, sihitaji kusikiaupuuzi wake." Lela alipiga kelele yawezekana Mimba ilimchefua.

     "Mikali ninaondoka, Asante sana kwa kuivunja ahadi yako." Nilitoka hima🏃‍♀️ndani ya nyumba yangu, nyumba niliyomkabidhi Mikali aisimamie hadi pale vita itakapokoma lakini ubaya wake Mikali aliivunja ahadi yetu.

      "Please Sheira, please usiondoke, usiniache." Alinikimbilia aliponiona nasepa zangu.

     "Mikali my love kumbuka mimi ni mjamzito, usiniache tafadhali"Lela alimpigia kelele Mikali lakini Mikali hakujali alinikimbilia hadi nje nilikotoka mara baada ya kuubutua mlango kwa hasira za ndimu.🍋👿💢


    "Please Sheiralulu usiniache,please l beg you." Alinishika mkono, nikausukumiza mkono wake kule mithiri ya mwiko unaompokonyoka msonga tonge asongaye nguna.

    "Niache nakwambia, niache Malaya mkubwa wewe haukua msubirivu kwangu." Nilimpokea kama matarumbeta yanayopiga kelele na kufoka.📯🎺

   "Bado upo moyoni mwangu Sheira, haikuwaipita siku, saa Wala tarehe ambayo sijakuwaza." Ninakupenda. Aliongea kwa bembelezo.

   "Kama ulikua unanipenda usingelinisaliti Mikali." Niliongea mishipa ya hasira ikiwa imenitoka shingoni, damu ya hasira ukiwa inakimbia vibaya mishipani. Yaani damu ilitamani kuipasua mishipa yangu nigeuke Zombie wa kuachwa.

   "Sikukusaliti💔 Love, nilijua uliishaaga Dunia sababu ulichelewa kurejea nyumbani." Alijitetea lakini sikujali utetezi wake. Nilielekea kwenye Gari niliyokuja nayo naye naye alinifata kama umbwa na mkia wake. Nikaingia kwa hasira upande wa Dereva nikashika ufunguo ili niiwashe gari yangu nitowekee mbali na peo za macho yake lakini kabla sijaiwasha ile Gari alinishika mikono yangu, nikamtazama na yeye akanitazama machoni. 👁️Wakati mie nimekabwa na hasira 😡yeye alihitaji kuyaweka mambo sawa.


      "Ninakupenda Sheira kumbuka Bado upo mtimani mwangu." Mikono yake ilijaa fukuto la moto wa mapenzi. Nilishangaa aliponisogelea, USO wake ukawa karibu na uso wangu, akanipapasa lips zake zilikaronia lips zangu, macho yetu yalizingirwa na viemoji tena viemoji vya moyo wenye hamu na tamaa ya mapenzi ulitegemea ni kipindi Cha muda mrefu Sasa sijakutana na Mikali wangu.

    Tulinuonyana ndimu ndani ya ile Gari dakika na sekunde zilipita taratibu tulianza kuvuana nguo zetu na kiweka pembeni ya Gari Kisha tukazamis nyuma ya Gari hapo hisia na matamanio ya ngono yalipamba moto. Kilichofusts ulikua ni kuogelea ndani ya dimbwi la Huba na kupigishana kelele za mahaba.

      Dakika harobaini baadae wote tulikua tumechoka na kuanza kuvaa viwali vyetu baada ya kuvaa tuliketi ndani ya lile Gari Mikali alianza up ya kuniomba msamaha na mie kwa moyo mkunjufu nilimsamehe
Mie kwa moyo wote nilimsamehe nikamwambia vitu vyote nilivyoviacha ndani ya nyumba yangu nakuachia sema kurudiana na wewe haitawezekana tena.


        'Ooooh! Jamani, uwiii saidia nakufa mimi!😢😭' Ghafla tulikatizwa maongezi yetu mara baada ya kusikia sauti ya  kilio ikitokeza Sebuleni.

       "Mkeo analia." Nilimwambia Mikali 

     "Sijui kapatwa na kadhia gani? Embu ngoja nikamtizame." Mikali alipotoka ndani ya Gari na mie nikamfuata. Tulipofika ndani tulimkuta mkewe akiwa amesimama pembeni ya sofa analia tumbo la uchungu wa kujifungua likiwa ulimemkamata, chupa yake ulikua tayari imepasuka. Tukafanya kumbeba mie upande wa kulia Mikali mashoto mzoemzoe tukampeleka nje ya gari kwa lengo la kumkimbiza Hospita, lakini mke wa Mikali aligoma kupelekwa hospitalu alidai mtoto yupo karibu kutoka.

     Nikaingia ndani ya Gari yangu nikatoka kijimkeka na kumlaza sakafuni, nikavaa grovu mikononi na Mikali pia akafanya hivyo hatua iliyofuata ulikua ni kumtaka Lela kwa u pole na kwa daraja avute pumzi na kumsukumiza mtoto ili atoke maana kichwa cha mtoto kilikua kikichungulia.

Kwa kilio na uchungu Lela alifanya kuvuta pumzi na kumsukuma mtoto mikono akiwa ameishikilia mikono ya Lela, mikono iliyokaza kuvuta hadi kuumiza wakati mie namchungulia mtoto aliyeanza kutoa kichwa chake kama Jua pevu la Alfajiri.

       "Vuta, vuta, vuta, kaza mwanamke" Nilimsihi Lela ajitahidi kupambana na hali yake, alitii, alijikaza naye akavuta mtoto alitoka taratibu na kukamilisha ujio wake Duniani. 

Tulikifunga kitovu cha yule Malaika na kukikata pia tukamwekaka mtoto kwenye tambarasafi, tukamhudumia Lela huduma ndogondogo muhimu. Mie baada ya kuimaliza kutoa msaada wangu nilimuaga Mikali 'kwaheri ninaondoka sintarudi tena' Mikali alianza kulia kiume, alinililia penzi lake la zamani lakini mie sikujali niliwasha gari yangu moto na kutoweka.



MIAKA SITA BAADAE (SIX YEARS LATER)


Lela akaomba kutengana na Mikali, kumbuka hapo tayari wamejaliwa kuwa na mtoto waliyempa jinale Shela. Sababu iliyompelekea Mikali kutengana na Lela ulikua ni Moja tu 'Mikali alipoteza hisia za kumpenda tena Lela baada ya kuniona mimi tu'. Mikali akawa kila siku ni mtu wa simanzi vilio na kudhoofika. Mikali akawa ni mtu wa kunit afuta Kila Kona ya Dunia lakini asinipate.


Nyakati za usiku wawapo kitandani Mikali alilitaja taja taja jina langu ndotoni. Walipokua katika tendo la ndoa Mikali hakumridhisha mkewe sababu moyoni mwangu hakunitoka, walipokua wakila chakula Bado tu akilini mwake sikumtoka, aliniwaza chakulani. Alikonda na kudhoofika hatimaye Lela alipogundua kuhusu jambo hili akaomba atengane na mumewe naye akabeba Kila kilicho muhimu kwake na kumuacha mtoto Shela mikononi mwa babaye Kisha akatoweka mbali na peo za macho.


Basi siku Moja mie Sheila Lulu na mwanangu Grace tulifanya kutoka nyumbani kwetu na kuelekea pahali pa kuyafurahia Maisha yetu, tulichagua Bustani nzuri yenye Kila aina ya michezo kwa watoto. Nilitaka mwanangu awe ni mwenye furaha hivyo nilimruhisu acheze michezo mbalimbali pamoja na watoto wenziwe. Mwanangu alifurahia kuruka kamba, kijificha na mengineyo.


Mie naliketi pahali nikilamba lamba ice cream yangu mdomoni ghafla dakika kadha zilipita pasina kumwona mwanangu Grace karibu yangu, alichelewa kurudi kutoka kwenye hiyo michezo yao. Ilinibidi nichukue jukumu la kumtafuta mwanangu nikiita ngeli yake 'Grace, Grace mwanangu Grace uko wapi?' wakati huo huo nalikua nikiisikia sauti ya mwanaume ikiita kwa nguvu 'Shela, Shela, Shela uko wapi mwanangu?' Nilihisi kama naifahanu ile sauti lakini sikuitilia maanani.

        'Shela, Shee....' Mola wangu we! Niligongana uso kwa USO na huyu mwanaume aliyekua akimtwfuta mwanaume aitwaye Shela. Nilipomtizama na yeye alinitizama Kisha akampiga ukelele kwa kuniita 'Sheila Lulu....' mie nae nikamwita kwa nguvu zote 'Mikali.' Alinikimbilia na kunikumbatia kumbato nililolimiss miaka mingi sana, akalia chozi na mie nilatokwa chozi zito.

      "Nilikumisi mpenzi wangu😢" Alitamka.

      "Nilikumisi pia Mikali wangu."🥹 Nilimjibu. Akanipiga kiss mdomoni😘 denda zito nikalipokea kwa mikono mkunjufu.

      "Kwanini ulinitesa?" Aliniuliza.

       "Nisamehe Dear,"Alimwaga chozi mie pia niliugua kwa machozi.

      "Dadiii," sauti ya mtoto wa kike iliita. Tuligeuka kumtazama.

      "Mamiiii." Sauti ya mwanangu iliita. Watoto wale wawili walikua wameshikana mikono kwa furaha. Shela akamkimbilia Mikali na Grace akanikimbilia. Watoto wakatukumbatia kwa furaha.

    "Una mtoto?!" Aliniuliza kwa mshangao.

     "Nadhani huyu ndiye mtoto wa mkeo Lela!?" Kabla sijamjubi swali lake nilimuuliza langu.

     "Ndio, lakini mie na Lela tuliishatengana." 

      "Oh! Pole," Nilimfariji Kisha nikamweleza jambo.

     "Mwanangu huyu anaitwa Grace ni mwanako pia, damu Yako." Alishangaa kivipi!!?

     "Ile siku Shela alipozaliwa, siku nilipotoka DRC vitani nilikuja nyumbani nikiwa katika siku za hatari yangu, Tulifanya ngono. Nilipojigundua kuwa nimeshika mimba sikutaka kuitoa nilitaka kukuzalia na kukutunzia kumbukumbu ya milele. Ninakupenda sana Mikali wangu." Nilimweleza, chozi 😢🥹 la furaha lilimbubujika.

    "Nakupenda pia Sheila Lulu, wewe ni mama Bora." Alinikumbatia.

     "Ninahitaji turudiane na kusamehe yaliyopita." Nilimwambia.

      "Asante Sheila nipo tayari hata Sasa." Alinikiss shavuni, 😘akatabasamu😊 na macho yake yakatoa Nuru 🤩ya mafanikio, akanipendeza tena 😍 akanipendeza zaidi ya zamani, zamani vita ilitutenganisha lakini Sasa mapenzi yametuunganisha. Wakati wa mapenzi umekua ni muda sahihi.

*'''''''''''*''''''''''''"""""''"*"""""
TCHAO 

Greetings in the name of Love 😘

*'''""""*""""""*""""''""*"""""

MY DARING CASANOVA

          




   MY DARING CASANOVA 


      Nilirejea ghafla nyumbani, 🚶‍♂️🏠nyumba aliyojenga mume wangu Wonder, siku hiyo niliaga Jeshini kwa lengo la kwenda kumuaga mume wangu Wonder maana ilibaki wiki moja tu msafara wa Jeshi letu kutoka Tanzania🇹🇿 uanze safari ya kwenda DRC ~Congo 🇨🇩 kuungana na vikosi vingine vya SADC  kulinda amani ya Congo.


         Kwanini sikutaka kuiingiza Gari🚘 yangu ndani ya Geti⛩️ la Jumba letu? Ok. Ni kwa sababu nilitaka niingie nikiwa na big surprise🎉 🎁💐 ukitegemea tarehe moja mwezi wa kwanza ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mume wangu Wonder, sababu hiyo niliandaa keki🎂🍰 nzuri ya birthday.

      Nilitembea hatua kwa hatua tena kijeshi nikapandisha ngazi za  kuelekea Veranda, mlango ulifungwa lakini sio kwa ufunguo, taratibu na kwa tahadhari niliufungua nikiwa nimeishika keki ya Birthday mkononi. Lakini ghafla nilipigwa butwaa baada ya kumuona mwanaume wangu akiwa nusu utupu, suruali👖 yake safi na nadhifu ilikua imeshushwa hadi magotini, mwanamke nisiyemjua alionekana kuwa bize akiunyonya uume wa mume wangu.🍆

       "Wonder!!" Niliita kwa sauti nzito,💥💢 kwanza alipotupa jicho lake kuelekea pahali niliposimama alishituka yule demu aliyekua akinyonya sehemu za siri za mume wangu alishituka pia akaacha kile kitendo haraka sana, mume wangu akafanya kuinua ile suruali yake iliyotua magotini na kuipandisha kiunoni kwake wakati huo yule mwanamke wake alikimbilia mgongoni kwa mume wangu lengo likiwa ni kujificha sababu aliingia woga aibu na hofu.😰

     "Unaogopa Nini? Embu Toka mgongoni kwangu" Mume wangu alijaribu kumparanganyua yule Dame.

      "Tumekwisha Wonder!" Dame alitetemeka hadi wigi lake kichwani lilitetemeka.

      "Ondoka, ondoka😡🧟,usimuogope." Wonder alimuamuru yule Dame, Dame kwa woga na wasiwasi alitoka nduki 🏃‍♀️🐎💨 ndani ya nyumba yetu. Mimi na wonder tukatazamana👁️👁️‍🗨️

    "What  have you done?" ⁉️Nilimuuliza kwa upole wakati huo Keki ya Birthday🎂 nimeiweka juu ya meza ya chakula.

    "Agirihanna ulitegemea ningelifanya nini kama wewe mwaka mzima upo Jeshini 🔫na mimi mumeo nateswa na hisia za kimwili?" Aliniuliza Kisha akaendelea kunena.👄

     "Sikufichi Agirihanna mimi mumeo nimepoteza hisia za kupenda 💔au kufanya tendo la ndoa pamoja na wewe."  Nilimsikiliza.

    "Unajiuliza kwanini umenifumania na yule mwanamke!? Ni hivi yule ni zaidi ya mwanamke na wewe nyumbani kwangu ninakuona kama kinyago cha mpapure tu! Kimya nilimsikiliza tena.

    "Ninataka mwanamke ndani ya nyumba sio Captain wa Jeshi la kujenga Taifa, sihitaji mwanamke ambaye atakuja kunitawala baadae na kuwa juu yangu." Lugha yake ilinifanya nipoteze uvumilivu machozi yalinidondoka. 😿😢 Akajaribu kunisogelea nikampigia kelele;🔊

    "Tafadhali usinisogele,👉 sikutaka kupoteza muda nikaiacha mizigo yangu yote niliyokuja nayo nikatoka nje kwa hasira, Wonder hakujishuhulisha wala kujali hasira zangu.👺😡

    Nilivurugwa kwa zile kauli za mume wangu haraka nikakimbilia Bustanini shamba la Maua na nyasi 🌺🥀kulikua kuna mpira wa maji 💦pembeni, nikauzoa zoa kisha kufunguli koki ya bomba nikajimwagia maji na kuoga nikiwa na nguo zangu za kijeshi (Ninakumbuka mwilini nilivaa kisingledi chepesi, kiunoni nilitupia Suruali na laba zangu nzito.)

      "What a wonderful girl!!" 💖 Sauti ya mwanaume aliyesimamisha Gari pembeni ya miguu yangu ilisikika. Alikua ni mtanashati 😍🥸mmoja ambaye sikujali Lugha yake.

      "Waooo! 😱😘Natamani kulala na Solder, Kwan kulala na Mwanajeshi ni bei gani kwa mfano!?" Alitoka ndani ya Gari yake ile nzuri aina ya Tesla.Gari hadimu kupatikana ndani ya nchi yetu. 

     "Shit!?" 🫥Nilipandwa hasira, Lugha ya yule mwanaume kijana haikunipendeza, nikamsogelea hadi pale aliposimama nikamshenyenta na kumzandika ngumu moja nzito ya kikomando iliyotua puani kwake, akagugumia kwa sauti ya maumivu makali maana damu zilianza kumchuruza kutoka puani 👃🩸


     Sauti ya maumivu ya yule mwanaume ilimfanya mume wangu Wonder atoke ndani mkuku mkuku akasimama pale alipoangukia yule mwanaume bila huruma alitishia kuniponda kwa ngumu na mateke, lakini angeweza!? Si anajua mie ni lron Lady mwanamke wa chuma.

      "Ndio maana nimekwambia siwezi kuishi na mwanamke mwenye mabavu dani ya nyumba yangu." Akamgeukia yule Bwana niliyempa kipondo cha pua. "Pole sana rafiki Bwana Casanova mwanamke huyu simtaki Wala Sina haja naye." Aliongea akininyoshea mkono.

     "Mbona hukuniambia kama umeoa na na unaishi na mwanamke mrembo kama huyu!?" Yule Bwana aliuliza.

    "Historia ndefu jirani yangu!?" Wonder alimjibu yule Bwana kwa kifupi. Akanigeukia akaendelea kunipa Lecture zake.

      "Agirihanna hatuwezi kuishi hivyo ninasema nimekuchoka hivi kwanini usiondoke tu hapa nyumbani kwangu kuliko kuendelea kuishi na mtu ambaye amekutoa mtimani 💔mwake. Nasema sikupendi fahamu pia majirani hawana hamu na wewe." Aliongea sana na kupiga kelele. Mapenzi nyie walisemaga wahenga :'Hata Mjeshi awe Mikali namna gani lakini kwa mumewe ujigeuza mtoto mpole' ndo' mie nilijigeuza mtoto  kwa mume wangu Wonder niliyempenda kwa dhati.

     "Ok. Naomba yaishe," Niliingia ndani nikalichukua begi langu kubwa lile nililokuja nalo kutoka kambini, nikatoka nje  na kuanza kuondoka.

     "Usirudi tena hapa, hata majirani hawakutaki, hawataki kuishi na Mjeshi." Alirudia kauli zake za awali, Wala sikumjibu maana mapenzi kati ya mimi na yeye yalichina.

     Kipindi naondoka nilimuona yule mwanaume niliyempa pondo la pua alikua akiangaika kufuta damu zilizomchuruza kutoka puani. Kwa uzito wa kile kipondo hakika pua yake ilitaka kupinda na kuregea. Nilisimama kwa sekunde chache nikamtazama Kisha nikajisemea mtimani:
    
      'Niifute past moyoni mwangu, niikaribishe future moyoni mwangu.' Nikatabasamu😊 na kuelekea kule alikosimama yule mwanaume mtanashati. Uzuri alisimama nyuma ya buti la Gari yake afutafuta damu puani.

   "Sikujua kama jirani yangu Wonder kaoa, samahani kwa hilo." Aliongelea puani na pua yenyewe ilivuja damu. Nilipohakikisha nimeweka begi langu ndani ya buti  nilimsogelea nikashika pua yake iliyolala upande nikaibinya kwa nguvu na kuiweka sawa. Akapiga kelele kidogo 'Aah! Taratibu utanivunja basi' Nikamcheka😂.

      "Nipeleke popote unapoona panafaa kwa mrembo kama mimi kwenda, kuanzia Leo Wonder sio mume wangu Bali ni Ex-husband." Nilimjibu

      "Utaenda wapi na utalala wapi!?" Aliniuliza

      "Popote nitaenda na popote Kambi nitalala." Nilimjibu tena.

   "Twende nyumbani kwangu ninachumba kizuri kulala." Damu zilizokua zikimtoka sasa zilikoma.

    "Haina shida twaweza enda." Alifunga buti ya Gari yake wawili tukajitoma Garini Safari ya kuelekea kwake ikapamba moto. Tulipiga story njiani Dereva wangu Alijitambulisha kwa jina la Casanova yupo singo na ni mmiliki wa makampuni makubwa hapa Afrika mashariki. Mie pia nikajitambulisha kwake na kumwambia cheo changu Jeshini yaani Captain wa Jeshi la kujenga taifa (JKT)

        Tulipofika nyumbani kwake Bwana Casanova alinikaribisha sebuleni na kuniandalia Kahawa nzito pamoja na vitafuno kwa kweli nilifurahia huduma yake. Basi tulianza kupiga story mbili tatu za hapa na pale mie sikumficha juu ya ile Issue ya kumfumania mume wangu Wonder akizini na kahaba wake, pia sikumficha juu ya kutimuliwa nyumbani pale alipojenga mume wangu Wonder kisa kikiwa ati alipoteza hisia za kunipenda milele.

      Casanova alionesha kujali, binafsi sikuutegemea upendo mkubwa alionionesha kutoka kwake alinieleza Kila kitu kuhusu upendo wake kwangu. Aliniambia ananipenda pendo la kupendeka, pendo tamu kuliko Pipi. Basi tulikula na kuinjoi pochopocho la mchana na pia usiku tulikula Dinner  Kisha tukaingia Master bedrooms kulala. Ajabu Casanova alikua akiogopa kufanya tendo la ndoa pamoja na mimi.


Nikajidamsha pale kitandani, nikajiketisha nikimtazama kisha nikamwagia swali: " kwanini wanifanyia hivyo?" Alitamani kujibu nikamzuia 'shhhhhh' nikanena tena.

     "Au wewe ni hanisi? Haunipendi waniongopea kwa sababu mimi ni Mjeshi." Casanova wangu akanijibu akiwa amelala juu ya kitanda chake.

     "Hapana Agirihanna mimi sio hanisi pia ninakupenda pendo la kupendeka.💖💝
      "Sasa kwanini  waogopa kufanya ngono pamoja na mimi......" Sikumaliza kauli yangu Casanova alinivamia pale kitandani akanilaza chalii akanipa ulimi wake.... Weuuuuwe!!! 😂Nilianza kunogewa..... Mechi yetu ilichezwa uwanjani dakika tisini tukawa hoi bin taabani juu ya Huba tulilopeana 

      *************

Penzi langu mie na Daring Casanova lilinoga, tulipopika hatukusita kupakua, tulipofua tulifua pamoja na kuoga tena ulikua ni mwendo wa kuogeshana. Matani na mipango Mingi mingine ya kimaisha iliitia fora. 


Baada ya wiki Moja kupita nikiwa ndani ya penzi la sweet Casanova siku moja nalikua nimejibwaga kitandani usingizi wangu ukinipa ongezeko la siku za kuishi
 Duniani. Niliifadhi Bastora🔫 yangu kitandani upande wa bega langu la kulia nilishtuka nilipomwona Darling Casanova akinyata kuelekea pahali ilipoo Bastora yangu. Nikaamka ghafla pale kitandani na kuiwai Bastora yangu Kisha nikampointishia na kumuuliza 'What are you doing?' Mpenzi wangu alitabasamu akajiketisha ule upande Bastora yangu ilihifadhiwa kisha akatoa Box dogo alilolifungua na kunionesha Pete yenye kito cha💍 Almasi, akatamka:

       "Will you marry me🤵💒.(Nataka kukuoa)" Nilishangaa Kisha nikamjibu.
      
     "Umerogwa mpenzi Casanova? Yaani ndani ya wiki Moja tu unataka kutangaza ndoa?" Wangu wa Huba akanijibu:

     "Mapenzi hayabagui, mapenzi hayachagui. Kwako nimekufa mazima nasubiri unizike tafadhali tamka neno 'Yes,👰💒 lwill marry you' (ndio ni tayari kuolewa na wewe)

     "No! I'm not leady (Hapana! sipo tayari.) Nilinena pasina kupepesa macho.

    "Why not (Kwanini hapana!?) kama ni suala la mumeo, mumeo tayari amekukataa tena Hana haja na wewe. Tafadhali naomba nafasi moyoni mwako niitumie."  Casanova alinibembeleza.

     "Hapana Casanova Nina hofia kukuweka katikati ya hofu"😱🤯
  
      "Hofu! Hofu gan Laazizi!?"Aliniuliza.

      "Binafsi unajua mie nimebakiza siku tatu tu nielekee DRC 🇨🇩 kushika hatamu. Hivi je nikirejeshwa mfu si ntakutia hofu, kilio, machungu stress na wakati mgumu!?"" Niliendelea kunena;


 "Nisiporejea wangu wa moyo utapata uchungu na presha. Kamwe haitapita siku pasina wewe kuniwaza" Ni kama vile hisia zilizochanganyika na hasira zilinivamia nikaamka pale kitandani na kubeba buti, Bastora na begi langu lenye vitu vyangu muhimu kisha nikafanya kutoweka na kumuacha huzuni mtimani.

""""""""""""""""""''''''''"""
     Siku ya kuondoka Tanzania na kuelekea DRC mie Captain Agirihanna nikafanya ukaguzi wa Jeshi langu ambalo ningeliondoka nalo kutoka Tanzania kwenda DRC.Basi katika pitapita ya ukaguzi wangu nilishtuka kumuona Casanova ametinga mavazi ya kijeshi tena amepanga mstari wa mbele pamoja na Wanajeshi wa kundi nililotakiwa kusepa nalo. Mie nikauliza swali:

     "Nielezeni hivi ni nani aliyemruhusu huyu mtu awepo ndani ya kundi langu!?" Hakuna aliyenijibu. Nikamwita  Casanova:

     "Casanova"

      "Yes captain" Aliniitikia kwa heshima na ukakamavu.
   
      "Sogea mbele." Alitii amri akasogea mbele  na kunipigia saluti.

      "Haraka uje Ofisini."

      "Yes captain" Alikubali wito.

 Nikaelekea Ofisini moyo wangu ukiwa umechanua kama Uaridi🌹tabasamu nene na pana lilinitoka kinywani💋 macho ya furaha na mapenzi yaling'ara na kunipendeza👁️


 Nilifurahia Casanova mtu ambaye amenipenda hata anifuate twende wote Vitani. Nilifurahia jinsi anavyojali ingawaje hajui jambo lolote kuhusu vita au Jeshi. Kwa sababu ya mapenzi Casanova ameacha Kila kitu muhimu maishani mwake ili tu anifuate mpenzi wa moyo wake. Ameacha cheo chake, mali zake na Kila kitu alichonacho ili tu awe karibu na mtu autesaye moyo wake na mtu huyo si mwingine zaidi ya mimi. Mtimani nilijiambia 

'l love you my Daring Casanova 💝💖🌹.



###########

TCHAO 💖

#######*****
    
     


Wednesday, April 30, 2025

I promise you

  

I PROMISE YOU.

(NINAKUAHIDI.)






SURA  YA KWANZA.


UBAYA WA POMBE.


“Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini lakini? Kwanini unanifanyia hivyo?” Brenda alinilalamikia. Machozi yake yakimtiririka kwa wingi kama mvua inayomwaga maji yake jangwani, mara baada ya ukame wa muda mrefu sana kulitikisa hilo jangwa.

               Ni ukame? Ndio ni ukame na ukame huo kwangu mimi Job naweza kuuita umasikini, umasikini uliokithiri, umasikini mkubwa haswa, umasikini wa kutupwa, umasikini ambao kamwe mpenzi msomaji hauwezi kuuokota, lakini looh! Sina jinsi ninakubaliana na hali halisi ya maisha  yangu mimi na huyu anipendaye Brenda. Machozi yake yanaumiza tena yanaumiza sana. Brenda wangu analia lakini nifanyaje mie job ningali bado ninafikra zile zile kwamba ipo siku mimi na Brenda tutakuja kuuaga umasikini na kuja kuishi maisha ya furaha na starehe.

                “Ipromise you, Ipromise you Brenda, I will fulfill all of your demand, you just have to wait , a beautiful time and a beautiful moment will come.” Ilo lilikua jibu langu, jibu ambalo nimekuwa nikimjibu Brenda kila siku ya leo, nikiziona hasira zake zinamtuma kugadhibika mambo yasije kuharibika.

               “Mpaka lini Job? Mpaka lini mpenzi? Niambie ni lini utatafuta mahari ili niwe wako  milele? Ni lini utaniweka ndani ya nyumba yako ili siku moja nije nipate kuishi kwa furaha pamoja na wewe? Ni lini Job?” Brenda aliongea tukiwa tungali ndani  pori lenye nyasi fupi,  wawili tupendanao .

             “Tambua kwamba na mimi pia ni mwanamke, tena ni mwanamke sawa sawa na wanawake wengine walio olewa, ndani na nje ya kijiji chetu wapo mikononi mwa waume zao wanafurahia mapenzi, nina imani kwamba mapenzi yao ni zaidi ya mapenzi, mapenzi matamu kama pipi, hayo ndiyo nina haja nayo, ya kwamba nina kuhitaji sana Job, ninahitaji niwe moyoni mwako nipate raha na furaha, nipendwe kama wanavyopendwa wanawake wengine” Brenda alilia.

               Nilimsikiliza tena nilimsikiliza vizuri sana Brenda wangu daima sina ile tabia ya kumkwaza mwanamke huyu, daima nimekuwa msikilizaji wa  wa shida na malalamiko yake lakini ubaya wa masikio dume niliyo nayo nimekua mgumu kumtimizia yale yote ambayo Brenda wangu amekuwa king’ang’anizi wa hayo anayo yatamani.

              “Hupaswi kutumia imani pekee mpenzi wangu Job, imani isipokuwa na matendo hiyo sio imani imani hiyo ni imani iliyokufa, imani batiri. Tafuta kazi, kazi nzuri itakayo kulipa mshahara mnono, au  jaribu kutafuta mtaji jiajiri, kazi yako binafsi. Mpenzi nimekuwa nikikushauri kila siku juu ya jambo hilo la thamani ajabu sikio la kufa halisikii dawa, unanipuuza mpenzi, wanisikiliza lakini hautendi kama ninavyokushauri, ushauri bora kama huu.” Brenda alinishutumu.

              Alikuwa na haki ya kunishutumu, kwa sababu mimi binafsi nimekuwa mzembe sana kwake,daima sina mbele wala sina nyuma, nipo nipo tu hapa kijijiini  goigoi ndilo jina langu, kila mwanakijiji ananijua na kunitambua kwa jina hilo, jina la goigoi, yaani mvivu mzembe, kijana dhaifu. Burudani yangu kuu ni kushinda kwenye bunge la walevi huko nitayapiga maji, nitapiga nitapiga hadi nivae miwani nikiisha kuvaa miwani nitajikokota kokota kwa kujilazimisha nifike nyumbani kwa babu na bibi yangu waliionilea kama yai la kuku. Njiani nitajibwaga bwagaza nitaongea kila neno la kilevi nitachekwa na wapitao njia, watoto watanizomea hilooo! Hiloooh! Hilooo! Yuuuuuu! Yuuuuu! Yuuuuu! Lilevi hilo, goigoi hilo!” loo! Mazomeo hayo ni mazomeo ya kila siku, watoto hawachoki kunizomea


            Watoto wataniimbia nyimbo za dhihaka, yote kwa sababu mimi mwenyewe ninafanya dhihaka. Pombe sio chai, tayari sarawili yangu imeloa mkojo, imezingarwa na inzi kibao wanaoimba ‘ziii….. ziii…ziii’ nyuma ya matako yangu, looh! Jamani kweli pombe sio chai, mwenzenu tayari nimejinyea tena nimeharisha. Vibaya mno, watoto hawakomi kunidhihaki kwa nyimbo zao.

Jobu akilewa lewa,
Anashindwa kujielewa lewa.
Kikojozi huyo, kikojozi huyo,
Avishwe nepi huyo, kajinyea huyo,
Huyoooo, huyoooo, huyooo,
Mtu mzima ovyo.

Oosh nyimbo zao haziniingi ndani ya ubongo wangu, ninaona ni kama burudani , nami ninaimba kwa kuwaigiliza, ninacheza kama wanavyocheza wenyewe, looh! Ama kweli pombe sio  chai, watoto wamenizoea vibaya sana, hawachoki kunikebehi kwa nyimbo zao haweshi kunizomea, haweshi kunirushia mawe haweshi kunipiga kwa bakora, yaani hadi aibu, aibu jamani aibu mtu mzima ovyo ninapigwa kwa bakora, ninapigwa kama mwanafunzi wa praimari skuli.

                 Hili jicho langu la mashoto halijapotea bure, nimekuwa chongo kwa sababu ya kujitakia mimi mwenyewe, nilijitakia kijana wa kijijini, ndo’ kusema pombe sio chai, walinena wahenga; “kipofu akimwongoza kipofu mwenziwe wote watatumbukia ndani ya shimo.” Mimi ni kipofu wa pombe (ulevi) na pombe yenyewe pia ni kipofu ambaye hachoki kunipotosha pamoja na kunipitisha njia zenye hitilafu.

                Pombe ni kipofu, ndio ni kipofu, kwa sababu haoni mdudu huyu, haoni mbele, haoni nyuma, kazi yake kubwa kupotosha vijana wa kijiji ninacho ishi.
Ninaukumbuka ule usiku usio na mbalamwezi, usiku ambao almanusura niwe kipofu wa macho yangu yote mawili lakini hata hivyo ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, niliponea chupu chupu kufa, nusu kufa, mjiti uliniingia ndani ya jicho langu la kuume, duh! Ni kama vile ulikua mtego, mtego uliotegwa kwa makusudi ili unikomeshe mie goi goi nisiye taka kufanya kazi.

               Niliteleza kwenye tope ambalo lilijikusanya pahali mara baada ya mvua kunya usiku kucha. Ilikua ni usiku, usiku usio na mbalamwezi, sikumbuki ilikua yapata saa ngapi, usiku ule mie kijana goi goi mvivu nisiyetaka kufanya kazi nilitoka kwenye bunge letu, bunge la walevi. Nimegida mitungi ya kutosha, sina hofu, nimekwisha kuzoea kwenda bungeni saa za majogoo na kurejea nyumbani saa za kulia kwa mabundi na mapopo. Mimi ni Mbunge mtiifu wa  gongo, changaa na matapu tapu mengine mengi yaliyopitwa na wakati.

Daima nipo, sikosekani kwenye bunge letu la walevi wa kijiji chetu,  huu ni mwaka wangu wa tano ningali bado nipo bungeni na uzuri wake  kwa sababu nina maudhurio mema sina budi kujitapa kwa cheo chema nilichopewa na walevi wa kijiji chetu. Spika wa bunge la walevi, hilo ndilo jina langu, jina tukufu ulevini.

                Nisikufiche mpenzi msomaji, nilijikuta najistafisha kuhudhuria vikao vya bunge la walevi, nilijiuzuru mimi mwenyewe pasina shinikizo la wabunge au mawaziri wa bunge letu, bunge la walevi, sababu kuu ikiwa ni kukumbwa na mkosi huu mzito wa kugeuka chongo na chongo yenyewe niliivuna kutokana na ulevi wangu wa kupindukia.

                Usiku ule nilikua bize nagara gara ndani ya dimbwi lenye tope, ili nipate chance ya kujiokoa na kutoka ndani ya lile dimbwi nililo tumbukia kutokana na ulevi. Nilikuwa bwii kwa pombe ya gongo,  nilifanya kila niwezalo nipate kujiokoa kutoka kwenye lile shimo lenye tope,  nikiwa bado ndani ya lile dimbwi nilijiuliza nitatokaje ili nipate chance ya kwenda nyumbani kwa babu na bibi nikajibwage kitandani, niusake usingizi wa pono ili nipate kujiandaa  asubuhi na mapema niwahi bungeni  kupiga mitungi. Haki nilikuwa mlevi, mlevi mbwa, mlevi aliyeshindikana.

Jitihada za kutoka ndani ya lile dimbwi hazikuzaa matunda, nikajikuta napiga kelele za zilizotokana na maumivu makuu, maumivu yasiyo na kipimo, maumivu yasiyo na kikomo.

                 “uwiii! Uwiii! Uwiiii! Yallah toba we! Jicho langu jamani jicho langu! Nafwa mie, nafwa jamaa” kilio kilinitoka, kilio cha mlevi mwendawazimu, kumbe nilidondoka, kumbe nilidondokea kwenye shimo lililokuwa na miiba mirefu, mikavu iliyochongoka kama pini, ikauchoma choma mwili wangu na ubaya wake jicho langu la kuume(kulia) halikupona lilikua ni miongoni mwa sehemu zilizoonja shubiri ya mwiba, lilikua kwenye ile ajari ajari ya mlevi, ajari ya kujitakia.

                Ndio maana nimekwambia mpenzi msomaji nilijikuta naachana na ulevi, nilijikuta naachana na mazowea ya kwenda kwenywe bunge la walevi, nilijikuta najiuzuru cheo na wadhifa wakuwa spika wa bunge la walevi, ilinibidi niachane kabisa na pombe. Walisema wenye hekima asiye fundwa na mamaye ulimwengu utamfunda. Mama na baba yangu walikwisha tangulia mbele za haki sikupata nafasi ya kufundw a na wazazi wangu, malezi yaliyo jaa madekezo mapendeleo na matunzo ya kiyai yai ndiyo niliyapata kutoka kwa babu na bibi wazazi wa baba.

                Mapendeleo yasiyo  na kipimo, mtoto toka utotoni hadi baleghe sikua na nafasi ya kujishughurisha na shughuri yoyote ile ndani ya nyumba ya babu na bibi yangu, ni madekezo tu madekezo na mapendeleo, nililishwa vizuri, nilinyweshwa vizuri, niliogeshwa, nilibebwa nikapewa kila kitu nilicholilia na baya zaidi nikawa mtoto msumbufu, mwenye masumbufu makuu.

                Kila lenye mwanzo halikosi mwisho, kwenye kuzaliwa kuna kufa, kwenye raha kuna karaha, kwenye amani vita pia ipo, sikutilia imani mawazo hayo hapo juu , ubongo wangu ulikorea pombe, pombe ya matapu tapu, ubongo huu mbovu usojua la muadhini au mnadi swala maisha yangu yalikua ni maisha ya kunywa matapu tapu ya aina mbali mbali, iwe umkombothi, iwe ulanzi, iwe mbege, iwe chibuku, ubwala, gongo, pombe ya minazi, pombe,  pombe, pombe,  pombe…….. Kila aina ya pombe kali mie nilikunywa, pombe kali kuliko sumu ya panya mie nilikunywa, pombe chungu kuliko nyanya chungu mie nilikunywa, nilijisikia fahari kunywa, nikalewa, nikasaza nikaburudika nikausuuza mtima wangu.

                 Leo nimeona wacha nifanye maamuzi magumu, maamuzi ya kuachana na pombe, pombe ni kipofu hawezi kuniongoza, ndiye aliyesababisha nitumbukie kwenye dimbwi lenye tope na katika harakati za mie kujiokoa nikajikuta natumbukia tena kwenye shimo lenye miiba iliyonigeuza chongo  jicho la kulia. Leo nifanye maamuzi ya kuikacha pombe, sio tu kuikacha pamoja na kujiweka mbali na pombe kusisitisha yale mazoea ya kwenda bunge lao bunge la walevi. Kama ni hasara jamani hasara kubwa nimeipata, hasara ya kulipoteza jicho langu la upande wa kuume. Sio hasara hiyo tu pia kuna ile hasara ya kujifedhehesha na kujiaibisha mbele ya watoto waliokuwa wakinizomea na kunichapa bakora.

                Katika kipindi chote hicho Brenda alinivumilia, Brenda hakuniacha japo nilikuwa mlevi nisiye na kikomo, na uzuri wa Brenda yeye kama mwanamke alijiweka tayari kunishauri niachane na hiyo tabia mbaya ya kupiga miknge, nalikuwa sikio lililokufa halisikii dawa, Brenda aliponiongelesha sikio la mashoto mie  nilijigeuza kiziwi, tena kiziwi anayesikia sauti lakini maneno hayaingii sikioni, Brenda akiniongelesha sikio la kulia bado nalijigeuza kiziwi nisielewe wala nisijielewe.

                Wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, tena wanasema ukijenga urafiki na mwendawazimu tegemea na wewe pia kuwa mwendawazimu, waswahili wako sahihi . mwanzo mgumu, lakini mwisho ni mazoea Brenda aliyekuwa kinara wa kunipinga nisinywe  matapu tapu kwa utundu wangu mie mwenyewe nikamuweka mtu kati nikamwonjesha matapu tapu kidogo kidogo, pole pole ndio mwendo, tabia ni mazoea Brenda akawa nguli wa kunywa matau tapu, akaifuata tabia yangu, tabia ya kunywa  kama mwendawazimu na kwa hilo mwenzangu mbona alitia fora. Alikunywa zaidi ya chupa kumi  za matapu tapu, zile chupa zenye ujazo wa bia aina ya Safari zilimtosha  usiku na mchana, Jua likichomoza jua likizama siku nzima.


                #########################################

Itaendelea



 love is all Given and found,🌹 It's all around,🥰 It's hard to tell about,😍 Easy to show,🤩 One sure thing when you feel it You kn...