NILIMKOMESHA MISS EVIL.
Tuesday, December 3, 2024
MlSS EVIL
THE WORST FRIEND
JEALOUS FRIEND 🤢👺
(RAFIKI MBAYA)👿
THE WORST ONE.👹
"Ma. Nimepata rafiki" 💑Cadabra Jesse mwanangu wa darasa la tatu alirejea nyumbani akiwa ni mwingi wa furaha, cheko na bashasha. 😹Nilishangaa kusema kweli imepita miezi Tisa sasa tangu Baba yake aage Dunia kutokana na Car accident (Ajari ya Gari)♿🚗 mwanangu alikua Hana Raha Wala furaha zaidi ya huzuni, upweke, na kujitenga baada ya kifo Cha DadieJesse.
"Cadabra mwanangu Leo umefurahi sana kwani huyo rafiki anaitwa nani vile?" Nilimuuliza maana siku ya Leo mwanangu ameujaza moyo furaha,💖 anacheka na kuchangamka. Ukitegemea tuna wiki tatu tu toka tuhamie Gogolamboto tukitokea Chanika. Kwa maana hiyo sisi ni wageni hapa Gogolamboto.
"Jinale Hellena Jully. Tumekula pamoja🍛🍜🎉 na kucheza pamoja tena tumefurahia kununya Pipi na Biscuit."🍬🍫🍭 Siku ile Cadabra wangu aliongea kwa uchangamfu ambao hajapata kuwa nao muda mrefu tangu Babake aage Dunia.⚰️
"Waooo!😘😚😜 My Baby boy basi nenda kabadili nguo za shule ukuje tupate Lunch kidogo Kisha ukaoge🛀 tucheki katuni ya Lucas yule samaki🐟🐬 anayebadilika kuwa binadamu." Niliufurahia uchangamfu wa mwanangu Cadabra
Unaweza kuniita Singo mama, sikatai ndio ujane ulivyo. Nina biashara zangu hapo Kariakoo, sina njaa, Sina kiu na mwanangu anapata kila kitu utotoni mwake. Kinachonisumbua ni huzuni inayoleta upweke wa kuondokewa na mume wangu mpenzi Jesse Babaake Cadabra.
Basi kuanzia siku ile mwanangu Card Kila aliporejea kutoka Shule hakuacha kumtaja taja rafiki yake ampendaye Hellena Jully alinitajia sifa za huyo Hellena kwamba ni mpole, mwenye huruma na upendo pia alimsifia anavyopendeza na kushirikiana naye katika michezo🤸🤽♀️⛹️🏌️♀️🎾🤾♂️👯 skuli 🏫🎒 kwa kifupi aliirudisha furaha aliyoipoteza.
Basi siku moja tukiwa tunapata pochopocho🍕🍟🌮🍜🧆 na mwanangu mwenyewe akaniambia juu ya jambo lake.
"Ma. Hellena amenikaribisha nikapaone na kupajua nyumbani kwao."Card alimega mkate na kushushia maziwa fresh kwa furaha 🍞🥪 🥛
"Wacha we! Lini hiyo? Vipi unayo nambari #️⃣🚪1️⃣ya Nyumba yao." Nilimuuliza mwana aliyeboreka furaha.
"Jumamosi Mama, nambari ya Nyumba yao amenipa pia."Cadabra aliongea kwa furaha.
"Nimefurahia Sweetheart 👩❤️👨 Wacha na mie nikamuone huyo mchumbako unayemtajataja," Nilimtania my Son.
"Nipatie nambari ya simu🤳 ya Mama Hellena kama unayo." Nilibahatisha jambo la kushangaza, kumbe mwanangu alipewa pia nambari ya simu ya Mama wa rafiki yake. Akakimbilia chumbani kwake akachukua nambari alizozitunza kwenye begi lake. Nikachukua nambari ya mama Hellena nikamtumia Text message.
"Hallow! Mama Hellena mama Cadabra hapa naongea"📱 Nilijitambulisha.
"Ooh! Mama Card karibu sana, karibu Mama."Alinikaribisha kwa furaha.
"Asante mama Hellena. Card ameniambia jumamosi ya wiki hii Hellena amemkaribisha aje apaone nyumbani kwako." Nilimtumia Text message tukachati.
"Ndio, Mama Card umefanya vizuri kuuliza juu ya jambo la watoto wetu, tuwape watoto wetu furaha."Mama Hellena alichangamka.
"Vipi mwanamke mwenzangu naomba na mimi kesho iyo nije ili nipajue pahali ambapo mwanangu atafikia."🏘️🛣️ Niliomba lengo langu wazazi tufahamiane na tujuane zaidi ikiwezekana tusaidiane baadae juu ya watoto wetu.
"Haina shida Mama Card karibu sana tunaweza kushea mambo mazuri juu ya maendeleo ya wanetu na yetu pia." Text message za mama Hellena zilijaa upendo.💖💝
"Naomba niambie kama Kuna chochote Cha mno nibebe kwenye kutaniko letu la Jumamosi!? Nilihitaji kujua.
"Hakuna la zaidi itapendeza na kuchangamsha iwapo utabeba Wine ya Mzabibu🥂🍾🍷" Mwenzangu aliongea.
"Poa Mama lake. Naomba nikutakie usiku mwema🌑 mlale unono👋" Nilimuaga na yeye vivyo hivyo akaniaga.
🛌🛌🛌🌙🌜🛌🌑😴😴😪💤😫
Siku iliyofuata ilikua ni Jumamosi njema, niliichukua Gari yangu ya matembezi🚗 nikampakia mwanangu Cadabra tayari kwenda Mombasa nyumbani kwa best ake ampaye furaha na kumsahaulisha machungu ya kufiwa na Baba mzazi.
Tulifika salama Mombasa (ile ya Ukonga sio ya Kenya😆) nyumbani kwao Hellena rafiki wa Card kwa msaada wa nambari ya Nyumba ambayo Card alinipatia. Tulienda Moja kwa Moja kugonga mlango. Hellena akatokea kutufungulia, alipomwona Card mwanangu akamrukia kwa furaha nao wakakimbizana sebuleni kwenda kucheza michezo ya kitoto.🧩♟️🔫🎲🎭🧸 Mie mgeni nilimsubiria mwenyeji wangu Mama Hellena akuje kunilaki muda si mreefu Mwanadada mreefu, mwembamba mwenye rangi ya chocolate iliyokooza alitokea, nilishituka mshituko mkuu nilipomwona.
Nilimtazama mama yake Hellena na yeye alinitizama, hakuna aliyeamini milima🏔️🗻 haikutani ila binadamu tunakutana. 🧗🚵♂️Tisa kumi kwa mimi kukutana na Mama yake Hellena niliingia kichefuchefu, roho mbaya ikanivamia, macho yangu meupe yakaiva wekundu, nilitamani kumrukia na kummeza🦈 mama Hellena lakini acha tu nilivumilia uchungu wangu.
"Joyce bado upo vile vile mkondefu, mchafu usiyebadilika." Neema mama yake Hellena aliongea kunikebehi.
"Neema nakushangaa bado unavaa vimini vinavyoonesha nguo yako ya ndani 👙 inayowavutia wadudu wadogo wadogo wanaokunyemvua nyemvua." Nilirudisha madongo yaliyojaa mafumbo.
"Nyoo! Huna jipya Umbwa 🐕Malaya wewe." Alinikasirisha nilitamani kumrudishia jibu baya lakini nilijizuia sababu watoto walikuja pale mlangoni isingelipendeza kuwaona wanasikiliza kelele zetu.
"Mama Card karibu ndani." Mtoto Hellena Alinikaribisha. Niliachia tabasamu la unyonge nikimtizama hasimu wangu Mama Hellena, mtimani nilijuta inakuaje ninakutana na adui yangu wa miaka ya Chuo kikuu.
"Karibu pita ndani kwa furaha ya watoto wetu." Neema Alinikaribisha pasina kinyongo nilikubali nikaingia ndani na kuketi sofani, watoto wakarudia michezo yao. Wine 🍷 ya Mzabibu ilifunguliwa lakini jamani nilishindwa kuinywa zaidi ya kuangalia tu. Wakati watoto wetu wanafurahia sie tulitazamana kwa chuki na mahasira.
Jioni ilipoingia niliwasha Gari yangu na kuondoka pamoja na mwanangu Cadabra kurejea nyumbani. Kichwani nilivurugwa nikikumbuka jinsi Neema alivyonitendea Chuo.
''''"""""""""""""""""""""""""""""
Tulipokua Chuo kikuu Cha Makumira Arusha, Neema alikua na wivu sana, alijaa wivu, husda na gere. Hakunipenda sababu nilimzidi urembo na uzuri pale Chuo. Sema yeye alijiona kama Malkia wa University. Mara kwa mara alinipatia kazi nzito ili kunishusha nionekane chombo dhaifu.
Alikusanya nguo zake chafu na kuniletea ili nimfulie tena hakujali kama ndani ya zile nguo Kuna vyupi vyake vilivyochoka na kukomaa, alinilazimisha nimpigie deki chumba chake au kwenda soko kumnunulia mahitaji yake. Alifanya hivyo maana pale Chuo alijiita Malkia 👸 wa Chuo tena alikua na wafuasi wengi waliomuunga mkono.🤝
Nilipokosea mambo madogo madogo ambayo hayakua na tija yeye alituma wanaume makundi makundi waje wanipige na kunitesa. Mara nyingi niliponea kubakwa au kulawitiwa, kilichoniokoa ni zile mbio za Farasi 🎠🐎 nilizozitimua kuwakwepa wafuasi wake.
Nilipomriport kwa viongozi wa Chuo🎓, nilisikilizwa malalamiko yangu?❓❔ Hakuna kitu kama hicho, Viongozi pia Walimheshimu maana ni wafuasi wake: Walimheshimu, walimsikiliza na kumtii Malkia wa Chuo kutokana na kuheshimiwa kule Neema alivimba na kujiona ana nguvu za Simba au tembo jike.🦁🐘
Tukio Moja ambalo linakataa kufutika moyoni mwangu ni Lile tukio lililonifanya kukonda na kudhoofika hatimaye kulazwa Hospitali ya Mirembe kama kichaa mwendawazimu, na ukichaa niliupata. Neema aliniibia Boyfriend wangu Jully mwanaume ambaye tulikubaliana kufunga ndoa👰💍💒 na kuanzisha familia
Na hili kunikomoa Neema alimteka Jully mazima akanidhoofisha na kunifanya niwe mtu wa kulialia😹 na kujiona Nina mikosi. Baya zaidi katika mitihani yangu ya mwisho ya kumaliza Chuo📃📝 rafiki huyu aliwahonga Malectures mamillioni ya pesa (Rushwa)💵💰 ili wanifelishe nionekane nimeyakosea maisha. Nashukuru Mungu Rushwa aliyoitoa haikufua ndafu, wakufunzi walinionea huruma maana waliyajua mateso ninayopitia, wakanisahihishia vema mie nikapasua na kazi nzuri niliipata tena maisha niliyapatia.
Nilipata mume mzuri, kazi nzuri inayolipa vema, nikajaliwa mtoto mzuri wa kiume tena tukajenga bonge la Mjumba ili kuishi. Sema Mungu Baba alimchukua mume wangu mapema mno.
***************
Nilipoondoka nyumbani kwa Neema Sikutaka tena kumsikia sembuse kuwasiliana naye ingawaje Bado mwanangu Cadabra aliendelea kuufurahia utoto wake na rafikie Hellena. Siku moja simu☎️📞 kutoka Shule kwa mwanangu Card iliita: 'Mama Cadabra tafadhali ukuje haraka Shule Kuna jambo la kujadili kuhusu mwenendo wa mwanao Card.' Mkuu wa Shule alinisistizia.
'Ok. Madame naja.' Niliachia kazi zangu za kiofisi nikafunga Safari hadi kufika Shule asomayo mwanangu Card na rafikiye Hellena. Nilipofika nilishangaa kumkuta Neema amejaa tele ndani ya Ofisi ya mwalimu mkuu. Nilistaajabu. Baada ya salamu maongezi yalipamba moto🧨
"Mwanao Card amebadilika sana siku hizi yaani anafikia hatua ya kumpiga rafikiye Hellena hadi kumuumiza."Mkuu alitoa mashitaka juu ya mwanangu Card.
"Mwanangu hawezi kufanya hivyo angali ni mdogo kupigiana "Nilimtetea mwanangu.
"Usiseme ni mdogo kupigana ukiwa wewe haumchungi Wala kumuongoza kwa adhabu." Neema aliyenishitakia mwanangu alinikisoa.
"Kama mwanangu Card amempiga Hellena mbona wewe kama Mama Hellena haujaniambia zaidi ya kukimbilia kwa Mwalimu mkuu? Je, Sina haki ya kujua? Nilimuulizaswali ambalo mwalimu mkuu aliliafiki.
"Sema wewe umekosea kumlea vizuri mtoto wako hilo ni tatizo kubwa yamkini Bado anamkumbuka marehemu Baba yake." Neema alinikasirisha nilijua tu anautafuta ugomvi.
"Tafadhali neema usinikumbushe juu ya kifo Cha marehemu mume wangu, habari za kifo cha Baba Card hazihusiani na kikao hiki." Nilimkaripia.
"Kikubwa wewe tafuta Mwanasaikolojia amjenge mwanao na pia akujenge wewe maana mnaonekana mnevurugwa." Neema alizidi kunichokoza hapo ndipo mwalimu mkuu akayatamka maneno makali ya kuumiza.
"Nikiendelea kupokea taarifa mbaya kama hizi ninakuapia Mama Cadabra nitamfukuza mwanao asiendelee kusoma shule hii." Nilijua tu Neema keishatoa Hongo ili nitishike lakini kamwe sikutetereka Wala kuogopa.
########
Basi nilichofanya mimi ni kumkataza mwanangu Card asithubutu kuenda nyumbani kwao Hellena tena asithubutu kucheza na Hellena jambo hilo lilimuumiza sana mwanangu. Upweke ukamvamia tena na unyonge ukamrudia, furaha yake ikatoweka lakini siku moja niliskia mlango wa sebuleni yangu ukigongwa nikatoka kwenda kuufungua kidogo nishituke na kushangaa. Hasimu yangu Mama Hellena alisimama mlangoni, usoni akiwa mnyonge mwenye huzuni.
"Nisamehe 🙇♀️Joyce, nisamehe tafadhali."Alianza kuongea
"Usijari karibu ndani tuyajenge." Nilikua mpole, aliingia ndani, tukaketi sofani nami nikaanda wine 🍷 ya Mzabibu tukaanza kunywa🥂
"Ninajuta Joyce, ninajuta kwa mabaya yote niliyokufanyia Chuo hadi huku nyumbani, nilikua ninakuchukia bila sababu maana ulinizidi uzuri na mwonekano. Kila jambo ulifanikiwa ukiwa Chuo na ulikua na akili nyingi kuniizidi mimi."Aliongea.
"Haya yashapita ule ulikua ni utoto na ujana." Niliurainisha mtimani wangu.
"Ninaomba mwanao Card arudi kuongea na mwanangu Hellena sababu Hellena huko nyumbani hataki kula Wala kulala analia tu maskini, anamlilia Card."
"Nimeanza kuogopa jinsi anavyoipoteza amani, nina hofu nitampoteza mwanangu." Neema alichukua kitambaa cha mafua akaanza kujifuta machozi yaliyoanza kumdondoka.😿
"Pole Neema lakini ni heri wewe uliye na mume anayeweza kumfariji mwanao" Niliongea kiuchokozi kumkumbushia kuhusu Jully Boyfriend wangu aliyenipokonya Chuo
"Mbona tuliishaachana na Jully, baada ya kumzaa Hellena nilimwona kama hafai na tena Hana maana. Nilimtimua kwangu kama Umbwa,🐶 mwanaume yule hajui kulea mtoto, Hana mapenzi ya kweli, yupo yupo tu yeye kula, kunywa, na huduma zote nimpatie mie."Neema alilalama kwa uchungu.
"Pole, ulichagua fungu la kukosa." Nilimfariji
"Lile halikua fungu langu." Alinifurahiaha kisha akatamka:
"Kesho nitaenda kumuona mwalimu mkuu, yule mpendwa Rushwa. Nitaenda kueleza ukweli kwamba nilidanganya Cadabra hakumtendea ubaya Binti yangu. Nitaenda kulisafisha jina la Card, mipango yangu michafu itaniumbua."
"Kweli kabisa, fanya hima maana sisi binadamu hatujakamilika." Nilimwambia, alinielewa. Kuanzia siku ile audui kati ya mimi na Neema ulikatika, t
ulipendana upya na watoto walituunganisha.
:::::::::::::::::::::::::
TCHAO
❤️👨❤️👨👩❤️💋👨💝 Let love lead.
*************
Monday, December 2, 2024
SOME TIME SANE, SOMETIME INSANE.
MUME WANGU ALIMTIMUA🏃 NYUMBANI🏠 MAMA YANGU MZAZI MWENYE CHANGAMOTO YA AKILI🤪 MARA BAADA YA MAMA KUMFUMANIA AKIGONOKA NA CHANGUDOA. 💏
NJAMA CHAFU (A CONSPIRANCY)
Sunday, December 1, 2024
KIKULACHO KIMO NGUONI MWAKO
HERENI ZENYE KITO 💎CHA KIJANI💚 KINACHONG'AA (EMERALD GREEN) ZILISABANISHA NIJUE MUME WANGU ANACHEPUKA NA SHOGANGU WA DAMU.
I promise you
I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...

-
Simulizi MBOSSO SEHEMU ya kwanza KIZINGITI “Wasemaje mwana mpuuzi wewe? Hivi una akili za kutosha kichwani hata uta...
-
Karibu sana Hadithi tamu za kusisimua Kwa mawasiliano kakaelia26@gmail.com
-
Ndege ya British Air wing ilitua katikati ya kiwanja cha kimataifa, ARUSHA INTERNATIONAL AIR PORT. Ndege hiyo ilikuwa ikitoke...