Friday, August 8, 2025

ZEE LA ZAMANI

 



SEHEMU YA KWANZA.


HOTELINI


Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JANE wameketi wanapiga Soga, vinywaji baridi juu ya Meza vinasuuza koo zao. Zee anamshawishi Jane, Moyoni Jane anasuasua kumpatia jibu Mwalimu Zee. Ghafla BRAZA JERO akaingia ndani ya Hoteli Paradiso, aliwaona vizuri wale wawili wanaojadiliana kuhusu mapenzi. Jero akajibanza kunako kona moja ya ile Hoteli pasina kuonekana, yamkini Braza Jero anawafuatilia kwa udi na kwa vumba. Sijui kwanini? Tutajua mbele ya Safari.


            “Kama ni kukupenda usiusamehe Moyo wangu Jane, Moyo haujafanya kosa kukupenda sababu kupenda sio kosa kila Mwanadamu ana Haki ya kupenda na kupenda huko Mwanadamu mwenye tamanio la mapenzi humchagua yule wa kumpenda sababu hiyo nimekupenda sana Jane.” Zee lazamani alimchombezea mtoto Jane, Kinda sawa sawa na mwanaye wa kumzaa.


            “Akah! We Zee mie bado Kifaranga sihitaji kuyaharibu Maisha yangu.” Jane binti wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Benjamini alijishaua mbele ya Zee lazamani.


            “Waogopani? Je, waogopa ati utatimuliwa Shule? No no no, Jane hakuna wakukutimua kama vumbi pale Benjamini.Tafadhali niamini mimi, mimi ndio Zee lazamani Mwalimu mkongwe wa wakongwe, Mwalimu mkuu wa wakuu, mtetezi wako, pendo lako na Sabuni ya Moyo ukichafuka. Sidhani kama kuna mwingine zaidi ya mie.” Zee alijigamba.


            “La, hasha! Siogopi kufukuzwa pale Benjamini, binafsi sina interesting ya kuendelea na masomo sababu siyapendi nafanya kulazimisha tu ilimradi kulisukuma Gurudumu liende kama vile Ng’ombe apelekwaye chinjioni. Hofu yangu ni kuingia penzini na matokeo ya kuingia penzini ninayajua mie.” Jane alijifarangua akionesha sura iliyojaa wasiwasi na woga kwa mbali.


            “Mie ndiye Mlinzi wako, Malaika mwema, ninaahidi kukulinda. Sema je, wanipenda? walipokea ombi la Mtima wangu? Tuanze kuyadumisha mapenzi yakadumu na kudumika, tupendane daima.” Zee akagugumia funda mbili tatu za kinwaji chake baridi akaachia tabasamu na kufurahia.


            “Moyo wangu bado haujahamasika, sioni kama umenishawishi nikashawishika au labda ningerejea tena masomoni, uniache nitulie nisiyafikirie sana mapenzi, nirejee Darasani nikajikite ndani ya dimbwi la masomo.” Jane alichanganya maneno.


            “Wanipa muda tena!? Je, ninapaswa kukusubiri umalize Kidato cha Nne? Miaka miwili ni muda mrefu sana. Mmmh!” Zee aliongea kwa sauti ya deko na miguno.


            “Mwalimu mpenzi, sioni baya sababu mvumilivu hula penzi bivu. Je, una shida nyingi zinazousumbua Moyo wako? Mke unaye, Bi. Mkubwa. Hawara pia unaye na mie Jane wanitaka niwe miongoni mwa wakezo? Huna haya weye, ‘mfyuuuu.’ Jane akambitulia domo Zee lazamani.


            “Watakaje kwa mfano? Je, utaniruhusu nimuache Bi. Mkubwa ili nikuoe weye? Au nimteme na kumtapika Hawara wangu ili niwe na mtoto nyanya, mchele mchele kama weye? Tambua nina haja ya kuishi nawe ili nikurithishe Mali na fahari za uzee wangu. Nina Mali nyingi sidhani kama waweza kuzikadiria kwa siku moja.” Zee alitoa kiapo Jane akacheka pasina kujua kuwa Braza Jero anayasikia maongezi yale Jane akanena.


            “Sijataka Mali zako Mwalimu, sijakushauri unipe Mali, hayo ni maamuzi ya ghafla. Ningependa nikuombe uniache kwanza ili nitulie masomoni niitafute elimu na mafanikio yanifuate.”


            “Ninakusikiliza lakini ninaomba wewe pia unisikilize tulianzishe penzi haba haba, ndo! Ndo! Ndo! Mdogo mdogo taratibu tutafika.” Zee alijaribu tena kuitupa Karata yake kwa huyu Binti wa kumi na saba.


            “Ni bora niyaogope mapema Zee langu. Nijuavyo mie Mwonja Asali haonji mara moja ataonja tena na matokeo ya lamba lamba ni kulichonga Gogo la Asali. Mie ninaisikiliza vema sauti yako lakini nawe pia yaheshimu sana mawazo yangu.” Jane aliongea Zee alishindwa kuendelea kunena, aliyapima maneno ya Jane yakapimika. Kwanza maneno ya Jane yana msimamo legelege pili maneno ya Jane yanayumbayumba, hapo ndipo Zee aligundua Jane anafeli. Mtimani Zee alikuwa akiyatengeneza maneno ambayo kwake binafsi alihisi yatamchochea na kumshawishi Jane aingie kwenye Hamsini zake.


Kama ni suala la uharibifu Zee amewaharibu sana Mabinti wa Shule, amewarubuni na kutumia kila aina ya vishawishi, vizawadi na pesa zake za Posho. Kwa muda ule mfupi aliweza kumsoma Jane, alimsoma kama Binti aliyekubali ingawaje anayachanganya maneno. Anadhiirisha kuwa amekubali ombi lake na wakati huo huo anakataa kwa visingizio kedekede viso na nguvu ya kuyashinda maneno ya Zee.


            Braza Jero akiwa amejibanza Koridoni asionekane na Mtu akaiwasha Kamera ya Simu yake, Samsung Galax 7 akapiga Picha mbili tatu, Moyo wenye wivu ukamfunika, akajisika gere. Je, atafurahia vipi akimuona Jane wa Moyo wake akipangiwa mipango dhalimu na ya kulichuja penzi lao? Jero akachukizwa na yale maongezi aliyoyanyaka. Naam, Jero alifanikiwa kupata picha halisi ya kila kinachoendelea miongoni mwa Mwanafunzi na Mwalimu wake. mmoja akishawishi ili apate yale anayotamani wakati mwingine akiyakataa mashawishi ingawaje anaonesha dalili za kuyatamani hayo mashawishi. Basi Jero akalitega sikio lake asipitwe na maneno.


            “Utanifurahia nikileta Posa nyumbani kwa Baba na Mamayo?” Zee aliuliza.


            “Jamani Mwalimu, mbona papara!? Wamaanisha umedhamiria kunioa kabisa!?” Jane aliuliza kwa mshituko kidogo.


            “Sikutanii mtoto nimekupenda, uzuri wa umbo lako na mabadiliko ya mwili wako ni moja ya vitu vinavyo nishawishi na kunihamasisha nikupende.Wacha nifanye hima nisichelewe sababu Waswahili wanasema chelewa chelewa wakuta Kuku sio wako.” Zee aliongea na kucheka.


            “Mmmh!” Jane aliguna akanyanyua Bilauri pale mezani akagugumia funda moja taratibu kwa madaha, akaitwaa Tishu akafanya kuyafuta mabaki ya ile Sharubati mdomoni.


            “Katika mapenzi umbo la nje na mwonekano wake ni vitu ambavyo vinaushawishi mkubwa kuliko umbo la ndani ambalo ni Moyo.” Zee aliongea kipuuzi.


            “Sio kweli Zee wan’danganya.”Jane alimkosoa Zee.


            “Nakudanganyaje? Embu nieleze nikuelewe ili nami nipate kufafanua maana ya kauli yangu.” Zee alimpa Jane nafasi ya kujieleza.


            “Moyo ndio wenye nguvu na ushawishi mkubwa mapenzini, mwili umejaliwa tamaa. Kwa maana hiyo Moyo huanza kupenda mwili hufuata matakwa ya Moyo. Je, umenipenda Moyoni au umenitamani mwilini?” Jane hakumpa nafasi Zee ajieleze badala yake akamuachia swali ambalo Zee hakulipatia jawabu stahiki.


            “Nisikilize Jane umbo la nje ni zaidi ya matamanio ya Moyo, umbo la nje linabeba na kukumbata Sura nzuri yenye umbo la Yai ling’aaro kama Taa, Ngozi nyororo yenye rangi ya Dodo lililoiva, Macho ya Kungu yanayomvuta Mwanaume tamaa. Ujaponitazama ninayaona mapenzi mazito yenye rangi ya Dhahabu iliyokooza. Umejaaliwa kinywa chenye maneno yanayomtoa Chatu Pangoni, Shingo ndefu ya Twiga mbungani kiuno bila mfupa hicho ni kiuno cha Nyingu jike, tumbo jema bichi lisilochoka na kuchosha, mapaja mazito yaliyonona na kutononoka kama nyama nono ya Nguruwe bado sijakusifia Makalio yako yanesanesa kama Tanda la Banko, haki! Mbona Mtoto wanitamanisha Mie…… Uwii! Nimesahau kukusifia chuchu zako bora kama Zabibu na Divai. Basi Mrembo usinipe tabu nikachoka, fanya kuniruhusu niingie Mtimani nitalii vigeni vilivyo ndani.” Zee alimmwagia sifa Jane, Jane akacheka na kuchoka.


            “Ungali bado haujanijibu swali langu. Je, umenipendea mwili au umenipenda pendo la Moyo wa dhati? Zee akaona isiwe tabu ngoja amjibu mtoto Jane.


            “Wataka nirudie kunena? Nipo tayari. Basi nikueleze, mie nimekupendea pendo la nje, penzi la mwili na matamanio ya raha za kimwili ndiyo shida yangu kuu. Macho hayana pazia kionekanacho wazi ndicho kinizuzuacho Machoni hata nishindwe kula au kulala. Ninasema kweli siwezi kupenda visoonekana sababu mie sio Jini mie ni Binadamu mwenye mapungufu na madhaifu yangu.”


            “Mmmh! Sawa nimeilewa nia yako Mwalimu Zee hauna haja ya kunipenda mimi wataka penzi la kunichezea na kuniacha kapa mwenye hasara isiyoweza kubebeka.” Jane alionesha wazi kuchukizwa na kukasirishwa na yale maneno ya Mwalimu wake akanyanyuka Kitini na kutaka kuondoka.


            “Umewaza tofauti Jane.”


            “How come? Kivipi?”


            “Uhalisia wa mapenzi ni kuchunguzana ili hapo baadae wawili turidhiane. Hivi je, bado haujaona ninavyokuchunguza mwendo na mwenendo wako? Acha niseme tayari nimeridhia ndio maana matamanio yangu ni kuleta Posa nyumbani kwa Baba na Mamayo haraka iwezekanavyo ili ukimaliza Kidato cha Nne nikuweke ndani, niwatimue wale Wanawake Wazee na wachovu Mahabani, nikupe miliki na urithi wa wanangu, nikupe raha na fahari zote unazozitamani.” Maneno yale yalimfurahisha sana Jane akatabasamu tabasamu lake zuri kama Uaridi likampendeza Zee.


            “Nayafurahia maneno yako basi acha niondoke, Jumamosi ya Leo imekuwa ni siku njema kwangu yamkini nitalala na kuamka vema. Maneno yako yameanza kupooza hisia zangu mbaya juu yako.”


            “Usinichukie Mtoto Jane, basi niambie ni lini tena tutatapata nafasi ya kunena mazuri kama haya? Je, waniacha upwekeni nilikose busu lako shavuni ili mie nijisikie kweli wanipenda?” Zee alimbembeleza Jane, Jane akatabasamu.


            “Jumamosi twaweza kukutana Mikadi Beach, Kigamboni. Busu langu kamwe sikupi hadi siku utakaponitolea Posa, hatua itakayofuata ni kufunga ndoa na Sherehe kubwa ya bei gharama itadondoshwa, tule, tunywe, tusaze Majogoloo.” Maneno ya Jane yakamfurahisha Zee, Zee akamshuhudia yule Tausi mwenye maringo na madaha akijongea na kupotea mbali na peo za Macho yake. Zee akaendelea kunywa kinywaji chake kwa taratibu, Moyoni akijipongeza sababu Ndege mzembe hunasa mtegoni.


 Itaendelea



I MISS YOU CHUGA

 CHOMBEZO: I MISS YOU CHUGA



SEHEMU YA PILI


(ILALA DAR ES SALAAM)


       Nikarudi chumbani nikamkuta Jerome amelala mie sikutaka kulala sababu nilitibuliwa na mawazo lukuki juu ya mchepuko wangu Obi basi nikafanya hima hima kuzikusanya nguo chafu za mie na Jerome nikaelekea kuzifua Faster faster mawazo hayaishi juu ya Obi mchepuko wangu nilipomaliza kufua nikakusanya vyombo vichafu nikavikosha na pia nikapuguta deki faster faster saa moja juu ya alama kazi zangu zote za pale nyumbani zilifikia tamati.


Jerome tayari alikwisha kuondoka akaelekea kazini kwake Posta, anabiashara zake, kwanza anaduka moja kubwa anauza simu za kila gharama, pili ana duka lingine kubwa la vipuri vya magari, mie na Jerome hatunaga shida sema bado tunakaa uswahilini sababu Mzee baba (Jerome) anafanya kujenga nyumba yetu sie wenyewe huko CHANIKA nje kidogo na mji wa Ilala. Mie na Jerome hatunaga shida sababu pesa ipo na uzuri wa pesa Jerome ananikatia kingi, na ubaya wa mie Sonia hicho kingi ninampatia Obi Mchepuko wangu. kutokana na mazoea ya kumpatia Obi pesa mingi, Obi amejenga tabia na mazoea ya kuni ‘distrub’ ati nimpe zaidi na zaidi nikimyima pesa nayeye ananinyima penzi lake tamu kuliko asali.

Alright, mie nilipomaliza kazi za pale nyumbani, Sharifu shamba, nikatoka na kuufunga vizuri mlango wa chumba chetu kimoja tulichopanga hapo Sharifu nikawaaga majirani zangu, jamani eeh mie ninatoka sintakawia kurejea.

Bajaji ilinidondoshea hapo kituo cha Polisi Pangani, nikafanya faster kumlipa dereva mwendesha Bajaji, nikaingia ndani ya kituo cha Polisi Pangani nimebeba pesa za kutosha angarau moyoni nilijisemea wakihitaji Pesa ili Obi atoke hapo kituoni nipo radhi kuwapa kidogo kidogo.


“Hallow, Aunty habari yawewe, pole na majukumu yote,” nilimsalimia Polisi wa kike, ameshiba vizuri yule mwanamke mwenzangu weupe wake amenizidi, mzigo huko nyuma nimemzidi, kazisuka vizuri nywele zake, ana miwani machoni, yupo kuandika andika ndani ya daftari la kuandikia kesi zinazoletwa pale kituoni.


“Habari ya mimi nzuri, kimajukumu nimepoa, nikusaidie nini Aunty?”


“Ninashida Aunty, kuna mtu wangu wa karibu anaitwa Obi, nimepigiwa simu alfajiri ya leo nimeambiwa amekamatwa, ana kesi ya kujibu, hivyo nimekuja kusikiliza Tatizo lake nini haswa?”


“Ok Auny embu nipe dakika sifuri nicheki cheki kwenye Buku la kesi ili nijue tatizo la mtu wako wa karibu, maana mimi nimeingia shift muda si mrefu, kesi kama hii iliandikwa na Askari wenzangu waliokuwepo ‘On duty’.” Yule Aunty alichukua daftari lenye kesi za watuhumiwa mbali mbali akaanza kulitafuta jina la Obi Mchepuko wangu akalipata, akanisomea kesi ya Obi kisha akaniambia.


“Jana usiku yapata muda wa saa tano, Obi alivamia chumba cha Bi.dada mmoja jinale Rehema, Bila ruhusa Obi aliingia, Jirani walimuona. Na kwa sababu muda ule Rehema hakuwepo nyumba Jirani walihisi Obi ni mwizi, hivyo wakamvamia mule chumbani na kumtoa nje, Jirani wakamhoji Obi ana shida gani kuvamia chumba cha mtu ambaye hayupo ndani?”


Mmmh! Maelezo yale yalinitia wivu,nilihisi Obi tayari kampata demu mwingine, kwanini avamie chumba cha mtu usiku? Mtu mwenyewe hayupo, je Obi na huyu Rehema wana mahusiano gani? Sikupata jawabu la moyo wangu, Askari aliendelea kunena.


“Aunty inasemekana kuwa Rehema aliupoteza ufunguo wa chumba chake, ndio sababu ya Obi kuingia na kuvamia, ile anatolewa ndani ya chumba cha Rehema Obi alikuwa amelewa chakali, akatumia Lugha chafu kuwatusi wale watu waliomlazimisha kuondoka.”

“Nimekuja KUMF*****Rehema, sina shida na nyinyi, embu niacheni Choko nyie.”Askari aliongea kama vile nayeye alikuwepo mbele ya tukio.


“Bwabwa nini wewe? Unamwita nani CHOKO, wewe ni Jambazi, huwezi kuingia ndani ya ya chumba cha mtu bila ruhusa,” Majirani walimpigia kelele Obi ambaye bado pombe zilimtawala.”


“Nasema sitoki hadi nimfir* Rehema, umbwa nyie msiniharibie Starehe yangu.”


“Nani umbwa? Tumevumilia sana matukano yako, sa’ ngoja tukuoneshe kuwa jeuri yako si kitu. Ghafla majirani wakamshambulia Obi, wakamponda vibaya mno nayeye alivyo jeuri akawarudishia vipondo vyao, mapigano yao yalisababisha Obi aletwe kituoni.”


Oooh! Masikini, hisia zangu zilikuja kuwa kweli, kumbe Obi ana demu mwingine zaidi ya mie.’Mfyuuuu’ nikafyonya kwa hasira. Si bure nimuache tu afie Jela ili huyo Rehema aje kuuzika mzoga wake.


“ Naweza kumuona Aunty?” Nilihitaji kumuona Obi.


“No problem keti hapo kwenye Siti nipe dakika sifuri, Obi atakuwa pamoja na wewe,” Askari aliongea akaenda ‘Cello’ chumba kimoja kidogo ndani y a kile kituo, akafungua mlango wa hicho chumba kisha akaita jina la Obi, Obi akaitikia Askari akamwambia ‘nifuate’,


 Obi akamfuata. Lo! Nillipomwona mchepuko wangu, nilimuonea huruma kwa jinsi alivyo onekana amevimba mwili mzima, damu iliyogandiana mwilini imegandiana pia kwenye nguo zake. Haki Obi alipewa kipondo cha kufunga mwaka.


“Obi pole Mpenzi,” Nilimtia faraja zile chuki za kumchukia Obi ati sababu ampata bibi mwengine ziliyeyuka zikanitoka na kupotea, nikatuliza moyo, huruma na machozi juu ya mchepuko wangu.


“Asante Mpenzi,nimepoa.”


“Obi kwanini unanifanyia hivyo Sweet heart.” Nilimfuta futa Obi damu zilizogandiana mwilini kwa kutumia kanga yangu Moko.


“Nisamehe Sonia, nisamehe lavu pombe, ilinitawala”


“Mbali na pombe kumbe Obi unaye demu mwingine?”Niliongea kwa hasira kidogo.


“ Ni pombe Sonia, ni pombe lavu, pombe zilinipitia. Naomba nisamehe, sintarudi, Obi alinisihi akiwa anatia huruma kibao Usoni.


“ Sonia fanya juu chini mie nitoke hapa kituoni, Umbu wananing’ata balaa.” Obi aliongea.


“Nikikutoa sitaki kusikia habari za huyo Rehema, mwambie nitaua mtu mie nina wivu wangu mwenyewe, sikubali kuibiwa kizembe.” Nilimuonya Obi, Nikasimama pale tulipoketi nikaelekea Kaunta niongee na Polisi yule demu mrembo haswa


ITAENDELEA

MWENZENU N'SHAPENDWA


MWENZENU N'SHAPENDWA 



Sehemu ya tisa (Mwisho)


     "Nina kuua mwanamke wewe, ninakuaa unieleze kwanini unipokonye mume wa moyo wngu," Maua alinikimbiza mie pia nilikimbia pamoja na ujauzito wangu. Pindi Maua ananikimbiza ndio mabadiliko mbali mbali yalitokea mwilini mwake, kichwa chake kiliota pembe mbili ndefu kama kama za Ng’ombe, meno yake yale madogo yakawa marefu kama pembe za mbuzi, kucha zake zikaongezeka zikatisha zaidi, Maua akaongezeka urefu akawa mrefu tena mrefu zaidi.

        
      “Mwenyewe ulimkataa sasa wamtakani?” niliongea kwa ujasiri nimedondoka chini ya aridhi mara baada ya kukimbia na kuchoka.


           “Sijali maneno uyasemayo ninachojali ni kumrudisha Pompo wangu. Nasemaje utamrudisha Pompo mikononi mwangu au hautamrudisha?” Safari hii mdomo wa Maua ulikuwa ukitema damu, niliogopa mie, niliogopa hali ile, niliogopa sana, kumbe Maua ni Jini, lo! Ama kweli leo nimepatikana.



          “Kamwe, Pompo haumpati tena usijisumbue bibie, acha nijilie vyangu, mwenzio n’shapendwa wewe endelea kukonda na kudhoofika.” Nilimjibu Maua ambaye alizidi kunisogelea pale nalipokuwepo anatisha kweli, nguo zake kuukuu kama vile mfu aliye fufuka muda si kitambo.



           “Wanijibu jeuri si ndio, sasa nataka nikuue wewe na mtoto wako ili nimpate Pompo wangu Maua alinitisha alinitisha zaidi tena zaidi sana. Nikasikia miungurumo ya radi, mvua ilianza kunya taaratibu tna kwa ghafla.


         “Ninasema hivi mie sifi, Pompo hafi wala mwanangu, kama ni kufa utakufa wewe mwenyewe tena utakufa kifo kibaya kifo cha kugongwa na gari. Nilimtolea kiapo Yule mwanamke mwenzangu.



           “ Umbwa wewe mwenye bahati, mie ningelijua nibora nisingeli muacha Pompo wangu,tamaa na starehe za dunia ndizo zilizo niponza. Ona mwanamke mwenzio mie leo ninajuta.” Jini Maua aliongea kwa kusikitika.



         “lwe fundo kwako na kwa wenzio, iwe fundo kwamba umpendaye mpende, akupendaye usimuache solemba, haijalishi ana maisha ya kikabwela, ana ulema au ulemavu, kasoro, hali ya umasikini au utajiri. Mpende kiroho safi na uzuri wa mapenzi Mwenyezi Mungu atajalia.leo hii Mume wangu kaanza kuusimamisha mjengo wa Horofa tatu na wewe kimburukutu fukara umeanza kuutamania, leo hii Mume wangu kanunua Tax gari yake mwenyewe weye mjaa tama umetamania, nakwambia hivi mazuri mengi yanazidi kutufuata.” Nilijigamba


          “Ndo’ maana waswahili wanasema yajayo yanafurahisha, ulimdharau, yule muuza kahawa, mzibua vyoo, mwosha magari, muuza pipi na karanga, msukuma guta, fundi mjenzi asiyechagua. wala kubagua kazi, leo hii amefika mbali kimaisha ndio weye mjaa laana umtake.” 👌🙊 Niliongea kwa kirefu, Maua tayari alikwisha fika magotini kwangu ananitazama kwa hasira, macho yake yalikuwa yakiwaka moto, mvua nayo haikukoma, hakika siku ile niliyatimba mtoto wa kike, kifo kilikuwa karibu yangu, lakini yote tisa kumi mie nilijitetea.


        “Tukubaliane jambo moja," Maua alionge amejaa tamaa ya kunipoka roho wangu.


         “Kuniachia Pompo wangu au kufa kwa ajili ya Pompo wangu.” Jini Maua aliongea na mie nikamwambia.


         “Sikia Maua, tukubaliane jambo moja, waniachia Pompo wangu au kufa kwa ajili ya Pompo wangu,”


           “ Teh teh teh,😅😅 aaah!” Jini Maua alicheka sana, damu zikimtoka mdomoni radi ikapamba moto. Mie nikaogopa zaidi nikatetemeka tetemeko kuu.


          “Unajitia jeuri au sio , nilikwisha kuambia mie ndio Maua mtoto wa kizaramo, nimezaliwa uzaramoni nimekulia uzaramoni, nimefundwa nikafundika ninafanya kwa kadri moyo wangu unavyonitaka nifanye.” Maua aliongea kwa hasira.👿


            “Na mie nilikwambia mie ndiye Mamsapungo toto la kitamga , nimezaliwa Tanga, Lushoto ndio nyumbani kwetu, nimefundwa nikafundika, Mapenzi ninayajua tena mapenzi ninayaweza, thubutu jaribu kushindana na mie ili uone kuwa sinaga utani na mtu.” Nilimjibu Maua


           “Sasa ninakuchagulia kifo kama komesha yako, Maua alinitisha zaidi, ingawaje nilipoteza matumaini lakini nilikuwa na moyo wa imani na ujasiri wa kuokoka, Mungu alibaki kuwa tumaini langu.


             “Sifi wala nini kufa utakufa wewe usiyeyajua mapenzi, usiyejua uvumilivu tena usiyejua nini maana ya kupenda.” Nilimnanga adui yangu.


Mara ghafla –pasina muda kupoteza Jini Maua alikinyanyua kile kisu chake chenye makali kuwili, Mola we Uwii! Alikitua katikati ya tumbo langu pale alipolala mwanangu mtarajiwa, maumivu, maumivu makali maumivu ambayo sijapata kuyaona, Maua akaachia tabasamu, tena akacheka kicheko kikuu kicheko chenye makali ya radi, Mie nikapiga ukelele mkuu.


            “Mama nakufaaaaa”🔊😭😭😭


            “Mamasapungo, Mamsapu, Mamsapu…….” NILISHITULIWA NA SAUTI YA Pompo roho wangu, nikashituka shituko kuu, macho pima kama Jusi 🦎 aliyebanwa mlangoni, nikiangaza huju na huko nisijuwe nipo wapi hapo.


             “Pompo nipo wapi hapa.” 😶‍🌫️Bado fahamu hazikurudi kiwepesi.


              “Upo nyumbani, nyumbani Kigamboni, mama wa moyo wangu.”


              “ Mbona damu sizioni tumboni kwangu,” Nilijikagua kagua sehemu ambayo nilisadiki kuwa Maua kanichoma kwa kile kisu chenye makali kuwili.

                “Ni ndoto Mamsapungo, ni ndoto moyo wangu, ndoto ndiyo iliyokufanya uweweseke.” Pompo alinifungua milango ya fahamu. Mara kwa ghafla nikaanza kusikia maumivu ya tumbo, ni uchungu, uchungu wa ghafla uliotokana na kushituka, shtuko kuu shituko lililotokana na ile ndoto yangu ya usiku ule mzito wa manane.


                 “Pompo maumivu, uwiii…..Maumivu….ya tumbo.” Nalianza kulia, nikijishika urwanda rwangu ( tumbo langu)


                    “TATIZO NINI WANGU WA MOYONI?” Pompo alihoji.

                  “Uchungu Baba, uchungu roho wangu, naumia mie.” Pompo alinishangaa hakutaka muda kuupoteza alihitaji kunisaidia.

                “Pole love, pole sweet heart, twende Kigamboni Hosptali. Haraka sana Pompo alibadili nguo za kulalia akavaa za kutembelea usiku ule, tayari keisha nibebea vitu vyangu muhimu vinavyohitajika Hosptali, kanitoa njee ya nyumba yetu na sasa ananipeleka Kigamboni Hosptali, kwa ile Tax gari yetu.


           “uwiiiii, uwiiii, uwiii! Oooh! 😢😢😢😿Nafwa mie” Nalilia nikiwa nyuma ya gari ambayo Pompo alikuwa akiiendesha.

             “Pole moyo wangu, Subira yavuta heri, ngojea weye mwenyewe utafurahia.” Pompo alinifariji Gari ikazidisha mwendo.


                    ##################


“Pole sana dadangu” Nesi aliyenihudumia usiku wa jana alinifariji.

           “Asante sana Nesi, Mwanangu anaendeleaje.” Nilimuuliza Nesi tabasamu langu mdomoni, hamu ya kumuona Malaika wangu ilinipanda.

             “Nesi, mdogo wangu mbona wanikalia kibubu, nijibiwe mie mzazi, leo ninafuraha ya kuitwa Mama, nimeleta mtu katika familia, heshima kubwa katika jamii inizungukayo.” Niliongea na yule Nesi aliyeekuwa angali bado kimya ananitazama mie kama kitu kipya machoni kwake. zilipita sekunde chache yule Nesi akafungua kinywa chake.


                 “Nina masikitiko bibie.” Nesi hakuonesha furaha tena, mara ile nikamuona Pompo roho wangu, akiufungua mlango mkuu wa kile chumba nalicholazwa, akaingia Maua 💐mkononi, Juisi 🧃na matunda mkononi.🍇🍌🥭


                 “Niambiwe Nesi wasikitikani?” naliingiwa na hofu, Pompo alisogea karibu na kitanda nilicholazwa ayasikie maongezi yetu.


                  “Mwana uliyemzaa, hatunaye tena mtu huyo, si riziki yako Mamie” Nesi aliongea kwa masikitiko. 


                “What!?” Mie na Pompo tulitamka kwa umoja.


               “ Wamaanishani Nesi?” Pompo alimuuliza Nesi.

                “ Mwanao alipotoka tumboni akaaga Dunia, tusijue nini kilichomuua lakini bwana Dakta kasema mtoto alishindwa kupumua mara baada ya kuzaliwa.” Nesi aliongea kaniachia SIMANZI Mie na roho wangu Pompo. Machozi yakanisururuka, nikalia mie, nikalia Mamsapungo, nikalia masikini.


         “Pole sana mke wangu.” Pompoj alinifariji, ningali bado namwaga machozi.


          “ Asante sana roho wangu ya Mungu mengi, ametupa na wakati huo huo ametuchukulia"


             “Ipo siku atatupa tena.”

            “ Najua Pompo najua Love.” Nililia kwa uchungu, nililia kumpoteza pacha wangu.


             “ Unasikia my love,” Pompo alihitaji kuendelea


             “ Nakusikia my love” Mie nikamwaga tena bomba la machozi ikawa ni kazi ya pompo kunifuta yale machozi na kunifariji.


            “Kuna habari mbaya nimeipata kuhusu Maua, Maua hatunaye mtu huyo,”

             “ Mmh!" Niliguna mie nikamtazama roho wangu Pompo nisitake kuamini yale ayanenayo.

            “Maua kaaga Dunia?!” nikamhoji Pompo.


             “Ndio kagongwa na Gari, asubuhi ya leo, kagongwa vibaya sana,kichwa kule, kiwiliwiili kule. Ati alichanganyikiwa kama majiranize wanavyo sema, akili zillimruka, aeshi kulitaja jina langu🔊, Pompo pompo, pompo kama mwendawazimu” Pompo kanieleza.

        “Oooh! “ nilisikitika nikaikumbuka ile ndoto niliyoiota usiku wa kuamkia jana. Je, ndoto niliyoiota jana inaendana na matukio yaliyotokea siku ya leo? Nilijiuliza nisipate jibu.


          “Mola amlaze pazuri Maua.” M ie niliongea


          “ Nyota mbaya imedondoka.” Pompo kaongea, mie mawazo yananizidia kichwani.


          “Shauri ya wivu na tamaa, ndio sababu ya kufa kile kifo, ona sasa ,ona wivu kidonda, wivu unaua.” Pompo alizidi kumlaumu marehemu.


         “Acha Pompo , acha usiendelee kunena, acha ujue kuwa na sie tushampoteza Malaika wetu. Roho wetu, mtu wetu katika familia.hatunaye tena mtu huyo.” Niliongea machozi yamenijaa tele.


           “ Nikwambie Pompo,”Nilimwambia Moyo wangu.


           “SEMA Love, mama wa watoto wangu.”


            “Yaliyopita si ndwele, tulilinde penzi letu lisiingiwe na soko.” Nliongea ningali bado nina sikitika.


             “Tutalilinda my love, kwa nguvu zetu zote, ata kwa bunduki na kwa risasi.” Pompo aliongea.


            “Kwa amani upendo, furaha uvumilivu na ustahimilivu.” Nikamjibu Pompo

               “Penye chuki pawe upendo, penye dhiki pawe faraja, penye mateso pawe raha na amani tele.”


              “Ujue mie napenda sana amani Pompo, amani hiyo ni kila kitu kwangu, amani hiyo ni wewe unitulizaye mtima wangu, nakupenda sana Pompo roho wangu, nakupenda mume wangu, ninafuraha kupendwa na wewe.” Niliongea.


             “Ninakupenda pia amani wa moyo wangu, pompo alinikumbatia nikampiga mabusu 👩‍❤️‍💋‍👨elfu nyingi na yeye akaniiiibusu elfu nyingi😚😘, faraja ile ilinifanya nijisikie kupendwa. Aki! Mwenzenu n’shapendwa, sijui nyie shoga labda niwaambieni, ukipendwa pendeka, mpende akupendaye, mwache asie kupenda ukimpenda aso kupenda atakutesa mtu huyo. Aku! Mie n’shapendwa.


           ******************************


   Nyonyo mie nipo kuuguza tumbo langu, tumbo la uzazi, nipo kwenye machungu ya kufiwa na Malaika wa moyo wangu, faraja zenu shoga zangu faraja zenu niambiwe “Pole Mama la kitanga, ugua pole” ili mie shoga yenu niliyependwa nipoe nifarijike,


            Nyonyo, shoga zangu, mie nakomea hapa, naomba tukutane tena kwenye simulio langu la pili linalo enda kwa jina “ WATABAKI NA LABDA.” Usingoje mwaya, usingoje kuambiwa, macho hayana pazia, kama huwezi kusoma basi picha tazama.



          “Mie nipo kuugua. Nauguza mwenzenu.”             

BARUA YA MPENZI NUHU

        


      MAMA ALITAKA NIOLEWE NA MABWANA HARUSI WAWILI KWA MPIGO.

         Nilijigeuza juu ya kitanda changu kikubwa cha sita kwa sita🛌 kitanda chenye matandiko safi na mito mikubwa laini ya kulalia, taa💡 ya chumba changu ilikua ingali inawaka na kukifanya chumba changu kionekane katika ubora wake, kikang'ara mfano wa chokaa mpya. Niligeuka upande wa kulia kisha nikaupiga mwayo wa nguvu Aaaahhh😮' ile nafumbua macho yangu nilijikuta nashtuka mshituko 😱 uliotaka kuuvunja mtima wangu.

   Jesu!! 😳 Wewe nani? Macho yangu yalikutana na sura ngeni ya mwanaume mmoja tanashati ametinga suti moja nyeusi kwa rangi, Tai safi nadhifu, uso wake umeboreshwa kwa mafuta na mapodali. Aliniangalia.

      "Mie Bwana Harusi?"🤵💒Aliongea kwa tabasamu nono lisilokauka mtimani.

      "Mie pia,"💒🤵 🤗Ghafla niliisikia sauti nyingine ya kiume nyuma ya mgongo wangu. Nilijigeuza kwa hofu na woga nikakumbana na mwanaume mwingine  zaidi ya tanashati, suti yake ya Blue na tai Moja safi akiwa amelala juu ya kitanda changu.

         "Jamani nyinyi ni wakina nani,❗ mbona siwaelewi?" Nilihisi nipo ndotoni japokua haikua ndoto zaidi ya uhalisia.

       "Funua blanketi, mwenyewe utaamini," Haraka pasina kupoteza muda nililifunua blanketi langu pale kitandani, Toba!🥺 Nilishangaa kuliona gauni zuri la Bibi Harusi likiwa limekaa mwilini mwangu.👗

      "Mambo yote haya yametendekaje? Nilijiuliza mtimani.🙃

       Ghafla mlango wa chumba changu ulifunguliwa. Mama aliingia akiwa ameshikilia Bunda la Maua,  💐🏵️alipofika kitandani kwangu akalitupa lile bunda la Maua katikati ya mapaja yangu  kisha akanena.🙄

       "Pamela nimeisubiria sana siku ya Leo, tayari umetimza miaka ishirini na mmoja nimekubembeleza sana mwanangu tafuta mchumba akuoe💍 lakini ulivyo 'mkaidi hafaidi' umenipuuza, hautaki mwanaume, hautaki kuolewa sasa nakuambia hivi utaolewa na hawa wanaume wawili👬 kwa siku moja. Toba! 🥹Mamangu alinishtua.

     "Mama sitaki kuolewa na kamwe haitatokea."Nililalamika.

     "Kama hautaki kuolewa na wanaume hawa wawili naomba uondoke ndani ya nyumba yangu" Mama alinifokea.

          Sitaki na  tena sitaki" Nilimpinga Ma'

   "Mimi sio muongeaji sana Pamela, wacha niingie chumbani kwako nikutolee kila ulichonacho nitupe nje ili tuone sasa nani mshindi kati ya wewe au mimi." Mama alidhamiria kunidharilisha. Akaelekea chumba changu cha siri, chumba nilichomficha mpenzi wangu Nuhu Mziwanda, yule ninayempenda na yule tutakaye funga pingu za Maisha siku moja. 💍


      "No Mama." Nilitoka pale juu ya kitanda nikakimbia mbio 🏃‍♀️kuelekea mbele ya mlango wa chumba changu cha siri kule nilikomficha Nuhu. Nikasimama mlangoni, nikamzuia na kuziba Mama asiingie asijemkuta niliyemficha chumbani.


       Mama tafadhali naomba usiingie chumbani, ninaomba unipe muda wa dakika ishirini nitafanya maamuzi na machaguzi juu ya mchumba nimtakaye." Wakati huo nilikua nimeziba mlango wa chumba changu taiti Mama asiingie.


      "Ok. Ninakupa dakika 🕛ishirini tu uwe tayari sebuleni kufanya maamuzi la sivyo nitakuvuruga Binti yangu." Mama aliongea kwa hasira 😡moyoni sikupendezwa na maamuzi yake. Nilimwona akielekea sebuleni pamoja na wale wachumba alionichagulia. Mie haraka nikaingia chumba cha siri, chumba nilichomficha Nuhu Mziwanda.


Chumba nilichomficha Nuhu sio chumba kama vyumba vingine vya kulala bali ni  sebule fulani yenye Meza ndogo, sofa  chache, 🛋️bafu la kukogea, choo 🚻na kitanda ambacho Nuhu mpenzi wangu angelitumia kulala Mama asimwone. Hakika kile lilikua ni chumba cha siri.


   
       Haraka haraka nikalibadili lile gauni la Harusi, gauni ambalo sikuelewa muda gani nilivishwa, yamkini nilipuliziwa dawa za kunipa usingizi nisielewe kinachoendelea. Nikalivaa shati la Nuhu,Suruali ya Nuhu na singled ya Nuhu, wakati huo Pete nzuri alionivisha Nuhu miaka mitatu iliyopita iling'ara na kung'ang'ania kidoleni kwangu.💍


       Nuhu hakuwepo chumbani lakini nilijua pahali alipo, 'Bafuni' sababu asikiapo kelele 🔊za Mama ujificha bafuni mama asipate kumuona. Nilielekea bafuni nikamkuta Nuhu ameketi chini, pakavu, nadhifu, safi pasipo na tone la maji, miguu yake ameikuja kama mwislamu alaye daku na waislam wenziwe. 🕋☪️🇵🇰🕌Nikamtazama na yeye akanitazama, macho yake mazuri yaliyojaa 👁️😍 Huba yalikutana na macho yangu. Lips zake nene zilizonona ziliachia tabasamu.👄😚 Nikamwambia:


        "Nuhu mpenzi ninajua umesikia Kila neno ambalo Mama ameongea kuhusu ndoa ya lazima lakini mpenzi ninakupenda 💙na sintakuacha maisha yangu yote." Nuhu alinitazama lakini hakusema neno.🥸

       "Ninakupenda pekee yako wewe ndie mwanaume wa moyo wangu. Bado Nuhu alitabasamu akinitazama kwa jicho la Huba zito. Nilipomaliza kuongea na aNuhu nikatoka pale shower nikaelekea sebuleni kule Mama ameketi na wale vijana wawili aliotaka kuniozesha kwa lazima. Nikiwa ninateremka ngazi za Horofa ya pili kuelekea chini sebuleni nilijisemea mtimani.

     
      'Mama anadhani nitamuacha Nuhu"😂😂  Anajidanganya Nuhu ameingia moyoni mwangu.💕


      "Nitafanya Kila kituko kuhakikisha ninawakataa hawa wanaume ili niolewe na Nuhu, nimpendaye nimemuweka moyoni mwangu naye ametulia" Nikatelemka ngazi, chini nikafika, uso wangu ukamkabili Mama.


      " Siwezi kuolewa iwapo sijawajaribu Hawa wanaume ili nifahamu kama kweli wananipenda au la!" Nilimwambia Mama.


       "Ilo tu! sio tatizo tunaweza kuanza."Mama Aliongea.


        "Nitakuwa wa kwanza katika jaribio lako, ninakupenda" Bwana wa Kwanza Aliongea.☺️


     "Mimi pia ningehitaji kuanzia jaribio lako"Bwana wa pili mpole mwenye uso wa tabasamu Aliongea.☺️


      "Wewe  MPUMBAVU NINAOMBA UKAE KIMYA UTULIE mimi niliyewai nianze majaribu," Bwana wa Kwanza mwenye sura chungu, hasira na haraka alidakia.🥴 Mama akasema.


        "Bwana Harusi wa kwanza mfate Bibi Harusi chumbani kwake mkaongee."


       "Very nice." Bwana Harusi wa kwanza akifurahia akanifuata tukaelekea chumbani kuongea, chumba CHANGU cha siri chumba nilichomficha Nuhu Mziwanda ambaye Bado alikua ameketi bafuni akiogopa kama Mama angelimuona ingekua mtihani.


 ##############

         Tuliketi juu ya sofa zilizo ndani ya kile chumba pembeni ya kijimeza kulikua na mvinyo wa bei ghari ambao yule Bwana aliuleta. Bila kupoteza muda alipiga magoti chini akatoa pete yenye kito cha Diamond akaniambia "Naomba nikuvishe Pete." Hapo tayari goti chini amepiga.


         "Sawa niviishe." Nilimwambia nikiwa nimesimama akanivisha Kisha akaongea.


       "Hii Pete ni Pete ya bei Kali Sana nikikuoa nitahakikisha Maisha Yako yote unavaa Vito vya bei gharama, unatembelea usafiri wa bei gharama, Kila kitu chema ukitakacho kitakua ni cha bei ya kutupa."Alijigamba akijua kuwa nitafurahia mali zake.


        "Hayo ndiyo malengo uliyoyaweka tukiwa ndani ya ndoa ?" Nilimuuliza,


     "Sasa kumbe! Ninataka uishia Maisha ya anasa wakati wote utahudumiwa na vijakazi, utaishi kama Malkia mie nikiwa Ofisini nikitafuta pesa."Bado tu hakunishawishi.


      "Bado haujanishawishi Bana Joshua  unanipenda kwa dhati?"Bila kutarajia Joshua aliyejitambulisha kwangu alinijibu.


      "Sikiliza Pamlela sio kwamba nimekupenda kutoka moyoni mwangu, Kuna kitu muhimu ninakitafuta kutoka kwako."


      "Ni kitu gani hicho?" Yule tajiri akanijibu.


        "Mama Yako amenileta hapa akishinikiza nikuowe kwa sababu nyumbani kwetu kuna matatizo kibao, Moja ya tatizo linalosumbua nyumbani ni utajiri na mali nyingi alizozoacha Baba yangu aliyefariki hivi karibuni," Alimeza mate na kupumzika kunena,

        "Pole kufiwa na Babako" Nilijua kumfariji.


      "Asante. Baba ameacha makampuni mengi na hisa nyingi ndani ya hayo makampuni, hivyo basi ndugu zangu hawataki kunipa mgao wa hizo hisa na Mali nyingine nyingi  kwa shariti moja tu ni lazima nioe haraka ndipo wanigawie mali, wana hofu kubwa kuwa nisipooa nitachezea huo mgao nitakaopewa lakini nikiona mke , mke atakua mshauri mzuri wa maendeleo yetu, ninakuhitaji  tafadhali kubali nami nipewe mgao wangu wa hisa alizoziacha marehemu Baba." Alimaliza kunena.


      "Sidhani kama itawezekana Bana Joshua maana sikuoni kama una mapenzi ya dhati kwangu ninachoona mimi kwako ni hamu yako ya kukomboa utajiri na Mali ulizoahidiwa na ndugu zako. Yamkini ukiisha fanikiwa kuzipata mali hizo haraka utanigeuka na kunitupa"


        "Na hii Pete yako ninaitoa siitaki na Wala sikutaki," Kwa hasira niliivua ile Pete ya Diamond nikaitupa ndani  ya Birauli lililojaa ule mvinyo wa bei gharama,


      "Naomba uondoke na uniache ninahitaji kuwa mpweke" Nilimfukuza naye akatoa kiapo kwamba  mimi ni wake na kunioa lazima anioe,  machozi yalinitoka nikiwa ndani ya chumba changu Nuhu alisimama pembeni ya mlango wa Shower alinitizama kwa hasira kama vile anataka animeze, Nuhu alipoteza natumaini juu yangu,

       "Nuhu mpenzi ninaomba unisamehe kamwe sintakubali kuolewa na yule mwanaume asiye na malengo na mimi zaidi ya kunicheza kama karata ili avune utajiri,"Nikaangalia kidoleni Pete alionivisha Nuhu sinayo, Uwii! Nilipagawa tena haraka haraka nilianza kuitafu ile Pete aliyonivalisha Nuhu Miaka mitatu nyuma, hakika nilivurugwa, NIKAANZA kuitafuta Kila Kona ya kile chumba.........  Sofani na mezani nilitafuta Pete ya Mziwanda hatimaye nilikuja kiona Pete aliyonivisha Mziwanda kisha kwa furaha nilimuonesha Mziwanda wangu.

      "Hii ni Pete uliyonivisha Mziwanda wangu, nitawezaje kuitupa ikiwa wangu wa moyoni Bado ungali upo nami"Ghafla mlango wa chumba changu ulifunguliwa Nuhu  aliingia haraka ndani ya bafu na kufichama,

       "Ulikua unaongea na nani wewe?" Mama aliniuliza baada ya kuingia chumbani na yule Bwana Harusi wa pili.
 
       "Sijaongea na mtu Mama?"  Nilimjibu haraka kumzuia mama kuijadili ile ishuu.

        "Haya nenda Jikoni na mchumba wa pili kuna kahawa ☕na kashata nimekuandalieni ni matumaini yangu kwamba mtaelewana,"  👏Mama litoka chumbani, mimi pamoja na yule Bwana Harusi wa pili tulitoka tukaelekea Jikoni kunywa Kahawa,
     
                ###

Jikoni tulisimama karibu na karo ya kukoshea vyombo yaani Sink la vyombo upande wa kushoto kulikua na fridge yetu nzuri na kati kati ya Jiko letu Meza ya mviringo pamoja na viti vya mbao havikukosekana achilia mbali Jiko letu zuri linalotumia gesi ⛽ oven na umeme.

       "Ni kweli unahitaji kuishi na mimi?" Nilimuuliza na yeye akanijibu

       "Yes of course ninahitaji kuishi na wewe?

   "Nitaamini vipi kama una malengo ya kuishi na mimi au labda upo hapa kunichezea" Yule kijana mwenye uso mtanashati wenye nyingi aibu na macho mazuri yaliyojaa huruma kwangu alijitambulisha kwa jina la Mode Mario, Akanijibu,

        "Subiri,"Nikamwona afungua fridge na kutoa kopo kubwa lenye pilipli pamoja na vikombe viwili kisha akamimina ile pilipli kwenye vile vikombe naye akatamka

       "Kila ukweli nitakao sema kwako nitameza kikombe cha pili pili na wewe pia Kila ukweli utakao Nena kwangu utameza kikombe cha pili pili." Nilimshangaa, maana ukali wa pilipli MWENZENU ninajua

       "Mario pilipli kawaida ina ukali na uchungu"


         "Yes, ukweli pia lazima uwe mchungu" Alinijibu, Kisha akanipa nafasi ya kuuliza maswali

        "HAUNIJUI NA MIMI SIKUJUl KWANINI UNATAKA KUISHI NA MIMI?"

            "Nafasi inaniruhusu kufanya hivyo,"

       "Je, unanipenda?" Hakunijibu swali langu zaidi ya kunitazama machoni na kugugumia funda la pipipili ile nzito na chungu,

         Uwii! Nilibaki nashangaa Mario pale alipogugumia lile funda la pilipili nzito na chungu lakini pia nilianza kumpenda nakumfurahia moyoni mwangu. Aliniingia akilini mwangu kwa kasi ya ajabu, haraka haraka nikakimbilia fridge na kuifungua Kisha nikayachukua maziwa fresh nikampa ayanywe, akayagugumia yale maziwa kama mwendawazimu baada ya dakika chache mbele yetu tukatazamana kwa vicheko kisha tukafanya kuhamia pahali Meza na viti vilipo kisha tukaketi pale.

         "Nataka kumjua mtu ambaye ulikua unaongea naye pindi mimi na Mama yako tulipoingia chumbani kwako"

          "Ni boyfriend wangu."Nilimjibu kwa ufupi.

       "Kwahiyo unae Boyfriend?"

         "Ndiyo na NINATARAJIA yeye ndie atakae nioa mbeleni"Nilimjibu bila kupepesa macho naye akaniuliza swali lingine zito.
      
       "Je, unanipenda na upo tayari nikuoe?" Nilishindwa kujibu haraka zaidi ya kumimina ile pilipili mdomoni mwangu, Uchungu wa ile pilipili hakika siwezi kuhadithia. Mario akafanya haraka kuelekea kwenye fridge na kuniletea maziwa niliyoyagugumia kama mwendawazimu,

         "Pole,"Alinifariji.

           "Duh! Ama kweli ukweli lazima uwe mchungu,"Wawili tulicheka kwa furaha, tabasamu likatufanya tujisikie kama tumezaliwa upya,

       "Naomba tupeane ahadi" Mario aliongea

     "Nipo tayari."Nilianza kumpenda yule kijana asiye na makuku

      "Anza wewe kunipa ahadi yako na mie nitaitekeleza" kama nilivyosema Mario amenyimwa roho ya majivuno akanitaka nianze kumpa ahadi yangu,

        "Naomba uniache niishi pekee yangu," sikumtania nilimaanisha

        "Sawa, kwa sababu natambua unaye Boyfriend  nipo tayari kukuacha uishi naye. Alikubali matamanio yangu. Ikawa zamu yake kueleza ya moyoni,

      "Kuna kipande cha barua nimekiona ukikiweka mfukoni muda ule tulipoingia Jikoni ninaomba nikisome nijue kinahusu nini?!" Duh! Alinishitua.

    "No! Kipande cha barua yangu hakikuhusu" Nilichelewa kujizuia Mario akanivamia na kukichukua kile kipande cha barua niliyoihifadhi juu ya mfuko wa shati nililovaa, shati la mpenzi wangu Nuhu,

         "Hapana tafadhali usithubutu kukifungua kipande cha barua iyo na kukisoma," Niliisha chelewa Mario alikwisha fungua kile kipande cha barua naye akasoma:

           MPENZI  PAMELA
NINAJUA UNANIPENDA SANA NA MIMI NINAKUPENDA ZAIDI YA UNAVYONIPENDA, NAOMBA NIKUAMBIAE JAMBO MOJA. HUU UGONJWA WANGU UMEZIKATAA DAWA NA MIMI SIJAKATA TAMAA LAKINI MUDA WANGU UMEFIKIA KIKOMO .........

Mario hakuweza kumaliza kusoma kile kipande cha barua naye akaniuliza:
  
     "Mpenzi wako anaumwa?!"Sikua na jibu zaidi ya kumwambia Ndio.

       "Ok. Basi nenda kamuuguze" machozi yalianza kunibubujika nikatoka Jikoni na kukimbilia sebuleni lengo langu lilikua ni kumfuata mpenzi wangu Nuhu kule chumbani nilikomwacha mpweke

     Nilidhamiria kumwomba Msamaha Daring Mziwanda maana nilijiaibisha kuongea mambo yanayohusu mapenzi  na wanaume wengine. Nilipofika sebuleni nilimkuta Mama ameketi pamoja na Bwana Joshua wanasubiria Jibu langu. Mama alisimama kisha akaniuliza.


       "Eeh! Niambie jaribu limefika mwafaka gani?"


       "Nimemwambia Mario aniache niishi pekee yangu.


     "Kwahiyo Mario ameshindwa mtihani?"Mama aliniuliza. Kabla sijajibu Joshua alidakiza.


        "Nilisema mimi, nilisema utakuja kuwa wangu, Ona sasa, ona ninaenda kujinyakulia urithi kiulaini"Alijigamba haraka haraka akaja kunikumbatia kwa nguvu,

  
       "Sasa tuondoke"Alianza kutumia nguvu kuniondoa pale sebuleni.


      "Hapana, Bwana Joshua mambo Bado na taratibu lazima zizingatiwe"


      "Mambo gani? Taratibu zipi? Mama sitaki ushenzi wa kunipotezea muda wangu mzuri. Nasema hivi Binti yako ni Mali yangu, ndoa lazima ifungwe Leo hii hii," Aliendelea kujipamba.


       "Umenileta hapa nyumbani kwako ili kunionesha Binti yako ulidhani nitashindwa kumpata? Chezea hella ooh!" Akamsukuma Mama yangu kwa nguvu Mama akaanguki juu ya sofa akakibamiza kichwa chake ukutani nakwambieni maumivu aliyoyasikia mbona alijuta. Bwana Joshua aliendelea kunikaba mabega akanikokota kwa nguvu na kwa lazima ya kuondoka kama Mbuzi aliyenunuliwa Mnadani.


        'Nguuuuuu,' Ngumi nzito ilitua juu ya uso wa Bwana Joshua, Joshua aliona kizunguzungu akaanguka chini kama zigo la mapumba, moja kwa moja akazima na kupoteza fahamu.



        "Mshenzi mpuuzi huyu"Mario aliongea. Ngumi nzito aliyomlisha Bwana Joshua ilitosha kuniokoa. Tuliketi juu ya sofa ili kumhudumia Mama ambaye kidogo alianza kupata ahueni.


     "Niruhusu niende chumbani nikampe taarifa mpenzi wangu Nuhu." Nilimwambia Mario. Hata kabla sijapewa ruhusa nilichoropoka pale tulipoketi Mimi, Mama na Mario nikakimbilia chumbani kwangu 

     "Anampenda sana Nuhu, ngoja nikamuona huyo Nuhu maana ameniambia anaumwa?"Mario alimwambia Mama.


          "Mpenzi gani?"Mama alimvuta Mario sofani akamketisha na kumpa simulizi.


         "Pamela Hana mpenzi wala mchumba huyo Nuhu aliyekuambia alikuwa ni mpenzi wake aliyefariki miaka mitatu iliyopita. Nuhu aliugua kansa ya koo basi tangu afariki Pamela haachi kumuwaza huyo marehemu. Amini usiamini kila siku Pamela anavaa nguo za Nuhu, huu ni mwaka wa tatu amevurugwa na amechanganyikiwa. Imekua kama Hadithi kila siku Pam anaongea pekee akilitajataja jina la Nuhu Mziwanda." Mama alihadithia juu ya Nuhu mpenzi wangu

      "Unataka kuniambia huyo Nuhu ni kivuli tu kisumbuacho Pamela"Marioo alimuuliza Mama.


    "Ndio sababu y mimi kuwatafuta wanaume wawili mumshawishi Pamela hadi akubali kuingia ndoani, jambo la kushangaza mnaniangusha hadi mnaanza kupigana ajili yake."

     "Mama NINAKUAHIDI jambo Moja mimi sio mama zuzu Joshua. Nipe dakika chache nikamshawishi PAMELA amini usiamini nitaibuka kidedea" Mario alimwaminisha Mama.


      "Haya Baba  ninakutakia fanikio jema."Mario alipanda Horofa ya pili akaelekea ndani ya chumba nilalacho akanikuta nimepoa juu ya kitanda nimelala nikiitazama sehemu ulipo mlango wa bafu.


       "Pamela."Aliniitia, akajiketisha juu ya kitanda changu.


    "Abee!"Niliitikia wito.


    "Bado unampenda Nuhu?"Aliniuliza.


     "Ndio tena sana, tumepanga mipango Mingi sana ya maisha yetu, nilimpa ahadi ya kutomwacha,"


      "Lakini Pamela Nuhu alikwisha kufa na kutangulia mbele za haki. Ukionacho mbele yako ni kimvuli chake, kivuli  ksichotulia zaidi ya kukuwinda na kukupumbaza."


      "Hapana, Nuhu yupo hai Wala hajafa, ninatazamana naye, yule pale amesimama pembeni ya mlango wa bafu."


      "Nikuulize swali." 


      "Uliza tu Bwana Mario."

      
          "Tangu Nuhu alipokukabidhi icho kipande cha barua je, umewai kukisoma"


        "La, asha!" Mario akaingia woga na hofu ya kutaka kujua ni niniNuhu alichoniandikia miaka mitatu iliyopita.



     "Hilo ndilo tatizo inaonekana mzimu wa Nuhu unakufuata popote pale ulipo, ukiwa umelala unamuona, ukiwa unaoga unamuona, ukiwa unakula unamuona, kivuli cha Nuhu hakijapumzika kwa amani, hivyo basi jaribu kuifungua hiyo barua uisome" Mario alinishauri .


        "I cant Mario, I cant please!"


       "Unaweza."Mario akaitoa ila barua aliyonikabidhi Nuhu Kisha nami nikaisoma."


        NINAKUPENDA NA NITAENDELEA KUKUPENDA......... Nilishindwa kumaliza kusoma kile kipande cha barua machozi yalinibubujika maana nilimuona Nuhu amesimama pembeni ya mlango wa shower akitabasamu.


       "I cant finish reading it Mario." Chozi lilinibubujika


        "Nipe nikusomee." Nilimpa Mario akisome kile kipande cha barua Mario akasoma.


NINAJUA SINTAWEZA  KUENDELEA KUISHI DUNIANI UGONJWA HUU UNANIMALIZA BASI NINAKUOMBA MPENZI WANGU IKITOKEA UMEPATA MPENZI MWINGINE KUBALI KUISHI NAE, OLEWA UISHI KATIKA MAPENZI.


         SINA MENGI ZAIDI YA KUSEMA NINAKUPENDA.


        WAKO AKUPENDAE,


NUHU.

Mario alipomaliza kukisoma kile kipande cha barua nilimuona mpenzi wangu Nuhu akinipungia mkono wa kwaheri, ghafla akatoweka ndani ya chumba changu, kuanzia siku ile sikupata kumuona tena Nuhu wangu. Mario alifanikiwa kunioa mapenzi yetu yalipamba moto tukapendana na kuishi katikati ya raha na starehe. Uzuri wa mapenzi mwaka huu ninatarajia ifikapo mwezi wa Tisa niingie Leba, niilete nyumbani zawadi Bora ya maisha.

     Kila nikikumbuka Mama yangu, Mama mpole mwenye huruma na busara alitaka niolewe na wanaume wawili mmoja mwenye majivuno na mwingine mwenye busara nikikumbuka mie nachekaGa tu.


~~~~~~~~

TCHAO 💖 

~~~~~~~~



   


          
       

   

Monday, August 4, 2025

MWENZENU N'SHAPENDWA



MIPASHO YA MAMSAPU


MWENZENU N'SHAPENDWA 


Sehemu ya 8 

 Roho wangu hakuwa na amani siku ile na mie pia sikuwa na amani, Maua katutia Stress, mawazo mgeni huyu aso tutakia mema, katuvuruga siku ya leo, hatukuweza kula vizuri, hatukueza kulala vizuri, basi kati kati ya usiku wa siku ile mie nikamuuliza roho wangu Pompo, nikamwambia.

             “Je, Babu utaniwacha kwa sababu ya Maua.?”

             “Nianze tu! N'taanzaje kumrudia yule msaliti, mbovu aso yajua mapenzi.” Pompo aliendelea kunena.

                 “Love💖 ninakupenda pekee yako huyo mwingine kwangu ni kama makapi, atupwe jahani hafai kulivuruga vuruga penzi  tuliloloshikilia.” Maneno ya Pompo yalinipooza kidonda alichokileta Maua.

             “Moyoni umenikaa , moyoni umenikaa,
               ingia moyoni mwangu.
               Damu yangu imekupenda wewe,
               mimi nimekupenda, 
               ingia tena moyoni mwangu,
               Mimi nimekupenda na wewe
               ukinipenda mapenzi milele," 

Pompo alilikoreza pendo kwa maneno matamu yalozidi kukiponya kidonda changu.

         “Nikuache niende wapi? Mapenzi najua, mapenzi wayajua. Huyo mgeni mapenzini porojo na vimombo vilipomzidia akageuka Fisi tamaa, Fisi tamaa ajapochanganyikiwa uchana msamba, njia mbili zijapomshinda. Pompo alinichekesha kwa manenoye.

             “Uboya wake mwenyewe,” Mie nikachangia hoja.

              “akafie mbali, kibudu yule.” Pompo kamlaani yule mwanamke.

               “yashamkuta tayari na sasa anasaka naafu ya kuliponya donda limtesalo.” Pompo aliongea tena.

                “Sikia love, nishamchunguza,nishapata taarifa zake, leo anaumia kuachwa.” Pompo aliliamsha dude la masimulizi.

             “kwni kaachwa? Je, aliolewa tena?” Maswali ya mie yakaanza kusambaa kichwani kwa Pompo roho wangu.

               “Yes kaaachwa, katupwa jahani kama takataka,  nani amzo? Hakuna”

                “ Teeh teeh teeh,(😂😂😘nalicheka mie) na hata akizolewa atatupwa tena?” alizidisha porojo.

              “Mie ninatamani nisimwone tena abadani,” Roho wangu aliongea.

               “kumbuka tayari ushazaa naye!”

              “Kuzaa majaliwa hata wadudu wanazaa, sembuse ndege na mimea, hayo yote mapenzi ya Mola silioni tatizo hapo, tatizo ni usaliti wake na kuniacha solemba.” Pompo  aliongea. Leo mwanga wa taa tuliuona hafifu ingawaje taa ilikuwa na mwanga wa kutosha.

               “Mwenyewe ushamsikia, kakataliwa na jamaaze, nduguze, mashogaze na jiranize, kafanya juu chini apate kunitia machoni na kwa hilo kasha wini....... nini sasa? Nini ananidai? Atoke huko,😂👌 mie simtaki wala sitaki kumwona abadani,  akamrudie mwarabu wake.? Pomp leo kajaa hasira.

             “Mwarabu!?” mie kuuliza.

             “Yes, aliponzwa na mashogaze wasojua thamani  ya ndoa za wengine,akaolewa na mwarabu wake, ndoa ya bei ghrama. Bibie kawekwa ndani hapati mapenzi ya dhati anapangiwa kulala na mumewe sababu mumewe ana bibi watatu wakubwa na  yeye ndo’ Bibi wanne tena Bibi mdogo.”

             “ Mmh! Mwanamke huyu, lo! Tumpe pole.” Mie nikaongea.

           “Alie tu kayakaosa mapenzi, kaumia kaumizwa, baya zaidi magubu ya wake wenza yalivyo kuwa hadimu kupurukutika, huyo kimburukutu yakamshinda, akawa hana mbele hana nyuma, kutwa kuchwa ni kulia na kusikitika, kutwa kuchwa ni kujuta kwa maamuzi yaliyo jaa pupa.”

            “ Ndio akome mwanamke mwenzangu,” Naliongea.

              “Dunia hadaa, ulimwengu shujaa, hakufundwa na Mamaye sasa ulimwengu umemfunda.” Pompo alitia mafumbo.

             “Ona, mshika mbili moja lampokonyoka.”

             “ Aibu Pompo!”

             “ Amtake nani sasa, wote wanaomtaka wanamtaka kama mtumwa na kumwacha kama mzoga, analazimisha ndoa na hiyo ndoa asiipate.”

             “Teeh teeh teeh, 😂😂😘kageuzwa danguro la wahuni,” Nalicheka kimapozi mtoto wa kike.

              “Kwani kaachwa!?” Pompo alinigea masikio nimsikilize vizuri.

             “Yeye ndiye aliye muacha huyo Mwarabu, kamkimbia kule Pemba, kaona heri amrudie yule aliyemtema.”

              “Na aliyemtema kamtema zaidi.”  Nilitia neno.

               “Hayo ni matapishi, uchafu utiao kinyaa, sipotayari kuyarudia matapiko.” Pompo alizidi kuongea, leo analitoa povu limtokalomoyoni.

                “Mie nalijua kaachwa Pompo? Nikachombeza kutafuta umbea.

              “Akome kuringia uzuri wake, sikia Love wasoyajua mapenzi daima uchagua, ubagua na kupangua,utazama mali na fahari za Dunia, kama kigenzo ch kuyaendeleza mapenzi, usahau uvumilivu, ungojevu na ustahimilivu, ni watu wenye haraka zilizo jaa pupa.” Pompo roho wangu alinijaza maneno.

              “Tuachane na huyo Umbwakoko, keisha na keisha kuchoka, kachunwa sana na kabakia mifupa, liwe fundo kwake na kwa hao shogaze,” Nilimtaka Pompo tulale tushaongea mengi siku ya leo, Maua asituumize vichwa vyetu bado tuna nafsi ya kusonga mbele, mbele kwenye yetu maendeleo.”

           ######################

Ilipita miezi kadhaa Maua akijaribu kila njia ya kumshawishi wangu wa moyoni ayarudishe majeshi yake ndani ya moyo wa Maua, wangu hakuhitaji kuusikiliza ule upuuzi, hakuhitaji kusumbuliwa na yule kibibi mpuuzi, kama ni kumtema tayari keisha kumtema, kama ni kumfuta mtimani Pompo hana haja naye.

             Mie kibedi changu hakikunitupa kikazidi kuongezeka na kutupa matumaini ya kumleta mtu nyumbani, mtu wa kutupa raha na furaha ya ndoa, basi miezi ikapita, ikapita, ikapita, ikapita isirudi nyuma, mie na kibedi🤰 changu, kibedi kikainuka kikatuna kikichezacheza kwa furaha na Raha tumboni mwangu, matumaini makubwa ya kukileta Duniani kile kibedi👼🤱 yakaongezeka.

            “Atazaliwa mtoto a jinsia gani?” Nalijiuliza mie na moyo 💙 wangu, nikatatizika sana lakini yote tisa kumi Pompo alikuwepo ubavuni kwangu.

         “Labi atazaliwa wa kiume?” Pompo aliongea.

        “Aka! Babu we,mie namtaka mtoto wa kike.” Nilimtania Pompobwa ubani.

         “Mitoto ya kike kazi yao kuzaa zaa ovyo, usinilete litoto kama Maua, nitalitupa jahani mie.” Pompo alitania zaidi😂
          “ Teeh teeh teeh😁😅😆🤣 Aloo!👌,” nalicheka pompo pia alicheka zaidi.

        “Nitakuletea mtoto wa kutusaidia uzeeni, kwanza tumwache akue ili akoshe vyombo, apugute deki, atufulie, akwende kwa soko na kadhalika.” Nalitania.

         “Ujue mie napenda toto la kiume sweet love,maana toto la kiume litarithi mali.

          “ Ebo! Babu we, kwani mtoto wa kike hawezi kurithi mali?” nalijifanya kuchukia kumbe la! Ndo’  mahaba nibembeleze hayo yashan'jaa.

           “Mmh! We mwanamke, mtoto wa kike arithi mali zangu, waumeze watampora na kumpunja.” Teeh teeh teeh, Pompo kacheka mie nikapata raha.

           “Kwa hiyo mtoto wa kiume akirithi mali wakeze hawawezi kumpora?” Nilimtega Pompo.

          “Mmmh! Mwanamke una maneno weye, mbona wanitega Pompo alipata aibu yake.”

              “Si nyie waume zetu ni wakoloni, mwamkandamizaje mtoto wa kike, mwamwona kama vile yeye ni dhaifu na hawezi.” Nilizidisha maneno kuntu.

           “Mie sijanena hivyo.” Pompo kajitetea.

           “Kwa hiyo kwa maoni na kwa mtazamo wako ungelipenda tumlete Malaika gani hapa Kigamboni, nyumbani kwetu.?” Nikamtwanga Pompo swali tamu

           “Malaika Gabrieli.” Pompo alinijibu na kuniacha nacheka kicheko kikuu.

           “ The teeh teeh teeh🤣😆😅😁😂 Aloo! ” nilicheka sana kwa furaha ile nacheka tu mtoto👼 wetu karuka ndani ya tumbo langu.

            “Wacha matani Pompo mie nauliza jinsia ya mtoto na weye waleta maneno.

           “Weye wataka mtoto wa kike na mie nataka mtoto wa kiume, tupo njia panda, basi tufanye kukubaliana jambo moja.” Pompo roho wangu akamemeza mate kisha akanena tena.

             “Tuzae mtoto mwenye jinsia mbili, Tomboy au hapo unasemaje?” Pompo alinichekesha sana.

             “ Makubwa!🙊🤣Pompo wangu utaniua mie kwa furaha unipayo."

              “Au we unasemaje?” Roho 👨‍❤️‍💋‍👨♥️wangu kanihoji tena.
              “Na mie ninakubaliana na mawazo yako, Pompo tuuzike mgogoro wetu, tuksribishe mapacha, dume na Jike.”

              “Sio Tomboy mwenye jinsia mbili? Pompo alitania tena.

              “Pompo nawe usinitakie mabaya mie toto la kitanga, naombea mapacha na weye wakazia mtoto mwenye jinsia mbili.” Naliongea nikajifanya kuchukia lakini kumbe ni nyodo zangu, nyodo 👌za mwanamke.

             ##########################

    “Mama nakufaaa, nakufaa, nakufaa mie, Pompo niokoe” Nilkipiga ukelele mkuu, nikiendelea kutoka mbio ndani ya kichaka chenye nyasi mingi maua alizidi kunikimbiza, mkononi mwake amekamata kisu kikali chenye makali kuwili.

           ITAENDELEA.

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...