Tuesday, December 3, 2024

MlSS EVIL




 NILIMKOMESHA MISS EVIL.


      Semeni ndo' jina langu, jina nililopewa na wazazi wangu. Oysterbay ndo' pahali ninapoishi kwa sasa. Mume wangu alichaguliwa na umoja wa mataifa kwenda Haiti๐Ÿ‡ญ๐Ÿ‡น kutuliza fujo na ghasia za Mahaba mia wa huko Haiti kwahiyo nyumbani nipo mie tu pamoja na wanangu wawili Evla mwenye miaka sita na Pedro mwenye miaka miwili.

       Mbali na uwepo wetu sie watatu nyumbani tunao Nyau ๐Ÿˆ๐Ÿ˜ปwawili kidume mwite Marioo na kijike mwite Selenna. Tumejituliza ndani ya hii nyumba yetu mpya tuliyohamia wiki mbili kabla mume wangu hajaenda Haiti kulinda Amani (Niombeeni ๐Ÿ›๐Ÿ“ฟwangu wa roho๐Ÿ‘ฉ‍❤️‍๐Ÿ‘จ๐Ÿ’ž arejee salama salimini)

       Sikilizeni kisa changu ninachowaletea lazima kiwafunde ujasiri wacheni woga wenu nyie! Baada ya kuhamia nyumba yetu mpya wiki mbili zilopita nilizoeana na majirani wachache wakiwemo Bibi Pili, Dada Maimuna na Bwana Heri Hamduni. Tunaishi private private ingawaje twashirikiana.

Takataka zangu za Nyumba (Waste disposal) Zilijaa full tank, nikaisubiria Gari ya taka iwasili. Mungu mzuri ilipowasili mie Semeni nilijaza viroba vyangu na kuelekea kuvitupa ndani ya Gari ya taka.๐Ÿ—‘️๐ŸŽ️

    "Evla na Pedro jiandaeni tutoke twende Shopping Dears!"  Niliwaambia wanangu waliofurahia ule mtoko maana walijua huko hawatakosa vipipi ๐Ÿญvya bure, tu lce cream ๐Ÿฆ๐Ÿจtwa bure na tududu dudu twa kucheza ๐Ÿฆฅ๐Ÿฆœwatoto๐Ÿฐ๐Ÿฆ„๐Ÿ‰๐Ÿฆ–๐Ÿฆ•๐ŸŠ๐Ÿ๐Ÿ‡. Tulitoka tukaenda zetu Shopper kujumua jumua Viwalo๐Ÿ‘’๐Ÿ‘•๐Ÿ‘–๐Ÿ‘— na viatu ๐Ÿ‘ก๐Ÿ‘ž๐Ÿฅฟpamoja na mahitaji mengine ya nyumbani.

     Baada ya manunuzi na kuufurahia Mji wa Kariakoo tulirejea Oysterbay Nyumbani. Ilikua ni mchana mzuri wa Jua la saa sita๐ŸŒฅ️ Jua lilitupa hamu ya kunywa vitu soft baridi๐ŸงŠ๐Ÿธ๐Ÿน. Mie na wanangu Evla na Pedro tulipofika nyumbani tulipigwa butwaa๐Ÿ˜ฑkukuta mazingira yanatisha, hayatamaniki. Ubaraza wangu wote ulijaa takataka nyingi zilizooza na kuharibika. Kulikua na pedi zenye mikojo na vinyesi vya watoto tena zilinuka. Mikate iliyokooza,mifupa na shombo la Samaki na Dagaa ilinuka baya zaidi mlango wangu wa Sebule niliosahau kuufunga kwa bahati mbaya ulifunguliwa na Sebule ilitisha kwa wingi wa takataka, karatasi, pedi, mifupa ya samaki, makopo ya biadhaa za viwandani na kadhalika. Niliogopa na kushangaa 

      "Mama Nyumba inanuka."Evla  mwanangu mkubwa aliongea.

    "It's ok Daring, nitaisafisha " Nilimjibu mwanangu Evla aliyeiziba Pua kwa kutumia madole ya mkono wake. Pedro wangu alijificha mgongoni asiuone uchafu ule. Niliwakuta Nyau wangu wameketi Sofani wakishangaa.

     "Mpuuzi gani amenifanyia hivi!?" Nilijiuliza haraka mie na wanangu tulitoka nje na kwendraa kujaribu kuhoji majirani ni mtu gani aliyelitengeneza jambo Ovu kama Lile!?

     "Pole sana Dear! "Bibi Pili alinifariji nilipoenda kwake kuuliza

     "Aliyekuchafulia nyumba si mwingine bali ni Miss Evil, yule Dada yupo very wicked, anachukiza." Nilimsikiliza Bibi Pili.
    
    "Yule Dada ni mchawi tena mwogope kila mtu hapa Oysterbay anamwogopa , hasogelewi." Bado nilimsikiliza.

      "Ana kawaida Moja ya kunusa nusa na kupeleleza ajue ni nani aliyehama au aliyehamia nyumba mpya na baada ya ugunduzi wake atafanya uovu wa kumwaga Takataka ndani ya nyumba ya huyo aliyehama au aliyehama." Bibi Pili alinisimulia.

      "Nakusihi usijaribu kumsogeleea sababu huyo ni Mlozi na mrogaji. Ukimkorofisha anakuroga unageuka na kuwa kipofu au kiziwi." Bibi Pili mwenye kadirio la miaka themanini alionesha hofu yake.

     "Bibi jambo hili niachie mimi wewe mwenyewe utakuja kunishukuru mara baada ya kumfanyizia huyo Miss EVIL." Niliongea pasina kupepesa macho.

     "Mjukuu wangu we huogopi!?" Alitia hofu

     "Hadi asame!" Niliongeza Msamiati.

     "Ubaya Ubwela... Kisa mkasa." Nilifanya kuondoka nyumbani kwa Bibi Pili mtimani nimeshiba mahasira yenye hasara.

    "Huyu Miss Evil ndo' nani atakaye kumjua mke wa Mwanajeshimpiganaji?" Niliongea pekee yangu.

      "Lazima nimfunde ili siku nyingine awaheshimu wenyeji na wageni!" Nilijiambia

       "Uchawi ndio Nini? Ina maana mtu anakuja kuchafua mazingira ya wengine ili tu aogopwe kwa sababu ni mchawi?" Nilijiuliza.

     "Sasa ngoja ataniheshimu." Nilitoa kiapo mie Semeni nlikatoka na kwenda kununua magunia mwawili makubwa yaliyoshiba. Baada ya kununua yale magunia nikaanza kupita nyumba moja baada ya nyingine kuhoji jirani zangu:

     "Nipe vinyesi vyote, vinyesi vya Umbwa, Nyau, Ng'ombe, Nguruwe na hata kama ni vya watoto wadogo nipeni" Nilidai. Majirani wakishangaa lakini pasina kuhoji walianza kunipa mioyoni mwao walihisi nimerukwa na akili..... Sio kwa hasira zile nilizotembea nazo.

     "Nipeni tafadhali, nipeni. Baada ya dakika Harobaini na Tano ninaomba mje nyumbani kwangu muone ubaya ninaotaka kumtendea Miss Evil " Walipolisikia jina la Miss Evil, Mchawi wanayemeuogopa pale Oysterbay. Yule mchawi ambaye hajaolewa zaidi ya kuishi Single sister walistaajabu na tena walitamani kujua nini kinaenda kuiva huko?!

      Mie Semeni nikayapakia magunia yangu mawili yaliyojaa vinyesi kunako Toroli Kisha nikayaburuta hadi nyumbani kwangu, huko nilijua mie mwenyewe ninaenda kufanya jambo Gani?
 
       Babaye Evla alinifunda kutengeneza Baruti za kurusha kwa mikono kupitia ujuzi ule nikafanya hima kufungasha vinyesi ndani ya mifuko midogo yenye umbo la duara kisha vile vifungasho vyenye kinyesi na umbo la Baruti nikaviweka ndani ya Magunia na kuvipakia ndani yaToroli muda si mreefu majirani wakaitana na kutimia ishirini na wote wakanifuata nyumbani wakiwa na shauku ya kutaka kujua naelekea kumtendea nini adui wa wageni Miss Evil.

      "Twendeni." Niliwaamuru wakanifuata kama Umbwa na mkia wake wamejaa shauku na kiu ya kutaka kujua nini naekekea kumtendea Miss Evil yaani ni ubaya na ubwella. Nyumba ya Miss Evil ilikua ni ya sita kutoka nyumba yangu, tulifika nyumbani kwake.

    'Knock! Knock! Knock' Nilibisha hodi mara tatu nyumba ya Miss Evil bila woga bila wasiwasi, majirani kundi zima walitazama  lango la Miss Evil. Alifungua mlango hapo ndipo akakutana na macho yangu. Mie nilitegemea kukutana na kipipa furani chenye sura ya Simba dume, kumbe wapi! Kile chifupi chikondefu ndicho kinachoogopwa na watu wote pale mjini.๐Ÿ˜†๐Ÿ˜…

       "Eeh! Bibi naomba maelezo unieleze kwanini umefanya uamuzi wa kwenda kumwaga takataka zako barazani na sebuleni kwangu?" Nilimuuliza yule chifupi cha Umbwa.

       "Sasa kama nimemwaga barazani na sebuleni kwako unataka kunifanya Nini? Aliniuliza kijeuri akiibetua midomo yake.

    "Umepata Nini chenye faida baada ya kumwaga takataka zako nyumbani kwangu na kuichafua nyumba yangu?" Nilihoji.

      "Ndio utamaduni wangu lazima Kila mhamiaji aonje taka na Kila mgeni lazima aonje taka." Alijibu kipumbavu watu wakamshsngaa.

     "Wewe pia unahamu ya kuonja taka?" Nilimuuliza moyo ukiniambia mrukie huyo, mponde huyo hadi asagike mifupa. Uzuri roho iliniambia mwambia mwaibishe apate onyo na fundo. Hakunijibu, basi nikamvamia na kumsukumia pembeni akaanguka chini puu! Kama gunia la mama, Nikaingia sebuleni kwake nikayatoa yale mabomu ya baruti kunako ile mifuko miwili mkubwa niliyokua nayo. Nikaanza kurusha yake mabomu ya baruti yaliyowaogipesha watuwote pamoja na Miss Evil.

     Sikukomea hapo Bado tu nikiendelea kuichafua nyumba yake kwa milipuko baruti zenye vinyesi: jiko lake lilichafuka,masofa yake yalichafuka na tena yaliunguavpasina kuteketea, Sebule yake ilitapakaa vinyesi ilitisha na kuogopesha. Nilitamani kufanya umafia ndani ya chumba anacholala sema roho iliniambia Sasa tosha. Nikatoka nje na kuwakuta majirani wote a Moja na Miss Evil wanaogopa na kutetemeka. Mkononi nilishika bomu lenye baruti yenye kinyesi nikamsogelea Miss Evil aliyeanguka pale chini akishangaa kisha nikakwambia.

     "Huu ni mwanzo, lwapo nitakuja kusikia kesi yoyote ile inayohusu nyumba ya mgeni au mhamiaji, imetibuliwa na kuchafuliwa na uchafu wako ninakuapia nitayazoa mapipa ya vinyesi chooni nije nipakaze kuta za Nyumba yako. Mpuuzi mdogo weye" Nilimnyoshea madole na hasira zilinikamata. 

Alitetemekatetemeka, akashindwa kuongea tena jeuri zake.

      "Ita Polisi kama unataka" Nilimwambia Bado alikua akitetemeka. Nikaondoka nyumbani kwa mwovu yule kadamnasi ya watu walinisindikiza, wakipiga makofi, vifijo, nderemo na shangwe.

      "Semeni mjukuu wangu wewe ni Jasiri." Bibi Pili alinipongeza.

       "Kwangu wewe ni Legendary hajapatikana mtu mwenye moyo wa kishujaa kama wewe." Bibi Pili aliongea tena.

      "Umemuangusha Goliath yule lnzi aliyepigwa kwa kinyesi." Bibi Pili aliichekesha hadhira. Tuliondoka eneo la Miss Evil tukiwa ni wenye wingi wa furaha. 

Nakuambieni huu ni mwaka wa pili Miss Evil hajapata kufanya upuuzi aliozoea kuwafanyia wageni. Ametulia kama sio yeye aliyekua akiogopwa kwa Ulozi.

...................

TCHAO  ๐Ÿ–️๐Ÿฆ‡๐Ÿฆ‰๐Ÿพ๐ŸŽƒ๐ŸŽญ



No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...