Friday, October 4, 2024

KUCHEPUKA SIO dili... Sehemu ya 3




Sehemu ya tatu

ONYO.

                  Asha alikua yupo bize ana ‘typing’ mara baada ya kumuona Bwana Mawe amekuja shagalabaga, moyoni alimcheka, tai haikufungwa vema, shati lake jeupe halikufungwa vema, kifungo kimoja juu kingine chini, mkanda wa suruali uliachwa  haujakizunguka kiuno cha yule mwanaume, juu ya nywele zake kuna chanio, chanio hilo limeshikilia nywele zake.

                  “Vipi Asha bosi amefika.” Leo mdomo wa bwana Mawe ulitoa denda la ajabu.

                  “Ndio amefika, lakini mbona leo umechelewa namna hiyo? Alafu umekuja nyang’a nyang’a? Embu jitizame kwenye kioo kilicho juu ukutani.”         Asha alimwambia yule mwanaume kijana ambaye hakuweza kulijibu lile swali la kwanza kuulizwa alitii lile agizo la kujitizama kwenye kioo.

Loo! Mawe aliona aibu kwa mwonekano ule juu ya kioo, haraka haraka alikimbilia bafuni, bafu lililo nje kidogo na Ofisi yao, huko akajiswafisha swafisha kwa kuukosha mwili wake, kujipaka mafuta, kujipulizia marashi, kusafisha kinywa na kuzichana nywele zake. Mara baada ya dakika 40 alijitizama kwenye kioo kilicho ndani ya bafu lile, akajihesabia kuwa safi salama.

              “Wacha sasa niingie Ofisini kwa bosi, Bwana mawe akiwa nadhifu wa kupendeza aliongea na Secretary.

              “Samahani bwana Mawe.” Mrembo Asha aliongea.

              “Bosi yupo kuongea na mgeni.”

              Eeeh! Mfyuuuu, mawe aliubetua mdomo wake kuashiria kuwa hajapendezwa na ujio wa wageni hasubuhi na mapema.

             “Ni mgeni gani huo?” Alihoji.

             “Ni yule mwekezaji ambaye jana wlipanga wakutane Kipepeo Hoteli,”

             “Ok. Sawa…..Mmmh! akiisha toka naomba nipigie simu, unishitue ili nije kunena na bosi wangu.” Mawe aliongea wakati huo huo tayari amekwisha elekea kunako mlango wa Ofisi yake ili aendelee na kazi.

             “Poa!” Asha alijibu kimkato. Baada ya kupita masaa mawili, Asha aliuinua mkongojo wa simu ya Ofisini akimtaarifu bwana Mawe kwamba yule mgeni tayari amekwisha ondoka, Nafsi ipowazi kwa Bwana Mawe kuongea na bosi. Bwana Mawe alielekea moja kwa moja Ofisini kwa bosi wake. Bwana Viviani Vladimili ni mtu mzima mwenye umri wa miaka hamsini na ushee, ameketi ofisini kwake, anachora chora kwenye karatasi iliyopo juu ya meza yake

               “Karibu sana Bwana mawe, karibu keti kitini,” Bosi alimkaribisha Mawe.

              “Asante sana bosi, ninashukuru kwa ukaribisho,” Mawe aliketi kitini.

             “Eeh, una shida gani mawe niweze kukusaidia.” Bosi alisahau kutanguliza Salamu.

                 “Habari za tokea juzi, pole na majukumu, jana hatujaonana kabisa bosi wangu.”

                 “Nzuri sana Bwana Mawe, Nimepoa kimajukumu, lakini hata hivyo jana nilitoka nje kikazi, ndio maana Jana hatujaonana.”

                 “Ok. It’s good to hear from you,” M awe aliendelea kunena.

                 “Jana nimepokea ujumbe wako kutoka kwa Asha Secretary lakini kwa bahati mbaya sikuelewa vizui ulikua una maanisha nini bosi wangu..” Mawe alihitaji kujua.

                 “Aaah! Si wewe umeoa!?

                 “Ndio bosi wangu.”

                 “Vema, embu nieleze siku zote tunatoka kazini saa ngapi?”

                 “Saa nane bosi wangu.”

                 “Na wewe mara baada ya kutoka hapo uwa unafika nyumbani saa ngapi.?”

                 “Saa kumi  na mbili bosi wangu.”

                 “Are you sure, una hakika na unacho ongea? Bosi alikua na shaka.

                 “Nina uhakika bosi.”

                 “Haki ya Mungu!!” Bosi alitilia mkazo, Mawe alishindwa kuendelea kunena, akatizama chini kidogo, ndani ya sekunde chache alijibu.                

                 “Jana nilichelewa kutoka, sababu nilikua nikikusubiri, ili tuje tuongee suala hili.”

                 “Sawa hilo halina tatizo na pale Buzi bar, daima waenda saa ngapi?” Mawe alipigwa na butwaa asitake kuamini kama bosi wake amekuwa akimfuatilia hadi Buzi bar, Ukitegemea  Buzi bar ipo vichochoroni  na kwenye vificho, bar hiyo ni yenye hadhi ndogo kwa watu wa daraja la chini sio jambo la kawaida kumuona mtu kama bosi wake akinywa matapu tapu.

                  “Mbona haunijibu, hilo mimi nanalijua sana, daima nmekua nikikuchunguza, kila ukitoka hapa kazini, nisingelipenda ujieleze sana ila ningeliomba ujirekebishe na utimize majukumu yako wewe kama baba mwenye familia.”

                  “La..La…La…La….Lakini bo…siiii” Mawe alikamatwa na kigugumizi.

                  “Mbona umekamatwa na kigugumizi, ok. Embu nenda ukaendelee na kazi zako za kiofisi.”

                  “Sawa bosi.” Mawe alirudi ofisini kwake akiwa na mawazo chungu nzima , siku ile alifanya kazi mdogo mdogo naye akapitiwa na usingizi kisha akadozi. Alipokuja kushituka ilikwisha timu saa nane kamili, pasina kuchelewa. Mawe alifunga kazi.

                  “Duh! Ama kweli kulala  noma, yaani nimelala kwa muda mrefu haswa, wacha nifunge  kazi, kwa leo, halafu kesho niwahi mapema bwana Mawe, aliongea yeye na moyo wake,mawazo yalimzoga kichwani akajikuta anasahau ushauri aliopewa na bosi wake. Pasina kutarajia alijikuta anadondokea Buzi  bar bar ambayo Bosi wake alimwambia hapo awali kamwe asijaribu kuigusa, asipite wala asifanye mazoea ya kwenda hapo, kamwe asiendeleze tabia ya kukesha na kushinda bar.

                  Bosi aliongea hivyo kwa kumtaadharisha kwa sababu ulevi wake ulikua ni chachu ya utendaji mbovu kazini, mbovu usiotamanika, ulevi wake ulimfanya mara nyingi ashindwe kufanya kazi kwa bidii na matokeo yake sasa akawa ni mtu wa kuchelewa kufika kazini, mtu wa kulala ofisini akiwa amechoka kutokana na kukesha bar, mtu wa kuja hovyo hovyo na kumtia aibu bosi wake mbele ya wageni waliomtembelea huyo bosi.

                                 ******************* 

 


KUCHEPUKA SIO dili...sehemu ya pili


               


Sehemu ya pili

TAHADHARI.

Juma tatu ya leo Bwana Mawe alimuaga mkewe, akamwambia asingelichelew kurejea kutoka kazini lakini yote tisa kumi, bwana Mawe alikua  akimvisha kilemba cha ukoka mkewe, alimficha ilihali akijua fika kuwa yeye sio mkweli wala yeye sio mwaminifu.

               “Kwa heri mke wangu mimi ndio naelekea kazini, ninakutakia mchana mwema wenye mafanikio, “ Akilegeza regeza tai aliyo jifunga ili ipate kukaa vema.

               “Sawa mume wangu ninaomba usichelewe kurejea, mpenzi ukumbuke kuwahi kurejea nyumbani ujumuike na familia.”

              “Ok my wife, I love you all, ninawapenda wote. Ilove you so much, ninakupenda sana, ninakuahidi jambo moja zuri la kupendza sintachelewa kurejea, nitawaletea watoto zawadi wazipendazo.” Akalibeba begi lake mkononi huyo tayari kuondoka.

              “vipi mume wangu mbona unaondoka pasina kuacha pesa za matumizi ya  hapa nyumbani Bi. Neema alimkumbusha mumewe.

              “Pesa  za matumizi zipo ndani ya lile kabati letu la nguo, tafadhari uzitumie vizuri, ujuwe namna ya kuzigawa kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani.” Mawe alimpiga mabusu mawili matatu mkewe kisha akaondoka.

Mkewe alijua fika kwamba ile shilingi elf tano aliyo kabidhiwa isingelitosha kwa ajili ya matumizi ya pale nyumbani hata hivyo bwana Mawe aliweka kiasi cha shilingi elfu hamsini kibindoni kwa ajili ya starehe zake.

 Kwa vile aliondoka nyumbani kwake Sinza kijiweni yapata saa mbili  aubuhi, aliweza kuwasili kazini kwake yapata saa tatu na nusu kwa sababu ya foleni na msongamano wa magari. Alipofika kazini kwake, Secretary alihitaji kuongea na yeye mawili matatu.

              “ Habari za asubuhi, bwana Mawe.”

              “Nzuri tu secretary wangu, je hawajambo wote waliopo kazini?”

              “Sio kwema sana bwana Mawe.”  Asha Secretary alimjibu bwana Mawe kwa ufupi.

              “Una maana gani kusema hivyo bibie?!” Bwana mawe alidadisi kidogo.

               “Bosi amenipa ujumbe nikufikishie.”

               “Oooh! Ujumbe ni ujumbe gani ten huo? Bwana mawe alikua na shauku ya kutaka kujua juu ya huo ujumbe.

               “Labda ungeliketi hpo chini kwenye kiti ili nikutupie ujumbe wako.” Asha aliongea.

               “Ok. It’s not bad.” Bwana mawe aliketi kwenye moja ya viti viwili vitatu vilivyo mbele ya ile ofisi akisubiri kusikia  maneno mawili matatu kutoka kwa Secretay.

               “Bosi amesema hapendezwi natabia zako, nadhani kufika hapo umenielewa.”Asha aliongea kama vile anamjua kwa undani zaidi yule Bwanamkubwa.  

               “Tabia, eeh! Tabia gani haswa.?” Mawe alihitaji kuambiwa.

               “Nisingependa kukufunulia jungu, nikitambua kuwa mwenye macho ahambiwi tazma.”

                  “Kwa kifupi Habari yenyewe ni hii,” Asha alianza kumweleza bwana Mawe.      “Bosi anayajua machimbo yako yote, angependa kusikia umejirekebisha kabla maji hayajamwagika, kabla maji hayajazidi unga.” Asha aliongea kwa mafumbo.

                   
                  “Asha una manisha nini haswa, sipati picha na uhalisia wa maneno uyanenayo.” Mawe alihoji

                  “Mimi binafsi bosi hajanieleza kwa undani zaidi, hata hivyo kama una maswali zaidi ingelikuwa vema kama utamuona bosi mwenyewe anaweza kukusaidia.” Aliongea Asha akaendelea kuchapisha chapisha kazi za kiofisi.

                   “Bosi yupo Ofisini?” Mawe alihitaji kujua.

                  “Hapana bosi hayupo ofisini, amekwenda Kipepeo Hoteli kuonana na mwekezaji, kuna mambo ya kusaini mikataba.

                    “Je alisema atarejea Ofisini au atapitia nyumbani kwake?”

                    “ Alisema atarejea jioni ya leo.”

                    “Sawa ninashukuru kwa taarifa.”

                    “Ok. Have a nice job.” Asha yule binti mmoja mrefu, mwembamba, mrembo, chotara wa kiarabu na kipemba aliongea. Mawe ni mwanaume mwenye umi wa miaka 35 mtu mzima mwenye masharubu, ana umbo la miraba minne aliingia Ofisini kwake akaendelea na kazi zake, kichwani alikua akifikiria  kwa kina yale maneno aliyo nena Asha.

                     Saa nane mchana ni muda wa kumaliza kazi za kiofisi mara baada ya kumaliza kazi za kiofisi Mawe hakuitaji kurejea nyumbani kwake mapema aliamua kumsubiri Bosi wake anene  pamoja naye mara akirejea, bosi hakurejea.

                     “Sijui atarudi huyu bosi, mmmh! Ngoja ngoja yaumiza matumbo Mawe aliendelea kumsubiri bosi pasina darili za kumuona. Ilipotimu saa mbili usiku Mawe alikata shauri la kurejea nyumbani kwake, akajipa matumaini kwamba kesho angelimwona mkubwa wake.

Alirejea nyumbani kwake ni mwingi wa mawazo, amenuna kweli, mashavu yake yalionekana kutuna kama vile yameunguzwa  kwa amfuta ya kula, hana salamu, hana neno, moja kwa moja alipitiliza na kuingia chumbani kwake, kufika huko akajibwaga na kujitupa kama gunia lenye mpunga.

                    “Habari za kazi mume wangu? Pole na majukumu ya leo.” Bwana Mawe kimya.

                    “Mume wangu kwanini haunijibu salamu yangu tena?” Mama alimshangaa baba alivyoganda kama barafu mara ile bwana Mawe alishituka na kugutuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo.

                    “Eeeh! Aaah! Unasemaje mke wangu?” aliongea na kumtizama mkewe kwa mshituko

                    “Mume wangu nina kusalimu, ninakuuliza habari za kazi?

                     “Nzuri tu mama watoto.”

                     “Pole na majukumu  mbali mbali ya huko kazini,”

                      “Asante sana mke wangu.”

                      “Mbona ninakuona kama haupo sawa kifkra mume wangu umekumbwa na nini?”

                      “Nipo sawa mke wangu.” Mara ile Bwana mawe alitoka na kwenda bafuni kukoga na baada ya kukoga alirejea chumbani kwake akalala, mkeweaijishika tama kutokana na kuona mabadiriko makubwa kutoka kwa mumewe.

                      “Ana nini mume wangu siku ya leo, mbona anaongea kama yupo ndani ya mawazo mazito, hajala, hajanywa siku nzima ya leo, oooh jamani! A mepatwa na kadhi gani mume wangu? Mmmh! Makubwa haya madogo yana naafu.”

Hata hivyo kesho yake bwana Mawe alichelewa sana kuamka apate kwenda kazini kwake. Kama sio kuamshwa na mkewe basi angeliendelea kuuchapa usingizi mzito hata ufike mchana wa siku ile.

                   “Mme wangu, mme wangu” mkewe alimuamsha mumewe aliyelala usingizi wa Fofofo.

                   “Eeeh! Nini tena mie niko bize nimelala bwana.” Mawe alijipangusa tongo tongo machoni.

                   “Mme wangu tizama leo umechelewa sana kuamka, sasa ni saa tatu yaelekea saa nne, sijui utamjibu nini bosi ajapo kukemea kwa uchelewaji huu.”

                   Bwana Mawe akakurupuka pale kitandani. “Mungu wangu we! Ama kweli usingizi mtamu na mnono.” Shagalabaga, hakuoga wala hakupiga  mswaki moja kwa moja alivaa ovyo ovyo  akazichana nywele zake ovyo ovyo na kukimbilia kazini kwake, huku nyuma akimuacha mkewe anaishangaa hali ya mumewe, hali ambayo ajapata kuiona tangu wafunge ndoa ya kanisa.





KUCHEPUKA SIO DILI... Sehemu ya kwanza



Sehemu ya kwanza

 ANATOKA HOME.

Maisha ya leo yamebadilika sana, maisha ya leo ni tofauti na maisha ya zamani, dunia ya leo sio kama ile dunia ya zamani, dunia ya zamani watu walifanya kazi kwa muda mrefu sana pasina kuchoka waliwekeza nguvu zao  zote kwenye shughuri zilizo waletea kipato. Starehe kwao haikupewa kipaumbele kwa sababu ngoma ziliwatosha watu hawa kujiburudisha mara baada ya kufanya kazi nzito, pombe ilikua ni kinywaji cha burudani, hadithi ziliwafunda na kuwaonya kutokana na hayo mazuri waliyo jivunia jamii zao zilionesha mabadiliko sio kidogo bali mengi yenye wingi.


                  Dunia ya sasa watu hawataki kujibidisha kwenye shughuri  kama kilimo, uvuvi na uwindaji, lakini watu hao hao ndio wanao ongoza kwa kuhama na kukimbilia mijini wakidai kuwa huko ndiko kwenye maisha mazuri, huko ndiko kwenye kazi nzuri kwenye raha burudani na starehe, hwataki kurudi Vijijini, hwataki kuyakumbuka mashamba mifugo na mali asili zingine, hawataki kuzisikia shida zilizopo vijijini wanacho taka wao ni raha, furaha na  uzuri wa maisha yasiyotumia nguvu nyingi.


                      Hawa wapendao starehe, wamo ndani ya majiji makubwa makubwa na yale yaliyo endelea kama vile Dar es saalam, Arusha, Mwanza, Mbeya na sehemu zingine. Baadhi ya hawa watu wengi wao ni wale walio oa na kuolewa wanategemewa na familia zao, wanafanya kazi kwa masaa nane kwa siku. Zaidi ya hapo wapo wale ambao hawajaoa na kuolewa  baadhi yao sio waaminifu katika maisha yao, hawawajali wenzi wao, wanawatoroka wenzi wao na baya zaidi wana wasaliti (wanachepuka) wenzi wao na pia hawahudumii familia ipasavyo.


                Embu ungana nami katika kisa cha bwana mmoja aliye julikana kwa jina la Mawe, bwana huyu aliishi maeneo ya Sinza kijiweni ndani ya jiji la Dar es saalam. Ana kazi nzuri, aliajiriwa katika kampuni moja iliyopo Kariakoo. Mshahara wake mkubwa na mzuri uliweza kutosheleza familia yake yenye mke na watoto watatu.  Wahenga walisema masikini akipata matako ulia bwata. Mshahara wake hakuutumia vizuri yeye binafsi aliutumia mshahara wake kwenye burudani anasa na starehe. Hayo ndiyo mambo ambayo bwana Mawe aliyapenda maishani mwake.


                 Kwa ufupi bwana Mawe hakuwa na ile tabia ya uvivu kazini, alikua ni miongoni mwa wale wachapa kazi, watu wenye juhudi zao, watu wanaojituma zaidi kazini kwao. Lakini siku zote kizuri hakikosi kasoro. Ikawa hivyo tena aliutumia mshahara wake  wote, aliutumia vibaya tena vibaya na ubaya wayeye kutumia vibaya mshahara wake hakuonesha kuijali familia yake.


Aliacha pesa kidogo sana nyumbani kwa ajili ya familia, wakati huo huo fedha zake nyingi alizitapanya kwa wanawake wanao chuna mabuzi na sasa aliangukia chini ya miguu ya mwanadada mmoja aliye itwa Rehema. Huyu ndiye alikuwa akimchuna na kumlia pesa zake, Rehema alifanya kuzitafuna pesa za bwana Mawe mara tu apatapo mshahara.


                 Rehema alizishobokea pesa za buzi lake, hakukoma kuagiza vitu vya bei gharama, hakuchoka kulipangia buzi lake sehemu za burudani, starehe na anasa, Rehema alijiona yeye ni mwenye neema sana kuzitafuna pesa za bwana Mawe.


                 ####################



Ndoto ya kutisha.. sehemu ya nne

 

4


Ndoto ya kutisha

SEHEMU YA NNE

 Nilippozinduka nilijikuta ndani ya andaki, nimelazwa kitandani, nikiwa nimevalishwa mavazi na maumivu yakiwa yamepungua kwa uchache wake, kwani nilikuwa kama mtu aliyepewaa huduma ya kwanza. Niliangaza huku na kule nikaiona miale, miale miwili ya moto inanijia, miale ile ilileta mwanga, nikagundua nipo mapangoni. Miale ile ya moto  ni mwenge uliyoshikwa na wanaume wawili wakimwangazia njia mwanamke  mmoja aliyeonekana kupewa heshima zote.

             Kundi lile la watu watatu lilimfikia kiumbe mtukufu yule aliyekuwa akimulikiwa njia, ni yule mwanamke katiri aliye ghairisha kifo changu. Wanaume wale vijakazi hwakuwa Wangunjwasi niliowatambua kwa mionekano yao haswa idadi ya makovu waliyo nayo na  mavazi waliyoyavaa hawakuwa na alama za makovu maalumu ya kingunjwasi na walivalia mavazi sare na mimi. Lakini na wao walikuwa na ulemavu mbali mbali.

  Yule mnwanamke aliniaangalia kwa hasira ksha akaniambia;

“Piseletigo kweila   pwiyageropitoku –swa,  pyekeriso

Lukanelolukaku   pgi-pgo-pswairezimu, pumpu

Pumnpyaswilahegi   pgoti-pommkwiranyizapi ppesai”

( Nimekuokoa usibanikwe jikoni, kwa kusudi mojatu, uungane na hawa wenzako kunitengenezea jeshi, ninahitaji kuwapindua wazee wote wa hapa niwe kiongozi wao). Alipoweka nukta nilikuwa nimelowa tepe tepe kwa mate yake yanukayo.

               Nilimjibu kwa kumuomba animalizie kuniua kwani hapa nilipo nipo mguu mmoja hauaini mwingine umautini siwezi kujipigania mwenyewe nitampiganiaje mtu? Nilimwambia “Nashukuru kwa kuniongezea masaa ya kuishi naomba uniue.”


                Aliniita kwa jina jipyaJigani kisha akaiambia kwa kinjwasi ya kuwa bado nino uwezo, bado ninayo nafasi ya kujisimamia na kuishi tena kwa furaha, nikamkatalia kwanza siitwi Jigani safari hii nikiwa na mzuka hadi nikafanikiwa kukaa kitandani kwa sekunde kadhaa alafu nikadondoka, aliita kwa nguvu Powenzeo (jeshi) ghafla mamia kwa mamia ya wanajeshi wake wakamkusanyikia, wakatoa heshima zao wakamsujudia wakanyamaza kimya kusikiliza. Akaendelea kwa kusema “leo tumempata Jigan tuliyekuwa tunamsubiri sasa tayari kwa vita alinyamaza akaninyoshea kidole akawaambia wale wanajeshi “Jigan!!” wote walipig kelele za shangwe


 akaja pale kitandani kwangu akasema “ Umechaguliwa na Miungu yangu kuwa Jigani yaani mwanaume baada ya Malkia mimi kwenye serikali yangu ijayo lakini ni lazima ushiriki vita ya kuwaangusha wale wangunjwasi wazee ninao uwezo wa ajabu nitakurudishia viungo vyako vyote huwa nafanya hivyo nikiwahitaji wanajeshi wangu waende vitani ila wewwe Jigani nitakupatia milele.


                   Alipomaliza kuongea hivyo, nilikuwa na moyo mwepesi kumkubalia kwani viungo vyangu vyote vilivyopotea vilinirudi kasoro nywele, nilisimama kijasiri nikaonesha kichwani kama mtu anayeuliza huku vipi? Nywele zikaanza kuchomoza toka kushoto kwenda kulioa zikiwa kati kati ya kichwa kwenda kulia mamia ya wanajeshi walitenganishwa kulia na kushoto tena Joka likapita juu yao. Moja kwa moja likatujia mimi na yule mwanamke kwa hasira kuu likatuangalia.


                 Na hapo ndipo niliposhtuka toka usingizini na kupiga ukelele hadi msimamizi wa mtihani akashtuka na wanafunzi wenzangu wakaniangalia. Kamwe sitoisahau ndoto hii ya kutisha niliyoiota ndani ya chumba cha mtihani wa kidato cha nne kwennye somo la Hisabati

Mwisho.


Ndoto ya kutisha... Sehemu ya tatu.

 3


Ndoto ya kutisha

SEHEMU YA TATU.



 Psevejicho-kudopto           pyave                                                                                              

Psevejicho- kudopto            pyave

(Tu wajinga tumekosa)         (sisi)

 

Pitukubashite-piziro               petee

Pitukubashite-piziro                petee

(tunaomba tusamehe)            (wote)

 

Pjigijigi –patuko                        pisele

Pjigijigi –patuko                        pisele

( Ewe wetu mtukufu)               (Mungu)

 

Fahamu ziliponirudi, nilihisi maumivu makali mno usoni kwangu, yaani maumivu yasiyoelezeka kwa jicho moja nililobaki nalo, nililitambuausiku ulishaingia na nikaliona kundi la wanawake wangunjwasi likiimba, ni wakina mama wa makamo wamenizungukuka wakiwa kama walivyozaliwa. Miili yao inatisha, nilitumia mwanga hafifu wa mbalamwezi kuwaangalia lakini nilikuja kugundua kuwa walikuwa na michubuko na makovu ya aina mbali mbali kwenye robo tatu ya miili yao kama ilivyoikuwa kwangu pia.

                 Walipogundua nimezinduka waliacha kuimba wakawa wanaomboleza kwa chini chini mwishowe nikanyamaza kabisa kisha wanawake wawili wakajongea katikati ya duara nilipolazwa. Mmoja akakaa upande wangu wa kuume mwingine upande wa kushoto pale chini nilipolala. Kisha mbibi mmoja akatusogelea akatumwagia vitu vilivyo katika hali ya unga unga ambavyo viliniuma sana vilipoingia kwenye vidonda haswa kidonda cha jicho. Alipomaliza kutumwagia akawaamuru wale wanawak e wasimame, halafu akawapa visu vidogo kila mmoja kisha akawaambi kwa kinjwasi kuwa ili tambiko la kumzuia Joka kuwauwa wao litimie ni lazima wao kwa mikono yao waniue mimi.


                      Nilijikuta maumivu yamekata, nikaanza kuomba kimoyo moyo, nikiwa kati kati ya sala mwanamke mmoja aliyararua mavazi yangu nami nikawa kama wao, kisha kwa gadhabu akanikata viungo vyangu vya siri, nilipata maumivu ambayo nilijihoji kwanini asingeniua kabisa, halafu kwa kwa kile kisu kinachovuja damu damu yangu alinichana shavuni. “aaahgh!” nililalamika yule mwanamke alimalizia kwa kunidunga kisu kwenye kiganja changu cha mkono w a kushoto.


                Nilihagaika pale chini nisipate msaada zaidi ya makofi ya shangwe yaliyowatoka wakina mama walionizunguka huku nikishuhudia mmoja akizitafuna sehemu zangu nyeti, wengine wakimchochea yule mwanamke mwingine animalize. Maumivu yalitawala mwili wangu kuanzia kwenye ncha ya unywele hadi unyayoni. Huyu mwanamke wa pili alikuwa na sura ya kikatili zaidi na alipoonesha kuniinamia anishughulikie wote walishangilia, aliponisogelea zaidi wote walinyamaza wakisubiria kwa hamu kuona kifuatacho.


             Nilishukuru mungu kwa muda wote niliokuwa aridhini nikamshukuru na babu yangu mzee Kidasi kwa kunilea vema na kunifundisha kuwinda ambapo leo Swala amenifikisha hapa, hapa nilipo. Nikawakumbuka wanakijiji wenzangu na marafiki zangu waliopo Mg’etta ambao bila shaka watakuwa wananitafuta kwani sio kawaida yangu kuwinda mpaka usik ofu. Masikini mzee kidasi wangu, nilishangaa jicho langu nasubiri kifuatacho.


              Ghafla nikasikia kelele za shangwe nisijue linaloendelea, nilipojaribu kufungua jicho niliuona mguu wangu ukiwa umetengana nami kiha nikakiona kisu kinanijia moyoni, ila alipofikisha kifuani alikilaza kisu baada 

ya kunichoma. Niliganda kwa muda. Wote walishangilia kisha kile kibibi kikasema pingingoswera pswira pshaka shenme mingizi( tumuacheni halpo afe taratibu, kesho tuifate nyama yetu.) wote waliafiki wakatawanyika.


                               #########################################


      “Uwwwwuuuuuuuuuu!!” Ni sauti za umbwa mwitu nilizo zisikiaa baada ya kuzinduka kabla sijazimia kwa kitambo. “ Uwuuuuu!!” sauti ziliendelea huku upepo wa baridi ukivuma taratibu uhuuuu! Uhuuuu! Taratibu pia nikaanza kuhisi maumivu ambayo nilkikuwa siyasikii kutokana na kupitiliza kwake. Nikajifanyia tathimini fupi ya mwili wangu nikagundua sina jicho, sina mguu sina sehemu za siri, sina vidole saba vya mikononi sina nywele, sina meno ya mbele sina sikio la kulia hakuna hata kiungo kimoja kilichopo mahali pale ina maanisha vyote walikula hadi nywele.


               Nikaendelea kujitathimini, nikatambua mwili wangu ni vidonda vitupu, ukiacha sehemu ambazo nimekatwa viungo, shavuni mimechanwa, makalioni nimetobolewa mikononi nimechorwa reli kwa visu mguu mmoja nao uliobaki umetobolewa tobolewa vya kutosha pia kwenye paji la uso nina michaniko ya kila aina. Nililia sana nililia kwa uchungu nililia kwa sauti. Ni kama kilio change kilisikika punde mtu akatokea ni Mgunjwasi, mwanamke aliyeshika kisuu mkononi. Kwa hasira nilimlaani nikamtukana yeyena jamii yake ili animalize vizuri, kwani hali niliyokuwa nayo ni heri umauti.na kuwa chekundu kutokan na wingi wa damu nyingi iliyonitoka. Sijui kama niulimuona vizuri au la! Kwani uoni wangu haswa kwa jicho moja ulizidi kuwa mtihani, sekunde hata sekunde ila nilimuona yule mwanamke wa pili mwenye sura ya kikatili ambaye alipopewa nafasi ya kuniua alikilaza kisu kifuani kwangu badala ya kunichoma aniue huku wenzake wakiwa hawana habari kutokana na giza. Akiwa amenikanyaga kifuani alinipiga mateke mawili kichwani, ndipo nilipozimia.


            Ingawa nilikuwa natamka maneno kama mtoto anaye jifunza kuonge lakini adhima yangu ilifanikiwa, yule mwanamama alipandwa na hasira akanijia na kunirukia kwa miguu yake kifuani, zikanitoka damu nyingi sana kifuani hadi kufikia sasa kile kipande cha aridhi niliyolala kiligeuka

Ndoto ya kutisha.... Sehemu ya pili

.. 2



Ndoto ya kutisha

Sehemu ya pili


SEHEMU YA PILI

Kishindo changu aridhini kilimshitua  Joka kubwa Iililolojikunja pembeni ya njia tuliyokuwa tunapita. Fysaa Joka lilijichanua likaziba njia yote. Mimi niliyekuwa upande wa mkia nilipigwa naule mkia ulioniusogeza  ukanisogeza umbali wa miguu kumi na mitano  wale wawili waliokuwa upande wa kichwa wakangaliana uso kwa uso na lile joka.

              Nilipokuwa nnanyanyuka nilipodondoshwa na Joka ili nianze kukata mbuga sikuwaona wale wangunjwasi wawili waliokuwa wakiangaliana na Jokai la niligundua vishindo vya mate na Joka lilipotua aridhini nilikimbia eneo la tukio kwa mwendo wa mwanga huku nikikubaliana na maeno ya wahenga waliposema mambo mazuri hutokana na mabaya

               Baada yam bio za mwendo mfupi katika eneo refu nilianza kuhisi maumivu mgongoni, ndipo niligundua kuwa ninabubujikwa na damu nyingi sana pale nilipopigwa na Joka nilipogeuka nyuma nilikuwa nimezitiririsha njia nzima na kuacha michirizi ya damu.  Michirizi ambayo iliwasaidia wale aWangunjwasi wengine wanifatilie kwa urahisi kwani kabla sijaugulia kidonda changu cha mgongoni niliwaona kwa mbali wakinijia kwa hasira wakiongozwa na yule kiongozi wao niliye bahatika kumuona paji la uso na macho akiruka kwani walikuwa wanatokea kwenye kajibonde.

               Nilipoangalia huku na huko hamna pa kutokea, Mungu si athumani, nikaliona shimo. Haraka nikakata shauri la kujificha humo. Lakini kadri walivyozidi kuja hofu ilinizidi,  ilinibidi nitoke ndani ya shimo kwani nilijihisi siko salama mule nilipogeuka nizianze mbio nililiona shimo lingine nikalifata. Hili lilikuwa kubwazaidi

                Ndiposa niliingia kwenye lile shimo nijifiche ila sasa ndo’ nagundua sauti ya vuu! Lilikuwa ni jiwe kubwa lililotupwa ndani ya shimo nililo jificha, nami nisijue nikakimbia sasa nimejikuta nina vidonda utosini na maeneo mengine ambayo siyahisi uso wangu umepambwa na michirizi miyekundu mingi inayoendelea kushuka kama maporomoko ya maji ya Udizungwa.

                Sasa turudikwa yule Mkwiranyinza aliyekuwa akinihoji maswali ya hapa na pale  kiukali sana. Huku akinilaumu mimi kuwa sababu ya yeye kupoteza vijana wawili wachapakazi tena akidai kwamba kumezwa na Joka kwenye jamii yao ni ishara mbaya kwani Joka lile umeza watu wa jinsia mbili tofauti. Hivyo basi kama Joka amewameza wale vijana wa kiume ni ishara kwamba atawatafuta hata wake zao apate kuwameza.

                    Mwili wangu ulikuwa umefadhaika sana mambo yote niliyasikia lakini nilishindwa hata kutingisha kope cha zaidi niliangalia mbele tu ambapo macho yangu yaligongana na kifua cha Mkwiranyiza ambacho kilikuwa na makovu  ya mishale mingi iliyoingia pale. Mkwiranyizwa  alivyokuwa anaongea kwa ghadhabu kuu juu yangu , asijue  jambo baya la kunipa kama adhabu itakayonipasa. Ghafla yule kiongozi mfupi wa porini alinisogelea mkononi akiwa ameshika chuma kilichochongoka mbele, ambacho kimewekwa motoni mpaka kimekuwa cha rangi ya machungwa. Chenye kutoa moshi, Kisha akajaribu kunichoma nacho machoni asifanikiwe kutokana na kimo chake.


                   Baada ya miruko kadhaa akilihusudu jicho langu Mkwiranyinza alimbeba na kumleta usawa wa kifua chake akimwangalizia kwangu. Kisha eneo zima la wangunjwasi lilisimama na kushitushwa kwa kelele niilizozitoa kwa maumivu ya kutolewa jicho langu la kulia kwachuma chenye moto. Nikapoteza fahamu.


 


 



NDOTO YA KUTISHA sehemu ya 1

 1


Ndoto ya kutisha.

SEHEMU YA KWANZA

Nilipo liona shimo kubwa zaidi sikujishauri mara mbili mbili, nilifata kshia nikajitumbukiza ndani bila kujali kilichomo ndani nilitumia sekunde kadhaa ku kuifikia sakafu ya shimo lile, kulikuwa na giza nene haijawahi tokea, nilishindwa hata kuviona viungo vyangu binafs. Hewa ilikuwa ni nzito sana, nilipapasa papasa nikagunduwa kuwa upande moja ulikuwa unaendelea yaani kama andaki, moyo ukiendelea kuruka mapigo, akili imesimama na macho hayafanyi kazi, nilisikia sauti ya vuuu ikivuma ghafla kimya kilinitawala halafu sikujuaa kinachoendelea

              Jina langu ni Rashidi Mbwana Kidas, nilijibu kwa sauti ya kukwama kwama wkati yule Mkwiranyinza yaani mkuu wa wazee akiendelea kunihoji pia fahamu zangu zilikua zikinirudi taratibu taratibu hadi pale nilipokuja kugundua kuwa nimerudi tena mikononi mwa Wangunjwasi watu ambao wanakula nyama za binadamu wenzao. Mapema asubuhi  ya leo nilikuwa porini nikiwinda nijipatie kitoweo na kwa mbali nilipomuona  swala aliyenona nilimlenga na mshale, kituuu! Tumboni kwa kawaida huwaga sikosei.

 Ila kabla swala hajadondoka chini alipigwa na rungu lenye ncha tofauti tofauti tena lile rungu lina visu vya chuma  pande mbili za kupigia. Nililistaajabu lile rungu nikashindwa kulitolea majibu hata babu yangu mzee Kidasi aliyemiliki maarungu mengi kuliko mtu yeyote kijijini kwetu Mng’ta hakuwahi kuwa na rungu la aina hiyo yaani halielezeki. nikajishauri atakuwa ni mwindaji mwenzangu ngoja nisoge tukagawane nyama. Nilipofika swala alipo sikuamini Macho yangu hawa ni binadamu au?”  Nilijihoji.

                 Kwa upande wa uso walikuwa wana macho makubwavyenye viini vyekundu, macho yenye nyusi chache. zilizo onekana zimenyofolewa kwani vinaacha vidonda ambayvyo damu yake iliyoganda  inaacha alama nyekundu juu ya vidonda, wanapua kubwa zenye matunndu ya kutosha kupitisha mdomo wa chupa ya soda na nafasi ya kidole kimoja ikabaki

 Midomo yao ni mipana yenye meno yaliyo achana takribani sentimenta mbili unusu kutoka kwenye mjino hadi mjino tena miisho ya midomo yao imechanika chanika harafu ina rangi nyeupe kama vifaranga vya kuku ndimi zao nyembamba ndefu nyekundu zilizo chanika chanika yote tisa kumi midomo yao ilitoa harufu kali iliyonipa kizungu zungu kwani muda wote wao wana kenua. Watu hawa hawaongei Kiswahili wanaongea kwa kinjwasi lakini uwezo  wa ajabu ulinijia nikawa nawajibu kwa kinjwasi pia. Wangunjwasi wapatao sita walinizunguka mimi na yule swala wakiniangalia kwa dharau kisha mmoja ambaye ni mfupialiyeonekana kuwa kiongozi alinifata  akaanza kunihoji;

MGUNJWASI: Pesechuki pesika?  Pwipenshupata (umefata nini kwenye  himaya yetu?)

MIMI: Pswitanjei (Nisamehe)

MGUNJWASI: Potatakisepwetikwapa (umetokea wapi?)

MIMI: Pistwanjei (Nisamehe)

 MGUNJWASI:Pwipwi pistwasnjewo pisgoteda (Mbebeni atasamehewa nyumbani)

Aliwaamuru wenzake wanibebe nikibubujika na machozi nilizidi kumuomba msamaha lakini nilikuwa nampigia mbuzi gitaa.

            Yeye aliye kiongozi alitangulia na mmoja kuondoka akifuatiwa na mwingine mmoja aliyeonekana ‘bodguard’  ingawa ndiye mzee kati ya wote. Kisha wawili walimbeba swala na wawili wengine walinibeba mimi kutokana na uzito wangu kundi hili la mwisho lilikuwa linatembea taratibu taratibu kwa sababu hiyo katika kuhangaika kwangu nilifanikiwa kujirusha toka mabegani na wale wenzao waliokuwa mbele hawakuyajua yanayoendelea nyuma kwani walituacha umbali kidogo.

 

 

 


 

 love is all Given and found,🌹 It's all around,πŸ₯° It's hard to tell about,😍 Easy to show,🀩 One sure thing when you feel it You kn...