Saturday, April 12, 2025

MIPASHO YA MAMSAPU

 


 MIPASHO YA MAMSAPU



WATABAKI NA LABDA


Sehemu ya kwanza





                “Teeh teeh teeh,😂😂 ai babu we!”👌  Nacheka mie, nacheka vizuri, nacheka kwa furaha, nacheka tena narudia kucheka, ‘teeh the teeh,’ 🤣😘basi shoga nakwambieni hadi raha, raha nijipe mie mwenyewe si walisemaga wahenga “ MWENYE WIVU AJINYONGE” basi na mie ninasema “WENYE GERE WASAGE CHUPA, WENYE KIJICHO WAKAJITOSE BAHARINI,”🌊🏄‍♂️ maisha haya ni yangu mie Mamsapu na mume wangu Pompo, kiwaumacho nini? Kinachowauma kiwaume tu, tena mlie nyie mabibi wenye sura mkomavu, hata podali inawakataa, ndo’ iwe Rosheni, teeh teeh  🤣 mlie tena mliage, hamna haya nyie, kutwa kuchwa kunisakama kwa maneno ya  umbea na ushambea, nawambieni “MTABAKI NA LABDA!”


              Washazoea na sasa ninawakanya mtoto wa  mwenzenu na mie ninae mama kamwe mama yangu hakukwama kanilea kwa hekima, saburi na busara, hadi hapa nilipofika ni mkono wa mama yangu🤱, tuone sasa tuone kama mtaja kufikia levo zangu, levo za majuu JUU KAMA MAWINGU.🌪️🌤️🌁 Niwaambie  tena niwaambie HIZI NI ANGA ZANGU, ANGA ZA MWENYEWE,  anga zangu mie Mamsapu mama la kitanga kule mapenzi na mahaba yalipozaliwa, si nyie KIGOMA MWISHO WA RELI, teeh teeh (nacheka mie)  mshakuwa KATERERO  michepuko nyie, VITONGA nyie, nyie ni miteremko WATU WA OOOOVYO.🎃


                  Kutwa kuchwa kunijazia list ya maneno ya USHILAWADU (umbea) na kwa huo ushilawadu wao kamwe siwapi posho, wenyewe wanajua fika kuwa UMBEA HAUNAGA POSHO, Nyoooooo….. walie tu, kuzifikia levo zangu mbona watangoja, tee teeh teeh (nacheka mie) watangoja hadi yesu✝️ arudi tena kuwachukua kondoo, 🐑teeh teeh teeh teeh nicheke mie tena nacheeeeka kwa dharau, maringo na kebehi


            Kucheka haki! Tena haki yangu au sio Shoga? Kucheka kwaniongezea kalenda za kuliona jua, maisha ya Kobe, marefu kama vocha, sifi siozi Wala Sina baya. Enyoooo eti Mwaya kwanini nisiwacheke maboya hawa? Maboya ambao mie najua fika kuwa MIDOMONI MARAFIKI LAKINI KUMBE MIOYONI MAADUI, aku! 👌Babu we, waniteme na tena wanitapikie mbali, waniache jamani, waniache mie nina HAMSINI ZANGU sijala cha mtu, sidaiwi na mtu na kwa kifupi mie mama wa kebehi niawaambia hivi “ KULA🌮🍔🍝 HAMLI MTAISHIA KUNAWA,”  washa sahau fika kuwa MWENYE NYUMBA 🏡HAKIMBII  UVAMIZI WA SIAFU, Umbwa hawa, UMBWA KOKO midomo 🤐tu yawasumbua.

               Mie Mamsapu sio MDOGO DOGO, kama wao wanaojifunza maisha kwa kukopi na kuigiliza, nasemaje NISHAFUNDWA tena NIKAFUNDIKA  nimepitia UNYAGONI sasa  mie ni KUNGWI, NAFSI HIYO NINAYO,NGUVU NINAZO, UWEZO NINAO NA FURSA HII KWANGU HAINIPITI, inanitafuta kila kona ya dunia ai! Waooo, MWENZENU N’SHAPENDWA,  natambua fika kuwa maisha yetu ni wakati na wakati ni mida, mida inaniruhusu NIWASUTE, NIWACHAMBUE CHAMBUE KAMA KARANGA Mabedui 👿👹na mahayawani hawa, YA KWAO YAMEWASHINDA SIJUI YA KWANGU WATAYAWEZA?


          Mmmh! (Naguna mie) Hawana ishu za maana hata  wakijiweka bize ili kuyapeleleza ya moyo wangu nasema hivi hawatakamilisha ripoti zao chafu chafukoge, nishatulia na wangu wa moyoni Pompo💖👩‍❤️‍💋‍👩 ni mtu mzima anaye jielewa, anayaelewa maisha yakoje na maisha yanataka nini? Sio nyie MAZUMBUKUKU  hamyawezi MARUDI, yamewapiku marudi ndio mbaki kujuta majuto ya mjukuu ‘teeh teeh teeh’ nacheka mie, au sio shosti  HUU MCHEZO HAUITAJI HASIRA upole ni nafsi yake. Mie natoka TATU BILA  ⚽⛹️ati wananilazimisha NGOMA DROO, Neva! HAFIKI MBALI KIPINGU HATA AKENDA MBINGUNI    .


Na leo nayamwaga 💦tuone sasa kama watayazoa, YAMEWAFIKA SHINGONI wangali wanatapatapa, yangu mie macho,👀 hivi ninavyo ongea mbona kila mtu huko kitaani anawa NYANYAPAA kama vile wana ugonjwa wa UKOMA. Nishasikia maneno kibao jamii inawasuta kwa kuwaambia shoga zao, WAOGOPENI WATU HAWA, washalaaniwa MBELE HAWANA NYUMA HAWANA, hawaeleweki wapi mwanzo wapi mwisho” Teeh teeh teeh, 🤤😆n’cheke mie.

           WIVU KIDONDA, WAKISHIRIKI WATAKONDA, nishawasoma zamaani wanajua fika kuwa mie ninae mwandani, laazizi wa moyo💞💝 wangu, sioni haja ya kuirudia hiyo sentensi bali ukweli wajue kuwa mie Mamsapu na Pompo ni wawili tulofungamana, asiwepo wa kutufungua zaidi ya Mola muweza, kwanza               YA  MUNGU NI MENGI YA WANADAMU MACHACHE , sioni mfadhaiko kusema ukweli kwa kutumia mifano   iso na mafumbo, wao binafsi walijua fika kuwa itakuwa simpo kumpata wangu wa moyoni pompo.

              HATA WAKISUGUA BENCHI mara milioni zaidi lakini kamwe hawawezi kifikia LEVO HII nipo kwenye anga zangu, wacha nijilie vyangu, vyangu ni VINONO vilo NONOKA, vilo TONONOKA si kama vyao vya kutapika na kutia kinyaa na kichefu chefu  Mmmh! Shoga unajua fika kuwa vya kwao ni matapishi? Na matapiko hayo wakayatupe jahani sio ati wanijazie Inzi kwenye SITA KWA SITA zangu, enyoooo WALIE TU.

             Acha basi Nyoyo nikupe mfano mdogo mdogo wa huyu bibie mwenye kijicho na kidudu mtu aitwaye MARIAMU jinale zuri lenye wingi wa Baraka lakini ubaya wake ni kwamba Baraka alizopewa hawezi kuzitumia, MAMBO  HAYAWEZI, MAPENZI HAYAJUI, MARUDI YAMEMPIKU NA KUMSHINDA, yupo yupo tu mtoto mwenyewe ni mtoto wa jana  bado MCHELE MCHELE (dogo dogo) japo uzuri ni wake, sura ni yake, mrefu sio  mwembamba sana lakini kwa yale yaliyo moyoni mwake tofauti na uzuri alionao.



 MWAYA KWA LEO NAKOMEA HAPA TUONANE KESHO MAJALIWA, NIKUPE UONDO UONDOKE.










                 “

SHOGANGU ZUHURA

 




NILIUHARIBU UHUSIANO💕💔 WA MUME WANGU NA

 GIRLFRIEND 👩‍❤️‍💋‍👨 WAKE BAADA YA VIFO ⚰️☠️ VYAO

 NILlSHANGAA NALETEWA MTOTO WAO 👧 NIMLEE.


      Ninakumbuka ilikua ni mwaka 2010 nilienda 🚶 kutembelea kaburi la Mume wangu Dylan aliyenitoka baada ya kupata ajari ya Gari na kuaga Dunia. Siku hiyo nilikwenda kuweka shada la Maua juu ya kaburi lake. Machozi mengi yalinibubujika.😢 nikiwa katikati ya maombi kumuombea🛐🤲 Dylan Mume wangu nilihisi kuguswa bega la mashoto, ubaridi ulipenya mwilini mwangu nikatetema.

Nilipogeuka nikakutana na uso wa mwanamke mzee mwenye kadirio la miaka themanini  akiwa👵 amemkumbatia mtoto ambaye kama sikosei alikua na umri wa mwaka mmoja.👩‍🍼
     
     "Tafadhali mchukue huyu Binti ni Binti aliyemuacha Mume wako." Pasina salamu aliongea yule Bibi kizee. Nilimtazama Kwa sekunde chache nami ⏲️nikahisi yawezekana ni Mwendawazimu."

      "Bibi chunga kauli yako, Mume wangu tangu amefariki imepita miezi sita sasa hatukuwa na mtoto Wala hatukujaliwa mtoto." Nilimjibu

      "Huyu ni mwanaye na Mimi ni Bibi kizee unataka nimpeleke wapi kama sio kwako wewe kumchukua." Aliongea.

     "Usiniharibie siku wewe Bibi kizee nimekwambia mimi na Mume wangu hatukuwa na mtoto, huyo mtoto mpeleke pahali popote pale hata kama ni kituo Cha kulelea watoto yatima." Nilimwambia Kwa hasira. Nikatoka pale Makaburini kuelekea pahali nilipoifadhi gari yangu Ili niondoke. Nilipofika kwenye Prado yangu nyeusi🚐 nikaifungua mlango upande wa Dereva. Nilipoufungua tu mlango jamani nilipigwa butwaa  baada ya kumkuta mtoto yule yule ambaye Bibi kizee nisiye mfahamu alimbeba.

      "Toba!🙄🧐 amemuingizaje mtoto ndani ya Gari ikiwa Gari yangu ilifungwa." Nilijiuliza.

     "Huyu Bibi kizee vipi au ni mchawi? Ananifosi nimchukue mtoto ambaye simjui" Nilitizama kila pembe ya Gari yangu kuangalia kama yule Bibi yupo lakini sikumuona nikambeba yule mtoto na kurejea naye pale nilipokutana na yule Mbibi yani kule Makaburini lakini ajabu sikumkuta.🪦

       "Mume wangu hakuwa mchepukaji, Mume wangu alikua ni mwanaume mtulivu na mwaminifu asingeliweza kuzaa nje ya ndoa.🤔" Niliwaza. Nikarejea ndani ya Gari yangu tayari kuiwasha moto na kuondoka. Nilimtazama yule Malaika 🧚 kusema kweli alikua ni mzuri wa kuvutia machoni. Moyoni Nikajisemea: 

'Ama niende Hospital🏥 nikachukua vipimo vya DNA'

'Mmh! Dylan Mume wangu hakuwa mchepukaji, alikaa  akatulia na Mimi tu👩‍❤️‍👨.'

'Wacha niende Hospital nikachukua vipimo vya DNA🧬' Nikaikimbiza Gari kuelekea Hospital, bahati nzuri nilipitia supermarket🛒 kumnunulia yule mtoto vichache vya kula, kunywa🍼🧋 na kutafuna Ili asije kunisumbua mbeleni.

'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
       "Nahitaji kumifanyia Partenity Test huyu mtoto ili nijue kama kweli ni mtoto wa marehemu Mume wangu.'' Niliongea na Dakta🥼🩺.
       
       "Madame Doka ombi lako sio mzigo kwetu tutalifanyia kazi ila itakubidi usubirie siku mbili au tatu tutakupatia jawabu tosha."Dakta lsmael aliongea.

       "Dakta nipo tayari kutoa pesa nyingi💷💰 ilimradi 
ili jambo lifanyike haraka na majibu nipatiwe Leo🔬 Leo."Nilimwambia Dakta lsmael.

      "Safi sana Madame kama utatoa pesa nyingi basi Leo Leo utapewa matokeo.📄" Yule Dakta mpenda pesa alikenua meno ya😁 furaha kisha akachukua Sampuli muhimu ajiri ya kumpima yule Binti nisiyemjua jinale zaidi ya kumwita Alicia.

Ikawa kusubiri matokeo forever, mtoto alipolia nilimbembeleza Kwa kumpatia maziwa, alipojisaidia haja kubwa na ndogo nilimbadilisha Pampasi, alipotaka kulala nilimbembeleza naye akalala, 🤱kazi ya malezi na kulea mwana yataka moyo. Hakuna marefu yasiyo na mwisho nikaitwa Ofisini kwa Dakta lsmael nikakabidhiwa Report na matokeo ya DNA 🧬  yalisomeka asilimia99.9 💯Mtoto Alicia ni wa Dylan Mume wangu yaani ni Copyraity
Mmh! Nilishangaa Dylan alikua na Siri ambayo hakutaka nisijue, Dylan alizaa na mwanamke pasina mimi kujua sembuse kuambiwa. Ona Sasa, ona amekufa na baada ya kifo chake mie naletewa kesi ambayo inageuka mzigo kwangu. Nikarejea nyumbani kwangu nikiwa mnyonge niliyejaa mawazo.

       Wiki mbili kupita nikiwa na mtoto Alicia naangaika kufanya Kila kitu kuhusu kumlea na kumpatia mahitaji yake yote nilibuka na wazo zuri nilihitaji kufahamu  Mama wa Alicia ili nimkabidhi mwanaye aanze kumlea na iwapo Mama yake Alicia hana uwezo kiuchumi  nitajitoa kumuwezesha ili afanikiwe kupata kazi au biashara.

       Mie Dorcka na Dylan hatukubahatika kupata mtoto, tumeishi wote miaka 42 ndani sio mbaya Alicia amerudisha heshima ya mume wangu Dylani basi Wacha nimsake Mama yake Alicia.

   'Duh! Nitaanzia wapi? Mwanamke simjui sijui nitaanzia wapi kujua pahali anapoishi?' Nilijiuliza.

      'Yule Bibi aliyenikabidhi Alicia pia sijui wapi anapoishi? Jamani mtihani huu!!' Niliwaza.

     'Ok, ok 👍 yanipasa nianze kusechi sechi mtandaoni, Ofisini na nyumbani yamkini nitapata kitu.' Basi mie huyo nikaingia mitandaoni: Fb, Wasap ya mume wangu, Twitter, Reddit, YouTube, na kila mtandao alioutumia marehemu mume wangu nikisoma Kila jumbe na kuangalia kila picha lakini sikuona Darili za Dylan kunena  au kupiga picha akiwa pamoja na mwanamke 

      Nikafanya hima kupangua pangua nguo zake kabati lote lakini wapi! Nikaingia Ofisini kwake na kuivuruga vuruga Kila kilicho Ofisini lakini wapi! Sikupata kitu. Taratibu nilianza kukata tamaa. Ghafla ninakumbuka ndani ya Gari yake alifunga kamera iliyomuongoza kujua wapi anakwendra, wapi yupo au anaongea na nani ndani ya Gari. 


Nikafurahia na kufanya hima kuichunguza ile kamera iliyopachikwa ndani ya Gari. Nilichunguza Kila sehemu alizoenda lakini hakuna sehemu nilipoona akiwa na mwanamke, nilichunguza kila mwanamke aliyeongea nae ndani ya Gari lakini sikuiona picha yoyote ya mwanamke ndipo akili zangu zikapata mwanga💡 niligundua Kuna sehemu alizoea kwenda, nikafurahia na kuhapo naweza kupata kufahamu wowote kuhusu mwanamke aliyezaa na Mume wangu Dylani.

    'Njia ya Pugu Sekondari Barabara ya Majohe karibu na kituo cha Mjomba Kuna Pub imeandika Paris Pub. Nyumba nambari mbili.' Nilisoma Direction ndani ya ile kamera. Hapo ndipo Dylan upendelea kwenda zaidi ya mara mia.

Nikamchukua Alicia tukapakia ndani ya Prado Gari yangu mie Bosy Lady tukatoka pale Oysterbay pahali ninapoishi nyumba yangu mwenyewe na Safari ya kwenda Gogolamboto njia ya Majohe iliwadia.Tulifika Paris Pub, nikachunguza chunguza niipate nyumba nambari tatu bahati nzuri nikaiona.

  'Ngoo ngoo ngoo' Nikiwa nimembeba Alicia mgongoni nikabisha lango, halikufunguliwa na aliyefungua  alikua ni yule yule Mbibi niliyekutana naye makaburini, yule Mbibi aliye to seenidhiria mtoto akamtekeleza na kupotea kama mchawi.

    "Jesu!"  Alishituka. Aliponiona.

    "Umekuja kuniadhibu mie mwanamke mzee nisiye na nguvu za kumlea mtoto wa mpangaji aliyefariki miezi Saba iliyopita." Aliongea machozi yakimtoka.

  "Mpangaji." Mpangaji aliyefariki ndie aliyezaa na Mume wangu?" Nilijikuta  nauliza lakini hakunijibu ila akatamka maneno yafuatayo

    "Kwanini usiondoke na huyo mtoto ukamlea jamani mie kizee nitapata wapi nguvu za kunywesha uji na maziwa, nitapata wapi nguvu za kumfulia au kumbadilisha pampasi? Miguu yangu imechoka kwenda Clinick, jamani Marehemu Zuhura kwanini unaniadhibu mimi." Alilalamika na kumwaga chozi akitazama juu mbinguni.

    "Zuhura!? Zuhura Ambrose au Zuhura nani?" Nilijikuta nauliza.

    "Ndio, Zuhura Ambrose. Je wamjua?" yule Bibi aliacha kulia akauliza.

   "Embu tuingie ndani tuyajadili yamkini ninaweza kupata picha juu ya huyu Zuhura na Mume wangu Dylani. Nilimwomba yule kibibi tukaingia ndani na kuketu sebuleni, akaniandalia  Kahawa na vipande vya karanga taratibu maongezi yakapamba moto 

""""""""""""""""""
"Huyu ndiye Zuhura mpangaji wangu akiwa na mwanaume aliyezaa nae." Yule Bibi aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Cesilia alinionesha photo moja kubwa aliyopiga mume wangu  pamoja na Zuhura Ambrose. Nilipoitazama almanusura nidondoke na kuzirai.

     "Yupo wapi huyo Zuhura?" Nilimuuliza yule Mbibi.

   "Alifariki miezi Sita iliyopita. Alifariki kwa msongo wa mawazo. Mara baada ya kupewa taarifa juu ya kifo cha hawara yake Bwana Dylan. Kuja nyumbani kwako nilibahatisha tu ila ukweli ni kwamba Zuhura na Dylan walikua ni wasiri sana. Hawakutaka habari zao mtu azijue. Bibi Cesilia aliongea.

    "Naomba unieleze jinsi unavyomjua Zuhura." Bibi Cesilia aliongea. Nikayapangusa machozi yaliyonibubujika kama kisima kisha nikaanza kumsimulia Bibi kisa na mkasa kuanzia pale nilipomjua Dylan hadi siku ile nimemwaribia Shoga yangu Zuhura mipango yake 

   "Mume wangu Dylan alikua ni aina ya wanaume wanaojua kupenda hata mwanamke asimuache, mwanaume anayejua kubembeleza mwanamke akabembelezeka. Mcheshi, mpole,mwenye huruma." Nilianza kumsifia marehemu Mume wangu Dylan.

     "Mimi na Dylan tulikutana Chuo kikuu Dar es salaam kampasi ya Mlimani. Tulipendana sana, tukitoka usiku kula Dinner, tukienda beach, kumbi za burudani kucheza dance kumbi za sinema na....." Machozi yalinitoka nilipovuta kumbukumbu.

 "Tulikubaliana ndoa mara baada ya kumaliza Chuo lakini mwaka wa tatu wa masomo yetu Dylan alikuja Hosteli na kunipa Taarifa zilizouvunja💔 moyo wangu 

 'Dorka listen me carefully nimepata mpenzi mpya anaitwa Zuhura. Asante kwa mapenzi yako na muda wako naomba tuachane tu." Aliongea hivyo.

   "What do you say... Nini?" Nilikua nafunga vifungo vya gauni langu lakini vifungo vikanikataa na gauni likanipwerepeta.

    "Ndo hivyo Dorka sitaweza kuendeleza na wewe naomba penzi lifikie tamati"

     "Haiwezekani Dylan, haiwezekani mimi na wewe tumekubaliana Ndoa mara baada ya kumaliza Chuo Sasa kwanini unitende hivyo?" Nililalamika kulilinda penzi langu.

     "Nimempenda Zuu Ambrose, ameingia moyoni mwangu, naomba ukae kando." Aliongea kama vile hayajui mapenzi ya kuachwa yanavyoumiza.

   "siwezi, tafadhali siwezi Dylan, siwezi Daring Bado ninakupenda mimi tena ninakuhitaji kivile." Nilimpigia kelele.

    "Kelele zako ni kelele za kumpigia Mbuzi gitaa acheze Muziki. Nmesema penzi letu lifikie tamati. Dylan aliondoka ndani ya chumba changu Cha Hostel.

    "Dylan ..... Dylan ...... Daylan....." Nilimkimbilia nikiwa uchi mtupu hata nisiogope walionitazama wakinishangaa lakini Dylan hakunisikiliza zaidi ya kuondoka kurejea kwa Zuhura Ambrose 

********

Kama alivyosema haitaji kampani yangu, Dylan alimaanisha haniitaji kuanzia siku ile Dylan alianza kuambatana na Zuu wakinionesha mahaba yao hadi basi! Mie mwenzao wivu na uchungu wa kuachwa ukiniumiza sana. Nikageuka kilizi nikililia penzi lililonikataa, nikakonda na kudhoofu, masomo yalikua magumu na yasiyotamanika. Ajabu penzi la Zuu Ambrose na Dylan lilizidi kuchepua.


    Kila kituko kisa na mkasa niliwafanyia  ilimradi tu waachane lakini wapi! Hawakuachana, niliwai kukodisha mwanamke wa mchongo ili kumteka kihisia Dylan ili Zuu apate wivu lakini wapi! Mchogo ulibuma. Niliwakodisha na kuwalipa mashababi wenye sura safi na miili ya vyuma ili wamtongoze Zuu lakini wapi! Haikuzaa matunda.


    Nikaenda kwa wanganga na wachawi ili wamroge Zuu aachane na Dylan wangu lakini wapi! Sikufua ndafu dawa za wanganga na wachawi hazikuzaa matunda. Mbona hata kwa Apostle Mwamposa kununua mafuta ya upako niliwai kwenda ili kuliombea penzi la Zuu na Dylan lianguke na kumeguka vipande vipande ili mie nirudiane na Dylan wangu ajabu kama nilikosea vile penzi lao lilizidi kustawi na kupendeza. Hatimaye pesa nyingi zilipotea, muda mwingi ulinipotea, akili na maarifa yalinikimbia.

      Basi nikapata wazo, yamkini wazo langu lingenisaidia. Asubuhi Moja nilidamka Hostel kabla ya kunywa au kupiga kifungua kinywa nikaenda Domintory anayolala Dylan bahati nzuri nilimkuta akijipa zoezi🏋️‍♀️ la kuruka kamba ili kuuweka mwili wake fit.

    "Umefuata Nini huku Dorka? Nimekwambia achana na mimi sikutaki." Alinipigia kelele.

      "Sawa najua haunitaki lakini je haumtaki hata mwanao tarajiwa." Niliongea kwa tabasamu la kumvuta nyoka kutoka pangoni.

    "Mwanangu!?"⁉️ Aliuliza kwa mshangao.

    "Ndio mwanao, kama haumtaki si useme ili nimtoe." Nilijifanya kumtisha.

    "Ina maana Dorka una mimba!!!!!?*🫥😶‍🌫️🤔😱 Alizidi kushangaa

    "Sasa kumbe?!" Unafikiri mimi ni Binti wa hasara kama Zuu anayekuchuna pesa zako  Nikalikoleza.

    "Usinitanie Dorka, tafadhali sema ukweli." Niliona furaha yake usoni ikichomoza moyoni nilianza kujipongeza maana niliona Sasa mwanaume ameanza kulainika.

     "Nikudanganye wewe kama nani? Ni lini nimetamka uongo kwako Dylan? Sikiliza Dylan nakupa sharti Moja kama kweli unataka kuitwa Baba tafadhali rudi kwangu tuitunze na kuilea mimba yetu mtoto azaliwe. Kama hautaki kuitwa Baba niambie nikaitoe hii mimba ili nikuachie uhuru wako wako wa kuponda starehe pamoja na mpumbavu wako Zuu." Nilibwata.

    "Hapana Dorka naomba usiitoe hiyo mimba nipo tayari na pia ninatamani kuitwa Baba." Dylan akanisogelea na kunikumbata kumbato nililolimiss muda mrefu mapenzini.

   "Achana na tena mfute Zuu kuanzia Leo." Nilimuonya 

    "Lazima niachane nae mama wa watoto wangu." Alinikumbata zaidi.

    "Vipi kuhusu mipango yetu ya ndoa." Nilimkumbusha.

      "Kabla sijajifungua mtoto Ninahaitaji ndoa." Nilideka kwake.

       "Ndoa ipo Daring hata kama ukihitaji Leo nipo tayari kumwita
Padre atufungashe ndoa." Alipoa na kulainika kama barafu Juani.

""""""""""""
Zuu Ambrose aliposikia ati mie na Dylan tumerudiana Alifura kwa mahasira hasara, alimwaga chozi na kupoteza tumaini la kumpatia Dylan wangu. Msongo wa mawazo ulimkamata alitamani kujiua kwa kujinyonga (Mie huku na mimba yangu bandia tukicheka kwa furaha.😆😂.) Wazazi wake Zuu wakaingia hofu na wasiwasi juu ya Binti yao kipenzi haraka wakafanya kuhamia Nairobi Kenya huko Zuu akatulia na kiyashikilia masomo.

""""""""""
Mie na Sweet Dylan tukafunga ndoa yetu ndani ya kabisa la mtakatifu Cuthbert mahaba yakarejea tena. Basi kila siku asubuhi Dorka mie nikawa mtu wa kujifanya natapika ovyo ovyo, nalilia kula embe mbichi na ndimu, nalala lala makusudi, nabagua vyakula na kudeka kwa sana Deko ambazo Dylan mpenzi wangu alizikoreza zikakorea na kwa jinsi anavyoyajua na kuyaweza mapenzi eeh!😅🥰 Nijimiminie mie.


      Waswahili wanasema mimba haifichiki na kitanda hakizai haramu, wengine wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha .Hofu ya kugundulika kuwa ninadanganya ulinisumbua yaani ipo siku yakimwagika hayazileki,io siku mwenye mtoto wa bandia akija kugundua kuwa Sina mimba napachika matambaa tumboni basi nitumbuka mie.😅😅

    Nikamuaga mpenzi Dylan 'Babu ninakwea Hospitali' nilipofika Hospitali nikampanga Dakta wangu, pesa sabuni ya roho, 💰Dakta akapokea sabuni ya roho mate yakimwagika kama Zombie  mpango wetu ukatick. Dylan akapigiwa simu 'Please, haraka njoo Hospital,' Akafanya hima akanikuta nimelazwa juu ya kitanda Cha Hospital, damu na maji naongezewa.

     "Pole sana bwana Dylan mimba ya mkeo imechoropoka kabla ya wakati wake ni kwa sababu alianguka pindi anapanda ngazi za kupandia Hospital." Dakta Mpenda pesa aliongea.


      "Duh! Pole sana mke wangu Dorka, Mungu amepanga iwe hivyo na Mola atapanga mema yatufuate."Mume wangu aliongea chozi likitamani kuanguka.


      "Asante sana Mume wangu nilitamani sana kumleta mwanetu afurahi pamoja na sisi lakini imekua hivyo tena" Nililazimisha kulia machozi ya kinafik yalinitoka.


     "Usilie Daring ninakupenda sana Docka wangu." Mume wangu alinifuta machozi, uongo na mchongo ulifauru. Tukarudi Hostel kuendeleza masomo hata baada ya masomo tulipata ajira. Miaka nenda miaka rudi sikubahatika kushika mimba  lakini Bado Dylan alinipenda sana hakuonesha Darili za kunicheat au kupenda mwanamke mwingine zaidi ya mimi.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Nikamaliza kumsimulia Bibi Cesilia ile simulizi ya wivu wa mapenzi. Bibi alishangaa kukisikia kile kisa hata yeye poa hakujus vip Dylan na Zuhura walivyokutana zaidi ya kumuona Dylan akija mara kwa mara pahali anapoishi Zuhura.

Niliondoka nyumbani kwa Bibi Cesilia nikarejea Oysterbay nyumbani kwangu nikiwa na Alicia mwanangu ambaye nilijiapia kumtunza, kumlea na kumpatia mahitaji yake yote.


      Moyoni nilijiona Nina majuto na hatia kwanza nililiharibu penzi la Dylan na Zuhura waliopendana sababu mie sikupendwa pia sikujua mipango yake Mola juu ya maisha yangu. Pili, katika miaka yote niliyoishi na Dylani sikupata kushika mimba sembuse kulea mtoto wa kusingizia kutokana na uongo wangu nimeponzeka.😢 

     Dylan amekufa kwa sababu ya ajari na Zuhura kutokana na msongo wa mawazo ya kumpenda Dylan baya zaidi nimeachiwa mtoto yatima wajibu wangu kumlea kama mwanangu. Nina imani Zuhura atanisamehe huko aliko.


MIAKA KUMI NA SABA BAADAE

Alicia mwanangu akawa ni mtu mzima Sasa, mtu mzima mwenye kumi na nane zake. Siku moja nilimwita sebuleni nikamweleza kisa chote na mkasa juu ya maisha yangu, Mamaye Zuhura na marehemu Dylan mume wangu. Mwanangu Alicia hakuumia Wala kusikitika alipojua kuwa mie sio mama yake, alichonena yeye alisema:

     Ananipenda mimi kama mama yake mzazi haijalishi hata kama mie kwake ni Godmother kamwe hatoniacha zaidi ya kunipenda.
        
       "Mama yangu umeitunza, umenilea na kunipatia kila kitu kwa upendo na mapenzi yako mimi nimekula vizuri, nimelala pazuri, nimedeka na kudekezwa. Ninakupenda sana na nitakupenda milele." Akanikumbatia na kunipiga mabusu shavuni mie nilikua huku ninalia kwa uchungu.😭

********
TCHAO

💞💕

********

Wednesday, April 9, 2025

INFIDELITY





 MUME WANGU ALIMTIMUA🏃 NYUMBANI🏠 MAMA YANGU MZAZI MWENYE CHANGAMOTO YA AKILI🤪 MARA BAADA YA MAMA KUMFUMANIA AKIGONOKA NA CHANGUDOA. 💏


      Baada ya sherehe ya Noel na Mwaka mpya kufika ukingoni wanangu wawili Rashford na Josea 👩‍👧‍👦walihitaji kurudi shule,🏫🎒👨‍🏫 shule ya boarding, 🛌shule Binafsi ya kulipia.💰llikua ni kawaida ya my Husband kuwapeleka skuli 🚖Kila ifikapo January mosi. Mie nilibaki na mama yangu mwenye changamoto ya akili🧠 yaani kuna wakati akili zake ukimbia anakua kama sio yeye naye atafanya Kila kituko cha kuudhi 🤯au kuchukiza, utoto mwingi hadi tutamchoka. Atavua nguo zake, atapiga kelele, atavunjavunja vyombo na kuharibu pia baada ya muda akili zake zingerudi na kuwa sawa, hapo angelitulia tuli kama maji mtungini.🚰🏺.


    Uzuri wa changamoto ya kupoteza ufahamu🤯 pale inapofika ukomo mama yangu urejea katika hali yake ya kawaida. Hali ya kujutia matendo yake ya utoto, 🥹hali ya kujionya kutorudia tena matendo haribifu,😮‍💨 hali ya utulivu, amani na furaha🫡. Ajabu changamoto yake ingelirejea tena.😵‍💫


       Basi mume wangu Dionice aliniambia kwa mwaka huu 2024 January niwapeleke watoto warejee kusoma nje ya Mkoa yaani Tanga mjini sikupinga Wala kukataa nilimuomba anitunzie mama yangu mwenye changamoto ya ufahamu, kwa moyo❣️ mkunjufu Dionice alikubali Ombi langu. Safari yangu mie Gigyfriday na wanangu Rashford na Josea ilipamba moto.


"""""""""""""""""""""""


"Hallow! Gigy"☎️ Siku ya tatu baada ya kuingia Tanga mjini mume wangu alinipigia simu.


"Hallow! Daring😘"Nilimwitikia wakati huo nipo ndani ya Moja ya hoteli 🏨🏩za kifahari.


"Kuna tatizo kubwa limetokea nyumbani" 🏡Toba!😶 Dionice alinishitua kidogo.  


"Tatizo!?"🤭 Niliuliza kwa mshangao kidogo Wine yangu niliyokua nikiinywa imwagike.


     "Ndio tatizo my wife, ni tatizo kubwa" Aliongea


     "Tatizo gani? Tafadhali nieleze." Nilikaa mkao wa kula kuisikiliza ile changamoto.


     "Bibi mama mkewe ametoweka nyumbani nisijue ni wapi alipoelekea. Safari hii ile grass 🍷🍾ilinidondoka chini puuuu ikadondoka na kuvunjika. Maana nilipata mshituko.


     "Ametoweka! 🏃‍♀️Ametowekea wapi na lini ametoweka?" Maswali mfululizo yalinitoka, hofu na wasiwasi juu ya Mamangu mwenye changamoto ilinivamia.


      "Ametoweka leo🏃‍♀️,sijui ni wapi alipotowekea!? Ningali ninamtafuta." Dionice alinijibu.


     "Vipi ushaenda Police👮‍♂️🚓 kutoa taarifa?" Nilimuuliza, jibu alilonipa lilinivunja maini.


    "Bado nakusubiri wewe uje tuangaike pamoja kumtafuta." Sikutaka kuendelea kuongea kwenye simu,📱nikakurupuka kuondoka ndani ya ile Hoteli 🛋️nikiwa nimeacha Kila kitu changu chenye thamani💰 na kisicho na thamani. Nikashuka ngazi za ile Horofa haraka haraka nikakimbilia uwanja wa Ndege🛫 ilikuwai Ndege ✈️itakayoondoka siku ya Leo kwenda Dar es saalam🌇.


      Niliingia Tanga nikiwa na Gari yetu lakini baada ya kusikia habari juu ya tatizo lililompata Mama ilibidi niiache Gari yetu pale pale Airport, nikapanda Ndege iliyokua inaelekea Dar es saalam. Moyoni nikijilaumu kwanini niliruhusu Dionice amtunze Mama yangu mwenye changamoto? Ni heri na ni bora kama ningelibaki kumtunza mimi mwenyewe.


   "Labda alimuachia ufunguo wa Geti kuu?⛩️" Nilijiuliza, nikiwa nimepagawa yote kwa sababu nilimpenda sana mama yangu na kuumia moyo ilikua lazima.


    "Mama umekwenda wapi rudi tafadhali." Nilisali kimoyomoyo 🛐📿


    "Ninakupenda Mama yangu, ninakupenda Dear." Nililia pekee yangu ndani ya ile Ndege. Safari yangu haikua ndefu sababu kutoka Tanga kwenda Dar ni masaa ⏰machache baada ya kuingia Dar nikafanya pupa pupa kukodi Uber🚖 ilonikimbiza moja kwa moja hadi nyumbani kwangu nilikomkuta mume wangu amekula pozi sebuleni macho kodo kwenye Tv📺 anafuatilia Tamthilia ya Juakali.🌞


     "Daring badala ya kuangaika mitaani kumtafuta Mama yangu wewe umepiga pozi namba nne kwenye Video📺 unatizama Tamthilia" Nililalamika mara baada ya kuingia pale sebuleni.

      

     "Gigyfriday, unastahiri kupumzika kwanza ndipo nikupe taarifa kamili." Alinipokea Kisha akanitaka nipumzike sofani🛋️ akafanya hima kuniletea maji baridi Jokofuni 🧊lakini wapi! Hayakupita kooni. 


     "Muda huu unaoingia ndo' na mimi ni naingia, mwenzio nimekesha🌗 nikimtafuta Bibi Mama mkwe nisimpate." Aliongea. 


     "Ushaenda 🏃Polisi?👮, Polisi nao wanasemaje?" Maswali yalinitoka. 

    

     "Nimeenda, nao wameahidi kutusaidia watampata tu." Alinipooza. 


    "Tatizo nini hadi Mama akimbie nyumbani?" Nilihoji. 


    "Gigyfriday si unajua changamoto inayomsumbua Bibi Mama mkwe?" 


    "Duh! Mola wangu amwepushie mabaya Mama yangu" Niliropokwa. 


    "Amka basi twende tukaendelee kumtafuta." Ninavyompenda Mama yangu nilikua tayari kufanya jambo lolote ilimradi apatikane.


       "Gigy my Daring Nimechoka please." Alidekadeka. 


     "We! Mwanaume wa wapi? Embu Amka hapo tukaangaike." Nilimpigia kelele haraka haraka. Ttulichangamka kumtafuta. Tulimtafuta sana Mama yangu, tulimtafuta ndani ya majalala ya takataka🗑️🚮 tukidhani labda amekwenda huko, tulizunguka mtaa kwa mtaa tukiuliza na kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki 👥na majirani lakini wapi! Ma. Hakupatikana. Hatukukata tamaa tuliendelea kumtafuta Mama.


       ::::::::::::::::::::::::


Siku ya tatu tulijisikia kuchoka sana maana tulikua tunapumzika na kulala popote pale ili tubahatike kumpata Mama. Tuliamua kuelekea nyumbani kwenda kukoga na kubadili nguo maana kwa zaidi ya siku tatu hizi hatukubadili nguo Wala kugusa maji mwilini.


    "Kwanini tusiende kulitangaza🔊🔉 jambo letu kwenye Mablogu.📃 Televisheni 📺na Radion!📻📡"Nilitoa ushauri.


     "Wazo zuri" alinijibu kwa ufupi.


    "Tutangaze donge nono💰 kwa mtu au watu watakao mpata Mama." Nilitoa wazo.


     "Unamaanisha pesa, 💶💸 , kiasi Gani? "Dionice aliniuliza.


    "Nipo tayari kutoa Million Tano 💳💸kwa mtu atakayebahatika kumpata Mama yangu."Nilimjibu Dionice.


    "Gigy pesa zote hizo? Pesa za kufanyia jambo la maana." Alinijibu kama vile hakupendezwa na wazo langu.


     "Najua Dion, lakini pia Mama yangu ni mtu wa maana." Nilimziba mdomo.🤫 Tukasikia muungurumo wa gari ikiingia uwanjani kwetu, ilikua ni Gari ya Polisi. Sie tulikodoa macho kodo kwenye Dirisha ili kujua kuna Nini? Nikaingiwa na furaha baada ya kumuona Mama yangu akiteremshwa kutoka kwenye ile Gari ya Polisi. Polisi walifanya kazi nzito ya kumsaka hadi kumpata Mama yangu.


     "Twende tukampokee." Nilimwambia Dionice kwa furaha.


    "We, nenda tu ukampokee!" Mume wangu hakuonesha furaha. Nikatoka kwenda kumlaki Mama yangu kwa furaha na kumkuta akiwa mzima mwenye afya, pasina makovu au ubaya mwilini mwake. Nikampokea na kumkaribisha tena Nyumbani kwetu. Aliingia sebuleni na mimi pia niliingia, Mabwana Polisi nao waliingia. Ile tunaingia tu, Mama aliponwona mume wangu alianza kupiga kelele kama amemwona Pepo mchafu.🦹‍♀️👿


      "Mkamateni huyu fedhuli ☠️na firauni mjaa laana." Alimnyoshea dole mume wangu, aliyeanza kuogopa.


      "Kwani amefanya nini Mama!?" Nilimuuliza kwa mshangao⁉️


     "Huyu fedhuli ndio sababu ya mimi kuondoka hapa nyumbani." Nilimsikiliza, Askari walimsikiliza pia.


    "Tatizo nini!? Embu tueleze."Askari mmoja alimtaka mama yangu afungue kinywa ayatoe yaliyofichama moyoni. Mama akaanza kueleza.


     "Gigyfriday huyu mumeo ni shetani👹 asiye na huruma."Alimnyoshea mkono👉 mume wangu aliyeketi sofani kimya akisikiliza.


      "Ulipoondoka kwenda Tanga kuwapeleka wajukuu zangu Shule usiku mmoja nilikua nimelala chumbani kwangu lakini nikaja kuamshwa na milio ya chaga za kitanda 🛏️chumbani kwenu. Mbali na sauti za chaga niliskia mili ya sauti za mahaba, mwanzo nilivumilia moyoni nilijisemea sauti hizi na vilio hivi vikuu vya mahaba sijazoea kuvisikia ndani ya nyumba hii." Mama aliongea wote tulimsikiliza.


     "Nikajiwa na wazo kwamba labda Binti yangu Gigyfriday amerejea kutoka Safarini, lakini kwanini arejee pasina kuniambia sembuse kuja chumbani kwangu kunitakia hali? Basi mie nikateremka ngazi za Horofa na kuelekea chini kule sauti za chaga na mahaba zikiendelea kulindima. Bahati nzuri au mbaya mlango wa chumba chenu ulikua umeachwa wazi." Mama alipumzika kidogo kuongea🙇


   "Nikausukuma ule mlango, taa zilikua zinawaka💡. Salale! Macho yangu yalitua kitandani nikamuona Mkwe wangu Dionice akifanya zinaa na mwanamke mwingine."Mama alitoboa Siri.


     "Bibi Mama mkewe ni mwongo👺" Dionice alimpinga Mama yangu.


      "Kama mimi ni mwongo yule mwanamke ni nani haswa pale kitandani unapopaswa kulala na mkeo Gigy?" Mama alimuuliza Dionice.


     "Mwanamke aliyelala kitandani alikua ni Ombaomba niliyemuokota mitaani nikampa maji, 💦chakula🥪 na pahali pa kulala🛌 kama hifadhi. Dionice alijitetea sie twalimsikiliza.


    "Na ile sketi kimini👗, kitopu,👙 wigi🦰 la bei gharama, mkoba mwekundu👜, viatu virefu vya mchuchumio 👠 baya zaidi amepakaza mdomo wake lips nyekundu💋💄 wote mlikuwa mmelewa bwiiiii 🍻🍺msitamanike." Maneno yaliyomtoka Mama yalitushangaza 😂😶‍🌫️


    "Dionice ni kweli ayaongeayo Mama!?"Nilimuuliza. 


    "La! Hasha, Bibi Mama mkewe anadanganya. Lakini Gigy si unajua kwamba Mama ana changamoto ya kuvurugwa akili? Yamkini akili zake zilihama ndio maana anaongea wendawazimu." Dionice aliongea mikono yake na miguu ikipata kitetemeshi.


     "Mume wangu lakini si ni wewe ndiye unayedai kuwa ulimleta Ombaomba ndani ya chumba chetu Sasa yawezekana vipi Ombaomba akalala chumbani kwetu wakati vyumba vya wageni vimejaa tele na baya zaidi wote wawili mlilewa?" 🍺🥂Nilimuuliza kwa hasira.👿


       "Alafu tangu Mama ametoweka mbona hukuniambia kama ulimleta Ombaomba chumbani kwetu?" Nilimuuliza.❓


    "Kumbe mimi ninawapeleka watoto shule wewe unafanya ngono na Malaya unaowaita Ombaomba? Hakunijibu zaidi ya kuangalia chini kwa aibu. Mama yangu akaendelea kunena:


    "Nilipomuuliza mkwe wangu kwanini unafanya ngono na Malaya chumba ulalacho na Binti yangu mkwe akanijibu jeuri na kuniambia 'hii ni nyumba yake, ana haki ya kufanya kitu chochote kile.' " Toba! Nilishituka yaani nyumba niijenge mie alafu mwanaume amjibu kunya 💩 Mama yangu.


      "Mkwe wangu akaniambia niondoke haraka ndani ya hii nyumba sababu hii nyumba ni yake, mimi na mwanangu Gigy hatuna chetu hapa." Mama alianza kulia.🥹 Mimi pia chozi lilinitoka 


     "Hii ni nyumba yako 🏡Dion? Ulijenga wewe?" Nilimuuliza, hakunijibu.


      "llibidi niondoke Gigyfriday, niliondoka akinitazama wakati huohuo amemkumbatia Malaya." Mama aliongea kwa uchungu.


     "Nisamehe Gigy, nisamehe Daring....💞 Pombe zilinidanganya " Aliongea.


     "Siwezi kukusamehe, umemvunjia heshima Mama yangu." Nilianza kulia chozi.😭😢


      "Mama kwa sababu sisi hatulioni kosa alilolitenda huyu Bwana Dionice pia hili jambo ni la kifamilia tungependa tuwaachie hii kesi muimalize nyie wenyewe." Bwana Askari aliongea Kisha wakaondoka na kutuacha sie twalumbana na kupigiana kelele ndani ya nyumba.


     "Beba Kila kilicho chako 🧳na uondoke ndani ya Nyumba yangu, muuaji mkubwa wewe."Nilimpigia kelele.


    "Nisamehe Gigyfriday, nisame sweetie. Ibilisi😈👹 alinipitia." Alijitetea


     "Na wewe kampitie huyo lbilisi. Mkeo sikutoshi hadi ufikie hatua ya kutembea na Malaya!? Eeh!? Baya zaidi unalala nae kitanda ninacholala na wewe." Nilimfokea.


       "Nisamehe Daringi 🙇‍♂️please." Sikujali Wala sikumsikiliza.


       "Nasema beba vigagula vyako uondoke. Nilitilia mkazo, akaingia chumbani na kusomba vilago vyake safari ya kuondoka ilifuata.


     "Barua ya Taraka utaipata kwa Mwanasheria ⚖️ infidelity mkubwa wewe." Nilimkemea kwa hasira😡😤


    "I'm Sorry Gigy lm sorry please."Alibembeleza sana


     "I don't care please leave my house now." Nilifoka, Aliondoka akiwa mnyonge na mwenye huzuni



***************

(Embu nishaurini wenyewe, nimsamehe au nimbwage kwa Mwanasheria !? Ningali katika machozi na kuvurugwa 🥲) 


***************


TCHAO 😢🥹😭🤯


""""""""""""""""'""'''''''''''




     


    




   

      

Saturday, March 29, 2025

TUNDA LA FARAJA

 """"""

   




TUNDA🍇🍒🍓 LA FARAJA 🧑‍🍼




         Nilimpenda Jerry👩‍❤️‍💋‍👨, nilimpenda sana hatimaye Mimi na yeye tulikuja kufunga ndoa 👰💍💖ambayo ilikuja kujibu baada ya Mwaka mmoja wa furaha ya ndoa binti yetu Zuena 🚼 (Basi tumwite Zuu🐝)alizaliwa mapenzi yetu yakawa matamu ya kudumu. Mie Isha, Jerry na Zuena tulikua na utaratibu mmoja mzuri ambao hatukuuacha 'Kutoa zawadi siku ya Christmas 🎄 🎁 ⛄ na Mwaka mpya🎊🎉🎇' kutoa zawadi Kwa Mamia ya watoto waliokuwa wakiifurahia siku ya Noeli 🧑‍🎄na New year🎊.


      Ya Mungu mengi Binti yetu Zuu alikuja kuugua🤒🥵 sana, aliugua Maralia kali iliyopelekea kudondoka na kuzima 🌠 🕯️huzuni ikavamia nyumba yetu, furaha ikapotea na kutoweka lakini bado tuliendelea na ule utamaduni wetu wa kutoa zawadi Kipindi cha sikukuu ya Noel na mwaka mpya Zawadi nyingi walizozipenda watoto ni Pipi,🍭🍬🍫 Biscuits🍪, Big G, Maputo 🎈na midoli ya kuchezea 🎎🪆.


         Bahati ya kuishi na Mume wangu Jerry ikaingia mdudu, Jerry akanikataa wazi wazi,💔 Jerry hakutaka kuishi na Mimi Tena. Alinitamkia kuwa hanipendi, amenichoka, Hana hamu ya kuishi na Mimi. Nilipigania ndoa💍 yangu kutaka kujua sababu kuu inayofanya Mume wangu wa ndoa kutaka kuishi pekee, kujitenga na kuondoka nyumbani.🏡 Jawabu nililolipata kutoka Kwa Jerry: 'Niache ✋nipumzike'. Nikanywea lakini bado kila ifikapo Noeli na mwaka mpya Zawadi zilimiminika Kwa watoto🧸🐅🐰. Utamaduni huo niliuedeleza nikiwa pekee yangu.


        ******************

Noeli ya mwaka 2023 niliipenda japokua upweke ulinimeza, 👤upweke wa kutokuwa pamoja na Mwanangu Zuu,🧑‍🍼🚼 upweke wa kuachwa na Mume wangu mpenzi Jerry.🏌️‍♀️ Baada ya kugawa zawadi 🎁💐🎅Kwa watoto nikapata wazo niende kulitembelea kaburi la mwanangu Zuu, 🪦nikamwage chozi😿😢 nimuombee🛐📿 kipenzi changu abaki palipopema salama peponi☁️🌉


         Nilifika lakini pembeni ya kaburi la mwanangu Zuu Kuna kitu nilikiona nacho kikaniogopesha na kunishitua. Nilikuta kapu, kapu lililoachwa hapo. Nikalisogelea baridi ilikua ikinipiga,⛄🌨️🧊 meno yalitetemeka, nikakisogelea kile kikapu na kuchungulia kilicho ndani ya kapu.


     Jesu! 😶Nilishituka mie nisiyaamini macho yangu, nikatazama ndani ya kapu, moyo ulikufa ganzi.


       'ng'aaa ng'aaa ng'aaaa' 😢sauti ya kitoto akilia ilisikika baada ya kuniona. Nikayageuza macho yangu👁️ huku na huko kutazama iwapo Kuna mtu ameacha mtoto pale Makaburini lakini sikubahatika kuona mtu. Nikabaki na butwaa 🤔mtoto aliendelea kulia.


Akili zikaniambia mchukuehuyo mtoto , nikafanya taratibu kumtoa ndani ya lile kapu nikamtoa mtoto aliyekua akilia, mwili mzima ulipigwa baridi, mtoto alitetemeka.


      "Oh! Baby usilie, hivi ni nani anayeweza kufanya ukatili huu wa kukuacha pekee Makaburini?" Niliongea na katoto nikijua fika hakawezi kutoa jibu. Nilipomnyanyua yule mtoto kutoka ndani ya lile kapu,🧺 macho yangu yakakiona kikaratasi kidogo cheupe,🗒️🖇️ nikainama na kukichukua ndani ya lile kapu, nikakutana na maandishi yameandikwa:



       'BINTI HUYU ANAITWA AMANDA, UMRI : MWAKA MMOJA' 



Hakuna maandishi mengine yaloongezwa. Nikakigeuza kile kikaratasi labda nitaambulia nambari za simu za aliyembwaga Amanda pale makaburini⚰️🪦 lakini wapi! sikuziona. Mazingira ya Makaburini yalikua tulivu asionekane mtu akipita. 🚶‍♂️🚶‍♀️Nifanye nini? Nilijiuliza.🧐❓Wacha niondoke, sikuweza kulitimiza lengo lililonileta pahali pale, lengo la kumuombea Binti yangu pamoja na kumuombolezea🤲😢 mpendwa wangu Zuu. Lundo la mawazo yalinisumbua kichwani.😤🤯



      Nilipofika nyumba🏘️ nikamkagua kagua yule Binti aliyekua amejinyea, 💩nikamfuta kinyesi na kumtafutia mavazi mapya. 🧦👚Baada ya masaa kadhaa nilipata wazo la kwenda Polisi kuripoti juu ya kumuokota mtoto Makaburini. Polisi walinipokea nami nikawaeleza kila kitu kwa hakika walishangaa🥺🤭 sababu ingelikuwa ni vigumu kumpata tena mzazi au mlezi wa Amanda maana mzazi au mlezi hakujulikana.🤷🙍


Polisi walinishauri nimchukue na kumpeleka kituo Cha kulelea watoto yatima, moyoni niliona sio Poa😞👎. Nikawaomba nimchukue yule mtoto na kuishi niishi nae, mtimani nilijiona nina bahati.💗 Nimefiwa na Binti yangu na sasa nimeokota tunda🍇🍒 la faida na faraja Tena tunda Hilo nimeliokota pembeni ya kaburi la Binti yangu. Aah!🙃😶 Jamani! Hii ni bahati, 🌠 ikiwezekana nitafanya process za kuasili mtoto (Adoptation) Ili awe Mali yangu.



                     %%%%%%%%%%%


          Amanda Akawa wangu na Mimi wa Amanda, ikawa kila siku nikiamka ni mwendo wa kumfuta kinyesi alichojinyea, kumuogesha, kumpikia👨‍🍳🍚 uji na kumpatia maziwa. 🍼Nilikesha kumbembeleza Binti yangu iwe usiku iwe mchana yaani hadi nikawaomba waajiri wangu wanipunguzie majukumu Ili tu niwe karibu na Binti yangu.👨‍🍼 Nashukuru Mungu mtoto aliendelea kukua na kutimiza mwaka mwingine🥳🎂🎊🧡 akiwa mikononi mwangu. 



Ndani ya mwaka huo mzima sikupata kupokea simu 📱ya kuitwa Polisi 👮‍♂️kupokea taarifa juu ya kupatikana Kwa Mama au mlezi wa Amanda. Noeli🎅🎄 ilipoisha baada ya mie na Binti yangu Amanda kugawa zawadi Kwa watoto🐰🦎🐉🦄🍿🧃🎁🎐 nilisikia mlango wa sebule yangu ukigongwa 🚪nikambeba Amanda wangu mgongoni Kisha tukatoka kwenda kumfungulia mgongaji.


Mlangoni nilikutana na sura ya polisi👮‍♂️ aliyeambatana na Bibi kizee👵 mwenye kadirio la miaka sabini. Baada ya salamu Nikawakaribisha 'Karibuni' 🙋‍♀️ 


      "Pole na majukumu Mama Amanda." Polisi aliongea nikafurahia kuitwa Mama Amanda.


     "Asante nimepoa, ni muda mrefu Sasa tangu tumeonana " Nilimwambia yule Polisi.


      "Mmh! Isha Kuna jambo Moja muhimu lililonileta kwako Leo nikiambatana na huyu Bibi kizee." Alimnyoshea 👉 👵mkono yule Bibi kizee mwenye makunyanzi usoni.


    "Bila shaka ongea." Nilimpa nafasi yule Ofisa kuongea 🔊lililowaleta.


    "Mama Mlezi wa Amanda amepatikana, huyu Bibi umuonaye ndiye mama mlezi wa Amanda." Ofisa wa Polisi alinishitua nikageuza shingo yangu kumtazama yule Bibi kizee.


     "Kwa hiyo lsha Bibi yake Amanda amekuja kumchukua mjukuu wake."


      "Toba!"⁉️ Nilitetemeka, "Kwa hiyo Leo mwana nimpemdaye anachukuliwa?" Nilimuuliza yule Ofisa huku Macho yakianza kunijaa machozi.

 

      "Damu🩸🅾️ nzito lsha,"Polisi aliongea kwa ufupi.


     "Hata kama Bwana Polisi Bado ninampenda Binti yangu." Nilijitetea.


     "Ninatambua lsha lakini ni vizuri mwenye mali apewe mali yake." Bwana Polisi aliongea. Niliona kama Dunia inataka kuniangukia, mtoto👶 niliyemzoea, niliyemhudumia Leo hii anakuja mtu mwingine kunipokonya.


     "Tufanye nini sasa Isha, mlezi wa mtoto Sasa amekuja na sisi Polisi tunatimiza wajibu wetu.Sikulielewa jambo analoliongea yule Bwana Polisi. Nilichopaswa kufanya ni kumkabidhi mtoto kwa mlezi husika tena ajabu hata sikuambiwa kisa cha huyo mtoto kutelekezwa makaburini ⚰️. Baada ya majadiliano ya muda mrefu tulikosa mwafaka lakini asiyekubali kushindwa si mshindani Bibi yule alimchukua Amanda akaniacha katikati ya uchungu na kuteteleka. Nikalia mie machozi la damu 😭😢🩸

    

      Nikazama maombini 🛐 nikimuiliza Mola wangu: 'Kwanini unanipa zawadi🎁 njema alafu unanipokonya.' Mola wangu hakunijibu kwa wakati akaniachia Ziwa la machozi.


      "Chukua bahasha hii." Bibi yake Amanda alinipatia bahasha niliyoipokea nisijue Nini kilichomo ndani ya bahasha, mtimani sikua na furaha ya kuondokewa na mtoto nimpemdaye ingawaje sio wangu wa damu. Bwana Polisi na Bibi yake Amanda wakaondoka na mie nikaelekea tandani kujibwaga nikiwa na wingi wa mawazo yaliyonisumbua na kuninyima Raha, nikamuwaza mwanangu Amanda niliyemuokota.


    "Saa sita mchana niliamka kutoka ndani ya dimbwi la mawazo huzuni na upweke nikakichukua kile kibahasha nilichopewa na Bibi yake Amanda, wala sikujua Nini kilichoandikwa ndani ya ile bahasha. Yule Bibi amemchukua mtoto bila kuniachia hata senti Tano labda ndani ya kile kibahasha Kuna karatasi ya Bank cheque nikajichotee mapesa Bank?😅💖 Nikaifungua ile bahasha taratibu na kukutana na kijikaratasi cheupe kilichoandikwa

 

     "ASANTE SANA NlNASHUKURU UMEMTUNZA NA KUMLEA AMANDA."


Moyo wangu uliripuka 💔🔥mara baada ya kuona mwandiko ambao nilihisi kuutambua. Haraka haraka nikakimbilia kwenye droo ya kabati 🗄️la nguo nikafanya kupekenyua na kupekenyua Kila kitu, nikakitafuta kile kikaratasi ambacho kiliachwa ndani ya kapu ile siku Amanda ametelekezwa makaburini. Nilikipata nikakichukuana kukiunganisha pamoja na kile cha pili nilichopewa na Bibi yake Amanda.


      Jesu!! 🫥 Nilishangaa. 'Mbona mwandiko huu wa Bibi yake Amanda na huu uliopo kwenye kikaratasi nilichokipata kwenye kapu ile siku Amanda ametelekezwa miandiko inafanana?!' ⁉️ Nilijiuliza.

 

     'Hapana, 🙅‍♂️ Kuna kitu hapa labda huyu Bibi Hana nia nzuri, labda huyu Bibi sio mtu mzuri.' Nilipata wazo.


    'Yamkini ni yeye ndiye aliyemtelekeza Amanda mwaka mmoja uliopita na Sasa amekuja kumchukua. Huu sio uungwana.' Niliwaza.Haraka haraka nikiwa nimevurugwa. Nikapata mawazo mawili; Mosi niende Polisi kuripoti hili jambo, pili nimtafute mume wangu Jerry mwanaume wangu aliyetaka kuishi pekee baada ya kifo Cha Binti yetu Zuu. Wazo la kwendra🚶‍♀️ Polisi sikulitilia maanani ila wazo la kumpigia Simu☎️📞 Jerry liliniingia kichwani. Haraka nikaichukua simu yangu ya mkononi na kubinya vitufe.📱


     "Hallow, Jerry habari Yako!?" Nilimsabahi.


    "Sijambo lsha. Habari za masiku!?" Alinisabahi pia.



     "Nzuri, nina jambo Moja la haraka ninaomba uje nyumbani kigamboni tujadiliane." Nilimwomba.


     "Nina kazi za kiofisi, lsha labda tukutane baadae."


     "Hapana Jerry ni jambo la haraka naomba uje tulijadili." Nilimsihi kwa mabembelezo.


     "Ok. Baada ya dakika therathini nitakuwepo hapo." Alikubali ombi langu, ndani ya dakika therathini Jerry alikuwepo sebuleni tukayajadili.



    """""""""""""


  "Mwandiko huu katika karatasi hii na mwandiko huu katika karatasi nyingine unafanana. Nina mashaka juu ya huyu Bibi yamkini anania mbaya juu ya mtoto Amanda." Nilimwambia Jerry baada ya kumsimulia Kila kitu kuhusu mtoto Amanda, jinsi nilivyomuokota, jinsi nilivyoenda Polisi kuripoti hadi pale niliporuhusiwa na mabwana Polisi nichukue mtoto Amanda na mwisho ujio wa Bibi aliyedai Amanda ni mjukuu wake pia nilimsimulia nilivyoachiwa ujumbe wenye mwandiko ulionitia shaka.


   "Yamkini huyu Bibi ni mtapeli nia yake ni kumuuza mtoto Amanda." Jerry aliongea.


       "Sina imani kama yule Bibi anania ya kumuuza Amanda lakini swali langu ni kwanini alimtelekeza mtoto Amanda makaburini?!" Niliongea.


     "Hukumuuliza?!" Jerry aliniuliza.

     

      "Nilivurugwa Jerry huo muda 🕣wa kumuuliza ningeliupata wapi?"


      "Tusiandike mate wino ukiwepo labda huyu Bibi siye aliyemtelekeza mtoto Amanda." Mume wangu Jerry alijirudi.


 "Kwanini tusiende Polisi kuripoti na kufungua faili 📑 la mashitaka." Nilishauri.


     "Nitakua bega kwa bega pamoja na wewe." Jerry aliniunga mkono. Tulielekea kituo cha Polisi tukatoa taarifa na kufungua faili kumshitaki yule Mbibi anayedai Amanda ni mjukuu wake, Mbibi aliyemtelekeza Amanda juu ya makaburi Kisha kuja kumchukua bila sababu ya msingi. 


       """"""""""""""""

Kesi ilianza kuunguruma Mahakamani , Bibi yake Amanda alijitetea sana na kutuvunja moyo💔 wa kufanikiwa kumrejesha mtoto Amanda. Kila tulipoudhuria Mahakamani Mahakama ilimpa nafasi ya kushinda ile kesi 👨‍⚖️ lakini uzuri sikuwepo pekee katika ile kesi Jerry Alisimama pamoja na mimi kumpinga Bibi yake Amanda 


     Kesi ilizidi kuwa chungu, maswali mazito yaliyotua mbele ya Bibi yake Amanda yalimfanya aonekane ule ushindi alojivunia kupata ungelimdondokea puani. Akasarenda hatimaye akaieleza ukweli Mahakama akasema:


😭😭😭😢


     "Sophi mama yake Amanda alifariki akiwa Leba, alifariki akiwa anajifungua. Bahati nzuri Amanda alizaliwa salama nikamchukua na kuanza kuishi naye kama mjukuu wangu kwa kipindi Cha mwaka mmoja." Aliendelea kuisimulia Mahakama 


     "Lakini ukweli ni kwamba sikua na furaha ya kumlea mjukuu wangu Amanda maana nilihisi mjukuu wangu anauchoma moyo na roho yangu. Mwanangu Sophia amekufa akiwa anamzaa Amanda." Bibi alianza kulia😿😭😢Mahakama haikumuacha mtupu ilimkamua hadi kubaki mifupa, ikamtaka yule Bibi aeleze vizuri, akaieleza.


     "Kifo Cha mwanangu Sophia kiliniachia huzuni na uchungu, Sophia alikua ni Binti yangu wa pekee hakustahiri kufa"😭 Mahakama ilimuelewa.


    "Hakustahiri kufa lakini mtoto Amanda aliisababisha huzuni kuingia moyoni mwangu. Mjukuu alizaliwa pasina mie kumjua Baba wa mjukuu nikaona mzigo umenielemea. Kumtunza kazi na kumlea kazi baya zaidi mjukuu wangu alikua akaniletea kumbukumbu zilizoniumiza na kuuchoma mtima wangu."Aliendelea kujieleza. 


     "Hatimaye nilibuka na wazo lililoniambia siwezi kukaa na mjukuu anileteaye kumbukumbu zinazoumiza mtima wangu, niliona Bora nikamtupilie mbali na upeo wa macho yangu. Nikafanya tendo baya la kwenda kumtupilia makaburini pahali alipozikwa mama yake mzazi." Maelezo ya yule Bibi yaliishangaza Mahakama.👩‍⚖️


    "Wewe ni muuaji, wewe ni muuaji."🤬 Kelele nyingi zilizopigwa Mahakamani zililindimaa, watu walioudhuria ile kesi walipigia makelele.,🔊


        "Naomba nisamehewe ndugu zangu, hata ivyo suala la kumrudisha mjukuu wangu ni ndoto zinazonisumbua usiku na mchana juu yake. Ninaumia, ninateseka na pia najutia kufanya maamuzi yasiyo sahihi."Alijitetea 


Mahakama haikumsikiliza tena, Mahakama iliamuru yule Bibi apokonywe mtoto Amanda. Mtoto alipokonywa Mahakama iliamuru mie Isha nikabidhiwe yule Malaika.👼 Waooo!😘 Furaha isiyomalizika ilinivamia nilipokabidhiwa mtoto Amanda akawa mikononi mwangu Bibi yake Amanda aliachwa akilia kwa uchungu😭 na Bado tu alifunguliwa kesi nyingine, kesi ya kumtupa na kumtelekeza Amanda Makaburini 😁😅 Lazima ajute.😅


*************


     Muda wa kutoka Mahakamani watu wengi walinipongeza kwa roho nzuri na ujasiri wa kumpigania mtoto Amanda. Jerry alikua anaondoka kuwai kazi zake za kiofisi, nilimkimbilia na kumwambia; 

 

 "Karibu jioni ya Leo nitaandaa chakula, tujipongeze na kuufurahia ushindi wa kumkomboa mtoto Amanda. Jerry alifurahia naye alikubali kuja jioni ya Leo.


"""""""""""


Basi mapenzi yangu mie na Jerry taratibu yalianza kufufuka. Jerry mume aliyenitupa zamaani akataka uhuru wa kuishi pekee yake Sasa akaanza kurudi taratibu, taratibu nyumbani kwangu. Amanda ameufanya moyo wa Jerry ulainike, Amanda amefanya mimi na Jerry kupatana, tumekua familia Sasa, sawa tulimpoteza Zuu wetu lakini mola hajatuacha ametukabidhi Amanda wetu.



""""""""""

TCHAO



From Amanda With love 😘💖


""""""""""''





     ."

Friday, March 28, 2025

I love 💕 you Papa

 


Ninakumbuka mtoto yule alianza kama utani, kila niliporejea kutoka kazini nilimuona akiwa amesimama dirishani kwao yaani juu ya Horofa wanaloishi kisha akacheka kitoto toto, sikujali sana Kisha niliingia nyumbani kwangu Horofa ya pili nikamkuta mke wangu anapika na kupakua. Busu zito lilinipokea kwa furaha, akanikumbatia kama anavyonikumbatiaga Kila siku akanipokea makabrasha yangu kwenye brief case Kisha mke wangu akaniambia ' Pole na kazi Dady' Mie ufarijika na kumjibu 'Nimepoa Mamy'

      Naitwa Babiloni au kwa kifup niite 'Babi' Nimeajiriwa katika shirika la ndege Tanzania, mimi ni Lubani. Ninamke ambaye kwa Sasa ni mjamzito. Ni mama wa nyumbani hunipikia vinono na kunipakulia vinono vyenye Sukari na asali. Nimepanga apartment yangu   katika shirika la nyumba la Taifa (NHC) Horofa yangu ipo mita chache kutoka Horofa nyingine inayotazamana na niliyopanga hapo Kila siku mtoto wa jirani unichungulia, unipungia mkono, utabasamu na kucheka kwa furaha

  Tendo la yeye kunipungia mkono sio mara ya kwanza, kufanya mara kwa mara Sasa ni zaidi ya miezi mitatu tangu nimuone akiniona tu utabasamu, upunga mkono na kucheka kwa furaha. Moyoni nilijisemea ni utoto angali Bado mdogo kufahamu mengi siku zilizima na mpya zikazimuka maisha yakaendelea nilipotoka kazini, niliingia ndani kama kawaida  mke wangu Sarafina alinipokea akanipiga kiss la pole na kazi nami nilimrudishia lile la Asante Baby nimepoa akiisha kunipokea mizigo yangu mie huyo nikapitiliza juu ya mazingira ya Horofa Dirisha linalotazamana na Horofa anayosimama  yule mtoto, nikamuona akinipungia mkono na mimi nikampungia mkono akatabasamu, nikatabasamu pia kisha yule Malaika akacheka kwa furaha nikatoweka na kumuacha angali anatamani kuniangalia tena

     "Sarafina, nilimwita mama watoto aliyekua akikaangiza samaki mekoni

     "Abee! Baba watoto." Aliniitikia kwa furaha.

     "Njoo Mama." Nilimwitaji naye alikuja haraka, akakaa 
pembeni ya sofa nililoketi. Nikaanzisha maongezi.

    "Mke wangu nimekuita hapa nikueleze kuhusu mtoto wa Horofa inayofuata, Horofa inayotazamana na yetu."Sarafina mke wangu alinisikiliza.

   "Sifahamu huyu Malaika ana lengo Gani na mimi ni mwezi wa tatu Sasa  Kila nikirudi kazini au nikiwepo nyumbani nikitizama nje ya Dirisha ni lazima nimuone na yeye pia lazima anione Kisha atatabasamu na mimi pia nitatabasamu, atanipungua mkono na mimi vivyo hivyo Kisha kwa furaha yule Malaika atacheka. Kwanini ananifanyia hivyo?" Nilimuuliza mama kijacho wangu.

      "Mbona kawaida mume wangu, kawaida ya watoto, watoto wetu ni Malaika, upenda kujifunza." Mke wangu alinijibu.

   "Lakini Kila siku? Kawaida Gani hiyo?" Nilimuuliza kijingajinga.

     "Babi mume wangu je unahisi huyo mtoto anaubaya kama vile uchawi utotoni? Swali la Sarafina lilinishitua 

     "Hapana sijafikia kuwaza hivyo." Nilimjibu Sarafina mke wangu.

      "Basi elewa huo ni utoto wa watoto,watoto wanakupenda na wewe unatakiwa uwapende." Aliongea wingi.

    "Kweli mke wangu binafsi ninawapenda watoto tumwombe Mola atupe watoto wengi." Niliongea kwa furaha.

      "Ungelipenda tuwe na watoto wangapi? Safina alinitania.

       "Kumi na mbili." Nilitania pia.

        "Yesu! Thenashara!" alishangaa

        "Wa mwisho tutamwita Yuda msaliti." Nilitania.

      'Teh teh teh' Alicheka." Wa kwanza ataitwa Petro. Alitania tena"

    "Nitafurahia." Nilimwambia.

     "Embu ngoja nikimbilie mekoni mboga yaungua."Alisimama pale alipoketi na kuelekea mekoni kuendeleza mapishi.

            """""""""""''''''''''""""""""""
Usiku ulipoingia🌆 tulielekea kitandani🛏️ kujilaza basi katikati ya usingizi niliota ndoto 💭nikamuona yule mtoto tukiwa wawili pekee ndani ya msitu twakimbizana kwa kujificha (Hide and seek). 🏃🏃‍♀️Mara tulionekana tukichuma matunda tukayala 🍇🍓kwa furaha. Mara tulionekana tukiogelea kwenye mto wenye maji safi yaburudishayo mioyo🏊‍♀️🏊‍♂️ yetu. Malaika yule alikua na wingi wa furaha akinishika mikono yangu asitake kuniacha.

    Nilipogutuka usingizini nilijihapia kuwa lazima nitaamkia kwenye apartment 🏘️yao ilinimjue zaidi ni nani haswa yule mtoto ambaye mbali na kunipungia mkono ninamuona ndotoni.

       Asubuhi mapambazuko🌄 nilimweleza mke wangu sarafina juu ya ile ndoto yangu nzuri niliyoiota usiku, katika maongezi yetu nilimwomba mke wangu ruhusa ya kwenda kumjua zaidi yule mtoto, angarau moyo  wangu utulie sio ndotoni nimuone na mwangani nimuone. Ni nani yule mtoto ❓

    Kuwa makini Mume wangu🤔 usijepatwa na baya tambua ile ni nyumba ya watu. "Alinitaka niwe makini.

      "Nitakua makini Daring, l promise nitarudi salama."Sarafina mke wangu alinisindikiza hadi chini ya ile Horofa yetu kisha akaniacha niende nikafanye uchunguzi wangu ili kumjua vizuri yule mtoto, ni nani haswa hadi anitokee ndotoni?"

'Ngo ng'o ng'o, hodi' nilibisha hodi lakini nikajichekesha 😂mimi  mwenyewe kumbe Kuna kengere🔔 ya kubonyeza ili alie ndani asikie. Nikakibinya kitufe Cha kengere iliyolia tiiii tiii tiiiii baada ya dakika chache kupita mlango wa ile🚪 apartment ulifunguliwa. Nilishituka na moyo wangu kidogo nizimie nilipomuona mwanamke ninayemjua.

     Alikua ni Linda, Ex-geri🧍‍♀️ wangu wa zamani, mwanamke niliyeachana naye kitambo nikaanza upya maisha yangu. Linda hakushituka zaidi ya kuniangalia tu. Hazikupita dakika tano yule Malaika niliyezoea kumuona akinitazama dirishani aliingia aliponiona tu alinikimbilia akanipokea kwa furaha mwilini mwake.

      "Waoo! Dady, l love you Dady." 😘🤗
 Nilishangaa kusikia akiniita Dady.

"Dady!" Nilijikuta natamka kwa mshangao. Nisijue yule Malaika anamaanisha nini?

   "Karibu 🙋Babiloni, ingia ndani tuongee." Linda alinikaribisha ndani.

     "Asante." Niliingia nikiwa na shauku ya kutaka kujua ni nani haswa yule Malaika aliyeniita Dady.🧍‍♂️

      "Utatumia kahawa au Tangawizi." Linda Alinitaka nichague.☕🍵

      "Kahawa☕ itanitosha." Linda akaelekea mekoni kuniandalia kahawa ambayo haikuchukua dakika tano alirejea akiwa na bakuri lililojaa vipande vya kashata.

    "Huyu ni mwanao!?"🤱 Nilimuuliza nikiwa naendelea kutafuna vipande vya kashata

    "Ndio ni mwanako pia."Alinijibu nisimuelewe maana miaka mitano iliyopita nilipoachana na Linda hakuwa na mimba 🤰wala mtoto. Vipi Sasa anipakazie kuwa huyu Malaika ni mwanangu? Linda akanisimulia.

   "Babi, tulipoachana miaka mitano iliyopita sikujua kama nilikua na ujauzito wa mwezi mmoja hadi pale nilipopima na kugundua tayari nishanasa ujauzito. Kama ningelikua mwanamke mjinga hakika ningeliishia kutoa ile mimba ila kwa hekima zangu niliiacha nikailea kwa tabu hadi nikajifungua nisijue nitakupata wapi maana wewe binafsi uliikwisha hama Mji.🌇 Aliongea.

     "Babiloni nilikutafuta sana Dear, nilikutafuta nisikupate hatimaye mimi pia nilihama Manzese nikaja kuishi huku llala boma, miezi mitatu iliyopita. Bahati nzuri baada ya kuhamia hapa siku moja nilikuona ukiteremka kutoka ndani ya gari yako 🚗nilitamani kukukimbilia lakini nilipomuona mkeo moyo wangu uliogopa nisije kuivuruga ndoa Yako, nikaacha yapotee. Uzuri nikawa ninakuona mara kwa mara ukiteremka ngazi za Horofa yetu lakini wewe hujawai niona. Nikamwambia Dolla mwanangu yule ni Baba yako, kuanzia siku ile Dolla aisikiapo Gari Yako ikiunguruma ukimbilia Dirishani akikupungia mkono na kucheka cheka.😹😹 Linda alieleza.

     "Duh! Mtoto ninayemuota ndotoni ni mwanangu?!" ⁉️Nilishindwa kuamini nikamweleza Linda sababu ya mimi kuja pale, Binafsi alifurahia. Baada ya maongezi ya takribani nusu saa niliaga na kundoka nikarejea nyumbani kuonana na mke wangu Sarafina. Nilipofika nyumbani nikamweleza Sarafina mke wangu baada ya kisa mkasa. Nikamweleza kuhusu Linda Ex-geri wangu yeye binafsi alishangaa lakini kwa hekima zake akaniambia:

    "Wanawake sisi sio watu wa kuaminika tuna roho za vinyonga, labda Kuna ukweli juu ya jambo hilo. Ninashauri mume wangu uende ukapime Partenity test (DNA) 🧬ili ujue kama ni kweli Dolla ni mwanao au la! Usije ukauziwa mbuzi 🐐kwenye gunia nilimsikiliza Sarafina nikakubaliana na mawazo yake. Asubuhi ya siku iliyofuata nikarejea tena nyumbani kwa Linda mama yake Dolla. Alinipokea nami nikamweleza suala la kwenda kupima DNA, mbona aliwaka 🔥🥵

      "Yaani baada ya kukuambia Dolla ni mwanao na wewe unakurupuka kuniambia kuhusu hayo ma  DNA 🧬 yenu." Aling'aka.🤬

    "Sio hivyo Linda ni kupata uthibitisho kamili na mimi niwe sehemu ya mtoto huyu ili nitoe majukumu yangu kwake."

    "Wanaume mpewe nini ili mtushukuru sisi wanawake!?"Alifura.👿

    "Nikuhakikishie mara ngapi kwamba Dolla ni mali yako?" Alihoji⁉️

     "Embu ondoka tafadhali rejea kwa mkeo." 😤😧😾Alikasirika sana, nilijiona mpumbavu niliyekurupuka lakini siku give up nikafunga safari Moja kwa Moja hadi vingunguti nyumbani kwa mama👧 yangu nikamweleza Kila kitu kuhusu yule mtoto Dolla na kikwazo nilichokutana nacho kutoka kwa mama yake. Uzuri mama alikua anamfahamu vizuri Linda akaahidi kunisaidia na kweli Mama alifunga safari hadi nyumbani kwa Linda huko waliketi na kuongea takribani masaa matatu hatimaye akaniletea majibu safi ya kuuridhisha moyo☺️😺 'Linda amekubali mkapime DNA ili kujua uhakika wa mtoto kama ni wako au la!'

    Siku tatu mbele mie, Linda na Dolla tulikua ndani ya Hospitali🏥👨‍⚕️😷 kubwa ya Muhimbili tukichukua Partenity test yaani DNA. Majibu ya DNA yalipotoka ilionesha asilimia 99.5 Linda hakudanganya mtoto Dolla alikua ni wangu, mwana wangu, mwana niliyemuota ndotoni, mwana aliyezoea kunipungia mkono wa furaha, tabasamu na cheko.

     Tulirejea nyumbani nikamweleza mke wangu Sarafina pamoja na mama yangu majibu safi ya DNA asilimia 99.5 Dolla ni mwanangu niliyempata kwa bahati tu familia yangu ikafurahia na uzuri, wote tulikubaliana kuandaa bonge la party 🎊💃🥳🎈 kuwakaribisha Linda na Dolla waungane nasi


""""""""

TCHAO

💝💕

""""""""""

Tuesday, December 3, 2024

MlSS EVIL




 NILIMKOMESHA MISS EVIL.


      Semeni ndo' jina langu, jina nililopewa na wazazi wangu. Oysterbay ndo' pahali ninapoishi kwa sasa. Mume wangu alichaguliwa na umoja wa mataifa kwenda Haiti🇭🇹 kutuliza fujo na ghasia za Mahaba mia wa huko Haiti kwahiyo nyumbani nipo mie tu pamoja na wanangu wawili Evla mwenye miaka sita na Pedro mwenye miaka miwili.

       Mbali na uwepo wetu sie watatu nyumbani tunao Nyau 🐈😻wawili kidume mwite Marioo na kijike mwite Selenna. Tumejituliza ndani ya hii nyumba yetu mpya tuliyohamia wiki mbili kabla mume wangu hajaenda Haiti kulinda Amani (Niombeeni 🛐📿wangu wa roho👩‍❤️‍👨💞 arejee salama salimini)

       Sikilizeni kisa changu ninachowaletea lazima kiwafunde ujasiri wacheni woga wenu nyie! Baada ya kuhamia nyumba yetu mpya wiki mbili zilopita nilizoeana na majirani wachache wakiwemo Bibi Pili, Dada Maimuna na Bwana Heri Hamduni. Tunaishi private private ingawaje twashirikiana.

Takataka zangu za Nyumba (Waste disposal) Zilijaa full tank, nikaisubiria Gari ya taka iwasili. Mungu mzuri ilipowasili mie Semeni nilijaza viroba vyangu na kuelekea kuvitupa ndani ya Gari ya taka.🗑️🏎️

    "Evla na Pedro jiandaeni tutoke twende Shopping Dears!"  Niliwaambia wanangu waliofurahia ule mtoko maana walijua huko hawatakosa vipipi 🍭vya bure, tu lce cream 🍦🍨twa bure na tududu dudu twa kucheza 🦥🦜watoto🐰🦄🐉🦖🦕🐊🐍🐇. Tulitoka tukaenda zetu Shopper kujumua jumua Viwalo👒👕👖👗 na viatu 👡👞🥿pamoja na mahitaji mengine ya nyumbani.

     Baada ya manunuzi na kuufurahia Mji wa Kariakoo tulirejea Oysterbay Nyumbani. Ilikua ni mchana mzuri wa Jua la saa sita🌥️ Jua lilitupa hamu ya kunywa vitu soft baridi🧊🍸🍹. Mie na wanangu Evla na Pedro tulipofika nyumbani tulipigwa butwaa😱kukuta mazingira yanatisha, hayatamaniki. Ubaraza wangu wote ulijaa takataka nyingi zilizooza na kuharibika. Kulikua na pedi zenye mikojo na vinyesi vya watoto tena zilinuka. Mikate iliyokooza,mifupa na shombo la Samaki na Dagaa ilinuka baya zaidi mlango wangu wa Sebule niliosahau kuufunga kwa bahati mbaya ulifunguliwa na Sebule ilitisha kwa wingi wa takataka, karatasi, pedi, mifupa ya samaki, makopo ya biadhaa za viwandani na kadhalika. Niliogopa na kushangaa 

      "Mama Nyumba inanuka."Evla  mwanangu mkubwa aliongea.

    "It's ok Daring, nitaisafisha " Nilimjibu mwanangu Evla aliyeiziba Pua kwa kutumia madole ya mkono wake. Pedro wangu alijificha mgongoni asiuone uchafu ule. Niliwakuta Nyau wangu wameketi Sofani wakishangaa.

     "Mpuuzi gani amenifanyia hivi!?" Nilijiuliza haraka mie na wanangu tulitoka nje na kwendraa kujaribu kuhoji majirani ni mtu gani aliyelitengeneza jambo Ovu kama Lile!?

     "Pole sana Dear! "Bibi Pili alinifariji nilipoenda kwake kuuliza

     "Aliyekuchafulia nyumba si mwingine bali ni Miss Evil, yule Dada yupo very wicked, anachukiza." Nilimsikiliza Bibi Pili.
    
    "Yule Dada ni mchawi tena mwogope kila mtu hapa Oysterbay anamwogopa , hasogelewi." Bado nilimsikiliza.

      "Ana kawaida Moja ya kunusa nusa na kupeleleza ajue ni nani aliyehama au aliyehamia nyumba mpya na baada ya ugunduzi wake atafanya uovu wa kumwaga Takataka ndani ya nyumba ya huyo aliyehama au aliyehama." Bibi Pili alinisimulia.

      "Nakusihi usijaribu kumsogeleea sababu huyo ni Mlozi na mrogaji. Ukimkorofisha anakuroga unageuka na kuwa kipofu au kiziwi." Bibi Pili mwenye kadirio la miaka themanini alionesha hofu yake.

     "Bibi jambo hili niachie mimi wewe mwenyewe utakuja kunishukuru mara baada ya kumfanyizia huyo Miss EVIL." Niliongea pasina kupepesa macho.

     "Mjukuu wangu we huogopi!?" Alitia hofu

     "Hadi asame!" Niliongeza Msamiati.

     "Ubaya Ubwela... Kisa mkasa." Nilifanya kuondoka nyumbani kwa Bibi Pili mtimani nimeshiba mahasira yenye hasara.

    "Huyu Miss Evil ndo' nani atakaye kumjua mke wa Mwanajeshimpiganaji?" Niliongea pekee yangu.

      "Lazima nimfunde ili siku nyingine awaheshimu wenyeji na wageni!" Nilijiambia

       "Uchawi ndio Nini? Ina maana mtu anakuja kuchafua mazingira ya wengine ili tu aogopwe kwa sababu ni mchawi?" Nilijiuliza.

     "Sasa ngoja ataniheshimu." Nilitoa kiapo mie Semeni nlikatoka na kwenda kununua magunia mwawili makubwa yaliyoshiba. Baada ya kununua yale magunia nikaanza kupita nyumba moja baada ya nyingine kuhoji jirani zangu:

     "Nipe vinyesi vyote, vinyesi vya Umbwa, Nyau, Ng'ombe, Nguruwe na hata kama ni vya watoto wadogo nipeni" Nilidai. Majirani wakishangaa lakini pasina kuhoji walianza kunipa mioyoni mwao walihisi nimerukwa na akili..... Sio kwa hasira zile nilizotembea nazo.

     "Nipeni tafadhali, nipeni. Baada ya dakika Harobaini na Tano ninaomba mje nyumbani kwangu muone ubaya ninaotaka kumtendea Miss Evil " Walipolisikia jina la Miss Evil, Mchawi wanayemeuogopa pale Oysterbay. Yule mchawi ambaye hajaolewa zaidi ya kuishi Single sister walistaajabu na tena walitamani kujua nini kinaenda kuiva huko?!

      Mie Semeni nikayapakia magunia yangu mawili yaliyojaa vinyesi kunako Toroli Kisha nikayaburuta hadi nyumbani kwangu, huko nilijua mie mwenyewe ninaenda kufanya jambo Gani?
 
       Babaye Evla alinifunda kutengeneza Baruti za kurusha kwa mikono kupitia ujuzi ule nikafanya hima kufungasha vinyesi ndani ya mifuko midogo yenye umbo la duara kisha vile vifungasho vyenye kinyesi na umbo la Baruti nikaviweka ndani ya Magunia na kuvipakia ndani yaToroli muda si mreefu majirani wakaitana na kutimia ishirini na wote wakanifuata nyumbani wakiwa na shauku ya kutaka kujua naelekea kumtendea nini adui wa wageni Miss Evil.

      "Twendeni." Niliwaamuru wakanifuata kama Umbwa na mkia wake wamejaa shauku na kiu ya kutaka kujua nini naekekea kumtendea Miss Evil yaani ni ubaya na ubwella. Nyumba ya Miss Evil ilikua ni ya sita kutoka nyumba yangu, tulifika nyumbani kwake.

    'Knock! Knock! Knock' Nilibisha hodi mara tatu nyumba ya Miss Evil bila woga bila wasiwasi, majirani kundi zima walitazama  lango la Miss Evil. Alifungua mlango hapo ndipo akakutana na macho yangu. Mie nilitegemea kukutana na kipipa furani chenye sura ya Simba dume, kumbe wapi! Kile chifupi chikondefu ndicho kinachoogopwa na watu wote pale mjini.😆😅

       "Eeh! Bibi naomba maelezo unieleze kwanini umefanya uamuzi wa kwenda kumwaga takataka zako barazani na sebuleni kwangu?" Nilimuuliza yule chifupi cha Umbwa.

       "Sasa kama nimemwaga barazani na sebuleni kwako unataka kunifanya Nini? Aliniuliza kijeuri akiibetua midomo yake.

    "Umepata Nini chenye faida baada ya kumwaga takataka zako nyumbani kwangu na kuichafua nyumba yangu?" Nilihoji.

      "Ndio utamaduni wangu lazima Kila mhamiaji aonje taka na Kila mgeni lazima aonje taka." Alijibu kipumbavu watu wakamshsngaa.

     "Wewe pia unahamu ya kuonja taka?" Nilimuuliza moyo ukiniambia mrukie huyo, mponde huyo hadi asagike mifupa. Uzuri roho iliniambia mwambia mwaibishe apate onyo na fundo. Hakunijibu, basi nikamvamia na kumsukumia pembeni akaanguka chini puu! Kama gunia la mama, Nikaingia sebuleni kwake nikayatoa yale mabomu ya baruti kunako ile mifuko miwili mkubwa niliyokua nayo. Nikaanza kurusha yake mabomu ya baruti yaliyowaogipesha watuwote pamoja na Miss Evil.

     Sikukomea hapo Bado tu nikiendelea kuichafua nyumba yake kwa milipuko baruti zenye vinyesi: jiko lake lilichafuka,masofa yake yalichafuka na tena yaliunguavpasina kuteketea, Sebule yake ilitapakaa vinyesi ilitisha na kuogopesha. Nilitamani kufanya umafia ndani ya chumba anacholala sema roho iliniambia Sasa tosha. Nikatoka nje na kuwakuta majirani wote a Moja na Miss Evil wanaogopa na kutetemeka. Mkononi nilishika bomu lenye baruti yenye kinyesi nikamsogelea Miss Evil aliyeanguka pale chini akishangaa kisha nikakwambia.

     "Huu ni mwanzo, lwapo nitakuja kusikia kesi yoyote ile inayohusu nyumba ya mgeni au mhamiaji, imetibuliwa na kuchafuliwa na uchafu wako ninakuapia nitayazoa mapipa ya vinyesi chooni nije nipakaze kuta za Nyumba yako. Mpuuzi mdogo weye" Nilimnyoshea madole na hasira zilinikamata. 

Alitetemekatetemeka, akashindwa kuongea tena jeuri zake.

      "Ita Polisi kama unataka" Nilimwambia Bado alikua akitetemeka. Nikaondoka nyumbani kwa mwovu yule kadamnasi ya watu walinisindikiza, wakipiga makofi, vifijo, nderemo na shangwe.

      "Semeni mjukuu wangu wewe ni Jasiri." Bibi Pili alinipongeza.

       "Kwangu wewe ni Legendary hajapatikana mtu mwenye moyo wa kishujaa kama wewe." Bibi Pili aliongea tena.

      "Umemuangusha Goliath yule lnzi aliyepigwa kwa kinyesi." Bibi Pili aliichekesha hadhira. Tuliondoka eneo la Miss Evil tukiwa ni wenye wingi wa furaha. 

Nakuambieni huu ni mwaka wa pili Miss Evil hajapata kufanya upuuzi aliozoea kuwafanyia wageni. Ametulia kama sio yeye aliyekua akiogopwa kwa Ulozi.

...................

TCHAO  🖐️🦇🦉🐾🎃🎭



 love is all Given and found,🌹 It's all around,🥰 It's hard to tell about,😍 Easy to show,🤩 One sure thing when you feel it You kn...