BAADA YA KUMFUKUZA 🏃♀️🏃♂️MKE WANGU WA NDOA MAMA NA DADA YANGU WAKAKIHARIBIU💀 KIZAZI🩸 CHANGU.
"Hamza!" Mama aliniita kwenye Rununu yake📲" Nilisikia sauti ya kwikwi😿 Ma. Alikua akimwaga chozi.
"Naam, Ma. Mbona kama nasikia unalia" 🥲Nilimuuliza moyoni nimejaa maswali kibao.⁉️
"Acha nilie my son. Mkeo huyu ni shetani mkubwa, shetani Ibilisi 🦹♀️👿kwa haya anitendeayo nimevumilia miaka yote lakini nimeona mvumilivu ninakula mbovu, Bora nikuambie" Safari hii alitoa kilio kikuu, moyo wangu ulinidunda uchungu ulinivaa kusikia kilio cha Mama mpenzi.
"Tatizo Nini Ma, acha kulia."😤😠 Niliongea simuni.📱
"Sijalia miaka mingi tangu baba yako achukuliwe na Mungu🪦⚰️, Leo acha nilie tu sababu Mkeo ananinyanyasa, ananitesa, ananishusha kwa matukano baya zaidi ananidunda mwili wangu umejaa makovu sema nashindwa kukwambia mwanangu. iiiiiiii😿iiiiiiii uwiii 🥲." Alipaza sauti ya kilio.
"Nini👺? Jasimini anakutesa, anakupiga, anakunyanyasa" Nilipaza sauti 🗣️safari hii hasira zilianza kuninyanyasa.
"Nitafanya nini mwanangu zaidi ya kuvumilia, Leo tu ameniambia niondoke nyumbani hapa, ananifukuza na kunitimua ndani ya nyumba uliyojenga mwanangu,🏘️ ananifukuza kama vile ni yeye aliyejenga nyumba hii" Ma. Alinisimulia.
"Nasema haiwezekani Ma, haiwezekani..... Ngoja nije nimuoneshe kwamba anapaswa kukuheshimu, mpumbavu mkubwa huyo." Nilibwata nikiwa Ofisini✍️ kwangu hima hima nikachukua funguo ya Prado 🚗yangu nikaikoki na kutimua vumbi moja kwa moja hadi Oysterbay nyumbani moyoni nikimlaani mke wangu.👩❤️👨
"Mpumbavu huyu hajui jinsi nilivyoishi na mama yangu Kwa tabu, shida na mahangaiko."
"Mama alikua akiuza mbogamboga, nyanya na vitunguu ili Mimi nisome na nimesoma kwa tabu hadi kupata Diploma yangu ya Sheria ⚖️👨⚖️alafu mjinga yule anampiga na kumnyanyasa Mama yangu."Nilivurugwa.
"Leo atanikoma, ama zangu ama zake ni mwendo wa kutimuliwa tu."Nilibwata ndani ya Gari nikaikimbiza ovyo Hadi masikani huko mlinzi wa geti alinifungulia haraka nikaenda moja kwa moja hadi sebuleni.
"Yu wapi huyo mpuuzi anayekunyanyasa Mamangu."Nilifoka.👺
"Amelala chumbani kwake😴, Ma. Alikua Analia Hadi kamasi zilimchuruza.😪 Nikaenda chumbani alipolala mke wangu nikaubamiza mlango mbaaaaa Mama Jasimini mke niliyezaa naye watoto wawili:Jasimini na Ali alishituka baada ya kusikia sauti kuu ya mlango ule.
"Twende sebuleni,"Nilimvamia pale kitandani nikamvuta mkono wake kinguvu karibia niutengue ukavunjika Nikamburuta na kumtoa nje kuelekea barazani nilipomuacha Mama.
"Kuna Nini Baba Jasimini? Kuna Nini?" Sikuisikiliza sauti yake. Nikamsukumia sebuleni pale Mama alipokua Analia Kwa uchungu.
"Bibi Mama mkwe mbona unalia umepatwa na Nini? Mke wangu alimuuliza Mama yangu maana alionekana kushituliwa na kilio cha Mama.
"Unajifanya haujui Mama Jasimini yaani kila siku unanitukana, unanipiga na kuniambia niondoke kwenye nyumba aliyojenga mwanangu Hamza."Ma. Aliongea akilia.
"Mimi!!? Mimi ni wa kukupiga 💪wewe, kukutukana na kukufukuza." Mama Jasimini aliongea kwa mshangao na mshituko. Nilisikiliza tu wakibishana.
"Sasa kumbe! unataka kuniua ndani ya nyumba ya mwanangu wa kumzaa." Mama aliongea Kwa uchungu mzito.
"Bibi Mama mkwe!!" 🤯Mama Jasimini bado alipigwa na butwaa.
"Naomba uingie chumbani na ubebe kila kilicho chako Kisha uondoke."🛅🧳🛍️ Nilimwambia Mama Jasimini kwa hasira.
"Baba Jasimini Bibi Mama mkwe haongei ukweli, hakuna jambo kama hilo mimi kumtenda." Mama Jasimini alijitetea.
"Mama yangu hawezi kudanganya, Mama amenilea katika tabu, shida, na maumivu makuu leo hii kimburukutu wewe unampiga na kutaka kumuua." Nilimfokea Mama Jasimini.
"Siwezi kufanya jambo kama hilo Mume wangu, wallah!! Bilali! Ninakuapia."Alijitetea machozi yakitaka kumdondoka lakini mie sikusikiliza, kwanza yeye sio damu yangu na sio ndugu yangu kuna baya gani nikimtimua?❓
"Kabebe nguo zako zote utoweke." Nilimsukumia chumbani.
"Nisikilize Baba Jasimini nisikilize Dear!"Machozi yalimdondoka.
"Namsikiliza Mama yangu sikusikilizi wewe mpumbavu." Nilipoona anachelewa kuingia chumbani kubeba vigagula vyake nikaingia Mimi na kutoa kila kila chake na kumfukuzia nje kama Jibwa🐕 lisilotakiwa nyumbani
"Nisikilize Baba Jasimini naomba nipe nafasi nijieleze."Lakini wapi sikumtetea niliegemea upande wa Mama tu.
"Ondoka na Tena ondoka nyumbani kwangu,"Niligeuka mnyama mwenye hasira.🐉🦍🦁
"Basi nipe nafasi ya kuondoka na wanangu."z👨👦 Alilia.
"Neva eva, hauna watoto hapa. Watoto Hawa ni wa kwangu ulikuja mikono mitupu na uondoke mikonoz🙌 mitupu." Nilikua namsukuma aende nje ya Geti, baada ya kumtoa nje nikamuacha pale Analialia na kugonga geti ahurumiwe.⛩️ Sikujali. (I didn't care)
--------*****--------*****
Mama Jasmin hakukata tamaa kila siku akawa ni mtu ni wa kuja Ofisini ✍️akilia kwa uchungu akidai hajawai kumtendea Mamangu ubaya, aliomba aonane na wanangu. Lakini bado sikumpa nafasi hiyo. Basi akafanya kwenda ustawi wa jamii kudai haki ya kuwaona watoto tuliozaa pamoja, Hilo nalo sikulitaka kabisa na kwa vile mie ni Hakimu 👨⚖️na pia nina pesa nyingi 🤑🪙💲💰nikatoa rushwa kubwa kubwa wamnyime haki hiyo, kwa asilimia kubwa wale watu wa ustawi walipokea rushwa na kumnyima ile haki ya kuwaona watoto.
Mwanamke hakuchoka bado tu aliendelea kunisumbua Ofisini na nyumbani. Nikacheka kwa ule usumbufu wake nikaanza kumtisha kwa kumwambia iwapo ataendelea kunisumbua nitamfanyia 🥷kitu kibaya ambacho hatokuja kukisahau maishani mwake. Akanywea na kuogopa..... Nilidhamiria kumwaribia maisha yake sababu pesa ninazo na cheo ninacho.
Baada ya miezi sita kupita baada ya kuachana na mke wangu Dada yangu Aisha alihamia nyumbani kwangu maana alikua amegombana na Mume wake na Taraka juu aliachiwa. 📝📜Aisha hakuwa na pahali pa kukimbilia zaidi ya nyumbani kwangu akaambatana na Jumanne mwanaye mwenye umri wa miaka kumi na Mitano. Wakati huo wanangu hawakukoma kuniuliza kuhusu pahali alipokwenda mama yao, niliwajibu uongo nikawaambia Mama yenu hawapendi, amewakimbia, hawataki na pia hataki kabisa kuwasikia. Wanangu waliamini hivyo hivyo nilivyowadanganya.
Kwa vile Mimi ni mtu mwenye pesa zangu basi nikafanya kuwaajiri vijana wawili wawe wanamfuatilia mke wangu na kumchunguza:anafanya Nini?Anapanga mpango gani? Anatembea na nani? Miaka ilivyozidi kwenda nilikuja kuambiwa tayari ameolewa hapo ndipo nilipopata mwanya wa kumwandalia Taraka. Akala Taraka yake na tena sikujali nilipokuja kuambiwa amejifungua mtoto wa kiume. kwani anafaida gani kwangu, ⁉️❓sikuona umuhimu wake.
-------------------------------
Nilikua ni mtu wa bize bize kazini, mtu wa kazi kazi.kama ningeliondoka saa kumi na moja Alfajiri basi ningerejea saa sita au saba usiku, muda huo ningeliwakuta watoto wangu wamelala, Mama na Dada yangu wamelala pia moyoni Nilifurahia nikijua kuwa familia yangu inaishi kwa furaha. Nilitembea na Ufunguo wangu wa nyumba, nirejeapo kutoka kazi ningelifungua mlango kwa Ufunguo wangu na niondokapo kurejea kazini ningelifunga kwa Ufunguo wangu. Mama na Dada pia walikua na funguo zao za akiba
Ilipita miaka Saba pasina mke niliyempa Taraka kunifuatilia. Siku moja nilijisikia kuumwa mwili💉🥵 wangu wote nikaaga Ofisini mapema yapata saa tatu usiku,🌆 nikaeleka nyumbani kwangu Tabata nipate kupumzika. Kama kawaida niliutumia Ufunguo wangu kuingia nyumbani kwangu nikalilaza Gari langu na kuelekea chumbani kwangu.
Ile napita karibu na mlango wa chumba cha Dadangu nikayasikia maongezi ya majibizano kati ya Mama na Dadangu, nikatega sikio nisikilize nini wanachobishaniana.
"Sophia nilikuambia lile tendo la kumfukuza Jasmin mke wa kaka yako lingelileta matatizo ni Bora tungelimwacha alee watoto wake."
"Lakini Mama hata wewe ulishiriki kusababisha Jasimini mke wa kaka Hamza afukuzwe nyumbani hapa."Dada alimjibu Mama.
"Kumbuka ni wewe ndiye uliyenishawishi nitunge uongo na kujifanya naigiza mbele ya kaka yako Ili kumpumbaza aamini kuwa Jasimini alikua ananipiga, ananitukana na kunidharau." Mama aliongea Mimi niliyekua nimetega sikio pale mlangoni nilishangaa maongezi yao.
"Sasa Mama ningelienda wapi ikiwa Mume wangu alinifukuza na pahali pa kukimbilia sikua napo zaidi ya nyumba ya kaka Hamza."Sophia Dadangu alimjibu Mama.
"Haya Sasa tuachane na hayo maji yashamwagika hayazoleki, ⛲embu niambiwe Sasa tunafanyaje kuhusu Ali mwana wa kaka yako? Je ataendelea kujinyea hivi hivi hadi lini? Tena la zaidi nimekuomba sana mchunge mwanao Riziki tendo la kufanya mapenzi na Aisha mwana wa kaka yako litasababisha majanga mazito ikiwemo kuharibu kizazi cha Aisha au kubeba mimba katika umri madogo."Uwii! Maongezi yao yalinipa Presha.😤🥶🥵
"Mama punguza lawama, Riziki alianza michezo ya ngono tangu akiwa Shule ya Boarding🏫 walimu walipomgundua wakapelekea afukuzwe Shule na Mimi kupewa Taraka na Mume wangu. Sasa Mama ningefanya Nini ikiwa sikuwa na pa kukimbilia zaidi ya hapa nyumbani kwa Kaka."Dada alijitetea.
"Nimesema tuachane na hiyo Topic yakuachwa na Mumeo, tujadiliane kuhusu hali mbaya ya Ali mwana wa kakayo kutokwa na choo kikubwa bila speed, 🚽mkanye Riziki kuendeleza mchezo huo pia muamishe Riziki ndani ya chumba alalacho na Ali, kumbuka Ali ni mtoto madogo mwenye umri wa miaka nane tu."Maneno ya Mama yalinifanya nianze kuona kizunguzungu na kuanguka.
"Nimemkanya Riziki mara ngapi wala asinisikie!?"
"Na Kaka yako akifahamu itakuaje??"
"Tutatunga uongo mama....." Sikutaka kuendelea kusikiliza maongezi yao nilikwishajua kuna kitu hakipo sawa pale nyumbani. Nikausukuma mlango wa chumba cha Dadangu nikaingia kwa fujo ile wananiona tu walishituka na Ili kutoonesha darili ya kwamba wameyasikia maongezi yao wakajifanya kuibadilisha Topic, wakaanza kujadiliana mambo mengine.
"Nielezeni vizuri kuhusu Mtoto wangu Ali na Dada yake Aisha." Nilipaza sauti, hawakuamini kama nilikwisha yasikia maongezi yao wakajitetea kwamba hawajui jambo lolote linaloendelea. Nikawabana sana Ili waongee ukweli wa mambo hatimaye mwisho wakajieleza. Mama akaeleza ukweli kwamba yeye na Dada walipanga njama mke wangu atimuliwe pale nyumbani kwangu Ili Dada aje aishi pale nyumbani maana Dada alipewa Taraka na mumewe kwahiyo hakuwa na pahali pa kukimbilia.
Wakaeleza Riziki mtoto wa Dada mwenye umri wa miaka kumi na Tisa umwingilia Aisha Binti mwenye miaka kumi na moja umbaka mwanangu Hadi aridhike na tena hatosheki umwingilia kinyume na maumbile mwanangu Ali ambaye tayari ameharibika anajinyea. We! Nilicharuka nikawa Mbogo mnyama wa porini nilitamani niwapige Dada na Mama yangu nilichofanya ni kuwafukuza pale nyumbani kwangu wote waondoke warudi kijijini. Hasira zilinipanda baada ya kujua kumbe mama na Dadangu walipanga njama chafu Ili nimfukuze mke wangu mpenzi wao waishi kama Malaika pale nyumbani kwangu. Moyo uliumia na kusikitika.
Nikafanya mpango wa kuwatafutia Madaktari wanangu. Mishipa ya haja kubwa ya Ali mwanangu iliregea na kusababisha kinyesi kiwe kinamtoka ovyo. Aisha mwanangu alikua kama teja la ngono kila alipokua ameketi peke yake alilia anataka mtu amwingilie wafanye ngono. Hali ile iliniumiza sana maana ukikaa nae tu angelilia mwanaume wa kusex nae inaonekana Riziki alimzoesha ule mchezo mchafu
Niliwaomba Madaktari 🥼🩺👨⚕️wanisaidie, nikatafuta wataalamna Wanasaikolojia. Loh! Masikini majuto yaliniandama.
Ikawa sasa ninautumia muda mwingi wa kukaa na wanangu, 🕐nilitamani kutafuta wasichana wa kazi lakini sikuwaamini kabisa, nilitamani kuacha kazi Ili niwe karibu na wanangu nikaona haitoshi wacha nimtafute Mama yao nimuombe turudiane. Mama yao niliyempa Taraka alikwisha olewa na mtu mwingine. Nilipompa taarifa juu ya kile kisa cha Mama na Dada Wala hakuumia au kusikitika alichosema yeye alisema: "Sasa Mimi nifanye nini kama watoto wameharibika basi pambana warejee kama zamani. Ulikataa katakata nije niwaone na kuwasabahi na sasa imepita miaka Saba ndo' unadai turudiane? Haiwezekani mie nina maisha yangu."
Kilio kilinitoka nilimpoteza mke mwema kwa ujinga wa kumsikiliza Mama yangu, Mama yangu na Dada wamekula njama na kushiriki kuniharibia kizazi changu. Masikini mimi ni Bora kama ningelimpa mke wangu Jasimini nafasi ya kujieleza kuhusu lile sakata lakini ubaya wake nilimsikiliza Mama yangu.
""""""""""""""""""""""""'""
TCHAO
🥲😥😢🤧😭
""""""""""'"""""""""""""""""
No comments:
Post a Comment