Friday, March 28, 2025

I love 💕 you Papa

 


Ninakumbuka mtoto yule alianza kama utani, kila niliporejea kutoka kazini nilimuona akiwa amesimama dirishani kwao yaani juu ya Horofa wanaloishi kisha akacheka kitoto toto, sikujali sana Kisha niliingia nyumbani kwangu Horofa ya pili nikamkuta mke wangu anapika na kupakua. Busu zito lilinipokea kwa furaha, akanikumbatia kama anavyonikumbatiaga Kila siku akanipokea makabrasha yangu kwenye brief case Kisha mke wangu akaniambia ' Pole na kazi Dady' Mie ufarijika na kumjibu 'Nimepoa Mamy'

      Naitwa Babiloni au kwa kifup niite 'Babi' Nimeajiriwa katika shirika la ndege Tanzania, mimi ni Lubani. Ninamke ambaye kwa Sasa ni mjamzito. Ni mama wa nyumbani hunipikia vinono na kunipakulia vinono vyenye Sukari na asali. Nimepanga apartment yangu   katika shirika la nyumba la Taifa (NHC) Horofa yangu ipo mita chache kutoka Horofa nyingine inayotazamana na niliyopanga hapo Kila siku mtoto wa jirani unichungulia, unipungia mkono, utabasamu na kucheka kwa furaha

  Tendo la yeye kunipungia mkono sio mara ya kwanza, kufanya mara kwa mara Sasa ni zaidi ya miezi mitatu tangu nimuone akiniona tu utabasamu, upunga mkono na kucheka kwa furaha. Moyoni nilijisemea ni utoto angali Bado mdogo kufahamu mengi siku zilizima na mpya zikazimuka maisha yakaendelea nilipotoka kazini, niliingia ndani kama kawaida  mke wangu Sarafina alinipokea akanipiga kiss la pole na kazi nami nilimrudishia lile la Asante Baby nimepoa akiisha kunipokea mizigo yangu mie huyo nikapitiliza juu ya mazingira ya Horofa Dirisha linalotazamana na Horofa anayosimama  yule mtoto, nikamuona akinipungia mkono na mimi nikampungia mkono akatabasamu, nikatabasamu pia kisha yule Malaika akacheka kwa furaha nikatoweka na kumuacha angali anatamani kuniangalia tena

     "Sarafina, nilimwita mama watoto aliyekua akikaangiza samaki mekoni

     "Abee! Baba watoto." Aliniitikia kwa furaha.

     "Njoo Mama." Nilimwitaji naye alikuja haraka, akakaa 
pembeni ya sofa nililoketi. Nikaanzisha maongezi.

    "Mke wangu nimekuita hapa nikueleze kuhusu mtoto wa Horofa inayofuata, Horofa inayotazamana na yetu."Sarafina mke wangu alinisikiliza.

   "Sifahamu huyu Malaika ana lengo Gani na mimi ni mwezi wa tatu Sasa  Kila nikirudi kazini au nikiwepo nyumbani nikitizama nje ya Dirisha ni lazima nimuone na yeye pia lazima anione Kisha atatabasamu na mimi pia nitatabasamu, atanipungua mkono na mimi vivyo hivyo Kisha kwa furaha yule Malaika atacheka. Kwanini ananifanyia hivyo?" Nilimuuliza mama kijacho wangu.

      "Mbona kawaida mume wangu, kawaida ya watoto, watoto wetu ni Malaika, upenda kujifunza." Mke wangu alinijibu.

   "Lakini Kila siku? Kawaida Gani hiyo?" Nilimuuliza kijingajinga.

     "Babi mume wangu je unahisi huyo mtoto anaubaya kama vile uchawi utotoni? Swali la Sarafina lilinishitua 

     "Hapana sijafikia kuwaza hivyo." Nilimjibu Sarafina mke wangu.

      "Basi elewa huo ni utoto wa watoto,watoto wanakupenda na wewe unatakiwa uwapende." Aliongea wingi.

    "Kweli mke wangu binafsi ninawapenda watoto tumwombe Mola atupe watoto wengi." Niliongea kwa furaha.

      "Ungelipenda tuwe na watoto wangapi? Safina alinitania.

       "Kumi na mbili." Nilitania pia.

        "Yesu! Thenashara!" alishangaa

        "Wa mwisho tutamwita Yuda msaliti." Nilitania.

      'Teh teh teh' Alicheka." Wa kwanza ataitwa Petro. Alitania tena"

    "Nitafurahia." Nilimwambia.

     "Embu ngoja nikimbilie mekoni mboga yaungua."Alisimama pale alipoketi na kuelekea mekoni kuendeleza mapishi.

            """""""""""''''''''''""""""""""
Usiku ulipoingia🌆 tulielekea kitandani🛏️ kujilaza basi katikati ya usingizi niliota ndoto 💭nikamuona yule mtoto tukiwa wawili pekee ndani ya msitu twakimbizana kwa kujificha (Hide and seek). 🏃🏃‍♀️Mara tulionekana tukichuma matunda tukayala 🍇🍓kwa furaha. Mara tulionekana tukiogelea kwenye mto wenye maji safi yaburudishayo mioyo🏊‍♀️🏊‍♂️ yetu. Malaika yule alikua na wingi wa furaha akinishika mikono yangu asitake kuniacha.

    Nilipogutuka usingizini nilijihapia kuwa lazima nitaamkia kwenye apartment 🏘️yao ilinimjue zaidi ni nani haswa yule mtoto ambaye mbali na kunipungia mkono ninamuona ndotoni.

       Asubuhi mapambazuko🌄 nilimweleza mke wangu sarafina juu ya ile ndoto yangu nzuri niliyoiota usiku, katika maongezi yetu nilimwomba mke wangu ruhusa ya kwenda kumjua zaidi yule mtoto, angarau moyo  wangu utulie sio ndotoni nimuone na mwangani nimuone. Ni nani yule mtoto ❓

    Kuwa makini Mume wangu🤔 usijepatwa na baya tambua ile ni nyumba ya watu. "Alinitaka niwe makini.

      "Nitakua makini Daring, l promise nitarudi salama."Sarafina mke wangu alinisindikiza hadi chini ya ile Horofa yetu kisha akaniacha niende nikafanye uchunguzi wangu ili kumjua vizuri yule mtoto, ni nani haswa hadi anitokee ndotoni?"

'Ngo ng'o ng'o, hodi' nilibisha hodi lakini nikajichekesha 😂mimi  mwenyewe kumbe Kuna kengere🔔 ya kubonyeza ili alie ndani asikie. Nikakibinya kitufe Cha kengere iliyolia tiiii tiii tiiiii baada ya dakika chache kupita mlango wa ile🚪 apartment ulifunguliwa. Nilishituka na moyo wangu kidogo nizimie nilipomuona mwanamke ninayemjua.

     Alikua ni Linda, Ex-geri🧍‍♀️ wangu wa zamani, mwanamke niliyeachana naye kitambo nikaanza upya maisha yangu. Linda hakushituka zaidi ya kuniangalia tu. Hazikupita dakika tano yule Malaika niliyezoea kumuona akinitazama dirishani aliingia aliponiona tu alinikimbilia akanipokea kwa furaha mwilini mwake.

      "Waoo! Dady, l love you Dady." 😘🤗
 Nilishangaa kusikia akiniita Dady.

"Dady!" Nilijikuta natamka kwa mshangao. Nisijue yule Malaika anamaanisha nini?

   "Karibu 🙋Babiloni, ingia ndani tuongee." Linda alinikaribisha ndani.

     "Asante." Niliingia nikiwa na shauku ya kutaka kujua ni nani haswa yule Malaika aliyeniita Dady.🧍‍♂️

      "Utatumia kahawa au Tangawizi." Linda Alinitaka nichague.☕🍵

      "Kahawa☕ itanitosha." Linda akaelekea mekoni kuniandalia kahawa ambayo haikuchukua dakika tano alirejea akiwa na bakuri lililojaa vipande vya kashata.

    "Huyu ni mwanao!?"🤱 Nilimuuliza nikiwa naendelea kutafuna vipande vya kashata

    "Ndio ni mwanako pia."Alinijibu nisimuelewe maana miaka mitano iliyopita nilipoachana na Linda hakuwa na mimba 🤰wala mtoto. Vipi Sasa anipakazie kuwa huyu Malaika ni mwanangu? Linda akanisimulia.

   "Babi, tulipoachana miaka mitano iliyopita sikujua kama nilikua na ujauzito wa mwezi mmoja hadi pale nilipopima na kugundua tayari nishanasa ujauzito. Kama ningelikua mwanamke mjinga hakika ningeliishia kutoa ile mimba ila kwa hekima zangu niliiacha nikailea kwa tabu hadi nikajifungua nisijue nitakupata wapi maana wewe binafsi uliikwisha hama Mji.🌇 Aliongea.

     "Babiloni nilikutafuta sana Dear, nilikutafuta nisikupate hatimaye mimi pia nilihama Manzese nikaja kuishi huku llala boma, miezi mitatu iliyopita. Bahati nzuri baada ya kuhamia hapa siku moja nilikuona ukiteremka kutoka ndani ya gari yako 🚗nilitamani kukukimbilia lakini nilipomuona mkeo moyo wangu uliogopa nisije kuivuruga ndoa Yako, nikaacha yapotee. Uzuri nikawa ninakuona mara kwa mara ukiteremka ngazi za Horofa yetu lakini wewe hujawai niona. Nikamwambia Dolla mwanangu yule ni Baba yako, kuanzia siku ile Dolla aisikiapo Gari Yako ikiunguruma ukimbilia Dirishani akikupungia mkono na kucheka cheka.😹😹 Linda alieleza.

     "Duh! Mtoto ninayemuota ndotoni ni mwanangu?!" ⁉️Nilishindwa kuamini nikamweleza Linda sababu ya mimi kuja pale, Binafsi alifurahia. Baada ya maongezi ya takribani nusu saa niliaga na kundoka nikarejea nyumbani kuonana na mke wangu Sarafina. Nilipofika nyumbani nikamweleza Sarafina mke wangu baada ya kisa mkasa. Nikamweleza kuhusu Linda Ex-geri wangu yeye binafsi alishangaa lakini kwa hekima zake akaniambia:

    "Wanawake sisi sio watu wa kuaminika tuna roho za vinyonga, labda Kuna ukweli juu ya jambo hilo. Ninashauri mume wangu uende ukapime Partenity test (DNA) 🧬ili ujue kama ni kweli Dolla ni mwanao au la! Usije ukauziwa mbuzi 🐐kwenye gunia nilimsikiliza Sarafina nikakubaliana na mawazo yake. Asubuhi ya siku iliyofuata nikarejea tena nyumbani kwa Linda mama yake Dolla. Alinipokea nami nikamweleza suala la kwenda kupima DNA, mbona aliwaka 🔥🥵

      "Yaani baada ya kukuambia Dolla ni mwanao na wewe unakurupuka kuniambia kuhusu hayo ma  DNA 🧬 yenu." Aling'aka.🤬

    "Sio hivyo Linda ni kupata uthibitisho kamili na mimi niwe sehemu ya mtoto huyu ili nitoe majukumu yangu kwake."

    "Wanaume mpewe nini ili mtushukuru sisi wanawake!?"Alifura.👿

    "Nikuhakikishie mara ngapi kwamba Dolla ni mali yako?" Alihoji⁉️

     "Embu ondoka tafadhali rejea kwa mkeo." 😤😧😾Alikasirika sana, nilijiona mpumbavu niliyekurupuka lakini siku give up nikafunga safari Moja kwa Moja hadi vingunguti nyumbani kwa mama👧 yangu nikamweleza Kila kitu kuhusu yule mtoto Dolla na kikwazo nilichokutana nacho kutoka kwa mama yake. Uzuri mama alikua anamfahamu vizuri Linda akaahidi kunisaidia na kweli Mama alifunga safari hadi nyumbani kwa Linda huko waliketi na kuongea takribani masaa matatu hatimaye akaniletea majibu safi ya kuuridhisha moyo☺️😺 'Linda amekubali mkapime DNA ili kujua uhakika wa mtoto kama ni wako au la!'

    Siku tatu mbele mie, Linda na Dolla tulikua ndani ya Hospitali🏥👨‍⚕️😷 kubwa ya Muhimbili tukichukua Partenity test yaani DNA. Majibu ya DNA yalipotoka ilionesha asilimia 99.5 Linda hakudanganya mtoto Dolla alikua ni wangu, mwana wangu, mwana niliyemuota ndotoni, mwana aliyezoea kunipungia mkono wa furaha, tabasamu na cheko.

     Tulirejea nyumbani nikamweleza mke wangu Sarafina pamoja na mama yangu majibu safi ya DNA asilimia 99.5 Dolla ni mwanangu niliyempata kwa bahati tu familia yangu ikafurahia na uzuri, wote tulikubaliana kuandaa bonge la party 🎊💃🥳🎈 kuwakaribisha Linda na Dolla waungane nasi


""""""""

TCHAO

💝💕

""""""""""

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...