""""""
TUNDA🍇🍒🍓 LA FARAJA 🧑🍼
Nilimpenda Jerry👩❤️💋👨, nilimpenda sana hatimaye Mimi na yeye tulikuja kufunga ndoa 👰💍💖ambayo ilikuja kujibu baada ya Mwaka mmoja wa furaha ya ndoa binti yetu Zuena 🚼 (Basi tumwite Zuu🐝)alizaliwa mapenzi yetu yakawa matamu ya kudumu. Mie Isha, Jerry na Zuena tulikua na utaratibu mmoja mzuri ambao hatukuuacha 'Kutoa zawadi siku ya Christmas 🎄 🎁 ⛄ na Mwaka mpya🎊🎉🎇' kutoa zawadi Kwa Mamia ya watoto waliokuwa wakiifurahia siku ya Noeli 🧑🎄na New year🎊.
Ya Mungu mengi Binti yetu Zuu alikuja kuugua🤒🥵 sana, aliugua Maralia kali iliyopelekea kudondoka na kuzima 🌠 🕯️huzuni ikavamia nyumba yetu, furaha ikapotea na kutoweka lakini bado tuliendelea na ule utamaduni wetu wa kutoa zawadi Kipindi cha sikukuu ya Noel na mwaka mpya Zawadi nyingi walizozipenda watoto ni Pipi,🍭🍬🍫 Biscuits🍪, Big G, Maputo 🎈na midoli ya kuchezea 🎎🪆.
Bahati ya kuishi na Mume wangu Jerry ikaingia mdudu, Jerry akanikataa wazi wazi,💔 Jerry hakutaka kuishi na Mimi Tena. Alinitamkia kuwa hanipendi, amenichoka, Hana hamu ya kuishi na Mimi. Nilipigania ndoa💍 yangu kutaka kujua sababu kuu inayofanya Mume wangu wa ndoa kutaka kuishi pekee, kujitenga na kuondoka nyumbani.🏡 Jawabu nililolipata kutoka Kwa Jerry: 'Niache ✋nipumzike'. Nikanywea lakini bado kila ifikapo Noeli na mwaka mpya Zawadi zilimiminika Kwa watoto🧸🐅🐰. Utamaduni huo niliuedeleza nikiwa pekee yangu.
******************
Noeli ya mwaka 2023 niliipenda japokua upweke ulinimeza, 👤upweke wa kutokuwa pamoja na Mwanangu Zuu,🧑🍼🚼 upweke wa kuachwa na Mume wangu mpenzi Jerry.🏌️♀️ Baada ya kugawa zawadi 🎁💐🎅Kwa watoto nikapata wazo niende kulitembelea kaburi la mwanangu Zuu, 🪦nikamwage chozi😿😢 nimuombee🛐📿 kipenzi changu abaki palipopema salama peponi☁️🌉
Nilifika lakini pembeni ya kaburi la mwanangu Zuu Kuna kitu nilikiona nacho kikaniogopesha na kunishitua. Nilikuta kapu, kapu lililoachwa hapo. Nikalisogelea baridi ilikua ikinipiga,⛄🌨️🧊 meno yalitetemeka, nikakisogelea kile kikapu na kuchungulia kilicho ndani ya kapu.
Jesu! 😶Nilishituka mie nisiyaamini macho yangu, nikatazama ndani ya kapu, moyo ulikufa ganzi.
'ng'aaa ng'aaa ng'aaaa' 😢sauti ya kitoto akilia ilisikika baada ya kuniona. Nikayageuza macho yangu👁️ huku na huko kutazama iwapo Kuna mtu ameacha mtoto pale Makaburini lakini sikubahatika kuona mtu. Nikabaki na butwaa 🤔mtoto aliendelea kulia.
Akili zikaniambia mchukuehuyo mtoto , nikafanya taratibu kumtoa ndani ya lile kapu nikamtoa mtoto aliyekua akilia, mwili mzima ulipigwa baridi, mtoto alitetemeka.
"Oh! Baby usilie, hivi ni nani anayeweza kufanya ukatili huu wa kukuacha pekee Makaburini?" Niliongea na katoto nikijua fika hakawezi kutoa jibu. Nilipomnyanyua yule mtoto kutoka ndani ya lile kapu,🧺 macho yangu yakakiona kikaratasi kidogo cheupe,🗒️🖇️ nikainama na kukichukua ndani ya lile kapu, nikakutana na maandishi yameandikwa:
'BINTI HUYU ANAITWA AMANDA, UMRI : MWAKA MMOJA'
Hakuna maandishi mengine yaloongezwa. Nikakigeuza kile kikaratasi labda nitaambulia nambari za simu za aliyembwaga Amanda pale makaburini⚰️🪦 lakini wapi! sikuziona. Mazingira ya Makaburini yalikua tulivu asionekane mtu akipita. 🚶♂️🚶♀️Nifanye nini? Nilijiuliza.🧐❓Wacha niondoke, sikuweza kulitimiza lengo lililonileta pahali pale, lengo la kumuombea Binti yangu pamoja na kumuombolezea🤲😢 mpendwa wangu Zuu. Lundo la mawazo yalinisumbua kichwani.😤🤯
Nilipofika nyumba🏘️ nikamkagua kagua yule Binti aliyekua amejinyea, 💩nikamfuta kinyesi na kumtafutia mavazi mapya. 🧦👚Baada ya masaa kadhaa nilipata wazo la kwenda Polisi kuripoti juu ya kumuokota mtoto Makaburini. Polisi walinipokea nami nikawaeleza kila kitu kwa hakika walishangaa🥺🤭 sababu ingelikuwa ni vigumu kumpata tena mzazi au mlezi wa Amanda maana mzazi au mlezi hakujulikana.🤷🙍
Polisi walinishauri nimchukue na kumpeleka kituo Cha kulelea watoto yatima, moyoni niliona sio Poa😞👎. Nikawaomba nimchukue yule mtoto na kuishi niishi nae, mtimani nilijiona nina bahati.💗 Nimefiwa na Binti yangu na sasa nimeokota tunda🍇🍒 la faida na faraja Tena tunda Hilo nimeliokota pembeni ya kaburi la Binti yangu. Aah!🙃😶 Jamani! Hii ni bahati, 🌠 ikiwezekana nitafanya process za kuasili mtoto (Adoptation) Ili awe Mali yangu.
%%%%%%%%%%%
Amanda Akawa wangu na Mimi wa Amanda, ikawa kila siku nikiamka ni mwendo wa kumfuta kinyesi alichojinyea, kumuogesha, kumpikia👨🍳🍚 uji na kumpatia maziwa. 🍼Nilikesha kumbembeleza Binti yangu iwe usiku iwe mchana yaani hadi nikawaomba waajiri wangu wanipunguzie majukumu Ili tu niwe karibu na Binti yangu.👨🍼 Nashukuru Mungu mtoto aliendelea kukua na kutimiza mwaka mwingine🥳🎂🎊🧡 akiwa mikononi mwangu.
Ndani ya mwaka huo mzima sikupata kupokea simu 📱ya kuitwa Polisi 👮♂️kupokea taarifa juu ya kupatikana Kwa Mama au mlezi wa Amanda. Noeli🎅🎄 ilipoisha baada ya mie na Binti yangu Amanda kugawa zawadi Kwa watoto🐰🦎🐉🦄🍿🧃🎁🎐 nilisikia mlango wa sebule yangu ukigongwa 🚪nikambeba Amanda wangu mgongoni Kisha tukatoka kwenda kumfungulia mgongaji.
Mlangoni nilikutana na sura ya polisi👮♂️ aliyeambatana na Bibi kizee👵 mwenye kadirio la miaka sabini. Baada ya salamu Nikawakaribisha 'Karibuni' 🙋♀️
"Pole na majukumu Mama Amanda." Polisi aliongea nikafurahia kuitwa Mama Amanda.
"Asante nimepoa, ni muda mrefu Sasa tangu tumeonana " Nilimwambia yule Polisi.
"Mmh! Isha Kuna jambo Moja muhimu lililonileta kwako Leo nikiambatana na huyu Bibi kizee." Alimnyoshea 👉 👵mkono yule Bibi kizee mwenye makunyanzi usoni.
"Bila shaka ongea." Nilimpa nafasi yule Ofisa kuongea 🔊lililowaleta.
"Mama Mlezi wa Amanda amepatikana, huyu Bibi umuonaye ndiye mama mlezi wa Amanda." Ofisa wa Polisi alinishitua nikageuza shingo yangu kumtazama yule Bibi kizee.
"Kwa hiyo lsha Bibi yake Amanda amekuja kumchukua mjukuu wake."
"Toba!"⁉️ Nilitetemeka, "Kwa hiyo Leo mwana nimpemdaye anachukuliwa?" Nilimuuliza yule Ofisa huku Macho yakianza kunijaa machozi.
"Damu🩸🅾️ nzito lsha,"Polisi aliongea kwa ufupi.
"Hata kama Bwana Polisi Bado ninampenda Binti yangu." Nilijitetea.
"Ninatambua lsha lakini ni vizuri mwenye mali apewe mali yake." Bwana Polisi aliongea. Niliona kama Dunia inataka kuniangukia, mtoto👶 niliyemzoea, niliyemhudumia Leo hii anakuja mtu mwingine kunipokonya.
"Tufanye nini sasa Isha, mlezi wa mtoto Sasa amekuja na sisi Polisi tunatimiza wajibu wetu.Sikulielewa jambo analoliongea yule Bwana Polisi. Nilichopaswa kufanya ni kumkabidhi mtoto kwa mlezi husika tena ajabu hata sikuambiwa kisa cha huyo mtoto kutelekezwa makaburini ⚰️. Baada ya majadiliano ya muda mrefu tulikosa mwafaka lakini asiyekubali kushindwa si mshindani Bibi yule alimchukua Amanda akaniacha katikati ya uchungu na kuteteleka. Nikalia mie machozi la damu 😭😢🩸
Nikazama maombini 🛐 nikimuiliza Mola wangu: 'Kwanini unanipa zawadi🎁 njema alafu unanipokonya.' Mola wangu hakunijibu kwa wakati akaniachia Ziwa la machozi.
"Chukua bahasha hii." Bibi yake Amanda alinipatia bahasha niliyoipokea nisijue Nini kilichomo ndani ya bahasha, mtimani sikua na furaha ya kuondokewa na mtoto nimpemdaye ingawaje sio wangu wa damu. Bwana Polisi na Bibi yake Amanda wakaondoka na mie nikaelekea tandani kujibwaga nikiwa na wingi wa mawazo yaliyonisumbua na kuninyima Raha, nikamuwaza mwanangu Amanda niliyemuokota.
"Saa sita mchana niliamka kutoka ndani ya dimbwi la mawazo huzuni na upweke nikakichukua kile kibahasha nilichopewa na Bibi yake Amanda, wala sikujua Nini kilichoandikwa ndani ya ile bahasha. Yule Bibi amemchukua mtoto bila kuniachia hata senti Tano labda ndani ya kile kibahasha Kuna karatasi ya Bank cheque nikajichotee mapesa Bank?😅💖 Nikaifungua ile bahasha taratibu na kukutana na kijikaratasi cheupe kilichoandikwa
"ASANTE SANA NlNASHUKURU UMEMTUNZA NA KUMLEA AMANDA."
Moyo wangu uliripuka 💔🔥mara baada ya kuona mwandiko ambao nilihisi kuutambua. Haraka haraka nikakimbilia kwenye droo ya kabati 🗄️la nguo nikafanya kupekenyua na kupekenyua Kila kitu, nikakitafuta kile kikaratasi ambacho kiliachwa ndani ya kapu ile siku Amanda ametelekezwa makaburini. Nilikipata nikakichukuana kukiunganisha pamoja na kile cha pili nilichopewa na Bibi yake Amanda.
Jesu!! 🫥 Nilishangaa. 'Mbona mwandiko huu wa Bibi yake Amanda na huu uliopo kwenye kikaratasi nilichokipata kwenye kapu ile siku Amanda ametelekezwa miandiko inafanana?!' ⁉️ Nilijiuliza.
'Hapana, 🙅♂️ Kuna kitu hapa labda huyu Bibi Hana nia nzuri, labda huyu Bibi sio mtu mzuri.' Nilipata wazo.
'Yamkini ni yeye ndiye aliyemtelekeza Amanda mwaka mmoja uliopita na Sasa amekuja kumchukua. Huu sio uungwana.' Niliwaza.Haraka haraka nikiwa nimevurugwa. Nikapata mawazo mawili; Mosi niende Polisi kuripoti hili jambo, pili nimtafute mume wangu Jerry mwanaume wangu aliyetaka kuishi pekee baada ya kifo Cha Binti yetu Zuu. Wazo la kwendra🚶♀️ Polisi sikulitilia maanani ila wazo la kumpigia Simu☎️📞 Jerry liliniingia kichwani. Haraka nikaichukua simu yangu ya mkononi na kubinya vitufe.📱
"Hallow, Jerry habari Yako!?" Nilimsabahi.
"Sijambo lsha. Habari za masiku!?" Alinisabahi pia.
"Nzuri, nina jambo Moja la haraka ninaomba uje nyumbani kigamboni tujadiliane." Nilimwomba.
"Nina kazi za kiofisi, lsha labda tukutane baadae."
"Hapana Jerry ni jambo la haraka naomba uje tulijadili." Nilimsihi kwa mabembelezo.
"Ok. Baada ya dakika therathini nitakuwepo hapo." Alikubali ombi langu, ndani ya dakika therathini Jerry alikuwepo sebuleni tukayajadili.
"""""""""""""
"Mwandiko huu katika karatasi hii na mwandiko huu katika karatasi nyingine unafanana. Nina mashaka juu ya huyu Bibi yamkini anania mbaya juu ya mtoto Amanda." Nilimwambia Jerry baada ya kumsimulia Kila kitu kuhusu mtoto Amanda, jinsi nilivyomuokota, jinsi nilivyoenda Polisi kuripoti hadi pale niliporuhusiwa na mabwana Polisi nichukue mtoto Amanda na mwisho ujio wa Bibi aliyedai Amanda ni mjukuu wake pia nilimsimulia nilivyoachiwa ujumbe wenye mwandiko ulionitia shaka.
"Yamkini huyu Bibi ni mtapeli nia yake ni kumuuza mtoto Amanda." Jerry aliongea.
"Sina imani kama yule Bibi anania ya kumuuza Amanda lakini swali langu ni kwanini alimtelekeza mtoto Amanda makaburini?!" Niliongea.
"Hukumuuliza?!" Jerry aliniuliza.
"Nilivurugwa Jerry huo muda 🕣wa kumuuliza ningeliupata wapi?"
"Tusiandike mate wino ukiwepo labda huyu Bibi siye aliyemtelekeza mtoto Amanda." Mume wangu Jerry alijirudi.
"Kwanini tusiende Polisi kuripoti na kufungua faili 📑 la mashitaka." Nilishauri.
"Nitakua bega kwa bega pamoja na wewe." Jerry aliniunga mkono. Tulielekea kituo cha Polisi tukatoa taarifa na kufungua faili kumshitaki yule Mbibi anayedai Amanda ni mjukuu wake, Mbibi aliyemtelekeza Amanda juu ya makaburi Kisha kuja kumchukua bila sababu ya msingi.
""""""""""""""""
Kesi ilianza kuunguruma Mahakamani , Bibi yake Amanda alijitetea sana na kutuvunja moyo💔 wa kufanikiwa kumrejesha mtoto Amanda. Kila tulipoudhuria Mahakamani Mahakama ilimpa nafasi ya kushinda ile kesi 👨⚖️ lakini uzuri sikuwepo pekee katika ile kesi Jerry Alisimama pamoja na mimi kumpinga Bibi yake Amanda
Kesi ilizidi kuwa chungu, maswali mazito yaliyotua mbele ya Bibi yake Amanda yalimfanya aonekane ule ushindi alojivunia kupata ungelimdondokea puani. Akasarenda hatimaye akaieleza ukweli Mahakama akasema:
😭😭😭😢
"Sophi mama yake Amanda alifariki akiwa Leba, alifariki akiwa anajifungua. Bahati nzuri Amanda alizaliwa salama nikamchukua na kuanza kuishi naye kama mjukuu wangu kwa kipindi Cha mwaka mmoja." Aliendelea kuisimulia Mahakama
"Lakini ukweli ni kwamba sikua na furaha ya kumlea mjukuu wangu Amanda maana nilihisi mjukuu wangu anauchoma moyo na roho yangu. Mwanangu Sophia amekufa akiwa anamzaa Amanda." Bibi alianza kulia😿😭😢Mahakama haikumuacha mtupu ilimkamua hadi kubaki mifupa, ikamtaka yule Bibi aeleze vizuri, akaieleza.
"Kifo Cha mwanangu Sophia kiliniachia huzuni na uchungu, Sophia alikua ni Binti yangu wa pekee hakustahiri kufa"😭 Mahakama ilimuelewa.
"Hakustahiri kufa lakini mtoto Amanda aliisababisha huzuni kuingia moyoni mwangu. Mjukuu alizaliwa pasina mie kumjua Baba wa mjukuu nikaona mzigo umenielemea. Kumtunza kazi na kumlea kazi baya zaidi mjukuu wangu alikua akaniletea kumbukumbu zilizoniumiza na kuuchoma mtima wangu."Aliendelea kujieleza.
"Hatimaye nilibuka na wazo lililoniambia siwezi kukaa na mjukuu anileteaye kumbukumbu zinazoumiza mtima wangu, niliona Bora nikamtupilie mbali na upeo wa macho yangu. Nikafanya tendo baya la kwenda kumtupilia makaburini pahali alipozikwa mama yake mzazi." Maelezo ya yule Bibi yaliishangaza Mahakama.👩⚖️
"Wewe ni muuaji, wewe ni muuaji."🤬 Kelele nyingi zilizopigwa Mahakamani zililindimaa, watu walioudhuria ile kesi walipigia makelele.,🔊
"Naomba nisamehewe ndugu zangu, hata ivyo suala la kumrudisha mjukuu wangu ni ndoto zinazonisumbua usiku na mchana juu yake. Ninaumia, ninateseka na pia najutia kufanya maamuzi yasiyo sahihi."Alijitetea
Mahakama haikumsikiliza tena, Mahakama iliamuru yule Bibi apokonywe mtoto Amanda. Mtoto alipokonywa Mahakama iliamuru mie Isha nikabidhiwe yule Malaika.👼 Waooo!😘 Furaha isiyomalizika ilinivamia nilipokabidhiwa mtoto Amanda akawa mikononi mwangu Bibi yake Amanda aliachwa akilia kwa uchungu😭 na Bado tu alifunguliwa kesi nyingine, kesi ya kumtupa na kumtelekeza Amanda Makaburini 😁😅 Lazima ajute.😅
*************
Muda wa kutoka Mahakamani watu wengi walinipongeza kwa roho nzuri na ujasiri wa kumpigania mtoto Amanda. Jerry alikua anaondoka kuwai kazi zake za kiofisi, nilimkimbilia na kumwambia;
"Karibu jioni ya Leo nitaandaa chakula, tujipongeze na kuufurahia ushindi wa kumkomboa mtoto Amanda. Jerry alifurahia naye alikubali kuja jioni ya Leo.
"""""""""""
Basi mapenzi yangu mie na Jerry taratibu yalianza kufufuka. Jerry mume aliyenitupa zamaani akataka uhuru wa kuishi pekee yake Sasa akaanza kurudi taratibu, taratibu nyumbani kwangu. Amanda ameufanya moyo wa Jerry ulainike, Amanda amefanya mimi na Jerry kupatana, tumekua familia Sasa, sawa tulimpoteza Zuu wetu lakini mola hajatuacha ametukabidhi Amanda wetu.
""""""""""
TCHAO
From Amanda With love 😘💖
""""""""""''
."